Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1384 | 1385 | (Page 1386) | 1387 | 1388 | .... | 3348 | newer

  0 0

   Mshambuliaji wa Ndanda FC, Omary Mponda akichuana na kiungo wa African Lyon, Omary Salum katika mchezo wa LigiKuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. African  Lyon ilishinda 1-0. (Picha na Franis Dande)
   Mshambuliaji wa Ndanda FC, Omary Mponda (kushoto) akiwania mpira na beki wa African Lyon, William Otong.
   Beki wa African Lyon, Milaji Seleman (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa Ndanda, Riphat Hamis.

  0 0

  Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin ataonesha mitindo yake kama mgeni mwalikwa kwenye "Plus Size Fashion Show" inayotegemea kufanyika huko Zanzibar leo Jumamosi  Tarehe 8 August 2016 katika Hotel ya Grand Palace. 

  Asya amejipatia Shavu hili,kupitia kampuni ya mitindo ya Zanzibar inayo tambulika kama "Style House" chini ya C.E.O Mama Titi ambaye anaishi uingereza. Ingawa Asya anaishi Marekani lakini kwa sasa yupo  hapaTanzania kwa ajili ya onesho hilo lenye dhumuni kubwa la kuchangia "Breast Cancer Zanzibar"

  Mbali na Mama wa mitindindo, designers wengine pia watashiriki kikamilifu kwenye ufanisi Onesho hilo. Special Apperance atakuwa ni mwigizaji Wastara Sajuki, Burudani itatolewa na 

  Khadja Kopa. 


  0 0

  TAASISI isiyo ya kiserikali ya Mathayo Suleiman Foundation yatoa msaada wa vyakula katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman, amesema kidogo walicho nacho kinaweza kuwasogeza siku mbili tatu watoto wanaoishi katika kituo hicho kwani kinakabiliwa na uhaba wa chakula kwa kiasi kikubwa sana.

  Pia amesema kuwa katika maisha tumetofautiana ndio maana wanachama wa taasisi hiyo wameona watoe kile kidogo walichokuwa nacho kwani kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.

  Nae Mratibu wa Kituo  cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Isa Buzohera amewashukuru wanachama wa Taasisi hiyo kwa kutoa mchango wao kwani taasisi ilikuwa katika hali mbaya sana ya ukosefu wa chakula.

  Amesema kuwa kituo hicho  Dogodogo Maltiporpuse Training Centre  mpaka sasa kinawatoto 39 wasichana 10 na wavulana 29 amesema kituo hicho Kilifunguliwa 2003 kwa lengo la kuwapika kiufundi watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kujitegemea wakiwa na nyenzo mhimu ili waweze kujikwamua kiuchumi.

  Amesema kuwa uhaba wa chakula ukiendelea kituo hicho kitafungwa kwani mpaka sasa wanahitaji zaidi ya Milioni 205 kwaajili ya chakula pamoja na vifaa vya kuwapa kila mhitimu wa mafunzo yanayotolewa katika kituo hicho. 
  Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman (Mwenye suti nyeusi katikati) akikabidhi mbuzi kwaajili ya nyama kwa Mwalimu wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Rosemary Nyabuzuki leo. Wengine ni wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman.
   Mratibu wa Taasisi ya Mathayo Suleiman, Banga Suleiman(Mwenye Suluali Nyeupe) akishirikiana na wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation wakikabidhi unga kwa watoto wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo.
   Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Isa Buzohera katika kituo hicho leo.
   Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman akizungumza mara baada ya kupata maelezo ya kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre.


  0 0
 • 10/08/16--10:13: autofest 2016


 • 0 0

  MFUKO  wa Uwekezaji wa Pamoja  (UTT-AMIS)  umesema  kutokana na utafiti walioufanya  kwa muda wa miaka 10, unaonyesha Watanzania walio wengi  hawana  uelewa  wa   kuwekeza fedha zao  kwenye hati fungani (bond).
   Kauli hiyo  imetolewa  jijini Dar es Salaam na  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa  UTT,  Daudi Mmbaga , alisema  watu wengi wanakuwa na fedha nyingi lakini hawajui  jinsi ya kuwekeza  fedha zao.
   Alisema  kutokana na  changamoto iliyopo kwa Watanzania  ya kutokuwa na uelewa wa  jinsi ya kuwekeza , wameamua kuanzisha huduma ya  Usimamizi wa Mali  itakayomsaidia mwananchi  jinsi ya kuweza kuwekeza fedha zake na kutengeneza faida.
  “ Watu wengi   wanakuwa  na fedha nyingi  lakini  zimelala tu, na wengine  wamewekeza   kwenye maeneo yasiyowapa faida  ndio maana tuamua kuanzisha huduma itakayowasaidia  kuwekeza  fedha yao  inayoitwa  Usimamizi wa Mali,” alisema.
   Aidha, alisema huduma hiyo  kwa sasa imeshaanza kutumika na  mwelekeo   ni mzuri  kutokana na  watu wengi  kupenda kuwekeza fedha zao, ambapo kiwango cha kuanzia ni sh. Milioni  tano.
   Mmbaga  alisema   kiwango  cha elimu  nchini  kikijikita vizuri kitasababisha  kuwepo  na soko la uhakika   na kusababisha  kuwepo na maendeleo   ya kiuchumi.
   Hata hivyo  aliwashauri wananchi kujitahidi kuwekeza katika mifuko  ya uwekezaji  kwa kuwa  kutasaidia  kuwa na imani na fedha zao.
  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Uwezeshaji (UTT-AMIS), Daud Mbaga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu huduma yao mpya ya usimamizi wa mali. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Issa Wahichinenda. 

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  NCHI nne zinatarajiwa kushiriki mbio za Dar Rotary Marathon 2016 zitakazofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 14 mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ambaye atashiriki matembezi ya Km. 5.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla, mbio hizo za kila mwaka huandaliwa na Dar Rotary Club kwa kushirikiana na Bank M zikiwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia shughuli za kijamii na Mwaka huu wataelekeza nguvu zaidi kwenye ujenzi wa wodi ya watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Zavalla, amesema waandaaji mwaka huu wametoa nafasi kwa nchi za Kenya, Malawi, Rwanda na Ethiopia kushiriki mbio hizo za Km 21. "Tayari sisi kama shirikisho tumetuma mialiko kupitia mashirikisho ya nchi husika na tayari wametujibu na kututumia majina ya wanariadha na makocha watakaokuja kushiriki, isipokuwa Ethiopia tu bado hawajatuma ingawa walisema watashiriki,” amesema Zavalla.

  Katibu Msaidizi huyo, amesema Kenya itawakilishwa na wanariadha saba ambao ni Timothy Raibuni, Martin Musyoka, Patrick Munyithya, Willy Mwangi, Patrick Mutunga huku wanawake ni Damaris Maundu na Shelmith Muriuki wakiwa na Kocha James Mbiti.

  Kwa upande wa Malawi itawakilishwa na wanariadha sita ambao ni Francis Khanje, Happy Mcherenje, Chancy Master, Rashid Taimu, Grevazio Mpani, Elija Kanyenda huku wanawake ni Cecilia Mhango na Kocha ni A. Sande na  Rwanda itawakilishwa na wanariadha wawili Eric Sabahire na Salome Nyirarukando.

  Aidha, Zavalla amebainisha kuwa pia waandaaji wametoa ufadhili kwa baadhi ya wanariadha wa Tanzania ambako watagharamia usafiri na malazi, ambao ni Emmanuel Giniki, Ismail Juma,  Panga, Fabian Joseph, Dickson Marwa, Gabriel Gerald, Mshindi wa tano Marathon Olimpiki Rio 2016, Alphonce Felix huku wanawake ni Catherine Lange na Mary Naali wakiwa na Kocha Francis John na kutoka Zanzibar ni Filipo Mambo, Mohamed Mgeni, huku wanawake ni Maria Michael na Asma Mukhandi wakiwa na Kocha Hamza Haji.

  Kwa upande wa zawadi, Zavalla amesema mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Sh. Milioni 3, wa pili milioni 2 na watatu milioni 1. Pia washindi wa nne hadi kumi watakuwa na zawadi.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu  ya Jamii 
  MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva kutoka kundi la Wanaume Family Chege Chigunda , leo ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea hospitlai ya Rufaa ya Temeke na kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya Watoto waliozwa hapo kutokana na matatizo mbalimbali. 
  Akizungumza na Mwandishi wa blog hii Mapema leo Hospitalini hapo chege alisema kuwa imekuwa tofauti sana kwa watu kupenda kusheherekea katika nyumba za starehe lakini yeye ameamua kukaa na watoto hao wagonjwa hili kurudisha kile ancho kipata kwa jamii. 
  “Chege Chigunda amezaliwa leo hivyo ndio maana nipo hapa mtoto wa Mama Said kusherekea siku yangu ya kuzaliwa na wagonjwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kama mnavyoziona Pampers , Dawa za Mswaki na Dawa kwa ajili ya wagonjwa ambao awana uwezo wa kujijinunuli a hivyo katika siku ya leo wamepata fursa ya kununuliwa madawa na mimi” anasema Chege. 
  Anasema kuwa maisha yamebadilika sana na inapaswa watu kurudi nyuma na kufanya yale yaliyoa mazuri yanayompendeza Mungu kwa kusheherekea siku zao za kuzaliwa na watu ambao wanamatazo na wenye uhitaji hili kuweza kuwapa faraja ambayo wakuwa wameikosa kwa muda kutokana na matatizo yaliyowakuta. 
  Alimaliza kwa kutoa wito kwa wasanii na watu maharufu kuwa na utamaduni wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mablimbali kila wanapopata nafasi na kiasi kidogo kwani kutoa akuhitaji kuwa na utajiri mkubwa bali ni moyo tu.
   Msanii wa Muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chigunda akiweka sawa baadhi ya zawadi alikuwa ameziandaa kwa ajili ya Wagonjwa Temeke Hospitali.
   Chege Chigunda na baadhi ya Wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe wakielekea wodini
   Chege Chigunda akitoa baadhi ya Zawadi kwa wagonjwa
   Mhe Temba akiingia wodini  kupeleka zawadi kwa Wagonjwa

  Mhe Temba  na Chege Chigunda wakitoa  Zawadi kwa wagonjwa.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0


  0 0

   Ujumbe wa wataalamu wa Fedha, Sera na Uchumi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose (hawapo Pichani), Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington DC, Marekani, ambapo unafanyika Mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo ambayo Tanzania ni Mwanachama, wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Sera Augustine Ollal, Kamishna wa Bajeti John Cheyo na Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje Mamelta Mutagwaba.
   Ujumbe wa wataalamu wa Fedha, Sera na Uchumi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose (hawapo Pichani)
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose walipokutana ofisini kwake Jijini Washington DC, Marekani, ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na namna Benki hiyo ilivyojipanga kuhakikisha kuwa inaiwezesha Tanzania kufikia ndoto yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025
   Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakishikana mikono kuonesha umoja na mshikamano mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya ujumbe huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, Jijini Washington DC nchini Marekani, ambako ujumbe huo unahudhuria Mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo.

  0 0

   Meneja Mauzo ya Rejareja wa Tekno, Moses Mtweve akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ubora wa simu aina mpya ya Tekno Phatom 6Plus.
   Afisa Masoko wa Tekno, Fred Kadilana akitoa ufafanuazi juu ya simu mpya ya Tekno Phatom 6Plus kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa simu hiyo Mpya. 
  Afisa mauzo wa Tekno kulia akitoa maelekezo kwa mteja wakati wa uzinduzi wa simu mpya aina ya Tekno Phatom 6Plus jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika tamasha la madhehebu ya Bohora leo Oktoba 08, 2016, ambayo yanafanya maadhimisho ya dunia ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kiislam Jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Oktoba, 2016 amehutubia katika tamasha la madhehebu ya Bohora ambayo yanafanya maadhimisho ya dunia ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kiislam Jijini Dar es Salaam.
  Maadhimisho hayo yamewaleta nchini wafuasi zaidi ya 30,000 kutoka nchi mbalimbali duniani na kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS).

  Akihutubia wafuasi wa Bohora katika Msikiti wa Hakimi uliopo Upanga Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amemshukuru Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa kukubali kufanya maadhimisho ya mwaka mpya wa madhehebu hayo hapa nchini na amewashukuru na kuwapongeza wafuasi wa madhehebu hayo kwa kukubali kuja hapa nchini na kukaa kwa siku zote za maadhimisho yaani kuanzia tarehe 02 Oktoba, 2016 walipoanza hadi tarehe 11 Oktoba, 2016 watakapomaliza.
  Rais Magufuli, amewapongeza viongozi na wafuasi wa madhehebu ya Bohora kwa kutumia maadhimisho haya kuhimiza amani, upendo na mshikamano na pia amewashukuru kwa kushiriki katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwemo mchango Dola za Marekani 53,000 zilizotolewa na Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa Serikali kwa ajili ya kuchangia kampeni ya utengenezaji wa madawati, na kuwaleta madaktari kutoka Hospitali ya Saifee ya India waliotoa matibabu bure kwa wananchi wa Arusha.

  Aidha, Rais Magufuli amewakaribisha wafuasi wa Bohora duniani kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Uvuvi, Misitu, Mifugo, Madini na Gesi kwani soko la uhakika lipo ndani ya nchi, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu takribani milioni 400.
  Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS) amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana na wafuasi wa madhehebu ya Bohora katika maadhimisho hayo na amesema wafuasi wote wa Bohora wanahimizwa kushirikiana na mamlaka zilizopo katika nchi wanazoishi, kuwa raia wema na kufuata sheria.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  08 Oktoba, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akiwasili  kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga 
  jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya ya 
  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin mara alipowasili kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam  ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akihutubia mbele ya waumini na  Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako 
  alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akiagana   Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016

  Sehemu ya waumini kinababa kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam   sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
  Sehemu ya waumini kinamama na watoto kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam   sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016

  0 0

  Na Luteni Selemani Semunyu,  JWTZ

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Brigedia Jenerali Davis Mwamunyange ambaye ni Mlezi wa Klabu ya Jeshi  ya  Lugalo Golf Club  ameimarisha safu ya uongozi wa klabu hiyo kwa kuwateua Naibu katibu Mkuu na Mkuu wa Miundombinu kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

  Jenerali Mwamunyange amemteua Kanali Rajabu Mohamed Mwenyumbu kuwa Naibu Katibu wa klabu na Kapteni Kitego Kuwa Mkuu wa Miundombinu ya Klabu(Ground Member) kuchukua nafasi ya Kanali Jackson Nsigaye aliyehamia Bukoba kikazi.

  Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa Klabu hiyo Generali Michael Luwongo alisema  Hatua hiyo inalenga kuboresha klabu hiyo ambayo inamikakati mikubwa ya kuboreshwa na kuwa kitovu cha Michezo cha kisasa che nye hadhi ya Kimataifa.

  Wakati huo huo wachezji wa Timu ya Golf ya  Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ya  Jijini Dar es Salaam wako katika maandalizi ya mwisho kujiwinda na Mashindano ya  Arusha open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha.

  Akiongea na Waandishi wa Habari katika Klabu hiyo Kapteni Japhet Masai alisema mashindano  hayo ambayo ni muhimu katika kupandisha viwango vya wachezaji yanatarajiwa kufanyika  Jumamosi na Jumapili ya Oktoba 15 na 16 huku ikihusisha wachezaji wasio wa kulipwa (Amature).

  Alisema Klabu ya Lugalo inatarajia kuingiza wachezaji  wa Daraja la A,B,C senior huku  wachezaji watoto ambao ni Junior watashindwa kushiriki kutokana na kuwa mashuleni katika kipindi hichi.

  “ Mashindano haya ni Muhimu kwa Wachezaji wetu lakini pia itatupa fursa kwa wachezaji wetu wenye viwango kupata nafasi kuchezea timu ya Taifa iwapo wataonekana. Alisema Kapteni Masai.

  Kapteni Masai alisema kumbukumbu ya Matokeo mazuri katika mashindano ya Tanzania open  kwa kuchukua ushindi wa Kwanza na wa Pili gross huku Daraja B ikichukua Ushindi wa Kwanza na katika mashindano ya Moshi Open kuchukua nafasi ya Kwanza Mshindi wa Jumla.

  Kwa upande wake  Afisa Utawala wa Klabu hiyo Kapteni Amanzi Mandengule alisema Jumla ya wachezaji 10 wanatarajiwa kwenda kushiriki michuano hiyo wakiwemo wanawake watatu na wanaume Saba.

  Aliongeza kuwa kikosi cha wachezaji hao Kitaongozwa na  Kapteni Amanzi Mangengule, Kapteni Japhet Masai, Kapteni Kibuna Shabani, Juma Likuli,Noel Mheni,Nicolous Chitanda ,Michael Obare, Amina Hamisi,Sara Denis  na Sophia Mathias.

  Afisa huyo wa Utawala alisema maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni Baraka za Mwenyeki wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo ili kuhakikisha wanakwenda kuwakilisha vyema  Jeshi kwa kurejea na Ushindi.
   Mpiga Golf Sara Denis Amina wa Klabu ya Golf ya Lugalo Jijini Dar Es Salaam akiwa katika Mazoezi  kujiwinda na Mashindano ya Arusha Open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha Nyuma ni Amina Hamisi,Sophia Mathias wachezaji wenziei wa klabu hiyo


   Nahodha  wa Klabu ya Golf ya Lugalo Kapteni Japhet Masai (katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Operation na Mafunzo wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu(OTO) Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba alipotembelea viwanja vya golf vya Lugalo Jijini Da r es Salaam katika mashindano ya CDF Trophy 2016.
   Mnaadhimu Mkuu Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzani Luteni Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) Akisalimiana na Meneja wa Klabu ya Golf Lugalo Kanali Gerlard Omary, alipowasili katika Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam kusuhudia mashindano  ya Mkuu wa majeshi yaliyomalizika hivi karibuni Katikati ni Mwenyekiti wa klabu hiyo Brigedia Jenerali Michaele Luwongo
   Mnaadhimu Mkuu Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzani Luteni Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) Akisalimiana na Mwenyekiti wa klabu Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michaele Luwongo mara alipowasili katika klabu hiyo Jijini Dar es Salaam kushuhudia CDF Ttophy iliyomalizika hivi karibuni.
  Baadhi ya Wachezaji Wanawake wa Klabu ya Golf ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Mazoezi kujiwinda na Mashindano ya Arusha Open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha ( Picha na Luteni Selemani Semunyu) 

  0 0

  Jana Oktoba 08, 2016 kuamkia leo jumapili Oktoba 09, 2016 ilikuwa Shangwe kubwa kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake kwenye tamasha kubwa la "The Nyama Choma Festival" lililofanyika kwenye viunga vya Rock City Mall.
  Msanii AY aliwapagawisha wakazi wa Jiji la Mwanza huku wakipata nyama zilizochomwa kwa ustadi wa hali ya juu huku #LakeFmDjz wakidondosha burudani pamoja na DjK3 kutoka Jijini Dar es salaam. Kumbuka 102.5 Lake Fm ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa waliofanikisha tamasha hilo.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Kishapu, Mhe, Nyabaganga Taraba mara baada ya kuwasili Kijiji cha Bubiki kabla ya kuanza kwa mbio zake.

   Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa katika maeneo mbalimbali mara baada ya kuwasili wilayani Kishapu.
   Kikundi cha ngoma cha Makirikiri kikionresha manjonjo yake katika ufunguzi wa mradi wa stendi kuu ya mabasi na kituo cha polisi eneo la Mhunze wilayani Kishapu wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru. 
  0 0
  Benny Mwaipaja, MoFP
  Washington DC, Marekani
  8.10.2016

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Serikali imedhamiria kuimarisha sekta ya kilimo na Utalii ili ziweze kutoa mchango mkubwa kuinua uchumi wa Taifa pamoja na kuwaondoa wananchi wake kutoka katika lindi la umasikini.

  Waziri Mpango ameyasema hayo Jijini Washington DC, nchini Marekani, wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, ambapo viongozi hao wamezungumzia masuala yanayohusu utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na taasisi hiyo.

  Amesema kuwa kilimo kinaajiri asilimia kubwa ya watanzania hivyo mapinduzi yanayokusudiwa katika sekta hiyo ni kuendesha kilimo biashara kwa kuongeza uzalishaji na  thamani ya mazao ya wakulima.

  Kuhusu sekta ya Utalii, Dkt. Philip Mpango anayeongoza ujumbe wa wataalamu wa Uchumi na Fedha katika Mkutano wa Mwaka ulioandaliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF, amesema kuwa serikali inakusudia kupitia upya kodi zinazoleta kero mbalimbali katika sekta hiyo pamoja kilimo.

  Eneo jingine alilotaka Benki ya Dunia kuingilia kati, ni kuipatia Tanzania Mkopo na ruzuku utakaosaidia kukabiliana na madeni yake makubwa inayodaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja madeni ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini, TANESCO, ili shirika hilo liweze kujiendesha kwa faida na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa haraka.

  Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, ameihakikishia Tanzania kuwa pamoja na miradi mingine, itafadhili mradi mkubwa wa kilimo wa ukanda wa kusini “Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT)” ili kukifanya kilimo kuwa na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

  “Mimi nimefika Tanzania na ninaifananisha nchi hiyo kuwa itafikia ama kuzidi hadhi ya Dubai kutokana na rasilimali nyingi ilizonazo ambazo zikisimamiwa vizuri zitaibadili kabisa nchi hiyo kimaendeleo” alisema Larose.

  Ameitaka Tanzania kutosita kuitumia ipasavyo benki hiyo kufanikisha malengo yake ya maendeleo na kwamba yeye mwenyewe binafsi pamoja na kwamba anaongoza kundi la nchi 22 za kiafrika katika Benki hiyo, atahakikisha Tanzania kama zilivyo nchi nyingine, inanufaika na uwepo wa Taasisi hiyo.

  Mkurugenzi huyo Mtendaji amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, namna anavyosimamia mambo kwa nguvu zake zote na ametoa pole kwa nchi hiyo kutokana na madhara iliyoyapata kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera na mikoa mingine jirani.
  Ameahidi kuwa Benki hiyo itatuma wataalamu watakaosaidia kufanya utafiti na kuishauri nchi kitaalamu na kimiundombinu namna ya kukabiliana na majanga ya matetemeko pamoja na vifaa vitakavyosaidia kutoa tahadhari kabla ya kutokea kwa majanga kama hayo.
    Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose walipokutana ofisini kwake Jijini Washington DC, Marekani, ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na namna Benki hiyo ilivyojipanga kuhakikisha kuwa  inaiwezesha Tanzania kufikia ndoto yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025

  0 0

  Askofu  wa kanisa la  Kiinjili la  Kilutheri  Tanzania (KKKT)  Dayosisi ya  Iringa Dkt  Owdenburg Mdegela (katikati)  akiwatambulisha  mbele ya waumini wa kanisa  kuu  la Iringa askofu  mteule wa dayosisi  hiyo mchungaji  Blaston  Gavile (wa  pili kushoto)   na mkewe  pamoja na msaidizi wa askofu huyo mchungaji Himid Saga  (wa pili  kulia)  na mkewe.
  Askofu  wa  Dayosisi ya  Iringa Dr Mdegela  (kulia)  akimtambulisha rasmi Askofu mteule wa Dayosisi hiyo Mchungaji Blaston Gavile na mkewe mbele ya  waumini wa kanisa kuu la Iringa leo.
  Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYAHAPA


  0 0


  0 0

   Wataalamu wa Masuala ya Uchumi na Fedha kutoka Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakifuatilia mazungumzo ya mkutano kati ya Shirika la Fedha Duniani-IMF na Wizara ya Fedha na Mipango, mkutano uliofanyika katika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
   Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakiwa katika kikao cha kazi na uongozi wa juu wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, ambapo masuala kadhaa yanayohusu hali ya uchumi na maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na shirika hilo ilijadiliwa, Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
   Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye mkutano na Magavana kutoka nchi mbalimbali za kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini Washington DC nchini Marekani, akielezea juu ya ukuaji wa uchumi katika shughuli za mawasiliano, madini,  huduma ya fedha, bima na huduma za uzalishaji wa viwandani pamoja na changamoto zilizopo..
   Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt. Natu A. Mwamba akifafanua juu ya changamoto zinazoikumba Tanzania katika kukuza  uchumi hasa katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu, akiwa mmoja wa wachokoza mada wengine kutoka nchi kadhaa za Kiafrika kwenye mkutano uliojadili kuhusu hali ya Afrika,  Jijini Washington DC –Marekani.
   Baadhi wa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa hali ya ukuaji wa uchumi katika Nchi za Afrika wakati Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania alipokuwa akiwasilisha mada, Jijini Washington DC-Marekani.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James akiwa na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndullu wakibadilishana mawazo baada ya kushiriki mikutano ya siku ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, nje ya ukumbi wa mikutano ya Benki ya Dunia Jijini Washington DC- Marekani.

  0 0


  Kiongozi Mkuu wa kampuni ya Simtank, Alpesh Patel (kulia) Akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo pamoja na wafanyakazi wa Simtank.
   Kiongozi mkuu wa kampuni ya Simtank, Alpesh Patel (kulia) akimkabidhi funguo ya pikipiki Ravil Patel wakati wa ugawaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la Simtank  uza ushinde.
  Kiongozi Mkuu wa Kampuni ya Simtank, Alpesh Petel(Kulia) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki  Shabbir Suleiman wakati wa makabidhiano ya washindi wa shindano la Smtank uza ushinde jijini Dar es Salaam.
  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  SHINDANO la SIMTANK uza ushinde limefikia tamati kwa washindi watano kupatiwa zawadi zilizokuwa zimeandaliwa kwa washiriki kufikia malengo ya mauzo, ulipaji kwa wakati na uaminifu.
  Akizungumza na waandishi wa habari, Kiongozi Mkuu wa Simtank Alpesh Patel amesema kuwa muda huu ni muhimu sana kwa kuwapongeza wateja wetu ambao wamefanya vizuri katika kutengeneza daraja baina ya bidhaa zetu na jamii.

  Patel amesema, kwa uhakika Simtank kwa namna yoyote imegusa maisha ya wauzaji na wake wanaotumia katika jamii kwani ni namba moja katika kipengele cha kuhifadhi maji kutokana na utumiaji wa malighafi bora kabjsa za viwango vya kufungia bidhaa za chakula na zilizoweza kuhimili mwanga wa jua.

  Shindano hilo lililoanza June 1 na kumalizika Agosti 31 lilifanikiwa kupata washindi watano kwa kuangalia kipengele cha nne na kila mmoja kupatiwa pikipiki baada ya kufanyika kwa promosheni hiyo.

  Washindi wa shindano hilo ni Mohamed Mohamed, Bulk Distributors Ltd, Mwanza Huduma, Shangwe Hardware Ltd na Aim Steels na Patel kuzitaka kuendelea na kauli mbiu ya kujenga mahusiano imara baina yao na wadau wa biashara.

older | 1 | .... | 1384 | 1385 | (Page 1386) | 1387 | 1388 | .... | 3348 | newer