Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1383 | 1384 | (Page 1385) | 1386 | 1387 | .... | 3348 | newer

  0 0

  UJENZI WA HOSPITALI YA KISASA YA KUFUNDISHIA WATAALAMU WA AFYA NA KUTOA HUDUMA SHIRIKISHI YA MUHIMBILI ILIYOPO MBEZI ENEO LA MLOGANZILA TAKRIBAN KILOMETA 25 TOKA JIJINI DAR ES SALAAM UMEKAMILIKA NA INATARAJIWA KUANZA KUFANYA KAZI IFIKAPO MWEZI JANUARI 2017 KWA KUFUNDISHIA FANI ZA AFYA NA KUTOA HUDUMA YA MATIBABU KWA WAGOJWA. PATA MWANDANI WA TAASISI HII KUBWA NA YA KISASA  - BOFYA MSHALE MWEUPE:

  0 0

   The Collection aim to support MSICHANA INITIATIVE, Bicycle for Enhancing Girl Education in Bahi, Dodoma. 
  Msichana Initiative is a non profit organization in Tanzania established to advocate for girl's right to education in Tanzania. This includes addressing and finding solution for key challenges, which limits girls right to education. The initiative seeks to ensure this inherent right is given to all human beings.
  THE NEED:
  Most of secondary school students in rural areas walk to school. School location and distance from household limits girl performance in the classroom, pose challenge in the regular school attendance as well as participation in extra-curriculum activities and after school events. Those who walk long distance to school arrive late and most of the time physically exhausted, which affect their ability to learn. This situation puts girls at a high risk of sexual harassment, pregnancies and early marriages causing them poor academic performance and/or forcing them to drop out of school. The situation therefore limits opportunity for the girl student to access education and constitutes gender disparity in school settings.
  THE OPPORTUNITY:
  ILAVA will to donate 20% of MSICHANA COLLECTION towards Bicycle for Enhancing Girl Education in Bahi, Dodoma. 
  THE GOAL: 50 Bicycles by the of 2017. 

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Felchesmi Mramba, (kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton baada ya kusini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme (transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. Shirika hilo limeingia mkataba na makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za Kimarekani
  309.26
   Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton wakisaini mkataba huo
   Mhandisi Mramba, (kushoto), na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba
   Mhandisi Mramba, akibadilishana hati na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, baada ya kusaini mkataba.

  0 0
  0 0

  UMOJA wa Wafanyabiashara wa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo (DRC)  Bw. Sumael Edward, ametangaza kurejea kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo kutumia Bandari ya Dar es Salaam. 
  Bw. Edward alisema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa iadara ya Habari Maelezo.
  “Sisi kwa moyo mmoja tumeamua kurejea Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya Baba zetu wote wawili Rais John Magufuli na Joseph Kabila kukubaliana mambo mazuri ambayo sisi kama wafanya biashara tunaona yana tija kwetu katika kukuza umoja wetu kati ya Tanzania na DRC”amesema Edward.
   Aliongeza kuwa kwa sasa wanashukuru mizigo yao kwa sasa haikai bandarini kwa kuchelewa na hakuna ubabaishaji wa kupelekwa bandari pasipokuwa na lazima.
   Alimaliza kwa kusema kuwa kwa sasa wananchi wa DR Congo wote wameanza kurejea Tanzania na biashara zote zitakuwa kama zamani na maduka yote Kariakoo yatapata wateja.
  Rais wa Wafanyabiashara wa nchini DR Congo Bw. Sumael Edward akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Tiganya Vicent. 
  Picha na Habari na Humphrey Shao wa Globu  ya Jamii

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  leo ametoa majibu kuhusu na hatma ya kijana Said Ally (anayemfariji juu pichani) aliyetobolewa macho na mtuhumiwa aitwaye Scorpion maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena. Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa amesema:

  "Nianze kuwashukuru ndugu zangu wa Clouds hasa kipindi cha #LeoTena kwa sauti zao mpaka kumfikia ndugu yetu Said ambaye alitobolewa macho kinyama na  kwa sasa haoni tena.... 
  "Majibu ya daktari yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi.  Majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote.

  "Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam imejitolea k
  umpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena.

  "-•Kumpatia Elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira.
  "-•Serikali ya Mkoa imetoa Gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake.
  "-•Vilevile Serikali yetu itatoa kiasi cha Shilingi milioni 10 kama sehemu ya Mtaji. Kabla ya kupatwa na ulemavu Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwa kuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja".

  #KutokaOfisiYaMkuuWaMkoa
  Said Ally akifarijiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Mhe. Paul Makonda.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam Mhe. Paul Makonda katika majonzi.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa, Balozi  Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hamisi Kigwangwalla katika picha ya kumbukumbu   na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016.
  Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe Jack Mugendi Zoka akichangia mada wakati wa mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe Jack Mugendi Zoka baada ya kuongea na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016 

  KWA PICHA ZAIDI BOFYAHAPA
  0 0
 • 10/08/16--06:07: Article 24


 • 0 0


  0 0

  Kwaya ya Wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule ya sekondari KORIDO iliyopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wakiimba kwaya kwenye mahafali ya 7 Toka kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2009.
  Picha na Yeremias Ngerangera

  0 0

  Na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM -Mbeya

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewashauri vijana kutumia ngoma za asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.

  Ametoa ushauri huo leo Mjini Mbeya alipokuwa akifunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 na kuwahimiza vijana kutosubiri kuajiriwa ikiwa wanaona wana uwezo wa kufanya kitu ambacho kitawasaidia kupata kipato na kuendesha maisha yao.

  “Ngoma za asili ni chanzo cha ajira kwa vijana na sisi kama Serikali tutashirikiana na wadau wa Sanaa na Utamaduni ili kutengeneza ajira na kudumisha mila na desturi za nchi yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.

  Aidha kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa fursa pekee kwa vijana kujiajiri kupitia shughuli za Sanaa na Utamaduni kwani ndio sekta ambazo zimetoa ajira kwa vijana wengi duniani kwa sasa.

  “Nawashauri vijana wa kitanzania kuangalia na upande huu wa Sanaa na Utamaduni kuna ajira pia na sisi tupo pamoja nao na tutawapa ushirikiano ili wafikie malengo” alisema Mhe. Tulia.

  Tamasha hili liliondaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson linafanyika kwa siku mbili na limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili vipatavyo 62 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( wa pili kulia) akifurahia jambo na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson (kulia) wakati wa KUFUNGA Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016  liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016. 
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za kiutamaduni Wwakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016 kulia ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu Mtendaji BASATA Geodfrey Mngereza. 
  Kikundi cha Utamaduni cha Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM. 

  0 0

   Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam,wakishiriki katika mazoezi ya viungo yaliyoandaliwa na EFM radio na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Wakifanya mazoezi katika kiwanja cha Magunia Msasani jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam,wakishiriki katika mazoezi ya viungo yaliyoandaliwa na EFM radio na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Wakifanya mazoezi katika kiwanja cha Magunia Msasani jijini Dar es Salaam.
  Msanii chipukizi wa mziki wa singeli, Yohana Mruta akiimba baada ya mazoezi ya viungo kuisha yaliyoandaliwa na EFM radio na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania katika kiwanja cha Magunia Msasani jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Editha Karlo wa 
  Globu ya Jamii,  Kagera

  MAMA mmoja na watoto wake wanne wakazi wa kijiji cha Nyamilanda kata ya Kyebitembe wilaya ya Muleba Mkoani kagera wamefariki dunia jana baada ya kula chakula aina ya ugali unaosadikiwa kuwa na sumu.

  Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamilanda Trasias Baltromeo amesema watu hao waliofariki ni mama na watoto wake wanne ambao walikula ugali majira ya saa tisa mchana na kuanza kutapika na hatimaye kufariki dunia wakipelekwa Kituo cha Afya Kimeya kilicho jirani na kijiji hicho

  Baltromeo amewataja waliofariki kuwa ni mama wa watoto Julitha Julius (35) Haujeni Julius (14) Superius Julius (12), Gabriel Julius (4) na Paschazia Julius mwenye umri wa miezi sita.
  Mwenyekiti huyo alisema katika tukio hilo mama aliandaa mboga aina ya dagaa na kwenda kwa mama mkwe wake nyumba jirani kutafuta unga wa muhogo na walipomaliza kula yeye na watoto wake wakaanza kutapika na kuanza kuhangaika hatimaye wananchi wakafika lakini juhudi za kuokoa maisha yao hazikuzaa matunda.
  "Nilipofika nilikuta hali ni mbaya wakitapika na kuamua kwenda kutoa taarifa polisi Kyebitembe lakini walipofika wakati wanawakimbiza hospitali ndogo ya kimeya wakawa wamefariki watoto wanne na mama yao”Alisema Mwenyekiti.
  Tukio la Kifo kama hilo limetokea mwaka jana kata ya Kasharunga tarafa ya Kimwani jimbo la Muleba kusini wilayani humo ambapo watu saba wa familia moja walikula chakula chenye sumu na kuokoka watu watatu pekee wanne walifariki dunia.
  Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi ameongea na mtandao huu naye pia amekiri kupokea taarifa hiyo na kwamba hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusishwa na vifo hivyo lakini uchunguzi wa wataalamu wa afya unaendelea ili kujiridhisha na kutambua aina ya sumu iliyotumika hadi watu hao wakapoteza maisha yao.
  Mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi Richadi Ruyango amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba jopo la wataalamu wa afya na jeshi la polisi limekwenda kituo cha Afya Kaigara na Hospitali ya Rubya kufanya uchunguzi kwa miili ya marehemu hao.
  Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi katika tarafa ya7 kimwani kuwa makini na vyakula wanavyokula kwani hilo ni tukio la tatu la familia kula vyakula vyenye sumu na kupoteza maisha kijijini hapo

  0 0

  SIMU.tv: Fahamu kauli ya  katibu mkuu wa baraza la michezo Tanzania kuhusu vilabu vya Yanga na Simba kubadili mfumo wa kiundeshaji; https://youtu.be/gjLJ0qy5bZU

  SIMU.tv: Wakuu wa wilaya wametakiwa kuwachukulia hatua kali wahandisi wa maji kwa kushindwa kuwalipa wakandarasi kwa wakati ; https://youtu.be/oNjXRh7V-JI

  SIMU.tv: Rais John Magufuli awataka mabalozi wa Tanzania kutilia mkazo wa diplomasia ya uchumi katika kutimiza lengo la Tanzania ya viwanda; https://youtu.be/cz4Ce1m31FE

  SIMU.tv: Serikali visiwani Zanzibar imewataka wananchi kutokuvamia maeneo ya shule kwa ajili ya shughuli zao binafsi; https://youtu.be/tdAIp1GYtNM

  SIMU.tv: Shirika la Elimu Tanzania HAKIELIMU laifagilia serikali kwa hatua iliyochukua kwa walimu waliompiga mwanafunzi huko mkoani Mbeya; https://youtu.be/ivU7vmNmumQ

  SIMU.tv: Ripoti ya madaktari kutoka hospitali ya Muhimbili inaonyesha kijana Said Ally aliyetobolewa macho hataona tena. https://youtu.be/ajvFmbjkyXw

  SIMU.tv: Watendaji wa ngazi ya vijiji hadi wilaya katika wilaya za Tunduru na Namtumbo wametakiwa kusimamia vyema  ununuzi wa zao wa korosho; https://youtu.be/c7QHSDH7xVc

  SIMU.tv: Wazee nchini wametakiwa kujitokeza katika fursa zilizowekwa na serikali za wazee kupatiwa bima za afya; https://youtu.be/RuI9w0mnbqE

  SIMU.tv: Makamu wa Rais Samia Suluhu awataka watanzania kutumia bidhaa zinazotengezwa nchini ili kukuza uchumi wa taifa; https://youtu.be/76G8gTLXlnw

  SIMU.tv: Serikali yawahakikishia walimu kulipwa malimbikizo ya madeni yasiyo ya mshahara;https://youtu.be/Lzv7pNcCroo

  0 0

  Mshindi wa kwanza Kitaifa kwenye shindano ya uandishi wa barua, Denis Bahati Stephen, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
   Mshindi wa pili Kitaifa katika shindano ya uandishi wa barua, Samweli Lufungulo Somelo, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
  Afisa Masoko, Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Mponda, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
  Mkuu wa Shule ya Saint Mary's Seminary, Maximillian Buluma, akipokea zawadi ya shule hiyo baada ya kuwa shule iliyotoa washindi kitaifa pamoja na washiriki wengi. Amepokea mpira pamoja na Cheti kutoka Shirika la Posta.
  Kulia ni Meneja wa Posta Mwanza, Julius Chifungo, akimkabidhi mgeni rasmi zawadi. Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  Kongamano la mtoto wa kike lililofanyika leo mjini Shinyanga limeitaka serikali kuweka juhudi za makusudi kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia hasa kwa watoto wanaoozeshwa ndoa za utotoni kutoka kwa wazazi na walezi wao.

  Maadhimisho haya yanaendelea kufanyika mjini Shinyanga ili kuungana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike inayoendelea kuadhimishwa Mkoani hapa ambayo kilele chake ni tarehe 11 Oktoba 2016.


  Maadhimisho hayaufanyika kila mwaka ikiwa ni mwitikio wa Azimio la Umoja huo lililopitishwa mwezi Desemba mwaka 2011.


  Akiongea katika kongamano la watoto mkoani shinyanga Mkurugenzi wa Watoto Bi. Magereth Mussai kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amelaani wale wote wanaoozesha watoto ambao wako katika umri wa kwenda shule kwasababu ndoa za utotoni uwafanya watoto hawa kushindwa kufikia ndoto zao ikiwemo haki ya kupata elimu ya juu.


  Wakati huo huo watoto wawili ambao hawakutaka majina yao kutajwa kwasababu ya kulinda haki za watoto wametoa ushuhuda wao wa ni namna gani ndoa za kulazimishwa wakiwa wadogo zilivyoelekea kukatiza ndoto yao kabla ya kuokolewa na shirika la AGAPE kuwaokoa

  na kuwaendeleza kielimu.


  Mmoja wa Watoto hao ambaye jina limeifadhiwa amesema ndoa yake ya utotoni iligubikwa na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mme wake ambaye alimpatia ujauzito na baadae kumtelekeza yeye na mtoto.


  Alendelea kusema kuwa inamuuma sana kama mlengwa kuwa mzazi na wakati huo kuwa mwanafunzi anayesoma kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali huku baadhi ya wazazi na walezi wakiendeleza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.  


  Watoto wao kwa pamoja wameitaka serikali na vyombo vya habari kuwekeza nguvu zao kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa za utotoni ambazo zimekuwa kikwazo kwa mtoto wa kike kufikia ndoto zake.


  Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), inakadiriwa kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo wasichana wapatao milioni moja wanatarajiwa kuwa wameolewa katika umri wa chini ya miaka 18 duniani kote.

  Mkurugenzi wa Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Magereth Mussai akiongea na Watoto hawapo pichani katika kongamano la mtoto wakike linaoendelea mjini Shinyanga.


  Baadhi ya Watoto Wakifuatilia jambo katika kongamano la watoto linaloendelea leo jijini Shinyanga
  Afisa Maendele ya Jamii Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Anna Muhina akiongea na Watoto hawapo pichani katika kongamano la mtoto wakike linaoendelea mjini Shinyanga.

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  (kushoto) katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa ukitokea Kishapu Mkoani Shinyanga.
   Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisoma taarifa ya Mkoa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016, Ndg. George Mbijima katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Shinyanga.

   Baadhi ya wasanii wa Ngoma ya Wagoyangi kutoka Maswa wakitoa burudani kwa kucheza ngoma wakiwa na nyoka aina ya chatu, mbele ya wananchi wa Wilaya hiyo waliofika katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Wigelekelo.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe.

  0 0

  MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Mhe Deogratius Ndejembi

  MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deogratius Ndejembi amekifunga Chuo cha Ualimu cha Nkuruma kilichopo Mkoka na kuagiza uongozi wa chuo kurudisha fedha zote za ada walizolipa wanafunzi ili ziwasaidie kulipia vyuo vingine.

  Alitoa agizo hilo wakati wa mkutano na wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo hicho kuhusu kutafuta suluhu ya mgogoro ambao ulianza Septemba 16, mwaka huu. Chuo hicho kilidahili wanafunzi 77 kwa lengo la kuwafundisha ualimu, walipofika wakaambiwa wanasoma masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

  “Baadaye wakaambiwa wanabadilishiwa masomo sasa wanasoma Maendeleo ya Jamii, hii yote wamefanya kwa kuwa chuo hakina usajili wowote.Ada wamechukua na hakuna kinachoendelea,” alisema Ndejembi.

  Ndejembi alifikia hatua ya kukifunga chuo kutokana na wanafunzi kugoma kufanya mitihani ya chuo ya kumaliza mwaka wa masomo kwa madai chuo hakitambuliwi na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

  Alisema kukifungia chuo pekee haitoshi wanatakiwa kurudisha fedha zote za ada walizolipwa na wanafunzi katika mwaka huo wa masomo uliopita ili kuwasaidia kulipa vyuo vingine.

  “Kuwarudishia fedha sio mwisho wa jambo hili kwa sababu mmepotezewa muda wenu na haki yenu ,mmeonewa, mmedhulumiwa kwa kusema hivyo namwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya na timu yake kuwakamata sasa hivi na wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria ili haki iweze kutendeka,” alisema.

  Amewataja wanaotakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria kuwa ni mmiliki wa chuo, Mathew Nkurlu, Msajili wa Chuo, Yohana Michael, Mhasibu Elieth Ruben, wakufunzi Pendael Petro na Christopher Mabatian.

  Ndejembi alitaja sababu za kuagiza wakamatwe viongozi hao wa chuo ni kuwa walihusika kushiriki katika kufanya udanganyifu na kuwatapeli wanafunzi hao huku wakijua kinachoendelea.Aidha, alisema serikali itawasaidia katika utaratibu wa kupata vyuo vingine kwa wale wenye sifa za kujiunga na vyuo katika kozi ambayo walianza kusoma.

  Alisema kama ikitokea chuo hakina fedha za kuwarudishia wanafunzi, majengo yao yatatumika kama dhamana ya ada kwa vyuo ambavyo vitawapokea wanafunzi hao. Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho, Mhoja Matando aliishukuru serikali kwa kuwasaidia kujua hatma ya kutimiza ndoto yao ya kielimu. 

  0 0

   katibu wa Hospitali ya  Litembo Anna Mwenda kulia,akizungumza  leo kabla ya kupokea msaada wa shuka 46 kutok kwa benki ya NMB Tawi la Litembo wilayani Mbinga,wa pili kulia meneja wa NMB Litembo Kennedy Chinguile na wa tatu kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo Dkt Maurus Ndomba.
   Katibu wa hospitali ya Litembo wilayani Mbing Anna Mwenda kulia akimshukuru mmoja kati ya wafanyakazi wa BENKI  ya Nmb tawi la Litembo baada ya kupokea msaada wa shuka 46 kwa jili y amtumizi katika hospitali hiyo.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Nmb tawi la Litembo wilayani Mbinga wakitoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa  waliolazwa katika hopitali ya Litembo wilayani Mbinga.
   Mmoja wa wagonjwa aliylezw katika hospitali ya Litembo   wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma  Folkwati Komba(4)akimwamkia  mkono mfanyakazi wa benki ya Nmb ambaye hakufahamika jina lake mara baada ya benki hiyo kutoa msaada wa mashuka na vitu mbalimbali.

  0 0

   Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif akizungumza na wana CCM na Wananchi wa Matawi ya Mangapwani na Mangapwani Bondeni katika Mkutano wa kutoa shukrani baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu.
   Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mh. Bahati Ali Abeid akisisitiza Jambo wakati wa Mkutano wa kushukuru wapiga kura wake baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu hapo Tawi la CCM Mangapwani.
  Baadhi ya Viongozi wa Kamati za Siasa na wana CCM wa Matawi ya Mangapwani na Mangapwani Bondeni wakifuatilia hotuba ya Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Mahonda hawapo Pichani Balozi Seif na Mh. Bahati waliofika kutoa shukrani baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1383 | 1384 | (Page 1385) | 1386 | 1387 | .... | 3348 | newer