Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1408 | 1409 | (Page 1410) | 1411 | 1412 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Nteghenjwa Hosseah - Longido 

  Wananchi wa Kijiji cha Orgirah Kilichopo Kata ya Mundarara Tarafa ya Engarenaibor Wilayani Longido wamelazimika kutumia nguvu zao binafsi kujenga daraja la chini kwa ajili lengo la kuunganisha mawasiliano ya barabara kati ya kata hiyo na kata ya Gelai.

  Aidha wamelalamikia kero ya maji tangu mwaka 2013 hadi leo hii hakuna maji yanayotoka kwenye mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) unaolenga kusaidia vijiji vitano kwenye kata hiyo.

  Wakiongea na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye anaendelea na ziara yake kwenye wilaya hiyo jana, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Orgirah, Mathayo Laizer alisema mradi huo wa daraja ni muhimu kwao kwani unafungua fursa za kimaendeleo katika kata mbili za Mundarara na Gelai.

  Alisema mradi ulianza mwaka jana na walipata michango mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambayo ilitoa Sh. 400,000, Ofisi ya Mkurugenzi Sh, 640,000 na wananchi walichanga Sh, milioni 5.3 lakini ili waweze kukamilisha ujenzi wa daraja hilo wanahitaji mifuko ya saruji 135 pamoja na ndono za kuweka kingo pembeni ya daraja hilo zenye thamani ya Sh milioni 2.9
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akimkabdihi Mkuu wa Shule ya Sekondari  Engaranaibo  Mwl. Petro Sabatho Tsh 500,000 kwa ajili ya  kuchangia ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule hiyo wakati wa ziara yake inayoendelea katika Wilaya ya Longido.

     Hili ndilo daraja ambalo wananchi wa Kata ya Mundarara wamejitolea fedha na nguvu zao kuhakikisha ujenzi wa daraja unakamilika na kufanya barabara zinazounganisha vijiji vyao kupitika kipindi chote cha mwaka.

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyeko kwenye mtaro) akishiriki ujenzi wa daraja la chini linalojengwa na wananchi wa Mundarara.

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akihamasisha wananchi waendelee kuchangia ujenzi wa daraja la Mundarara ili liweze kukamilika kwa wakati.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0  0 0
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu watumie nyumba za ibada kuhubiri uislamu na misingi yake.

  Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Oktoba 28, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Nunge mjini Dodoma. Amesema dini ya Kiislam inafundisha kwamba sala ndiyo msingi mkubwa unaopaswa kufuatwa na kila muumini hivyo ni lazima wafanye ibada kwa wakati.

  “Nasisitiza kwamba wote tutumie muda wetu vizuri pamoja na mambo mengine tufanye ibada kwani dini inatuekeza kuwa sala ndiyo msingi mkubwa kwenye Uislamu. Tunayo kazi ya kuimarisha misingi ya dini kwa kutumia nyumba za ibada,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema Waislamu wana jukumu la kufundisha watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema.

  “Dini inajenga maadili mema kwa mtoto na hata mtu mzima. Pia dini inajenga misingi ya uvumilivu na inamuwezesha mtu kumtambua Mwenyezi Mungu. “Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kidini ili wakikua waweze kuiendeleza kwa vizazi vijavyo,” amesema.

  Waziri Mkuu ambaye ametumia fursa hiyo kujitambulisha kwa waumini wenzake wa mkoa wa Dodoma baada kuhamia rasmi, ameahidi kutoa ushirikiano kwao na pia amewaomba wampe ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

  “Nimekuja kujitambulisha. Mimi ni kijana wenu, ndugu yenu. Nimekuja Dodoma rasmi nyumbani na kikazi. Naomba mnipokee na naamini katika kipindi chote nitakachokuwa hapa nitapata ushirikiano nanyi na pia nitawapa ushirikiano,” amesema.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwaomba waumini hao wawaombee dua wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajia kuanza mitihani ya kuhitimu Novemba Mosi, mwaka huu ili waweze kufaulu.

  Waziri Mkuu amewaomba waumini hao waendelea kuwaombea viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao na kufikia malengo yanayotarajiwa na wananchi.

  Aidha, Waziri Mkuu amechangia sh. milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ujenzi wa zahanati katika msikiti huo. Miradi inayojengwa na waumini wa msikiti huo kwa sasa ni zahanati, madarasa ya shule ya awali na shule ya ufundi.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba na Sheikh Shabaan Kitila baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam baada ya Sala ya Ijumaa kwenye msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Dua ya kuwaombea wanafunzi wote wa Tanzania wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Nne ili wafanye vizuri akiwa katika Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa ziara ya kibinafsi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa ziara ya kibinafsi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi iliyotolewa na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa Zanzibar.


  0 0

  Kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa A.Mussa, (alietangulia) akikagua ujenzi unaoendelea wa kituo cha Polisi Mkuranga, huku akiwa ameongozana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Bonaveture Mshongi (katikati), pamoja na viongozi wengine wa Jeshi la Polisi toka Makao Makuu alioongozana nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao katika mkoa wa Pwani, jana.
  Kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa A.Mussa, akizungumza na maafisa watendaji kutoka wilaya ya Mkuranga pamoja na Waalimu wa shule ya msingi ya Kimanzichana, wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao katika mkoani Pwani, jana. (Picha zote na Jeremiah Mbuge – Jeshi la Polisi).

  0 0

  Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeli, kudhihaki, kukatisha tamaa, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania. 

  Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania. 

  Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na kuichafua taswira ya nchi yetu. 

  Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni Watanzania. Je ni tamaa ya madaraka tu au mengine? Hakuna anayepinga ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema kwa nchi. 

  Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita ya tathmini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015. 

  Ndugu Christopher Ole Sendeka, Msemaji wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa akizungumza kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo tarehe 28/10/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam. 


  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Ileje

  MKUU wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude ameongoza kamati ya ulinzi na usalama kwenda kufukia mfereji uliochimbwa na wananchi wa kata ya Bupigu kuchepusha maji kutoka mto Kalembo kwenda mashambani.

  DC Mkude amefanya zoezi hilo ikiwa ni siku chache tangu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Janauary Makamba ,kuagiza kusitishwa na kufukiwa kwa mfereji huo.

  wakati wa zoezi hilo la ufukiaji Dc Mkude alimuagiza mkurugenzi wa wilaya hiyo Haji Mnasi kupeleka wataalamu wa umwagiliaji kutoa elimu juu ya ujenzi wa Skim ambazo aziathiri Mazingira.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wilaya hiyo amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kujichukulia maamuzi wenyewe kwenye vyanzo vya maji na misitu ya Serikali.

  Ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Bupigu kuwa wavumilivu kwani serikali hii ni ya Wanyonge hivyo wanafanya mpango wa kuwawezesha kwa namna nyingine kumudu kilimo cha umwagiliaji kupitia Rasilimali walizonazo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude (kulia) na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Haji Mnasi wakishiriki zoezi la kuziba mfereji uliochimbwa kuchepusha Mto Kalembo na mmoja wa Wakazi wa kata ya Bupigu kijiji cha Bungu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi, akiwa na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo kuziba maji katika eneo lilichimbwa na mmoja wa wakazi wa Kata ya Bupigu kwa lengo la kuchepusha mto Kalembo kwenda kwenye Mashamba .
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje ,Haji Mnasi, akivuta maji yaliyowekwa kuziba mto Kalembo uende sehemu nyingine hali inayohatarisha mazingira katika eneo hilo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ileje ,Joseph Mkude akizungumza jambo na mkurugenzi wa wilaya hiyo Adji Mnasi, juu ya atahari za mfereji huo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi ya Finland kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya nishati katika kipindi hiki wakati ambapo taifa la Tanzania linaelekea katika uchumi wa viwanda.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem.

  Makamu wa Rais amesema kuwa mkakati wa sasa wa Serikali ni kuhakikisha taifa linajitosheleza ipasavyo katika nishati ya umeme hatua ambayo itasaidia wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali Duniani kuja kuwekeza nchini kutokana na nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika utakaotumika katika viwanda vitakavyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.

  Makamu wa Rais pia ameishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na kuwezesha makundi mbalimbali ya kijamii hapa nchini ikiwemo ya wanawake,yatima na vijana.Makamu wa Rais amemweleza Balozi huyo kuwa kwa sasa jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya Tano zimeelekezwa katika uimarishaji wa miundombinu ikiwemo reli, bandari na barabara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kote nchini.

  Kwa upande wake, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi ya Finland itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia uimarishaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kuwezesha wajasiriamali ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

  Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Finland yamewezesha Watanzania zaidi ya 500 kuishi nchini humo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kimasomo.Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem aliongozana na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto) masuala mbali mbali ya uwekezaji,elimu na uwezeshaji Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu watumie nyumba za ibada kuhubiri uislamu na misingi yake.

  Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Oktoba 28, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Nunge mjini Dodoma.

  Amesema dini ya Kiislam inafundisha kwamba sala ndiyo msingi mkubwa unaopaswa kufuatwa na kila muumini hivyo ni lazima wafanye ibada kwa wakati.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016.

  “Nasisitiza kwamba wote tutumie muda wetu vizuri pamoja na mambo mengine tufanye ibada kwani dini inatuekeza kuwa sala ndiyo msingi mkubwa kwenye Uislamu. Tunayo kazi ya kuimarisha misingi ya dini kwa kutumia nyumba za ibada,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema Waislamu wana jukumu la kufundisha watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema.

  “Dini inajenga maadili mema kwa mtoto na hata mtu mzima. Pia dini inajenga misingi ya uvumilivu na inamuwezesha mtu kumtambua Mwenyezi Mungu. “Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kidini ili wakikua waweze kuiendeleza kwa vizazi vijavyo,” amesema.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Dua ya kuwaombea wanafunzi wote wa Tanzania wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Nne ili wafanye vizuri akiwa katika Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016.

  Waziri Mkuu ambaye ametumia fursa hiyo kujitambulisha kwa waumini wenzake wa mkoa wa Dodoma baada kuhamia rasmi, ameahidi kutoa ushirikiano kwao na pia amewaomba wampe ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

  “Nimekuja kujitambulisha. Mimi ni kijana wenu, ndugu yenu. Nimekuja Dodoma rasmi  nyumbani na  kikazi. Naomba mnipokee na naamini katika kipindi chote nitakachokuwa hapa nitapata ushirikiano nanyi na pia nitawapa ushirikiano,” amesema.
  Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes, Anil Tambay (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuelezea juu ya maadhimisho ya miaka 40 kwa kutoa huduma bure za uzazi wa mpango na uchunguzi wa kansa ya mlango wa kizazi kama maadhimisho ya miaka 40 ya Marie Stopes International. Maadhimisho hayo yanatarajia kufanyika Novemba 2-4, 2016 kwenye kliniki na hospitali zake zote nchini Tanzania.
  Marie Stopes Tanzania itatoa huduma za uzazi wa mpango na uchunguzi wa kansa ya mlango wa kizazi bure kuanzia tarehe 2 hadi 4 Novemba kwenye kliniki na hospitali zake zote nchini kama sehemu ya kuadhimisha miaka 40 ya Marie Stopes International, na hivyo kuongeza idadi ya akina mama ambao wamewezeshwa kuwa na maamuzi juu ya mustakabali wa maisha yao wa kupata watoto kwa utashi na si kwa kubahatisha.

  Marie Stopes Tanzania ni sehemu ya Marie Stopes International, shirika la kimataifa linalojihusisha na kutoa huduma za afya ya uzazi na lilianzishwa mwaka 1976. Katika wiki inayoanzia Oktoba 31, tutakuwa tuaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Maries Stopes International.


  0 0  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco,  Mtukufu Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa ziara ya kibinafsi.
  Mfalme wa Morocco Mtukufu  Mohammed VI(kulia) akisalimiana na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga mara baada ya kuswalisha Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa ziara ya kibinafsi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi iliyotolewa na Mfalme wa Morocco  Mtukufu Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco Mtukufu  Mohammed VI, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka nje ya Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco Mtukufu a
  Mohammed VI, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja. Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa ziara ya kibinafsi.

  0 0

  WE ARE THE MOST AFFORDABLE AND RELIABLE SHIPPING AGENT IN U.K

   

        CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 850 (TILBURY/ SHERNESS PORTS)

  CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 750 (SOUTHAMPTON/ NEWCASTLE PORT)

  4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 910 (SOUTHAMPTON PORT)

  4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 945 (NEWCASTLE PORT)

  4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 930 (TILBURY/ SHEERNES PORTS)
          40’ CONTAINER TO DAR £ 1750
  40’ CONTAINER TO MOMBASA £ 1750 HC
  40’ CONTAINER TO ZANZIBAR £ 2300
  20’ CONTAINER TO DAR £ 1220
  20’ CONTAINER TO MOMBASA £ 1220
  20’ CONTAINER TO ZNZ FROM £ 1600
          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2650(TILBURY PORT)
          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2400(SOUTHAMPTON)

          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2450(NEWCASTLE)

          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM 2612.50(IMMINGHAM PORTS)
          TRACTORUNITS(KICHWA)TODARORMOMBASAFROM£2612.50(KILLINGHAM)

          ALSOWECAN      ARRANGEPRE SHIPMENTINSPECTIONFORYOUTOAVOIDINCONVINIENCES.

  ·       GOOD NEWS FOR AIR CARGO CUSTOMERS FOR NAIROBI,MOMBASA AND DAR ES SALAAM!!!!!.

  ·         NOW WE SHIP AIR CARGO FROM CHINA,US, AMSTERDAM,UK AND TURKEY TO EAST AFRICA AT A VERY COMPETITIVE RATES

  ·         WE SHIP AIR CARGO TO NAIROBI FOR ONLY £2(EXCLUDING CLEARANCE).

  ·         WE SHIP AIR CARGO TO MOMBASAFOR ONLY £2.50(EXCLUDING CLEARANCE)

  ·         WE SHIP AIR CARGO TO DAR ES SALAAM FOR ONLY £2.50(EXCLUDING CLEARANCE)

  ·         WE SHIP AIR CARGO TO DAR ES SALAAM WITH CLEARANCE ONLY FOR £ 5

  FORMOREDETAILSPLEASE  CONTACTUSONOURCONTACTSBELOW:- EXTENDED SERVICES LIMITED, CLIPPER HOUSE, TILBURY FREEPORT, TILBURY, ESSEX, RM18 7SG Tel:+441375767890, mobile:+447438145815,EMAIL:info@extendedserviceslimited.co.uk,www.extendedserviceslimited.co.uk


  0 0


  0 0
  0 0


  SIMU.TV: Wamiliki wa vyombo vya usafiri nchini wameshauriwa kuvikaguia vyombo vyao kabla ya kuanza safari ili kupunguza ajali za barabarani nchini. https://youtu.be/Ryy3Qre48-U

  SIMU.TV: Benki kuu ya Tanzania BOT imetangaza kuchukua umiliki wa benki ya Twiga kutokana na benki hiyo kukosa mtaji wa kutosha. https://youtu.be/1BZ6Y58mY0U

  SIMU.TV: Chama cha mapinduzi CCM kimeridhishwa na utendaji wa rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kuzuia mianya ya rushwa na kuimarisha nidhamu ya utendaji kwa watumishi wa umma. https://youtu.be/Nu38NtgkSq0

  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amemaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya mafundi gereji wa Tegeta na mwekezaji uliodumu kwa miaka mingi wakigombania ardhi. https://youtu.be/lZAdPDHk-Qw

  SIMU.TV: Vijana wengi hususani waishio mijini wanatarajia kunufaika na mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali ili kuweza kujikomboa kiuchumi. https://youtu.be/k4hpPr2cZRI

  SIMU.TV: Wananchi wa kata ya Mundarara wilayani Longido wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa barabara na daraja jambo linalowafanya kushindwa kufika vijiji vingine kipindi cha mvua. https://youtu.be/MhQy__3pens

  SIMU.TV: Serikali imepongeza juhudi zinazochukuliwa na kampuni ya simu Tanzania ili kuboresha utendaji wa kampuni pamoja na kukidhi utoaji wa huduma bora. https://youtu.be/3XpPdqo8Rzs

  SIMU.TV: Wananchi wa kitongoji cha Mnazi Mmoja katika mji wa Kilwa Masoko wamefika katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Kilwa ili kujua hatma ya fidia zao ili waweze kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kilwa. https://youtu.be/sDYHG-nuuH8

  SIMU.TV: Klabu ya Azam Fc imeendelea kupeleka machungu kwa klabu ya Kagera Sugar baada ya kuifunga mabao mawili kwa moja kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara. https://youtu.be/rO5o4yM3g44

  SIMU.TV: Serikali imeshauriwa kurudisha mitaala ya michezo katika shule za msingi na sekondari ili kuwafanya vijana kuwa na hamasa ya michezo. https://youtu.be/7k3DhYoQsu4

  SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Tarime amekabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya Forodhani Cargo inayojishughulisha na uvushaji wa mizogo katika bandari ya Sirari. https://youtu.be/crO8-4dYpaQ

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza na wakulima wa Bonde la Mto Katengela Kijiji cha Kinonko Wilayani humo wakati wa ziara yake.
   Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akilima moja ya shamba la mkulima.
  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaomba wakulima wa Bonde la Mto Katengela Kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko kulima mazao yao kwa misimu miwili ya Kiangazi na masika kitaalamu zaidi na kujiunga kwenye vyama vya ushirika.

  Ndagala pia amewataka wakulima hao kuacha tabia ya kuuza mazao yote kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu inayoweza kupelekea maeneo mengi kukosa chakula.
  Akizungumza na wakulima wa Bonde la Mto katengera jana wakati wa ziara yake , vijiji vya Kinonko,Nyamibuye na Rumashi,  Ndagala alisema wakulima wengi wamekuwa na tabia ya kuuza mazao yote na kupelekea kubaki wakilia njaa baada ya mazao yao waliyo lima kuisha ,pia wakulima wanatakiwa kuunda vikindi vya ushirika vitakavyo wasaidia kupata mikopo,pembejeo na masoko yatakayo wasaidia kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu.
  Alisema Wakulima wakiweza kulima misimu yote miwili ya Kiangazi na masika bonde hilo linauwezo wa kuhidumia wananchi wote wa Kakonko kutokana na mkulima mmoja katika hekali moja anauwezo wa kuzalisha gunia tatu za mpunga kwa msimu mmoja wa mavuno na hali inayo weza kuikomboa wilaya hiyo isikumbwe na janga la njaa.
  Aidha Ndagala amewaomba maafisa kilimo wa Wilaya hiyo kuwawezesha wakulima kulima kwa misimu miwili na kuwapa mbinu za kulima kitaalamu kwa kutumia pembejeo zinazotolewa na Serikali ilikuweza kupata Mazao mengi na  kuweka tahadhali kutokana na hali ya hewa inayo weza kupelekea ukosefu wa mvua.
  "Niwaombe wananchi kwa mwaka huu mlime mazao yanayo weza kustahimili ukame kama Vile mihogo, mtama na viazi na yale yanayo stawi haraka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi yaliyojitokeza hali inaweza kusababisha mwaka huu chakula kika kosekana kabisa pia mjenge tabia ya kuhifadhi chakula msikiuze chote tusije tukaanza kuomba misaada wakati uwezo wa kuhifadhi chakula tynao",alisema Ndagala.
  Kwa upande wake Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,Muhdin Alfani alisema  bonde hilo lina zaidi ya kilomita 29 na linawakulima 310 na mradi wa kukamilisha ujenzi wa bonde hilo la umwagiliaji ni shilingi milioni 312 na kila hekari moja inazalisha gunia 18 kwa msimu mmoja wa kilimo.
  Alisema lengo la Halmashauri kuanzisha mradi huo ni kuwasaidia wananchi wa Wilaya hiyo kulima na kupata mazao ya kutosha yatakayo wasaidia kuilisha wilaya na Nchi jirani ya Burundi ambayo inategemea chakula kingi kutoka kwa Watanzania katika masoko ya ujirani mwema na kuweza kuiongezea serikali pato la taifa.
  Nao baadhi ya wakulima wa bonde hilo,Issa Masumo na Shedrack Milembe  wameiomba Halmashauri hiyo kuwawezesha kupata masoko na kupangiwa bei maalumu itakayo wasaidia kuepukana na unyanyasaji wa Wafanya biashara wanaokuja kununua mpunga na kuwapunja wakulima na kukosa haki yao ya msingi wao kama wakulima.

  0 0

  Wachezaji wa Azam Fc wakimpongeza Nahodha wao John Bocco dakika ya 86 baada ya kuwapachikia bao la ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Vodacom VPL leo kwenye Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini. Bao hilo limeiwezesha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam kuibuka na pointi  tatu muhimu  baada ya kuinyuka Kagera Sugar mabao 3-2 katika mchezo ulifanyika leo Mkoani Kagera.Kikosi cha Azam Fc kilichoanza dhidi ya Kagera Sugar leo kwenye Uwanja wa Kaitaba


  Timu zilivyokuwa zinaingia Uwanjani
  Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar.
older | 1 | .... | 1408 | 1409 | (Page 1410) | 1411 | 1412 | .... | 3283 | newer