Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1397 | 1398 | (Page 1399) | 1400 | 1401 | .... | 3348 | newer

  0 0


  SIMU.TV: Jeshi la polisi jijini Dar es Salaam limewakamata vijana wadogo kumi na tano wa kundi la panya road katika eneo la Temeke. https://youtu.be/ZM69VE_qVJM

  SIMU.TV: Kaimu mkuu wa mkoa wa Geita Herman Kapufi ameagiza kuondolewa kwa askari polisi wasio waaminifu katika kituo cha polisi cha Nyarugusu. https://youtu.be/n2WTbpw-mGI

  SIMU.TV: Japokua asilimia kubwa ya uzalishaji wa mazao ya vyakula na biashara kwenye kilimo hufanywa na wanawake  bado kundi hilo halijapewa haki ya kumiliki ardhi sawa na wanaume. https://youtu.be/2ieYhc3Se1c

  SIMU.TV: Shehena ya magogo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17 yaliyovunwa kinyume na utaratibu yamekamatwa na yanashikiliwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Rufiji. https://youtu.be/240JZplKMaU

  SIMU.TV: Asilimia 30 ya tembo barani Afrika hupungua kila mwaka kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ujangili kwa wanyama pori. https://youtu.be/zWRgsC3MABg

  SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limefanikiwa kumuua mtuhumiwa wa ujambazi anayedaiwa kuhusika na matukio kadhaa ya ujambazi katika wilaya za mkoa wa Kigoma.https://youtu.be/opXHv_5dqRE

  SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa kiwanda cha kukamua mafuta ya Karanga kilichopo wilayani Nachingwea kupeleka nyaraka zinazoonesha kuuziwa kiwanda hicho na serikali kipindi cha ubinafsishaji. https://youtu.be/rit_FgoSx_o

  SIMU.TV: Kampuni ya uwekezaji ya TCCIA imejipanga kuiunga mkono serikali kwa kuwekeza katika sekta ya viwanda. https://youtu.be/Oa2YNQo_PfI

  SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema ameuagiza uongozi wa soko la samaki Ferry kuongeza idadi ya matundu ya vyoo katika soko hilo. https://youtu.be/Zhb0phD6Q8E

  SIMU.TV: Ligi kuu Tanzania bara inatarajiawa kuendela tena kesho wakati timu mbalimbali zinatarajiwa kuingia uwanjani. https://youtu.be/v39Tk_ADB14

  SIMU.TV: Serikali wilayani Rorya mkoani Mara imesema itahakikisha inaendeleza vipaji kwa vijana wanaopatikani kupitia ligi mbalimbali. https://youtu.be/x-xqYAX5AdU

  SIMU.TV: Kampuni ya urushaji wa matangazo kwa njia ya digitali ya Multichoice inayomiliki ving’amuzi vya DSTV imetangaza punguzo la bei kwa vifurushi vyake.https://youtu.be/_hfUzjWoV60

  SIMU.TV: Kampuni ya Vodacom Tanzania imemtangaza Bi Paulina Kulwa kuwa mshindi wa jumla wa shindano la M Pawa linalohamasisha wananchi kujiwekea akiba.https://youtu.be/D9pwGQv0qEk

  0 0  LICHA ya kupewa zaidi ya mwezi mmoja tangu Bunge lilipoweka hadharani Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari, wadau mbalimbali wa Habari wameshindwa kuwasilisha maoni yao kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii kwa madai ya kutousoma na hivyo kulazimika kupewa siku saba zaidi.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba alipokuwa akitoa marejesho kwa Waandishi wa Habari mara baada ya kukutana na wadau mbalimbali wa habari nchini kujadili na kupata maoni kutoka kwa wadau hao kuhusu muswada huo.

  “Niwapa wadau wiki moja wawe wameleta maoni yao kwa maandishi yaani mpaka Jumatano ya wiki ijayo wawe wameyawasilisha kwa Kamati kwa kuwa leo tumewaita wakasema hawakupata muda wa kusoma,” alisisitiza Mhe. Serukamba.

  Mhe. Serukamba ameongeza kuwa mchakato wa kuunda sheria unashirikisha wadau husika kwa kuleta maoni yao juu ya Mswada husika na maoni yao yanasaidia katika kutengeneza sheria iliyo nzuri kwa ajili ya Tasnia ya Habari na maendeleo yake kwa ujumla.

  Ameeleza kusikitishwa na wadau hao kushindwa kusoma muswada huo au kuonekana wana ajenda yao na kusisitiza kuwa anaamini kwa muda ambao Kamati imetoa kwa wadau kuwasilisha maoni yao kwa kamati watakuwa wamewasilisha maoni kwa wakati ila kamati iyapitie kabla ya kupelekwa kwa Spika wa Bunge na kuanza kujadiliwa Bungeni.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akizungumza wakati wa majadiliano kati ya wadau wa Habari na Kamati hiyo leo Oktoba 19, 2016 Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba(katikati) pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kushoto) na Naibu Sppika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson wakiwasiliza baadhi ya wadau wa habari (hawapo pichani) wakitoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kikao kilichofanyika leo Oktoba 19,2016 Mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel (kushoto) wakiwasiliza baadhi ya wadau wa habari (hawapo pichani) wakitoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kikao kilichofanyika leo Oktoba 19, 2016 Mjini Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati wakifatilia maoni yaliyokuwa yakitolewa na wadau wa Habari kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kikao kilichofanyika leo Oktoba 19,2016 Mjini Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati wakifatilia maoni yaliyokuwa yakitolewa na wadau wa Habari kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kikao kilichofanyika leo Oktoba 19,2016 Mjini Dodoma.


  0 0

  Neema Mwangomo, MNH

  Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa kifaa maalumu cha kusaidia kuimarisha utendaji wa misuli (training balance and coordination). Msaada huo umekabidhiwa na Profesa Henrik Hautop Lund kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Denmark Copenhagen.Profesa Henrik amesema Fiziotherapia Utengamao ni moja ya matibabu ya misuli iliyoathiriwa na magonjwa yaliyoathiri ubongo kutokana na kiharusi au mtindio wa ubongo kutokana na majeruhi wakati wa kuzaliwa.

  Profesa Henrik amekuwa na ushirikiano wa kiutafiti wa utengamao na Dk Khadija Malima ambaye ni Mtafiti Kiongozi ( Afya) kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia. Utafiti huo unahusu vifaa (Tiles) vya teknolojia ambayo hutumika kutibu misuli, mwendo na kuchangamsha akili kwa watoto wenye mtindio wa ubongo wa kiasi.“Vifaa hivi humwezesha mgonjwa kufanya mazoezi na pia kufurahia kama mchezo, hivyo wateja wanufaika ni wale wenye kiharusi waliopata ajali na hawawezi kutembea, lakini wanahitaji kuimarisha misuli.

  “Lengo ni kufanya utafiti utakaothibitisha faida ya teknolojia hii ili kusambaza huduma ya matibabu ya utengamao sehemu zote nchini hata kwenye jamii kwani teknolojia hii inatumia betri kuchaji na inakaa saa 20,” amesema Dk Malima.Pia teknolojia hiyo imetolewa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Inuka Rehabilstiona centre.
  Kutoka kushoto ni Mtafiti Kiongozi wa Afya katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk Khadija Malima na Profesa Henrik Hautop Lund wa Chuo Kikuu cha Denmark Copenhagen wakikabidhi kifaa maalumu cha mazoezi ya fiziotherapia utengamao kwa Physiotherapist, Abdalah Raphael Makala na Kaimu Mkuu wa Idara ya Physiotherapy katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Alex Gomwa.
  Mmoja wa watoto wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akifanya mazoezi ya fiziotherapia utengamao leo.

  Mmoja wa watoto wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akifanya mazoezi ya fiziotherapia utengamao leo.
  …………………………………………………………

  0 0

  Na Grace Michael

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni imewahukumu wakazi wawili wa Mkoa wa Dar es Salaam kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi Milioni moja kwa makosa ya kujipatia huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa njia za udanganyifu.

  Hukumu hiyo imetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mwandamizi Bweguge Obadia ambaye alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashitaka umeithibitishia mahakama pasipo shaka ya aina yoyote kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo.

  Waliohukumiwa kifungo hicho ni pamoja na Bw. Michael Francis na Bw. Godfrey Nyika ambao ni washitakiwa wa pili na wa tatu huku mshitakiwa wa kwanza Bw. Rashid Kidumule akiaachiwa huru baada ya kuthibitika kutotenda kosa hilo.

  Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Bw. Obadia alisema kuwa hakuna shaka yoyote juu ya washitakiwa hao kutenda makosa ya kujiwakilisha katika duka la dawa la Nakiete kwa lengo la kujipatia huduma ya dawa kwa kutumia kitambulisho cha matibabu cha mshitakiwa wa tatu ambaye ni Bw. Nyika.

  “Ushahidi wa mashahidi wa mashitaka unathibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa mshitakiwa wa pili Bw. Francis alijiwakilisha dukani kwa lengo la kupata dawa kwa kutumia kadi isiyo yakwake na hakuna shaka kuwa mshitakiwa wa tatu ambaye ndiye mwenye kadi alimpatia kadi hiyo mshitakiwa wa pili hivyo kwa ushahidi huu Mahakama inawatia hatiani,”anasema Hakimu Mkazi Bw. Obadia.
  Mkazi wa Dar es Salaam Bw. Michael Francis baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja kwa kosa la udanganyifu katika huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
  Mshitakiwa wa Pili na wa Tatu wakiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa hatiani na kuhumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
  Mshitakiwa Bw. Francis muda mfupi baada ya kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya udanganyifu.
  Mshitakiwa Bw. Godfrey Nyika ambaye ndiye kitambulisho chake cha matibabu kilitumiwa isivyo halali na BW. Francis baada ya hukumu.


  0 0


  Wajumbe wa Kamati Tendaji ya BAMMATA wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa maandalizi ya michezo ya majeshi Tanzania itakayofanyika Zanzibar mwaka huu.
  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya BAMMATA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maandalizi ya Michezo ya Majenshi Tanzania itakayofanyika Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) Brigedia Generali Civil Mhaiki akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud kufungua mkutano wa Kamati Tendaji ya Bara hilo unaofanyika Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia Mtoni Mjini Zanzibar, (kulia) Makamu Mwenyekiti wa BAMMATA, CDR wa KMKM Muhammed Ali Bakar.
  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud akifungua Mkutano wa Kamati Tendaji ya BAMMATA wa maandalizi ya michezo ya Baraza hilo unaofanyika Makao Makuu ya Valantia, Mtoni Mjini Zanzibar.
  Wajumbe wa Kamati Tendaji ya BAMMATA wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa maandalizi ya michezo ya majeshi Tanzania itakayofanyika Zanzibar mwaka huu.

  0 0

  Kabla ya kufanyika mkutano Mkuu wa dharura wa klabu ya Yanga,siku ya Leo kamati ya Mwafaka wa wazee wa timu hiyo imezungumza na waandishi wa habari kuhusu maamuzi ya mwenyekiti Yusuf Manji kutaka kuitumia nembo ya Yanga kwa miaka 10 ili awe mmiliki halali.

  Akizungumza katibu wa kamati hiyo Ibrahim Akilimali ,amesema kuwa kitu ambacho anataka kukifanya Manji kinapelekea kwenye vurugu kubwa kuzidi hata ile ambayo ilishawahi kutokea kipindi cha nyuma kwani atawagawa wanachama pamoja na mashabiki wanaotaka mfumo huo na wale wanaokataa mfumo huo pia.

  “Sisi hatutaki kabisa kurudi kule ambapo tulipokuwepo katika migogoro ya miaka nane na mwaka 2002 ndipo tulipata mwafaka wa suluhisho na kukubaliana kuwa tutumie jina ambalo lilidhiwa na waasisi wetu na kuwa na Yanga sport club na Yanga Cooperation”alisema Akilimali
  Aidha amesema kuwa Yanga kampuni ilikufa na tukaweka utaratibu wa kuwa na hisa ambazo ni 51 asilimia ni ya Yanga pamoja na asilimia 49 ni ya wanachama na tulizunguka mikoa mingi mno kwa ajili ya kuondoa migogoro,kesi na kuomba radhi wanachama wa klabu hiyo.

  Hata hivyo amesema kuwa tulukuwa na mwanasheria ambaye alikuwa mwenyekiti mpaka anamaliza muda wake aliiachia Yanga Mil 200 na hapo hapo tukampata tena mwanasheria mzuri bahati mbaya Nchunga alijiuzulu baada ya kukaa miaka miwili na hatimaye tukampta bwana Manji naye akaongoza miaka miwili kwa sababu ya mahaba yetu ikabidi tuikanyange katiba kwa kumuongezea muda tena na tulimchagua tena.

  “Sasa tunashangaa haijapita hata miezi nane linakuja deni la billioni 11 na laki 6 kitu ambacho kimetushutusha mno wanayanga na pia limekuja swala la kuleta hoja kuwa akodishwe Yanga na nembo ya klabu kwa muda wa mika 10 ila sisi tunasema kuwa Yanga ni kubwa sana na haiwezi kukodishwa kama masufuri ya kwenda msibani na mimi na wazee wa kamati kwa pamoja tunasema hatukubaliani na jambo hilo kwa asilimia mia”alisema Akilimali
  Kwa upande wa aliyekuwa mwenyekiti wa matawi ya jiji la Dar es salaam ya Yanga,Mohammed Msumi amesema kuwa kutokana na Manji kuwa na mahitaji makubwa na timu hiyo ni vyema akakaa pembeni au kuanzisha timu yake mwenyewe na kuiacha Yanga ili iweze kujiendesha kwa mfumo wa kisasa.

  “Tujiulize maswali ivi ni kwanini anataka mchakato huu ufanyike haraka huku alishawahi kusema kuwa Yanga inajiendesha kwa hasara ni mtu gani huyu anakaa sehemu ya aina hiyo na kama hawezi kufuata utaratibu wa klabu na kushindwa kufuata katiba kama anauwezo aanzishe timu yake na kuacha kutumia pesa zake kwa mabavu iili aichukue Yanga”alisema Msumari.
  Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Yanga Mzee Ibrahim Akilimali akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotoa msimamo wa kamati hiyo na baadhi ya wanachama wa Yanga kuhusu ukodishwaji wa Nembo ya timu hiyo.
  Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Yanga Mzee Ibrahim Akilimali akionyesha baadhi ya vipengele vilivyokosewa katika kukodisha timu ya Yanga kwa na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotoa msimamo wa kamati hiyo na baadhi ya wanachama wa Yanga kuhusu ukodishwaji wa Nembo ya timu hiyo.

  0 0

  Akikabidhi mifuko hiyo , kwa uongozi wa serikali ya Mkoa wa Songwe, Meneja wa benki ya Posta mkoa wa Mbeya, Humphrey Julius amesema benki hiyo iliguswa na suala la ujenzi wa majengo mapya ya ofisi za Mkoa wa Songwe hivyo kuona umuhimu wa kuchangia ikiwa kama faida wanayoipata kutoka kwa wateja wanaowahudumia.

  Amesema, mbali na kutoa msaada huo wa mifuko ya saruji, pia benki hiyo imeshakabidhi madwati 130 kwa baadhi ya shule za msingi za Wilaya ya Tunduma, Ileje zilizopo Mkoani Songwe na dawati 30 kwa shule ya Mbeya Day Mkoani Mbeya.Amesema, serikali pekee haiwezi kufanya mambo yote ni lazima wadau zikiwemo Taasisi, Mashirika, Asasi na mtu mmoja mmoja kuingiza mikono yao ili kuipungizia serikali mzigo.

  Hata hivyo, akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu Chiku Galawa, aliishukuru benki ya Posta kwa msaada huo, muhimu kwani serikali ya Mkoinahitaji zaidi ya mifuko 50 elfu ya saruji na mabati laki moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo ya ofisi pamoja na shule na Zahanati.
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe (katikati) Luteni Mstaafu Chiku Galawa akipokea msaada wa Cement mifuko 125 yenye thamani ya shilingi mil 2 kutoka kwa benki ya Posta Tanzania (TPB) tawi la Mbeya.kulia aliyevalia T.shart Meneja Benki ya Posta Mbeya Humphrey Julias ,kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo na Meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduma Teddy Msanzi aliyshikana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Songwe. 
  Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo akishukuru mara baada ya kupata msaada wa Cement1 kutoka benki ya Posta Tanzania (TPB) 
  Mkuu wa Mkoa Songwe Picha ya Pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Songwe na wadau mbalimbali . 
  BENKI ya Posta Tanzania(TPB) kupitia tawi lake Mkoani Mbeya, imetoa msaada wa mifuko ya saruji 125 thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa serikali ya Mkoa mpya wa Songwe.

  0 0

  Kocha Khalfan Ngassa amekuwa kwenye benchi la timu ya mpira wa miguu ya Toto Africans ya Mwanza akiwa kocha msaidizi kwa mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini. 

  Khalfan Ngassa aliongoza timu kwenye mchezo Na. 62 dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 7, 2016; mchezo Na. 67 dhidi ya Mbao FC uliofanyika Oktoba 12, 2016 na Mchezo Na. 79 dhidi ya Majimaji ya Songea uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu. 

  Kwa mujibu wa Kanuni ya 72 (3) (5) ya Ligi Kuu, Kocha Mkuu anatakiwa kuwa na Leseni ya chini kuanzia Daraja B ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) na Daraja C kwa Kocha Msaidizi pia kutoka CAF. 

  Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa Kocha Khalfan Ngassa hana leseni yoyote kati ya hizo, hivyo hastahili kukaa kwenye benchi la timu ya Toto Africans kama kocha mkuu au kocha msaidizi. 

  Kitendo kinachofanywa na Toto Africans ni ukikwaji wa kanuni na ni vema uongozi wa Toto ukamwondoa Khalfan Ngassa kwenye benchi ili kuepuka adhabu. Kipendele cha (7) cha kanuni hiyo ya 72, inaelekeza adhabu kuwa inaweza kutozwa si chini ya Sh 500,000 (shilingi laki tano). 

  Pia tunazikumbusha klabu zote kuwa kuanzia msimu ujao wa 2017/18 wa Ligi Kuu ya Vodacom, kocha anayestahili kukaa kwenye benchi ni yule mwenye leseni Daraja A kwa nafasi ya Kocha Mkuu na angalau Leseni Daraja B kwa kocha msaidizi..

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

  MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) imeanzisha mafunzo ya Ushonaji Nguoa kwa watu wasioona ambayo yatatolewa kwa miezi mitatu kuendeshwa na fundi mahiri wa nguo za kushona, Abdallah Nyangalio.

  Akizungumza na katika uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia watu wasioona kuweza kujiajiri na kuongeza kipato cha kuacha kuombaomba.

  Amesema kuwa mwanafunzi mmoja ambaye atafanya vizuri katika mtihani wa mafunzo hayo atatoa cherehani ikiwa ni pamoja na mwanafunzi mmoja wa Temeke kwa kila mzunguko atatoa cherehani moja.

  Nae Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Edwin Rutageruka amesema kuwa kuendesha mafunzo hayo ni kutaka watu wasioona waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa mafunzo ya ushonaji nguo.

  Rutageruka amesema kuwa Mamlaka imeona kendesha mafunzo katika wilaya tano kwa kuanzia kwa Manispaa ya Temeke kwa kila Darasa litakuwa na watu saba.Mkufunzi wa mafunzo hayo, Abdallah Nyangalio amesema kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kufanya kila kitu na kuwa hivyo sio kigezo cha kufanya kuombaomba.
  Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva (kulia) akimkabidhi zawadi ya Cherehani Mkufunzi wa Mafunzo wa ushonaji kwa wasioona Bw. Abdallah Nyangalio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam,wa kwanza kusoto ni Bw. Edwin Rutageruka Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Picha na Benjamin Sawe Maelezo).
  Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva (kulia) akiongea na Mkufunzi wa Mafunzo wa ushonaji kwa wasioona Bw. Abdallah Nyangalio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam ambapo Mkuu wa wilaya hiyo amewaasa watu wenye ulemavu kutokata tamaa kimaisha kwani jambo lolote ukiwa na nia nalo na kulifanya kwa nidhamu na kujituma utafanikiwa(Picha na Benjamin Sawe Maelezo).

  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Wito umetolewa kwa jamii ili waweze kuwa na maisha bora wawe na shughuli za halali za kufanya zitakazo waingizia kipato,ili wasiwe tegemezi katika familia zao na jamii kwa ujumla. 

  Kauli hiyo imetolewa na Jaggy Singh ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa ushirika ( FGBMFI) wa Kimataifa wa wafanyabiashara Wakristo,ambapo amewataka watu kufanya shughuli zao katika misingi iliyo halali ,katika uadilifu na waepuke udanganyifu.

  Sigh amesisitiza kuwa lengo kuu la mkutano ni kuwaleta wafayabiashara pamoja, kubadilishana mawazo na changamoto wanazopitia,kuonyesha umuhimu wa kuishi maisha ya uhalisia na kufanya kazi kwa bidii zaidi,ambapo amewataka kuepuka udanganyifu wasiipige serikali chenga kwa kutokulipa kodi ,wafuate utaratibu na sheria za nchi. 

  Kwa upande wake raisi wa (FGBMFI) nchini Tanzania Injinia John Njau amesema ushirika huo wa wafanyabiashara wa Kimataifa hawajishughulishi na biashara peke yake bali wanahubiri Injili kamili kwa kutoa ushuhuda wa vitendo hata kama wafanyabiashara wengine hawaamini wao wanatimiza wajibu. 

  Ameainisha kuwa nchini Tanzania kwa sasa wana matawi ya ushirika huo wa wafanyabiashara Wakristo yapo(7) ambayo ni kama ifuatavyo,Mbeya,Mwaza,Shinyanga,Kilimanjaro,Arusha,Dar es-salaam,Manyara pamoja na Zanzibar ,na kwa upande wa Kmataifa kwa ujumla yapo 169,ambapo kila tawi linafanya kazi kutokana na taaluma walizo nazo. 

  Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo John Majo ,ambaye pia ni mwenyekiti wa tawi la Arusha ,amesema kuwa ushirika huo wa wafanyabiashara wa Kikristo mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga maadamu anajishughulisha ,awe ameajiriwa ,mfanyabiashara ,au mjasiriamali anaruhusiwa nia yao kuu ni kuwaleta pamoja ili wamjue Mungu zaidi pia. 

  Aidha amewataka vijana wa kiume wasipende maisha ya urahisi ya bali wachape kazi kwabidii,wajitume waache tabia mbaya ya kuwa tegemezi kwani wananguvu Mungu amewapa wazitumie ili kujiingizia kipato kwani itawajengea heshima katika jamii 

  “Unamkuta kijana yupo tu mtaani hataki kujishughulisha ukimtazama hana ulemavu wowote ,anapenda maisha ya kifahari nay a starehe lakini kazi hataki kufanya matokeo yake anajikuta amejiingiza kwenye mambo ya aibu na fedheha kubwa katika jamiii,inatuhuzunisha sana sisi kama wazazi badilikeni mjitume “alisisitiza John. 

  Katika Kongamano hilo la Kimataifa la kila mwaka mwaka wasemaji walikuwepo sita ,ambao waliongozwa na raisi wa( FGBMFI )kutoka nchini Nigeria Injinia ,Ifeanyi .H.Odedo ambaye anasimamia matawi madogomadogo 3500 nchini Nigeria

  0 0

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexander (pichani mwenye mafaili) kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kushindwa kusimamia ujenzi wa kituo cha kuzalisha maji katika Manispaa ya Lindi.

  Waziri Mkuu amemkabidhi Mhandisi huyo kwa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi, Bw. Stephen Chami na kumuelekeza afanye uchunguzi zaidi juu ya suala hilo.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 19, 2016) wakati alipotembelea mradi wa maji wa Ng'apa ambapo ameagiza nafasi hiyo ikaimiwe na Mkurugenzi Msaidizi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Idrisa Sengulo.

  "Kamanda wa TAKUKURU fanya mapitio ya kina ya mshahara wake. Yeye anasema analipwa Wizarani, mimi najua analipwa na LUWASA. Angalia kazi aliyokwenda kuifanya Dar es Salaam kama inalingana na siku alizokaa,” amesisitiza Waziri Mkuu.

  Mhandisi hiyo anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za ofisi pamoja na kupokea mshahara bila la kulipa kodi ya mapato ya mshahara (PAYE), kujilipa kiwango kikubwa cha posho pamoja na kusafiri kwa muda mrefu.

  Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumilia kuona wananchi wanapata shida huku watendaji waliopewa dhamana ya kuwatumikia hawaonekani kwenye vituo vyao vya kazi. "Huyu nimemuita mimi aje huku, hadi jana alikuwa Dar es Salaam."

  Alipoulizwa sababu za kutokuwepo ofisini kwake kwa muda mrefu, Mkurugenzi huyo alisema kwamba alikuwa Dar es Salaam akiandika maombi ya fedha kwa ajili ya kutatulia changamoto mbalimbali zinazoikabili mamlaka hiyo.

  "Unatumia siku ngapi kuandika proposal, msomi unatumia mwezi mzima kuandika proposal na unakaa Dar es Salaam hata Katibu Mkuu wako hajui na huko unajilipa posho tu! Tena baada ya kulipwa sh.120,000 kwa siku wewe unajilipa sh.150,000. Hatuwezi kuvumilia hali hii,” amesema.

  Waziri Mkuu amemaliza ziara yake siku tatu mkoani Lindi na amerejea jijini Dar es Salaam.


                              
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 - DAR ES SALAAM
  JUMATANO, OKTOBA 19, 2016.

  0 0

  jioni maeneo ya Salasala Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Polisi wakishirikiana na Kikosi kazi cha kuzuia uharibifu wa miondo mbinu ya Shirika la umeme Tanzania Tanesco lilipata taarifa toka kwa raia mwema kuwa kuna watu wanaohujumu miundo mbinu ya Shirika hilo.

  Kikosi hicho kilifika eneo hilo katika nyumba ya Willfred Barutti (45) mkazi wa Makumbusho na kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo ambapo walivipata vifaa mbalimbali Line Meterial ambavyo hutumika kwa ajili ya kuunganisha umeme vya Kampuni ya Tanesco.Polisi walikwenda katika nyumba nyingine mali ya Betrice Emmanuel (42) mkazi wa Salasala Mabanda wakafanya upekuzi na kufanikiwa kukamata vifaa vifuatavyo;

  Nyaya aina ya Drums'02,roller ya waya aina ya AICC ya umeme wa 50 mm ambazo hutumiwa na tanesco kituo cha Kilimahewa huko Kawe Wilaya ya Kinondoni.

  Thamani ya vifaa hivyo vinakadiliwa kuwa Tsh.61,000,000,Watuhumiwa wawili wanashikiliwa kwa mahojiano na Upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani 
  Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Leila Muhaji akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wizi huo wa vifaa vya umeme vyenye thamani ya milioni 61 na kukamatwa,Kulia ni Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.
  Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi. 
  Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi. 


  0 0  0 0

  WE ARE THE MOST AFFORDABLE 
  AND RELIABLE SHIPPING AGENT IN UK
    
        CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 850 (TILBURY/ SHERNESS PORTS) 
  CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 750 (SOUTHAMPTON/ NEWCASTLE PORT)
  4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 910 (SOUTHAMPTON PORT)
  4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 945 (NEWCASTLE PORT)
  4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 930 (TILBURY/ SHEERNES PORTS)
          40’ CONTAINER TO DAR £ 1750
  40’ CONTAINER TO MOMBASA £ 1750 HC
  40’ CONTAINER TO ZANZIBAR £ 2300
  20’ CONTAINER TO DAR £ 1220
  20’ CONTAINER TO MOMBASA £ 1220
  20’ CONTAINER TO ZNZ FROM £ 1600
          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2650(TILBURY PORT)
          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2400(SOUTHAMPTON)
          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2450(NEWCASTLE)
          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM 2612.50(IMMINGHAM PORTS) 
          TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2612.50 (KILLINGHAM)
          ALSO WE CAN       ARRANGE PRE SHIPMENT INSPECTION FOR YOU TO AVOIDINCONVINIENCES.
  ·       GOOD NEWS FOR AIR CARGO CUSTOMERS FOR NAIROBI,MOMBASA AND DAR ES SALAAM!!!!!.
  ·        WE SHIP AIR CARGO TO NAIROBI FOR ONLY£2(EXCLUDING CLEARANCE).
  ·        WE SHIP AIR CARGO TO MOMBASAFOR ONLY£2.50(EXCLUDING CLEARANCE)
  ·        WE SHIP AIR CARGO TO DAR ES SALAAM FOR ONLY£2.50(EXCLUDING CLEARANCE)
  ·        WE SHIP AIR CARGO TO DAR ES SALAAM WITH CLEARANCE ONLY FOR £ 5
   
   FOR MORE DETAILS PLEASE  CONTACT US ON OUR CONTACTS BELOW:- EXTENDED SERVICES LIMITED, CLIPPER HOUSE, TILBURY FREEPORT, TILBURY, ESSEX, RM18 7SG Tel:+441375767890mobile:+447438145815,EMAIL:extendedservicesltd@gmail.com,www.extendedserviceslimited.co.uk

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Byakanwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji vinne vilivyoko kata ya Machame Narumu akitoa uamuzi juu ya mgogoro wa ardhi wa shamba la Fofo estate.
  Baadhi ya Wananchi waliofika katia Mkutano huo.
  Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Byakanwa (aliyenyoosha mikono) akitoa ufafanzi wa jambo mara baada ya kutangaza kurejesha eneo lenye mgogoro kwa Halmashauri ya wilaya ya Hai.
  Baadhi ya wananchi wa vijiji vinne vya Urori,Tella ,Mula na Usali waliohudhria mkutano wa Mkuu wa wilaya ya Hai wa kutoa maamuzi juu ya mggoro wa shamba la Fofo estate. 

  0 0


  0 0

  Serikali imewataka watumishi wote nchini walioajiriwa na Serikali, yakiwemo mashirika ya Dini na Taasisi  nyingine ambazo haziko kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya Serikali lakini zinapata ruzuku kutoka Serikalini; kuwa wamesajiliwa katika zoezi  la Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma linaloendelea kote nchini, kufikia Oktoba 31, 2016.

  Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, katika mkutano wa pamoja ulioitishwa kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

  Bi Kairuki amesisitiza; “waajiri na watumishi watakaoshindwa kutekeleza zoezi hili watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo”

  Akifungua mkutano huo uliolenga kutoa tathmini ya mwenendo  wa zoezi linaloendelea la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma lilioanza nchi nzima tangu Oktoba 03, 2016, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu L. Nchemba (Mb) amesema mpaka sasa Mamlaka ya  Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  imefanikiwa kusajili zaidi ya asilimia 50% ya watumishi wote nchi nzima na baadhi ya mikoa kukamilisha usajili kwa zaidi ya asilimia 95%. Ameutaja mkoa wa Geita kuwa mkoa unaoongoza kwa kufanya vizuri katika zoezi hilo

  Amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizokwamisha zoezi hilo kukamilika kwa wakati uliopangwa; Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wameamua kuongeza muda wa kukamilisha zoezi hilo kwa wiki mbili zaidi hadi Oktoba 31, 2016.

  Amewataka watumishi kuondokana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watumishi kwamba zoezi hilo limelenga kuhakiki vyeti na badala yake wajitokeze kwa wingi kusajiliwa kwani Serikali imelenga kuunganisha taarifa za mfumo wa mishahawa wa Serikali na NIDA, ili mbali na kutatua tatizo la watumishi hewa; kupitia mfumo huu wa kielektroniki unaomtambua mtu kwa alama zake za kibaiolojia kuwa na maslahi mapana kwa taifa na kwa watumishi; kwa kuunganisha mifumo mingine ya Serikali ukiwemo mfumo wa Kodi, mifuko ya Hifadhi za Jamii, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Bima ya Afya, Uhamiaji, RITA Na Benki ili kutoa manufaa mapana kwa mtumishi.

  Amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kuwezesha kusambazwa kwa vifaa vya usajili nchi nzima, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Taasisi na Mashirika yote ya Serikali waliojitoa kufanikisha zoezi la Usajili.

  Kupitia zoezi la Usajili Watumishi wa Umma, Tayari NIDA imefungua ofisi za usajili nchi nzima, ngazi ya Wilaya kusogeza karibu zaidi huduma inayotolewa kwa wananchi. Kwa mujibu wa Waziri Mwigulu Pindi zoezi  la usajili watumishi litakapokamilika usajili wa wananchi utaanza mara moja nchi nzima kwani zoezi la usajili vitambulisho vya Taifa limelenga kila mwananchi, Mgeni anayeishi kihalali nchini na Mkimbizi.

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba (Mb) akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari mkoani Dodoma kuhusu mwenendo wa zoezi linaloendelea la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) na Bi. Rose Mdami, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati, akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba (Mb) Akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu zoezi la kusajili watumishi wa Uma nchi nzima. kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba akipokea maelezo ya namna shughuli za usajili zinavyo ratibiwa na ofisi ya usajili Wilaya ya Dodoma Mjini ; alipofanya ziara ya ukaguzi na kukutana na viongozi na watumishi wa Umma waliofika kupata huduma


  0 0


  0 0


    The Government of the Democratic Republic of Congo (DRC) has announced the reduction of Visa fee for Tanzanians and Ugandans from US $100 to US $50 effective November 1st, 2016. 
  The decision comes just about a month after the DRC Ambassador to Tanzania his Excellency Jean-Pierre Mutamba and the Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (TTFA) Executive Secretary Capt Dieudonné Dukundane, Chief Operating Officer Mr. Sayiba Tambwe Patient held a meeting with DRC high level officials in Kinshasa on September 5th, 2016. 

  An official statement issued this week by DRC’s Director General of Immigration Mr. François Beya Kasonga, said the move was part of Visa harmonization process for Central Corridor Member Countries (Burundi, DRC, Rwanda, Tanzania and Uganda). 
  Already Burundi, DRC and Rwanda enjoy Visa free movement among themselves under the Economic Community of the Great Lakes Countries (CEPGL) arrangement. 
  Harmonization of Visa was also one of the agreed issues during the 7th Ordinary Meeting of the Inter-State Council of Ministers of the TTFA held in Dar es Salaam on August 11th, 2016. 
  Commenting on the new development Capt. Dukundane hailed DRC Officials for this move that will reduce struggles and facilitate trade within Central Corridor member countries. He also commended the useful guidance provided by the DRC Ambassador to Tanzania, Mr. Jean-Pierre Mutamba towards the achievements made so far throughout this process.

  Capt. Dieudonne Dukundane

  EXECUTIVE SECRETARY
  From left to right: TTFA Chief Operations Officer Sayiba Tambwe Patient, TTFA Executive Secretary Captain Dieudonne Dukundane, Director General of DRC Immigration François Beya, Ambassador of DRC in Tanzania, H. E. Jean Pierre Mutamba and Deputy DG of DRC Immigration, Jean Claude during a meeting held in Kinshasa in September 5th, 2016. 


  0 0

  Leo Oktoba 19, 2016 Kamati ya Shindano la Maandalizi ya Miss Tanzania 2016 imesema Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29,10, 2016 katika viunga vya Rock City Jijini Mwanza, litakuwa bora zaidi kutokana na maandalizi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika.

  Na BMG
  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hashim Lundenga (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Rhino Agency inayoandaa Miss Tanzania, amesema baada ya mashindano hayo kufanyika Jijini Dar es salaam miaka yote, kamati hiyo imeamua yafanyike Jijini Mwanza na kwamba yatafanyika kwa miaka mitano mfululizo.
  Amesema washiriki wote 30 katika shindano hilo ni bora hivyo yeyote atakayeibuka mshindi ataliwakilisha vyema taifa kwenye mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika Disemba 18, 2016 Jijini Washingtone DC nchini Marekani.
  Viingilio katika shindano hilo ni shilingi 20,000, 50,000 na 100,000 ambapo inategemewa kwamba wasanii Ali Kiba pamoja na Christian Bella ikiwa wataafiki makubaliano watadondosha burudani katika shindano hilo huku washiriki wakijipatia fursa mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza kujishindia gari.
  Washiriki wa shindano hilo wamesema wamejiandaa vyema na bado wanaendelea kujinoa zaidi ili kuhakikisha atakayeibuka mshindi anaiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano ya dunia huku wakielezea furaha yao kubwa kwa mashindano hayo kufanyika Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.
  Kamati ya Miss Tanzania 2016 ambapo kutoka kulia ni Hashim Lundenga, Pamela Irengo, Flora Lauwo.
  Mkutano baina ya Kamati ya Miss Tanzania 2016 na Wanahabari Jijini Mwanza
  Washiriki wa Miss Tanzania 2016 katika ubora wao

older | 1 | .... | 1397 | 1398 | (Page 1399) | 1400 | 1401 | .... | 3348 | newer