Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1378 | 1379 | (Page 1380) | 1381 | 1382 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0


  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

  Serikali ya Tanzania na Cuba zimeahidi kuendeleza ushirikiano uliopo, ambao umeasisiwa na viongozi wa mataifa hayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania pamoja na Fidel Castro Rais mstaafu wa Cuba.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Ikulu leo jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, amesema kuwa Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa ameitikia mwaliko huo wa kuja nchini kwa vile nchi hizo mbili zimekua na ushirikiano na mahusiano mazuri kwa muda mrefu.

  “Ziara hii ni moja ya jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili ili kuhakikisha mahusiano yaliyopo yanaimarika zaidi” alisema Makamu wa Rais

  Katika ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Cuba nchini, mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo masuala ya Afya, Elimu, Michezo, na Utamaduni, ambapo katika sekta ya afya nchi ya Cuba imepiga hatua na kuahidi kushirikiana na Tanzania ili kujenga kiwanda cha kisasa cha kutengeneza madawa ya binadamu.

  Aliongeza kuwa Tanzania imeomba Serikali ya |Cuba kuendelea kusaidia sekta hiyo kwa kufundisha wataalamu wa afya, ambapo tayari madaktari 24 kutoka Cuba wako nchini kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za kitabibu na mafunzo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.

  Masuala mengine yaliyojadiliwa katika ziara hiyo ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya elimu, biashara, utalii na uwekezaji.Ambapo pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu amesisitiza nia ya Serikali ya Tanzania kudumisha ushirikiano huo ikiwa ni pamoja kupongeza jitihada za kuboresha uhusiano wa Cuba na Marekani.

  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa nchi yake na kuahidi kuendelea kutoa msaada kwa Tanzania.“Tumeamua kuendelea kuboresha mahusiano yetu na Tanzania kwa kuongeza ushirikiano wetu katika sekta nyingine ambazo hatukuwa tunashirikiana hapo awali kama vile sekta ya utalii” alisema Makamu wa Rais wa Cuba

  Aidha, Mhe. Mesa ameiomba Tanzania kuendelea kuiunga mkono Cuba katika masuala ya kimataifa ili kuendeleza ushirikiano na kukuza uchumi kwa nchi zote mbili.

  Makamu wa Rais wa Cuba aliwasili nchini jana jioni kwa ziara ya siku tatu ambapo alipata fursa ya kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakati alipokutana naye Ikuu leo kwa mazungumzo ambapo wamezungumzia jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.(PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Tanzania na Cuba.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha ya mnyama Chui anayepatikana katika mbuga za wanyama za Tanzania Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa , Kulia ni Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.

  0 0


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii -Mkuranga

  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amewataka wananchi kufanya maendeleo na sio siasa kwa muda huu.

  Hayo ameyasema leo katika katika ziara ya vijiji vya kata ya bupu, Ulega amesema kuwa wakati umefika kwa kabila yake kusomesha watoto kwa ajili ya maendeleo kutokana dunia ya sasa inahitaji watalaam.

  Ulega amesema kuwa changamoto zilizo katika kata ya Bupu ni maji pamoja na miundombinu ya barabara hivyo vinatakiwa kupatiwa ufumbuzi ili wananchi waondokane na changamoto hizo.

  Mbunge huyo ameahidi kutoa Bati 50 katika shule mpya inayojengwa katika kitongoji cha kikonga kutokana watoto wa kitongoji hicho wanatembea kilomita sita. Ulega amesema changamoto zilizopo wilaya ya mkuranga zinatakiwa zitatuliwe kutokana na kuomba kazi ya kuwatumikia wananchi.

  Amesema kuwa suala mfuko wa afya ya jamii CHF dawa hazipatikani na kufanya wananchi wengine washindwe kujiunga. Aidha amesema wananchi waliojiunga na CHF ni 65 ikiwa nia serikali ni watu wote wajiunge ili wasipate adha ya kupata huduma za afya.

  Hata hivyo amesema nia ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni kuona wananchi wanafurahia huduma zinazotolewa na serikali na sio vinginevyo. 
   Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa kukagua jengo linalotarajiwa kuwa shule mpya katika kitongoji cha kikonda katika ziara yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuru wananchi kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. 
    Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Kikonda akiwa katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja na kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
    Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano wa wananchi wa kitogoji cha Kikonda juu ya changamoto zinazowakabili akiwa katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Kimataifa ya Mfuko wa misaada ya OPEC unaofadhili miradi mbalimbali chini Mfuko wa Tasaf nchini,Solomon Amieyeofori kutoka Vienna ,Austria(kushoto)akiwa na maafisa wa Mfuko wa Tasaf nchini kukagua miradi katika Jiji la Arusha.

  Ujumbe huo ukakagua ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Azimio jijini Arusha.

  Mmoja wa wanakikundi cha Ushonaji eneo la Kambi ya Fisi Kata ya Ngarenaro,Bupe Anyingise ambaye ni miongoni mwa wanufaikaji wa kunusuru Kaya maskini akishona nyumbani kwake ,Tasaf imewanunulia Vyerehani,Meza na vifaa mbalimbali kuwawezesha kujipatia kipato vilivyogharimu zaidi ya sh 28 milioni.


  0 0


  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemchangia vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo Mkazi wa Kitoma Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

  Akimkabidi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya hivyo baada ya kuona kupitia vyombo vya habari jitihada za Mjane huyo kuanza kuijenga nyumba yake upya kutokana na kuharibika baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo mapema mwezi septemba.

  Aidha Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa wito kwa wananchi ambao hawajaanza juhudi za kurejesha makazi yao waige mfano wa mjane huyo kwa kuanza ujenzi wa nyumba zao.Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Bi. Agripina alisema kuwa anamshukuru Rais kwa mchango huo kwani vifaa hivyo vitamsaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba yake na hatimaye kupata mahali pa kuishi yeye na familia yake baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi.

  Vifaa alivyokabidhiwa mjane huyo ni pamoja na Mbao pisi 30, Mabati 35 ya futi kumi ,Saruji mifuko 25 ,Misumari ya mabati kilo 4, Misumari ya kenchi kg 7 na waya za kufungia makenchi kilo 3.

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu akimkabidhi Vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani Kagera kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
  Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani Kagera akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu nyumba aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September
  Nyumba ya Mjane Mjane Agripina Angelo aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema  mwezi September.SYLVESTER RAPHAEL-AFISA HABARI-KAGERA 

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka taasisi na mashirika ya umma yaliopo chini ya mkoa wake kuiunga mkono Kampuni ya Simu ya kizalendo Tanzania (TTCL) kwa kuanza kuzitumia bidhaa za kampuni hiyo hasa kwenye shughuli za mawasiliano ili kuonesha uzalendo kwa vitendo. 

  Makonda ametoa kauli hiyo leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa kampuni ya TTCL, huku akiahidi kuzishawishi taasisi na mashirika ya umma yanayofanya kazi chini ya utawala wake kuhakikisha wanatumia huduma za TTCL ili kuiunga mkono kampuni hiyo ya kizalendo ya mawasiliano. 

  Alisema Serikali imeonesha nia njema ya kuirejesha TTCL katika hali nzuri baada ya kuirejesha kwa asilimia 100 chini ya umiliki wake, hivyo kuyataka mashirika na taasisi za umma kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kuirejesha kampuni hiyo chini ya umiliki wa serikali kwa asilimia 100. 

  Alisema yete kama kiongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam atahakikisha ofisi zote za umma zilizopo chini ya mkoa wake zitatumia huduma za TTCL na endapo watendaji wa TTCL sinazosita kutumia watoe taarifa ili yeye ahoji ni kwanini wanapinga agizo hilo. 
   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) wakigonganisha glasi za mvinyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na mwenyeji wake huku akionesha alama ya mabadiliko inayotumiwa na TTCL.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JNIA.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya heshima yake. 
  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.


  0 0

  Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii.
  JESHI la Polisi  nchini linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi kuacha mara moja, kwani takwimu za makosa ya kujichukulia sheria mkononi yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi katika kipindi cha Januari hadi Agosti 2016 ni matukio 705, Katika matukio hayo yaliyoripotiwa, Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 393. 

  Hayo yametolewa katika taarifa kwa waandishi wa habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi  Makao Makuu ya Polisi, ACP Advera Bulimba jijini Dar es Salaam leo, tarifa hiyo imeeleza kuwa  kuzipuuza sheria za nchi zilizopo na wakati mwingine kuzikiuka kwa makusudi na mbaya zaidi baadhi yao kufikia hatua ya kuwaua watu wasio na hatia kwa hisia. 

  Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mwananchi yeyote anapaswa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mhalifu au mtu yeyote wanayemtilia mashaka katika maeneo yao.
  Aidha, Jeshi la Polisi nchini, litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa kufuatilia na kuwakamata watu wote wanaojihusisha na tabia za kujichukulia sheria mkononi. 

  Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watu wote wakiwemo wenye ushawishi mkubwa katika jamii kuendelea kukemea na kutoa elimu juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wananchi kuendelea kutii na kufuata sheria za nchi zilizopo.

  0 0

  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

  MKOMBOZI Commercial Bank ambayo ni moja ya benki zinazokuwa kwa kasi nchini, jana imekabidhi madawati mia moja(100) kwa shule ya  Msingi Ngarama ikiwa ni katika juhudi za kuunga mkono wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wa kuchangia madawati mashuleni.

  Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bibi  Edwina A. Lupembe katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya  shule hiyo na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo ambaye alipokea rasmi madawati hayo.

  Akikabidhi madawati hayo Mkurugenzi  wa banki hiyo Edwina Lupembe  alisema wao kama benki wameguswa na tatizo hili la madawati na kuona ni jambo la busara kuchangia ili watoto waweze kusoma bila matatizo.

  “Sisi Benki ya Biashara ya  Mkombozi tunathamini sana elimu na tunaunga mkono jitihada mbalimbali za serikali za kuboresha elimu hasa katika hili la madawati ambapo hapo nyuma tulishuhudia wanafunzi wengi wakikaa chini. Wahenga walisema; Kama mpango mkakati wako ni wa mwaka mmoja panda mpunga kama mpango wako ni  wa miaka kumi panda miti lakini kama mpango mkakati  wako ni wa miaka 100 somesha watoto. Wote tutakubaliana kuwa mpango mkakati wa selikali yetu katika elimu ni wa miaka 100.” alisema.

  Alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa uongozi wa shule hiyo kuhakikisha madawati hayo yanatumiwa vizuri ili wanafunzi wengi zaidi waweze kufaidi, na kwa wanafunzi aliwataka wafanye bidii katika masomo yao kwani sasa mazingira ya kusomea yatakuwa bora zaidi na kwamba elimu ni ufunguo wa maisha bora.

  Bibi  Lupembe alisema mbali na mchango katika jamii, benki yake imekuwa katika mstari wa mbele kuanzisha huduma ambazo zinalenga kuwasaidia wananchi hasa wenye kipato cha chini kama vile huduma ya mikopo ya Mfuko wa Bima ya Afya kwa wakopaji wa vikundi.

  “Huduma hii ni endelevu  na napenda kutoa rai kwa wazazi na walimu waliopo hapa wajiunge katika huduma ya mikopo ya  vikundi inayotolewa na Benki ya Biashara ya Mkombozi kupitia tawi lake la hapa Bukoba ambavyo vitawasaidia kupata mikopo hii ya Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa,alisema na kuongeza kuwa hii italeta afueni kubwa kwani wanafunzi pia wataweza kulipiwa kadi zao za matibabu kupitia bima za wazazi wao ambao watakuwa wamejiunga na vikundi vya mikopo kutoka Benki ya Biashara ya  Mkombozi.
   Mkurugenzi wa benki ya Mkombozi, Edwina Lupembe akikabidhi msaada wa madawati 100 kwa shule ya msingi Ngarama Wilayani Karagwe kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mjini
   Viongozi wa Wilaya ya Karagwe na viongozi wa banki ya mkombozi wakiwa wamekaa kwenye moja ya dawati yaliyotolewa msaada na banki ya mkombozi kwa shule ya msingi Ngarama.
    Wanafunzi wa shule msingi Ngarama wakifurahia madawati waliyopewa msaada na banki ya mkomboz

   Wanafunzi wa shule ya msingi Ngarama wakibeba madawati yao waliyopewa msaada na banki ya mkombozi.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu  Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali ndani nje ya nchi wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela akizungumza mapema leo,alipokuwa akimkaribisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Katika kongamano hilo kauli mbiu yake ni “Uwekezaji katika tafiti zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia.”. 


  Dkt Mwele alieleza pia Mada zitakazojadiliwa ndani ya kongamano hilo kuwa zitajikita zaid kwenye maeneo kama vile 1. Mkakati wa kuboresha afya ya uzazi, ya mama, watoto wachanga na vijana. 2. Magonjwa sugu yasiyoambukiza na changamoto zake,3. Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria,4. Usalama wa Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi,5. Mkakati wa afya moja katika kudhibiti magonjwa ya milipuko,pamoja na 6. Magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele.

  BOFYA HAPA KUSOMA HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS KUHUSU KONGOMANO HILO, KUSOMA HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU WA NIMR DKT MWELE MALECELA BOFYA HAPA

  Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya 200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu. 


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo,kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo kufungua Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kati ni Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala.


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiagana na mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi nchini.

  .....................................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameondoka nchini mchana huu baada ya kumaliza ziara ya kiazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

  Lengo la ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba hasa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya,utamaduni,michezo na utalii.

  Katika sekta ya utalii, Serikali ya Cuba imeahidi kuisaidia Tanzania katika kuendeleza utalii katika fukwe pamoja na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa hapa nchini katika sekta hiyo ili kusaidia kuongeza pato la taifa kupitia shughuli za utalii nchini.


  Aidha kwenye sekta ya viwanda Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana katika ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kutengenezea madawa ya binadamu nchini.

  Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameagwa na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuhitimisha ziara yake nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimsindikiza mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi nchini.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wageni waliohudhuria Sherehe ya Siku ya Watu wa Korea Kusini iliyoadhimishwa jana jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia, na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini Bw. Song, Geum-young (katikati), wakikata keki kama ishara ya kujenga mahusiano mema baina ya nchi hizo mbili katika Sherehe ya Siku ya  Watu wa Korea Kusini iliyoadhimishwa jana jijini Dar es Salaam.
  Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0  Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano huo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James na katikati ni Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji nchini, Lord Hollick.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati nchini hususan nishati jadidifu. Katikati ni Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji kwa Tanzania, Lord Hollick. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke. 
  Wajumbe wa mkutano uliokuwa ukijadili fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nishati nchini wakiendelea na mkutano husika ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (katikati mbele). Upande wa kushoto ni Ujumbe kutoka Serikali ya Uingereza na kulia ni Wataalam kutoka Wizarani.
  Ujumbe kutoka Serikali ya Uingereza ukiongozwa na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji nchini, Lord Hollick (kulia) aliyeambatana na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (wa pili kutoka kulia) wakijadiliana jambo.

  0 0

  Na Theresia Mwami TEMESA. 

  Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wameshauriwa kujituma kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

  Ushauri huo umetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt Musa Mgwatu alipokutana na watumishi hao kutoka katika Mikoa/vituo vya TEMESA vilivyopo nchi nzima katika kikao kazi kilichofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

  Dkt Musa Mgwatu amesema kuwa ana muda mchache tangu aanze kutekeleza majukumu yake na ameanza kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Wakala huu na kuahidi kupita katika vituo vilivyopo mikoani ili aweze kujifunza zaidi.

  “Naahidi kushirikiana nanyi katika kuijenga TEMESA Mpya na naomba ushirikiano wenu na muwe wafatiliaji wa mambo kwani kazi zetu zinahitaji sana ufatiliaji wa kina” Alisema Dkt Mgwatu.

  Ameongeza kuwa amepanga mikakati ya kuiimarisha TEMESA katika maeneo ya Matengenezo ya magari kwenye karakana za TEMESA, namna ya kuyatambua madeni ya TEMESA pamoja na utunzaji wa taarifa zake, utendaji kazi chini ya kiwango wa baadhi ya karakana, mawasiliano kati ya TEMESA makao makuu na mikoa au vituo vyake na utendaji kazi na watu au kampuni zilizosajiliwa.

  Amesisitiza kuwa watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa dhana potofu iliyojengwa juu ya TEMESA kwa wateja wake, wajiimarishe katika utendaji kazi kwa kasi, ubora, weledi uadilifu, ufuatiliaji, na uwajibikaji.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za uendeshaji TEMESA Bw. Senzo Gwanchele amesema kuwa kikao kazi hicho kimelenga kuondoa baadhi ya matatizo yanayojitokeza katika utendaji wa kila siku ikiwemo hoja mbali mbali za ukaguzi, ulipaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) pamoja na uzingatiaji wa sheria ya Ununuzi wa Umma.

  Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) hivi karibuni imepata Mtendaji Mkuu mpya ambaye amekuja na mikakati ya kujenga na kuimarisha TEMESA kwa kupambana na changamoto zinazoikabili Wakala kwa sasa.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bw.Senzo Gwanchele (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam. 
  Mkurugenzi wa idara ya ushauri wa kitaalam wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase LeKujan (wa pili kulia) akizungumza na viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam. 
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),Dkt.Musa Mgwatu (Katikati) akitoa maelekezo kwa viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam. 
  Viongozi na Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wakimsiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt.Musa Mgwatu (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam. 

  0 0

  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Ubungo leo jijini Dar es Salaam.   
   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba akikata keki maalum kuashiria uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kampuni ya TTCL yazinduwa kituo cha huduma kwa wateja Ubungo.
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba akilishwa keki na Mkuu wa Biashara wa TTCL kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwakalebela wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha huduma kwa watejaa engo la Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo.

  Na Mwandishi Wetu.
  KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imezinduwa kituo kipya cha huduma kwa wateja kilichopo katika Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, kituo kitakacho toa huduma kwa wateja mbalimbali wa kampuni hiyo pamoja na wananchi wengine wanaoitaji huduma za TTCL.

  Akizinduwa kituo hicho, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alisema uzinduzi huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2016, ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wateja kutumia huduma za kampuni hiyo na kuchangia maendeleo ya kampuni hiyo na taifa kwa ujumla.

  Kindamba alisema uzinduzi wa kicho hicho cha huduma kwa wateja hasa wa eneo la Ubungo ni sehemu ya mpango wa TTCL katika kuboresha vituo na maduka yake nchi nzima ili yaweze kutoa huduma bora na kwa ufanisi zaidi. Alisema kutokana na mahitaji ya wateja, TTCL imedhamiria kuongeza idadi ya vituo hivyo pamoja na maduka yake ikiwa ni mpango wa kusogeza zaidi huduma kwa wateja maeneo anuai.

  "Kituo hiki cha huduma kwa wateja cha Ubungo ambacho kinazinduliwa leo, kitahudumia wateja kutoka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Eneo hili la Ubungo ni lango la kuingia katikati ya jiji huku maeneo yanayozunguka yakiwa na idadi kubwa ya watu, hivyo tunategemea kupata wateja wengi wanaoingia jijini Dar es Salaam pamoja na wanaoishi maeneo ya jirani ikiwemo Sinza na Mabibo..," alisema.

  Aidha aliongeza kuwa kutokana na maboresho makubwa ambayo kampuni hiyo ya kizalendo imeyafanya imejipanga kufanya kazi kwa ufanisi na kutekeleza falsafa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya 'Hapa Kazi Tu, huku ikitumia rasilimali za nchi vizuri na kuchangia mageuzi yanayoendelea nchini ya kuifanya Tanzania kupiga hatua kuelekea nchi ya uchumi wa kati na nchi ya viwanda.

  Kituo hicho kipya kitatoa huduma mbalimbali zikiwemo kuunganisha wateja wa huduma za intaneti, kurejesha namba iliyopotea, kufanya malipo ya ankara za huduma za TTCL, kusajili namba za simu za 4G, kuuza muda wa maongezi, kuuza modemu zenye ofa kabambe, kupata Routers na kuunganishwa na huduma za T-TV inayowezesha wateja kutazama matangazo ya vituo vya luninga moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi na vifaa vingine vya kisasa vya mawasiliano.   

  0 0

  MKURUGENZI wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, amewataka wateja wa benki hiyo ndani na nje ya nchi kutumia vema fursa ya kutoa maoni ya namna ya kuboresha huduma ndani ya benki hiyo.

  Mwambapa alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua wiki ya huduma kwa wateja Duniani, ambako alizinadi Akaunti mbili za Dhahabu na Thamani, ambazo zimetajwa kuwa na faida na riba kubwa kwa wateja watakaofungua na kuzitumia.

  Alibainisha ya kwamba benki yake imejipanga kupokea maoni yote kutoka kwa wateja ambayo yatachakatwa na kufanyiwa kazi ili kuboresha huduma zao kwa wateja ambao ndio mhimili mkuu wa mafanikio ya CRDB.

  “Maazimio yetu mwaka huu yako chini ya kauli mbiu isemayo: Tunasikiliza, Karibu, Tukuhudumie. Matarajio yetu ni kuona wateja wakiibeba na kuitumia kauli mbiu hiyo kwa ustawi wa huduma za kibenki tunazowapatia,” alisema.

  Aliongeza ya kwamba, benki yake imetumia takribani miaka mitano katika kuiweka kwa vitendo kauli mbiu ya CRDB isemayo: Benki Inayomsikiliza Mteja, hivyo sasa ni wakati wa kupokea mrejesho kutoka kwa wateja juu ya wapi wanakopaswa kuboresha.
  Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay (kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa na wa pili kushoto ni Mdhibiti wa tawi la Azikiwe, Bertha Mwakibete.
  Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la PPF Tower, Cornell Meseyeck wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
  Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay akisalimina na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi (kulia), wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la PPF Tower, Cornell Meseyeck wa pili kulia.


  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Taifa Najma Mwita Giga akizungumza na viongozi wa CCM mkoa Magharibi Kichama baada ya kuzindua Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa Magharibi, Mwera.

  Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Najma Mwita Giga akizungumza na viongozi wa CCM na Jumuiya ya Wazazi baada ya kuzindua Ofisi ya Jumuiya hiyo Mkoa Magharibi Mwera.
  Viongozi waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Najma Mwita Giga wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Jumuiya hiyo mkoa wa Magharibi.

  Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Najma Mwita Giga akimkabidhi Komputer na Printer Katibu Mkuu wa Wazazi wa Mkoa wa Magharibi kichama Mohd Abdi baada ya kuzindua Ofisi ya Jumuiya hiyo huko Mwera. Picha na Salmin Said Nasor/Maelezo Zanzibar.

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi katika viwanja vya Mwambisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa Mkoani humo. Naibu Waziri Makani ametoa wito kwa wananchi kutumia vizuri fursa ya maeneo ya misitu yaliyotengwa kwa shughuli za ufugaji nyuki kwenye ukanda wa wazi (buffer zone) kwa kutundika mizinga mingi na siyo kutumia maeneo hayo kwa shughuli nyingine za uharibifu wa mazingira kama uchomaji mkaa kwa kuwa kufanya hivyo kutasadia uhifadhi wa misitu na kuongeza uzalishaji bora wa mazao ya nyuki. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (wa pili kushoto).
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati) akizindua Manzuki ya Makonga katika shamba la Miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa yaliyofanyika Wilayani humo. Manzuki hiyo itatumiwa kama shamba darasa la kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa nyuki kwa njia za kisasa zitakazowezesha kuzalisha mazao bora ya nyuki. Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (wa pili kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Daniel Isala (kushoto).
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akitundika mzinga wa nyuki katika shamba la Miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa Wilayani humo. Kushoto anaeshiriki nae ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana na kushoto kwa Mkuu wa Wilaya ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
  Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto) akikagua miche ya miti katika shamba la miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa yaliyofanyika Mkoani humo. Shamba hilo lina jumla viriba vya miti milioni moja kwa ajili ya kupandwa katika shamba hilo na maeneo mengine nchini. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kushoto).


  0 0

  UONGOZI wa klabu ya Yanga umetuma barua ya maomb kwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Visiwani Zanzibar kuomba kutumia  Uwanja wa Amani kwa ajili ya michuano yao mbalimbali na kuutumia kama uwanja wao wao wa Nyumbani.
  Na Zainabu Nyamka, Globu ya Jamii.

  HATUA hiyo imekuja baada ya Serikali kuzifunia timu za Yanga na Simba kutumia Uwanja wa Taifa kutokana na vurugu zilizotokea Oktoba 01 kwenye mechi ya Ligi kuu ya Vodacom timu hizo zilipokutana na kusababisha kungolewa kwa viti na kuvunjwa kwa geti la kuingilia na mashabiki wa pande zote mbili.

  Klabu ya Yanga imeandika barua hiyo na tayari imeshapokelewa na uongozi wa  Wizara husika visiwani Zanzibar, umeomba kutumia Uwanja huo kwa ajili ya mechi za ligi kuu na hata michuano ya Kimataifa itakapoanza.

  Katibu mkuu wa ZFA Khasim Haji Salum amesema kwamba kwa upande wao kama uongozi  umekubaliana na jambo hilo lakini maamuzi kamili ya kuruhusiwa uwanja huo ni jukumu la Serikali ambao wao ndio wenye mamlaka kamili.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema wametuma barua tayari na wana imani kuwa majibu watayapata kwa kuda muafaka kabisa kwani kuanzia wiki ijayo ligi  taendelea tena na wanataka kutumia Uwanja huo na benchi la ufundi limeridhia kutokana na hali halisi ya Uwanja ulivyo.

  Kutokana na maombi hayo, katika Kanuni za ligi kuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeweka wazi kanuni za ligi , “endapo timu yoyote haina uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mchezo wa ligi kuu inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au mkoa  jirani mkoa  wa timu husika ndani tya Tanzania bara ilimradi uwanja uwe na sifa zinazokubalika na uthibitishwe au kuidinishwa na TFF, baada ya uteuzi wa uwanja timu haitaruhusiwa kubadilisha uwanja  huo kinyume na sababu za kikanuni”.

older | 1 | .... | 1378 | 1379 | (Page 1380) | 1381 | 1382 | .... | 3272 | newer