Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1399 | 1400 | (Page 1401) | 1402 | 1403 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairuki leo amefanya ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAF.

  Mh. Kairuki alianza ziara hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa hua Mh. Ally Hapi.
  Akiwa ofisini hapo Mh. Kairuki alisaini kitabu cha wageni na kusalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi, wakuu wa wilaya za Ilala, Temeke, Kigamboni na Katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam.

  Mara baada ya kusaini kitabu cha wageni, Mh. Angela Kairuki alifanya mkutano na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na waratibu wa TASAF Mkoa na manispaa za Dar es salaam ambapo alipokea taarifa mbalimbali za manispaa na Mkoa mradi wa kuondoa umasikini wa TASAF.

  Katiba hotuba yake Mh. Kairuki amewataka waratibu wa TASAF wa Mkoa na manispaa kujipanga vema, kusimamia mradi kwa makini na kuondoa wale wote wasiostahili kupata fedha hizo katika orodha ya wanufaika wa TASAF.

  Akitoa salam za Mkoa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi amemshukuru Mh. Kairuki kwa ziara hiyo na kumfahamisha kuwa Mkoa wa Dar es salaam unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa TASAF ikiwemo watu wasiostahili majina yao kuingizwa miongoni mwa wanufaika, kuingizwa kwa majina hewa, kubaguliwa kwa baadhi ya wananchi masikini kwa itikadi za kisiasa na ufuatiliaji duni unaofanywa na waratibu wa TASAF ngazi mbalimbali.

  Ziara ya Mh. Angela Kairuki iligusa pia maeneo ya Kata za Kigogo na Msasani ambako Mh. Waziri alipata nafasi ya kuongea na wananchi wanufaika wa TASAF katika mikutano ya hadhara mitaa ya Kigogo Kati na Mikoroshini (Msasani).

  Wananchi waliojitokeza wameishukuru serikali kwa mradi huo ambao umekua msaada mkubwa kwao katika kujikwamua na umasikini.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akizungumza na mmoja wa wakazi wa Kinondoni,
  mara baada ya kufanya ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAFkushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,akiendelea na ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAFkushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi


  0 0
 • 10/20/16--09:00: RWANDAIR: TENDER ADVERT


 • 0 0
 • 10/20/16--12:24: TOYOTA RAV4 INAUZWA

 • Make:Toyota
  Model:Rav4
  Body type:Station wagon 
  Color:Black
  Year of man:2006

  Contact:+255754710458 
  or +255755311477


  0 0
 • 10/20/16--12:30: POLISI BANDIA ADAKWA MWANZA

 • 0 0


  0 0

  Na Yusuph Kileo
  Takwimu za uhalifu mtandao zimeendelea kukua huku wana usalama mtandao wakiendelea kutafuta suluhu ya kudumu dhidi ya uhalifu mtandao maeneo mengi duniani. Hivi sasa tumefikia wakati wa kila tunavyotumia ku unganishwa kwenye mtandao (Internet of Things – IoT) ambapo Televisheni, Friji , Majiko, Magari na kadhalika vimekua vikiunganishwa mtandaoni ili kurahisisha maisha ya watumiaji. 
  Hali hii imepelekea wimbi kubwa la uhalifu mtandao kuendelea kukua na imetabiriwa kadri muda unavyoendelea tishio la uhalifu mtandao litakua kubwa zaidi – Kuliangalia hili Mkutano wa wana TEHAMA wa Nchi za Afrika (AfICTA) wa mwaka huu 2016 ambao uliofanyika jijini Windhoek Nchini Namibia ulipata kujadili mengi kuhusiana na hili ambapo pande mbili za faida na changamoto ziliangaziwa kwa karibu. 
  Binafsi, Nilipata kushiriki kuongoza mijadala miwili ambapo tuliangazia changamoto za ukuaji wa uhalifu mtandao kutokana na wimbi wa vitu vingi kuendelea kuunganishwa mtandaoni na pia kujadili mapendekezo ya mambo ya msingi ya kuzingatia ili kubaki salama pamoja na mambo ya msingi kwa wadhibiti wa uhalifu mtandao wanayopaswa kuzingatia ili kuweza kudhibiti hali hii. Kusoma zaidi BOFYA HAPA. 
   Usiku wa Jana jijini #Windhoek, Namibia, Mdau mkuu wa Usalama wa Mtandao wa Tanzania Yusuph Kileo amepokea  Tunzo yake ya Kwanza ya kimataifa Kubwa  katika kutambua mchango wake mkubwa Barani katika swala la Usalama mtandao! Yusupha hakika amemefurahi sana! Kwani jina lake  litaingia katika majina yanayotegemewa kujadiliwa ili kuingia katika bodi ya wana TEHAMA wa Nchi za Afrika! Hatua muhimu kwake na Tanzania.

  0 0

  Kukua kwa msitu wa saruji wa jiji la Dar es salaam kunaendelea kutokomeza nyumba zilizoezekwa na mabati maarufu kama  "Mbavu za Mbwa" zilizokuwa zinatawala maeneo ya Jangwani na Karianoo kama inavyoonesha picha hii ya drone iliyopigwa na Karim Michuzi.


  0 0

   Mkurugenzi na Mmiliki wa Ndauka Advert, Rose Ndauka akizungumza  leo katika uzinduzi  wa  Alama (Lebo) yake ya muziki inayoitwa Ndauka Music na kumtambulisha Msanii wake wa kizazi kipya, Kassimu Said a.k.a Casso  (kulia) leo jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa kizazi kipya, Kassimu Said a.k.a Casso, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi  wa  Alama (Lebo) ya muziki inayoitwa Ndauka Music leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

  0 0

  Jumla ya watoto sita waliozaliwa wakiwa na vichwa vikubwa mkoani Tabora wamefanyiwa upasuaji huku wengine 30 wakipata maelekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hiyo bila ya kuwa mzigo kwa jamii iliyowazunguka katika awamu ya nne ya kambi tiba za GSM Foundation zinazoendeshwa kea kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Upasuaji na Mifupa ya Muhimbili MOI.

  Idadi hii inasababisha jumla ya watoto waliotibiwa na kambi tiba hizo zilizoanza mwezi Aprili mwaka huu na kupita zaidi ya mikoa 15  kufikia watoto 196 huku kambi ikiwa bado inaelekea kuifikia mikoa mitatu zaidi ya Tanzania Bara na baad ya halo kuelekea Visiwani Zanzibar mapema mwezi Novemba mwaka huu.

  Akiongea na wanahabari kabla ya kufunga kambi tiba hiyo inayotembea na madaktari Bingwa wanne, amnesie wanne na mabwana usingizi wawili, Kaimu Mkuu wa kambi tiba hiyo Dk Hamis Shaaban amesema bado kuna changamoto ya uelewa kwa wazazi wenye watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa ambapo wengi wao bado hawaamini kwamba tiba za kitabibu zinaweza kumaliza tatizo la watoto wao.

  “Wengi wao bado wanaamini kwamba tatizo hili ni la kulogwa hivyo huwaficha watoto wao kwa waganga wa kienyeji, na mpaka tunapowafikia tunakuta muda wa kuweza kuokoa afya na maisha yao kwa ujumla unakuwa umeshapita”, alisema Dk Shaaban

  Kwa upande wake Afisa Habari wa GSM Foundation, Bw Khalphan Kiwamba amewaomba wananchi walioa mikoa ya Kagera, Kigoma, Rukwa na Zanzibar ambako kambi tiba hiyo inaelekea kujitokeza ili kuipata fursa hiyo ambayo hakuna hakika kwamba inaweza kutokea tena katika miaka ya karibuni.

  “Gharama ya kumtibu mtoto mmoja mwenye  kichwa kikubwa ni karibia shilingi milioni moja za kitanzania, lacinié GSM Foundation imelipia gharama zote za tiba kwh mikoa yote ya Tanzania kea mwaka huu na huenda mwakani tussle na kambi za namna hii. Kwa hiyo tujitahidi kuchangamkia fursa”, alisisitiza Kiwamba.
  Dk Pascal Joachim akimsikiliza mzazi wa mtoto Seleman Said kabla ya kupatiwa matibabu katika kambi tiba ya GSM Foundation katika Hospitali ya Kitete Mkoani Tabora.
  Madaktari wakiwa katika Kliniki.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwamri akiwa emembeba mmoja kati ya watoto waliohudhuria kambi tiba ya GSM Foundation.
  Mtoto Mjema Gilbert akiwa kwenye foleni ya Kambi tiba ya GSM Foundation akiwa na Mama yake.

  0 0


  0 0


  SIMU.TV: Uongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam DARUSO na shirikisho la vyuo vikuu TAHILISO umeonana na waziri wa elimu kutafuta suluhisho la utoaji wa mikopo isiyokidhi haja za wanafunzi. https://youtu.be/_zAn3g3mYb0

  SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa auagiza uongozi wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF kukusanya madeni yote kwa wadaiwa sugu. https://youtu.be/o2VTu36Cgmw

  SIMU.TV: Serikali imeunganisha taasisi 72 katika mtandao wa mawasiliano wa mkongo wa taifa ili kupunguza gharama ya mawasiliano kwa taasisi za serikali. https://youtu.be/SoMGs-yWmxU

  SIMU.TV: Serikali imehimiza halmashauri zote nchini kutumia vyanzo vyake vya mapato kununua vifaa tiba kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza badala ya kusubiri bajeti ya serikali. https://youtu.be/1awXWiy1avA

  SIMU.TV: Wananchi wa vijiji vya Nyabagi na Nyamikoma wameiomba serikali kuwasaidia eneo la makazi ili waweze kuendesha maisha baada ya kuondolewa eneo la hifadhi.https://youtu.be/NG-V4JtNVds

  SIMU.TV: Maafisa wa polisi katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wamemkamata mwanamke mmoja raia wa Brazil kwa kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Cocaine. https://youtu.be/TlNRTkGD16o

  SIMU.TV: Wafanyabiashara na watu wenye kipato kikubwa wameshauriwa kuwekeza kwenye masoko ya mitaji na dhamana ili kuibua fursa nyingi kwa wananchi.https://youtu.be/H_ryoApYgRg

  SIMU.TV: Waziri wa viwanda na biashara amesema hakuna bidhaa yeyote itakayoingizwa nchini bila kukaguliwa na mamlaka za TBS na TFDA ili kulinda walaji.https://youtu.be/vvjKG7EVTlc

  SIMU.TV: Vinara wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Simba imeendelea kufanya vizuri baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Mbao fc leo. https://youtu.be/Hgu4a-itYdU

  SIMU.TV: Mashabiki wa timu ya Majimaji wameipongeza timu yao kwa kuanza kuonesha umahiri kwa kushinda michezo miwili ugenini tangu msimu wa ligi kuu uanze.https://youtu.be/3Vmlw1BSx4o
  SIMU.TV: Wachezaji watatu wa timu ya gofu ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania wameteuliwa kujiunga na timu ya taifa ya gofu. https://youtu.be/S9zau4-aJYU


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  NDEGE sita kufunika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius K. Nyerere katika ujio wa Mfalme wa Morocco Mohamed Vi akiongozana na wafanyabiashara 1000.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ziara hiyo ina manufaa kwa watanzania hivyo fursa ambazo zinaibuliwa kutokana ujio viongozi mbalimbali zitumiwe vizuri katika kujiletea manufaa.

  Amesema kuwa ujio huo wa Mfalme wa Morocco utakwenda sambasamba na kusaini baadhi ya mikataba 11 kwa ikiwemo ya mahusiano, Reli ya Mchuchuma na Liganga, Uvuvi, Kilimo, utalii, siasa na mahusiano.

  "Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa akifanya kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania hivyo kila mtu atumie fursa hiyo kwa vitu vitakavyoibuliwa"Amesema Makonda.

  Kutokana na ujio huo, watanzania wametakiwa kwenda kuulaki ujio wa kiongozi huyo ikiwa ni kuonyesha ukarimu wetu wenye amani.

  Mkuu wa Mkoa huyo amesema Mfalme wa Morocco atazindua jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti Bakwata.

  Katika ziara hiyo wafanyabiashara watanzania watakutana na wafanyabiashara wa Morocco na kujifunza jinsi ya kushirikiana kibiashara kwa maendeleo ya taifa.

  Ziara hiyo inatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 27 na kuondoka nchini saa 10 jioni
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ujio wa Mfalme wa Morroco hapa nchini.Picha na Humphrey Shao.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akisalimiana na mmoja wa wazazi alipowasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Bwawani kushiriki Mahafali ya 13 ya Shule hiyo.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Kidato cha nne katika Mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya hotuba ya Mgeni rasmi.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akitoa neno kwa wahitimu katika Mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia), Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka kushoto, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wanne kutoka (kushoto), Mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakwanza kushoto.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara. Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840 na ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (katikati) kwa kushirikiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, James Metairon (kulia) wakikata utepe wakati wa ufunguzi wa kuzindua maonesho ya sekta ya Fedha, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani city,  jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya sekta ya Fedha, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani city,  jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya sekta ya Fedha, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani city,  jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KAMPUNI ya Bollore Transport and Logistics Tanzania Limited imeweka mikakati ya kuendelea kusaidia jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyoo mashuleni na miundombinu ya maji katika wilaya ya Ilala.

  Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa jina hilo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa nchi za Tanzani, Rwanda na Burundi Regis Tissier amesema kuwa wameweza kushirikiana na manispaa ya wilaya ya Ilala katika ujenzi wa bomba la maji  kutoka Buguruni Mivinjeni na baada ya kuharibiwa na mvua za mwaka jana na kuwa na dalili za kutokea magonjwa ya milipuko.

  Tissier amesema, kampuni ya Bollore imeweza kusaidia Shule ya Msingi Msasani kwa kuweka mradi wa gesi asilia ambapo inaweza kuja kutumika kwa matumizi ya kupika vyakula vya mashuleni na mengine pia.

  Kuweza kuendelea kuleta maendeleo nchini, Ballore imeweka mikakati ya kuchukua hatua ya kuhakikisha wanasaidiana katika maendeleo katika jamii, kuajiri wafanyakazi wengi ambapo mpaka sasa asilimia 98 ni watanzania na kushirikiana na makampuni mengine katika biashara.

  Ballore wana mikakati ya kuendelea kutanuka zaidi kibiashara na kuleta mirdi mipya zaidi nchini ambapo mpaka sasa wanahusika na masuala mbalimbali ikiwemouchimbaji wa nishati ya mafuta na madini, wakala wa forodha na usafirishaji wa mizigo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bollore Transport and Logistics Tanzania, Rwanda na Burundi Regis Tissier akizungumza wakati wa utambulisho wa jina jipya la kampuni hiyo jana Jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bollore Transport and Logistics Tanzania, Rwanda na Burundi akiwa pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo  Branko Ng'inja (kulia) na   Meneja mkuu wa AMI-ICD Augustin Ayishashe (Kushoto)

  0 0  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa majadiliano ya amani na ulinzi kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) unaofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mkutano huo unarajia kujadili kuhusu masuala yafuatayo; Aina za chaguzi na jinsi zinavyosimamiwa miongoni mwa nchi wanachama, Vijana wa Afrika wanaokimbilia Ulaya kutafuta maisha, tishio la amani ya Kanda na Dunia.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (katikati) akifuatilia Mkutano. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (kushoto)
  Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza Waziri Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
  Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano na Watendaji wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka SADC na EU.
  Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika mahojiano na wanahabari

  0 0


  Na Lydia Churi-Mahakama

  Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Majaji wengine wamepongezwa kwa kumaliza vizuri kesi za uchaguzi zilizofunguliwa katika Mahakama Kuu kanda mbalimbali nchini na pia kutenga muda wa kujadili changamoto zilizotokana na kesi hizo.

  Akizungumza na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo jijini Arusha, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amewapongeza Majaji hao kwa kujitoa katika kusikiliza kesi hizo na kuzitolea hukumu kesi nyingi kwa kipindi kifupi licha ya kesi chache kubakia mahakamani.

  Jumla ya kesi 53 za Ubunge zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 zilifunguliwa katika Mahakama Kuu kanda za Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mtwara na Mwanza. Kanda nyingine ni Shinyanga, Songea, Sumbawanga, na Tanga. Kati ya kesi hizo, kesi 31 zilimalizika katika hatua za awali na kesi 22 ziliendelea, mpaka sasa kesi 19 zimemalizika. kesi tatu bado ziko mahakamani.

  Hata hivyo kesi zote 196 zilizotokana na uchaguzi wa madiwani zilimalizika mapema katika Mahakama mbalimbali za Hakimu Mkazi nchini. Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu nchini, zaidi ya asilimia 94 ya kesi za uchaguzi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu zimemalizika wakati asilimia 100 ya kesi zote za udiwani zimemalizika.

  Aidha, Jaji Mkuu amewataka Majaji hao kuweka mikakati ya kuhakikisha kasi ya kupunguza kesi mahakamani hasa zile za muda mrefu inaongezeka ili kupunguza malalamiko yanayotokana na kuchelewa kutoa hukumu na kutopatikana kwa nakala za hukumu kwa wakati.

  Mheshimiwa Chande amewataka Majaji kusimamia suala la maadili ndani ya Taasisi hiyo ili kurejesha imani ya wananchi kwa Mahakama yao.

  Kuhusu suala la Maadili kwa Mahakimu, Jaji Mkuu amesema wameomba ushauri Tume ya Utumishi wa Mahakama kuwa endapo hakimu atashtakiwa kwa kosa la rushwa ataondolewa kazini kwa maslahi ya Umma hata kama atashinda kesi hiyo.

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (hawapo pichani) leo jijini Arusha. Katika Mkutano huo, Jaji huyo aliwapongeza Majaji kwa kuziendesha vizuri kesi zilizohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015PICHA NA LYDIA CHURI-MAHAKAMA .

  0 0


  Na George Binagi-GB Pazzo
  Wadau wa elimu mkoani Mwanza wametakiwa kushirikiana na serikali katika kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za waalimu katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza.

  Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Florence Sam, ametoa rai hiyo wakati wa hafla ya kupokea vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta pamoja na printa, vilivyotolewa na wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo mwaka 1993.

  Mwalimu Sam amesema shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 1,800 huku vyumba vilivyopo vikiwa ni 18 hali inayosababisha kuwa na upungufu wa vyumba 32 ambapo ametumia fursa hiyo kuwaasa wadau mbalimbali kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

  Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule hiyo, Mwalimu Benadetha Athanasi, amesema wanafunzi hao wameamua kusaidia kutatua baadhi ya changamoto za shule hiyo ili kutoa mwamko kwa wadau wengine kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu nchini.

  Vifaa vilivyotolewa na wanafunzi hao ni pamoja  na vifaa vya michezo kwa wanafunzi,kompyuta pamoja na printa ambavyo vimegharimu Zaidi ya shilingi Milioni Mbili.

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi Afisa Mtendaji wa Kata ya Muhandu ilipo shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Mbali na vifaa hivyo, pia wanafunzi hao ambao miongoni mwao ni wafanyabiashara na watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, wametoa vifaa vya michezo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ikiwemo mipira na jezi, pamoja na zawadi mbalimbali kwa ikiwemo kompyuka kwa baadhi ya waliokuwa waalimu wao kipindi hicho.
  Na BMG

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakiwakabidhi baadhi ya waalimu pamoja na kamati ya shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakikabidhi vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, wakiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa shule hiyo walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.


  0 0

  Afisa masoko Platinum Credit Tanzania, Gideon Lufunyo (kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji ambayo ni sawa na tani 15 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu ikiwa ni msaada wa taasisi hiyo kwa waathirika wa tetemekonla Ardhi mkoani humo.
  Kampuni ya Platnum Credit Tanzania Leo imekabidhi msaada wa mifuko 300 ya sumenti kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani humo.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo, Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo,Gideon Lufunyo alisema  tetemeko hilo limeleta madhara makubwa ambayo yamewagusa na kuamua kusaidia serikali katika kurejesha miundombinu yake hasa katika mshule katika hali nzuri ili masomo yaendelee na watoto wapate elimu.

older | 1 | .... | 1399 | 1400 | (Page 1401) | 1402 | 1403 | .... | 3353 | newer