Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1386 | 1387 | (Page 1388) | 1389 | 1390 | .... | 3348 | newer

  0 0  0 0


  Bondia nyota nchini, Abdallah “Dulla Mbabe” Pazi atapanda jukwaani Oktoba 28 kupambana na bondia kutoka China, Zheng Chengbo katika pambano la kimataifa uzito wa Super Middle. Mbali ya Mbabe, bondia mwingine wa Tanzania, Ibrahim Class ambaye ni bingwa wa kimataifa wa World Professional Boxing Federation (WPBF) na Universal Boxing Organization (UBO) naye atapanda ulingoni kuwania ubingwa wa kimataifa wa WBF kwa kupambana na bondia kutoka Afrika Kusini Bedeman ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa light wa vyama vya WBA na IBO. 

  Akizungumza jijini jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hall of Fame Boxing Promotions Jay Msangi alisema kuwa mapambano hayo yatafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall na mabondia hao watawasili nchini wiki moja kabla ya pambano.
  Msangi alisema kuwa maandalizi ya mapambano hayo yamekamilika na mabondia wote walikuwa kwenye maandalizi makali chini ya makocha wao. 

  Alisema kuwa Mbabe kwa sasa anasimamiwa na kocha wake, Shomari Kimbau wakati Class yupo chini ya kocha nyota nchini, Habib Kinyogoli na bingwa wa zamani wa Dunia, Rashid Matumla. “Maandalizi yapo vizuri na mabondia wote wapi katika morali ya juu, Mbabe anataka kudhihirisha ubora wake nchini katika uzito wa Super Middle kwa kumchapa Mchina ambaye kwa sasa yupo katika timu ya Olimpiki ya China na ni moto wa kuotea mbali,” 

  “Class baada ya kumchapa Cosmass Cheka na kutwaa ubingwa wa UBO mwaka huu na kuchmapa Mzambia Mwasa Kabinga kwa TKO raundi ya tisa, sasa anataka kuonyesha kuwa ni nyota mpya ya ngumi za kulipwa nchini kwa kumchapa bondia huyo wa Afrika Kusini,” alisema Msangi. Kwa upande wake, Mbabe alisema kuwa amejiandaa vizuri na anasubiri siku ya pambano lenyewe ili kuwapa raha Watanzania. 

  “Namsubiri Mchina kwa hamu sana, hatofika raundi ya tatu, sitataka adumu jukwaani kwa zaidi ya dakika 15,, nataka kumpa kipigo cha kihistoria ili aende kuwaambia wenzake kuwa kuna bondia hatari sana na wa kuogopwa hapa nchini,” alisema Mbabe. 


  Class alisema kuwa hana shaka na pambano na ushindi ni jadi yake. “Nipo fiti kwa ajili ya pambano, nipo tayari kwa changamoto, najua naye anajiandaa kama mimi, sitawaangusha Watanzania siku hiyo,” alisema Class.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hall of Fame Boxing Promotions Jay Msangi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na pambano la bondia Ibrahim Class ambaye atapambana na bondia Jason Bedeman wa Afrika Kusini kuwania mkanda wa Light wa uzito wa Chama Cha WBF na Abdallah Pazi (Dulla Mbabe) ambaye atapambana na bondia , Zheng Chengbo wa China katika pambano la kimataifa. 
  Bondia Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ (kulia) akizungumza katika mkutano huo. Pazi atapambana na bondia Zheng Chengbo wa China katika pambano la kimataifa la uzito wa Super Middle. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotions, Jay Msangi 
  Bondia Ibrahim Class (kulia) akizungumza katika mkutano huo. Class atapambana na bondia Jason Bedeman wa Afrika Kusini kuwania mkanda wa Light wa uzito wa Chama Cha WBF. Kushoto ni bondia Abdallah Pazi 

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akisoma tamko la kupinga adhabu ya kifo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio na kushoto ni Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga.
  Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
  Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga akizungumza katika mkutano huo.

  Na Dotto Mwaibale.
  KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefungua kesi ya kikatiba kuhusiana na ulinzi wa haki ya kuishi na urekebishwaji wa sheria ya kanuni ya adhabu juu ya ulazima wa kutolewa kwa adhabu ya kifo katika makosa ya uhaini na mauaji.

  Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali wakitaka ufafanuzi zaidi juu ya adhabu ya kifo, wakibainisha kuwa adhabu hiyo haimpi nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi.

  Kituo hicho kimesema endapo Tanzania itatekeleza hukumu ya kifo kwa sasa inamaanisha watu wapatao 228 na zaidi watapoteza maisha yao huku wengine 244 wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.

  Akizungumza wakati akitoa tamko la kupinga adhabu ya kifo Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen- Kijo Bisimba alisema hadi mwaka 2015 jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa.

  Alisema kituo kinaiomba serikali kurekebisha sheria ya kanuni ya adhabu na sheria ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, uhaini na ugaidi.

  Dk. Bisimba alisema kituo kina sababu za kupinga adhabu hiyo ya kifo na hawafurahii watu kuua wengine na ndio maana hawapendi pia hata muuaji auawe.

  “Adhabu ya kifo ni vigumu kuhakikisha kuwainatekelezwa tu kwa wale watu ambao huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na mianya ya makosa na hivyo maisha ya mtu yanaweza kupotea bure,” alisema Dk. Bisimba na kuongeza kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inaweza kuzuia watu wengine kutokutenda makosa kama hayo.

  Alisema licha ya adhabu hiyo kutokutekelezwa nchini kwa takriban miaka 22 , taaarifa zinaonesha kuwa watu 72 ambao walishawahi kunyongwa kutokana na adhabu hiyo.

  Hata hivyo aliiomba serikali kutengeneza utaratibu wa kuelimisha jamii juu ya kuheshimu haki za binadamu hususani haki zakuishi na kuweka mazingira ya kuiheshimu haki hiyo, pia ibadilishe sheria kwa kuondoa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na kwa wafungwa waliopo mfano vya muda mrefu gerezani.

  0 0

  Ally Daud-MAELEZO.
  MFUMUKO wa bei wa umeshuka kwa asilimia 4.5  mwezi Septemba kutoka asilimia 4.9 ya mwezi Agosti mwaka huu kutokana na kupungua kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi uliopita.

  Hayo yamebainishwa na  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Ephraim Kwesigabo (Pichani)wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

  Kwesigabo amesema kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei kumetokana na kupungua kwa kasi ya upandajiwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali ikilinganishwa na Mwezi Agosti .
  “Mfumuko wa bei mwezi Septemba umeshuka ukilinganisha na mwezi Agosti kutoka asilimia 4.9 hadi kufika asilimia 4.5 kutokana na kushuka kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma”. Alisema Bw. Kwesigabo.

  Aidha aliongeza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji Baridi vimepungua hadi kufika asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 mwezi agosti mwaka huu.

  Kwesigabo amesema kuwa ushukaji huo wa bei za vyakula na vinywaji baridi umetokana na kupungua kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoisha kwa mwezi Septemba mwaka huu.

  Mbali na hayo Kwesigabo amesema kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania imefikia shilingi 97.4 katika kununua bidhaa na huduma kwa mezi septemba ikilingfanishwa na shilingi 96.83 mwezi Agosti.

  Aidha Mkurugenzi Kwesigabo amesema kuwa anawaomba wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Ofisi za takwimu Za Mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwi,u mbalimbali kwa maendeleo ya nchi yetu.

  0 0

  Na Ally Daud-MAELEZO

  DAWA muhimu za binadamu zinapatikana kwa wingi katika Bohari kuu ya dawa MSD kwa masaa 24 zikiwemo dawa za kutibu Malaria, Kifua kikuu, Ukoma ,ARV , dawa za kutuliza maumivu pamoja na Anti- biotic ili kutimiza na kutekeleza sera ya mpango wa Afya wa awamu ya tano.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ili kuzungumzia hali ya upatikanaji wa dawa na chanjo nchini.

  “Dawa zote muhimu kwa binadamu zinapatikana kwenye bohari kuu ya dawa kwa masaa 24 kinyume na watu na Taasisi zisizo za kiserikali kusambaza maneno kuwa MSD imeishiwa dawa kitendo ambacho sio cha kweli dawa zipo na zinasambazwa kwenye vituo vyote vya afya” Alisema Mhe. Ummy.

  Aidha Ummy amesema kuwa ili kutekeleza mpango wa sera ya afya ya Serikali ya tano ,jumla ya shilingi bilioni 251 zimetengwa ili kuweza kuhakikisha dawa za binadamu zinapatikana kila wakati pindi zinapohitajika kutoka MSD ili kutoa huduma bora kwa watanzania.

  Aliongeza kuwa Serikali imetenga Bilioni 85 kwa ajili ya kulipa deni linalodaiwa na MSD ili kuhakikisha Bohari hiyo inajiendesha vizuri na kutokaukiwa dawa pindi zinapohitajika katika vituo vya afya na kutoa huduma za matibabu kwa muda muafaka kwa watanzania.

  Mbali na hayo Waziri huyo amesema kuwa tatizo la chanjo kwa sasa limepata ufumbuzi kwani zimeagizwa chanjo za watoto za kifua kikuu dozi milioni 2, chanjo za Pepopunda dozi milioni 1.2 na chanjo za Polio ambazo ni dozi 2 ili kuimarisha hali ya matibabu nchini.

  “Tulikuwa na tatizo la chanjo kama wiki nne zilizopita lakini tumejitahidi na tumeweza kuleta chanjo zote muhimu pamoja na kuagiza chanjo za surua ambazo zinatarajiwa kuja hivi karibuni ili kuhakikisha chanjo zinapatikana kwa wingi nchini” alisisitiza Waziri huyo.

  Aidha amesisitiza kuwa wanahitaji kununua na kufanya uzalishaji wa dawa katika viwanda vya ndani ili kuweza kuchangia uchumi wa viwanda vya ndani ili tufikie uchumi wa kati.

  Waziri Ummy aliwataka Wakurugenzi wa Vituo vya Afya pamoja na Waratibu wa Afya wa Wilaya kuagiza dawa MSD mapema bila ya kusubiri ziishe kabisa kwenye vituo vyao ili kuweza kuondoa usumbufu kwa wagonjwa.

  0 0

  Na Daudi Manongi,MAELEZO. 

  Wizara ya Fedha na Mipango imeanza zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na wizara hiyo katika mkoa wa Pwani, Kibaha. Uhakiki huu hautausisha wastaafu wanaolipwa kupitia mifuko ya hifadhi za jamii kama vile PSPF, NSSF, PPF na GEPF.

  Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mpango huo wa uhakiki ulioanza leo mkoani Pwani.

  “Uhakiki huu unatokana na utaratibu uliojiwekea Wizara ya Fedha na Mipango wa kufanya uhakiki wastaafu ili kuhuisha orodha ya malipo ya wastaafu na inasaidia kubaini mabadiliko ya taarifa za wastaafu kama vile kufariki na hivyo kuepuka kulipa wasiostahili”Alisema Bw.Mtonga.

  Aidha akizungumzia kuhusu utaratibu wa uhakiki huu amesema kuwa zoezi hili litafanyika nchi nzima na limeanzia katika Mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha na litafanyika kuanzia leo tarehe 10 mpaka tarehe 14 mwezi huu na kuendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa pwani mpaka tarehe 21 mwezi huu.

  Baada ya uhakiki katika mkoa wa Pwani zoezi litaendeshwa kikanda nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Songwe na Katavi kuanzia tarehe 31 Octoba mpaka tarehe 11 Novemba mwaka huu.

  Pia zoezi litafanyika katika kanda ya kati likijumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida kuanzia tarehe 21 mpaka 25 Novemba.

  Akizungumza na waandishi wa habari mwakilishi wa wazee wastaafu Bw.Benedict Kalaguza amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kufanya uhakiki huu wa wastaafu na kwamba zoezi limekuwa ni zuri lisilokuwa usumbufu wowote na limeboreshwa zaidi kwa kutumia teknolojia nzuri zaidi.

  Aidha Wastaafu wanaohakikiwa wanatakiwa kufika kwenye vituo hivyo wakiwa na nyaraka kama Kadi ya Benki, Picha za passport mbili, Barua ya Ajira ya Kwanza, Barua ya Kustaafu au kupunguzwa kazi kazini, barua ya Tuzo la Kustaafu, Nakala ya Hati ya Malipo ya kiinua mgongo au mkupuo, kitambulisho cha pensheni na barua ya Kudhibitishwa kazini.
  Mkaguzi wa Ndani wa Serikali Bi Joan John akimwelekeza Bw.Benedict kalaguza jinsi ya kujaza fomu za uhakiki wa wastaafu wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.Zoezi hilo limeanzia mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha leo na litafanyika nchi nzima. 
  Baadhi ya wastaafu mbalimbali wakiwa tayari kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki mkoani Pwani.Uhakiki huu unahusisha wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango Pekee.

  0 0


  SIMU.TV: Serikali inakusudia kuwepo kwa mpango wa uagizaji wa pamoja wa mbolea kama ilivyo mafuta ili kuweza kupanga bei elekezi. https://youtu.be/tvJ-CB08REk

  SIMU.TV: Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimeiomba serikali kufuta adhabu ya kifo kutokana na adhabu hiyo kuenda kinyume na haki za binadamu.https://youtu.be/M9Y0LB05Vo0

  SIMU.TV: Naibu waziri wa nchi TAMISEMI amefanya ziara katika shule mbalimbali wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam ili kujionea mafanikio yaliyopatikana katika kukabiliana na upungufu wa madawati. https://youtu.be/EFSZUp_OUKw

  SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekutana na mwenyekiti wa kampuni ya ujenzi ya CRCC ya China ambaye ameahidi kushirikiana na serikali katika kuboresha makao makuu ya nchi Dodoma. https://youtu.be/EXF6QqNSYsU

  SIMU.TV: Viongozi wa mila wa jamii ya kimasai wameaswa kusuluhisha migogoro ya ardhi pamoja na maeneo ya malisho ili kuondoa athari zinazosababishwa na migogoro hiyo.https://youtu.be/to1l10QkkNA

  SIMU.TV: Tanzania inaendesha utafiti wa mbegu mpya za mahindi zilizobadilishwa vinasaba ili kuwezesha zao hilo kuhimili hali ya ukame. https://youtu.be/8dRajuXwddc

  SIMU.TV: Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema inahakikisha visiwa hivyo vinajulikana kote duniani kutokana na kilimo na uzalishaji wa viungo. https://youtu.be/3N4629f6TFM

  SIMU.TV: Wakala wa usajili wa biashara na leseni BRELA umetoa muda wa miezi miwili kwa wafanyabiashara wanaotumia majina ya biashara kuyasajili. https://youtu.be/rW0u9Pgjvfc

  SIMU.TV: Klabu ya soka ya Simba ipo jijini Mbeya ikitarajiwa kushuka uwanjani jumatano hii kucheza na wenyeji wa mkoa huo Mbeya city. https://youtu.be/KQCrisrvUUo

  SIMU.TV: Pambano la ngumi la uzito wa juu kati ya bondia mtanzania Ibrahim Klass na bondia kutoka Afrika Kusini linatarajiwa kupigwa katika ukumbi wa Diamond jubilee tarehe 28.https://youtu.be/NYEphMJu1a0

  SIMU.TV: Timu ya JKT Mlale imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Polisi Moro kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza. https://youtu.be/TcJuNvNOTkY

  0 0


  0 0

  Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii
  MKUU wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (pichani) amepiga marufuku ukusanywanji wa ushuru wa biashara katika soko jipya la Pugu Kigogo fresh jijini Dar es salaam.
  Akizungumza wakati ya ziara yake katika Kata ya Pugu na Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam , Mjema alichukua hatua hiyo mara baada ya kusikiliza kero za Wafanyabiashara na Wananchi wa eneo hilo ambao walifika kumsikiliza katika mkutano uliofanyika Sokoni hapo.
  “Hapa kuna mambo mengi yanapswa kushughulikiwa hili pawe sawa hivyo Halamsahauri nawapa muda wa miezi mitatu wakurekebisha utaratibu huo hivyo kwa kipindi chote hicho ni marufuku kukusanya pesa kutoka katika soko hili mpaka hapo miundombinu mtakapo iweka sawa”amesema Dc Mjema.
  Aliongeza kuwa ni wajibu wa Halmashauri kutengeneza mazingira mazuri hili kuweza kurahisisha ufanyikaji wa biashara wenye tija ambao autarishi afya za watu na Mazingira kwa ujumla. 
  Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Wialya amefuta vikundi vyote vya ulinzi shiriki vya kata ya Pugu kwa kumtaka OCD wa kituo cha Staki Shari kusimamia agizo hilo hili kuweza kusuka upya mfumo wa ulinzi katika eneo kutokana malalamiko ya Wananchi wa kata hiyo
  Amesema kuwa wakazi wa kata ya Gongolamboto awana imani kabisa na vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyopo katika eneo hilo ndio maana anataka ufanyike utaratibu upya kwa mujibu wa katiba amabo utawasaidia kupata vijana walio waminifu.

  0 0

  Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unatarajia kukabidhi mchango wa maafa ya tetemeko la ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera baada ya siku ya awali iliyokuwa imepangwa ya Oktoba 14, 2016 ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kfo cha Mwalimu Nyerere kuingiliana na ratiba nyingine za kitaifa. 

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza katika mkutano wa wanachama jana alisema mpaka sasa fedha ambazo zinatarajiwa kukabidhiwa ni sh. 600,000 ambazo kati ya hizo 100,000 zimechangwa na wanachama katika mkutano huo.

  Alisema wakati maandalizi ya kukabidhi fedha hizo ukiendelea siku hiyo ambayo SHIWATA imetenga kwa ajili ya kufanya kazi za kumuenzi baba wa Taifa, Nyerere viongozi wa kitaifa ambao walikuwa wapokee mchango huo watakuwa mkoa wa Simiyu katika sherehe ya kuzima Mwenge wa Uhuru.

  Katika mkutano huo wanachama waliahidi kuendelea kuchangia matukio yote ya kijamii na wengi wameahidi kuwasilisha vifaa mbalimbali na nguo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.

  Wakati huo huo SHIWATA imetoa ofa ya Sh. Mil. 3.2 kwa wanachama wake watakaojenga nyumba za kuishi katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga. Akifafanua kuhusu ofa hiyo, Taalib alisema gharama za kusafirisha vifaa vya ujenzi, gharama za kusafisha eneo la kujenga na ekari moja ya kulima bustani watapewa bure.

  Alisema kasi ya wanachama kujenga na kuhamia kijijini inaridhisha mpaka sasa nyumba 200 zimekamilika na nyingine zinaendelea kujengwa. Taalib huduma za jamii kijijini hapo zinafanyiwa kazi ambapo huduma ya maji safi na salama ya kisima kirefu itapatikana mapema.
  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza na wanachama wa mtandao huo wakati wa mkutano wa kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi, Kagera.Picha na Mpiga picha wetu. 
  Mwanachama wa SHIWATA, Hamisi Kiondo akichangia hoja ya namna ya kusaidia waliopatwa na maafa Kagera. 

  0 0

  KAMPUNI ya Simba Motors imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunganisha magari aina ya pick-up ambacho kitaanza kuzalisha magari kabla ya Desemba 30, mwaka huu.
  Ahadi hiyo imetolewa leo mchana (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Jitesh Ladwa (kulia) mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.
  “Tumeamua kuunda magari aina ya pick-up kwa sababu ya mahitaji makubwa yaliyopo nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa mwaka Tanzania inanunua magari ya aina hii zaidi ya 4,000. Katika nchi za SADC mahitaji ni pick-up 35,000 kwa mwaka. Tutaanza na mtaji wa dola za Marekani milioni 200 na tumeomba ekari 200 katika eneo la EPZ,” amesema.

  “Eneo la kiwanda cha kuunganisha magari peke yake linahitaji ekari 50, kwa hiyo tukiweka na yadi za kupaki magari, eneo la viwanda vingine, eneo la kushusha na kupakia makontena yatakayokuwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani, ni lazima tutahitaji eneo kubwa zaidi,” amesisitiza.

  0 0


  0 0

   KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imesema itaendelea na utekelezaji wa kuboresha miundombinu ya mtandao wake wa simu za mezani, mkononi pamoja na huduma za data ili kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wake na kufikia kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano nchini. Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu 
   
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alipokuwa akizungumza na wateja mbalimbali kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa huyo wa TTCL, alisema kuwa maboresho ya miundombinu yanayofanywa kwa sasa katika shirika hilo yanaliwezesha kukabiliana na changamoto zilizokuwepo awali na kuwapa wateja weke fursa ya kufurahia huduma mpya na za zamani zinazotolewa kisasa na kwa umahiri mkubwa hivi sasa. 
   
  "Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inaendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wa simu za mezani, simu za mkononi na huduma za Data ili tuweze kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu na kufikia kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano," alisema Waziri Kindamba. 
   
  Aidha alifafanua kuwa TTCL inawaahidi wateja wake na taifa kwa ujumla kwamba itaendelea kutoa huduma bora, za uhakika na gharama nafuu katika kutengeneza mazingira mazuri ya kiteknolojia, kwani baada ya mabadiliko watumishi wake wameazimia kuongeza kasi ya kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu na uzalendo wa hali ya juu ili kwenda sambamba na mahitaji ya sasa na baadaye ya wateja wa sekta ya Mawasiliano.
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba akizungumza na wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki,ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Thomas Mushi (wa pili kulia) akipata picha na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Edwin Mashasi.


  0 0

  Watanzania wameungana na wenzao duniani kote kuadhimisha siku ya Afya ya Akili duniani huku Tanzania ikitajwa kuwepo kwa zaidi ya wagonjwa laki nne na nusu wanaougua maradhi hayo nchini. 

  Aidha mkoa wa Dar es salaam ndio unaongoza kwa kuwa na wagonjwa ambapo sababu kubwa inatajwa kuwa ni matumizi ya kupindukia ya madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na Bangi. Kadhalika, mkoa wa Dodoma watu 12 wanapokelewa kila siku katika hospitali ya rufaa ya wagonjwa wa akili ya Mirembe kutokana na tatizo hilo.

  Maadhimisho hayo ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma katika hospitali ya taifa ya magonjwa ya akili Mirembe ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 10 ya mwezi wa kumi. Kauli mbiu ya maandimisho hayo ni “utu katika afya ya akili, huduma za kisaikolojia na afya ya akili kuwa huduma ya kwanza kwa wote”

  Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme amewataka watanzania kuungana katika kupiga vita unyanyasaji na ukatili kwa wagonjwa wa akili na badala yake wapelekwe hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.

  Amesema tatizo la akili huathiri kufikiri,kuhisi,kutambua na kutenda na tatizo la akili kwa sasa linaongezeka ambapo takribani watu milioni 35 wanaishi na ugonjwa huo.
  Mkuu wa wilaya huyo amesema kwa mujibu wa taarifa ya akili na dawa za kulevya ya mwaka 2013/2014 za shirika la afya duniani(WHO)o mkoa unaoongoza kuwa na wagonjwa wengi ni Dar-es-salaam ambayo ina asilimia 2 ya wagonjwa ikifuatiwa na Mwanza yenye asilimia 1.2 huku mkoa wa mwisho ukiwa ni Rukwa wenye asilimia 0.2

  Naye Mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma, DK. James Kiologwe, amesema kwa mkoa wa Dodoma wagonjwa 1256 walipatikana katika kipindi cha mwaka 2015 na kila siku wanapokea wagonjwa 12 ambao wanaugua ugonjwa huo wa akili ambao wanatoka katika maeneo mbalimbali.

  Kwa upande wake, Mganga mkuu wa Hospitali ya rufaa ya wagonjwa wa akili Mirembe, Erasmus Mganga, ameeleza sababu kuu mbili zinazosababisha ugonjwa wa akili, kuwa ni ile ya mtu kuzaliwa na vinasaba vya ugonjwa huo ambapo vinakuwa ni vya kurithi na pia inatokana na magonjwa ambayo yanashambulia kwenye ubongo ambapo mtu anaweza kuugua ugonjwa wa Maralia, uti wa mgongo na mapafu ambapo huathiri ubongo.

  Amebainisha mgonjwa huyo akishatibiwa na kupona anabaki na tatizo kwenye ubongo na hivyo kupatwa na ugonjwa wa kichaa, kutokana na namna alivyoumwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhisho ya siku ya magonjwa ya akili Duniani iliyoadhimishwa katika hospitali ya rufaa ya maginjwa ya akili ya mirembe mjini Dodoma 
  Mganga mkuu hospitali ya rufaa ya magonjwa ya akili ya mirembe Dr Erasmus Mndeme akitoaa taarifa ya matatizo yanayochangia magonjwa ya akili wakati wa maadhimisho ya siku ya afya Duniani yaliyofanyika mkoani Dodoma leo katika hospitali hiyo. 
  Mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr James Charles akitoa maelezo kwenye maadhimisho ya siku ya afya ya akili Duniania iliyoaadhimshwa kitaifa katika hospitali ya rufaa ya magonjwa ya akili ya mirembe mjini Dodoma.


  0 0


  0 0


   Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea keshokutwa Jumatano Oktoba 12, 2016 kwa michezo saba huku ule mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukipangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini. 

  Kwa mujibu wa Kanuni ya 6 kipendelea cha kwanza, Young Africans wametambulisha Uwanja wa Uhuru kama uwanja wa nyumbani kwa sasa baada ya kuleta maombi Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) ambako baada ya kuyafanyia tathimini kwa mujibu kanuni hiyo ya sita, kipendelea cha sita, TFF imeiridhia klabu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, kutumia uwanja wa Uhuru.

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

  0 0
 • 10/10/16--13:18: Article 5

 • 0 0


  0 0

  Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unatarajia kukabidhi mchango wa maafa ya tetemeko la ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera baada ya siku ya awali iliyokuwa imepangwa ya Oktoba 14, 2016 ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa  Mwalimu Nyerere kuingiliana na ratiba nyingine za kitaifa. 
   Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza katika mkutano wa wanachama jana alisema mpaka sasa fedha ambazo zinatarajiwa kukabidhiwa ni sh. 600,000 ambazo kati ya hizo 100,000 zimechangwa na wanachama katika mkutano huo. 
   Alisema wakati maandalizi ya kukabidhi fedha hizo ukiendelea siku hiyo ambayo SHIWATA imetenga kwa ajili ya kufanya kazi za kumuenzi baba wa Taifa, Nyerere viongozi wa kitaifa ambao walikuwa wapokee mchango huo watakuwa mkoa wa Simiyu katika sherehe ya kuzima Mwenge wa Uhuru. 
   Katika mkutano huo wanachama waliahidi kuendelea kuchangia matukio yote ya kijamii na wengi wameahidi kuwasilisha vifaa mbalimbali na nguo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera. 
   Wakati huo huo SHIWATA imetoa ofa ya Sh. Mil. 3.2 kwa wanachama wake watakaojenga nyumba za kuishi katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga. 
   Akifafanua kuhusu ofa hiyo, Taalib alisema gharama za kusafirisha vifaa vya ujenzi, gharama za kusafisha eneo la kujenga na ekari moja ya kulima bustani watapewa bure. Alisema kasi ya wanachama kujenga na kuhamia kijijini inaridhisha mpaka sasa nyumba 200 zimekamilika na nyingine zinaendelea kujengwa. 
   Taalib amesema huduma za jamii kijijini hapo zinafanyiwa kazi ambapo huduma ya maji safi na salama ya kisima kirefu itapatikana mapema.
   Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza na wanachama wa mtandao huo wakati wa mkutano wa kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi, Kagera.
  Mwanachama wa SHIWATA, Hamisi Kiondo akichangia hoja ya namna ya kusaidia waliopatwa na maafa Kagera. 

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Itifaki Bw. James Bwana.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Oktoba, 2016 amepokea hati za utambulisho za mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
  Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.
  Rais Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.
  "Mhe. Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi asilia katika maadhi ya maeneo, ningependa uhusiano na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi"  amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.
  Dkt. Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na ufugaji.
  "Hivi sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.
  Aidha, Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.


  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam

  10 Oktoba, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.

older | 1 | .... | 1386 | 1387 | (Page 1388) | 1389 | 1390 | .... | 3348 | newer