Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1398 | 1399 | (Page 1400) | 1401 | 1402 | .... | 3353 | newer

  0 0


  SIMU.TV: Watu wanne wamefariki dunia mkoani Mbeya baada ya gari aina ya Coaster walilokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka. https://youtu.be/KVVqFN41Dbc

  SIMU.TV: Watu watatu wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa mkoani Tabora baada ya gari aina ya Noah walilokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu na kupinduka.https://youtu.be/XLQAMrmU_9Y

  SIMU.TV: Tanzania imependekeza umoja wa mataifa kufanya mageuzi makubwa kwa kulipa bara la Afrika viti viwili vya kudumu na vyenye uwezo wa kura ya turufu.https://youtu.be/k_PSKEhzA48

  SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepokea msaada wa mabati kwa ajili ya marekebisho ya hospitali ya wilaya ya Ruangwa. https://youtu.be/h5XcP5CVXEE

  SIMU.TV: Baraza la vijana wa chama cha demokrasia na Maendeleo BAVICHA limemuomba waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi kutoa ufafanuzi juu ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. https://youtu.be/CQXFZ8DC4Iw

  SIMU.TV: Waziri wa maliasili na utalii amebadilisha mfumo wa utendeaji wa bodi ya chuo cha utalii cha taifa kampasi ya Dar es salaam ili kuimarisha utendaji katika chuo hicho.https://youtu.be/PvzzNQuQaSo

  SIMU.TV: Mkazi mmoja wa Goba jijini Dar es Salaam ametoa shukrani kwa kituo cha Channel ten kwa kumwezesha mtoto wake kuchangiwa msaada wa kuokoa maisha yake baada ya kupata ajali. https://youtu.be/Vms40aqTp-c

  SIMU.TV: Wafanyabiashara mkoani Shinyanga wametakiwa kujitokeza kusajili biashara zao kwa wakala wa usajili na leseni BRELA ili kuongeza thamani ya huduma zao.https://youtu.be/rSY4lcIU4Vo

  SIMU.TV: Siku chache baada ya kuanza kwa minada ya zao la korosho mkoani Mtwara wakulima wameonekana kuendelea kunufaika baada ya bei kuongeza kwa mara nyingine.https://youtu.be/0aj7YVoQM64

  SIMU.TV: Serikali mkoani Geita imewataka wafanyabiasha wa viwanda na kilimo kutumia fursa zilizopo kukuza biashara zao badala ya kusubiri wageni kuja kuwekeza.https://youtu.be/_vW-ix4Dyzc

  SIMU.TV: Bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya timu ya Toto Afrka ya jijini Mwanza.https://youtu.be/CJD6jXYI6K0

  SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limempiga marufuku kocha Halfan Ngassa kuiongoza na  kuifundisha Toto Afrika kutokana na kutokidhi vigezo vya kuwa kocha.https://youtu.be/5F6PMRYFNfE

  SIMU.TV: Kocha mkuu wa Arsenal Arsene Wenger amesema hakuwai kufikiria kumuuza mchezaji wake Theo Walcoti japo msimu uliopita hakufanya vizuri kama msimu huu.https://youtu.be/NdpKOceL3qA

  0 0

  Kocha Khalfan Ngassa  (pichani) amekuwa kwenye benchi la timu ya mpira wa miguu ya Toto Africans ya Mwanza akiwa kocha msaidizi kwa mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini.

  Khalfan Ngassa aliongoza timu kwenye mchezo Na. 62 dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 7, 2016; mchezo Na. 67 dhidi ya Mbao FC uliofanyika Oktoba 12, 2016 na Mchezo Na. 79 dhidi ya Majimaji ya Songea uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu. 

  Kwa mujibu wa Kanuni ya 72 (3) (5) ya Ligi Kuu, Kocha Mkuu anatakiwa kuwa na Leseni ya chini kuanzia Daraja B ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) na Daraja C kwa Kocha Msaidizi pia kutoka CAF.

  Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa Kocha Khalfan Ngassa  hana leseni yoyote kati ya hizo, hivyo hastahili kukaa kwenye benchi la timu ya Toto Africans kama kocha mkuu au kocha msaidizi.

  Kitendo kinachofanywa na Toto Africans ni ukikwaji wa kanuni na ni vema uongozi wa Toto ukamwondoa Khalfan Ngassa kwenye benchi ili kuepuka adhabu. Kipendele cha (7) cha kanuni hiyo ya 72, inaelekeza adhabu kuwa inaweza kutozwa si chini ya Sh 500,000 (shilingi laki tano).

  Pia tunazikumbusha klabu zote kuwa kuanzia msimu ujao wa 2017/18 wa Ligi Kuu ya Vodacom, kocha anayestahili kukaa kwenye benchi ni yule mwenye leseni Daraja A kwa nafasi ya Kocha Mkuu na angalau Leseni Daraja B kwa kocha msaidizi..
  0 0

   MKUU wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE), Prof. William Anangisye (kushoto) akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Bw. David Keasi kwenye Mahafali ya Tisa ya Shule ya St. Thomas More Machrina High School iliyopo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Mwanzilishi wa shule hiyo Prof.Justinian Galabawa (katikati) na Mkuu wa Shule, Bw. Constantine Kirwanda.
  Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Nne wakiimba wimbo wa shule kwenye Mahafali ya Tisa ya Shule ya St. Thomas More Machrina High School iliyopo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kuna taarifa inasambazwa katika mitandano mbalimbali ya kijamii  leo hii ikidaiwa imetolewa na kitengo cha Mawasiliano, IKULU
  Kama inavyoelezwa hapo juu, taarifa hiyo si ya ukweli. Mnaombwa muipuuze. Ni taarifa iliotengenezwa na baadhi ya watu wenye nia ovu ya kupotosha ukweli. Hivyo mnaombwa kuipuuza.

  0 0

  Charity organisation ya You Touch Africa ambayo iko chini ya Father Aarbo Lekule, Mtanzania na ambaye ni Paroko wa Parokia ya Kidbrooke London, wametoa misaada ya computers  na School  uniforms ambazo zitagawiwa kwenye shule kadhaa zenye watoto ambao wana uhaba wa uniforms na nguo za kujikinga na baridi.
  Father Lekule amekua akizunguka barani Ulaya kuchangisha fedha na misaada mbali mbali kwa ajili ya shule na wasiojiweza nyumbani.
  Misaada hiyo imekabidhiwa rasmi leo kwa kampuni ya usafirishaji ya KC GLOBAL LINKS LTD ambayo pia inamilikiwa na Watanzania waishio UK ili waisafirishe kwa ndege kwenda KIA Tanzania
  Kama mchango wao, KC GLOBAL LINKS LTD wamechangia usafirishaji kwa kusafirisha kwa bei nusu. 
  KUTOA NI MOYO, WALA SIO UTAJIRI. 

  KC GLOBAL LINKS LTD, 
  SUITE 2 CLIPPER HOUSE, TILBURY FREEPORT, TILBURY ESSEX, RM18 7SG
  TEL; 01375 85 85 25  COMPANY REG; 09182321, VAT REG; 199156166
   Father Aarbo Lekule, Mtanzania na ambaye ni Paroko wa Parokia ya Kidbrooke London, akiwa na wadau wa paroko hiyo.
   Father Aarbo Lekule Paroko wa Parokia ya Kidbrooke London katika misa
   Father Aarbo Lekule Paroko wa Parokia ya Kidbrooke London akiongea na waamini na kuomba misaada kwa watoto wa Tanzania ambao wana uhaba wa uniforms na nguo za kujikinga na baridi.
  Taarifa za juhudi za Father Aarbo Lekule Paroko 
  zimekuwa zikiripotiwa sana magazetini

  0 0

  Wadau wote mnakaribishwa katika maonesho ya sanaa za katuni (Cartoon) yatakayo funguliwa rasmi kesho tar 20 saa 11 jioni, Masoud Kipanya atashirikisha historia ya maisha yake katika sanaa, na tar 21 saa 1 hadi saa 3 usiku LUMUMBA THEATRE watafanya onesho la Muziki wa asili, Ngomba za asili na Sarakazi, katika ukumbi wa kisasa wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar.

  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam.
  6
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini  ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akifungua kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani.Kushoto ni  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam.
  7
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kushoto  ni Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam.(
  8
  Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Mossi Ndozero, akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo, kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, Dar es Salaam.
  9
  Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Hamza Kasongo(kulia), akichangia mada wakati wa kujadili  taarifa ya maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo.Kushoto ni mjumbe wa baraza hilo Henry Bantu. Kikao hicho  kilifanyika katika ukumbi wa wizara, Dar es Salaam.

  (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu kiitwacho A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake,Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely pamoja na Balozi wa Uswis katika Afrika Mashariki Mhe. Arthur Mattli (kushoto) muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu kiitwacho A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake, kushoto ni Balozi wa Uswis katika Afrika Mashariki Mhe. Arthur Mattli,Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely , Balozi wa Uswis katika Afrika Mashariki Mhe. Arthur Mattli (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano Bi. Romana Tedeschi na Maafisa wengine muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu kiitwacho A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake,Ikulu jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipokea kitabu cha A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake kutoka kwa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu hicho, Ikulu jijini Dar es Salaam
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akifunua ukurasa wa kitabu cha A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake kama ishara ya kukizindua kitabu hicho mbele ya Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely , Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Mwaka huu Swaziland na Tanzania inatimiza miaka 50 ya mahusiano ya kidiplomasia baina baina ya nchi hizi mbili. Katika kuadhimisha shughuli hii, Ubalozi wa Swaziland umezindua kitabu kinaitwa A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake. Kitabu hiki kimezinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na. Eliphace Marwa – Maelezo 

  Watanzania watakiwa kuongeza thamani na uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini.

  WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka watanzania kuongeza thamani ya bidhaa na uzalishaji ili kuongeza fursa za ajira.

  Mwijage ameyasema hayo wakati akizungumza na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN zinazoratibiwa na Shirika la uhusiano wa kimataifa laJapan (JICA).

  “Tuko hapa hii leo kushuhudia sherehe za utoaji wa tuzo katika sekta ya viwanda ambayo ni matunda ya dhana za KAIZEN kwani tuzo hizi zinatolewa kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika kutekeleza mbinu za KAIZEN ili kuweza kutoa changamoto kwa makampuni mengine” alisema Mh. Mwijage

  Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa JICA ofisi ya Tanzania Bw. Toshio Nagase aliipongeza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na kitengo cha KAIZEN Tanzania kwa kuandaa sherehe yenye mafanikio kwa mara nyingine kufuatia ili iliyofanyika mwaka jana.

  “Baada ya uzinduzi wa mpango wa miaka mitano, sisi sote tumetambua umuhimu wa kukuza viwanda ili kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa Tanzania”, alisema Bw. Toshio

  Aidha Bw. Toshio alibainisha baadhi ya maeneo ambayo KAIZEN imefanikiwa kuwa ni pamoja na kuhakikisha ubora wa bidhaa na kubadilisha tabia pamoja na kutoa motisha kwa wafanyakazi.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi amesema kuwa anaamini kuitangaza KAIZEN nchini Tanzania ni jambo la muhimu ili kutengeneza viwanda vyenye ushindani na kufanikisha lengo la kukuza viwanda kuelekea mwaka 2025.

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam. 
  Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi akielezea mikakati ya KAIZEN kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam. 
  Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu toka kushoto waliokaa) pamoja na Balozi wa Japan nchini na Mwakilishi wa JICA Tanzania wakiwa katia picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi walioshinda tuzo wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam. 
  Picha na Eliphace Marwa – Maelezo 


  0 0  Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila akitoa Hotuba katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji (UN-HABITAT III, Quito – Ecuador)
  Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila baada ya kutoa Hotuba, akipongezwa na Profesa Anna Tibaijuka; Mbunge wa Muleba Kusini, wengine ni Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Sada Sekiete- Afisa Mipango Miji Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.  
  Katibu Mkuu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Sada Sekiete Afisa Mipango Miji Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika picha ya pamoja na viongozi wa UN-HABITAT Africa Region kutoka Nairobi
  Wajumbe kutoka Tanzania, kutoka kushoto ni; Katibu Mkuu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, Nehemia Mchechu Mkurugenzi Mkuu katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Fatma chullo Mkurugenzi wa sheria wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifuatilia Mkutano wa wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji (UN-HABITAT III, Quito – Ecuador)

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano – Wizara ya Ardhi 

  0 0

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali tayari imeshalipa sh. bilioni 722.7 kati ya sh. bilioni 964.2 za madeni ya michango ya jumla ambayo Serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

  Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 20, 2016) wakati akifungua Mkutano wa Sita wa wadau wa NSSF ulioanza leo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Arusha na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 600.

  Amesema sekta hiyo imekua kwa asilimia 15 kutoka sh. trilioni 8.9 mwaka 2015 hadi kufikia sh. trilioni 10.2 mwaka 2016. “Hadi kufikia Juni 2016, takwimu zinaonesha idadi ya wanachama imeongezeka na kufikia milioni 2.1. Rasilmali za mifuko zimefikia shilingi trilioni 10.28 na mafao yaliyolipwa kwa kipindi cha mwaka kinachoishia Juni 2016 ni shillingi trilioni 2.93. Michango ya wanachama kwa mwaka ni shilingi trilioni 2.15 uwekezaji katika nyanja mbalimbali umefikia kiasi cha shilingi trilioni 9.29,” ameongeza.

  Waziri Mkuu pia amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara awaandikie barua waajiri wote wanaodaiwa na shirika hilo na kuwataka wawasilishe fedha wanayodaiwa mara moja na wale ambao hawatalipa ndani muda utakaowekwa wafikishwe mahakamani na yeye apewe taarifa.

  “Kumekuwepo na changamoto ya muda mrefu ya baadhi ya waajiri kutolipa michango kwa wakati hali inayoleta usumbufu mkubwa kwa wanachama hasa wanapofikia muda wa kustaafu. Suala hili halikubaliki, hivyo natoa maelekezo kwa waajiri wote nchini waheshimu sheria na wawasilishe michango yao kwa wakati,” amesisitiza.

  Mbali ya kuwabana waajiri, Waziri Mkuu pia amewataka wanunuzi wa nyumba za shirika hilo na wapangaji wote wanaodaiwa wakamilishe malipo yao na wasipofanya hivyo ndani ya muda uliopangwa wafikishwe mahakamani.

  “Nimeambiwa pia lipo tatizo la wadaiwa wa nyumba yaani wanunuzi na wapangaji. Suala hili lilitolewa maelekezo na Waziri wa Nchi, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu. Nataka nisisitize kuwa watu wote walionunua nyumba za NSSF na bado hawajakamilisha malipo na wale waliopanga lakini hawalipi kodi wanatakiwa kulipa haraka au wakabidhi nyumba hizo kwa NSSF ziuzwe kwa watu wengine, vinginevyo nao wafikishwe mahakamani.”

  Akizungumzia utendaji wa shirika hilo, Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa shirika hilo na Bodi ya Wadhamini kwa uamuzi wake wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa sukari nchini. Amesema kiwanda kitakachojengwa, kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa Watanzania na hivyo kuongeza wanachama katika mfuko wa NSSF.

  Nimefurahishwa na uamuzi wa NSSF na PPF kuungana ili kukabiliana na tatizo la sukari nchini. Tumeelezwa hapa kuwa mashirika haya yatashirikiana kujenga Kiwanda cha Sukari kitakachozalisha tani 200,000 kwa mwaka. Kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la Mkulazi lililopo mkoani Morogoro,” amesema.

  Mapemaakielezea utendaji wa shirika hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara alisema limeboresha mafao ya wanachama wake kutoka sh. 80,000 hadi sh. 100,000 kwa mwezi.

  Alisema limeanza kufanya upembuzi yakinifu wa kujenga nyumba za watumishi Dodoma ili kuendana na uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma. “Upembuzi bado unaendelea lakini tumeshabaini kuna uwezekano wa kujenga nyumba 200 hadi 300 mkoani Dodoma,” alisema.

  Kuhusu uwekezaji kwenye ujenzi wa Daraja la Mwalimu Nyerere lililopo Kigamboni, Dar es Salaam, Prof. Kahyarara alisema uwekezaji huo unalipa kwa sababu makusanyo ya tozo kwa watumiaji yamefikia asilimia 109. “Tuna uhakika kwamba fedha tulizowekeza zitarudi,” amesisitiza.

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amepokea msaada wa tani 45 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 900 yenye thamani ya sh. milioni 15 kwa ajili ya waathirika wa tetememo la ardhi mkoani Kagera. Amepokea msaada huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Prof. Samuel Wangwe.

  Akiwasilisha msaada huo, Prof. Wangwe alisema wameguswa na tatizo lilitokea mkoani Kagera na wameamua kutoa mchango ili kusaidia juhudi za Serikali kukabiliana na maafa hayo. Pia alisema wamekamilisha ahadi yao ya madawati 6,000 yenye thamani ya sh. milioni 400 ambayo waliitoa awali.

  Waziri Mkuu aliwashukuru kwa misaada hiyo na kuwahakikishia kwamba itafikishwa kwa walengwa.

    
                              
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, OKTOBA 20, 2016.

  0 0

  AFRICA FEDERATION - SECRETARIAT
  Bilal Comprehensive School (BSC) a section of Bilal Muslim Mission of Tanzania marked the Muharram commemoration with majalises for different age groups in the first ashra (12 days) of Muharram 1438 A.H. The commemoration concluded with the annual Juloos (peaceful procession) on Sunday, 16th October 2016. There was a record turnout this time. For more CLICK HERE

  0 0


  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Kongamano la Nne linalohusu sekta ndogo ya mafuta na gesi lililoambatana na maonesho kuhusu sekta hiyo na kukutanisha Wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni zinazojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, Vyuo Vikuu, Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali limeanza kufanyika jijini Dar es Saalaam.

  Kongamano hilo lilifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo ambapo aliwaeleza wadau hao kuwa, usimamizi madhubuti wa sekta ndogo ya gesi na mafuta utaleta mapinduzi makubwa kwenye ukuaji wa viwanda na kuiwezesha Tanzania kuingia kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Katika kongamano hilo linalofanyika kuanzia tarehe 20 – 21 Oktoba, 2016, Dk. Pallangyo alisema kuwa kutokana na kiasi kikubwa cha gesi kilichogunduliwa ambacho ni futi za ujazo trilioni 57.2, kampuni mbalimbali za kigeni zimeanza kujitokeza na kuwekeza katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo gesi imegunduliwa

  Alisema kutokana na uwekezaji katika shughuli za gesi na mafuta, kumekuwepo na mabadiliko ya kiuchumi katika mikoa hiyo kama vile kuongezeka kwa fursa za ajira, malazi na utoaji wa huduma kwa wawekezaji.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) akifugua kongamano la nne linalohusu gesi na mafuta lililoambatana na maonesho , lililokutanisha wadau mbalimbali kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo vikuu, wizara na taasisi za serikali jijini Dar es Salaam. 
  Kutoka kulia; mwakilishi kutoka Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kongamano hilo. 
  Washiriki kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo vikuu, wizara na taasisi za serikali wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kongamano hilo. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya Musomba (kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa shirika hilo katika kufanikisha kongamano hilo. 


  0 0

   Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kufungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza   kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba  20, 2016
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya kupokea tani 45 za saruji  zenye thamani ya shilinigi milioni 15 zilizotolewa na NSSF  kabla ya kufungua  Mkutano wa  Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.


  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii


  Shirikisho la soka nchini TFF limeweka wazi kuwa beki wa kulia wa Yanga Hassan Kessy, aliyetokea Simba ruksa kucheza katika ligi kuu ya vodacom kutokana na  kanuni za ligi hiyo kwa kuwa swala kesi ni madai .  Afred amesema kuwa swala mchezaji huyo aliwezi kumzuia mchezaji huyo kucheza kwakuwa tayari swala hilo lipo katika hatua ya usuluhushu .

  "Lakini ikitokea usuluhishi alijafikiwa maamuzi hivyo kamati itachukua maamuzi kwa mujibu wa kanuni zinavyoeleza na majibu nitakuja kuwapatia"amesema Lucas.  Amesema kuwa Simba katika mkataba wake waliweka kipengele cha kulipa zaidi ya dola 600 kama faini hivyo tunasubiri maamuzi hayo hivyo kesi anapaswa kucheza mpaka hapo kamati itakapo toa maamuzi.

  0 0


  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Missenyi

  KIKOSI kazi cha jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)kutoka makao makuu ya Jeshi kimewasili Mkoani Kagera kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya serekali iliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoana hapa septemba 10 mwaka huu.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Kabambyaile Kata ya Ishozi Wilaya ya Missenyi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu alisema kuwa kikosi hicho kinawataalamu wa fani zote za ujenzi na wamekuja na vifaa vyote vya ujenzi.

  "Hiki kikosi kitafanya kazi kwa masaa 24 yaani watajenga usiku na mchana taasisi zote za umma zilizoathiriwa na tetemeko ikiwa ni pamoja na mashule na zahanati ili watoto waende shule na wagonjwa waendelee kupata matibabu"alisema.Alisema mpaka kufikia july mwakani ujenzi wa miundombinu utakuwa umekamilika kwa robo tatu na aliwataka wananchi wawape ushirikiano maeneo yote watakayopita kujenga miundombinu ya umma.

  Kiongozi wa kikosi hicho Meja Buchadi Kakura alisema kuwa kikosi hicho kimekuja Kagera kusaidia serekali ya Mkoa kurudisha miundombinu yote ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi katika hali yake ya kawaida.

  "Ni vigumu kusema lini tutakamilisha ujenzi ila sisi tutafanya kazi usiku na mchana ili ujenzi huu ukamilike ndani ya muda mfupi"Alisema Meja Kakura.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu(mwenye Suti)akisikiliza maelezo juu ya kikosi kazi cha askari waliokuja kujenga miundo mbinu ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi


  Kikosi kazi cha askari wa Jeshi la wananchi(JWTZ)kutokaakao makuu ya Jeshi kilichowasili Mkoani Kagera kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya umma iliyoathirika na tetemeko la ardhi.

  Greda la Jeshi likiandaa eneo linalotarajia kujengwa kituo cha afya kituo cha afya cha Ishozi kijiji cha Kyabaile.
   

  0 0

  Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

  SHIRIKISHO la soka nchini TFF limesema kuwa ligi kuu ya Wanawake inatarajia kuanza Novemba mosi mwaka huu katika viwanja mbalimbali nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Ofisa habari wa TFF,Alfred Lucas, amesema kuwa licha ya kukamilika kwa taratibu zote bado kuna tatizo la fedha kutokana kukosa kwa mdhamini wa ligi hiyo.

  Lucas amesema kuwa timu zote zipo tayari licha yakuwepo kwa malalmiko kadha na rufaa za usajili kwa wachezaji kwa baadhi ya timu kuzilalamikia timu zingine kuchukua wachezaji wao.

  Alizitaja timu ambazo zitashiriki katika ligi kuwa kutakuwa na makundi mawili ambapo kundi A zipo Viiva Queen ya Mtwara ,Mburahati Queen ya Dar es Salaam,Fair Play ya Tanga,Ever Green Dar es Salaam,Mlandizi Queen ya Pwani na JKT Queen ya Dar es Salaam.

  Kundi B Marsh Academy ya Mwanza,Baobab Queen Dodom,Majengo Women Singida,Sisters Fc Kigoma,Kagera Queens na Panama Fc.
  Ofisa habari wa TFF,Alfred Lucas, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Ligi ya wanawake itakayoanza kutimua vumbi Novemba Mosi kwaka huu ,jijini Dar es salaam.

  0 0


  0 0


  0 0

  bunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Zanzibar Mhe. Ibrahim Raza akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Kisauni alipofika kukabidhi madawati katika skuli hiyo na kuona changamoto zao.
  Mwalimu wa Biology wa Shule ya Kisauni Muh’d Ali Muh’d akimueleza Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza juu ya uhaba wa vifaa vya maabara katika skuli hiyo.
  Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza akimkabidhi msaada wa Madawati 80 Mwalim Mkuu wa Shule ya Kisauni Machalila Kulima Ndega kwajili ya shule hiyo.
  Sehemu ya madawati 80 yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza.
  Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza akizungumza na walimu na wanafunzi wa Skuli ya Kisauni baada ya kukabidhi madawati katika shule hiyo.

  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

older | 1 | .... | 1398 | 1399 | (Page 1400) | 1401 | 1402 | .... | 3353 | newer