Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MAELFU WASHIRIKI KATIKA MATEMBEZI YA AMANI YA SIKU YA ASHURA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Sheikh  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim (wa tatu kutoka kushoto) akiongoza matembezi ya Amani ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ni Imam Hussen (a.s) leo jijini Dar es Salaam. Siku ya mwezi 10 Muharram inajulikana kama ni siku ya Ashura. Imamu Husain (a.s.) aliuliwa kikatili pamoja na wafuasi wake wachache na ndugu zake. Masaibu haya yalitokea zaidi ya miaka 1300 iliyopita huko Kerbala (karibu na mji wa Baghdad katika nchi iitwayo Iraq hivi sasa). 
 Sehemu ya maelfu ya Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika matembezi ya Amani ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)  Imam Hussen(a.s) leo jijini Dar es Salaam.
 Mtembezi yakiendelea leo jijini Dar es Salaam.
 Mzungumzaji na Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania,Sheikh Hemed Jalala akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  matembezi ya Amani ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Imam Hussen(a.s) leo jijini Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza wakati wa  matembezi ya Amani ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Imam Hussen(a.s) leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA WODI ZA WAZAZI KATIKA HOSPITALI TATU JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutbia kwenye hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa wodi tatu za wazazi na watoto katika Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es salaam leo Octoba 11,2016. 
Kampuni ya Amsons Gropu imefadhili ujenzi wa wodi za wazazi katika hospitali ya Mwananyamala, Amana-Ilala na Temeke.Wodi  hizo za kisasa zitakuwa na vitanda 150 na ujenzi wake utagharimu bilioni 4.5 mpaka ukamilike.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akisoma maandishi yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na kulia ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya Amsons Group Bw. Suleiman K.Amour.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Waziri Mkuu apokea misaada ya waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera

$
0
0
WAZIRI MKUU  Mhe. Kassim Majaliwa amepokea michango yenye thamani ya sh. milioni 660.25 zikiwa ni fedha taslimu, hundi na vifaa mbalimbali kwa ajili ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, mwezi uliopita. 
Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo mchana (Jumanne, Oktoba 11, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wa kampuni ya ACACIA, Bw. Deodatus Mwanyika amesema wao wametoa sh. milioni 325 ambazo tayari wameshaziingiza kwenye akaunti ya maafa.
Amewaomba wadau wengine na taasisi nyingine hapa nchini wajitokeze kuisaidia Serikali kukabiliana na janga hili kwani mahitaji halisi ni makubwa kuliko kiasi ambacho kimekusanywa hadi sasa.
Wadau wengine waliochangia ni Balozi wa Japan nchini, Bw. Masaharu Yoshinda pamoja na Shirika la Misaada la Maendeleo la Japan (JICA) ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 220. Vifaa hivyo ni mahema 220, mablanketi 1,100; vigodoro vyepesi (sleeping pads) 1,110; madumu ya maji 250 na plastic sheets 22.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBC1, Dk. Ayoub Rioba ambaye alikabidhi hundi za sh. milioni 41.55, amesema kama taasisi waliguswa na tatizo la maafa ya Kagera kwa hiyo wakatafuta njia ya kuchangisha ili wapate fedha za kuisaidia Serikali kukabiliana na tatizo hilo.
“Tuliamua kufanya harambee na kuwahamasisha wananchi wachangie ambapo wengine walileta kwetu na wengine wakapeleka moja kwa moja Kagera. Na leo tunakabidhi kiasi ambacho tulikikusanya kupitia harambee hiyo,” amesema.
Wengine waliokabidhi michango yao, ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wenye Magereji Tegeta, Bw. Leonard Mwanjela ambaye ametoa fedha taslimu sh. milioni mbili kwa niaba ya mafundi gereji wilaya ya Kinondoni. Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Bw. Abdalla Mwinyi amesema walifanya harambee na kupata sh. milioni 60.8 ambazo wameamua kununua nguo na magodoro, unga wa mahindi tani 10.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea msaada wa mablanketi kutoka kwa Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.Kulia ni Mwakilishi Mkuu wa Shirika la JICA nchini Toshio Nagase.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 41.5 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)  Dkt. Ayoub Ryoba ikiwa ni kutokana na harambee iliyofanywa na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. 
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea moja ya misaada kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa kariakoo Bw.Abdallah Mwinyi ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya milioni 60 ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Picha na Daudi Manongi, MAELEZO. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Mzabuni achunguzwa ujenzi wa Barabara ya Oljoro - Muriet, jijini Arusha

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah - Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kuchunguza kwa undani juu ya zabuni aliyopewa mkandarasi anaye jenga Barabara   katika barabara ya Oljoro /Murriet Jijini hapa.
Gambo ametoa agizo hilo wakati alipokuwa katika ziara ya siku moja
 ya kukagua ujenzi wa Barabara ya Friends corner - Muriet  inayojengwa Kwa kiwango cha Lami na mradi wa Mpango Miji Mkakati ( Tanzania Strategic Cities Project)  unao tekeleza  Na Tamisemi pamoja Barabara hiyo ya Oljoro - Muriet inayojengwa Kwa kiwango cha Changarawe kwa Fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Amesema amegundua kasoro Kwa  Kampuni  ya Surchet Building and Civil
works   inayojenga Barabara ya Oljoro  Kwa kuwa Mkandarasi yuko  nyuma ya muda Na  huenda asimalize kazi Kwa wakati. Pia dhamana ya Utekelezaji wa Mradi aliyoweka Ni kubwa kulinganisha na inayotakiwa hali hii inaonyesha kuwa   zabuni hiyo ilitolewa Kwa  mianya ya rushwa au dhamana hiyo Ni feki.
Kwa kawaida Dhamana ya Utekelezaji wa Mradi ( Perfomance bond) huwa Ni 10% Mpaka 15% ya Gharama ya Mradi lakin  mkandarasi huyu amewasilisha 30% je dhamana hiyo ni halali kweli kwanini alete kiasi kikubwa zaidi ya kinachohitajika huenda Ni batili Ndio maana hana uchungu nayo  na  Mpaka sasa kazi iliyokamilika Ni ya ujenzi wa Mifereji tu sasa kupitia Ziara hii  nahitaji uchunguzi wa kina ufanyike Na kazi hii ikamilike ndani ya muda wa mkataba alisema  Gambo.
Barabara ya Oljoro Muriet inajengwa Kwa urefu wa Km 2.6 sambamba Na Mifereji ya kusafirishia maji yenye urefu km 1.1, Gharama Za Mradi Ni Tsh Mil 157.8 Na  Barabara hii inategemewa kukamilika Mwishoni mwa Mwezi Oktoba 2016.

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha (mbele kulia) akikagua ujenzi wa barabara ya Friends corner –Muriet inayojengwa kwa kiwango cha Lami kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) unaotekelezwa na Tamisemi. Barabara hiyo itajengwa kwa urefu wa Km 6.5

Kupitia Ziara hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisikiliza kero za wananchi wa eneo la soko Mjinga Kata ya Sokoni 1 ambapo kero kubwa ilikuwa ni kufungwa kwa barabara kutokana na ujenzi holela

 Kutoka Kulia ni Mhandishi wa Ujenzi Jiji Eng. Gaston Gasana akifuatiwa na Mhandisi Mshauri wa Mradi wakielezea kazi zitakazofanyika katika Mradi huu.

Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia) akiskiliza taarifa ya kazi zinazoendelea katika Dampo la kisasa la Muriet toka kwa Afisa Usafishaji wa Jiji Bw. James Lobikoki

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo (kushoto) akihoji kuhusu zabuni za ujenzi wa barabara ya Oljoro – Muriet kwa Afisa Manunuzi wa Jiji Bw. Seif Kasori(kulia). Mkandarasi anayejenga barabara hiyo toka kampuni ya Surchet Building and Civil works yuko nyuma ya muda na ametakiwa kukamilisha kazi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.

UFUNGUZI WA MKUTANO WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, UNGUJA

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Daniel F.Kigeda mara alipowasili katika  ufunguzi wa  Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi "B"Unguja. Katikati ni  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir ali Maulid.


 Baadhi ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akitoa hutuba yake katika  ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi "B"Unguja


 Sehemu ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akitoa hutuba yake katika  ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi "B"Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akitoa hutuba yake katika  ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi "B"Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mbunge Shrose  Bhanji mara baada ya    ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi "B"Unguja. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

TANGAZO LA MISA YA KUTIMIZA MIAKA 40 KANISA LA KISWAHILI LONDON

$
0
0

UJUMBE KWA WAONGEAJI 
WA KISWAHILI WAISHIO UK
Ni jumapili hii ijayo ya tarehe 16/10/2016 kanisa letu la Kiswahili hapa London linatimiza miaka 40. Tunawaomba waongea kiswahili wote mlioko UK mje kuhudhuria sherehe hii itakayorushwa live ili dunia nzima ione.
Mgeni rasmi atakuwa Dk. Alex Malasusa
Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Mimi pia nitakuwepo na nitaimba kwaya live. Wewe je unasubiri ninii?

Kwa maelezo zaidi  piga namba hizi chini
Moses Shonga  07914089734
Chris Lukosi     07903828119
BWANA ASIFIWE SANA

PIZZA HUT OPENS IT’S SECOND STORE IN MIKOCHENI.

$
0
0
 Pizza Hut, a division of Yum! Brands, the world’s largest restaurant company, today announced the opening of its second restaurant in Tanzania located at Shoppers Plaza Mikocheni.
Pizza Hut has inaugurated the launch of the new store by donating hot and fresh Pizza’s to the children at Chakuwama Orphanage Center in Sinza. With the support of Coca Cola Tanzania, they were also able to donate several cases of Minute Maid Juices. “The children had smiles from ear to ear,” said Pizza Hut employee Catherine.
 Pizza Hut is the world’s largest pizza chain with $12 billion in global sales and more than 15,000 restaurants in over 100 countries.

Dough Works Ltd has committed to a multimillion-dollar investment in the Pizza Hut brand and the launch of its second store at Shoppers Plaza Mikocheni, a 54 square meter store which is a dedicated outlet for pickup orders and delivery. 

The company has plans for rapid expansion and growth with a target of over 30 stores across the country, creating over 500 new jobs in the Quick Service Restaurant sector.
  

TUNAWAJIBU WA KUWATUMIKIA WANANCHI WA MKURANGA-ULEGA.

$
0
0
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza kwenye  mkutano wa baraza la madiwani  juu ya kufanya kazi kwa masilahi ya wananchi na sio kupelekwa kama Kondo leo mkoani Pwani.
 Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Saum Ally Papen ajifafanua jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani leo  mkoani Pwani.
Sehemu ha madiwani. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Mkuranga.
MBUNGE wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa baraza la madiwani wafanye kazi kwa masilahi ya wananchi na sio kupelekwa kama Kondoo.

Ulega ameyasema hayo leo katika baraza la Madiwani wa Mkuranga katika ulidhiaji wa Ekari 250 ambazo zitatimika katika miradi mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Amesema kuwa mchakato wa kupata ardhi hiyo ulianza muda mrefu hivyo ulipofikia ni pazuri kwa watendaji kijipanga.

Aidha amesema wananchi wanataka maendeleo na majukumu hayo ni madiwani ni kuwajibika pamoja na Wabunge."Mkuranga iko nyuma kimaendeleo hivyo kila kiongozi afanye kazi kwa ajili ya Mkuranga". Amesema Ulega.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid amesema ukusanyaji wa mapato uko chini hivyo kunahitaji nguvu katika ukusanyaji wa mapato.

TIMU YA GOLF YA JESHI YATAMBA KUREJEA NA USHINDI ARUSHA OPEN.

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa klabu ya gofu  ya  Lugalo ya Jijini  Dar es Salaam Kanali Rajabu Mwenyumbu  akiangalia Mazoezi  ya mwisho ya timu ya  klabu hiyo  ambayo inatarajia  kushiriki  katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika   Mwishoni mwa Wiki Hii Jijini Arusha. 
 Naibu katibu mkuu wa Klabu ya gofu ya jeshi ya Lugalo  Kanali Rajabu Mwenyumbu  akizungumza na  wachezaji wa gofu wa  klabu hiyo ya jijini Dar es salaam wanao tarajiwa  kushiriki katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika mwisho wa  Wiki hii Jijini Arusha.
Naibu katibu Mkuu wa Klabu ya Gofu ya Jeshi ya Lugalo Kanali Rajabu Mwenyumbu  akisalimiana na wachezaji wa gofu wa timu hiyo wanao tarajiwa  kushiriki katika mashindano ya wazi Jijini Arusha  mwisho wa  Wiki hii. 
PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)

TAARIFA KUTOKA MAKAO MAKUU YA JWTZ

$
0
0
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis  Mwamunyange (watatu kushoto), akiwa na Mkuu wa Jeshi la Anga la Zimbabwe luteni Jenerali (Air Martial) Penance Shiri (wapili kushoto), alipotembelea Makao Makuu  ya JWTZ Upanga Jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Octoba 2016.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis  Mwamunyange (kulia) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Anga la Zimbabwe luteni Jenerali (Air Martial) Penance Shiri, alipotembelea Makao Makuu ya JWTZ Upanga Jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Octoba 2016, wakati wa ziara ya kikazi nchini. 

MTENDAJI MKUU TEMESA AWAFUKUZA KAZI WAFANYAKAZI SITA NA KUWAPA ONYO WAWILI WA KIVUKO CHA MV KOME MWANZA.

$
0
0
Na Theresia Mwami TEMESA Mwanza

Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo kuwafuta kazi mara moja watumishi sita wa kivuko cha Mv Kome kuanzia 11/10/2016 pamoja na kuwapa onyo kali watumishi wengine wawili wa kivuko hicho kwa kuondoka katika eneo la kazi bila ruhusa ya mkuu wao wa kazi.

Ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha TEMESA mkoani Mwanza na kutembelea kivuko cha Mv Kome kinachotoa huduma ya usafiri kati ya Kome na Nyakarilo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.Dkt Mussa Mgwatu pia amemwagiza Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo kuhakikisha wafanyakazi wa karakana na kivuko wanawajibika ipasavyo ili kuondoka na uzembe kama uliojitokeza.

“Hatuwezi kuvumilia uzembe namna hii watumishi wanaamua tu kuondoka eneo la kazi bila kupata ruhusa kutoka kwa wakuu wao hii sio sawa kabisa na nakuagiza Meneja hawa watumishi waache kazi mara moja” alisisitiza Dkt Mgwatu.Aidha Dkt Mussa Mgwatu amemwagiza Meneja wa TEMESA Mwanza kuajiri watumishi wengine ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuzingatia weledi na uwajibikaji wawatumishi watakao waajiri.

Kwa upande Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo alikiri kuwa hakukuwa na ruhusa yoyote ya maandishi iliyotolewa kwa watumishi kutokuwepo kazini siku hiyo.“Mtendaji sina barua yoyote kutoka kwa watumishi hawa iliyofika kwangu kuomba ruhusa ya kutokuwepo katika kituo cha kazi.” alisisitiza Mhandisi Mishamo.

Mhandisi Ferdinand Mishamo amewaja watumishi waliachishwa kazi kuwa ni walinzi wanne Bw. Apolinary Kapulula, Bw. Marwa Nchagwa , Bw. Msomi Stanley na Joseph Mtokambali, wengine ni Bw. Baharia Geofrey Biseko na Mkusanya Mapato wa kivuko hicho Bw. Elisha Mbondo.

Amewataja Watumishi wanaopewa onyo kali ni Mkuu wa Kivuko cha Mv Kome Bw.Elias Mabushi na dereva wa kivuko hicho Bw.Juma Bugingo.Dr. Musa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo Kanda ya Ziwa ili kubaini changamoto zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Mussa Mgwatu (kushoto) akisikiliza taarifa ya kituo cha TEMESA Mkoa wa Mwanza kutoka kwa Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
Abiria wakiteremka katika Kivuko cha Mv Kome II kinachotoa huduma kati ya Nyakarilo na Kome wilayani Sengerema mkoani Mwanza.Picha Zote na Theresia Mwami TEMESA Mwanza.

MATEMBEZI YA HIYARI NA UCHANGIAJI DAMU KUFANYIKA MKOA WA MJINI MAGHARIBI ZANZIBAR.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed akitoa tarifa kwa wandishi wa habari kuhusu matembezi ya hiyari na zoezi la kuchangia Damu kwa Mkoa Mjini Magharibi yatayofanyika tarehe 16/10/2016. 
 Sehemu ya wandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alipokuwa akitoa tarifa kuhusu matembezi ya hiyari na zoezi la kuchangia Damu kwa Mkoa Mjini Magharibi.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Mahafali ya kidato cha nne Sullivan Provost yafana.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost,  Rachel Mwalukasa (kushoto), akizungumza wakati wa  mahafali ya pili ya kidato cha nne ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias mkoani  Pwani hivi karibuni. Wengine kutoka  kulia ni Mkuu wa Shule, Alex Nicholaus, Mhadhiri kutoka  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Dk Ellen Kilinga na Mhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya UDSM (COICT), Dk Suzan Lujara aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo. 
 Mhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya UDSM (COICT), Dk Suzan Lujara (wa pili kulia) akimpongeza Mohamed Ibrahim, mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri kimasomo na kujizolea kutwaa tuzo mbalimbali wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha nne ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Pwan​i hivi karibuni. Wengine kutoka Kulia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM, Dk Ellen Kilinga, Mkurugenzi Mtendaji was Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa na Mkuu wa shule hiyo, Alex Nicholaus.  
Wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost wakipozi katiaa picha ya kumbukumbu pamoja nja baadhi ya walimu, viongozi wa shule na mgeni rasmi wakati wa  mahafali yao shuleni hapo, Kihaba, Pwani.

WAKAZI WA TABATA KIMANGA JIJINI DAR WAOMBA KUONDOLEWA TAKATAKA BARABARANI.

$
0
0
Mchuuzi wa mbogamboga akipita karibu na takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na kituo cha daladala cha Tabata Kimanga mwisho Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
Takataka zikiwa kando ya barabara.
Mwendesha bodaboda akizikwepa takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na stendi ya daladala ya Tabataaa Kimanga mwisho jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wa Tabata Kimanga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kuondolewa kwa takataka zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali na mkandarasi aliyepewa tenda ya kuziondoa.

Akizungumza Dar es Salaam juzi mkazi wa eneo hilo, Mfaume Wakwetu alisema katika maeneo mengi ya Tabata Kimanga kunatakataka nyingi zimerundikwa kando ya barabara bila kuondolewa na wahusika.

"Takataka nyingi zimerundikwa katika eneo la stendi ya mabasi hapa Tabata Kimanga na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa stendi hiyo na wapita njia" alisema Mfaume.

Aliongeza kuwa takataka zilitolewa majumbani huwekwa katika madampo madogo yaliyoanzishwa kandio ya barabara lakini mkandarasi aliyepewa tenda hiyo hushindwa kufika kwa wakati kuziondoa hivyo kuwa kero kwao.

Aliongeza kuwa kutokana na takataka hizo kuachwa kwa muda mrefu bila kuondolewa husambaa hadi kwenye mifereji ya maji taka ambayouziba na kusababisha maji kushindwa kupita na kutoa hahrufu kali na kusababisha mafuriko mvua zinaponyesha.

DC Mjema atoa wiki tatu wananchi kupewa hati zao.

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, akizungumza na wakazi wa kata ya Msongola katika ziara za kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika wilaya hiyo.
 Mtendaji mkuu wa Kampunia ya upimaji na uuzaji Viwanja ya Tanzania Remex, Ali Hamadi, akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa kata ya Msongola ramaninya mipango miji katika eneo hilo .
Katibu tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro, akizungumza na wananchi wa Kata ya Msongola wakati wa ziara ya kutatua kero za wananchi katika maeneo yao . 

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesikiliza kero 126 za wananchi wakati wa ziara yake katika kata tatu za Vingunguti, Pugu, Gongolamboto na Msongola na kuipa wiki tatu kampuni ya Tanzania Remix kuwapatia wananchi hati zao za viwanja.

Mjema amesema kuwa wananchi hao wamesubiri kwa miaka mitatu sasa juu ya mpango huo bila kuona matumaini, hivyo hakuna haja ya kuendelea kusubiri.

"Sasa natoa wiki tatu kuhakikisha fidia za wenye viwanja zinapatikana na baada ya wiki mbili kila mmoja awe amepatiwa hati yake ambayo itamuwezesha kuuza au kukopa katika mabenki mbalimbali"amesema Dc Mjema.

Dc Mjema pia alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ulinzi katika kata ya Msongola kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uporaji na mauaji.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea soko kuu Mkoani Dodoma.

Article 15

$
0
0

Na Grace Singida.

Serikali na wadau mbalimbali wanatakiwa kuunganisha nguvu na kuzielekeza katika kuelimisha jamii juu ya athari za uchafu ili wahamasike na kuupinga kwa kujenga vyoo bora, kutumia maji safi na salama na kutumia huduma za usafi wa mazingira.

Ari hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mpango wa ‘Water Aid’ Tanzania Bw. Abel Dugange wakati wa kikao cha wadau wa maji wakati wa kuhuisha mipango ya sekta ya maji ya Mkoa wa Singida. Dugange amesema nguvu kubwa inatakiwa ielekezwe katika kutoa elimu kwa jamii ili wajenge vyoo bora na kuvitumia, watumie maji safi na salama ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali yatokanayo na uchafu.

Ameongeza kuwa serikali inapoteza fedha nyingi katika kuwatibu wananchi wanaogua magonjwa kama kipindupindu, kuhara pamoja na ukusanyaji na utekezaji wa uchafu huku wananchi pia hupoteza pesa kwa kujitibu huku wakipoteza muda wa kuzalisha mali kwenye matibabu.

Dugange amesema mpango wa ‘Water Aid’ kwa mwaka 2016 mpaka 2020 utalenga kuunganisha nguvu na kusaidiana na halmashauri katika kutekeleza mipango yao ya sekta ya maji na usafi wa mazingira ili kufikia malengo ya kitaifa katika sekta hiyo.

Amesema kwa tafiti za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa asilimia 58 ya watanzania hupata na kutumia maji safi na salama huku asilimia 18 tu hutumia huduma za usafi wa mazingira. Dugange amesema kwa upande wa upatikanaji na matumizi ya vyoo bora vya kwa Mkoa wa Singida mijini ni asilimia 31 wakati vijijini ni asilimia nane.

Katika majadiliano hayo wahandisi wa maji na maafisa mazingira wa halmashauri walitoa changamoto za sekta hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa hasa vya usafiri wa kutembelea na kukagua maeneo mbalimbali.

Changamoto nyingine ni pamoja na visima vingi vya vijijini kuchimbwa maeneo ya mashamba ya wanakijiji ambapo hawalipwi fidia na kusababisha uharibifu wa vyanzo na visima vya maji hasa ukataji wa miti.

Kumekuwepo na wizi wa vifaa katika miradi ya maji hasa solar huku wanakijiji wakiomba kuwekewa umeme wakati utunzaji wa miradi hiyo wakishindwa kuchangia huduma hizo. Kwa pamoja wadau wamekubaliana kuunganisha nguvu katika kutatua kero za upatikanaji wa maji pamoja na kuboresha usafi wa mazingira.

Mwakilishi Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Boniface Temba (katikati) akiwa katika kikao cha wadau wa maji kuhusu kuhusu kuhuisha mipango ya maji Mkoa, Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta Abdalah Dihenda na kushoto kwake ni Mhandisi wa Maji kutoka Sekretariet ya Mkoa Emaeli Nkopi. 
Kikao cha wadau wa maji Mkoa wa Singida kikiendelea mweye tai nyekundu ni Afisa Afya Mkoa wa Singida Habib akiwa na kushoto kwake ni mkurugenzi  wa mpango wa Water Aid Tanzania Abel Dugange. 
Wadau wa Maji Mkoa wa Singida wakiendelea na kikao. 
Wadau wa Maji Mkoa wa Singida wakiendelea na kikao. 

Serikali yaanza utafiti wa kuangalia hali ya upatikanaji wa nishati nchini

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Dar es Salaam

Serikali imeanza utafiti wa kuangalia hali ya upatikanaji wa Nishati Tanzania katika mikoa 26 ya Tanzania bara wa mwaka 2016 kuanzia Octoba 10, hadi Novemba 15 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa utafiti huo unafanya na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) kwa kushirikiana na kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS).

Dkt Kwesibago alisema kuwa lengo la utafiti huo ni kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali ya upatikanaji wa Nishati umeme katika ngazi ya jumuiya na kaya, matumizi ya umeme na nishati jadidifu pamoja na faida zake kwa maendeleo.

Sambamba na ukusunyaji wa takwimu hizo, Dkt Kwesibago alisema kuwa utafiti huo utahusisha ukusanyaji wa takwimu za kidemografia na za kiuchumi za wanakaya zikijumuisha umri, jinsia, hali za ndoa, elimu, shughuli za kiuchumi, matumizi ya muda pamoja na ushiriki wa jinsia katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aliongeza kuwa utafiti huo utahusisha jumla ya maeneo 676 ya vijiji na mijini yaliyochaguliwa kitaalam katika mikoa yote ya Tanzania bara na kuhusisha jumla ya kaya binafsi 10,140 pamoja na viongozi wa vijiji na mitaa 676 ambao watahojiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopatikana katika maeneo yao.

Aidha, alisema kuwa timu ya wadadisi wapatao 130 watahusika katika zoezi hilo la ukusanyaji taarifa ambapo kila mkoa utakuwa na wadadisi watano, msimamizi mmoja na wataalamu wengine kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu makao makuu.

Vile vile alisema kuwa upatikanaji wa takwimu hizo utasaidia katika kuandaa taarifa kuhusu hali halisi ya upatikanaji na usambazaji wa nishati ya umeme nchini na hivyo kuweza kupima na kuhakiki maendeleo yaliyofanikiwa na mafanikio ya juhudi za Serikali.

Pia taarifa za utafiti huo zitatumika katika kuendeleza mipango ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali itakayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati bora vijijini.

Mbali na hayo wananchi wameombwa kutochukua sheria mkononi kwa kuwadguru wadadisi wanapokuwa wakifanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kusaidia nchi yetu kupata takwimu rasmi zinazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw.Ephraim Kwesigabo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya utafiti watakaoufanya kwa pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini(REA) ukiwa na lengo la kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijijini.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga akizungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti ambao serikali itaanza kufanya kuangalia hali ya upatikanaji wa Nishati nchini hasa maeneo ya Vijijini.Kulia ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw.Ephraim Kwesigabo.

SADC ORGAN TROIKA MINISTERIAL ASSESSMENT MISSION

$
0
0


The Southern African Development Community (SADC) Troika of the Organ on Politics, Defence and Security Cooperation undertook an assessment mission to the Democratic Republic of Congo (DRC) from 10th to 13th October 2016. The objective of the mission was to conduct an assessment of the political and security developments in the DRC aimed at assessing the on-going efforts related to peace and political stability of the DRC. H.E. John Pombe Joseph Magufuli, President of the United Republic of Tanzania in his capacity as the Chairperson of the Organ on Politics, Defence and Security cooperation mandated the Mission.

The assessment mission was led by Hon. Dr. Augustine P. Mahiga, Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation of the United Republic of Tanzania and Chairperson of the Ministerial Committee of the Organ (MCO), who was accompanied by Hon. Georges Rebelo Chikoti, Minister of External Relations of the Republic of Angola and Deputy Chairperson of the MCO, Hon. Patricio Jose, Deputy Minister of National Defence of the Republic of Mozambique representing the outgoing chairperson of the MCO. The Mission was supported by the SADC Secretariat led by H.E. Dr. Stergomena Lawrence Tax, Executive Secretary of SADC. The mission also included SADC Ambassadors accredited in the DRC.

The Mission consulted with various stakeholders, including SADC Ambassadors accredited to the DRC, H.E. Edem Kodjo, African Union Facilitator of the National Dialogue, Hon. Raymond Tshibanda, Minister of Foreign Affairs and International Cooperation of DRC, Mr. Corneille Nangaa, and Mr. Nobert Katintima, Chairperson and Deputy of the Independent Electoral Commission (CENI) respectively, Senior Officials of the DRC Government, Representatives of Opposition Outside the  Dialogue (Rassemblement), Representatives of Opposition in the Dialogue, political parties in the Presidential majority led by Hon. Aubin Minaku, civil society and religious groups.


WAZIRI LUKUVI. HAKUNA MAKAZI HOLELA YATAKAYOBOMOLEWA JIJINI MWANZA.

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, ameziagiza halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.

Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo hii leo Jijini Mwanza alikofanya ziara ya kujionea utekelezaji wa urasimishaji makazi yaliyoendelezwa kiholela Jijini Mwanza ambapo amebainisha kwamba Serikali haina mpango wa kuwavunjia wananchi makazi yaliyojengwa kiholela na badala yake imeandaa mpango huo ili kutambua makazi hayo na kuwapatia wananchi hati miliki ya makazi yao.

Aidha amewatahadharisha wananchi kwamba, mpango wa kurasimisha makazi yaliyojengwa kiholela hautayahusisha makazi yaliyojengwa kwenye maeneo hatarishi ikiwemo kwenye mabonde, miinuko, mafuriko pamoja na hifadhi za barabara.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi na makazi mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza ambaye makazi yake yamerasimishwa kutoka makazi holela baada ya zoezi la upimaji kufanyika..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na watendaji mbalimbali Jijini Mwanza (Ilemela na Nyamagana).
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye mkutano huo baina ya waziri Lukuvi na watendaji mbalimbali wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Watendaji na wananchi wa Kata ya Buhongwa wakimsikiliza waziri Lukuvi (hayupo pichani).

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images