Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1418 | 1419 | (Page 1420) | 1421 | 1422 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

  Na  Mwandishi Maalum, New  York

  Rais wa  Mahakama ya   Kimataifa ya  Makosa ya Jinai ( ICC) Jaji Slivia Fernandez de  Gumendi,  jana  (Ijumaa),  amekutana na kufanya  mazungumzo na  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Matiafa,  Balozi Tuvako Manongi

  Katika  Mazungumzo  hayo baina ya   Jaji  Gumendi na  Balozi  Manongi  yaliyofanyika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania,   Rais wa ICC aliishukuru Tanzania kwa hotuba yake   iliyotolewa na Balozi  siku ya Jumatatu wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  lilipopokea na  kujadilia Ripoti ya  ICC.

  Kwa  mujibu wa  Rais wa ICC Jaji Slivia Fernandez  de Gumendi  hotuba  ya    hiyo ya  Tanzania  ilikuwa   yenye uwiano (balanced)  na pia  ilitoa  ushauri au mapendekezo ya namna gani  Mahakama hiyo  inavyoweza kuboresha uhusiano  na  wanachama wake  kwa mujibu wa Mkataba wa Roma.

  “  Nilikusikiliza  kwa makini sana  wakati  ulipokuwa unatoa hotuba  yako,   nilinukuu  kila  hoja   ulizokuwa unazizungumza . Hotuba   ya  Tanzania ilikuwa yenye  uwiano    (balanced) na ningependa  kuitumia   fursa hii kuishukuru   Tanzania kwa hilo.

  Rais   huyo wa ICC amekiri kwamba anadhani ni wakati  muafaka  kwa wadau wa pande  mbili  kukaa na kuzungumza  kama ambayo  Tanzania  na wanachama  wengine wameshauri hasa kutokana na kile  alichosema, kwamba, kila nchi imekuwa na  tafsri  tofauti  na  uelewa tofauti  kuhusu baadhi  ya  vipengere  (articles) zinazohusu Mkataba wa Roma  unaounda  Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.

  Kwa upande wake Balozi Manongi amesema,   ushauri na mapendekezo ambayo  yametolewa  na Tanzania pamoja na nchi nyingine hayalengi katika  kutaka  kubadili  Mkataba  wa Roma  au kuipunguzia  nguvu ya  kiutendaji  Mahakama hiyo.

  “Tungependa sana  ieleweke kwamba tunaposhauri kukaa na kuzugumza  kusitafsiriwe kana kwamba tunataka kupunguza nguvu ya utendaji wa  chombo hiki ambacho  wote tunaamini kwamba  kinastahili kuwapo. Tunashosema na kusisitiza, kwamba   kila  upande unahoja  za msingi basi tuzijadili kwa kuzungumza” akasisitiza  Balozi  Manongi.

  Rais wa  ICC na  Balozi Manongi  walibadilishana mawazo juu  na masuala mbalimbali kuhusu utendaji kazi wa Mahakama ya  ICC ikiwa ni pamoja na  kuangalia ni maeneo gani ambayo   Mahakama na wanachama  wake  wanaweza kujadiliana . 

    Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi akiwa  katika  mazungumzo  na  Rais  wa Mahakama ya   Kimataifa ya Makosa ya Jinai  ( ICC)  Jaji  Slivia Fernandez de Gumendi. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika  Ubalozi wa Tanzania,  Rais wa ICC alitumia fursa hiyo  kutoa shukrani zake kwa Tanzania  kwa   hotuba   ambayo si tu ilikuwa na  ushauri wa namna ya  kuimarisha  ushirikiano baina ya  Mahakama hiyo na  Wanachama wa Mkataba wa Roma  hususani kutoka nchi za Afrika lakini  pia kwamba ilikuwa ni  hotuba ya    uwiano.  Jumatatu  wiki hii Tanzania ilikuwa kati ya nchi zilizozungumza wakati  Ripoti ya utendaji kazi  ya ICC ilipowasilishwa katika Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa. 
  Balozi  Tuvako Manongi na Rais wa ICC Jaji Gumendi  mara baada ya kumaliza  mazungumzo yao ambayo  yaligusia  masuala mbalimbali  kuhusu Mahakama ya Kimataifa ya  Makosa ya Jinai ( ICC)

  0 0
 • 11/05/16--07:27: JARIDA LA WIZARA YA HABARI
 • Attachments area

  0 0

   Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu
  Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya
  Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.
  Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
   Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara,
  Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa
  Lumumba jijini Dar es Salaam
  Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Katibu
  Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao
  Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Msemaji
  wa CCM, Christopher Ole Sendeka, na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na
  Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana.

  (Picha zote na Bashir Nkoromo).

  0 0

  Bwana Harusi Ntibashima Edward ambae ni Mwajiriwa wa Kampuni ya Clouds Media Group inayomiliki Kituo cha Runinga cha Clouds pamoja na Clouds Fm, akimvisha Pete mke wake Bi Zitha Kannonyele, wakati wa Ibada ya ndoa yao iliyofungwa leo Katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam na Kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali walioalikwa kushuhudia tukio hilo muhimu kwa Wawili hao.
  Bi Harusi Zitha Kannonyele akisoma mistari mitakatifu iliyoandikwa ndani ya Biblia, huku Bwana Harusi Ntibashima Edward, aliyevaa suti akisikiliza kwa makini maandiko hayo, tukio hilo limefanyika leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Ibada ya ndoa yao, ambayo imefanyika katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over. 
  Maharusi hao wawili wakisoma mistari mitakatifu iliyoandikwa ndani ya Biblia, wakati wa Ibada ya ndoa yao iliyofanyika leo katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam na Kuhudhuriwa na wageni mbalimbali walioalikwa Kushuhudia tukio hilo Muhimu kwa wanadoa hao. 
  Sophia Kessy na James Lyatuu ambao Wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi Ntibashima Edward , wakiwa wamepozi mbele ya kamera ya habari360.com, kwa ajili ya kupata picha ya Kumbukumbu. 
  Hapa wakiwa wamepozi na Bi Harusi Zitha Kannonyele kwa ajili ya Kupata Picha ya Kumbukumbu. 

  0 0

  Umoja wa Ulaya (EU) umewekeza zaidi ya Euro milioni 1 na laki 7 katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kitengo kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Makumira ambapo chuo kikubwa cha sanaa kinajengwa pamoja na kumbi ya burudani itakayogharimu kiasi hicho.

  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer amefanya ziara chuoni hapo ambapo amejionea shughuli za ujenzi zinazoendelea katika chuo hicho na kusema kuwa kupitia chuo hicho cha utamaduni wa Tanzania na makabila yake utaendelezwa ili kuleta manufaa kwa vijana na jamii nzima.

  Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za kutunza utamaduni kwani vijana wataweza kutengeneza fursa za ajira kupitia sanaa za utamaduni.
  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akizungumza katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha,mara baada ya kutembelea kituo hicho.(Picha na Ferdinand Shayo).

  Meneja mradi huo Randall Stubbs amesema kuwa kwa sasa wanatoa mafunzo ya ngoma za utamaduni wa makabila ya wamasai, wameru na wachaga ikiwa ni pamoja na kufanya maonyesho ya utamaduni katika maeneo mbalimbali.

  “Ujenzi utakapokamilika kutakua na ukumbi wa kisasa, jengo maalumu la mafunzo kwa utamaduni wa bara la Afrika, Asia na Ulaya ili utamaduni uweze kuwa endelevu na kurithishwa vizazi na vizazi” alisema Randall.
  Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelekezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer alipotembelea kituoni hapo.
  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha, mara baada ya kutembelea kituo hicho.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 11/05/16--07:50: MAZUNGUMZO
 • Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida kwenye jengo la Utawala Bunge mjini Dodoma Novemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipokuwa akitoa hoja kabla Kamati ya Bunge zima kujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 ambao umepitishwa leo mjini Dodoma.
  Wabunge wakiwa kwenye mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya Watendaji wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) wakifuatilia mjadala wa Wabunge wakati wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya Watendaji wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) wakifuatilia mjadala wa Wabunge wakati wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.


  0 0
  Na Jacquiline Mrisho na Eleuteri Mangi – MAELEZO, Dodoma.

  Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ambapo hatua inayofuata ni kuridhiwa na kusainiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili uwe Sheria kamili ya nchi.

  Muswada huo umepitishwa leo Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Andrew Chenge.Wabunge walijadili Muswada huo kifungu kwa kifungu na kuunga mkono upitishwaji wake baada ya Waziri mwenye dhamana na habari kutoa hoja ili Muswada huo uweze kujadiliwa.

  Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupitishwa Muswada huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewashukuru wadau wote walioshiriki katika kutoa maoni juu ya Muswada huo kwani ndiyo yamepelekea kukamilisha mchakato mzima wa Muswada huo.

  “Kwa niaba ya Serikali napenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha tunatimiza malengo ya takribani miaka 20 iliyopita ya kuifanya taaluma hii ya habari kuheshimika kama zilivyo taaluma zingine”, alisema Waziri Nape.

  Waziri Nape ameongeza kuwa kwa sasa Muswada huo umeshapitishwa hivyo kilichobaki ni utungaji wa Kanuni ambapo ameomba wadau wa tasnia ya habari kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutoa maoni yatakayopelekea kuwa na kanuni zenye tija kwa wanahabari na taifa kwa ujumla.

  Aidha, Mhe. Nape amewaasa wadau wa habari kuunganisha nguvu kwa pamoja hasa katika kipindi hiki ambacho Muswada huo umepitishwa pia amewataka wadau hao wasiruhusu mgawanyiko utokee kati yao bali washirikiane na Serikali katika kutekeleza wajibu wao wa kihabari kwa jamii.

  Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ni mwanzo mpya wa tasnia ya habari nchini ambapo amewaasa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa habari kutambua kuwa haki mara zote huendana na wajibu, hivyo hakuna haki isiyo na wajibu.

  Muswada huo uliopitishwa leo umejadiliwa na Bunge hilo kwa siku mbili ambapo kwa mara ya pili ulisomwa mbele ya Kamati ya Bunge zima na hatimaye kusomwa kwa mara ya tatu ili kukidhi hatua za utungwaji wa Sheria nchini.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya hisani ya kilomita 4.3 ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi, wakunga 400 katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning nchini.

  Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwemo kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa Afya na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote nchini.

  Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha huduma za Afya zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa Serikali itaendelea kusimamia uwajibikaji kwa watumishi na watoa huduma za Afya mpango utaenda pamoja na kuongeza vitanda kwenye wodi za wazazi na utoaji wa huduma ya Afya bure kwa makundi maalum.

  Makamu wa Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi waendelee kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi nchini ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.


  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametumia sehemu ya hotuba yake kwa kulipongeza Shirika la AMREF Health Africa Tanzania kwa mipango yake ya kusaidia jamii ya Kitanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ukiwemo mpango wa kugharamia masomo kwa njia ya ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia duni kwa lengo la kuwawezesha kusomea cheti ya uuguzi ukunga.

  Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha vifo vya wanawake wajawazito na watoto nchini vinapunguzwa kwa kiwango kikubwa kutokana na Serikali kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kununua vifaa tiba na kuongeza idadi ya wataalamu.

  Katika harambee hiyo, Jumla ya shilingi milioni 290 zimechangwa na wadau wa maendeleo na lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 fedha ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na umati uliojitokeza kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan (katikati) akiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga ambapo alitembea kwa kilometa 4.3 kuanzia viwanja vya Green Ground na kupitia barabara ya Toure na kurejea na barabara ya Msasani ,Oysterbay jijini Dar es Salaam wengine pichani ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  (kushoto) na Mkurugenzi Shirika la AMREF Health Africa Dkt. Florence Temu (kulia).Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam 
  Sehemu ya Umati uliohudhuria na kushiriki Matembezi ya Hisani ya Kusomesha Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground.


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Gari aina ya Nissan x-trial ambalo namba zake za usajiri hazikuonekana kwa haraka likiwa limeanza kushika moto upambe wa mbele na kupelekea kuteketea gari lote. tukio hilo limetokea jioni hii kando ya barabara ya Nyerere na usoni kabisa mwa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii, Jijini Dar es salaam, huku baadhi ya wasamalia wakijaribu kuokoa sehemu ya vitu vilivyokuwemo ndani ya gari hilo. hakuna alepoteza maisha wala kujerugiwa katika ajali hii. Chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika. Picha na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  Moto ukiendelea kuwaka kwa kasi.
  Harakati ya kuokoa baadhi ya mali ziliyokuwepo ndani ya gari hilo zikiendelea.
  Baada ya muda moto ukaenea sehemu kubwa ya gari hilo, hali iliyopelekea waokoaji kushindwa kuendelea na zoezi hilo.
  Moto ukiiteketeza gari hiyo.

  0 0


  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID


  MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, ametembelea vituo vitatu vipya vya kupooza na kusambaza umeme vilivyo kwenye mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.

  Vituo alivyotembelea ni pamoja na kile cha katikati yajiji, (City Centre), kilicho jirani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kituo cha Kurasini na kituo cha Ilala Mchikichini.

  Kwa takriban mwezi mmoja sasa, TANESCO kwa kushirikiana na wahandisi kutoka kampuni za Kijapani, Yachiyo Engineering Co Limited, Sumitomo, Takaoka na National Construction Limited, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora wa hali ya juu.

  “Nimeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya kubadilisha miundombinu yetu ya umeme, wakazi wa jiji la Dar es Salaam, sasa watapata umeme wa uhakika na ulio na ubora wa hali ya juu, jambo la kufurahisha sana ni kwamba mabadiliko haya yamekwenda sambamba na mipango ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda, bila shaka umeme huu utawezesha kufikia azma hiyo ya serikali.” Alisema Mhandisi Mramba, baada ya kukagua kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha katikati ya jiji.
  Mhandisi Mramba alisema, nia ya TANESCO ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya kukatika umeme mara kwa mara au kupata umeme hafifu usio na nguvu. “Mmeona mitambo hii nimipya kabisa nay a kisasa inayotumia teknolojia ya kisasa.” Alitoa hakikisho.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza wakati alipotembelea kituo kipya cha kupooza na kusambaza umeme cha City Centre jijini Dares Salaam, Novemba 5, 2016. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
  Mhandisi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Kupoozea na kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam

  0 0

  Watalaam 25 wa afya kutoka nchi tisa za Afrika leo wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kupima masikio na kufundisha kuongea kwa watu wenye matatizo ya usikivu.

  Mafunzo hayo yamewezeshwa na Kampuni ya MEDAL ya nchini Australia na kuhusisha washiriki kutoka nchi za Rwanda, Uganda ,Kenya , Zambia , Zimbabwe, Nigeria , Ghana, Malawi na Tanzania . Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ni mwenyeji wa mafunzo hayo.

  Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru ameishukuru Kampuni ya MEDAL kwa kuwezesha kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yanaisaidia Hospitali kupiga hatua katika mipango yake hususani katika suala la kutoa huduma kwa wale wenye matatizo ya usikivu.

  Awali, Meneja wa Maendeleo Kanda ya Afrika Mohamed El Disouky amesema MEDEL wataendelea kushirikiana na wataalam mbalimbali wakiwemo wa Muhimbili ili kuhakikisha wanapata ujuzi wa kutosha katika kutoa huduma hiyo.

  Mafunzo hayo yalianza Oktoba 29 mwaka huu jijini Dar es salaam na kumalizika Novemba 5, mwaka huu.
  Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki kutoka Muhimbili, JohnBosco Kambanga.
  Mshiriki kutoka Rwanda, Fidel Munezero akipongezwa baada ya kukabidhiwa cheti Leo.
   
  Wadau wa Afya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kupima masikio na kuongea yalioanza Oktoba 29, mwaka huu na kufungwa leo Novemba 5, 2016 jijini Dar es Salaam.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).


  0 0  Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwausalama kwa mkoa wa Iringa leo , mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza zawadi maalum ya kamati ya usalama barabarani mkoa kutokana na mchango wake mkubwa kwa kamati hiyo

  Kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Iringa wakijiandaa kutoa elimu katika viwanja vya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani
  Baadhi ya wananchi na watu wenye ulemavu wakiwa katika viwanja vya maadhimisho hayo

  Mwakilishi wa wakala wa barabara mkoa wa Iringa akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa na watu mbali mbali waliotembelea banda hilo kuona shughuli zinazofanywa .


  0 0

   
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mount Meru,Profesa Harrison Olang(kushoto)akizungumza na Mbunge wa Singida Kaskazini ambaye alikua mgeni rasmi katika mahafali ya 12. 
   
  Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini.Lazaro Nyalandu(kulia)akifurahia jambo na familia ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mount Meru,Profesa Harrison Olang 
   
  Picha ya pamoja na wahitimu 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo amekutana na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika kikao kilichochadili maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na shirika hilo ikiwemo Mradi wa Kusindika Gesi Asilia, (LNG) na Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

  Katika kikao hicho Prof. Muhongo ameitaka Bodi na Menejimenti hiyo kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi husika kutokana na manufaa ya miradi hiyo kwa Maendeleo ya Taifa.

  Mbali na Bodi na Menejimenti ya TPDC, kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

  Aidha, wakati huo huo, Waziri Muhongo pia amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke ambapo wamejadili masuala kadhaa kuhusu sekta ya nishati ikiwemo chanzo cha Nishati Jadidifu.Pia, Waziri Muhongo amekutana na Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser ambapo wamejadili masuala kadhaa kuhusu Sekta ya Nishati.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza Jambo wakati wa Kikao chake na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
  Sehemu ya Menejimenti ya TPDC wakifuatilia kikao baina yao na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
  Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke (wa pili kushoto) na ujumbe uliofuatana na Balozi huo.
  Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooken (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake walipomtembelea leo ofisini kwake Jijijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
  Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser mara baada ya kumaliza mazungumzo yao wakati Naibu Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.


  0 0

  z4
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya  kulifungua jengo la Mahkama kuu ya Chake chake Pemba leo akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo,
  z5
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya  kulifungua jengo la Mahkama kuu ya Chake chake Pemba leo akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo,
  z6
  Baadhi ya wananchi kutoka shehia mbali mbali katika Wilaya ya Chake chake Pemba wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Ally Daud-MAELEZO
  HUDUMA ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto imeanza kutolewa rasmi nchini  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  baada ya wataalamu wa huduma hiyo kurejea wakitokea mafunzoni nchini India ili kuweza kusaidia watanznia hususani watoto wenye matatizo ya kusikia .
  Akizindua huduma hiyo kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Uisubisya amesema kuwa  Huduma hiyo imekua hadimu nchini hivyo kufanya kugharamia kiasi kikubwa cha fedha kwenda kuwatibia nje ya nchi.
  “Kwakweli huduma hii ya kupandikiza watoto vifaa vya usikivu italeta msaada mkubwa kwa watanzania na kuokoa gharama takribani shilingi milioni 80 kwa kila mtoto ambaye alitakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi” alisema Dkt. Ulisubisya.
  Aidha Dkt. Ullisubsya amesema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kugundua mapema matatizo ya watoto na kuwaleta katika Hospitali ya Muhimbili ili wapate taratibu za kupata huduma hiyo bila ya kuchelewa na kpata madhara makubwa.
  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema kuwa Huduma hiyo ambayo ilikua inafuatwa nje ya nchi sasa inafanyika nchini ikiwa ni jitihada za serikali katika kuokoa gharma za matibabu ya nje ya nchi.
  Aidha Prof. Museru amesema kuwa hadi kufikia Januari 2017 MNH itaanza kufanya upasuaji na kupandikiza vifaa vya usikivu ikiwa ni huduma iliyokamilika bila ya kwenda nje ya nchi hivyo kupelekea kupunguza gharama zaidi na kusogeza huduma karibu.
  “Hapa tulipofikia sio mwisho wa kutoa hudum hii , tunataka kufikia Januari 2017 tuwe tunafanya upasuaji kabla ya kupandikiza vifaa vya usikivu ikiwa ni huduma kamili na tutakuwa tumefikia baadhi ya malengo tuliyojiweka mpaka kufikia muda huo” alisema Prof. Museru
  Aidha Prof. Museru amesema kuwa Serikali ilianza jitihada  za kuileta huduma hii nchini miaka mitatu iliyopita kwa kushirikiana na kampuni ya kuuza vifaa vya kupandikiza vifaa vya usikivu ya Medel kutoka nchini Misri.
  Kwa upande wa Mzazi wa mtoto aliyepandikizwa kifaa cha usikivu Angel Ibrahimu (4) mkazi wa Mbeya amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa jitihada zake za kufanikisha huduma hiyo kwa mtoto wake kwani lilikua tatizo ambalo hakuweeza kulitatua kwa uwezo wake.
  Katika ufunguzi wa huduma hiyo ambayo itakua endelevu nchini imepandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 16 ambao wapepunguza gharama ya kwenda nje ya nchi takribani shilingi milioni 300 ambazo zitaenda kwenye huduma nyingine za maendeleo ya jamii.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika leo jijini  Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
   Mkurugenzi wa kampuni inayotoa huduma na kuuza vifaa vya usikivu ya Medel Bw. Mohamed Disouky wa kwanza kushoto akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wa pili kulia jinsi huduma hiyo inavyotolewa wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
  Baadhi ya wazazi wa watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa katika foleni ya kusubiri huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

  0 0
 • 11/06/16--03:11: KIBAJAJI AKICHANGIA BUNGENI

 • 0 0

  Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva) Ommy Dimpoz na Alikiba wanakualika kuangalia video ya wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la KAJIANDAE. ucheki hapo chini.

older | 1 | .... | 1418 | 1419 | (Page 1420) | 1421 | 1422 | .... | 3270 | newer