Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA BANYAK FILMS YA UINGEREZA KUPIGA TAFU RESI ZA NGALAWA ZA RAFIKI NETWORK!

$
0
0
Na A.O. Ali

Kampuni mashuhuri ya filamu ya Banyak kutoka nchini Uingereza, imetangaza nia na dhamira yake ya kufanya kazi pamoja na kampuni ya Rafiki Network  nchini Tanzania katika kufanikisha tukio lake la kwanza la resi ndefu za ngalawa litakalofanyika tarehe 18 Disemba, 2016, huko Vumawimbi kisiwani Pemba visiwani Zanzibar.

Akitoa taarifa huyo kwa mwandishi wa habari hii kupitia mazungumzo ya simu, Rais wa kampuni ya Rafiki Network Bwana Hamad Omar Hamad amethibitisha kuwa mazungumzo kati yao na kampuni ya Banyak yameshakamilika na kwa sasa kampuni hiyo inakamilisha utaratibu wa kujiandaa kwa ajili ya tukio hilo.
“ Napenda niwahakikishie kuwa baada ya kuliona wazo letu hili la kutaka kuanzisha resi  ndefu za ngalawa hapa Afrika Mashariki, wenzetu wa BANYAK wa kule Uingereza hawakufikiri mara mbili. Wamesema wako tayari kuja nchini kushirikiana nasi kikamilifu.”  Alisema Bwana Hamad.
Aidha Bwana Hamad amesema amefarijika sana kuwa licha ya kuwasiliana na wadau wengi wa biashara yakiwamo mashirika ya simu, ndege na usafiri wa baharini, imempa moyo sana kuona kwamba kampuni hii ya kigeni ndiyo imekuwa ya kwanza kuona fursa adhimu na kujitokeza kushiriki katika tukio hili adhimu na la kihistoria nchini.
“ Wenzetu wa Banyak hawakujali tukio hili linaandaliwa na nani, wapi na vipi. Baada ya kuona baadhi ya maandiko  na posta ya tangazo la tukio letu, imewatosha wao kuona kuwa kuna fursa kubwa katika tukio hili. Kwa kutambua umhimu wa tukio lenyewe wameamua kuchukua gharama na muda wao kuja kushiriki kikamilifu katika kufanikisha tukio letu hili. Kwa kweli ni habari njema sana kwetu!” Alisema Bwana Hamad.
Kampuni ya Banyak ni moja kati ya kampuni mashuhuri nchini Uingereza ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijishughulisha na kuandaa makala za video (documentary) zenye kuelimisha  jamii. Kampuni hiyo yenye makazi yake jijini London, itaingia makubaliano ya kurikodi tukio zima la resi za ngalawa zitakazofanika Pemba mwishoni mwa mwaka huu. Resi hizo ndefu zaidi kuwahi kutokea katika pwani ya Afrika Mashariki zitaanzia bandari ya Vuma wimbi na kuishia bandari ya Tumbe, takribani mwendo wa kilomita 30 za baharini.
Resi hizo zitashirikisha Ngalawa kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania sambamba na kuwashirikishi kikamilifu wamiliki wa ngalawa kutoka maeneo enyeji ya Tumbe, Shumba mjini, Kiuyu, Msuka, Tondooni na kwengineko ambapo ngalawa kati ya 30 hadi 50 zitashiriki.
Kampuni ya Rafiki Network imeanzishwa mwaka 2016 na kusajiliwa visiwani Zanzibar ambapo miongoni mwa kazi zake ni kuandaa matukio mbali mbai ya Elimu na Utamaduni kwa lengo la kuiwezesha jamii kimaisha kwa kufungua milango ya fursa za ajira sambamba na kukuza utalii wa ndani na wa nje hapa nchini.
Resi hizi za Ngalawa ndio tukio la mwanzo kubwa kuandliwa na Kampuni ya Rafiki Network ambapo wadau mbali mbali kama ZANTEL, TIGO, HALOTEL, ZSSF, Vigor Group of Companies, TASAKHTA Hospitals na Sun Tours zimeombwa kudhamini tukio hili. Kampuni nyengine ni Hotel ya Tembo, Serena na nyenginezo ambapo pia mashirika mbali mbali ya ndege pia yameombwa  kutoa udhamini.
“ Kwa hakika tuna tamaa kubwa ya kupata mashirikiano na wadhamini wetu. Hadi sasa TASAKHTA Hospital na Sun Tours wamejitokeza rasmi kudhamini sehemu ya tukio hili. Hata hivyo tunawakaribisha wadhamini wengine waweze kuiona fursa iliyopo mbele yao na wajitokeze kudhamini tukio hili lenye manufaa kwao na jamii kwa ujumla.” Bwana Hamad Omar alitoa wito sambamba na kuushukuru Uongozi wa Hospitali ya TASAKHTA na Kapmuni nguli ya utalii visiwani Zanzibar ya SUN Tours kwa kukubali kushiriki na kudhamini sehemu ya tukio hili.

Tukio hili sambamba na kudhaminiwa na mashirika mbali mbali linatarajiwa kuhudhuriwa na vyombo mbali mbali vya habari vya ndani na nje ya nchi ambapo idadi kubwa ya wageni na washabiki inatarajiwa pia kujitokeza kwa wingi kujionea tukio hili la kihistoria katika nchi yetu.

UFAFANUZI WA UVUMI KUWEPO KWA VOLKANO WILAYANI MISENYI MKOANI KAGERA

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Prof. Abdulkarim Mruma  (aliyeshika panga) akitoa ufafanuzi juu ya uvumi kuwepo volcano leo katika eneo la Katarabuga, kata ya Bwanjai wilaya ya Misenyi. Eneo la mbele waliposimama wananchi na viongozi  ndio limeungua moto na kusadikiwa kuwa ni volcano hatua ambayo imekanushwa na Mtendaji Mkuu wa Jioloji badala yake ulikuwa huo moto kawaida. Eneo la mbele waliposimama wananchi na viongozi lililoungua ndio lilisadikiwa kuwa ni volcano hatua ambayo imekanushwa na Mtendaji Mkuu wa Jioloji badala yake ulikua ni moto wa kawaida.
 Wananchi wakiwa katika eneo la Katarabuga, kata ya Bwanjai wilaya ya Misenyi ilipodaiwa kuwepo kwa volcano hatua ambayo imekanushwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Prof. Abdulkarim Mruma badala yake amesema huo ulikuwa ni moto wa kawaida. Eneo la mbele waliposimama wananchi na viongozi lililoungua ndio lilisadikiwa kuwa ni volcano hatua ambayo imekanushwa na Mtendaji Mkuu wa Jioloji badala yake ulikuwa ni moto wa kawaida.
 Baadhi ya viongozi wakiwasili eneo katika eneo la Katarabuga, kata ya Bwanjai wilaya ya Misenyi ilipodaiwa kuwepo kwa volcano hatua ambayo imekanushwa na Mtendaji Mkuu wa Jiolojia badala yake huo ulikuwa ni moto wa kawaida. Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba

Ziara ya Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini Mhe. Christopher Kourakis nchini

$
0
0
 Jaji Mkuu wa Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akizungumza jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika ofisi ya  Jaji Mkuu wa Tanzania iliyopo kwenye jengo la Mahakama ya Rufani Tanzania, jijini Dar es Salaam. Mhe. Jaji Kourakis yupo nchini kwa ziara ya siku tatu yenye lengo la kujenga ushirikiano katika utendaji kazi wa Mahakama baina  ya nchi hizo mbili. 
Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (kushoto)    akisoma kitabu kinachohusu Chama cha Majaji Wanawake   Tanzania wakati alipotembelea ofisini kwa Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman.

Article 18

TAARIFA KWA WANAJUMUIYA NA MARAFIKI JUU YA MISAADA ITOAYO TCO

$
0
0
 
TANZANIA COMMUNITY ORGANIZATION  
OF NORTHEN CALIFORNIA (TCO)  
912 Bayview Ave, Oakland, CA 94610  
510.290.9708, 510.472.7672 

Ndugu Watanzania na marafiki wa Northern California. 
Mwaka huu tutakuwa na fundraising nyingine ambayo itaambatana na kusheherekea kumbukumbu ya sherehe zetu za uhuru hapo Dec 10 2016.  Fundraising ya mwaka huu itakuwa ni kusaidia  vifaa/kifaa kwa zahanati (clinic) mojawapo kutoka kijiji kimojawapo Tanzania. 
Lakini kabla ya yote ni vizuri tuwape taarifa kwa ufupi juu ya juhudi zenu mlizofanya mwaka jana za kuwezesha kuchangia msaada wa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (albino)

Shughuli ilifanyika Dec 19 2015 katika mji wa Oakland - CaliforniaKatika mapato yaliyopatiakana basi Umoja wetu (TCO) uliweza kusaidia shule ya msingi ya Buhangija ambayo ni shule ya albinos  inayosaidia kuwasomomesha watoto hawa katika mazingira ya amani baada ya matukio ya kukatwa viungo kuwa mengi miaka michache iliyopita. 
TCO (Tanzania Community Organization) kupitia michango yenu iliweza kusaidia kiasi cha milioni 6, tisini na saba elfu (tsh 6,097,000)
Kiasi hiki kilitumwa kupitia kwenye serikali ya wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa shule ili kuhakikisha msaada uliwafikia walengwa.Matumizi yake yalikuwa kama ifuatavyoWanafunzi waliweza kusaidiwa : 
1.Mashuka 200 kwa gharama ya tsh milioni mbili (2,000,000 tsh) 
2. Kofia kubwa (kwa ajili ya jua) na tshirts 200 kwa gharama ya milioni moja na laki sita (1,600,000 tsh) 
3. Vyandarua 100 kwa gharama ya laki nane (800,000 tsh) 
4.Sweta 200 kwa gharama ya milioni moja laki sita na tisini na saba (1,697,000 tsh) 
Tunaomba wadau wote na watanzania kwa ujumla kwenye jumuiya yetu tuendelee kuwa mstari wa mbele katika kusaidia misaada mbalimbali katika jamii mbalimbali zenye mahitaji huko Tanzania. 
TCO itaendelea kuwa mstari wa mbele kila mwaka kuendeleza zoezi hiliKwa pamoja tutainuana. 
Karibu na changia kwa bidii tarehe 10 Dec 2016 Oakland- California kwenye hii. 
Tembelea website yetu 
Erick Byorwango 
(Mwenyekiti- Uhusiano na Uenezi TCO)





MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA TANZANIA KIPINDI CHA OKTOBA HADI DESEMBA 2016

TAARIFA KUHUSU ZOEZI LA KUCHANGIA DAMU SIKU YA ASHURA 09/10/2016

TFF latoa tahadhari kwa timu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kutoa tahadhari kwa timu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) juu ya kuwatumia wachezaji ambao imewasajili, lakini imebainika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwamba wana matatizo kwenye usajili wao. 

Majimaji ya Songea

Mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole ambaye pia amebainika kuwa ndiye Gerald Mpole wa Majimaji ya Songea amefungiwa kucheza soka kwa mwaka kwa kosa la kubadili jina akiwa na lengo la kufanya udanganyifu kwenye usajili. Majimaji imeagizwa kutomtumia mchezaji huyo kutoka Kimondo FC.

Mwadui FC ya Shinyanga

Mchezaji William Lucian aliyesajiliwa na Mwadui ya Shinyanga kutoka Ndanda ya Mtwara, naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kusajili Mwadui FC ilihali akiwa hajamaliza mkataba na Ndanda. Mwadui isimtumie mchezaji huyo.

Mbeya City ya Mbeya

Mchezaji Saidi Mkopi, pia amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kujisali timu mbili. Imebainika kuwa akiwa bado na mkataba na Tanzania Prisons ya Mbeya hivyo Mbeya City isi1mtumie mchezaji huyo.

African Lyon ya Dar es Salaam

Mchezaji Rehani Kibingu aliyesajiliwa na African Lyon ya Dar es Salaam, amesimamishwa kuchezea timu hiyo mpaka uongozi wa African Lyon kumalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam kabla ya Agosti 27, 2016. African Lyon isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.

Mbao FC ya Mwanza 

Mchezaji Emmanuel Kichiba aliyesajiliwa Mbao FC, naye amesimamishwa mpaka Mbao watakapomalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam, kabla ya Agosti 27, 2016. Mbao FC isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.




WLAC WAZINDUA AWAMU YA TATU YA KAMPENI YA ‘TUNAWEZA’ JIJINI DAR

$
0
0
Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue (kulia) na Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (katikati), na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally (wa pili kushoto) wakiinua Vipeperushi baada ya mgeni rasmi kuzindua Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (wa tatu kulia), na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally (wa pili kushoto) Mkaguzi wa Polisi Prisca Komba wa Dawati la Jinsia Polisi Kinondoni (kushoto) na Jackline Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia Oxfam, kwa pamoja wakiinua vipeperushi baada ya mgeni rasmi kuzindua Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ iliyofanyika kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, leo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mwacity Almas, akiimba na kucheza pamoja na baadhi ya kinamama waliohudhuria uzinduzi wa Awamu ya tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ ya Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), iliyozinduliwa leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Picha na Mafoto Blog 

Serikali yalaani mauaji ya Watafiti mkoani Dodoma, kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa mahakamani

$
0
0
SERIKALI imesema itahakikisha kuwa wahusika wa mauaji ya Watafiti mkoani Dodoma wanakamatwa na kufikishwa mahakamani ili waweze kujibu mashtaka yanayowakabili.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri ya Mambo ya  Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa mkutano na  waandishi wa habari juu ya mauaji ya Wataalamu hao yaliyotokea wilayani Chamwino.

Amesema kuwa Serikali imesikitishwa na hatua iliyochukuliwa na  baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino kuwaua watafiti hao ambao walikuwa kazini.

Kufuatia hali hiyo amewaagiza Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kushirikiana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika kufanya upelelezi wa mauaji ya wataalamu hao  ili wahusika waweze kufikishwa vyombo vya usalama haraka na haki iweze kutendeka.

Amesema kuwa ushirikiano huo utasaidia kuimarisha upepelezi  ambao utawezesha uandaaji wa mashtaka ili wahusika wote waweze kufikishwa Mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabili.

“Wizara inawataka Mkurugenzi wa Mashtaka DPP ajihusishe kikamilifu na upelelezi wa kesi  hii ya mauaji ya watafiti kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai DCI kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ya Uendeshaji  wa Mashtaka” alifafanua Dkt. Mwakyembe.

Ameongeza kuwa ili kukomesha wimbi la wananchi kuchukua sheria mkononi, Wizara itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika kwa namna moja ama nyingine kwa kushawishi, kuhamasisha au kuchochea, kupanga, kushambulia kwa mapanga na kushiriki kuchoma moto gari wanafikishwa mahakamani ili Sheria ichukue mkondo wake.

Katika hatua nyingine, Waziri Mwakyembe amewataka baadhi ya waandishi wa habari kubadilisha mfumo wa kutoa taarifa za matukio zinazochochea uvunjifu wa amani kama vile kuandika kuwa “wananchi wenye hasira kali” maneno ya aina hii hushawishi wengine kufanya hivyo kwa kisingizio cha hasira.

Mbali na hayo Waziri huyo amevitaka vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria kwa wote waliohusika na vitendo vya kuchukua sheria mkononi ikiwemo kuwafikisha mahakamani. 

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Harrison Mwakyembe akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mauaji ya wataalamu wa utafiti yaliyotokea hivi karibuni mjini Dodoma, kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Bw. Amon Mpanju. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 06.10.2016

WAKUU WA WILAYA ZA DAR NA PWANI WATEMBELEA MIRADI YA DAWASCO

$
0
0
KATIKA ziara iliyoandaliwa na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) kwenye mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu juu na Ruvu chini pamoja na katika miradi inayoendelea kwa wakuu wa wilaya zote za jijini la Dar es salaam pamoja na Pwani yenye lengo lakuonyesha hatua zinazofanywa kuboresha huduma ya Majisafi.

Akizungumza kwenye ziara hiyo Afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza lengo la kuwaleta wakuu hao wa wilaya kwenye miradi inayoendelea kuwa ni kuonyesha hatua ambazo shirika linafanya la kuongeza upatikanaji wa majisafi jijini Dar es Salaam.

‘’lengo la ziara hii ya leo nikutembelea miundombiu ya dawasco ili kuweza kuboresha huduma ya maji safi katika jiji la Dar es salaam na kuwaondolea kero wananchi juu ya uhaba wa huduma hii ya maji ili kuweza kuboresha hali zao, sisi kama dawasco tuna kauli mbiu ya mama tua ndoo kichwani ambapo kauli mbiu hii inalenga kumtua ndoo mama kichwani’’alisema Afisa Mtendaji wa Dawaasco Cyprian Luhemeja.
 
Luhemeja aliwataka wananchi kutunza miundombinu ya shirika hilo ili kuwawezesha wakinamama ambao wanamchango kubwa katika kuihuhudumia jamii kuweza kuwatua ndoo kichwani kuendelea na shughuli nyinginezo za kuihudumia jamii.
Meneja wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa akitoa maelezo mafupi kwa wakuu wa Wilaya za Dar es salaam na Pwani leo katika ziara iliyoandaliwa na Shirika la Majisafi na Majitaka (Dawasco).
Wakuu wa Wilaya wakiwasili kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu juu Mlandizi, Mkoani Pwani.
Afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya za Dar es salaam na Pwani, wakati wa ziara iliyoandaliwa na Shirika la Dawasco. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

RC Mahenge azindua ujenzi ya vyoo kwenye shule za Msingi na Sekondari Wilayani Tunduru

$
0
0
Wilaya ya Tunduru imezindua kampeni ya uchomaji tofali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye shule za msingi na sekondari.

Uzinduzi huo umefanywa jana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge alipofanya ziara ya kikazi kijiji cha Ligoma Tarafa ya Namasakata. Katika kuunga mkono juhudi za wananchi mkuu wa Mkoa ameshiriki kazi ya kupanga tanuri la matofali yaliyofyatuliwa na wananchi ili kuwezesha kijiji kujenga matundu ya vyoo kwenye shule ya msingi Ligoma

Katika uzinduzi huu jumla ya matofali 200,000 yamefyatuliwa na wanakijiji cha Ligoma mwezi uliopita ambapo kazi ya uchomaji itatumia Siku kumi na ñne hadi kukamilika. Akitoa taarifa ya utekelezaji a kampeni ya benki tofali kwenye wilaya ya Tunduru mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera alisema jumla ya tofali 7,070,000 zimefyatuliwa kwenye Tarafa zote saba za Tunduru
Aliongeza kusema wilaya yake imejipanga kukamilisha zoezi la matofali na kuahidi kuwa ifikiapo mwezi Desemba mwaka huu watakamilisha ujenzi wa vyoo kwani halmashauri kupitia makusanyo ya ndani watatoa vifaa vya kiwandani

Wakati huo huo mkuu wa Mkoa alikagua hali ya matundu ya vyoo kwenye hule ya msingi Ligoma na kujionea upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo vya wanafunzi. Shule ya msingi Ligoma yenye wanafunzi 656 na na walimu 8 ina matundu ya vyoo sita na upungufu uliopo ni matundu ya vyoo 24 wakati mahitaji kwa wasichana ni 18 na wavulana ni 12. Dkt. Mahenge amewapongeza wilaya ya Tunduru kwa jitihada walizofikia kupata matofali na kuwataka waanze kuchimba matundu ya vyoo

“Nawataka sasa muanze hatua ya pili kwa kuchimba mashimo ya vyoo ili halmashauri ya wilaya ilete saruji,nondo,mabati,na masinki na kuweka mfumo wa maji” alisisita mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Mkoa amewataka na kuwasisitiza wakuu wa wilaya zote kutembelea na kukagua hali ya miundombinu ya vyoo,madarasa na nyumba za walimu ili matofali yanayofyatuliwa sasa na wananchi yatumike kukamilisha ujenzi ya mundombinu hii muhimu. Aidha amewaagiza maafisa Elimu wote wa wilaya kutokaa ofisini na kutayarisha takwimu na zisizo na uhalisia.

Dkt.Mahenge alizindua kampeni ya ufyatuaji tofali kwenye Mkoa wa Ruvuma mwezi Agosti mwaka huu na kuelekeza kijiji vyote kuwa na benki tofali 100,000 zitatumika kujenga matundu ya vyoo kwenye shule,zahanati kwenye kijiji visivyo na zahanati.

Alisema ni lengo la Mkoa kuona unanza mwaka 2017 ukiwa umekamilisha ujenzi na matundu ya vyoo kwenye shule za msingi na sekondari ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kwenye mazingira ya usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge (aliekuwa chini) akiwa na mbunge wa Tunduru Kusini Idd Mpakate (wa pili kushoto) wakishiriki kazi ya kupanga tanuru la tofali pamoja na wananchi wa kijiji cha Ligoma wilaya ya Tunduru Jana.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge akikagua kazi ya kupanga tanuru la tofali aliposhiriki uzinduzi wa uchomaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule ya msingi Ligoma wilaya ya Tunduru Jana.

CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA KUTOA MAFUNZO MAALUM.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA CDA, ABAINI MADUDU UUZAJI VIWANJA DODOMA

$
0
0
*Kiwanja chauzwa kwa sh. milioni 240 lakini zilizoingia CDA ni milioni 6 tu
*Ahimiza kasi ya upimaji viwanja, asema waliolipa nusu wasinyang’anywe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Bw. Uledi Mussa afuatilie malipo ya kiwanja kilichouzwa na CDA kwa sh. milioni 240 lakini fedha iliyoingia ofisini ni sh. milioni 6 tu. 
“Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ninataka ufuatilie mauzo ya kiwanja namba 26 block AA eneo la Kikuyu East ambacho kimeuzwa kwa sh. milioni 240 lakini fedha iliyoingia CDA ni sh. milioni 6 tu. Nataka kujua nani ameingiza milioni 6 na nani kachukua hizo sh. milioni 234,” amesema. 
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Oktoba 6, 2016) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) kwenye ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma. 
Bila kutoa ufafanuzi zaidi, Waziri Mkuu amesema eneo hilo lilipaswa kuwa na kituo cha mafuta na akataka apatiwe taarifa mapema iwezekanavyo. 
Pia amemwagiza Katibu Mkuu huyo afuatilie mkataba wa upangishaji wa jengo la CDA ambalo wamepangishwa taasisi ya Tunakopesha Limited kwa madai kuwa mhusika alipewa bure na sasa anataka kulipangisha tena ili apate cha juu. 
Waziri Mkuu amewaonya watumishi hao pamoja na viongozi wao waache tabia ya kushirikiana na madalali kuuza viwanja na akawataka wachape kazi wakijielekeza na kasi ya Serikali ya kuhamia Dodoma. 
“Tabia ya watumishi kushirikiana na madalali kuuza ardhi sasa basi. Hata hivyo, nimefarijika kukuta mmeanza kuweka mfumo wa kielektoniki katika baadhi ya huduma. Ni lazima mauzo ya viwanja sasa hivi yafanyike kwa njia ya kieletroniki, madalali hawana nafasi,” amesisitiza. 
Ameutaka uongozi wa CDA uongeze kasi ya upimaji viwanja kwa sababu mahitaji ni makubwa lakini akaonya kuwa wakati zoezi hilo likifanyika, wananchi walionunua viwanja na bado hawajamalizia kuvilipia, wasinyang’anywe kwa kigezo cha kutaka kuwauzia wengine.
 “Mimi nataka idadi ya viwanja vilivyopimwa iongezeke. Lakini pia msitumie fursa hii kuwanyang’anya watu wenye umiliki halali eti kwa sababu Serikali inataka idadi ya viwanja vilivyopimwa iongezeke,” amesema. 
“Kama mtu amepewa offer au hati yake asinyang’anywe hata kama amelipia nusu asinyang’anywe. Ahimizwe kumalizia hilo deni na ninyi kazi yenu ni kupima viwanja vingine,” amesisitiza. 
“Natambua mnayo benki ya viwanja, lakini inabidi muongeze idadi ya viwanja vingi zaidi. Tumeita wawekezaji waje kujenga nyumba za kuishi watumishi, mahoteli na viwanda na maeneo yote haya inabidi yatengwe rasmi,” amesema.

Amesema jumla ya viwanja 70,000 vimepimwa tangu CDA ianzishwe mwaka 1973. Amesema kama wataendelea na kasi hiyo wakati mahitaji yameongezeka, itawachukua zaidi ya miaka 40 kukamilisha mahitaji ya viwanja 100,000 ambavyo vinatarajiwa kuanza kupimwa hivi karibuni. 
Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Eng. Paskasi Muragili amesema usanifu wa upimaji viwanja 20,000 umekamilika na kwamba wana lengo la kupima viwanja vingine 100,000 ifikapo Juni 2017. 
Waziri Mkuu alitembelea Ofisi ya CDA na kukagua mfumo wa utunzaji mafaili wa zamani pamoja na uhamishaji wa taarifa za wenye viwanja kwenye mfumo wa kompyuta. Pia alikagua mifumo ya uuzaji viwanja kwa njia ya mtandao ambayo hata hivyo bado haijakamilika. 
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepokea mchango wa zaidi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Wilaya wa Kongwa, Bw. Deogratius Ndejembi zikiwa ni kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa Kagera walioathirika kwa tetemeko la ardhi lilitokea Septemba 10, mwaka huu. 
Pia Waziri Mkuu amepokea mchango mwingine wa zaidi ya sh. milioni tano kutoka kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiasha wa Manispaa ya Dodoma wakiwemo wamiliki wa hoteli, nyumba za kulala wageni, waendesha bodaboda na madereva wa daladala. 
Akipokea msaada huo, Waziri Mkuu amewashukuru wafanyabiashara hao na kuwahakikishia kwamba fedha hizo zitapelekwa mkoani Kagera na kuwafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, OKTOBA 6, 2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Mamalaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
 Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu CDA wakimsikilizwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati  alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu CDA wakimsikilizwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati  alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

RC WA MBEYA AMOS MAKALLA ATOA TAARIFA YA AWALI KUFUATIA TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI WA MBEYA DAY

$
0
0


"Tukio lilianza tarehe Jumatatu 26/9/2016, ambapo Mwalimu Frank Msigwa, mwanafunzi kwa vitendo kutoka Chuo Kikuu cha  Dar Es  salaam ambapo alitoa assignment ya somo la Kiingereza kwa wanafunzi wa kidatu cha tatu.

"Baada ya kusahihisha, aligundua kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawakufanya. Hivyo, tarehe Jumatano 28/9/2016, alikwenda darasani na kutoa adhabu wale ambao hawajafanya kazi yake. Alianza kwa kuwapa adhabu ya push-up, kisha kupiga magoti na baadae aliwachapa viboko viwili viwli kila mmoja. Katika utekelezaji wa adhabu ile, mwanafunzi  Sebastian Chingulu alikataa kufanya  kutokana na kuumwa na goti.

"Baada ya kuigomea adhabu ile, Mwalimu Frank Msigwa na wenzake wawili, John Deo na Sanke Gwamaka, walimpeleka ofisini na kuanza kumshambulia kwa kipigo kama inavyoonekana kwenye video. Baada ya tukio hilo walimu hao walitoweka shuleni hapo.Wakati wanamshambulia mwanafunzi huyo, kulikuwepo na Mwalimu mwingine aliyewasihi wasiendelee kumpiga kijana huyo na ndiye aliyerekodi tukio hilo.

"Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu kadhaa pamoja na Mwalimu Mkuu kwa mahojiano pamoja na kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu hiyo. Kuhusu mwanafunzi aliyepigwa, nawahakikishia kuwa serikali itawasaka popote walipo walimu  waliofanya tukio hilo na kufikisha katika vyombo vya dola ili wapate haki yao kisheria.
"Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa na matibatibu.

"Hii ni taarifa ya awali, nitaendelea kutoa 

taarifa kwa kila hatua tunayoifikia..." 

Ni Mimi,Amos G Makalla
Mkuu wa Mkoa wa  Mbeya

OPENING OF PIZZA HUT AT SHOPPERS PLAZA IN DAR ES SALAAM

LIVE CONCERT in Dar es Salaam Friday 7th October

$
0
0
THE BEAT FESTIVAL
FRIDAY 7. October - 21.00 - 02.00 
Venue: Paparazzi Club, Slipway - Msasani Bay, Dar es Salaam
Entrance: 10.000 TSH only
join fb event; goo.gl/B6KrHJ
  ABOUT THE BEAT: The Beat is a monthly festival showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is powered by: Caravan Records, Paparazzi Bistro Club, Jameson, and Goethe Institut Tanzania. Info: CRTanzania@gmail.com web:www.facebook.com/TheBeatFestival
INSTAGRAM SHARING:
TEXT3 Live acts Friday 7th October. Great lineup for the#TheBeatFestival featuring Lumumba Theathre Band (afrofusion), Jinong´ite Band (trad / afrofusion) and Mzungu Kichaa (live Bongo Flava). Entrance; 10k only. Doors Open 21.00hrs. 

@paparazzi_bistro_club@thebeatfestival,@CRTanzania@GoetheTanzania,@MzunguKichaa



​After a studio session in 2012, James Mlanda decided to form a band, which would focus on the fusion between traditional and contemporary music. This became Jinong´ite, which means something that is fun and sweet at the same time. The group have showcased in Uganda at DOADOA together with Dbass Qanun. The group specializes in high-energy percussion based compositions that are guaranteed to make you move.


​The band, also known as Lumumba Theatre is made up of talented singers, dancers, actors, choreographers and musicians, based in Dar es Salaam. Established in 1997 by Director Dyuto Komba the group is made up of students from Lumumba Primary School, located in the heart of Dar es Salaam. To date the group has performed all over Tanzania and at festivals in Kenya, Uganda, Mozambique, and Europe.

​Mzungu Kichaa and his band Bongo Beat have created a unique style of live Bongo Flava, which has taken them around the world. Tonight Mzungu Kichaa will perform a selection of old and new songs together with his backing band Bongo Beat. The performance will also mark the launch of a new single by the artist.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0


SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli, ameliagiza shirika la umeme Tanesco kuhakikisha viwanda vyote vikubwa nchini vinapatiwa umeme wa uhakika; https://youtu.be/jayEKBxkcnM

SIMU.TV: Waziri wa Tamisemi George Simbachawene, ameagiza mamlaka husika kumvua madaraka mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya kutwa Mbeya;https://youtu.be/GnLYc7laaAo

SIMU.TV: Benki ya dunia inakusudia kuipatia Tanzania ruzuku na mkopo wenye masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni moja; https://youtu.be/n8pkdinO2x8

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa, ameagiza kufanyika kwa uchunguzi juu ya uuzwaji wa kiwanja cha CDA kilichouzwa zaidi shilingi milioni 200 huku CDA ikiambulia milioni 6 tu;https://youtu.be/Bpw_0p9y2gw
SIMU.TV: Kuelekea kilele cha maadhinmisho ya kifo cha Mwalimu Nyerere, tunaendelea kukuletea mfululizo wa baadhi ya hotuba zake muhimu kabisa kwa taifa letu;https://youtu.be/I0v8MefwvYU

SIMU.TV: Rais wa Zanzibar Dr Alli Mohamed Shein, ameutaka mfuko wa hifadhi za jamii visiwani humo ZSSF kubuni miradi ya kisasa ili kujiendesha kibiashara;https://youtu.be/PcP8G6wZ_tM

SIMU.TV: Wadau mbalimbali wa uchumi nchini wameiomba serikali kupunguza mlolongo mrefu wa upatikanaji wa vibali kwa ajili ya kujenga viwanda; https://youtu.be/v2xUy7WZLbI

SIMU.TV: Benki ya TIB imetumia wiki ya huduma kwa wateja kuongea na wateja wao ili kuweza kupata mrejesho wa huduma wanazotoa kwa wateja wake; https://youtu.be/gh15-ngVSAQ

SIMU.TV: Timu ya Simba imeliomba shirikisho la mpira TFF kuleta waamuzi kutoka nje ya nchi ili kuondoa uwezekano wa kutoa kwa vurugu; https://youtu.be/hCAsFQoMLcg

SIMU.TV: Kampuni inayosimamia tiketi za kielekitroni ya Selcom, imesema imefanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa Yanga na Simba;https://youtu.be/WxtdfBCWUCs

SIMU.TV: Wasanii wanaoshiriki shindano la kutafuta vipaji linaloratibiwa na TBC la Klabu Raha Leo show, wamepiga kambi katika shule ya Filbert Bayi Kibaha;https://youtu.be/YY30_yY0ixI  

TAMASHA LA VYAKULA NA VINYWAJI KUFANYIKA LEADERS CLUB OKTOBA 8 JIJINI DAR

$
0
0

KAMPUNI ya EM & U Investiment imeandaa tamasha la Chakula na Vinywaji litakalofanyika (Dar es Salaam Food & Drink Festival) Jumamosi Oktoba 8, 2016  katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Edward James amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake kwa kushirikisha wapikaji  wa vyakula vya asili ikiwa ni kufanya Watanzania kuvipenda vyakula hivyo.
James amesema kuwa watu wengi wanapenda kula vyakula vya asili lakini hawajui watavipata wapi hivyo tamasha hilo litafungua ukurasa mpya juu ya watu kuweza kupata chakula hicho na sehemu gani.
Amesema katika tamasha hilo kutakuwa na wapishi katika kila kabila kupata chakula chake cha asili katika mikoa yao hiyo itakuwa ni sehemu kuwajengea utamdauni wa kupenda chakula cha asili.
James amesema katika tamasha hilo wananchi pia watapata huduma ya kupima afyazao na magonjwa yote bure katika Tamasha hilo wasanii mbalimbali watatumbuza.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ya EM & U Investiment, Bw. Edward James akizungumza na waandishi wahabari juu ya tamasha la vinywaji na vyakula  litakalofanyika viwanja Leaders Club jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mratibu wa Tamasha hilo, Zahara Michuzi  na kulia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji, Rashid Chenja.
 Mratibu wa Tamasha hilo Bi. Zahara Michuzi  akielezea juu maandalizi ya  tamasha la vinywaji na vyakula  litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images