Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1387 | 1388 | (Page 1389) | 1390 | 1391 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mke wa Rais Mama janeth Magufuli leo amehudhuria kwenye msiba wa shemejie Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki Dunia katika hosptali ya Taifa muhimbili jijini Dar es salaam kwa kusumbuliwa na maradhi ya miguu. 
  Marehemu, ambaye ni Mama Mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete alifariki Jana asubuhi hospitalini hapo baada ya Kulazwa Kwa muda wa mwezi mmoja akisumbuliwa na maradhi ya hayo. Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya Mwanakalenge,wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na kuhudhuliwa  na mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali. Marehemu Bi Mariam ameacha watoto watatu na wajukuu wawili.
  Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo  Oktoba 10, 2016
  Mwanga, 
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie  (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (wa tatu kushoto) akiwa na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete (kulia) akimfariji Bi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa pole Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwafariji watoto wa  shemejie Rais Mstaafu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, Marehemu Mariam Ramadhani Saburi,    aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016.  0 0

  Benny Mwaipaja, MoFP-Washington DC, Marekani

  MAWAZIRI wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi mbalimbali za kiafrika, wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, wamekutana Jijini Washington DC, Marekan,i na kuzitaka Taasisi hizo kuweka mipango inayoakisi na kutatua changamoto zinazolikabili bara hilo ikiwemo, uhalifu, umasikini, mizozo ya kivita na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi

  Aidha, Viongozi hao wamezitaka taasisi hizo kuweka uwiano wa uwakilishi wa uongozi wa juu ili kuhakikisha kuwa maslahi mapana ya nchi hizo yanalindwa na maendeleo endelevu yanafikiwa kwa haraka.

  Akizungumza kwenye moja ya mikutano hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambaye kiutaratibu ni mmoja wa Magavana wa Benki ya Dunia na IMF, amesema kuwa mashirika hayo ya fedha ya kimataifa yanamchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania.

  Hata hivyo amesema kuwa mdororo wa uchumi duniani, ambao unaonesha kuwa viwango vya ukuaji wa uchumi vilivyokadiriwa kufikiwa kwa asilimia 3, havitafikiwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa ukuaji wake hivi sasa ni asilimia 1.5 tu, unaashiria namna nchi wanachama zinatakiwa kujipanga kuhakikisha kuwa uchumi unapanda.

  Dkt. Mpango amesema kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka lakini changamoto kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa uchumi huo unaonekana katika maisha ya kawaida ya wananchi wake. 
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Katibu Mkuu Bw. Dotto James (kulia) wakiandika pointi muhimu wakati Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim, alipowahutubia Mawaziri wa Fedha na Makatibu wakuu (Magavana) kutoka nchi za Kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini Washington DC-Marekani. 
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Fedha wa Swaziland kushoto kwake walipokuwa kwenye mkutano na  Mkurugenzi Mtendaji Bi. Christine Lagarde Jijini washington DC- Marekani. 
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya Afrika, Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe Hayupo pichani), Jijini Washington DC-Marekani. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu akifuatiwa na Naibu Gavana wa Benki hiyo Dkt. Natu Mwamba.
   Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato, akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kitabu Chenye maelezo mbalimbali ya miradi inayotekelezwa nchini Tanzania kwa ufadhili wa shirika hilo, ambapo Japani imeahidi kuendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kuendeleza miundombinu ya barabara na sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
  (Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango) 

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa makampuni ya Azam Bwana Said Salim Bakhresa ambapo alimueleza waziri mkuu nia yake yakuendelea kujenga viwanda zaidi vya kusindika matunda na chakula mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa waziri mkuu magogoni Dar es salaam leo.
  Picha na Chris Mfinanga.

  KAMPUNI ya Bakhresa Foods imedhamiria kuongeza viwanda vingine vya usindikaji matunda hapa nchini ili kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima.

  Ahadi hiyo imetolewa leo (Jumanne, Oktoba 11, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Said S. Bakhersa wakati alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.

  Bw. Bakhresa amesema wana mpango wa kujenga kiwanda kimoja kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watu wanapata usumbufu wa kusafirisha matunda hadi Dar es Salaam ndipo wayauze.

  “Kuanzia tarehe 15 Oktoba, tutaanza kupokea matunda kutoka Kahama na maeneo ya jirani, na kwa siku tunapata semi trela zaidi ya 30. Yakimalizika ya kule tunaanza kupokea mengine kutoka mikoa ya Pwani na Kusini.”

  “Tukijenga kiwanda Kanda ya Ziwa, tutapunguza adha ya wadau kusafirisha matunda kutoka kule hadi hapa kiwandani na badala yake sisi tutakuwa tunasafirisha concentrated juice na kuileta hapa kwa hatua zaidi za usindikaji,” amesema.

  Amesema wana mpango wa kuendeleza usindikaji wa vyakula vya nafaka kwenye mikoa ya Kusini na kwamba hadi sasa wameajiri wafanyakazi zaidi ya 8,000 wakiwemo Watanzania 180 ambao wameajiriwa kwenye matawi yake nje ya nchi. “Hawa tunawalipa kamaexpatriates,” amesisitiza.

  Amesema hivi sasa Kampuni hiyo imekwishafungua matawi mengine kwenye nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini.

  Kampuni ya Bakhresa Foods inatengeneza vyakula mbalimbali zikiwemo juisi, soda, maji, biskuti, ice-cream, vyakula vya nafaka kama ngano, mahindi, mchele na bidhaa za kuokwa.

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu amemhakikishia Bw. Bakhresa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano kushirikiana na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda kwani imedhamiria kukuza uchumi wa Tanzania kupitia uzalishaji wa viwandani.

  “Serikali inathamini mchango wa wenye viwanda katika nchi yetu. Tunawashukuru ninyi ambao ni wakongwe kwenye sekta hii, na kwa hiyo tunawaomba msikate tamaa, muendelee kufungua viwanda zaidi ili wananchi wetu wapate mahali pa kuuzia mazao au bidhaa zao,” amesema.

  Amemuomba Bw. Bakhresa aangalie maeneo mengine zaidi ya kuwekeza kama vile sekta za hoteli na utalii ili kusaidiana na Serikali kukuza uchumi wa Tanzania.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMANNE, OKTOBA 11, 2016.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  MAENDELEO ya Viwanda yanahitaji mali ghafi za kilimo hivyo Benki ya Maendeleo ya  Kilimo nchini (TADB) inawajibu ya kuwafikia wakulima ili matokeo ya viwanda yaweze kuonekana ikiwemo na kuwa na masharti ya riba nafuu au kuondolewa kabisa.

  Hayo ameyasema leo Naibu Waziri wa Fedha , Uchumi na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), amesema kuwa sekta ya kilimo inaajiri watanzania asilimia 70 huku ikichangia pato la Taifa kwa asilimia 28 ambayo ni kidogo kutokana na ukuaji wa sekta ambayo inatakiwa kwenda na viwanda ambapo TADB ndio yenye kuweza kuleta mapinduzi hayo viwanda kwa kuwafikia watanzania waliowengi.

  Amesema bodi ya wakurugenzi ya TADB inajukumu la kutekeleza na kuboresha sekta ya kilimo kwa kuwafikia watanzania wengi katika maeneo ya kijijini kutokana ni kuwa wazalishaji wa mazao mbalilmbali ambayo ndio yanaweza kuzalisha viwanda na nchi ikaweza kukua kiuchumi pamoja na kuongeza pato la taifa.

  Dk. Ashantu amesema benki ya kilimo ihakikishe wanatafuta vyanzo vya fedha ili waweze kukuza mtaji na kutoa mikopo kwa wakulima kwa masharti nafuu katika kumfanya mkulima kuweza kunufaika kilimo chake.

  "TADB ina deni kubwa kwa wakulima sasa ni wakati umefika wa bodi kufanya kazi kwa uadilifu katika kuinua sekta ya kilimo kwa kutoa mikopo na sio kwa bodi kufanya mikutano nje ya nchi na kuacha kutatua changamoto ya mikopo katika sekta hiyo" amesema Dk. Ashantu.

  Nae Mweenyekiti wa Bodi hiyo, Rosebudy Kurwijla ameiomba serikali kuiwezesha benki ili kuweza kufikia wananchi waliowengi na wanahitaji ya kukopeshwa na TADB katika kuendeleza kilimo.
  Amesema kilio cha TADB ni mtaji na bila kufanya hivyo itakuwa ni vigumu kuwafikia wananchi waliowengi.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas Samkyi amesema mpango wao ni kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika  katika kuweza kupata mtaji wa kuweza kuwakopesha wakulima ili kuweza kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.
  Mwenyekiti wa Bodi wa TADB, Rosebudy Kurwijila akizungumza katika uzinduzi juu ya majukumu ya bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Fedha, Uchumi na Mpango, Ashantu Kijaji akizungumza wakati uzinduzi wa Bodi ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Ashantu Kijaji akipokea mfano wa hundi ya Sh.milioni tano kwa ajili ya tetemeko la Ardhi mkoani Kagera leo jijini Dar es Salaam.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  SHIRIKISHO la Mpira Wa Miguu Tanzania (TFF)  limefunguka kuhusu jambo hilo la klabu ya Yanga kukodishwa kwa kampuni ya Yanga Yetu inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Yusuph Manji.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amezungumza kuhusu mabadiliko ambayo wameyafanya na kusema wao kama TFF bado hawajayatambua mabadiliko hayo na wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit ya kumtaka aonyesha mkataba ambao wameingia na kampuni ya Yanga Yetu.

  Mwesigwa amesama kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Yanga atupe nakala ya mkataba ule wa Yanga na Kampuni ya Yanga Yetu ili kama kuna wasiwasi hilo tatizo lishughulikiwe mapema maana hizi klabu ni za wanachama na wanaweza kuingia mikataba na wanachama wengine wakaja na mambo mengine.

  “Tunataka mkataba uwe wazi ili hata klabu zingine zijifunze, kwahiyo Yanga tumewaomba walete copy ya huo mkataba nini kinaazimwa na kipi kinauzwa, klabu itaendeshwaje na baada ya hapo kamati za TFF zitakaa kulijadili jambo hilo, kama itakuwa tofauti na kanuni zetu tutarudi kwao warekebishe mambo ambayo hayapo sawa,” amesema Mwesigwa.

  Mwesigwa amesema uendeshwaji lazima ubadilike kuendana na wakati lakini hatutaki mabadiliko yasababishe mvurugano ambao haukuwepo kwa muda mrefu na tumeshapokea barua nyingi za wanachama wa Yanga hadi wazee wamekuja wanasema wanataka kwenda kumwona mkuu wa nchi.

  Aidha amesema TFF bado inatambua Yanga inasimamiwa na uongozi wa klabu kama ilivyokuwa awali ikiongozwa na Mwenyekiti, Yusuph Manji na kama kutakuwa na jambo la tofauti watatoa taarifa baada ya kujiridhisha mfumo ambao Yanga itakuwa inautumia kukodisha timu kwa Kampuni ya Yanga Yetu.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe Augustine Mahiga yupo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 10 hadi 13 Oktoba, 2016.

  Mhe. Mahiga ambaye anaongoza ujumbe wa Mawaziri wa Asasi hiyo yupo nchini humo kwa maagizo ya Mwenyekiti wa Asasi, Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kutathmini hali ya siasa ilivyo nchini humo ili kushauri ipasavyo.

  Aidha, tathmini hiyo inafanyika kufuatia hali tete ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama nchini DRC iliyochangiwa na maandamano yaliyofanyika tarehe 19 Septemba, 2016 ambayo yaliandaliwa na vyama vya upinzani kwa lengo la kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya DRC (CENI) kutangaza tarehe ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu. 
  Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa sita kushoto) akiongoza kikao cha pamoja cha Mawaziri kilichofanyika katika Hoteli ya Pullman, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Wengine katika picha upande wa kulia ni Mabalozi wa Nchi wanachama wa SADC wanaowakilisha nchi zao DRC. 
  Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (wa tatu kulia) akiongoza ujumbe wa SADC katika kikao alichokifanya na Mhe. Raymond Tshibanda (wa nne kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC ambaye aliongozana na viongozi wa juu wanaoratibu uchaguzi nchini DRC. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, SAME
  MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Rosemary Staki Semanyule, (pichani), amesema wilaya yake inazo fursa za kutosha hususan kilimo cha Tangawizi na kuukaribisha Mfuko wa Pensheni wa PPF kujenga kiwanda cha kuchakata Tangawizi, ili kuongeza thamani ya zao hilo.Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo katika mazungumzo mafupi na MenejaUhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele, aliyemtembelea ofisini kwake Oktoba 10, 2016.
  “Same tunalima Tangawizi kwa wingi, wakulima hawapati faida ya kutosha kwa vile wanauza mara tu wanapovuna, tunahitaji viwanda vya kuchakata Tangawizi ili iwe katika mfumo wa unga (powder) na itakuwa rahisi kusafirisha nje na kuuza kwa bei ya juu zaidi na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima wetu.” Alisema Bi Staki.Bi. Staki pia alisema, ukiacha wananchikujishughulisha na zao hilo, pia Same wanalima mazao ya chakula kwa wingi.
  Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, alisema, PPF inaendelea na kampeni yake ya kuongeza wanachama hususan kupitia mpango wa “Wote Scheme” unamuwezesha Mfanyakazi wa sekta rasmi na isiyo rasmi, (wajasiruimali) kujiunga nao.
  “ Wote Scheme, ni mpango utakaowafaa sana wajasiriamali, ambao ni wakulima, waendesha bodaboda, mama lishe na baba lishe.” Alisema Bi Mengele.Akifafanua zaidi, Bi.Mengele alisema, Mwanachamaaliyejiunga na mpango huo, atafaidika na Mafao mbalimbali na kubwa zaidi ni kupata Bima ya Afya.
   Mkuu wa Wilayaya Same, mkoani Kilimanjaro, Bi. Rosemare Staki Senyamule, (kulia), akimkaribisha ofisini kwake, Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele Oktoba 10, 2016

  0 0

  Katika kusheherekea siku ya mtoto wa kike kimataifa, ninawaletea kisa kifupi chenye mafunzo muhimu kwa wasichana wote duniani, kisa hichi ni cha MAYA.

  Maya ni binti wa miaka 12 aishie na wadogo zake wawili wa kiume katika familia maskini. “Ndoto” yake ni kuwa mwalimu ili kuisaidia jamii yake. Umasikini wa familia yake wamfanya Maya kukaa nyumbani na wadogo zake kwenda shule. Ndoto yake imevunjika. 

  Maya hana elimu wala ajira (takwimu zaonyesha 1/3 ya wanawake Tanzania hawajasoma).

  Maya anajihatarisha kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI (huku asilimia 40 tu ya wasichana umri kati ya 15-19 wakiwa na elimu juu ya ugonjwa huu) au mimba ya utotoni kwa kujiuza ilia apate chakula, hifadhi na ulinzi.

   Anapata uja uzito akiwa na miaka 16 (huku ¼ ya wasichana kuaniza umri wa miaka 15 ni wazazi watoto). Anajifungua kwa matatizo mtoto Maryam ambapo anaamua kubadili msimamo wa maisha yake.

  Maya anajihusisha na kazi za kuajiriwa na biashara ndogo, anafanikiwa kufungua mgahawa. Sasa anaweza kumpeleka Maryam shule.

  Maryam anasoma kwa bidii na kupata udhamini wa kwenda chuo ambapo anafanikiwa kuhitimu kama Mwalimu. Mustakabali wake sasa uko mikononi mwake tofauti na ule wa Maya, na sasa Maryam anaweza kusaidia jamii yake, ndoto ambayo alikuwa nayo mama yake.

  Kumbuka: Ukimuelimisha mwanaume unamueleimisha mtu mmoja, ukimuelimisha mwanamke basi unalielimisha Taifa!
  Tazama video hii fupi hapa chini upate kuelimika.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Sheria namba 1.
  5: Goal Area
  Ni mistari miwili iliyochorwa ndani ya eneo la goli ikiwa ni 5.5m sawa na 6yadi

  6:Penalty area
  Ni eneo la ndani ya boksi ambalo ni 16.5m sawa na 18yad ambapo ndani ya eneo hilo kuna alama ya penati inayotumika kuweka mpira.

  *penalt mark
  Katika eneo la penati alama ya kupigia ipo katikati ya eneo la 18 lakini lenyewe ni 11m sawa na 12yad.

  *penalty arch 
  Ni eneo ambalo mchezaji atakapokuwa anapiga penati asivuke nusu duara lilipo nje ya boksi na akivuka hapo penat itarudiwa.

  7: The Corner Area
  Linajulikana kama eneo la kona na likitambuliwa kwa alama ya nusu duara kutoka katika mti kibendera ambapo urefu ni sawa  1yad.

  8:Flagposts

  Ni kibendera kinachotumika katika kila kona ya uwanja na kisheria kinatakiwa kuwa futi 5 kwenda juu.
  . katika Uwanja una uwezo wa kuweka vibendera 6 katila kila alama.

  9:Technical Area
  Ni sehemu wanayokaa benchi la ufundi na wachezaji wa akiba. Katika eneo hilo haruhusiwi mtu asiye ndani ya benchi la ufundi au kiongozi kuingia au kukaa.

  *1m kutoka touchline kutakuwa na mstari utakaotambulisha mwisho wa mtu yoyote kutoka benchi la ufundi kuvuka ambao uoana wake unaendana sambamba na mistari yote ya uwanjani.

  10: Goals
  Goli linajumuisha milingoti miwili iliyo nyoofu kwenda juu na mmoja uliolala ikiunganisha milingoti miwili na kupata mfano wa umbo la mstatili  ambapo milingoti hiyo lazima iwe meupe na vipimo sawa  vya 12cm sawa na 5Inchi.

  *Urefu wa mlingoti wa juu uliolala ni 7.32 sawa na  8yadi ambao ni kutoka mlingoti mmoha hadi mwingine.

  *urefu kutoka mlingoti nyoofu kuanzia chini mpaka juj ni 2.44m sawa na 8ft.

  *Kama mti wa goli ukichomoka basi mpira utasimama mpaka pale utakaporekebishwa.

  Kipengele cha 11 Goal line technology (ni kipana zaidi)

  12: Commercial Adv 
  Matangazo yote yanatakiwa yakae 
  1m kutoka  touchline , goal line na goal net hayaruhusiwi kukaa ndani ya maeneo ya Uwanja.

  13: Logos And Emblems
  Itaendelea sehemu ya tatu.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango

  Benny Mwaipaja, MoFP, Washington DC, Marekani
  SERIKALI ya Japan, kupitia Shirika lake la Maendeleo-JICA, imeahidi kuongeza kiwango cha ruzuku kwa serikali ya Tanzania ili kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo kilimo, Maji, miundombinu ya barabara na huduma nyingine za jamii ili kuisaidia kufikia maendeleo yaliyokusudiwa kwa wananchi wake.

  Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Jijini Washington DC, nchini Marekani.

  “Kabla ya mwaka 2013 tulikuwa tunatoa ruzuku ya dola milioni 1 kwa Tanzania kila mwaka, lakini kuanzia mwaka 2013 tumeongeza kiwango hadi kufikia dola milioni mia 3 kila mwaka na tunatarajia kuongeza kiwango hicho siku za hivi karibuni” aliongeza Makamu huyo wa Rais wa JICA
  Kato amesema kuwa Tanzania na Japan ni marafiki wa muda mrefu na kwamba nchi hiyo itaendelea kuisaidia kwa kutekeleza miradi mbalimbali yenye kuleta tija kwa uchumi wa nchi na maisha ya watanzania kwa ujumla.

  “Hivi sasa tunataka kuanza kutekeleza awamu nyingine ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha zao la mpunga ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo ni muhimu sana” Aliongeza Kato.

  Amesema kuwa Japan pia imeamua kuongeza kiwango cha ufadhili kwa Bara la Afrila kutoka Dola Milioni 13 ambazo nchi hiyo ilikuwa ikitoa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2013 hadi kufikia dola elfu 30 kwa mwaka kuanzia mwezi Agosti, 2016 kwa kipindi cha miaka 3 ijayo.

  Amesema pia kuwa ili kuwajengea uwezo na ujuzi vijana wa kiafrika, Japan imeanzisha program ya kutoa elimu ambapo hivi sasa vijana 60 kutoka nchi mbalimbali za kiafrika wamepelekwa nchini humo kujifunza kwenye vyuo vilivyoko huko na watapelekwa kwenye kampuni na mashamba makubwa yanayojihusisha na kilimo ili waweze kupata uzoefu na kuwa chachu ya mabadiliko watakaporejea katika nchi zao.

  Akiongea na Makamu huyo wa Rais wa Shirila la Maendleo la Japan-JICA, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Japan kwa kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbalimbali za kiuchumi na kijamii.

  Ametaja baadhi ya miradi ambayo nchi hiyo inafadhili nchini Tanzania kuwa ni ujenzi wa barabara ya Arusha hadi Holili hadi Taveta nchini Kenya, Ujenzi wa barabara ya Juu (Flyover) ulioanza eneo la Tazara ili kupunguza msongamano Jijini Dar es salaam, miradi ya maji na kilimo cha umwagiliaji.

  “Asilimia 75 ya wananchi wetu wanategemea kilimo kwahiyo uamuzi wa Japan wa kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi ya kilimo cha umwagiliaji ni jambo tunalolipongeza kwasababu kilimo kitakuwa na tija na kitaendeshwa kibiashara” Alisema Dkt. Mpango.

  Ameishukuru pia serikali ya Japan kwa kufanya utafiti na upembuzi yakinifu wa mradi wa kudhibiti mafuriko ya mto Kondoa, eneo la mkoa wa Morogoro ili kudhibiti mto huo usiharibu miundombinu ya reli ya kati.

  “Mradi huu ni muhimu sana kwasababu serikali imekuwa ikiingia hasara karibu kila mwaka kukarabati njia hiyo ya reli baada ya kusombwa na maji, hivyo tunaishukuru Japan kwa kutusaidia kufanya utafiti huo ambao utasaidia kukabiliana na hali hiyo” aliongeza Dkt. Mpango
  Ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kukusanya kodi na kuziba mianya ya upotevu wa fedha za serikali ikiwemo kuanzisha mahakama maalumu ya kushughulika na mafisadi ili kuleta nidhamu katika utumishi wa umma.

  0 0

   Na Ramadhan Ali/Maelezo Zanzibar      

  Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) imekanusha tuhuma zinazotolewa kuwa imesajili meli za Korea Kaskazini kinyume na Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi Machi mwaka huu za kuzikatalia usajili Kampuni za meli za nchi hiyo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurgenzi Mkuu wa ZMA Abdalla Hussein Kombo amesema tuhuma hizo zilizotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uchambuzi wa Taasisi ya NK News kupitia Jarida la NK Pro la Mjini Seoul, Korea Kusini sio za kweli.

  Amesema ZMA baada ya kupata taarifa ya Azimio hilo iliunda Kamati ya wataalamu kulifanyia uchambuzi na kutoa mapendekezo kwa Mamlaka juu ya hatua za kuchukuliwa."Azimio hilo limetaja majina ya meli 31 za Korea Kaskazini ambazo nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania, inazitaka kuzifutia usajili au kutozisajili," alisema Mkurugenzi Mkuu ZMA.

  Aliongeza kuwa ZMA ilifanya uhakiki wa meli zote zilizosajiliwa na Mamlaka hiyo na orodha ya meli zilizoainishwa kupitia Azimio hilo na kubaini kuwa meli moja yenye jina la First Cleam ilikuwa imesajiliwa kabla ya vikwazo vya usajili wa meli za Korea Kaskazini lakini ikaamua kuifutia usajili.

  Amesema kuanzia wakati huo, Mamlaka haijawahi kusajili meli yeyote ambayo ilikuwemo katika orodha iliyotolewa na Umoja wa Mataifa na imekuwa ikichukua tahadhari kubwa katika usajili wa meli.
   Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibari  (ZMA) Abdallah Hussein Kombo akizungumza na  waandishi wa Habari  kukanusha tuhuma za kusajili Meli za Korea ya Kaskazini kinyume na Azimio la Baraza  la Usalama la Umoja wa Mataifa.
   Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini  Abdallah Hussein Kombo wakati alipokutana nao Ofisini kwake Malindi .
  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji  Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe  akitowa ufafanuzi  wa masuala yaliyoulizwa na Waandishi wa Habari katika Mkutano huo. (Picha na Miza Othman Habari Maelezo Zanzibar).  0 0

  UMOJA wa Vjana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umelihimiza Jeshi la polisi nchini kutambua kuwa ujambazi, wizi wa kutumia silaha na uporaji bado ni tatizo linalohitaji kushughulikiwa kwa nguvu zote kama ambavyo nchi ilisimama na kutekeleza operesheni mbalimbali za ukombozi.

  Pia, umesisitiza kuwa usalama wa raia na mali zao unahitaji kulindwa ili kuepusha vifo, hasara, unyang’anyi wa mali na vilema vya maisha kutokana na matukio yanayoweza kuwakumba wasio na hatia mijini na vijijini.Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alieleza hayo jana alipomtembelea kumjulia hali majeruhi Said Ally, Mabibo Hostel.

  Saidi alijeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwa ni pamoja na kutobolewa macho katika tukio wizi wa kutumia silaha Buguruni mjini Dar es Salaam, Septemba mwaka huu.Shaka alisema tatizo la uhalifu, unyang’anyi, uporaji na ukwapuaji mali kwa kutumia nguvu na silaha, linahiaji kutazamwa kwa kina na upana unaostahili na vyombo vyenye dhamana vinavyosimamia usalama wa raia na mali zao.

  Alisema kuna haja ya polisi kubuni mbinu mpya za kukabiliana na makundi ya wezi, waporaji na majambazi kabla hawajaleta madhara na hasara kama ilivyomtokea Said ambaye sasa ni amesababishiwa ulemavu wa kudumu wa kutoona.“Kila siku mbinu za uhalifu, ujambazi, wizi wa kutumia nguvu na silaha hubadilika, jukumu la kupambana na matukio hayo hatari ni la polisi kwa kushirikiana na raia wema, janga hili likiachwa wananchi wataishi kwa mashaka na hawatajituma kujiletea maendeleo,”alisema Shaka.

  Alisema ikiwa wananchi wanajituma kwa bidii kutafuta fedha na kubuni miradi ya kiuchumi halafu majambazi na wanyang’anyi wanapora na kumfilisi aliyetafuta ndani ya saa chache, hilo linaweza kuwatia hofu mwananchi na wajasiriamali na kuwafanya washindwe kujituma kikamilifu jambo ambalo litakuwa na madhara makubwa katika kuzalisha mali na kukuza uchumi.

  Akizungumza kwa masikitiko na huzuni kubwa , Shaka alisema tamaa ya kupata utajiri kwa njia haramu kwa mtu mmoja mmoja au kikundi, kumemsibaishia hasara ya maisha dhidi ya Said ambaye kwa sasa amekoseshwa uwezo wa kuendelea kupiginia maendeleo yake ya kiuchumi na taifa kwa ujumla.  0 0

  Mwashungi Tahir na Fatma Makame/Maelezo Zanzibar

  Waziri wan chi ofisi ya makamo wa pili ya rais Mohammed Aboud Mohammed amesema uchumi wa Zanzibar     unazidi kuimarika kwa karibu ya asilimia saba na mfumuko wa bei bado upo kwenye tarakimu  moja na  pato la Taifa linazidi kukua.

  Ametoa maelezo hayo  ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi Serikali ya awamu ya saba kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein.

  Amesema katika awamu hii kwa ujumla harakati za uchumi zinaendelea vizuri na ishara zote za kuimarisha uchumi katika mwaka huu wa fedha zinatoa sura nzuri za mafanikio.

  Akizungumzia  suala la Muungano amesema unaendelea kuimarika na  vikao mbali mbali vya watendaji wakuu wa pande mbili wakiwemo  mawaziri vimeshafanyika na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ameshafanya vikao viwili vya kisekta kwa nia ya kutatua changamoto zilizopo.

  Waziri Aboud ameelezea kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekamilisha kazi ya kuipandisha hadhi iliyokuwa Idara ya upigaji chapa na mpigaji chapa mkuu wa serikali na kuwa wakala wa serikali wa uchapaji.

  Aidha amesema kazi ya kufunga mitambo mipya ya uchapaji imekamilika na mafundi wa kiwanda hicho wanaendelea kupatiwa mafunzo ili kuimudu teknolojia mpya ya mitambo hiyo ili kuongeza ufanisi  na kuongeza upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati.

  Sambamba na hayo Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kupitia Tume ya kitaifa ya kuratibu na udhibiti madawa ya kulevya imepania kutoa athari za madawa ya kulevya kwa jamii.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akitoa tarifa ya mafanikio ya Ofisi yake kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
   Wandishi wa habari wakifuatilia tarifa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa na mazungumzo nao  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa akijibu maswali ya wandishi wa habari katika Mkutano wake Ofisini kwake Vuga.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Wadau Iddi Janguo and Munira Kitundu wakipozi kabla ya kuelekea kwenye mnuzo viwanja vya Karimjee Hall jijini Dar es salaam baada ya kumeremeta wikiendi iliyopita.

  0 0


  0 0

  SEHEMU ya tatu ya Wanafunzi 220 waliochaguliwa kusoma kwa Scholarship nje ya Nchi chini ya udhamini wa Universities Abroad wameondoka kwenda Nchini China na Uingereza.
  Wanafunzi hao 35 wengi wao wakiwa kwenye fani ya Udaktari, Uhandisi na Biashara za Kimataifa watalipa ada ya mwaka mmoja tu wa kozi na wengine wakigharamia asilimia 50 ya gharama zote.

  Taasisi ya UAL inaendelea na udahili kwa wanafunzi watakaokwenda Novemba na Februari 2017 katika ofisi zao zilizopo Posta Mpya jengo la  Benjamini Mkapa Tower na Ofisi ya Kanda- Mwanza, Kenyatta Road na Exim Bank Ghorofa ya pili.


  Wanafunzi waliopata ufadhili wa Universities Abroad Link wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi, walezi wao wakati wa kuwaaga Uwanja wa Ndege.
  Mkurugenzi wa Taasisi  ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Ndegewa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa kuwaaga wanafunzi 220 waliopata udhamini  wa masomo kutoka Universities Abroad Link. (Picha na Francis Dande).
   Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0
  0 0


  Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Paulina Mashauri, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.
  Na BMG
  Haleluya Benjamin ambaye ni Katibu wa baraza la Watoto mkoani Mwanza, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.
  Mwanafunzi James John kutoka shule ya msingi Kitangiri A Jijini Mwanza akizumzia Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha ambapo amesema haungi mkono baadhi ya vitendo wanavyofanyiwa watoto wa kike ikiwemo unyanyasaji kama vile ubakaji, mimba na ndoa za utotoni.
  Msimamizi wa Watoto Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Karus Masinde, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali.

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushoto akibadilishana mawazo na Uongozi Mpya wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN) ulioambatana na Uongozi wa Gazeti la Zanzibar Leo mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
   Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN) Dr. JimYonazi wa Tatu kutoka Kushoto akifafanua jambo wakati Ujumbe wake ulipofanya mazungumzo na Balozi Seif.
   Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Zanzibar leo Nd. Yussuf Khamis wa kwanza Kutoka kushoto akimsikiliza kwa Makini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif hayupo pichani wakati wa mazungumzo yao.
  Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN) Dr. JimYonazi wa kwanza kutoka kulia akifuatilia mazungumzo ya Uongozi wake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif. Picha na – OMPR – ZNZ.  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0
 • 10/11/16--11:58: Article 7

older | 1 | .... | 1387 | 1388 | (Page 1389) | 1390 | 1391 | .... | 3285 | newer