Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

TTB YAMTAKA UNDERSON KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI MAREKANI

0
0
Na: Geofrey Tengeneza 


Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imemtaka kijana wa kitanzania ambaye pia ni mchezaji wa mpira wa kikapu Underson Simon (19) kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii nchini Marekani kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi kuitembelea Tanzania.

Underson ambaye ni tunda la kituo cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park cha jijini Dar es salaam amepata udhamini wa masomo kwenda kusoma shahada ya kwanza ya sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Georgia University kilichoko Atlanta Georgia nchini Marekani. 

Akizungumza wakati wa kumuaga Underson ofisini kwake jijini Dar esalaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi mchezaji huyo anayechipukia wa mpira wa kikapu nchini anayechezea timu mpira wa kikapu ya vijana (vijana Busketball Club) pamoja na kumtaka ajitahidi katika masomo yake, lakini pia amemtaka atumie fursa hiyo na ile ya kushiriki katika mashindano mbalimbali akiwa na timu yake ya chuo kikuu cha Georgia katika mchezo wa kikapu kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii.

“ Peperusha vema bendera ya nchi yetu na tumia kila jukwaa utakalopata ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii duniani” alisema Bi Mdachi na kuongeza kuwa TTB inakusudia kuanza mchakato wa kumpa heshima ya kuwa Balozi wa heshima wa Utalii wa Tanzania.

Mkurugenzi huyo wa TTB alimkabidhi mchezaji huyo wa mpira wa kikapu nchini, bendera ya Taifa na vielelezo kadhaa vinavyoelezea utalii wa Tanzania ili visaidie kumjengea uelewa zaidi kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania.

Kwa upande wake kijana huyo Underson Simon alielezea kufurahishwa kwake kupata nafasi hiyo lakini pia kutambuliwa na TTB kama mmoja wa wanamichezo wa kitanzania wanaoweza kuvitangaza vema vivutio vyetu vya utalii nje ya nchi na hivyo kuchangia kukuza sekta ya utalii. 

Naye mwalimu mwandamizi (kocha) wa mpira wa kikapu wa kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Bw. Bahati Mgunda amesema kituo chake kinajivunia mafanikio hayo ya mmoja wa wachezaji wao kupata ufadhili huo wa masomo ambao umetokana hasa na umahiri wake katika mchezo huo. 

Simon ameondoka saa 9.00 alfajiri ya leo kwa shirika la ndege la Uturuki kuelekea nchini Marekani tayari kujiunga na chuo kikuu hicho cha Georgia.

 Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi akimkabidhi Underson Simon bendera ya Taifa ishara ya kumtaka akaitangaze vema Tanzania nchini Marekani.

Underson Simon (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa TTB Bi devota Mdachi (wa pili kushoto) na baadhi ya maafisa aliofuatana nao katika ofisi za TTB muda mfupi baada ya kukabidhiwa bendera ya Tanzania na vielelezo mbalimbali vya utalii.

Taasisi za umma zatakiwa kuhuisha taarifa katika Tovuti zao

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu taasisi za Serikali kutekeleza agizo la kuhuisha taarifa na huduma katika Tovuti zao mapema kabla ya mwisho wa mwezi huu katika mkutano uliofanyika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (EGA) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto.

Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi hao leo jijini Dar es Salaam, kuhusu taasisi za umma kuhuisha taarifa katika Tovuti zao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akiwaonyesha waandishi wa habari mwongozo wa utengenezaji wa Tovuti za Serikali wakati wa mkutano wake na waandishi hao leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto. 

MKURUGENZI MTENDAJI WA CRDB ATEMBELEA TAWI LA MLIMANI CITY, ALA KEKI NA WATEJA WA TAWI HILO.

0
0
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akisalimiana na wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akishuhudia Mteja wa Muda Mrefu wa Tawi la Mlimani City, Mary Nderumaki akikata keki katika wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay  akimlisha keki Mteja wa mda mrefu, Mary Ndarumaki jijini Dar es Salaam leo.
 Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City  wakiwa katika picha ya pamoja  na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay jijini Dar es Salaam leo.

TIC YAPATA UGENI KUTOKA CHINA.

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.
MAKAMPUNI makubwa ya jimbo la Henan nchini China wametembelea Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (TIC), Clifford Tandari, amesema kuwa watu wenye makampuni  kutoka jumbi hilo wamekuja kuangalia uwekezaji katika maeneo viwanda, madini, pamoja tehama.

Amesema kuwa baada ya kutoka TIC watakwenda sehemu nyingine za serikali kuweza kupata maelezo zaidi ya juu ya uwekezaji.

Tandari amesema wamejipanga kufanya uwekezaji  nchini na kuweza kufikia uchumi wa viwanda. Aidha amesema kuwa katika kufanya uwekezaji TIC ndio imepewa dhamana hiyo .
 Picha ya pamoja ya kaimu Mkurugenzi Mtendaji akiwa watu wenye makampuni katika jimbo la henani leo jijni Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa bodi, Katibu wa Henan Investment Group co.Ltd. Lianchang Zhu akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara yao ya kuja kuangalia mazingira ya uwekezaji nchini.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Clifford Tandari (Kulia)akizungumza na waandishi wa habari juu makapuni ya jimbo la Henan walivyodhamiria kuwekeza nchini leo jijini Dar es salaam.

JIFUNZE SHERIA 17 ZA SOKA.

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Sheria namba moja ni Field of Play (Uwanja) na imegawanyika katika vipengele 13

1: Field surface.
*Katika sheria za shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA wameanisha aina ya uwanja unaotakiwa kuwa tukianzia na nyasi. Katika kupitisha kwao wamepitisha aina mbili za nyasi ambazo ni nyasi za kupanda (original) na nyasi bandia (artificial).

*Katika mechi zote za kimataifa kwa upande wa klabu au nchi viwanja vinavyotumika vinatakiwa vikidhi viwango vya FIFA.

*Nyasi hizo (nyasi za kupanda na nyasi bandia) lazima ziwe za kijani

2:Field Marking

*Umbo la uwanja linatakiwa liwe mstatili likiwa na mistari iliyochorwa kuonyesha mipaka ya uwanja huo.

*Mistari mirefu inajulikana kama Touchliness na mistari mifupi inajulikana na Goal line.

*Uwanja umegawanywa kwa mstari wa touchline unaopatikana katikati ya uwanja na duara likiwa na Radius (kipenyo) 9.15 sawa na yadi 10.

*Mistari yote inatakiwa kuwa na upana usiozidi 12cm na itafanana katika maeneo yote na hakutatakiwa kuwa na mabadiliko au michoro tofauti.



3:Dimensions(vipimo)
*Urefu (touchliness)
90m sawa na 100yad (minimum)
120m sawa na 130yad(maximum)

*Urefu(goal lines)
45m sawa na 50yad(minimum)
90m sawa na 100yad( maximum)

4: Dimension for international matches
*Urefu (touchlines)
100m sawa na 100yad (minimum)

110m sawa na 120yad (maximum)

*Urefu (goal lines)
64m sawa na 70yad (Minimum)
75m sawa na 80yad (Maximum)

NECTA WAANZISHA MFUMO MPYA WA NAMBA KWA SHULE ZA MSINGI

0
0
Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

Baraza la mitahani nchini limeanzisha mfumo mpya wa Kutunza Kumbukumbu za Wanafunzi wa shule za Msingi (PREM), Utakaosadia uandikishwaji wa wanafunzi wote.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jijini Dar es Salaam leo, Afisa Habari wa Baraza la Mitihani nchini, John Nchimbi, alisema kuwa mfumo huo utatoa namba Maalum ambayo itamtambulisha mwanafunzi katika ngazi zote za mitihani.

“Mfumo huu utakuwa na faida nyingi sana pamoja na kusaidia katika uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja kwenda nyingine ndani ya mkoa au nje ya mkoa hivyo kuondoa tatizo la wanafunzi hewa”alisema Nchimbi.

Aliongeza kuwa mfumo huu utasaidia katika uandaaji na utoaji wa Takwimu za Wanafunzi katika ngazi ya shule Wilaya ,Mkoa mpaka Taifa.

Alimaliza kwa kusema kuwa Baraza limeanza kufanya majaribio ya Mfumo huu katika mikoa miwili ya Mwanza na Ruvuma na Ifikapo Disemba mfumo utaimarishwa ili Januari hadi Mei 2017 utumiwe nchi nzima kwa shule za msingi.
Afisa Habari wa Baraza la Mitihani nchini John Nchimbi akizungumza na wanahabari juu ya mfumo huo mpya. Kushoto ni Afisa Mitihani wa Baraza hilo, Khaflan Katiki.

Wizara ya Nishati na Madini waandaa mpango mkakati wa matumizi ya Gesi asilia.

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na madini, Profesa James mdoe akizungumza na waandishi habari katika juu mkakati mpango wa gesi asilia leo jijini Dar es salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WIZARA ya Nishati na Madini iko katika hatua ya mwisho ya kutengeneza mpango mkakati wa matumizi ya gesi asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara na Nishati na Madini, Profesa James  Mdoe amesema mpango huo ni kuangalia matumizi ya gesi asilia kwa ndani ya nchi na kuweza kuchochea uchumi wa viwanda.

Profesa Mdoe amesema kuwa mpango mkakati  utasaidia katika kutengeneza  katika kuangalia soko la gesi asilia nje ya nchi.

Amesema kuwa matumizi ya gesi asilia  kinatarajia  kujengwa kiwanda kikubwa  kinachotumia gesi hiyo. 

Nae Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Kapuulya Naomba amesema  kuwa wataanza na kusambaza mabomba katika jiji la Dar es salaam kutokana matumizi ya mkaa.

WACHEZAJI UHAMIAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI.

0
0
 Kaimu Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji ya Uhamiaji, Victoria Lembeli, akipokea Kombe  la ushindi wa klabu Bingwa Taifa kutoka kwa Nahodha wa timu ya Uhamiaji , Neema Massawe wakati wa hafla ya kuwapokea wachezaji wa timu hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu ya Idara ya Uhamiaji wakiingia katika Ofisi za makao makuu ya Idara hiyoKurasini jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa Ngazi ya juu wa Idara ya Uhamiaji wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishiwahabari.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na  Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
WITO umetolewa kwa timu ya mchezo wa mpira wa pete ya Idara ya Uhamiaji nchini kuongeza juhudi katika michezo mbalimbali hili kuimarisha umoja na mshikamano uliopo nchini.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini , Victoria Lembeli, alipokuwa akipokea kikombe cha ushindi wa Klabu bingwa Taifa kwa timu ya mpira wa pete

“Hakika niwapongeze kwa ushindi mliopata kwani mmeweza kushindana katika ,mazingira magumu hivyo nilivyopata kusikia kuwa mmekuwa mabingwa sikuamini masikio yangu hivyo naomba muendelee na moyo huo huo kwa kuwa michezo ndio inadumisha umoja na mshikamano” anasema
Kamishna Lembeli aliongeza kuwa mshikamano na juhudi katika michezo viatachangia kuongeza utashi wa kazi .

Kwa uapande wake Nahodha wa timu hiyo ,Neema Massawe alisema kuwa wao kamatimu wamejipanga kushinda mishandano yote yaliyo mbele yao hili kuendelea kutetea nafasi walizonazo.

Alitamba kuwa Uhamiaji ndio timu pekee inayofanya vizuri katika mchezo wa mpira wa pete hapa nchini hivyo tasisi nyingine za serikali na majeshi zinapaswa kujipanga na kujifua sana hili kufikia wao walipo.

Aliongeza kuwa wameweza kucheza mashindano ya Klabu bingwa Taifa bila ya kufungwa hata mchezo mmoja na timu zote 12 jambo ambalo linathibitisha ubora wao.

WAZIRI MKUU AHOJI SABABU ZA MAGEREZA KUTENGEZA MADAWATI KWA WATU BINAFSI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Jordan Rugimbana kuchunguza ni kwa nini Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Bw Antonino Kilumbi amekwenda kutengeneza madawati kwa watu binafsi  badala ya karakana ya Magereza kama  ilivyokusudiwa na Serikali.

Magereza mkoa wa Dodoma ilipewa sh. milioni 24 na Serikali ili kutengeneza madawati 480 na kila moja lilitakiwa kugharimu sh. 50,000. Uongozi wa gereza hilo ulitengeneza madawati hayo kwa watu binafsi ambapo dawa moja limegharimu sh. 70,000.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mofisa wa Magereza wakati alipotembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga mjini Dodoma Oktoba 5, 2016.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2016) wakati alipotembelea Gereza la Isanga mkoani Dodoma akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo yanayotoa huduma za jamii mjini hapa.

Amesema kama gereza hilo halikuwa na uwezo wa kutengeneza madawati hayo kwa nini kazi hiyo wasingeipeleka kwenye taasisi nyingine ya umma, hivyo amemtaka Mkuu wa Mkoa Bw. Rugimbana kufuatilia ziada ya sh. 20,000 kwenye utengenezaji wa kila dawati inatoka wapi na inakwenda kwa nani.

“Nimesikia kwamba mnawachangisha askari kiasi kilichoongezeka kwenye utengenezaji wa madawati hayo. Ni marufuku askari kutoa fedha mifukoni mwao kulipia shughuli za Serikali,” amesisitiza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mofisa na Askari Magereza baada ya kutembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga mjini Dodoma Oktoba 5, 2016. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Parole Augustine Mrema.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

NMB YADHAMINI TIMU YA MASHUA KWENYE MASHINDANO YA MASHUA AFRIKA

0
0
Kwa kutambua umuhimu wa michezo kwa vijana nchini, benki ya NMB imedhamini vijana watano kutoka nchini kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya mashua ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Luanda, Angola kuanzia Oktoba 6 - 13, mwaka huu. Akizungumzia udhamini huo wa Milioni 10 na jezi kwa vijana hao.

 Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema NMB kama benki ya kitanzania inawathamini watanzania wote na inajivunia kuwa sehemu ya makampuni ambao yameidhamini timu hiyo ili ikaiwakilishe nchi katika mashindano ya mashua.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akizungumzia udhamini wa NMB kwa timu ya vijana ya mashua ambayo inataraji kushiriki Mashindano ya Afrika ya Mashua.

“NMB ni benki ambayo inaongoza Tanzania na ipo kwa ajili ya watanzania, moja ya sehemu ambayo tunaihudumia ni vijana, tunadhamini michezo mingi na tunaamini ni sehemu nzuri kwa vijana wadogo maana wanatakiwa kuandaliwa mapema,

“Mchezo wa mashua una wachezaji wengi, NMB inajivunia kuwa sehemu ya wadhamini kwa vijana hawa ambao watawakilishi nchi, na tunaamini watarudi kutoka Angola wakiwa na medali,” alisema Ineke.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Chama Mashua Tanzania (TSA), Philimon Nassari aliishukuru NMB kwa msaada ambao imewapatia na kuelezea changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiukabili mchezo huo kutokana na kutokuwa na wadhamini wanaowasimamia na kuwaomba NMB kuendeleza udhamini huo kwa kipindi kirefu zaidi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Mashua Tanzania (TSA), Philimon Nassari akiishukuru NMB kwa kuipa timu ya vijana udhamini na kuelezea changamoto ambazo zinawakabili.

“Chama chetu ndiyo kina dhamana ya kuongoza mchezo wa mashua nchini, mchezo huu sio mgeni hata watu wanaovua ngalawa wanatumia mashua, mchezo wetu unadumaa kwasababu hatuna udhamini na kama mnavyojua mchezo huu unachezwa sehemu ya wazi kwahiyo hakuna anayelipa pesa, muda wote niwa kujitolea,

“Mchezo huu kwa sasa nchini unakuwa kama unashuka, tulianza kushiriki na watoto 12 lakini kwa sasa tunakwenda na watoto watano, mwanzo mgumu lakini sisi tunaongeza juhudi na tunawashukuru NMB kwa hili wamelolifanya,” alisema Nassari.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akimkabidhi jezi Kocha wa Timu ya Mashua, Penny Alson.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Dar es Salaam Yacht Club, Robert Cunnane alisema klabu yao imekuwa ikiwasaidia watoto mbalimbali ambao wanacheza mchezo wa mashua kwa kuwapa nafasi ya kujifunza lakini pia muda mwingine kuwalipia fedha kwa ajili ya kwenda kujifunza mchezo huo na matarajio ya klabu hiyo ni kuona mchezo wa mashua unakuwa maarufu nchini.

“Tumekuwa tukisaidia mchezo wa mashua lakini kutoa udhamini kwa kutumia Milioni 24 kila mwaka kwa watoto kwenda kujifunza mchezo wa mashua na kwenda kushiriki mashindano mbalimbali, tunajivunia kuwa na hii timu na tunataka kuona timu hii inapata mafaikio,” alisema Cunnane.
Mwakilishi wa Dar es Salaam Yacht Club, Robert Cunnane akizungumzia jinsi klabu yao inavyoisaidia timu ya mashua.

MIXTAPE VOL. 2 KUZINDULIWA OKTOBA 9 MAISHA BASMENT JIJINI DAR.

0
0
DJ wa Maisha Basement, Ally Suleiman (DVJ Ally B) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa anatarajia kuzindua Mixtape ya Fresh From Kitaa Vol. 2 itakayofanyika Oktoba 9, mwaka huu Pale Maisha Basement Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Kulia ni Godwin Elia Dj (Godo).

Amesema kuwa Mixtape hiyo itakuwa ni mwendelezo wa Mixtape kwa miezi mingine itakayoendelea.

Pia amesema kuwa Mixtape hiyo itakuwa ni muunaniko wa nyimbo kali za wasanii hapa nchini pamoja na wasanii wa nje ya nchi ikiwa ni kuwaburudisha  mashabiki wa Mziki na kuwapa fursa ya kuzisikiliza live(Mbashara) yeye akiwa ndiye DJ wa kazi hiyo.

DJ Ally B amesema kuwa Mixtape Vol. 2 ameiandaa kwa utofauti sana kutokana na marekebisho makubwa ya maoni ya mashabiki wa Mziki waliyoyatoa.
Amesema kuwa katika uzinduzi huo kiingilio kitakuwa cha kawaida na cha shilingi elfu kumi pia kwa mashabiki wa kwanza kufika watajipatia CD ya Mixtape bure ili wakaisikilize nyumbani.
 Meneja wa kitengo cha Mawasiliano wa Maisha Basment, Robart Salehe katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na uzinduzi wa Mixtape Vol.2 katika Clabu ya Maisha Basement jijini Dar es Salaam. Kushoto ni DJ wa Maisha Basement, Ally Suleiman (DVJ Ally B) na Kulia ni Godwin Elia Dj (Godo) 
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

EAC SECRETARY GENERAL RECEIVES CREDENTIALS FROM IRISH AMBASSADOR

0
0
The Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko, today received credentials from the Ambassador of the Republic of Ireland to the United Republic of Tanzania, H.E Ambassador Paul Sherlock, who has also been accredited to the EAC.

In the Ambassador’s accreditation letter dated 30th August, 2016 addressed to the Secretary General of the EAC, the Irish Minister of Foreign Affairs, Mr. Charles Flanagan, appoints Amb. Paul Sherlock as the Irish representative to the EAC. 

The Secretary General warmly welcomed Amb. Sherlock to the EAC and briefed him on the current achievements in the pillars of the regional integration and development process. He said the Community had expanded tremendously within a short spell of time, which has necessitated the Community to review its institutional set-up and work on sustainable financing mechanism.

Amb. Mfumukeko further informed his guest of the reforms he had instituted within the Organs and Institutions of the Community aimed at cost cutting and prudent financial management.

In his remarks, Amb. Sherlock hailed the Secretary General for the good work he and his team were doing in deepening the regional integration agenda. He said achieving the Customs Union and the Common Market and moving towards a Monetary Union within such a short time for the Community was commendable

Amb. Mfumukeko and the Irish envoy discussed several issues including the status of the EAC-EU Economic Partnership Agreements (EPAs) and the Inter-Burundi Dialogue. They also explored areas of collaboration in trade and investment, agro-processing, tourism and ICT.

The Secretary General informed Amb. Sherlock that the EAC Secretariat was ready to mobilize and send an EAC Mission to Ireland to meet the Irish Chamber of Commerce and Industry, Tourism and Investment Agencies, and other stakeholders to concretize the specific areas of cooperation.

Also present at the accreditation ceremony were Mr. Robert Hull, the Second Secretary at the Embassy of Ireland in Dar es Salaam, Deputy Secretaries General Mr. Charles Njoroge (Political Federation) and Hon. Christophe Bazivamo, and other senior officials at the EAC Secretariat.
East African Community Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (right) holds talks with the Irish Ambassador to Tanzania and the EAC, H.E. Paul Sherlock, at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. The two leaders discussed various issues including the status of the EAC-EU Economic Partnership Agreements (EPAs) and the Inter-Burundi Dialogue.
EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (left) with the Irish Ambassador to Tanzania and the EAC, H.E. Paul Sherlock, after they held bilateral talks at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. They explored areas of collaboration in trade, investment, agro-processing, tourism and ICT.

TANZANIA YAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA AFCON KWA VYUO VIKUU BEIJING CHINA

0
0
Timu ya Tanzania iliyochukua kombe baada ya kuitoa timu ya Ghana kwa Mikwaju ya Penalti katika mashindano ya mpira wa miguu kwa wanachuo wote wa Afrika wanaosoma Beijing Nchini China, yaliyomalizika hivi karibuni wakishangilia ushindi wao huo wakiwa na kombe lao.
Baadhi ya wanafunzi hao wakiwa na Bendera ya Taifa pamoja Kombe lao.

SOMO LA SHERIA: NAMNA YA KURASIMISHA BIASHARA YAKO ILI UKOPESHEKE

0
0
Na  Bashir  Yakub.

Kurasimisha  biashara  kunazo  namna  nyingi.  Kufungua  kampuni   ni  moja  ya  namna  ya  kurasimisha  biashara. Kusajili  jina  la  biashara  nayo  ni  namna nyingine  ya  kurasimisha  biashara. Makala  yatazungumzia  hii  ya  pili  ya  kusajili  jina  la  biashara. Na  hii  ni  kwasababu  hii  ni  njia  nyepesi,  ya  haraka, na  ya gharama  ndogo  sana.

 Mfano  wa jina  la biashara  ni kama,   HK  bazaar, kinondoni  investment, Congo traders, Karoli  LTD  na  mengine  yanayofanana  na  hayo.

1.NINI  MAANA YA  JINA  LA  BIASHARA.
Jina  la  biashara  ni  lile  jina  linalotumiwa  na  mtu  kama  jina  la  utambulisho  wa  biashara  yake  inayofanywa  katika  mfumo  ambao  sio  kampuni.  Makampuni  yana  majina  lakini  majina  hayo  hayawezi  kuitwa  majina  ya  biashara  bali  ni  majina  ya  kampuni.

Jina  la  biashara  ni  kwa  yule  ambaye  biashara  yake  imesajiliwa   lakini  sio  kampuni.  
Aidha mwenye  biashara  ambayo  haijasajiliwa  lakini  analo  jina  fulani  analotumia  kisheria  huyo  hana  jina  la  biashara.Hilo  jina  sio  lake  na  mtu  mwingine  anaweza  kulisajili na  akamtaka  huyu  ambaye  hajalisajili  kuacha mara  moja  kulitumia . 
Ili  sheria  ikutambue  kuwa  una  jina  la  biashara   ni  pale  tu  unapokuwa   umesajili  jina  hilo.  

2. WAPI  WAWEZA  KUSAJILI  JINA  LA  BIASHARA.
Jina  la  biashara  husajiliwa  kwa  msajili  wa  biashara  na  makampuni ( BRELA). Ukifika   hapo  utawaeleza  kuwa  unataka  kusajili  jina  la biashara  watakupa  fomu  maalum  utaijaza .  Lakini  kabla  ya  hapo  utatakiwa   utume  maombi  maalum  hapohapo BRELA ukitaka  kujua  iwapo  jina  ulilochagua  kuwa  la  biashara   yupo  mtu  mwingine  analitumia au  lah.

Hii  ni  kwasababu  jina  ni  moja  Tanzania  nzima.  Hakuwezi  kuwa  na  majina  mawili  au  zaidi   yanayofanana  huku  yote  yakiwa  yamesajiliwa.

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI MKOANI MBEYA

0
0
Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo akisalimia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Maonyesho ya 13 Wajasiriamali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika katika Viwanja vya City Garden jijini Mbeya. PICHA NA KENNETH NGELESI.
Kaimu Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Mbeya, Yohana Mwambilija, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kulia) alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 13 ya Wajasiriamali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Mkaguzi wa NSSF Mkoa wa Mbeya Bupe Mwantole akimkabidhi mwanachama mpya fomu ya kujiunga na NSSF wakati wa maonyesho ya 13 ya wajasiriamali jijini Mbeya.


TAARIFA TOKA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

0
0
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa yeyote anayetaka kuwa Mdadisi au Mkusanyaji taarifa za kitakwimu rasmi katika tafiti mbalimbali zinazoratibiwa na ofisi hii, ni sharti awe amehitimu Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi angalau kwa ngazi ya cheti.

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Na. 9 ya mwaka 2015 inayoipa mamlaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya kuratibu na kusimamia ukusanyaji takwimu rasmi (official statistics) nchini. 

Hivyo, kuanzia sasa NBS itakuwa inawatumia wadadisi ambao wamehudhuria na kuhitimu angalau cheti cha Ukusanyaji Takwimu katika miradi mbalimbali ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.

Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika “Eastern Africa Statistical Training Centre” (EASTC) kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano zaidi na kujisajili wasiliana na:

Ofisi ya Msajili wa Chuo,
Eastern Africa Statistical Training Centre,
S.L.P 35103,
DAR ES SALAAM.
Barua pepe: info@eastc.ac.tz; 
Tovuti: www.eastc.ac.tz  
Simu namba: 022-2925000 au 0784784106.

Tangazo hili limetolewa na:    
Mkurugenzi Mkuu,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
DAR ES SALAAM.
05 Oktoba, 2016.

RAIS JOSEPH KABILA WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NA KUREJEA NCHINI KWAKE

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati akipanda ndege kurejea nchini kwake mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu hapa nchini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipunga mkono kuagana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila (hayupo pichani) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Shekhe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mara baada ya kuagana na mgeni wake Rais wa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila. kulia ni mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema.
PICHA NA IKULU.

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 05 Oktoba, 2016 amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini kwake.


Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Kabila ameagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


Viongozi wengine walioungana na Rais Magufuli wakati wa kumuaga Rais Kabila ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda na Viongozi wa Dini.


Katika hatua nyingine, mara baada ya kuondoka kwa Rais Kabila, Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.


Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.


Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili  walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.

"Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua" amesisitiza Dkt. Magufuli.


Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

05 Oktoba, 2016.

Disclaimer: AU Statement on US Travel Advisory

SHULE YA SEKONDARI TUSIIME YAPIGWA FAINI YA MILIONI KUMI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

0
0
 Naibu Wziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina alipokuwa akifanya ziara ya kukagua mazingira katika shule ya secondary Tusiime iliyopo tabata jijini Dar es salaam mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi ya utililishaji maji taka kwenye makazi ya watu kutoka shuleni hapo.                
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina (katikati)  akipata maelezo ya jinsi gani mfumo wa utililishaji  maji taka unavyofanya kazi katika shule ya secondary Tusiime.                    



Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuipiga faini ya million kumi shule ya secondary Tusiime iliyopo Tabata jijini Dar es salaam kwa uchafuzi wa mazingira

APPLICANTS ADMITTED TO JOIN THE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR FOR 2016/2017 ACADEMIC YEAR

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images