Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu kuzalisha lita milioni 2 kwa mwaka.

0
0
Na Daudi Manongi,MAELEZO 

Kiwanda cha Biotec Product kilichopo kibaha mkoani Pwani ambacho kinamilikiwa kwa ubia baina ya Serikali za Tanzania na Cuba kimekusudia kuzalisha lita milioni 2 za dawa za viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa malaria nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa katika kiwanda hicho.

“Kiwanda hiki kitasaidia katika vita yetu ya kupambana na malaria kwa kuwa ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua Watanzania na Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kuwatibu wagonjwa” alisema Waziri Ummy .

Waziri Ummy alisema dawa zinazotengenezwa kiwandani hapo zitaisadia tatizo hili na sekta ya Afya kwa kuwa uwezo wa Serikali ni kuzalisha lita milioni 2.5 kwa mwaka na wakati kiwanda hicho kinaweza kuzalisha lita milioni 2 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa katika Watanzania 100, watanzania 14 wanapatwa na ugonjwa wa malaria. Aliongeza kuwa dawa hizo zina uwezo kuua viuadudu hivi katika hatua za mwanzo za kuzaliwa kwa mbu na hivyo uzalishaji huo utapoanza utasaidia kupunguza gharama za kutibu malaria, kununua vyandarua na dawa za kuua wadudu wa mbu. 
Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa Mhe.Salvador Valdes Mesa(kushoto) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(katikati) wakimskiliza Meneja Teknolojia wa kiwanda cha Biotec Product Bi.Lourdes Gonzalez kinachozalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani. Picha na Daudi Manongi,MAELEZO .

Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha wakati makamu uyo alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Kushoto kwa makamu wa Rais wa Cuba ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.

Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha Biotec Product ambacho kinazalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria Bw.Alejandro Torres kilichopo Mkoani Pwani. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU ALAANI MAUAJI YA WATAFITI CHAMWINO

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelaani kitendo cha wanakijiji kuwaua watumishi wa Serikali waliokuwa wakifanya utafiti wilayani Chamwino mkoani Dodoma. 

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Oktoba 3, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na makundi mbalimbali.

Mauaji ya watafiti hao, Teddy Nguma, Jafari Mafuru na dereva wao Bw. Nicas Magazine yalitokea Oktoba Mosi, 2016 baada ya kushambuliwa na wakazi wa kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Amesema Serikali imesikitishwa na mauaji ya watu watatu wakiwemo watafiti wawili kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Seliani (SARI) kilichopo mkoani Arusha ambao walikuwa kazini kuchunguza sampuli za udongo ili kubaini kama matetemeko yataendelea kutokea.

“Kutokana na tetemeko lilitokea mkoani Kagera, Serikali iliamua kushirikisha watalaamu mbalimbali kufanya uchunguzi kuona kama tetemeko hilo ni endelevu au la katika maeneo mengine. Kitendo cha watu kujichukulia hatua mkononi na kukatisha uhai wa watumishi ambao walikuwa kazini hakikubaliki,” amesema

. Amesema watalaamu hao walifika katika Wilaya ya Chamwino na kufanya kazi kwa siku tano na siku ya sita ndipo walipoenda eneo la kijiji cha Iringa Mvumi kuendelea na kazi ambapo waliuawa wakiwa kazini.

“Serikali kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho’’ amesema. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewatoa wasiwasi watumishi wanaohamia Dodoma kuwa Dodoma ni salama na kila anayekuja yupo salama. “Dodoma ipo salama na tunatarajia kila anayehamia hapa atakuwa salama na hata wakazi wa hapa wataendelea kuwa salama,’’ amesema.

Akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, Waziri Mkuu amesema hali hiyo inajitokeza hivi sasa baada ya wananchi wengi kutambua thamani ya ardhi.

Amesema miaka ya nyuma watu wachache walitambua thamani ardhi hivyo kuchukua maeneo makubwa na kuyamiliki. Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa migogoro hiyo inamalizika kwa kuweka kuweka msisitizo kuwe mipango ya matumizi bora ya ardhi ikiwa ni pamoja na kupima ardhi yote na kutoa hati kwa wananchi.

“Tunataka ardhi yote ipimwe na kila mtu anayepewa ardhi apewe hati ya kumiliki na si vinginevyo’’ amesema. Wakati huohuo, Waziri Mkuu aliwaasa waandishi wa habari wawe makini na kazi yao na wajiepushe na upotoshaji kwenye taarifa wanazozitoa kwa wananchi. Amesema vyombo vya habari ni kiungo muhimu baina ya Serikali na wananchi, hivyo aliwataka viongozi wote wa umma washirikiane na vyombo vya habari kwa kutoa habari za utekelezaji wa kazi za Serikali.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepokea msaada wa sh. milioni 11.42 kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali mkoani Dodoma zikiwa ni kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.

Michango aliyopokea leo imetolewa na Mzee Thakar Singh na familia yake sh. milioni 5; NSSF Dodoma (sh. milioni 1.2); Shirika la Bima ya Taifa tawi la Dodoma (sh. milioni moja); Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (sh. milioni moja) na Ofisi Rais TAMISEMI (sh. milioni 2). Wengine ni TRA-Dodoma (sh. milioni moja); Dodoma FM (sh. 200,000) na Mwalimu Mstaafu, Mama Amina Mafuru aliyetoa sh. 20,000/-.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA. JUMANNE, OKTOBA 04, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Dodoma, Oktoba 4, 2016. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Dodoma, Oktoba 4, 2016.
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Dodoma, Oktoba 4, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SHIRIKA LA MAGEREZA NA MFUKO WA PPF WAINGIA UBIA WA UJENZI WA KIWANDA KIPYA CHA VIATU HAPA NCHINI

0
0


Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza,

Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la uzalishaji mali (Prisons Corporation Sole) limeingia Makubaliano na Mfuko wa Jamii wa PPF katika ujenzi na uboreshaji wa mradi wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumanne 04 Oktoba, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wanahabari, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Minja amesema uhirikiano huo unalenga kuliimarisha Shirika la Magereza ili liweze kujiendesha kibiashara pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara.

Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa uwekezaji katika kiwanda hicho utalisaidia Jeshi la Magereza kufikia kiu ya kuzalisha bidhaa za ngozi zenye ubora wa hali ya juu na zinazochochea ushindani katika soko la ndani na nje.

“Naamini uwekezaji huu wa Kiwanda kipya cha Viatu cha Karanga Moshi ni ishara tosha ya kuunga mkono dhamira ya dhati ya Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Tanzania mpya ya Viwanda inawezekana hivyo kutimiza malengo na Dira ya Taifa ya Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025”. Alisema Kamanda Minja.

. Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio wakibadilishana nyaraka mbalimbali za Makubaliano katika Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha. 
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya utiwaji saini wa Mkataba wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha Viatu. 
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiwaji wa Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza). 

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe,Mwigulu  Nchemba wakati alipofika kujitambulisha kwa Rais Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na kulu.]04/10/2016.
mig2

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe,Mwigulu  Nchemba wakati alipofika kujitambulisha   Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na kulu.]04/10/2016.

KIKOSI CHA KMKM CHAANDAA MBIO ZA KILOMITA 10 OKTOBA 29,2016

0
0
Mwenyekiti wa Kikosi cha Kuzuia Magenzo Zanzibar (KMKM) Sports Club Kapteni Khatib Khamis Mwadini akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mbio za Kilomita 10 zitakazofanyika tarehe 29 mwezi huu kuanzia Makao Makuu ya kikosi hicho Kibweni na kumalizikia Uwanaja wa Maisara Mjini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama cha riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas akitoa maelekezo juu ya mbio za Kilomita 10 zilizoandaliwa na Kikosi cha KMKM katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni. 

TAARIFA KWA WATAALAMU WA AFYA WANAOTARAJIA KUANZA MAFUNZO KWA VINTENDO (INTERNSHIP).

TCRA YAKIFUNGIA KIPINDI CHA TAKE ONE KWA MIEZI MITATU KINACHORUSHWA NA CLOUDS TV,WAPEWA ONYO KALI

0
0
Mtangazaji wa kipindi hicho cha Take One kilichokuwa kinarushwa na Clouds TV-Zamaradi Mketema.

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa kipindi kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema mapunda.

Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00

RC SHIGELLA AFUNGUA KIKAO CHA PILI CHA BODI YA BARABARA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akifungua kikao cha pili cha bodi ya barabara kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia akifuatilia makabrasha ya kikao cha bodi ya barabara leo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi,kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mlalo(CCM)Rashid Shangazi,Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM)Adadi Rajabu 
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini Tanroad Mkoani Tanga,Mhandisi Alfred Ndumbaro akiwasilisha taarifa ya mpango wa barabara kwenye kikao hicho 


ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID KUPAMBANA OKTOBA 22 DAR LIVE.

0
0
WAIMBAJI wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala.

Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab.

Mratibu wa onyesho hilo Hajji Mabovu amesema bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.

Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitishia mtandao huu kuwa wamefikia makubaliano ya kuonyeshana ubabe Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu.

Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo kamwe Isha hawezi kuyagoka.

Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.

RAIS DKT MAGUFULI ASHUHUDIA RAIS KABILA WA CONGO-DRC AKIWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange ameweka jiwe la msingi la jengo la Kituo cha Pamoja cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambalo limejengwa kwa lengo la kuwaweka pamoja wadau wote wanaotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma na kupunguza gharama kwa watumiaji wa bandari hiyo.


Hafla ya uwekaji jiwe la msingi la jengo hilo refu kuliko yote Afrika Mashariki na kati imefanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2016 na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


Akizungumza kabla ya kuwekwa jiwe hilo la msingi Rais Magufuli ameishukuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwa mteja mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam na amesema aliamua jiwe la msingi la jengo hilo liwekwe na Rais wa Kongo kwa kutambua umuhimu wa nchi yake katika biashara ya bandari ya Dar es Salaam na pia undugu na urafiki wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili.


Rais Magufuli amemhakikishia Rais Kabila kuwa kama ambavyo Serikali yake imechukua hatua kadhaa za kurekebisha kasoro zilizokuwepo katika bandari hiyo, itaendelea kujenga mazingira mazuri zaidi kwa wafanyabiashara wa Kongo kutumia bandari hiyo ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa, kuongeza muda wa kutunza mizigo inayoshushwa kutoka siku 14 hadi siku 30, kuanzisha bandari kavu katika eneo la Ruvu mkoani Pwani na kuinua ari ya wafanyakazi wa bandari kutoa huduma bora.


"Mhe. Rais Kabila bandari yetu ilifikia mahali pa kuandika rekodi ya kupotea kwa meli kwenye taarifa za bandari, kuna wakati hapa zilipotea meli 60, lakini pia mizigo ya watu ilikuwa inapotea na wafanyabiashara walikuwa wanaombwa rushwa.


"Kuna baadhi ya wafanyakazi wa bandari waliifanya hii bandari kama mali yao, walikuwa wanaondoka na fedha za rushwa kwenye buti za magari, naomba nikuhakikishie kuwa haya hayatatokea tena, na yakitokea Mhe. Balozi wa Kongo upo hapa njoo unieleze mimi au mwambie Makamu wa Rais au Waziri Mkuu"amesisitiza Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli pia amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha ujenzi wa jengo hilo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na kwamba anaamini litasaidia kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Kongo na nchi nyingine zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.


Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange amemshukuru Rais Magufuli kwa heshimu kubwa aliyompa yeye na nchi ya Kongo ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo na amesema kutokana na Tanzania kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha huduma za bandari ya Dar es Salaam mizigo ya Kongo itapitia bandari hiyo.


"Mhe. Rais Magufuli bandari hii ipo Dar es Salaam lakini bandari hii ni ya kwetu sote, mashariki ya Kongo inapakana na nchi nne za Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda lakini asilimia 50 ya mizigo inatoka Tanzania hususani katika bandari ya Dar es Salaam.



"Nimefurahi pia kuwa katika juhudi za Tanzania kuboresha bandari pia mnaboresha barabara na bandari ndogo ndogo za ziwa Tanganyika, hili ni jambo muhimu kwa sababu sasa mizigo ya Kongo itasafiri kwa urahisi na wafanyabishara wa Kongo waliokuwa wameacha kutumia bandari ya Dar es Salaam watarudi"amesema Rais Kabila.


Mhe. Joseph Kabila Kabange amesema katika miaka ya 70 na 80 Kongo ilikuwa ikizalisha shaba kiasi cha tani laki 1 lakini hivi sasa inazalisha hadi tani Milioni 1.2 na zote hizi zinategemewa kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es Salaam.


Ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kununua ndege mbili aina ya Bombardier Q400 na ameunga mkono mpango wa kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Kongo huku akibainisha kuwa nchi yake pia itanunua ndege kwa ajili ya kuimarisha zaidi usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili.


Mapema kabla ya Marais wote wawili kuzungumza, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deodatus Kakoko alisema jengo hilo lina ghorofa 35, urefu wa meta 157, ukubwa wa meta za mraba 65,115 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika tarehe 31 Desemba, 2016 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 130.


Rais Kabila ambaye aliingia hapa nchini jana tarehe 03 Oktoba, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu, jioni ya leo atahudhuria dhifa ya kitaifa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa kwa ajili yake na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam


04 Oktoba, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuli akimshuhudia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akifunua pazia kuashiria kuwekwa kwa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.PICHA NA IKULU.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuli akihutubia  katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akihutubia katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akipokea zawadi ya picha ya Bandari ya Dar es salaam kutoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya TPA  Bw. Ignas Aloys Rubaratuka  katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la wakipata maelezo toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko.

RC Arusha Mrisho Mashaka Gambo, asiimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akitangaza kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015.
Watumishi hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfuta cheo hicho,bwana Evansi Mwalukasa alikuwa mwekahazina wa halmashauri na  bwana Sembeli Sinayo yeye alikuwa mwanasheria wa halmashauri.
Maamuzi hayo yamefikia baada yakubainika kuna upotevu  wa fedha za uchaguzi takribani Milioni 188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa  wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata taratibu za manunuzi ya serikali.
“Kuanzi sasa nawasimamisha  kazi hawa watumishi watatu kwasababu wameisababishia serikali hasara ya takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha za uchaguzi”.
Aidha Mhe. Gambo alisema maamuzi hayo yametokana na taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda ya kuchunguza mapato na matumizi ya fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi ambazo amesema zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Amsema  fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi ambayo hayakufuata taratibu na sheria za manunuzi ya serikali  kinyume kabisa na taratibu za serikali katika maswala ya manunuzi.
Mhe. Gambo pia kasisitiza  watumishi wa serikali kufuata taratibu, sheria na kanuni mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano na uvunjifu wa sheria mahala pa kazi na kupelekea kupoteza ajira  zao.
Watumishi wa Halmashauri ya Ngorongoro, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (hayupo pichani) alipokuwa akitoa taarifa ya kamati ya uchunguzi aliyoiunda kuchunguza mapato na matumizi katika halmashauri hiyo.

KC GLOBAL LINKS LTD SEA AND AIR CARGO UPDATES...

0
0
*THE NEXT AIR CARGO NO 1001 TO DAR ES SALAAM WILL DEPART ON SATURDAY 01/10/2016. CUT OFF FRIDAY 30/09/16.

*OUR NEXT CONTAINER CARGO NO 1001 TO DAR ES SALAAM WILL DEPART ON 15/10/2016  CUT OF 14/10/2016

*PLEASE BRING YOUR CARGO NOW TO AVOID DELAYS....
AIR CARGO TO DAR £3.50 PER KG INCLUSIVE CLEARANCE

*AIR CARGO TO DAR £1.80 PER KG EXCLUSIVE CLEARANCE



*AIR CARGO TO NAIROBI £1.80 EXCLUSIVE CLEARANCE

MZIGO KWA MELI TO DAR £1.80 INCLUSIVE CLEARANCE
(KUMBUKA...CONTAINER ZINAONDOKA MARA MBILI KWA MWEZI)

YOU CAN BUY ANY ITEMS ON EBAY, AMAZON OR AUTOTRADER AND  HAVE THEM DELIVER TO OUR OFFICES AND WE WILL DELIVER IT TO YOU WITHIN 7 DAYS.

CONTACT US ON;
OFFICE; +44 1375 85 85 25
MOBILE; +44 7494 36 41 94

KC GLOBAL LINKS LTD
SUITE 2 CLIPPER HOUSE, TILBURY DOCKS, RM18 7SG
CARGO COLLECTION ANYWHERE IN LONDON IS FREE!

MKUU WA WILAYA YA KONGWA AFANYA ZOEZI LA KUVURUGA BUSTANI ZILIZOLIMWA KARIBU NA VICHOTEO VYA MAJI.

0
0
Mkuu wa Wilaya ya wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi  akisaidiana na wananchi kuvuluga bustani zilizopo karibu na vichoteo vya maji.
DC wa Wilaya ya Kongwa MH Deo Ndejembi Amelifanya zoezi hilo akiwa na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya Ndejembi ameamua kufanya zoezi lakutifua Bustani hizo Baada ya Wananchi wanaoishi karibu na vichoteo hivo kuamua kulima Bustani za Mboga mbona wakiwa wanatumia Maji ya Bomba ambayo hupaswa kusukumwa kujaza Tanki Kubwa.


Wananchi hao wamekuwa wanafungulia Maji ya Bomba nakumwagika chini ili kuelekea katika Bustani Zao, Hufanya hivo nyakati za usiku Muda ambao Pampu inasukuma Maji kuelekea Tanki la Mjini ili Lijae na Kuhudumia Wakazi wa Mjini Kongwa.

Kutokana na kutokujaa Tanki Hilo la Mjini kwa sababu ya wananchi hao kufungulia Maji nakumwagika nyakati za usiku basi Kongwa kumekuwa na Shida Kubwa ya Maji.

DC aliongozana na DAS wake Ndg Audiphace Mushi Ambae alishiriki kikamilifu ktk zoezi lakutifua Bustani hizo, Akiwamo Mkurugenzi Mpya wa Mamlaka ya Maji Ndg Hamisi Ally Anaekaimu nafasi hiyo  Baada ya aliekuwa Mkurugenzi mamlaka hiyo kumsimamishwa na DC Ndejembi wiki moja ilopita.

Pia Aliongozana na Mshauri wa Mgambo Sajent Taji Paul Nkwabi, Pia Alikuwapo Kaimu Afisa Tawala Ndg Denis Semindu nk....

Kabla yakuanza zoezi lakuvuruga Bustani hizo DC Ndejembi aliamuru wananchi Kuchuma mbonga zilizokuwapo ktk Bustani hizo, Pia Kuchukua Maji ambayo yalikiwa yamehifadhiwa ktk Bustani hizo kwa ajili yakumwagilia.
Lakini Pia Walifanya zoezi lakutafuta Mpira ambao Hutumika kuonganisha ktk Bomba nakupeleka shambani, Wamiliki wa Bustani hizo walikimbia na kuficha mipira hiyo.

Vichoteo hivo Viko Kijiji cha Ibwaga ambapo viliwekwa mahususi kusaidia Wanakijiji wa Vijiji vya karibu, Vichoteo hivo vilitobolewa katika Bomba Kuu ambao linaelekea Mjini na Walipewa Muda wakutumia Kuanzia Asubui mpaka Jioni saa 12 kisha wafunge na Kuacha Pampu isukume Maji Mjini ili kujaza Tanki kubwa, cha ajabu nikuwa wananchi hao wamekuwa hawafungi Mabomba hayo Usiku bali huendelea kuchota maji na wengine kufungulia kumwagilia Bustani.

KAMATI YA MAANDALIZI YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI, YAANZA KUKUTANA

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Profesa Justin Ntalikwa (mbele) akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya maandalizi ya  mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika  bandari ya  Tanga nchini  Tanzania. Kamati hiyo  inajumuishwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya  Fedha, Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (CAG). Lengo la kikao hicho  ni kujadili  maandalizi  ya ujenzi wa bomba hilo.
 Mratibu Miradi ya  Ubia wa Sekta Binafsi na Umma (PPP), Salum Mnuna  kutoka  Wizara ya Nishati na Madini (kulia) akielezea maandalizi ya  ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi  Tanzania katika kikao hicho. Kushoto ni Mjiolojia Mkuu kutoka Wizara hiyo, Adam Zuberi.
 Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) katika kikao hicho.




WAZAZI WATAKAOWAOZESHA WATOTO WAO BADALA YA KUWAPELEKA SHULE WILAYANI NZEGA KUKIONA CHA MTEMAKUNDE

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe Gedfrey Ngupula

Na Mathias Canal, Tabora.
Tatizo la Mimba za utotoni na kuozesha wanafunzi katika umri mdogo limetajwa kuwa ni kikwazo kikubwa katika jamii kwani watoto wa kike wananyimwa haki ya kupata elimu ili kujikwamua na fikra mpya katika uchumi na namna ya kuwa na familia bora na endelevu katika kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe Gedfrey Ngupula Ameyabainisha hayo katika mahojiano maalumu na Mwandishi wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com kuhusu mikakati ya kukabiliana na mimba za utotoni pamoja na wazazi kuwaachisha masomo watoto wao wa kike ili kuwaozesha kwa fikra potofu za kupata mali zikiwemo Ng'ombe na fedha.

Dc Ngulupa amesema kuwa jambo hilo limepigwa marufuku na serikali lakini bado linafanyika kimya kimya katika maeneo mbalimbali nchini hivyo endapo atabaini wazazi wanaofanya hivyo kuanzia sasa watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.

Amewataka wananchi kuachana na dhana hiyo potofu ya kujipatia mali kupitia watoto wao wa kike badala yake wahakikishe wanafanya kazi kwa bidii ikiwemo kuwekeza zaidi katika elimu, kilimo na ufugaji kwani ndio njia nyepesi katika mafanikio kuliko kuwa na mtazamo hasi.

Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo walimu katika utendaji wao ikiwa ni pamoja na uduni wa mishahara, Kitolipwa stahiki zao baada ya kupandishwa madaraja Dc Ngupula alisema kuwa serikali kuu kupitia Mhe Rais Dkt John Magufuli aliahidi neema kwa watumishi wote ikiwemo sekta ya afya na elimu hivyo amewataka walimu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki Rais anapopitia ripoti ya watumishi hewa aliyokabidhiwa hivi karibuni ili kujiridhisha na kuruhusu kuajiriwa kwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulipa madai ya walimu ambayo yana haki kimsingi na yamekuwa ya muda mrefu.

Hata hivyo Dc Ngupula amesema kuwa walimu wakuu wanapaswa kuendelea kutoa taarifa za ukweli kuhusiana na upungufu wa madawati ili kukabiliana na kadhia hiyo ambayo imekuwa ni tatizo kubwa katika shule mbalimbali nchini.

Alisema kuwa endapo uchunguzi anaoendelea kuufanya utabaini kuwa kuna upungufu wa madawati ilihali tayari awali walishatoa taarifa kuwa hakuna kadhia hiyo watachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kutoa fundishi kwa watumishi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wanaishi kwa mazoea pasina utendaji yakinifu.

Dc Ngupula amesema kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa katika utoaji wa takwimu za wanafunzi hewa kwani taarifa za awali zilieleza kuwa kuna wanafunzi hewa Wilayani Nzega zaidi ya 4000 lakini amesema kuna uwezekana wa kuwapo na wanafunzi wengine wengi hivyo endapo kama jambo hilo litabainika wale wote walioshiriki katika udanganyifu huo watachukuliwa hatua za haraka kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kazi.

Ili kuelekea kwenye uchumi wa Taifa la kati kuna kila sababu ya kuwa na Taifa imara lenye wasomi wa kutosha lisiwe Taifa la watu wajinga hivyo ni lazima kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata elimu kwani ndio njia pekee ya kujikwamua na umasikini uliokithiri nchini Tanzanaia.

CHURA WA SNURA AFUNGULIWA.

0
0
Msanii Snura Mushi 'Snura'akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha Video yake ya wimbo wa  chura mara baada ya kufunguliwa wimbo huo kupigwa na kuoneshwa kwenye vituo vya Luninga pamoja na wimbo wa chura kuanza kupigwa katika vituo vya Redio hapa nchini.
 Msemaji wa 'Snura', kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar e Salaam leo mara baada ya kukamilisha video mpya ya wimbo wa chura wa Snura na wimbo huo kuanza kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya Luninga pamoja na wimbo wa chura kuaza kupigwa kwenye vituo vya Redio.
Picha na Aviala Kakingo, Globu ya Jamii.

VIDEO mpya ya wimbo wa Msanii, Snura Mushi 'Snura' wa Chura ambao ulikuwa umefungiwa na Serikali, wimbo  huo umefunguliwa na kuanza kuchezwa na kuoneshwa kwenye vituo vya Luninga pamoja na kupigwa kwenye vituo vya Redio.

Hayo yamesemwa na Msanii, Snura Mushi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa wimbo huo ameurekodia Video mpya yenye maadili ya Kitanzania na yenye staa zote na inaelezea maana halisi ya chura kama alivyomaanisha kwenye utunzi wa wimbo huo.

BENKI YA DCB YAZINDUA UTARATIBU MPYA KWA WATEJA WAKE WA KUTOA MAONI KWA KUTUMIA MASHINE YA HAPPY OR NOT.

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya DCB imezindua utaratibu mpya kwa wateja wake wa kutoa maoni kwa kutumia mashine ya Happy or not katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Ubunifu- DCB, Samwel Dyamo amesema kuwa huduma hii mpya itasaidia kupata taarifa kwa mapema zaidi kwani zitakuwa ni kwa njia ya mtandao na zitatoa mrejesho kwa kampuni ili kuzidi kuboresha zaidi.

Dyamo amesema, kwa sasa wateja wetu watatumia mashine hiyi badala ya kutumia boksi la maoni kwani ni njia rahisi sana kuweza kuwafikia wao kwa mapema kwanj mrejesho utakuja haraka zaidi na mapema.

Kwa pamoja benki ya DCB waliweza kukata keki na kusherehekea na wateja wao huku baadhi wakisifia huduma nzuri zinazotolewa na wanapata mikopo kwa njia rahisi sana na kwa riba nafuu.

Fatma Simba, amesifia huduma za benki ya DCB na kusema kuwa wanatoa mikopo kwa urahisi sana ndani ya siku tatu kuanzia kima cha 50,000.

Wiki ya huduma kwa mteja inaadhimishwa dunia nzima kwa makampuni mbalimbali na taasisi, ambapo Benki ya DCB wamekuja na kauli mbiu ya Wewe ni mhimili wetu, tupo kwa ajili yako. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Ubunifu DCB, Samwel Dyamo akizindua kwa kubonyeza kutufe katika mashine ya Happy or Not jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo.       
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mind Source, Abubakar Faraji akielezea namna ya kuitumia mashine ya Happy or Not kwa wateja wa Benki ya DCB leo Jijini Dar es salaam kwenye wiki ya Huduma kwa Mteja.
 Wateja na wafanyakazi wa DCB Benki wakiwa wanashuhudia kukata kwa keki sambamba na wateja hao kukata keki.

WASHINDI WA M BET WAKABIDHIWA VITITA VYAO

0
0
WASHINDI wawili, Exaudi Mgeni wa Iringa na Joel Mwakagali wa Mbeya, waliojinyakulia jumla ya kitita cha Sh milioni 82, wamekabidhi wa fedha zao katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa, Abbas Tarimba.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mfano ya hundi yenye thamani ya fedha hizo, Tarimba aliipongeza m-Bet kwa kuendesha mchezo huo kwa ufanisi, lakini pia washindi hao kwa kuibuka kidedea.

Alisema bodi yake inafarijika kuona washindi hao wakiliingizia pato Taifa kupitia kodi watakayolipa kwa kushinda fedha hizo ambazo ni kama Sh milioni saba hivi, huku akiwataka kuhakikisha wanazitumia ipasavyo fedha hizo kuboresha maisha yao.

“Michezo ya –ku-bet’ tumeweza kuilea ili kutoa nafasi kwa wanamichezo kushiriki michezo hii ya kubahatisha ambayo ni neema kwa taifa na si janga kama baadhi ya watu wanavyodhani,” alisema Tarimba.

Alisema kwa kuonyesha jinsi michezo hiyo ilivyo na tija kwa taifa, mwaka 2014-15, ililiongezea taifa pato la Sh milioni 15 kupitia kodi, wakati mwaka uliofuata, iliingiza kiasi cha Sh bilioni 24.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa m-Bet, Dhiresh Kaba, alisema kuwa Mgeni na Mwakagali, walifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 12 za ligi za Ulaya kwa Super 12.
“Tunafarijika kuwakabidhi kitita chao cha Sh milioni 82 Joel na Exaudi kama washindi wa m-Bet ambao kila mmoja atapata Sh milioni 41 kabla ya makato ya kodi,” alisema Kaba.
Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Super 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote kama Mgeni na Mwakagali, unaondoka na kikapu cha siku.
“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Super 1x2 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-bet,” alisema Kaba.
 Mkurugenzi Mku wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abbas Tarimba akizungumza kwenye hafla ya kuzawadia washindi wa M-bet jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5, 2016.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimab (kushoto) akikamkabidhi mfano wa hundi ya  fedha ya 34,179,309/= kwa  mshindi  wa M-bet, Joseph Mwakagali, (kulia) kwenye hafla ya kukabidhi zawadi jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5,2016. Makabidhiano hayo yalihudhuriwa na Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba.

 Mshindi wa M-bet , Joseph Mwakagali (kulia) akishangilia mara baada ya kukabidhiwa hundi yake ya fedha ya 34,179,309/= kwenye makabidhiano ya zawadi kwa washindi wa M-bet jijini Dar es salaam leo Oktoba 5,2016. Wanaofurahia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimba (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi na katikati ni  Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba. 
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimab (kushoto) akikamkabidhi mfano wa hundi ya  fedha ya 34,179,309/= kwa  mshindi   mwingine wa M-bet, Exaud Mgeni (kulia) kwenye hafla ya kukabidhi zawadi jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5,2016. Makabidhiano hayo yalihudhuriwa na Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba.

MHAGAMA AMTEMBELEA MKE WA BABA WA TAIFA MAMA MARIA NYERERE

0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Jenista Mhagama akifanya mazungumzo na Mke wa baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam, leo tarehe 5 Oktoba 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TFF YAMFUNGIA MWAMUZI SEIF, MANARA, SIMBA, AZAM ZAPIGWA FAINI.

0
0
Ofisa wa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini(TFF), Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MWAMUZI Ahmed Seif amefungiwa kuchezesha mpira kwa miezi sita baada ya kutoa penati iliyokuwa sio sahihi pamoja na kupata alama chache ambazo haziruhusu kuchezesha ligi kuu katika mchezo baina ya African Lyon na Mbao uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF,kupitia kwa Ofisa habari wake Alfred Lucas amesema kuwa  klabu ya Simba imepigwa faini ya milioni tano
baada ya mashabiki wake kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa mali za serikali na kutakiwa kulipa gharama za uharibifu huo kupitia kanuni ya 42(3) na 24(7) huku Msemaji wa timu hiyo Haji Manara akipigwa faini ya laki mbili kwa kosa la kuingia ndani ya Uwanja pasi na kuwa kiongozi wa benchi la Ufundi kulingana na kanuni ya 14(10).


Simba wamepewa adhabu hiyo ya faini iliyotokea katika mchezo wao dhidi ha Yanga uliofanyika Oktoba 1, uliochezeshwa na Mwamuzi Martin Saanya ambaye mpaka muda huu kamati ya bodi ya ligi inaendelea na uchunguzi wa mchezo mzima ili kutoa maamuzi huku wakiifuta kadi nyekundu aliyepewa Nahodha Jonas Mkude kupitia kanuni ya 9(8).

Klabu ya Azam imepigwa faini ya milioni tatu kwa kosa la kuvaa nembo ya mdhamini katika mikono yote ikiwa ni kanuni ya 13(6), JKT Ruvu imepigwa faini ya milioni tano kutokana na kushambuliwa kwa msimamizi wa kituo na ofisa wa bodi ya ligi na mshabiki wa timu hiyo na tayari wamemfungia kwa kipindi cha mwaka mmoja na kama wataendelea na kitendo hicho basi wataufungia kutumika kwa Uwanja huo.

Wakati huo, kamisaa wa mchezo namba 5 na 7,  David Lugenge na Godbless Kimaro wamepewa onyo na bodi ya ligi baada ya kuandika ripoti isiyojitosheleza kwenye michezo hiyo.                         
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images