Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

WATUMISHI KISHAPU MABINGWA KOMBE LA NG’OMBE MASHINDANO YA MWENGE WA UHURU

0
0
Timu ya soka ya Watumishi FC wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga imenyakua ubingwa wa michuano ya Mwenge wa Uhuru kuwania Kombe la Ng’ombe.

Katika michuano hiyo iliyotimua vumbi jana jioni, timu hiyo inayoundwa na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iliibamiza kwa mikwaju ya penati Igaga FC mabao 4-2.

Mchezo huo uliochagizwa na hamasa kutoka kwa mashabiki ukichezwa uwanja wa shule ya msingi Mhunze, ulimalizika kwa dakika 90 huku ubao wa matokeo ukisomeka 1-1 yaliyofanya mikwaju ya penati zipigwe.

Katika matokeo ya mikwaju ya penati timu hiyo ya watumishi iliibuka kidedea na inatarajiwa kukabidhiwa zawadi yao ya ng’ombe Ijumaa katika kilele cha Mwenge wa Uhuru wilayani humo.

Awali kabla ya mchezo wa fainali kulikuwa na mechi kati ya Talents FC na Bodaboda zote za mjini Mhunze wilayani humo kutafuta mshindi wa tatu.

Hadi refa anapuliza kipyenga cha mwisho Talents walikuwa wameondoka na ushindi wa bao 1-0 na kuibuka washindi wa tatu.

Michuano ya kuwania kombe la ng’ombe ilianza wiki mbili zilizopita wilayani humo ikiwa na lengo la kuwajengea vijana ari ya kujituma na kujiletea maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba alishuhudia mtanange huo akiwa ameambatana na viongozi wengine akiwemo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Stephen Magoiga Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kengese , Mkuu wa Polisi wilaya, SP.E.Ulomi na Mshauri wa Mgambo Wilaya,  SSgt.Charles Lyashimba.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (kushoto) akibadilisha mawazo na mwenyekiti wa Bodaboda wilayani humo, Daniel Eva.

 Kocha wa Watumishi FC, Japhet Makelele akitoa mawaidha kwa wachezaji wake wakati wa kipindi cha mapumziko kwenye mchezo kati ya timu hiyo na Igaga FC.

 Mchezaji wa Watumishi FC mwenye namba 4 mgongoni akijaribu kuwatoka wachezaji wa Igaga FC huku wachezaji wenzake wakijiandaa kutoa msaada.

 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo waliojitokeza katika uwanja wa shule ya msingi Mhunze kushuhudia fainali za kuwania kombe la ng’ombe kama shamrashamra za mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwasili wilayani humo Ijumaa ya Oktoba 7, 2016.

 Wananchi wa wilaya ya Kishapu wakishuhudia mtanange wa fainali hizo.

Mashabiki wa Watumishi FC wakishangilia ushindi wa timu yao mara baada ya kupigwa kwa mikwaju ya penati.


RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA CHA BAKHRESSA FOOD PRODUCTS LTD. MKURANGA, MKOA MKOA WA PWANI LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa (wa kwanza kulia), Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega wakivuta kamba kwa pamoja kuashiria ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kusindika Matunda cha Bakhresa Mwandege mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa matunda kilichopo Mwandege mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Bw. abubakar Bakhresa, Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega na Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage na Mtendaji Mkuu wa Bakhressa Food Products Salim Aziz Salim. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhressa Said Salim Bakhresa wakiangalia mojawapo za hatua za usindikaji wa matunda aina ya maembe katika kiwanda hicho kilichopo Mwandege mkoani Pwani. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada ya kufungua rasmi kiwanda cha Usindikaji wa Matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege mkoani Pwani. Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA



Hotuba ya Swala ya Ijumaa: umuhimu wa mwezi mtukufu wa muharam

JAJI MKUU WA AUSTRALIA KUSINI AFANYA ZIARA NCHINI

0
0
 Jaji Mkuu wa  Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akipokea zawadi  ya picha  kutoka kwa  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika halfla fupi iliyofanyika  leo  tarehe 7.10 .2016 kwenye ukumbi wa maktaba wa   Mahakama  ya Rufani  ya Tanzania.
 Jaji Mkuu wa  Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kulia) akizungumza kuhusu ziara yake ya siku tatu aliyoifanya nchini na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya mafunzo, sheria na shughuli za kimahakama baina ya nchi hizo mbili. (Kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe. Mkutano  huo ulifanyika leo tarehe  7.10.2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba  na Sheria uliopo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE JAMHURI YA CZECH ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akizungumza na Ujumbe kutoka Jamhuri ya Czech, ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(wa kwanza kushoto), wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.
Mjumbe kutoka Jeshi la Polisi,Kamishna Albert Nyamhanga akijitambulisha kabla ya kuanza mazungumzo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Czech na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Hamad Masauni(kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek.Mazungumzo yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(kushoto), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Kenya, Pavel Rezac, akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA ALIYETOBOLEWA MACHO.

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Said Ally, ambaye ametobolewa macho hivi karibuni,pichani kati Mkewe Zara Sudi mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandish wa Habari.

Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii.
SIKU chache mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kosa la kumtoboa macho ndugu, Said Ally wa Buguruni kwa Mnyamani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda ameamua kuendelea kumsaidia kijana huyo katika hatua zake za zote za matibabu na mtaji wa Shilingi Milioni kumi.

Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kijana huyo kufika katika ofis za mkoa , Makonda alisema kuwa mara baada ya kufanyika uchunguzi na madaktari Bingwa wa Muhimbili imeonekana kuwa bado Said atoweza kupata tena nafasi ya kuona tena hivyo anahitaji matibabu ya ziada.
“Serikali ya mkoa imetoa gari ambayo atatumia kwa kipindi chote akiwa anaenda kupatiwa matibabu na shughuli zingine ambazo atakuwa anafanya mpaka hapo atakapokuwa sawa”alisema Makonda.

Kwa upande Ndugu Said Ally amesema kuwa anawashukuru madaktari kwa juhudi zote walizofanya na shukrani kubwa sana ziende kwa Gea Habibu wa Clouds Media na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa moyo wake aliounyesha kwa kujitoa kwa hali na mali.

“Kiukweli nimeona Mungu akiwa katika upande wangu kwa msaada ninaondelea kupata kutoka kwa mkuu wa Mkoa na watu wa Clouds na madakatari naomba mungu aweze kuwapa maisha marefu” alisema Said.
Makonda alimaliza kwa kusema kuwa Serikali ya mkoa inandaa utaratibu kwa ajili ya watu wengine ambao wanahitaji kujitolea kumsaidia Said hivyo jumatatu atatangaza rasmi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kumsaidia Bwana Said Ally ambaye alitobolewa machi jijini Dar es Salaam.

Hakielimu yaipongeza Serikali.

0
0
Mkurugenzi Mtendaji  wa Hakielimu, John Kalage, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya hatua zilizo chukuliwa na Serikali kwa Walimu wa Mbeya Day.

Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii.
TAASISI isiyo ya kiserikali inayosimamia mwenendo wa Elimu hapa nchini ya Hakielimu imeipongeza Serikali kwa hatua za kinidhamu zilichokuliwa kwa wale wote waliohusika kutoa adhabu ya kikatili kwa mwanafunzi wa kidato cha 3 ,Sebastian Chinguku wa shule ya sekondari ya Mbeya day.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dare s Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa wa tasisi hiyo, John Kalage amesema kuwa  wamepokea tarifa hiyo kwa masikitiko makubwa sana mara baada ya kuona ukatili uliopotiliza.

“tunaipongeza Serikali kwa kuchukua hatua za awali zikiwemo kuliagiza Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua za haraka dhidi ya wanafunzi waliokuwa wanafanya mazoezi ya kufundisha waliohusika katika tukio lile. Aidha tunampongeza Mwalimu aliyethubutu kukemea na kufichua ukatili huu uliopotiliza hivyo tunaomba mamlaka husika zichukue hatua madhubuti za kulinda uhai hata ajira ya mwalimu huyu jasiri” amesema Kalage.

Ameongeza kuwa Hakielimu inaitaka Serikali kuhakikisha suala hili linashughulikiwa kwa upana wake na kuendelea kuitaharifu jamii juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika na ukatili huu.

Alimaliza kwa kusema kuwa licha ya tukio la Mbeya linaonekana kuchukua mjadala mpana hapa nchini kwa sasa, tunapenda kuitaharifu serikali kuwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto wa mwaka 2011 imeonesha kuwa kuna ukatili wa kutisha sana kwa watoto katika shule nyingi hapa nchini vikiwemo vya kimwili na kingono.

Aliweka wazi kuwa adhabu kama hizi zinapotolewa kwa watoto, husababisha wato kutafuta namna ya kukwepa adhabu hiyoo na kupelekea kukimbia masomo yao na hatimaye kuacha shule kabisa.

BMT WAUCHINJIA MBALI MKATABA WA MANJI NA YANGA.

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la michezo Tanzania (BMT) limetangaza kutoutambua Mkataba wa ukodishwaji wa klabu ya Yanga kwa kuwa ni kinyume na katiba ya klabu hiyo.

Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema kuwa mkataba huo kati ya Baraza la Wadhamini wa Yanga na kampuni iliyoikodi klabu hiyo, haukufuata taratibu.

"Ili Yanga iweze kubadili jina na kuitwa Yanga Yetu ni lazima ipite kwa msajili. Wao hawajaenda kwa msajili wanaanza kutangaza jina jipya. Huko ni kupinga katiba," amesema Kiganja.

Baraza limeagiza klabu kutunia vikao mbalimbali vinavyotambulika kikatiba na viitishwe kuzingatia kanuni na taratibu ambapo kamati ya utendaji inatakuwa kukaa na kujadili jambo hilo kama lina faida au hasara.

Na wakishamaliza kulijadili waandike muhtasari na kuupeleka katika ngazi ya juu ya klabu waliangalie na baadae kufanya mabadiliko ya katiba na kisha kuisajili ili kuweza kuingia kwenye mfumo mpya.

Kiganja amesema kuwa kutokana na utaratibu walioutumia Yanga hautambuliki na hawataza kutambua mabadiliko hayo.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO KWA MFUKO WA NHIF LEO JIJINI DAR.

0
0
 .Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akizungumza na viongozi mbalimbali wa NHIF kuhusu kujifunza kutokana na uzoefu  wa kuendesha Mfuko wa bima ya afya, katika ziara ya mafunzo makao makuu ya NHIF leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu).
 Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) akitoa maelezo mafupi kuhusu shughuli za Mfuko leo makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

 MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepokea ugeni kutoka Wizara ya Afya ya Zanzibar katika ziara ya mafunzo iliyoongozwa na Mh.Mahamud Thabit Kombo ambaye ni Waziri wa Afya wa Zanzibar.

Katika ziara hiyo yenye lengo la kushiriki uzoefu wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo, Waziri na timu yake walipata melezo na kujionea shughuli mbalimbali za Mfuko huo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mh.Kombo alisema "tunahitaji kujifunza kutokana na uzoefu wenu wa kuendasha Mfuko wa bima ya afya, hatukuona haja ya kwenda mbali kwani tuna kaka na dada zetu hapa karibu na wana uzoefu wa kutosha".

Mh. Kombo alisema kuwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ina ushirikiano mkubwa sana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na  kusisitiza kuwa Wizara hizi zinafanya kazi kwa karibu sana na hii inasaidia kufanikisha maendeleo ya sekta ya afya kwa pande zote.

Akiwakilisha mada ya Utekelezaji wa shughuli za Mfuko,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga aliongelea umuhimu wa Bima ya Afya katika maendelea ya sekta ya afya nchini na kuanisha utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo ambapo alielezea pia mifumo imara ya uendeshaji wa Mfuko ikiwemo ya Tehama lakini pia mifumo  ya kubaini udanganyifu ili kuudhibiti.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) lielezea umuhimu wa Mfuko kujipanga kimuuondo katika kuhakikisha unaweza kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha afya bora kwa wote. "Pamoja na mambo mengine, elimu kwa umma ni suala la msingi sana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko na kuwapa nafasi wadau kuuliza na kujibiwa hoja zao"alisema.

Akitoa shukrani zake kwa NHIF katika ziara hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari, Waziri Kombo alishukuru Mfuko na kusema kwamba utabakia kwenye historia ya maendeleo ya sekta ya afya Zanzibar lakini pia alisisitiza umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa kusema "Bima ya afya ni Mkombozi wa wanyonge"

KIWANDA CHA WACHINA DAR CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 25 KWA KUKIUKA SHERIA YA MAZINGIRA NA KANUNI ZAKE.

0
0
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (kushoto) mara baada ya kuwasili na kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Murzer kilichopo jijini Dar e s salaam.  
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati) alipofanya ziara ya kukagua mazingira katika kiwanda cha kutengeneza viroba vya mifuko Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akikagua sehemu ya kuyeyushia viroba ya mifuko katika kiwanda cha Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam mapema hii leo.

KIWANDA cha kutengeneza mifuko maarufu kama viroba cha UNBERG INTERNATIONAL cha jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Raia wa China kilichopo katika eneo la viwanda Mandela Road jijini Dar es salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kukiuka vibaya sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Kiwanda ambacho kilikuwa hata hakijulikani kinachotengeneza mifuko itumikayo kufungia bidhaa mbali mbali kama sabuni, saruji na sukari, kimeonekana kufanya kazi ya uzalishaji katika mazingira hatarishi kwa wafanyakazi kiwandani hapo pamoja na mazingira.

Hayo yamebainika katika siku ya pili ya hitimisho ya ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu waRaisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpiga alipokua akikagua baadhi ya Mazingira ya jiji la Dar es Salaam na viwanda, ndipo alipoingia kiwan dani hapo kwa kushtukiza na kujionea namna ambapo raia hao wa China wanavyotiririsha uchafu wa kinyesi cha binadamu katika mto msimbazi.

Naibu Waziri Mpina alisema, “Tunawapenda na kuwajali wawekezaji ila kwa Uchafuzi huu mnaoufanya hapa hata kama ingekuwa nchini kwenu hii isinge ruhusiwa, nilitaka kiwanda hiki kifungwe kabisa lakini lazima taratibu za kisheria zifuatwe. Kiwanda hakina hata cheti kimoja kinachowaruhsu kuanya kazi hizi” Alisisitiza Mpina.  Pamoja na uchafu wa maji baada ya kuswafisha malighafi ya mifuko hiyo kiwandani hapo ambayo nimifuko ya bidhaa mbali mbali ikirejelezwa bila kujali wala kutibu maji na kuyaachia katika mazingira.

Akitaja adhabu katika kiwanda hicho mratibu wa kanda ya mashariki kutoka baraza la taifa  la hifadhi na usimamizi  wa mazingira NEMC Bw. Jafari Chimgege, amesema kuwa kiwanda kinatakiwa ,kulipa faini hiyo ndani ya siku saba na kuacha kutiririsha maji pamoja na kurekebisha wa usafishaji viroba kiwandani hapo, kupata cheti chatathmini ya athari za mazingira pamoja na vibali vingine vya uwekezaji nchini.

Kwa upande wake mtaalam wa maji Ardhini kutoka bonde la Wami Ruvu Bw. Msuda,amewataka wawekezaji na wenye viwanda nchini kufika katika ofisi za Bonde zilikzopo Ubungo maji jijini Dar es Salaam  ili waweze kufanya mchakato wa kupata vibali na vyeti vya kutiirisha maji machafu yaliyotibiwa kwa njia sahihi.

Naibu waziri mpina amehitimisha ziara yae ya siku mbili jijini Dar es salaam ya kukagua baadhi ya viwanda na mazingira.

WALIMU WATAKIWA KUACHA UKATILI - RIDHIWANI

0
0
Na John Gagarini, Chalinze

KUFUATIA tukio la walimu wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) na cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambao wanadaiwa kumpiga mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Mbeya walimu nchini wameambiwa kupiga wanafunzi siyo njia sahahi ya kufundisha wanafunzi.

Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete kwenye mahafali ya darasa la saba ya shule ya Msingi Kibiki.

Ridhiwani alisema kuwa baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia vibaya ualimu wao kwa kutoa adhabu ambazo haziendani na maadili ya kazi zao.
“Walimu nawaombeni mzingatie maadili ya kazi zenu kwani kuna taratibu za kutoa adhabu na ziko wazi lakini siyo kuwafanyia ukatili wanafunzi kama wale wa Mbeya ambao wameonyesha ukatili wa hali ya juu,” alisema Ridhiwani.

Alisema kuwa mwanafunzi anapaswa kueleweshwa na hata kama ni kupewa adhabu aadhibiwe kwa njia zinazostahili na zinafahamika ambazo si za ukatili na zinazozingatia utu wa mtu.
“Walimu nyie ni walezi hivyo ukiwa mlezi lazima umlee mtoto katika utaratibu kwani endapo unamfanyia ukatili kama huo unamjenga katika mazingira ambayo naye akikua ataona ni hali ya kawaida,” alisema Ridhiwani.

Aliwataka wahitimu hao kutojiingiza kwenye makundi ambayo yanakwenda kinyume cha maadili wakati wakisubiri matokeo ili wasije wakashindwa kusoma vizuri mara waendapo shule za sekondari.

Kwa upande wake mlezi wa shule hiyo Nasar Karama alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme barabara na maji.

Karama alisema kuwa shule inashirikiana na wazazi na walezi katika kukabiliana na changamoto hizo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri yenye elimu bora.

WAZIRI UMMY ATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO MKOANI KAGERA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kuhusu hatua iliyofikiwa na serikali katika kurejesha hali baada ya tetemeko lilitokea mkoani humo ambapo pia alimshukukuru Waziri Ummy kwa Misaada aliyoitoa wakati wanakabiliana na maafa ikiwemo, Madawa, Vifaa tiba na madktari iliyowezesha kusaidia kwa kiasi kikubwa waathirika wa tetemeko.
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kuipongeza kamati ya mkoa kwa namna walivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko pamoja na kuwahudumia waathirika.
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu misaada iliyotolewa na Bohari ya Madawa (MSD) waliotoa Dawa na Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 30.
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mashuka 250 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). PICHA NA ELEUTERI MANGI-MAELEZO

NEWS ALERT: MTU MMOJA ADAIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU MKOANI DODOMA LEO

0
0
 Ajali hii imetokea leo katika eneo la Emaus, Mkoani Dodoma ambapo imehusisha gari kubwa mbili na moja dogo aina ya Toyota Noah. Inadaiwa kuwa Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika mpaka sasa.
 Askari Polisi wakiwa eneo la tukio kuokoa majeruhi.

EALA SITTING FOR ZANZIBAR NEXT WEEK

0
0
The East African Legislative Assembly (EALA) shall hold its Sitting in Zanzibar, Tanzania, next week. The Plenary which takes place from Monday, October 10th, 2016 to Friday, October 21st, 2016, is the Second Meeting of the Fifth Session of the Third Assembly. 

The Assembly is to be presided over by the Speaker, Rt. Hon. Daniel F. Kidega. Top on the agenda during the two-week period is the Special Sitting on Tuesday, October 11th, 2016, which is expected to be addressed by the President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, H.E. Dr. Ali Mohamed Shein.

This is the first time the 3rd Assembly is meeting in Zanzibar as part of its rotational principle.   The 2nd Assembly on its part held a Sitting in Zanzibar in December 2007.

The Assembly is expected to dispense with three key Bills, the EAC Trafficking in Persons Bill 2016, the EAC Polythene Materials Control Bill 2016 and the EAC Gender Equality and Development Bill 2016.

The EAC Counter-Trafficking in Persons Bill, 2016, seeks to provide a legal framework, develop common measures, strategies and programmes to the prevention of trafficking in persons and the perpetrators of such actions. The Bill is being debated at a time when the region and the globe are reeling from major effects of counter-trafficking in persons.  

The Bill is to further develop partnerships for co-operation in counter trafficking in persons and provision of protection mechanisms and services for persons.  At the Sitting in Dar es Salaam in March 2016, the Assembly committed the crucial Bill to the Committee stage.

The EAC Polythene Materials Control Bill, 2016 moved by Hon. Patricia Hajabakiga, aims at providing a legal framework for the preservation of a clean and healthy environment through the prohibition of manufacturing, sale, importation and use of polythene materials.  The Bill was re-introduced during the Sitting held in August 2016 in Arusha, Tanzania.

The EAC Gender Equality and Development Bill 2016 on its part, sets out to make provision for gender equality, protection and development in the Community.

According to the mover, Hon. Nancy Abisai, the Bill seeks to consolidate and harmonise the various commitments on gender equality that have been made at regional, continental and international levels in the context of the EAC. 

The EAC Partner States appreciate the importance of women and men's participation in the integration process of the EAC. At the same time, the Partner States are signatories to and should adhere to the instruments and take cognizance of emerging threats such as feminization of poverty, globalization, and gender based violence – all of which impact negatively on citizens. 

The House shall also be furnished by a number of reports. They include Reports of the Committee on Communication, Trade and Investments, the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution and the Committee on Legal, Rules and Privileges. The Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources and the General Purpose Committee shall also be tabling their reports.

EALA Sittings are held under the principle of rotation in line with Article 55 of the EAC Treaty. EALA meets at least once in every year at its headquarter in Arusha, Tanzania. 

HESLB YASITISHA MIKOPO YA WALIMU WANAFUNZI WALIOMPIGA MWANAFUNZI MBEYA

0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inautaarifu umma kuwa imesitisha mikopo ya elimu ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa walimu-wanafunzi wanne waliosimamishwa masomo kwa kuhusika katika tukio la kumshambulia na kumuumiza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya. Walimu hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo.

Na.

Jina

Chuo Anachosoma

1.

Frank Msigwa

Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

2.

John Deo

Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

3.

Evance Sanga

Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

4.

Sante Gwamaka

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Kwa utovu huo wa nidhamu, wanafunzi hao wamesimamishwa masomo na mamlaka husika kwahiyo wamepoteza sifa za kuendelea kupokea mikopo. Mikataba inayosainiwa na wanufaika wa mikopo inawataka wanufaika kuzingagatia masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzingatia nidhamu na kufuata sheria na taratibu za vyuo na mamlaka halali.

Aidha, kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja.

Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaika wanaoendelea masomo kuzingatia masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanuni taratibu na kuwa mfano mwema katika jamii. Mikopo na ruzuku zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wema, waadilifu, na wachapa kazi ili kujenga uchumi imara na ustawi kwa wote.

MAWAZIRI WA FEDHA WAJADILI NAMNA YA KUPAMBANA NA UTAPIAMLO NA UDUMAVU WA AKILI WA WATOTO

0
0
Benny Mwaipaja, MoFP 
Washington DC 
7.10.2016 

MAKAMU wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitaka Benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha ili kutatua changamoto ya utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano kwenye nchi masikini na zinazoendelea ili kujenga kizazi chenye afya kwa maendeleo endelevu ya mataifa hayo. 

Makamu wa Rais ametoa wito huo Mjini Washington Marekani kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati wa mkutano ulioandaliwa na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Kim, ulioshirikisha mawaziri wa Fedha na wadau wengine kutoka nchi zaidi ya 180 wanaoshiriki mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo na Shirika la Fedha Duniani-IMF 

Amesema kuwa licha ya Tanzania kufanikiwa kupunguza utapiamlo na kiwango cha udumavu kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 kutoka asilimia 42 hadi kufikia asilimia 34, bado idadi kubwa ya watoto wanaokadiriwa kufikia milioni 2.7 wamedumaa akili huku wengine laki sita wakikabiliwa na utapiamlo mkali. 

Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kwa kutambua changamoto hiyo, serikali imepanga kutumia kiasi cha dola Milioni 115 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 254 kukabiliana na tatizo hilo katika kipindi cha miaka mitano kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka Mitano, kuanzia mwaka 2016/2021 

Ameitaka jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za mataifa masikini na zinazoendelea ili kuwaokoa mamilioni ya watoto wanaokabiliwa na tatizo hilo hivyo kuathiri mustakabali wa watoto kielimu na kimaisha. 

Kwa upande wake Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Kim, amesema kuwa asilimia 43 ya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano wanaokadiriwa kufikia milioni 250 katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati wamedumaa na kukabiliwa na utapiamlo mkali unaoletelezwa na umasikini pamoja na ukosefu wa elimu kuhusu umuhimu wa kuwapatia watoto lishe bora na unyonyeshaji wa maziwa ya mama, 

Ameahidi kuwa Benki hiyo itatenga fedha kupitia miradi mbalimbai inayotekelezwa kwa ufadhili wake na kushirikisha sekta binafsi ili lengo la kunusuru watoto katika hali hiyo ya utapiamlo na udumavu wa akili liweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka. 

Ameyataka Mataifa kuwekeza fedha katika ujenzi wa miundombini ya sekta ya afya, elimu, maji, na usalama wa chakula, kuwajali na kuwapenda watoto ili malengo ya kukomesha tatizo hilo yafikiwe kama yalivyopangwa.  
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha hotuba kuhusu ni jinsi gani Tanzania imejipanga kukabiliana na tatizo la utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano, alipomuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jijini Washington DC, Marekani.
Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akimpogeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, baada ya kuwasilisha hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo kuhusu watoto kupata lishe bora wakati wa kuzaliwa na kusisitiza wakinamama wanyonyeshe watoto ipasavyo ili kuondokana na tatizo kubwa la utapiamlo ambalo mara nyingi huwakumba watoto wanapokuwa wadogo na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa, Jijini Washington DC.
Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa na Mawaziri wa Fedha wa Afrika akiwemo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philiph Mpango(wa nne kutoka kulia),Jijini Washington DC.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, wa kwanza kushoto akisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, katika mkutano uliowahusisha Mawaziri wa Fedha kutoka nchi kadhaa duniani kama vile Cameroon, Ethiophia, Senegal na Indonesia ambapo rais huyo aliwataka mawaziri hao wasimamie rasilimali fedha vizuri hasa katika suala la kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano, mkutano uliofanyika Jijini Washington DC, Marekani.

SERIKALI YAAHIDI KUBORESHA OFISI YA MKEMIA MKUU,KUWA NA VIFAA VYA KISASA ZAIDI

0
0
 
Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii

SERIKALI imesema itaendelea kuisadia ofisi ya Mkemia mkuu kuwa na Vifaa vya kisasa ili iweze kupambana na changamoto mbalimbali za upimaji.

Hayo yamesemwa jioni ya leo na Naibu Waziri wa Afya ,Dk Hamisi Kigwangwala katika hotuba yake iliyosomwa na afisa utawala wa Wizara hiyo,Michael John katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi Kidato cha nne na cha Sita Mwaka jana.

“Tunashukuru kwa kazi mnayofanya na sisi kama serikali tunajipanga kwa kila namna kuhakikisha kuwa ofisi hii ya mkemkia mkuu inakuwa bora zaidi licha kutangazwa kuwa ndio bora kwa Afrika Mashariki” amesema

Alimaliza kwa kuwataka wanafunzi wote waliofanya vizuri katika masomo yao kuwa bado wanakazi kubwa ya kuongeza juhudi hili kufikia malengo waliyojipangia.

Afisa Utawala wa Wizara wa Afya, Michael John akikabidhi cheti kwa mshindi wa kwanza wa masomo ya Sayansi kwa Wanaume Mugisha Lukambuzi kutoka shule ya Sekondari ya Bendel Memorial ya Moshi
Afisa Utawala wa Wizara wa Afya, Michael John akikabidhi cheti kwa mshindi wa kwanza wa masomo ya Sayansi kwa Wanawake Naomi Sarakikya kutoka shule ya S't Mary's Mazinde juu.

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afunga rasmi kongamano la 30 la Wanasayansi Watafiti

0
0
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla amewaeleza wanasayansi hao watafiti kuwa Serikali inashirikiana nao bega kwa bega katika jukumu la maendeleo hapa nchini hivyo  uwepo wao ni kielelezo tosha cha maendeleo ya Taifa na watu wake hasa katika Nyanja za kiuchumi, Afya, Mazingira na mambo mengine  ya kimaendeleo.



Aidha, amebainisha kuwa changamoto za magonjwa ya virusi yanayotokana na Mbu ambapo ameahidi amewahidi wanasayansi hao na Wizara yake kushirikiana nao katika kulipitia ufumbuzi.



Dk.Kigwangalla amewahakikishia Wanasayansi hao  kuwa, masuala yote ya kuimalisha huduma za Maabara katika ngazi za msingi kwani suala hilo amekuwa akilifanya kila mahala anapokwenda kwenye ziara zake juu ya upatikanaji wa huduma  Maabara bora kwenye sehemu za Afya.



“Nimependa maombi yenu haya juu ya kuimalisha huduma za Maabara kwenye ngazi za msingi. Suala hili nimekua nikilifuatilia kila ziara zangu kwenye vituo vya Afya na Hospitali zote hivyo nitalibeba hili na nitaendelea nalo kwa sababu nina aamini kutoa huduma za afya bila kuwa na huduma madhubuti za Maabara ni kuchezea afya za watanzania wenzetu, Ni lazima tuwe na huduma bora za Maabra zetu na suala hili tutakaa mimi na Mh. Waziri kuona namna ya kufanyia maboresho zaidi.” Amesema Dk.Kigwangalla.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia Wanasayansi watafiti (Hawapo pichani) walioshiriki kongamano la 30 Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga kongamano hilo la siku tatu.
 Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela akielezea machache kabla ya kumwalika mgeni rasmi  kufunga mkutano huo
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpa shada la maua mmoja wa Staff member kwa namna walivyoweza kuandaa kongamano hilo
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi shada la maua mmoja wa wafanyakazi wa NIMR kwa namna walivyoweza kufanikisha shughuli hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 07.10.2016

KC GLOBAL LINKS LTD SEA AND AIR CARGO UPDATES...

0
0
THE NEXT AIR CARGO NO 1002 TO DAR WILL DEPART 
ON SATURDAY 08/10/2016. CUT OFF FRIDAY 07/10/16


CARGO 1001 IS READY FOR COLLECTION 
IN DAR FOR THOSE WHO ARE YET TO COLLECT
PLEASE BRING YOUR CARGO 
NOW TO AVOID DELAYS...
AIR CARGO TO DAR £3.50 PER KG INCLUSIVE CLEARANCE
AIR CARGO TO DAR £1.80 PER KG EXCLUSIVE CLEARANCE
MZIGO KWA MELI TO DAR £1.80 INCLUSIVE CLEARANCE
(CONTAINER ZINAONDOKA MARA MBILI KWA MWEZI)
CONTACT US ON;
OFFICE; +44 1375 85 85 25
MOBILE; +44 7494 36 41 94


KC GLOBAL LINKS LTD
SUITE 2 CLIPPER HOUSE, TILBURY DOCKS, RM18 7SG
CARGO COLLECTION ANYWHERE IN LONDON IS FREE
HAPA NI KAZI TU...!


Anaitwa Miss Hannah Towlmson ambae ni Mwingereza. Yeye akishirikiana na Mtanzania Benjamin Masuka, wameleta nchini tani saba za misaada kusaidia yatima  wenye ulemavu Tanzania. Katika mizigo hiyo kuna wheel chairs, michezo, maziwa, pampers na vitu vingine.

Na sisi KC GLOBAL LINKS kwa mchango wetu tutavisafirisha mpaka Tanzania na tutavilipia kila kitu
Kutoa ni moyo wala sio utajiri!
Mungu awabariki sana
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images