Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

NEC YAPONGEZWA KWA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA MKOANI SIMIYU.

0
0

Na. Aron Msigwa –NEC.Bariadi –Simiyu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepongezwa kwa kuanzisha programu endelevu  za utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao kote nchini.

Akitoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea Banda la Maonesho la Elimu ya Mpiga Kura la NEC wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Bariadi mkoani Simiyu,  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama amesema kuwa hatua ya NEC  kutoa elimu ya mpiga kura kupitia maonesho hayo inawasaidia wananchi kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na chaguzi za Tanzania.

“ Nawapongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuanzisha utaratibu huu wa kushiriki maonesho mbalimbali, mnafanya kazi nzuri, endeleeni hivyo hivyo kuwaelimisha wananchi” Amesema Mhe. Jenista.

 Ameeleza kuwa ushiriki wa NEC katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana unawapa fursa vijana wengi kupata elimu sahihi kuhusu wajibu wao na majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Kwa upande wake Afisa Habari wa Idara ya Elimu ya Mpiga Kura ya NEC Bi. Margareth Chambiri amwemweleza Waziri huyo kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha program endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura kwa kuhakikisha kuwa wananchi moja kwa moja katika maeneo mbalimbali nchini.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama (katikati) akikata utepe kufungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana leo mkoani Simiyu.   Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka (wa pili kutoka kushoto), Waziri Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus Kamani na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia).Picha na Aron Msigwa – NEC.
Wananchi wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakipata elimu ya Mpiga Kura kwenye banda la Maonesho la NEC leo.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama akipata maelezo kuhusiana na Elimu ya Mpiga Kura alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo mkoani Simiyu.
 Baadhi ya Wanachi wakifuatilia ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere wilayani Bariadi mkoani Simiyu leo.


MASAUNI ALITAKA JESHI LA MAGEREZA KUTEKA SOKO NDANI YA NCHI

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun aagiza Jeshi la Magereza kuzidi kuboresha viatu vinavyotengenezwa na kiwanda chao ili kujipatia soko kubwa ndani ya nchi na nje. 
Hayo aliyasema jana kwa wakuu wa Gereza la karanga na viongozi wa kiwanda hicho alipofanya ziara yake ya siku moja katika kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo, mkoani Kilimanjaro
Aidha, Naibu Waziri huyo alisisistiza Jeshi hilo kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi la Magereza, hivyo ni muhimu kuendelea kuzalisha bidhaa zilizo bora zaidi
Haiingii akilini maofisa wa majeshi mbalimbali nchini kuagiza viatu nje ya nchi wakati viwanda vya ndani vinauwezo wa kuzalisha viatu bora zaidi vinavyodumu kwa muda mrefu kuliko vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi, alisema Masauni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akijionea kiatu aina ya Safari buti kinachozalishwa na Kiwanda cha Karanga kilichopo Mkoani Kilimanjaro wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kiwandani katika Mkoa huo. Masauni amesisitiza kiwanda hicho kuzalisha bidhaa bora zaidi ili kuteka soko kubwa zaidi pamoja na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho Mrakibu Msaidizi, Michel  Minja na kushoto ni Ali Jambaraga Fundi Mkuu. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akiangalia kiatu kilichokuwa tayari kuvaliwa kilichotengenezwa katika kiwanda cha Karanga kilichopo Gereza Kuu la Karaga mkoani Kilimanjaro. Naibu Waziri huyo amesisitiza Jeshi hilo kuzidi kutengeneza bidhaa bora zaidi za viatu ili kuhakikisha wanapata soko kubwa ndani nan je ya nchi., kulia ni Kamishan Msaidizi Mwandamizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa aliye aambatana nae kwenye ziara hiyo. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun (aliyevaa koti) akitoa maelekezo kwa Wakuu wa Gereza la Karanga na kiwanda cha Viatu kilichopo gerezani hapo. Masauni amelitaka jeshi hilo kuzidi kutoa bidhaa bora ili kuendelea kuteka soko kubwa ndani nan je ya nchi. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MWANAFUNZI BORA SOMO LA BAILOJIA KITAIFA HUYU HAPA

0
0
 Mwanafunzi bora wa somo la bailojia kitaifa kwa mwaka 2016, Bi. Anab Faisal Issa (katikati) akiwa katika picha na wazazi wake, Bw. Faisal Issa (wa pili kulia) na Bi. Beng’i Issa (wa pili kushoto) pamoja na walimu wa shule ya sekondari Feza mara baada ya kupokea tuzo katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali kwa lengo la kuwatambua na kuwapa moyo wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.  Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Afisa tawala wa wizara ya afya Bw Michael John akikabidhi cheti kwa mwanafunzi bora wa somo la bailojia kitaifa kwa mwaka 2016 kutoka shule ya Feza  Bi.Anab Faisal Issa katika hafla iliyoandaliwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali kwa lengo la kuwatambua na kuwapa moyo wanafunzi wengine kupenda masomo ya sayansi.

Wanaofanya biashara kienyeji wapewa miezi miwili kuzirasimisha

0
0
Afisa Mkuu Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Frank Kanyusi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Alionya wafanyabiashara ambao hawajasajili majina ya biashara kufanya hivyo katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa au kuchukuliwa hatua za kisheria.


Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa muda wa miezi miwili kwa wafanyabiashara wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajiliwa wafanye hivyo haraka.

Akizungumza na waandishi wa waandishi wa jijini Dar es salaam  jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi alisema katika zoezi la kutoa elimu na kurasimisha majina ya biashara na kampuni linaloendelea katika mikoa mbalimbali imebainika kuwa wafanyabiashara wengi wanatumia majina ya biashara pasipo kuyasajili.

“Sheria ya majina ya biashara inamtaka mfanyabiashara kusajili jina la biashara yake ndani ya siku 28 toka aanze kulitumia,” alisema Bw.Kanyusi na kuongezea kuwa kinyume na hapo atakuwa amevunja sheria ya majina ya biashara.

Alisema baada ya muda huo kupita, patakuwa na msako nchi nzima ili kuwabaini wale wote wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria au kuwatoza faini.

Alisema kuwa sasa usajili wa majina ya biashara umerahisishwa kwani unafanywa kwa njia ya mtandao kwa kutembelea tovuti ya wakala huo ambayo ni www.brela.go.tz ili kupata maelezo yote ya namna ya kusajili jina la biashara.

Aliwataka wafanyabiashara wasiishie kusajili tu jina la biashara bali pia waende katika Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kupata namba ya Mlipa Kodi (TIN) pia waendele katika halmashauri zao kupata leseni ya biashara.

“Kwa kurasimisha biashara serikali itapata mapato kwani wigo wa walipa kodi utaongezeka na pia itakuwa faida kwa wafanyabiashara katika kujengewa mazingira bora ya kufanya biashara,” alisisitiza Bw.Kanyusi.

Alisema BRELA imejipanga kuzunguka mikoa yote nchini ili kutoa elimu juu ya urasimishaji wa majina ya biashara na makampuni kwani imeonekana wananchi hawana uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa urasimishaji.

Hadi sasa BRELA imefanya ziara katika mikoa ya Mwanza, Mara, Geita na Simiyu na wiki hii watakuwa mkoani Shinyanga kwa muda wiki moja katika kuhamasisha wafanyabiashara kurasimisha biashara zao.

Alisisitiza kuwa ni lazima kuhakikisha kuwa biashara zinarasimishwa ili serikali iweze kuwatambua walipa kodi wake ambao watachangia pato la taifa na kuiwezesha Tanzania kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Analoga official video Chaba ft. Hisia

EFM YAENDELEA KUSAKA VIPAJI VYA SINGELI

0
0

Kituo cha EFM kimeendelea na harakati zake za kuwasaidia na kuwainua vijana wanaojihusisha na muziki. Kwa kutumia shindano maalumu la singeli michano linalofanyika kila siku ya jumamosi kuanzia saa nne hadi saa sita mchana, EFM radio inasaka wasanii chipukizi wenye vipaji vya kuimba nyimbo za singeli na baadae kuwaendeleza katika muziki huo. 

Zoezi hili ni endelevu na litadumu kwa muda wa wiki 12 katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam na Pwani ambapo muziki mnene utafika.

Jumla ya wasanii 5 huibuka na ushindi na washindi hawa hupatikana kila eneo ambapo zoezi hili la kusaka vipaji vipya vya singeli (Singeli Michano) hufanyika.

Meneja matukio na mawasiliano ya efm redio Neema Mukuarsi amesema baada ya zoezi hili wasani hawa chipukizi watapata nafasi ya kupata semina kutoka kwa TCRA, BASATA na TRA pale Dar live siku ya ijumaa ya tarehe 14.10.2016 saa 8;00 mchana ili waweze kupata elimu ya kulipa kodi,waweze kuimba nyimbo zenye maadili na kuhakikisha nyimbo zao zinakuwa na maadili katika jamii. 

Msaani chipukizi, Jfari Salumu a.k.a Winnero akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.
Msaani chipukizi,Ramadhani Iddi a.k.a Sindano Simba akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa mziki wa nyimbo za singeli wakiendelea kupagawa katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS KABILA WA CONGO DRC KTK UZINDUZI WA JENGO LA TPA

ANZA MWAKA MPYA WA KIISLAM 1438 KWA KUCHANGIA KHEIRI (SADAQATUL JAARIYA).

0
0
Asaalaam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatu.
Katika kuu adhimisha Mwaka Mpya wa kiislam Hijria 1438  Siku ya Jumamosi ya Tarehe 1/10/2016 na Jumapili 2/10/2016 Kwa Uwezo wa Allah tulianza kuchimba Msingi katika Markaz yetu na Kuanza Ujenzi wa kituo cha MARKAZ SHAAFIYATUL AZHARIYA  huku Mbezi Salasala jijini Dar es salaam.
Leo Jumapili Tar 9/10/2016  ni mapumziko katika harakati zetu. Kesho Jumatatu Mungu akipenda tunaendelea na ujenzi. Malipo kwa Mafundi tayari tumetimiza Tshs 600,000/= Bado Tshs 400,000 /=. Fundi wa geti amefika na kataja gharama zake za kutengeneza geti milango miwili mkubwa na mdogo amehitaji Milioni Moja.
Hivi tunavyoongea mchanga umekwisha kabisa site (Muhimu kupatikana kwa haraka kukamilisha Ujenzi) Tshs 180,000 na Nondo 15 @ Kila Nondo Moja 15500/=. Michango inaendelea na kwa kidogo utakachotoa ndicho kitakachofanikisha haya yote. 
Kwa heshma na Taadhima nakualika wewe Mpenda kheiri ambae upo tayari kuja kuchangia kwa hali na Mali kukaribia katika zoezi hili. Kwa yoyote ambaye yupo tayari kushiriki kuja kuchimba Msingi namkaribisha 

Tafadhali tuma Mchango wako kupitia ama wsiliana nasi kwa Namba 0715800772 (CALL or SMS,  WHATSAPP, TIGO-PESA ) utazungumza na Na Mratibu Msimamizi  GHALIB N MONERO. 


 Sehemu ya uwanja kabla ya kuanza kazi ya kuchimba msingi

.


 Hatua ilipofikia wiki iliyopita
Hatua iliyofikia wiki hii. 

Kasesela cup

Kutoka VOA SWAHILI: Zulia Jekundu S1 Ep 95: Kim Kardashian, Barack & Michelle Obama, Selena Gomez, Rihanna

0
0
Mkamiti Kibayasi wa Idhaa ya Kimataifa ya 
Sauti ya America (VOA) kutoka Washington DC.
 Zulia Jekundu ni kipindi cha televisheni cha kila wiki ambacho hukuletea habari mbalimbali za burudani zinazotamba. Humu utapata kujua juu ya habari za mastaa zinazogonga vichwa vya habari, kujua baadhi ya wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa wiki husika na hata filamu 5 zilizoongoza kwa mauzo katika wiki hiyo.
KARIBU

Zoezi la Kubadilisha Hati za kusafiria kwa Watanzania Waishio Michigan, MAREKANI

0
0
Kwa niaba ya Wanajumuia ya Watanzania waishio Michigan Detroit, tunaomba kuwatangazia Watanzania wote wanaoishi Jimbo la Michigan na miji yote ya jirani kuwa kutakuwa na zoezi la kubadilisha pasipoti ambapo maafisa toka Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC watakuwa hapa kutoa huduma hiyo.
Zoezi hili litafanyika:
SIKU: Ijumaa Oktoba  14-16, 2016
MAHALI:
Quality Inn Hotel
26111 telegraph rd
Southfield, MI 48033

Mahitaji ya Jumla kwa Kupata Pasipoti Mpya
MAHITAJI YA JUMLA: 
1. Picha tano light blue colour background
2. Nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
3.Nakala ya Drivers License.
5. Pasipoti halisi na nakala yake.
Kwa waliopoteza pasipoti wahakikishe pia wanakuwa na Police report.
Tangazo la Gazeti na Maelezo ya namna pasipoti ilivyopotea. 
Kwa maelezo na mawasiliano zaidi wasiliana na  
Ndg. Phi Mzava kwa namba 248-417-5015
Kwa maelezo zaidi. Kwa mahitaji ya pasipoti 
tembeleeni tovuti ya Ubalozi wa Tanzania.
 Wote Mnakaribishwa

EFM 93.7 YAENDELEA KUSAKA VIPAJI VYA SINGELI

0
0
Na Emmanuel Masaka
Kituo bora cha redio cha EFM 93.7 kinaendelea na harakati za kuwasaidia na kuwainua vijana wanaojihusisha na muziki kupitia zoezi maalumu la "Singeli michano" linalofanyika kila siku za Jumamosi kuanzia saa nne hadi saa sita mchana.
Zoezi hili ni endelevu na litadumu kwa muda wa wiki 12 katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam  na Pwani ambapo muziki mnene utafika.
Jumla ya wasanii 5 huibuka na ushindi na washindi hawa hupatikana  kila eneo ambapo zoezi hili la kusaka vipaji vipya vya Singeli Michano hufanyika.
Meneja matukio na mawasiliano wa EFM  redio Neema Mukuarsi amesema baada ya zoezi hili wasani hawa chipukizi watapata semina kutoka TCRA, BASATA na TRA ukumbi wa  Dar Live Mbagala siku ya Ijumaa  tarehe 14.10.2016 kuanzia saa 8:00 mchana ili kupatiwa  elimu ya kulipa kodi na kuhakikisha nyimbo zao zinakuwa na maadili katika jamii.
 Msaani chipukizi, Jfari Salumu a.k.a Winnero akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za Singeli jijini Dar es Salaam.
 Msaani chipukizi,Ramadhani Iddi a.k.a Sindano  Simba  akionesha uwezo wake jukwaani
Sehemu ya mashabiki wa mziki wa  nyimbo za singeli wakiwa katika tamasha hilo.

WAAMBIENI WAJE TUKO TAYARI – Mbeya City Council FC

0
0
Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Mbeya City Fc leo kimeanza rasmi mazoezi kujiweka sawa tayari kwa mchezo mwingine wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba  Sc  uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine  jumatano ijayo hii  ikiwani siku tano tu baada ya suluhu ya bila kufungana na Stand United.  Kwa taarifa kamili na mengi mengineyo ya Mbeya City BOFYA HAPA

Nyumbani Na Diaspora Nyoni Kutoka China Season 3

Extended Services Limited: WE SHIP ALL TYPES OF CARGO (SEA FREIGHT AND AIR FREIGHT CARGO) TO EAST AFRICA AT UNBEATABLE RATES, i.e. BOUTIQUE STUFFS AND ACCESSORIES CONTAINERS, TRUCKS, CARS, MACHINERY ETC.

0
0

WE ARE THE MOST AFFORDABLE AND RELIABLE SHIPPING AGENT IN THE U.K.

      CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 850 (TILBURY/ SHERNESS PORTS)
CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 750 (SOUTHAMPTON/ NEWCASTLE PORT)
4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 910 (SOUTHAMPTON PORT)
4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 945 (NEWCASTLE PORT)
4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 930 (TILBURY/ SHEERNES PORTS)
        40’ CONTAINER TO DAR FROM £ 1600
40’ CONTAINER TO MOMBASA FROM £ 1575 HC
40’ CONTAINER TO ZANZIBAR FROM £ 2130
20’ CONTAINER TO DAR FROM £ 1000
20’ CONTAINER TO MOMBASA £ 970
20’ CONTAINER TO ZNZ FROM £ 1500
        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2650(TILBURY PORT)
        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2400(SOUTHAMPTON)
        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2450(NEWCASTLE)
        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM 2612.50(IMMINGHAM PORTS)
        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2612.50 (KILLINGHAM)
        ALSO WE CAN       ARRANGE PRE SHIPMENT INSPECTION FOR YOU TO AVOIDINCONVINIENCES.
·       GOOD NEWS FOR AIR CARGO CUSTOMERS FOR NAIROBI, MOMBASA AND DAR ES SALAAM!!!!!.
·         WE SHIP AIR CARGO TO NAIROBI FOR ONLY£2(EXCLUDING CLEARANCE).
·         WE SHIP AIR CARGO TO MOMBASA FOR ONLY£2.50(EXCLUDING CLEARANCE)
·         WE SHIP AIR CARGO TO DAR ES SALAAM FOR ONLY£2.50(EXCLUDING CLEARANCE)
·         WE SHIP AIR CARGO TO DAR ES SALAAM WITH CLEARANCE 
ONLY FOR £ 5
AUGUSTINE HAULE,
 EXTENDED SERVICES LIMITED, 
Registered Office Address: 
Clipper House,
Tilbury Freeport, Tilbury, Essex,
RM18 7SG,
Registered in England No:08617639 
Email: extendedservicesltd@gmail.com, www.extendedserviceslimited.co.ukTel: +44 1375767890, Mobile +44 7438145815 

MKURUGENZI MKUU WA PPF, WILLIAM ERIO AKAGUA ENEO LITAKALOTUMIKA KUJENGA KIWANDA KIPYA CHA KUCHAKATA NGOZI NA KUTENGENEZA VIATU, GEREZA LA KARANGA MJINI MOSHI

0
0
NA K-VIS MEDIA, MOSHI
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, ametembelele kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Oktoba 9, 2016, ili kuona eneo ambalo kitajengwa kiwanda kipya na cha kisasa.
Bw. Erio ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Steven Alfred, na Meneja Uhusiano, Bi.Lulu Mengele, pia alipata fursa ya kupokea taarifa ya uendeshaji wa kiwanda cha sasa na changamoto zinazokikabili. Bw. Erio alisema, ziara yake inalenga kujua mambo mawili ambayo ni kuona eneo patakapojengwa kiwanda kipya cha kutengeneza bidhaa za ngozi, lakini pia kupata uelewa wa nini kifanyike ili kuboresha kiwanda cha sasa ambacho kilijengwa mwaka 1977.

Maafisa wa kiwanda hicho, walimuonyesha maeneo mawili ambayo yanafaa kujengwa kiwanda hicho. “Kama mtakumbuka, wiki iliyopita mimi na Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), John Minja tulisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya PPF na Jeshi la Magereza katika kukiboresha kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga, lakini pia kujenga kiwanda cha kisasa cha kuchakata ngozi na kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.” Alianza kwa kusema.
Alisema, nia ya Mfuko ni kuona kazi ya ujenzi wa kiwanda kipya inakamilika ifikapo Desemba 2018 ili kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda. “Wakati tukisubiri ujenzi wa kiwanda kipya ukamilike, lazima pia tuboreshe hiki cha sasa kwa kuimarisha miundombinu iliyopo, na hivyo kuongeza uzalishaji na kupanua masoko ” alisema Bw. Erio.

Aliagiza wataalamu wa PPF kwa kushirikiana na wenzao wa Magereza (kiwanda cha Karanga), wakutane haraka ili kuainisha chamngamoto zinazokikabili kiwanda cha sasa, ili uboreshaji wa mitambo uweze kufanyika kwa haraka.” Alifafanua. 



Mkuu wa gereza la Karanga, mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, ambako ndiko kilipo kiwanda cha kutengeneza viatu, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP), Hassan Bakari Mkwiche, (kushoto), akionyesha kitu, wakati Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (wakwanza kulia), alipotembelea kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa cha viatu, Oktoba 9, 2016. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (wapili kushoto), Mkuu wa magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP), Anderson Kamtera.
Bw. Erio, na maafisa wake, wakipatiwa maelezo na maafisa wa Jeshi la Magereza alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho

Kamishna wa Magereza, (CP), Editha Malya, aliyemuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, (CGP), akizungumza wakati wa kikao cha kupeana taarifa na ujumbe wa PPF ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Erio Oktoba 9, 2016


Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred, wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA KAMPENI YA FAHARI YA TANZANIA NA UTOAJI TUZO KWA CHAPA BORA 50 ZA KITANZANIA

0
0
Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akifanya uzindu rasmi wa Tuzo hizo.
Mgeni rasmi, Mama Samia Suluhu Hassan akifurahi jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na Viongozi wengine baada ya Uzinduzi wa Kampeni ya Fahari ya Tanzania uliofanyika katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na TPSF Mlimani city jijini Dar es Salaam Oktoba 7 2016.
Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akikabidhi cheti cha shukrani kwa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma Kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully-Esther Mwambapa ambao ndio wadhamini Wakuu wa hafla hiyo.
 Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakiwa katika picha ya pamoja na waadaji, wadhamini, na washindi wa tuzo hizo. Kushoto (kwake) Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda (wa pili kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa TSPF, Godfrey Simbeye (kushoto) na viongozi wengine.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma Kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully-Esther Mwambapa ambao ndio wadhamini Wakuu akitoa neno la shukrani na kuwakaribisha wageni kwa chakula.  
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



KAMPUNI YA CRCC KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU MKOANI DODOMA.

0
0
 Waziri mkuu  Kassim Majaliwa  akipokea picha yenye sura yake kutoka kwa mwenyekiti wa kampuni  ya Ujenzi ya CRCC ya China Bw. Fengchao kulia ni katibu wa chama cha ushirikano na maendeleo kati ya china na Tanzania Bwana Joseph Kahama  ujumbe huo kutoka china ulifika ofisini kwa waziri mkuu  Magogoni jijini dar es salaam kwa mazungumzo ya kikazi nakutoa pole kwa tetemeko la kagera.
 Waziri mkuu  Kassim Majaliwa akiwa katika picha.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya CRCC ya China Bw. Fengchao Meng ambaye ameahidi kuwekeza kwa kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti huo ambaye aliongozana na Mwenyekiti wa Kampuni nyingine ya Ujenzi ya CCECC ya China, Bw. Yuan Li pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha  Urafiki kati ya Serikali za Tanzania na China, Bw. Joseph Kahama .

Akizungumza na Bw. Meng leo (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni uendelezaji wa Makao Makuu Dodoma.

Aliongeza kuwa China na Tanzania ni marafiki wa muda mrefu na mataifa hayo yanashirikiana vizuri katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali hivyo Serikali inatarajia mengi kutoka kwenye kampuni hiyo kupitia kwa mwenyekiti wake Bw. Meng.

“Dodoma kuna fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda. Mnaweza kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za makazi, ofisi, huduma za kijamii na viwanda ,”

Kwa upande wake Bw. Meng amesema kampuni yake itaungana na Serikali katika kuboresha Makao  Makuu ya Serikali na inatarajia kutuma wataalam wake mkoani Dodoma kuangalia maeneo ya uwekezaji.

‘Nataraji tutakuwekeza katika ujenzi wa miundombinu, nyumba za makazi, ofisi, maeneo ya kutolea huduma za jamii na teknolojia zitakazowezesha upatikanaji wa maji safi na salama.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, OKTOBA 10, 2016.

UONGOZI WA HOSPITALI YA MUHIMBILI HAUJAMKATAZA MGONJWA KUTOKA HOSPITALI KWA KUKOSA FEDHA.

0
0


 KUHUSU MGONJWA WA SARATANI KULIPISHWA FEDHA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI.

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unapenda kuutarifu Umma kwamba haijamzuia Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri kutoka hospitalini kwa madai ya kushindwa kulipa pesa za matibabu kama ilivyoandikwa na Gazeti la Jambo Leo lenye namba ISSN 7826 No 2589, hivyo taarifa hizo si za kweli.

Katika ukurasa wa mbele, gazeti hilo limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kinachosema “Mgonjwa saratani azuiwa Muhimbili miezi miwili ni baada ya kushindwa kulipa deni la Sh. 330,000”.

Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri kwa mara ya kwanza alilazwa Muhimbili Agosti 29, 2016  akitokea mkoani Morogoro na kuruhusiwa Septemba 10, 2016  na  Septemba 23, 2016  alilazwa tena na kuruhusiwa Septemba 24, 2016.

Baada ya vipimo vya awali kufanyika Septemba 29, 2016 alilazwa tena na kufanyiwa  upasuaji Septemba 30, 2016 na kuruhusiwa Oktoba 04, 2016 baada ya taratibu za matibabu kukamilika.
 Mgonjwa  aliingizwa kwenye utaratibu wa msamaha na kuchangia Shilingi 70,000 tu, kati  ya Shilingi 400,142.33. Hivyo si kweli kwamba mgonjwa alilipa Shilinngi 380,000 kama ilivyoandikwa na gazeti hilo.

Kuhusu tiba ya mionzi, Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri amefanyiwa vipimo vingine hivyo atatakiwa kurejea baada ya wiki tatu kwa ajili ya majibu na si kweli kwamba Muhimbili imezuia uhamisho wake kwenda Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa ajili ya tiba hiyo.
Imetolewa na;
Uongozi wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili
Oktoba  10, 2016.

WANANCHI CHANDAMA WALILIA MAJI.

0
0
Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya, akiangalia kisima kilichochimbwa katika Kijiji cha Chandama chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), kikiwa kimepigwa kufuli. Katikati ni mkazi wa kijiji hicho, Igwana Maulid na Yusuph Kijuu. 

Na Mwandishi Wetu, Chemba.
WANANCHI wa Kijiji cha Chandama, Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, wameshindwa kufanya shughuli za maendeleo, kutokana na kukabiliwa na tatizo la maji kwa miaka mingi.

Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo walisema, wanashangaa kuona wanapata shida ya maji, wakati kuna visima viwili vilivyochimbwa kijijini hapo na vyenye maji mengi, lakini hawafaidiki navyo kutokana na ukosefu wa miundombinu. 

Kutokana na shida hiyo, wananchi hao wamemwomba Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, afike kijijini hapo ili aweze kutatua kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Iddy Ijui, alisema kijiji hicho kinakabiliwa na shida kubwa ya maji, ambapo hivi sasa wanalazimika kununua pipa moja la maji kwa Sh 5,000.

“Kitendo cha kukosa maji kinatufanya tushindwe kufanya shughuli za maendeleo, kwani tunapoteza muda mwingi kutafuta maji.

“Hapa kijijini kuna visima viwili na vyote vina maji mengi, lakini vimefunikwa na magunia na kingine kimepigwa kufuli tangu 2011, sasa hatuelewi lengo lao lilikuwa ni kutuachia mashimo au kutoondolea kero ya maji,” alihoji.

Naye Igwana Maulidi, alisema katika kujitafutia huduma hiyo wananchi wa kijiji hicho wamechimba visima virefu vya kienyeji vinavyotumia kamba, kiasi cha kuhatarisha usalama wao.

“Visima viwili vimechimbwa lakini havitumiki, hatuwezi kupata maji kwa sababu havijafungwa mashine. Kibaya zaidi hakuna kiongozi anayezungumzia hatima ya hivi visima na jitihada za kumaliza hii kero, ndiyo maana tunaomba waziri wa maji aje hapa kijijini,” alisema.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Mustafa Kidunka maarufu kwa jina la Munguji, alisema wananchi wa kijiji hicho ni kama yatima, kwani hakuna kiongozi anayehangaika kutatua kero zao.

“Watu wanashida ya maji hakuna anayejali, kilichimbwa kisima hapa na wajapani, kimepigwa kufuli hadi leo hakijafunguliwa. Mwaka jana tena halmashauri ilichimba kisima kingine na chenyewe kimefunikwa tu, kama ni hasara ya viongozi tumeipata,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Said Mwaliko (Chadema), maarufu kwa jina la Machapati, alikiri kuwapo kwa kero hiyo na kusema uongozi wa juu ndiyo kikwazo cha kumaliza kero hiyo.

“Shida ya maji ni kubwa, watu wanaugua matumbo, mimi nafuatilia ngazi ya juu nimekuwa nikimpigia simu mbunge, ananiambia linashughulikiwa lakini sioni chochote na mimi hapa kijijini nasumbuliwa sana kuhusu tatizo la maji.

“Tukikaa kwenye vikao vya WDC (kamati ya maendeleo ya kata) diwani anasema suala hili linashughulikiwa mara anasema hela zimetengwa lakini ni muda mrefu sasa hatuoni chochote na wananchi wanaendelea kupata shida,” alisema.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Chandama, Titus Sindamwaka (CCM), alipotafutwa kuzungumzia kero hiyo aliwataka wananchi hao kuwa na subira, kwani kuanzia mwezi ujao tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi.

“Tumechimba visima viwili kimoja kipo Chandama na kingine kipo Mapango, tunasubiri bajeti ya Novemba 4, mwaka huu Baraza la Madiwani litakapokutana tuone tunakiasi gani tuanze kufunga miundombinu,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu kisima kimoja kupigwa kufuli kwa muda mrefu, Sindamwaka alikiri kisima hicho kuchimbwa 2011 na kueleza kuwa hakiwezi kufunguliwa, kwani hakijakabidhiwa rasmi katika Serikali ya Kijiji.
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images