Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS WA CUBA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa amewasili jioni hii katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa atafanya ziara ya kikazi ya siku Tatu hapa nchini na lengo la ziara hiyo ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya, utamaduni,michezo,kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.

Tarehe 3/09/2016 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba atakutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa pia atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu na baada ya mazungumzo hayo ya faradha viongozi hao watafanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo MBILI.

Nchi nyingine ambazo Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba anazitembelea ni Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo- DRC-,Botwana na Zimbabwe.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzanai Mhe.Samia Suluhu Hassan (kulia), akiwa na mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu hapa Nchini.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa akiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa akiangalia moja ya kikundi kilichokuwa kinatumbuiza kwa matarumbeta mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalaam ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

Timu za soka za Simba na Yanga zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

$
0
0
Timu za soka za Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa miumbombimu ya Uwanja  wa Taifa yakiwemo mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.
Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akikagua na kutembelea maeneo yalioathirika na uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba na Yanga katika mechi iliyochezwa Octoba Mosi 2016 katika Uwanja wa Taifa.
“Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki kuvunja mageti na kung’oa viti na sisi kama Serikali tumeamua kuzuia vilabu hivi vya Simba na Yanga kutotumia Uwanja wa Taifa mpaka tuitavyoamua vinginevyo hapo baadae” Alisistiza Mhe. Nnauye.
Mhe. Nape Nnauye ameongeza kuwa wameendaa mfumo wa kutumia kamera Uwanjani ili kubaini makosa yatakayokuwa yanafanyika ili kuzuia vitendo vya kihualifu na uharibifu katika Viwanja vya michezo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa wamesikitishwa sana na uharibifu ulitokea katika mechi ya Simba na Yanga na kusababisha uharibifu wa viti na mageti ya kuingilia Uwanjani.
Ameongeza kuwa kwa tathimini iliyofanyika mageti manne yameng’olewa na mashabiki kwa upande wa Simba na Yanga na pia kwa upande wa ndani jumla ya viti 1781 vimeng’olewa katika upande wa mashabiki wa Simba.
“Mara nyingi tumekubaliana kutunza Uwanja huu kwa ajili ya matumizi ya watanzania wote na kama wasimamizi tunasikitika kwa kitendo hiki kilichotokea na tujue kuwa ni kodi za wananchi ndio zilitumika kujenga Uwanja huu na pia ndizo zitazotumika kukarabati Uwanja tuwe na tabia ya kupenda na kutunza vya kwetu.
Klabu za Simba na Yanga zimekuwa na ushindani mkubwa katika soka la Tanzania na kumekuwa kukitokea mambo mbalimbali pale timu hizo zinapokutana ikiwemo uharibifu wa miundombinu katika Viwanja na vurugu kwa mashabiki pale mmoja wao anapofungwa.

 Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akiwa amekaa akiangalia jinsi viti vilivyong’olewa katika Uwanaja wa Taifa na Serikali   kuchukua uamuzi wa kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa na kuzuia mapato ya mechi waliyocheza mpaka watakapolipa fidia  kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.

Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na Serikali kufikia  uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.

 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimini iliyofanyika mara baada ya mechi wa jana kati ya Simba na Yanga na jumla ya mageti manne yamevunjwa na viti1781 vimeong’olewa katika Uwanja wa Taifa.
  Eneo liliong’olewa viti katika Uwanja wa Taifa katika mechi ya Simba na Yanga iliyofanyika Oktoba Mosi. 
Habari na Picha na Raymond Mushumbusi - MAELEZO

BOHARI KUU YA DAWA ZANZIBAR YAGAWA DAWA KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA

$
0
0
Na Ramadhan Ali/Maelezo Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itahakikisha kwamba Hospitali na Vituo vyote vya afya vinapatiwa dawa zote muhimu kwa ajili ya wananchi.

Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamada amesema Serikali tayari imeidhinisha shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya kununulia dawa na Wizara imeshatumia shilingi milioni 600 kununua dawa ambazo zitatosha katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Serikali imetenga shilingi bilioni tano kwa ajili ya kununulia dawa ambazo zinakidhi mahitaji ya wananchi katika kuendeleza azma ya Serikali ya kutoa huduma za afya kwa wananchi bila malipo.

Akisambaza dawa hizo katika Hospitali na vituo vya afya, Zahran amewaeeleza wafanyakazi kuwa Serikali imetumia fedha nyingi kununua dawa hivyo amewataka kuzitunza na kuwapa wananchi kwa mujibu wa mahitaji yao.

“Hakuna haja ya kuweka akiba dawa wapeni wananchi, dawa zipo zakutosha na utaratibu wa kuagiza nyengine umeshaanza, ”alisisitiza Mkurugenzi wa Bohari Kuu.

Alisema Wizara itaandaa utaratibu wa kufuatilia matumizi ya dawa hizo ili kuhakikisha zinawafikia wananchi na amewashauri viongozi shehia na wananchi kwa jumla kuwa walinzi wa dawa hizo.

Daktari Msaidizi wa Hospitali ya Makunduchi Dkt. Asha Salum Hassan amesema hali ya dawa hivi sasa inaridhisha na dawa nyingi muhimu zinapatikana isipokuwa dawa za maumivu na Anti biotic zinatumika kwa wingi hivyo baadhi ya wakati zinakwisha bila ya kuingizwa nyengine. Ameahidi kuwa dawa hizo zitatumika kama zilivyokusudiwa kwa ajili ya wananchi na atahakikisha kuwa hakutatokea ubadhirifu wowote ulio nje ya utaratibu uliopangwa na Wizara.
 Muonekano wa nje wa Bohari Kuu ya dawa Zanzibar iliyopo maeneo ya Marughubi nje kidogo ya Mjini wa Zanzibar. 
 Shehena ya dawa zilizoagizwa na S erikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zikiwa zimehifadhiwa kwenye Bohari kuu Maruhubi kabla ya kusambazwa katika hospitali na vituo vya Afya.
 Wafanyakazi wa Bohari kuu wakisambaza dawa katika Hospitali ya Wilaya Makunduchi ikiwa ni jitihada za serikali kuwapatia wananchi huduma hiyo bila malipo .
Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad akimkabidhi dawa  Daktari msaidizi wa Hospitali ya Wilaya  Makunduchi Asha Salum Hassa (wa pili kulia) kwa ajili ya Hospitali hiyo.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

WAZIRI MKUU ABAINI GYPSUM ZA NJE HAZITOZWI KODI

$
0
0
gyp2
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua  uzalishaji katika kiwanda  cha Gypsum cha Premalt cha mjini Dodoma wakati alipokitembelea Oktoba 2, 2016. (Picha na ofisi ya Wairi Mkuu)


*Aahidi kufuatilia suala hilo, asema lazima zitozwe kodi kulinda soko la ndani.*Apokea mchango wa sh. milioni moja kwa ajili ya waliopatwa na maafa Kagera

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atafuatilia ili ajue chanzo ni kwa nini bidhaa za gypsum zinazoagizwa kutoka nje ya nchi hazitozwi kodi.

Waziri Mkuu ametoa ahadi hiyo jana jioni (Jumapili, Oktoba 2, 2016) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa kiwanda cha Premalt Limited kinachotengeneza unga wa gypsum (gypsum powder) aina ya Afri Bond mara baada ya kukagua kiwanda hicho kilichopo Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Waziri Mkuu alisema: “Gypsum inayozalishwa Dodoma ina ubora kama ile inayozalishwa Mchinga, kule Lindi na hakuna gypsum yenye ubora kama huo hapa Afrika isipokuwa gypsum ya Tanzania.”

“Nilikuwa sielewi ni kwa nini gypsum ya wenzetu ilikuwa inakimbiliwa, lakini sasa nimetambua; ilikuwa na bei nafuu kwa sababu tumetoa kodi. Sasa hivi, hili jambo nalibeba, naenda kulishughulikia”.

“Nimeangalia kwenye orodha niliyopewa katika madini yote nimekuta kodi ya gypsum ni asilimia sifuri. Ni lazima tuweke kodi ili tutengeneze soko zuri kwa gypsum inayozalishwa hapa nchini. Ni lazima tuweke kodi kwenye madini yetu mengine kama makaa ya mawe ili tutengeneze soko zuri,” alisema.

Alisema wakazi wa Dodoma wamepata fursa kutokana na uwepo wa kiwanda kama hicho kwani kiwanda kinahitaji mali ghafi kwa hiyo ni jukumu la wakazi wake kuchangamkia fursa ya uchimbaji wa madini hayo.

“Natambua kwamba Mkurugenzi wa kampuni hii ataleta mitambo mikubwa zaidi hivi karibuni. Nendeni benki mkakope ili muweze kununua zana za kuchimbia madini haya. Yeye ukishafikisha hapa, ananunua ili aanze kusaga na kupata unga wa gypsum,” alisema.

Alitumia fursa hiyo pia kumpongeza mmiliki wa kampuni ya STJ Enterprises, Bi. Adella Nungu ambaye ni mmoja wa wajasiriamali wa Kitanzania wanaotumia gypsum kutoka Dodoma na kutengeneza mapambo mbalimbali ya kuezekea ndani ya nyumba. Bi. Nungu alikuwepo kiwandani hapo.

Bi. Nungu alisema anaponunua unga wa gypsum kutoka Dodoma, kwa wastani anaweza kutengeneza bidhaa za tani 20 hadi 25 kwa mwezi kutegemea na hali ya soko na oda kutoka kwa wateja wake.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


WAZIRI UMMY MWALIMU AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKA LA ENGENDER HEALTH.

$
0
0
 Mwakilishi Mkazi wa shirika la linaloshughulika na masuala ya Afya ya Uzazi na  Uzazi wa mpango kwa Wanawake na Wasichana  la EngenderHealth Richard Killian( katikati) akizungumza na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,jinsia,Wazee na Watoto mapema leo kwenye ofisi ya waziri huyo,Kushoto ni Rais na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo bi. Ulla Muller na kulia ni Waziri Ummy Mwalimu.
  Rais na Mkurugenzi wa EngenderHealth Bi. Ulla Muller (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo wakati alipomtembelea waziri wa afya na kuzungumza mikakati yao katika upande wa afya,rais huyo atatembelea Mkoa wa Manyara.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy mwalimu akiongea na Rais pamoja na Mwakilishi mkazi wa Shirika la EngenderHealth walipomtembelea ofisini kwakwe. Waziri Ummy amesema hivi sasa asilimia 27 ya wanawake wa Kitanzania ndio wanaotumia njia za uzazi wa mpango ambapo serikali ilijiwekea malengo mwaka 2012 kwamba ifikapo mwaka 2020 ifikie asilimia 50 ya matumizi ya njia ya uzazi wa mpango.

MKURUGENZI ARUSHA AFAFANUA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA JENGO LA UTAWALA KALIUA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha, Athumani Kahamia ametoa ufafanuzi kuhusu tuhuma ya matumizi mabaya ya fedha kiasi cha sh, 500 milioni zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya Kaliua na kusema kwamba fedha hadi anahamishwa fedha hizo hazikuwahi kuletwa katika halmashauri hiyo kutoka serikali kuu.

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma mbalimbali zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini ambapo Kahamia anatuhumiwa kutumia kiasi hicho cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya Kaliua wakati akiwa mkurugenzi wa Kaliua kabla ya kuhamishiwa jijini Arusha.

Akihojiwa na mwandishi Wa Habari hizi Kahamia alisema kwamba aliripoti mnamo febuari 2015 katika halmashauri hiyo na kukuta ujenzi wa jengo la utawala ukiendelea ambapo katika bajeti ya halmashauri ya Kaliua mwaka wa fedha 2015/16 waliomba fedha hizo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo katika awamu ya kwanza lakini serikali haikuleta pesa hizo.

Alisema ya kwamba lakini pamoja na kutenga bajeti ya fedha hizo halmashauri hiyo haikupokea kiasi hicho kutoka serikali kuu na kusisitiza kwamba hadi anaondoka Kaliua fedha hizo hazikuwahi kuzipokea.

"Hadi tarehe 30 juni mwaka huu hizo fedha tulikuwa bado hatujazipokea mpaka leo tunavyoongea hizo fedha hazijapokelewa taarifa kwamba nimezitafuna zinalenga kunichafua "alisema Kahamia

Hatahivyo, alifafanua tuhuma kwamba tayari ameandikiwa barua ya kurudishwa Kaliua ili kujibu tuhuma zinazomkabili na kusema si kweli kwani hadi sasa hajapokea barua yoyote wala wito kutoka mamlaka yoyote kumtaka arudi kujibu madai hayo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Rais Magufuli amthibitisha Prof. Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

WATEJA WA BENKI YA CRDB TAWI LA WATER FRONT WALA KEKI PAMOJA NA KUADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Keki ya Kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa wateja ya benki ya CRDB tawi la Water Front.
Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo akikata keki kwa niaba ya wateja wa tawi la Benki ya CRDB tawi la Water Front wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Water Front jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front, Donath Shirima akimlisha keki Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo.

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA CUBA, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Makamu wa Rais wa Cuba,Salvador Valdes Mesa kabla ya kuanza mazungumzo yao leo katika hotel ya Hyatt, Kilimajaro Kempiski jijini Dar es Salaam, leo.Kulia ni Msemaji wa CCM Christopher Ole SendekaKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa , leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Bashir Nkoromo

Tshs. Bilioni 374.5 zatolewa kwa ajili mikopo ya nyumba nchini

$
0
0
Na Jonas Kamaleki, MAELEZO

Shilingi bilioni 374.5 zimetolewa kwa ajili ya mikopo ya nyumba hapa nchini ili kuwawezesha wanachi kuwa na makazi bora ambayo ni haki ya msingi ya kila mwanadamu.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani.

“Ili kukidhi mahitaji ya nyumba yanayotokana na ongezeko kubwa la watu, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeshiriki katika utoaji wa mikopo ya nyumba ambapo soko la mitaji na mikopo ya nyumba nchini limeongezeka na kufikia asilimia 6.7 kwa mwaka jana,”alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, taarifa za Benki Kuu zinaonyesha kuwa idadi ya benki zinazotoa mikopo ya nyumba zimeongezeka kutoka tano kwa mwaka 2010 hadi kufikia 26 Desemba 2015.

Aidha. Lukuvi amesema kuwa utoaji wa mikopo ya muda mrefu ya nyumba umewezesha sekta binafsi na waendelezaji milki kuingia katika biashara ya kujenga na kuuza nyumba za biashara na makazi kwa kuwauzia wananchi kwa mkopo wa muda mrefu.

TASAF yakutana na Wadau wa Maendeleo

$
0
0
Wadau wa Maendeleo wanaoshirikiana na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN- wameanza mkutano jijini Dar es salaam kupitia mafanikio ya utekelezaji wa Mpango huo.

Akifungua Mkutano huo wa siku moja, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo amesema Serikali inathamini na kutambua mchango wa wadau hao wa maendeleo katika kusaidia jitihada za kutokomeza umaskini miongoni mwa wananchi.

Bwana Ilomo amesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF umekuwa wa mafanikio ya kuridhisha ambapo Zaidi ya kaya maskini Milioni Moja zimetambuliwa na kuorodheshwa kwenye Mpango huo nchini kote.

Aidha Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais amebainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa Mpango huo serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake ili malengo yake yaweze kupatikana kwa haraka na kuwanufaisha walengwa na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Bwana Ilomo amezungumzia hatua zilizoanza kuchukuliwa dhidi ya watu waliopenyezwa kwenye Mpango bila kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuziondoa takribani kaya 30,000 zilizokuwa zimeandikishwa kinyume cha kanuni za Mpango.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko huo umefanikiwa kulipa walengwa wa Mpango kwa awamu 17 nchini kote ambako katika maeneo mengi ya Mpango tayari mafanikio yameanza kuonekana ikiwemo walengwa kuboresha maisha,kusomesha watoto na hata kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwa lengo la kujiongezea kipato.

Wadau hao wa Maendeleo kesho watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini na kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kuona namna wanavyonufaika na ruzuku itolewayo na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF. 

Zifuatazo ni picha za tukio la ufunguzi wa mkutano wa TASAF na wadau wa Maendeleo uliofunguliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akifungua mkutano wa wadau wa maendeleo ulioandaliwa na TASAF. 
    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akizungumza na wadau wa Maendeleo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wadau wa maendeleo na watendaji wa TASAF wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa wadau awa maendeleo jijini Dar es salaam iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo( hayupo pichani). 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akitoa maelezo kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo jijiji Dar es salaam . 
 Wadau wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo baada ya ufunguzi wa Mkutano wenye lengo la kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini .

 Wadau wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo baada ya ufunguzi wa Mkutano wenye lengo la kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini .

DK KIJAJI: WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WASIINGILIWE, WAHESHIMIWE.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji katika mahafali ya saba yaliofanyika Oktoba Mosi katika viwanja vya Bodi jijini Dar es Salaam. 
Na Ismail Mohamed.
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amewataka Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wasiingiliwe katika taaluma zao na kwamba wanapaswa kuheshimiwa ili waweze kutoa huduma bora.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri huyo kwenye mahafali ya saba yaliofanyika Oktoba Mosi katika viwanja vya Bodi jijini Dar es Salaam.

Dk Kijaji amesema Serikali ya Awamu ya Tano, haitamvumilia mtu yeyote atakayetumia elimu aliyoipata kwa gharama za walipa kodi kwa kufanya kazi kwa manufaa binafsi  na kufuja mali za umma.

“Fani hii ina tija na ina mchango mkubwa katika taasisi husika na taifa kwa ujumla, Fani hii inapaswa kupewa heshima yake Kama vile wataalamu wa fani zingine wasivyoingiliwa katika utendaji wao, hivyo basi naagiza kuwa wataalamu hawa nao wasiingiliwe kwenye utendaji wao wa kitaaluma. Kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na ukiukaji wa sheria namba 23 ya mwaka 2007 na pia inawanyima wasifanye kazi zao kwa uhuru na kufuata misingi ya sheria na taaluma.

“Yeyote atakayepatikana akikiuka maadili ya kazi atachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweka fundisho kwa wengine na kuimarisha nidhamu katika utumishi wa umma. Mnapaswa kusoma kwa makini, Sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 na kanuni zake iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 ili kujua madhara ya kukiuka taratibu za ununuzi,” amesema Dk Kijaji.

Naibu waziri huyo amewataka wahitimu hao kutatua matatizo ya manunuzi holela na kuepuka kuingia kwenye mikataba mibovu ya ununuzi. 

Pia, amewataka wahitimu hao kuepuka vitendo vya rushwa katika ununuzi na ugavi kwani sheria zipo na kwamba zitatumia kuwabana endapo hawatazingatia sheria za ununuzi na ugavi. 
“Itakuwa ni aibu kwa fani hii ikiwa mtaalamu mmoja atabainika kuhusika na vitendo vya rushwa . Nawasihii sana, zingatieni kanuni za maadili mlizopewa  leo,”amesema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi, Dk Hellen Bandiho amesema mahafali hayo ni ya saba tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo na kwamba bodi hiyo inaendelea kusimamia na kukuza fani ya ununuzi na ugavi nchini.

Dk Bandiho amesema kuwa kati ya watahiniwa 81,771 waliofanya mitihani, 27,814 wamefaulu. Pia, amesema kwamba mafunzo yanayotolewa na bodi hiyo yamekuwa yamekuwa yakifanyiwa mapitio mara kwa mara na kurekebishwa ili kuhakikisha kwamba mafunzo yanayotolewa yanakidhi mahitaji ya sasa.

“Bodi kwa kushirikiana na vyuo vya mafunzo ya elimu ya juu imehimiza kuanzisha mafunzo mathubuti yanayohusu fani ya ununuzi na ugavi vyuoni ambapo zaidi ya vyuo 20 hapa nchini hivi sasa vinatoa shahada ya kwanza ya taaluma ya ugavi na baadhi shahada ya pili nay a tatu. Hatua hii inawezesha fani yetu kupata wataalamu wenye ubora wa juu kielimu,” amesema Dk Hellen Bandiho.

Katika mahafani hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa bodi hiyo ina jukumu la kuwasajili wataaluma na kuratibu mienendo ya wanataaluma kupitia miongozo ya maadili, mafunzo endelevu , kuwapa leseni wanataaluma wanaokidhi matakwa na kaguzi za kitaaluma.

“Katika kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi Juni 2016, Bodi imedahili na kuendesha mitihani ikiwa ni moja ya jukumu lake kisheria kwa wanafunzi3,327 katika ngazi za cheti cha awali, Cheti Msingi na Shahada ya ununuzi na ugavi ambapo kati yao 1,754 wamefaulu katika ngazi mbalimbali,” amesema Mbanyi.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA CUBA, IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha na kuongeza uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kwa manufaa ya wananchi wake.


Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amesema anatambua uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Cuba na kwamba Serikali yake imejipanga kuhakikisha uhusiano huu unaelekezwa katika maeneo yenye manufaa ya kiuchumi na ustawi wa jamii.


Rais Magufuli amemuomba Makamu huyo wa Rais wa Cuba kuwashawishi wawekezaji wa kutoka nchini mwake kuja hapa nchini kujenga viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu ili kurahisisha upatikanaji wa dawa na kupunguza gharama.


Pia, Rais Magufuli amemuomba Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa kuwashawishi wafanyabiashara wa Cuba kuja kuwekeza katika uzalishaji wa sukari na amewahakikishia kuwa wakiwa tayari Serikali ya Tanzania ipo tayari kuwapa ardhi kwa ajili ya kuendesha uzalishaji huo.


"Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa najua kuwa nchi yenu ina utaalamu wa kutosha katika uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa dawa za binadamu na masuala mengine mengi yanayohusu matumizi ya teknolojia katika shughuli mbalimbali za uzalishaji, nakuomba uwaambie wafanyabiashara wa Cuba kuwa tunawakaribisha waje Tanzania kuwekeza na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha"amesema Rais Magufuli.


Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali yake katika kuinua uchumi wa Tanzania na amemhakikishia kuwa Cuba ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa kutumia utaalamu na uzoefu wake.


Amesema kwa kuanzia Cuba italeta wataalamu kwa ajili ya kuangalia namna itakavyotekeleza ombi la kujenga viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu na pia atazungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Cuba na kuwashawishi kuja hapa nchini kuwekeza katika uzalishaji wa sukari.


"Mhe. Rais Magufuli natambua kuwa uhusiano wetu na Tanzania na Afrika ni wa kihistoria, sisi Cuba tumepiga hatua kubwa katika maendeleo ya uchumi na teknolojia, nimekuja kukuhakikishia kuwa tutauendeleza uhusiano huu ili ulete manufaa kwenu na kwa wananchi wa Cuba" amesema Mhe. Mesa.



Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

03 Oktoba, 2016
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa (kulia kwake) na ujumbe wake alipokutana nae Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016. Makamu wa Rais wa Cuba, yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu yenye lengo la kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, utamaduni, michezo, kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.
Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia walioketi) akiwa na mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa (wa tatu kushoto walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wao, mara baada ya mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya kuchora Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Valdes Mesa kabla ya kumkabidhi kama zawadi Ikulu.

Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Valdes Mesa akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

NMB yazindua Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya NMB, imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani kwa kuahidi muendelezo wa huduma bora kwa wateja na kupokea ushauri kutoka kwa wateja na wadau, huku ikisisitiza utayari katika kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika NMB Tawi la Msasani, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, amesema licha ya kuwa huduma bora ni kipaumbele cha kila siku, lakini wataitumia wiki hii kuboresha zaidi, ikiwamo kufanyia kazi maoni ya wateja.

Ineke amesema kwamba, kutokana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Magufuli, ya kuigeuza Tanzania kuwa ya viwanda, benki yake iko tayari kuendana na kasi ya mchakato huo, ambao unategemea sana ubora huduma za kibenki.

Ineke ameongeza , benki yake imekuwa kinara nchini sio tu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja, bali pia huduma bora za kijamii kwa ujumla, ambako imekuwa ikichangia katika sekta zote, zikiwemo za afya na elimu.

Aidha, katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, NMB imepanga kufanya ziara katika Kituo cha Kulelea Wazee kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambako pamoja na mambo mengine, watatoa msaada na kuhudumu kwa wazee waliopo kambi hiyo.

Ineke amewataka wateja wa NMB kuwa sehemu ya maendeleo ya benki hiyo kwa kutoa maoni yatakayoongeza kasi ya huduma bora, huku akiahidi kuyafanyia kazi maoni yote ya maboresho yatakayotolewa na wateja wao nchini kote.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker(Wapili kutoka kushoto) akizungumza na wateja waliofika asubuhi katika tawi la NMB Msasani na kuwaelezea malengo yao ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akimkabidhi Godliver Mwendo cheti cha mfanyakazi bora wa benki hiyo katika uzinduzi a wiki ya huduma kwa mteja tawi la Msasani Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tawi la NMB Msasani katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja leo Jijini Dar es salaam.

HASSANOO, KABURU WAULA TENA CHAMA CHA SOKA MKOA WA PWANI COREFA

$
0
0
NA VICTOR  MASANGU, MKURANGA 

CHAMA cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) kimepata safu mpya ya uongozi wataoongoza kwa kipindi cha miaka minne ambapo katika   nafasi ya mwenyekiti imekwenda kwa Hassan Hasanoo  baada ya kuchaguliwa kwa kishindo na wajumbe wa mkutano  mkuu uliofanyika katika ukumbi wa kiguza Wilayani Mkuranga.

Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa unasubiliwa kwa hamu na shauku kubwa na wadau wa mchezo wa soka ulihudhuriwa  na viongozi wa serikali,viongozi wa michezo kutoka wilaya mbali mbali za Mkoa wa Pwani, waangalizi kutoka shirikisho la soka Tanzania (TFF) wakiongozwa na mkurugenzi wa sheria na wanachama  Eliud Mvella.

Hassanoo ambaye hapo awali alikuwa katika nafasi hiyo ya mwenyekiti ameweza kutetetea kiti hicho kutokana na kuwa mgombea pekee aliyowania nafasi hiyo  baada ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi kumpigia kura za ndiyo zipatazo 22 katika ya kura 24 zilizopigwa huku akipigiwa kura mbii za hapana.

Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa Chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) Masau Bwire alisema kuwa nafasi ya Mwenyekiti imenyakuliwa na Hassan Hasanoo aliyepata kura 22 za ndiyo, huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikichukuliwa na  Shabani Kangale(Macho kodo) kutoka Wilayani Bagamoyo kwa kujipatia kura 14 dhidi ya mpinzani wake Said Baiza alipata kura tisa.

Kinyang’anyiro kingine  katika uchaguzi huo kilikuwa katika nafasi ya katibu mkuu, ambapo kulikuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na wagombea wote watatu waliokuwa wanaomba kura kuonekana kila mmoja kuwa na dalili za kuondoka na ushindi hivyo kuonekana muda wote wakiwa wana haha uku na kule.

Uchaguzi wa nafasi hiyo ya ukatibu mkuu ilibidi urudiwe kwa mara ya pili kutokana na wagombea wawili kupata kura sawa,ambapo  Robert Mnisi alipata kura (8) Abubakari alawi kura (8) huku aliyewahi kuwa  katibu  mkuu wa  zamani  COREFA Riziki Majala akipata kura 7, hivyo ikamlazimu Mwenyekiti wa uchaguzi kutangaza kurudia upya katika nafasi hizo mbili.

Baada ya uchaguzi huo kurudiwa tena  kwa  mara  nyingine , matokeo yaliweza kubadilika na kuacha midomo ya watu wazi kutokana na mwenendo mzima ulivyokuwa, ambapo Abubakari Alawi aliweza kupata kura 16 na kutangazwa rasmi kuwa katika mkuu, huku mpinzani wake wa awali  Robert Mnisi akipata kura 6 tu huku nafasi ya katibu msaidizi ikienda kwa Godfrey Haule kwa kupata kura 17 za ndiyo.


Katika nafasi ya Mweka hazina alichaguliwa Bernad Yomba Yomba kwa kupata kura 19 za ndiyo, wakati nafasi ya msaidizi wake ikinyakuliwa na Mohamed  Lubondo aliyejizolea kura 21 za ndiyo,kutoka kwa wajumbe wa mkutano  mkuu wa uchaguzi huo.


Makamu wa Rais wa klabu ya soka ya  Simba Godfrey Nyange (Kaburu) aliweza kuitetea nafasi yake ya mwakilishi wa mkutano mkuu wa TFF, baada ya kuweza kupata kura 21 za ndiyo, ambapo Juma Kisomo kutoka visiwani mafia aliweza kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa klabu Mkoa baada ya kupata kura zote 24 za ndiyo.

Kwa wa nafasi za wajumbe wa kamati ya utendaji ya COREFA,zilinyakuliwa na Mohamed Mbaruku kura (21) Shaban Mawingu (22) pamoja na mwamuzi mstaafu wa ligi kuu ya Tanzania bara Saimon Mberwa aliyepata  kura zote 24,huku nafasi maalumu ya mjumbe katika soka la wanawake ikinyakuliwa na Frorence Ambonisye kwa kupigiwa kura 23 za ndiyo.

 Mwenyekiti mpya wa Corefa Hassan   Hassonoo (mpiganaji) mara baada ya kutangazwa mshindi alitoa pongezi kwa wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumchagua tena na kuwahakikishia kwamba atashirikiana nao bega kwa bega katika kuleta mabadiliko chanya katika  kukuza mchezo wa soka katika Mkoa wa Pwani kuanzia ngazi za chini kwa kuanzisha ligi za vijana wadogo .

Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo mkuu Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Corefa Masau Bwire aliweza kutumia fursa katika mkutano huo  kutangaza rasmi kustaafu na kuachia nafasi hiyo kutokana na kuchukizwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimfanyika fitina , chuki na vitisho  katika kutimiza wajibu wake kulingana na kufuata  kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa.

VODACOM TANZANIA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

$
0
0
 Afisa Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Lwakatare akiongea na baadhi ya wateja waliofika kupata huduma mbalimbali katika duka la kampuni hiyo lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.

 Baadhi ya wateja wa Vodacom Tanzania waliofika kupata huduma mbalimbali katika duka la kampuni hiyo lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo wakichukua keki kutoka kwa Afisa Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Lwakatare(kushoto) ikiwa ni sehemu ya kufurahia kwa pamoja kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
 Mmoja wa wateja wa Vodacom Tanzania aliyefika kupata huduma mbalimbali katika duka la kampuni hiyo lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo akifurahi jambo wakati alipokuwa akipewa keki  na Afisa Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo,Harriet Lwakatare(kulia) ikiwa ni sehemu ya kufurahia kwa pamoja kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.

Baadhi ya maafisa waandamizi wa Vodacom Tanzania,wakiwa wamebeba keki tayari kwa kuwagawia wateja  na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kufurahia kwa pamoja kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.

PROF. MBARAWA AITAKA TTCL KUTAFUTA WATEJA.

$
0
0
 Msimamizi wa masuala ya TEHAMA Bw. John Chorai (kulia), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), namna kifaa cha kurekodia malipo kinavyofanya kazi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam. 
Mwakilishi wa Kibiashara kutoka Ubalozi wa Uingereza anayesimamia nchi ya Tanzania na Kenya Bw. Lord Hollick (wa pili kulia) akifafanua jambo  kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) wakati alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia masuala ya kuboresha miundombinu nchini. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Bi Sarah Cookie.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

UPELELEZI KINONDONI KUISHA NDANI YA SIKU SITINI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe akipokewa na mkuu wa kitengo cha Kuboresha usalama wa jamii ( DCP) Godluck Mongi alipokwenda kufungua mafunzo ya upelelezi kwa askari wa polisi 100. ( katika ni mkuu wa mafunzo wa Jeshi la Polisi DCP Ally Lugendo. Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha polisi kidatu yamefadhiliwa na Tasisi ya Hanns Sidel. Picha na Tamimu adam- Jeshi la Polisi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe( katikati) akiimba wimbo wa maadili wa ofisa wa Polisi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mafunzo ya upelelezi yanayofanyika katika chuo cha polisi kidatu. Mafunzo hayo kwa askari 100 yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns Sidel.
 (picha na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi)

Na. Tamimu Adam - Jeshi la Polisi
Mkuu wa mkoa wa Morogoro mhe. Dkt Kebwe Stevin kabwe amesema Jeshi la polisi Tanzania ni kioo kwa majeshi ya polisi yalipo Afrika mashariki na hata afrika kwa ujumla kutokana na umahili wake wa kutoa mafunzo mbalimbali ya uaskari kwa baadhi ya nchi zilizopo afrika mashariki .

Dkt Kebwe aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya miezi miwili ya upelelezi katika chuo cha Polisi kidatu yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Hanns Sidel kwa askari polisi 100 waliotoka katika mkoa wa kipolisi kinondoni ambalo wamechaguliwa kwa ajili ya kutekeleza kwa weledi mpango wa kuborewsha usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa huo wa kipolisi.

“Huwezi kwenda kujifunza katika nchi ambayo haifanyi vizuri, na ndioo maana nchi za jirani huja Tanzania kwa ajili ya kujifunza namna Jeshi la Polisi Tanzania linavyo weza kuimarisha usalama wa raia na mali zao” alisema Dkt Kebwe.

Aliwataka askari hao wanafunzi wa upelelezi kujifunza kwa makini ili kuboresha umahiri walionao katika kufanikisha upelelezi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kivitendo katika mkoa wa kinondoni kama eneo la mfano na hatimaye maboresho hayo yaweze kuenea na kutekelezwa katika mikoa yote nchini hivyo kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
Kusoma zaidi bofya HAPA.

MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI AMKABIDHI MHE. JAJI MKUU BENDERA YA TAIFA NA YA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  leo ofisini kwake jijini Dar salaam.

Na Mary Gwera, MAHAKAMA
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman amezitaka Wizara, Halmashauri na Taasisi nyingine za Serikali kutumia vielelezo vya Taifa kama bendera na nembo ya taifa katika ofisi zao ili kuenzi tunu na vielelezo vya Taifa.

Aliyasema hayo ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea rasmi bendera ya Taifa na Afrika Mashariki kutoka kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo.

Alisema kuwa  vielelezo hivi vya taifa vinalindwa kisheria kwa hiyo inabidi vipate heshima yake kwa kuwa vinawakilisha taifa.

“Sheria pia inavitambua vielelezo hivi hivyo ni muhimu vikapewa heshima yake, kwani hata mtu akichezea vitu hivi anaweza kufungwa kwa mujibu ya sheria,” alisisitiza Jaji Mkuu.

NSSF WACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA POLISI KILUVYA.

$
0
0
 Mkurugenzi wa NSSF, Godius Kahyarara akizungumza na waandishi wa habari katika makabidhiano ya hundi ya milioni 50 kwa jeshi la Polisi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni. 

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, CP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam baada ya kupokea hundi ya milioni 50 kutoka kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni.
 Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam  CP Simon Sirro akipokea hundi ya milioni 50 kutoka kwa  Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii  NSSF, Godius Kahyarara kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limechangia kiasi cha Milioni 50 kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni ikiwa ni katika kukabiliana na changamoto ya kukua kwa miji kwenda sambamba na ongezeko la uhalifu.

Akizungumza wakati wa kutoa hundi ya milioni 50, Mkurugenzi wa NSSF, Godius Kahyarara amesema kuwa huu ni utaratibu wao katika kuisaidia jamii katika nyanja za elimu, Afya, Mazingira, Michezo na maeneo mengine yaliyoainishwa katika sera.

Kahyarara amesema kuwa kutokana na polisi kupanua wigo ili kufika katika matukio kwa haraka zaidi jeshi linahitaji kuongeza vituo maeneo mbalimbali na NSSF imeona vyema kushiriki katika suala zima la kuhifadhi na kulinda jamii na mali zao.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, CP Simon Sirro ameshukuru kwa hatua iliyochukuliwa na NSSF kwa kuweza kuwasaidia katika ujenzi wa kituo cha Kiluvya Gogoni kwani ulisimama kwa muda kutokana na ukosefu wa hela.

Akipokea hundi amewaomba mashirika mengine kujitokeza kusaidiana na polisi kuweza kuwasaidia kwenye ujenzi wa vituo ili kusogeza huduma ya haraka zaidi kwa wananchi pale matukio ya kiuhalifu yanapotokea.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images