Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1376 | 1377 | (Page 1378) | 1379 | 1380 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mafanikio yaliyopatikana katika ziara za kuhamasisha wafanyabiashara katika mikoa ya Mwanza, Mara na Geita kurasimisha biashara zao, kumelazimu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kufanya zoezi kama hilo katika mkoa wa Simiyu leo.
  Baada ya Simiyu, mikoa ya Shinyanga na Tabora itafuata.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Bw. Frank Kanyusi alisema taasisi yake imejipanga kutoa elimu stahili na kuhamasisha wafanyabiashara kujitokeza na kurasimisha shughuli zao.
  “Wafanyabiashara katika mikoa hii wajitokeze kwa wingi ili kutumia nafasi hii adimu kwa ufanisi,” alisema Bw. Kanyusi.
  Aliwataka wajasiriamali, wafanyabiashara na watanzania wote wa mikoa hiyo wafike kupata elimu ya namna kurasimisha biashara zao na kuzifahamu huduma nyingine zinazotolewa na wakala kwa njia ya mtandao.
  Alisema tarehe 3 hadi 8 watakuwa mkoa wa Simiyu, tarehe 10 hadi 15 mkoa wa Shinyanga na tarehe 17 hadi 22 watakuwa mkoa wa Tabora.
  Alifafanua kwamba kuna faida nyingi za kurasimisha biashara; ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na serikali, kupata fursa mbalimbali, kuwa na walipa kodi wengi na kodi zao kutumika katika ujenzi wa taifa na huduma za jamii.
  “Tumeboresha huduma zetu na mtu anaweza kusajili jina la biashara mahali alipo bila ya kufika Dar es Salaam,” alisema Bw. Kanyusi na kufafanua kuwa wengi hawafahamu hilo na kwamba watumie fursa kupata elimu hiyo.
  Alisema zoezi katika mikoa ya Mwanza, Geita na Mara ilikuwa ya mafanikioa makubwa kwa vile watu wengi walishiriki na kusajili hapo hapo majina ya biashara kupitia mtandao.
  Katika mkoa wa Mwanza, makampuni 100 na majina ya biashara 150 vilisajiliwa; mkoa wa Geita majina ya biashara 60 na makampuni 50 na mkoa wa Mara majina ya biashara 45 na makampuni 30.
  Alisema wakala umejipanga kwenda katika mikoa yote nchini kutoa elimu ya urasimishaji biashara na maboresho waliyofanywa ambayo yanatoa fursa huduma kutolewa kwa njia ya mtandao.
  Alisema semina hizo pia zinalenga kusikiliza changamoto ambazo zinawakabili wajasiriamali, wafanyabiashara na watanzania wote juu ya huduma zinazotolewa na wakala na kuzifanyia kazi.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Bw. Frank Kanyusi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuanza kwa mafunzo na zoezi la urasimishaji biashara mkoani Simiyu leo. 

  0 0

  Vijana wa Kitanzania waliopata bahati ya kwenda kujifunza masuala mbalimbali kupitia programu ya kubadilisha vijana na nchi ya Ujerumani wametakiwa kuweka uzalendo mbele kwa nchi yao na kurudi nyumbani kuitumikia.
  Vijana wa Kitanzania wataungana na wenzao katika program ya kubadilishana vijana na nchi ya Ujerumani kujifunza masuala mbalimbali yahusuyo lugha, utamaduni na ufundi stadi. 
  Tanzania ilishinda programu hiyo kupitia asasi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition (TYC) baada ya kutuma andiko lake sambamba na mataifa mengine Afrika ambapo nchi tatu tu Tanzania ikiwa mojawapo ndizo zilizoshinda.
  Mpango huo wa kubadilisha vijana ni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 na vijana watakuwa wanaenda ujerumani kujifunza kwa muda wa mwaka mmoja mmoja.
  Akizungumza wakati wa kongamano la wadau lililotayarishwa na TYC mwishoni mwa wiki, Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa alisema vijana watakaokwenda Ujerumani wanatakiwa kujifunza kwa bidii, kupata maarifa mapya na kutengeneza mahusiano mapya kwa faida yao na nchi kwa ujumla.
  “Serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda na inategemea sana vijana ili kuendelea,” alisema na kuongeza kuwa ujuzi watakaopata ni wa muhimu na unategemewa.
  Katika kongamano hilo, asasi ya TYC ilikutana na asasi nyingine kutoka Benin na Afrika ya Kusini kujadili namna ya kutekeleza programu hiyo.
  Alisema NEEC ilishiriki kuanzia mwazo wakati programu hiyo ilipokuwa ikizinduliwa ujerumani na kwamba serikali imejipanga kusimamia vizuri programu za kubadilishana vijana na Ujerumani na nchi nyingine kwa faida ya taifa.
  Mkurugenzi wa TYC, Bw. Lenin Kazoba alisema warsha hiyo ilikuwa ya wadau ambao walijadili namna bora vijana wa mataifa hayo watakavyoshiriki katika programu hiyo.

  Asasi hiyo sasa itawakilisha nchi za Afrika Mashariki, wakati vijana toka Afrika Kusini watawakilisha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakati nchi ya Benin itawakilisha Jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
  Programu hiyo ilianzishwa baada ya serikali ya Ujerumani kukubaliana na Umoja wa Afrika (AU) kushindanisha nchi za Afrika na hatimaye asasi kutoka nchi hizo tatu kushinda.
  Asasi ya TYC inajumuisha vijana wa sekondari, vyuo vya ufundi stadi, vyuo vikuu na watu wenye mahitaji maalum.
  Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kushoto) akizungumza wakati wa kongamano lililotayarishwa na asasi ya kiraia ya Tanzania Youth Coalition (TYC) iliyoshinda nafasi ya mpango wa kubadilishana vijana na nchi ya Ujerumani.  Mpango huo wa miaka mitatu unaoanza mwaka 2017 unahusisha pia nchi za Benin na Afrika ya Kusini.  Kulia ni Mkurugenzi wa kitengo cha vijana, Umoja wa Afrika, Bi. Prudence Nonkululeko Sigwane na Mkurugenzi wa TYC, Bw. Lenin Kazoba (katikati).

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wakuu wa Ofisi yake  baada ya kuwasili Ofisini kwake mjini Dodoma Oktoba 1, 2016. Kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Ajira, Erick Shitindi, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, Dkt. Hamisi Mwinyimvua na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Makao Makuu, Dodoma baada ya kuwasili Ofisini hapo Oktoba 1, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni,  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Ajira, Eick Shitindi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera na Uratibu, Dkt. Hamisi  Mwinyimvua, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Antony Mavunde.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu, Makao Makuu, Dodoma baada ya kuwasili Ofisini hapo Oktoba 1, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu, Makao Makuu, Dodoma baada ya kuwasili Ofisini hapo Oktoba 1, 2016.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea risala ya Wazee kutoka kwa Mwakilishi wa Wazee Bw.Salum Ali Mata aliyoisoma katikasherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika  katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea taarifa ya Shirika la HELP AGE INTERNATIONAL Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Amleset Tewodoes mara baada ya kuisoma katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika   katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
   Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Mouldine Syrus  Castico akitoa salam zake kwa Wazee pamoja na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Wazee hao katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika  katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Wazee katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba (kushoto) Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Mouldine Syrus  Castico na Bw.Salum Ali Mata mwakilishi wa Wazee (kulia) . Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva akieleza mkakati wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa elimu ya Mpiga Kura kote nchini ili kuwajengea wananchi uelewa sahihi juu  majukumu ya Tume na  chaguzi zinazofanyika nchini. 
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0


  Dkt.Helen Kijo-Bisimba
  OKTOBA Mosi (1) ya kila mwaka ni siku iliyoteuliwa na Umoja wa Mataifa kuadhimisha uwepo wa wazee katika jamii kote ulimwenguni. 

  Siku hii ilianza kuadhimishwa rasmi Oktoba 1, 1991 kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu mambo yanayowalenga wazee ikiwemo kutoheshimu haki za wazee, kutazama mahitaji na maslahi ya wazee na kuhakikisha mzee popote alipo ulimwenguni anapata huduma za msingi za kijamii kama vile huduma bora za afya na matibabu. 

  Mahususi, siku hii imekuwa na lengo la kuutambua mchango wa wazee katika jamii kwa wakati husika na wakati uliopita katika mataifa yao. 
  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu tunatumia fursa hii kuwapongeza wazee wote duniani na hususan wazee wa Tanzania.  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Paskas  Mulagili baada ya kuwasili kwenye nyumba za CDA za Kikuyu mjini Dodoma kukagua ukarabati wa nyumba hizo, Oktoba 1, 2016. Katikati ni Wziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama.
    Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua ukarabati wa nyumba za  Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Paskas  Mulagili baada ya kuwasili kwenye nyumba za CDA za Kikuyu mjini Dodoma Pamoja naye  ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama.
    Nyumba za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)  za Kikuyu zinazokarabatiwa  ili zitumiwe na maofisa wa serikali  watakaohamia Dodoma
   Nyumba za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)  za Kikuyu zinazokarabatiwa  ili zitumiwe na maofisa wa serikali  watakaohamia Dodoma. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri wa habari, utamaduni,sanaa na michezo Mh. Mhe.Nape Moses Nnauye (katikati) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mh. January Makamba (kulia)pamoja na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto)wakifatilia mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,ambapo timu hizo zilitoka suluhu 1-1.

   Watoto wanaokota mipira uwanjani(Ball boys)  wakionyesha mabango yenye ujumbe maalum wa wiki ya nenda kwa Usalama barabarani jana, wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya simba na yanga uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,ambapo timu hizo zilitoka suluhu 1-1.


  0 0


  Na Hussein Makame, NEC

  Watanzania wengi hawaijui Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), majukumu yake na miongozo inayoongoza uchaguzi, hali inayosababisha manung’uniko mengi na upotoshaji kwa umma juu ya tume hiyo.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani (pichani) wakati akitoa tathmini ya elimu ya mpiga iliyotolewa hivi karibuni kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika wiki mbili zilizopita mjini Musoma.

  Bw. Kailima alisema kutokana na hali hiyo, NEC imeanza kutekeleza mkakati kabambe wa kutoa elimu ya mpiga kura kupitia njia mbalimbali ikiwemo kushiriki kwenye maonesho na mikutano inayojumuisha wadau muhimu wa uchaguzi. Taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita, unaofanyika  kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini Mwanza.
  Mhe. Mongella amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa uwazi masuala ya maadili kwa watumishi wa umma na kwamba yawe ajenda ya kudumu katika ngazi mbalimbali za utendaji serikalini hususani katika ngazi ya mahakama.
  Amesisitiza mkutano huo kutoka na maadhimio yanayohimiza mahakama kutenda haki na kuleta manufaa kwa wananchi na kuondokana na malalamiko kwamba mahakama hazitendi haki katika maamuzi yake.
  Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, chama hicho kinahakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kutenda haki na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa chombo hicho katika utoaji wa haki.
  Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma. 
  Na BMG
  Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe. Robert Makaramba, akizungumza kwenye mkutano huo.
  Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, akizungumza na wanahabari nje ya mkutano huo.
  Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi mkoani Mwanza, Mhe.Wilbert Martin Chuma, akizungumza kwenye mkutano wa robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu mikoa ya Mwanza na Geita, unaofanyika Jijini Mwanza. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  WAZIRI MKUU  Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza apatiwe orodha ya wadaiwa sugu wa taasisi zote za Serikali mkoani Dodoma ambao wamelimbikiza deni la sh. bilioni 1.4 zikiwa ni bili zao za maji. 

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 2, 2016) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) mara baada ya kukagua utendaji kazi wa chanzo cha maji cha Mzakwe nje kidogo ya mji wa Dodoma. 
  “Niletee haraka orodha ya wadaiwa wote wa Ofisi za Serikali na taasisi za umma ambao hawajalipa bili zao. Madeni yote ni lazima yalipwe,” amesema Waziri Mkuu. 
  Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya siku mbili ya kukagua maandalizi ya Serikali kuhamia Dodoma, anatembelea sehemu mbalimbali za kutolea huduma za jamii pamoja na kukagua miundombinu ya mkoa huo.  0 0


  0 0

  Kamati ya maafa mkoani Kagera imeendelea kupokea misaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kutoa michango yao kwa lengo la kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililoathiri mkoa wa Kagera.

  Akikabidhi msaada uliotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza Mratibu Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Burhan Mohammed amesema kuwa wao kama taasisi wamevutwa na kushikwa kwa moyo wa huruma na kuamua kuchukua hatua ya kuwasidia majirani zao wa mkoa wa Kagera. "Sisi sote ni Watanzania, tuliposikia wenzetu wamepatwa na matatizo, tumeamua kutoa mchango wetu kwa kushirikiana na wanachama wenzetu ili kutoa huduma za kuwapa chakula wenzetu wakati wa matatizo" alisema.

  Taasisi hiyo imetoa Mchele, chumvi, mafuta ya kula, Sabuni pamoja na katoni za maji ya kunywa ambapo vyote kwa jumla vinathamani ya sh. milioni 22. Aidha, Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Lwelu ya mkoani Kagera wametoa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni 2.1 ikiwa ni pamoja na sukari, unga na mchele.

  Wadau wengine waliotoa misaada ni kampuni ya Time to Help yenye makao makuu ya jijini Dar es salama ambayo inayomilikiwa Waturuki wametoa mablanket 500. Akipokea misaada hiyo kwa niaba ya Mkuu Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro amewaeleza wadau hao taswira mzima ya hali ya maafa katika mkoa Kagera ambapo amesema kuwa mahitaji kwa waathirika bado ni makubwa.

  Kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya Bw. Kinawiro amewashukuru wadau wote wanaendelea kutoa misaada kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Kagera ambao wameathirika wa tetemeko hilo na kuwataka wadau wengine kuendelea michango ya hali na mali katika kukabiliana na hali ya maisha baada ya tetemeko kutokea.
  Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro akiwashukuru Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu na kusema kuwa mahitaji kwa waathirika wa tetemeko la ardhi bado ni makubwa na misaada inahitajika ili kuwasaida waathirika hao.

  Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza Burhan Mohammed akitoa neno mwishoni mwa wiki mara baada ya ya kukabidhi msaada wa vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
  Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro (katikati aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu. (Picha/Habari na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba). 

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu amezindua kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa kuweka huduma ya intaneti kwa njia ya Wi-Fi katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu katika jiji la Dar es salaam ili kuongeza fursa kwa watanzania kutumia mawasiliano kwa manufaa ya Taifa katika kuleta maendeleo.

  Mheshimiwa Samia Suluhu alizindua huduma hiyo ya W-Fi katika viwanja vya Gymkhana katika uzinduzi wa Kampeni ya kupanda miti iliyofanyika jijini la Dar es salaam Oktoba mosi mwaka huu.

  Akizungumza na wakazi waliojitokeza katika viwanja vya Gymkhana, Makamu wa Rais alisisitiza wakazi wa Dar es salaam kupanda miti na kuitunza ili kuhifadhi mazingira hususani katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, pia alipongeza juhudi za uwekaji wa huduma ya intaneti kwenye maeneo ya jiji la Dar es salaam.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa huduma ya Wi-Fi ambayo itawekwa katika maeneo ya mkusanyiko ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya Tano kuhakikisha jiji linakuwa na huduma endelevu ya intaneti ambapo wananchi wataweza kupata huduma hiyo popote walipo, kutumia mawasiliano katika kujenga Taifa letu kimaendeleo na kupashana habari mbalimbali za kimaendeleo.

  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema kuwa kutokana na uwezo na uzoefu katika sekta ya mawasiliano TTCL iko mstari wa mbele katika kuchangia juhudi za serikali katika kuboresha huduma za TEHAMA kwa kuwafikia watanzania wengi zaidi kupitia huduma hii ya Wi-Fi itakayopatikana katika bustani za mapumziko jijini Dar Es Salaam.

  Pia, Kindamba alisema kuwa “Jitihada hizi kwa kushirikiana na wadau wetu mbalimbali zitaendelea na kuhakikisha kuwa sehemu nyingi zenye mikusanyiko ya watu wengi wanapata huduma hii ya Wi-Fi. Mathalani maeneo ya haya ni vituo vikubwa vya mabasi, viwanja vya ndege, vyuo, majengo makubwa yenye wakazi wengi, viunga vya mapumziko, viwanja vya mpira kwa kuwa dunia ya leo mawasiliano ni chachu muhimu katika kuboresha maisha yetu, na kupashana habari na matukio muhimu” Aidha, mpango huu wa Wi-Fi utakua endelevu kufikia lengo la kujenga miji na majiji yetu kwa kiwango cha “Smart City” ili pia kuimarisha ulinzi na usalama wa miji, watu na mali zao.

   Mkuu wa Kanda Kibiashara wa Dar es salaam wa TTCL, Jane Mwakalebela   na wadau  wakipanda miti katika viwanja vya Ghymkhana, Dar e salaam.
     Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Bw Waziri Waziri Kindamba akiwa pamoja na wanafunzi wa Skauti, viwanja vya Ghymkhana       Wafanyakazi wa TTCL  wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema, baada zoezi la kupanda kukamilika katika viwanja vya Ghymkhana. 


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akijiunga na mtandao kwa njia ya Wi-Fi kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya intaneti ya Wi-Fi inapatikana bure kwa wakazi wa jiji Dar es salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Sophia Mjema akishiriki zoezi la kutumia Wi-Fi katika banda la TTCL , ambapo TTCL ilikuwa ikitoa huduma ya intaneti Bure.
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba na Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo, Peter Ngota wakipanda miti katika viwanja vya Ghymkhana, ambapo TTCL iliweka huduma ya intaneti bure  ya Wi-Fi.

  0 0

  Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara katika Mkoa wa Kigoma huku akimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu tuhuma za wizi wa madawa na ujenzi wa wodi ya kina Mama ya Buhando na ujenzi ulio fanyika Katika zahanati zingine ndani ya Manispaa ya kigoma

  Hatua hiyo ya Jafo ilitokana na kutoridhishwa na utendaji wa mkuu wa idara ya Afya ya Manispaa ya Kigoma, John Maganga kutokana na usimamizi mbovu wa miradi hiyo katika idara yake sambamba na kuwepo kwa malalamiko mengi ya ubadhilifu wa madawa ndani ya Manispaa hiyo.

  Jafo alitembelea jengo la wazazi la Zahanati ya Buhanda ambapo hakuridhishwa kabisa na maelezo ya ubora wa jengo hilo na mganga mkuu huyo kushindwa kumpa Naibu Waziri maelezo ya kuridhishwa juu ya gharama za ujenzi wa jengo hilo ambalo limejengwa chini ya kiwango na kuwepo mashaka makubwa ya upotevu wa fedha nyingi katika ujenzi wa jengo hilo lililo zinduliwa kinyemela na DMO huyo.

  Kutokana na simtofahamu hiyo Naibu Waziri amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi na kwamba lengo la ziara hiyo ni kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi ndani ya halmashauri mbalimbali hapa nchini.

  Jafo katika Mikoa minne ya Mara, Simiyu, Geita na Kigoma ambapo alizifikia Halmashauri 19 na kuongea na watumishi zaidi ya 6000 pamoja na kukagua miradi mbalimbali 25 ya barabara, maji, afya, elimu na ujasiliamali imeleta tija sana kwa kuinua hamasa ya utendaji kazi kwa watumishi wa halmashauri za wilaya.

  Ziara hiyo aliifanya baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Taasisi za Serikali za Mitaa (ALAT) uliofungwa rasmi tarehe 24 September 2016 mjini Musoma Mkoani Mara. Ziara ya Naibu Waziri huyo ilianza tarehe 25 September hadi 30 September 2016 ambapo alikagua miradi na kuongea na watumishi.

  Jambo kubwa lililo sisitizwa Katika ziara hiyo ni umuhimu wa watumishi wa halmashauri kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma zao pamoja na kuweka maslahi ya Taifa mbele.Aliwataka wakurugenzi kuwekeana malengo ya utekelezaji na wakuu wao wa Idara, na wakuu wa idara kuwekeana malengo na watendaji wao wa chini wanao waongoza.

  Kadhalika, Aliwataka watendaji wa halmashauri wabadilike katika utendaji wao. Amewataka wakuu wa idara kutowabagua baadhi ya watumishi katika idara zao.  Naibu Waziri Selemani Jafo akiwa na mtoto wa baba wa Taifa Madaraka Nyerere pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Edo Mapunda, nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere Butiama.

  Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Mbogwe Silivester Massele wakikagua jenereta la kusukuma maji Katika wilaya ya Mbogwe.


  Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akikagua mradi wa Maji Katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

  Naibu Waziri Selemani Jafo akikagua ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mara mjini Musoma
  Naibu Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo akikagua kiwanda cha vijana cha kutengeneza Chaki mjini Maswa mkoani Simiyu.

  0 0


  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ili kuzungumzia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. 

       Katika Mkutano huo Makonda amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza au kuondoa kabisa changamoto zinazowakabili ikiwemo, vibaka, dadapoa na uchafu wa mazingira, akisema, ikiwa wananchi watashitiki kikamilifu ni rahisi kukomesha tatizo la vibaka kwa sababu vibaka na dadapoa wanatoka miongoni mwa familia zao na hali kadhalika uchafu wa mazingira unatokana na takataka wanazozalisha wananchi wenyewe.

  Kamanda wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uliofayika leo jioni Buguruni kwa Mnyamani 
   Viongozi waandamizi katika Wilaya ya Ilala, wakimsikiliza mkuu wa mkoa Paul Makonda wakati akihutubia wananchi katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani leo jioni. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela, Ofisa Tawala wa Manispaa hiyo, Edward Mpogolo, Naibu Meya Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Segerea wilayani humo Bona Kalua
   Mjumbe wa Shina namba tano, Katika Kata ya Myamani, Buguruni Zubeda Lugiga, akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara leo jioni
   Mkazi wa Buguruni, Sadik Mgaya akieleza changamoto na kero zinazowakabili wananchi wa eneo hilo wakati wa mkutano huo wa Makonda.


  0 0


  Nteghenjwa Hosseah – Arusha

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo mwishoni mwa wiki hii amekutana na wadau wa taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na makampuni yanayoendesha shughuli zao katika Wilaya ya Ngorongoro lengo ikiwa ni kusikia namna wadau hao wa maendeleo wanavyoendesha shughuli zao halkadhalika Wilaya hiyo inavyonufaika na uwepo wa wadau hao katika maeneo hayo.

  Akizungumza wakati wa kufungua Kikao hicho Rc Gambo alisema malego ya Kikao hiki yanaendana sambamba na maandalizi ya Safari yake ya kikazi ya siku tano katika Wilaya ya Ngorongoro itakayoanza tarehe 03-08/10/2016 hivyo angependa kufahamu kwa upana namna ambavyo wadau hawa wanachangia katika kuleta maendeleo ya Wilaya hii ambayo kwa kipindi kirefu imekua nyumba kimaendeleo.

  Alisema sielewi kwa nini kwa miaka yote hii Wilaya ya Ngorongoro haina hata kilomita moja ya barabara ya Lami, Stendi ya Kisasa wala masoko yenye hadhi ya kuwahudumia wageni ambao wengi wao ni watalaii wakati kuna taasisi za Kiserikali na siziso za Kiserikali ambazo zina uwezo wa kutosha kuboresha huduma hizi kwa manufaa ya wananchi na wageni wanaotembelea eneo hilo.

  Wananchi wa Ngorongoro wamekua na maisha duni na matatizo yasiyoisha, hakika sasa umefika wakati wa kufahamu kazi zinazotekelezwa na kila mdau na tufahamu kwanini uwepo wao hauchangii kulete mabadiliko chanya katika Wilaya hii, huenda mipango kazi yao iko tofauti na malengo na matarajio yetu hivyo tusije tukawalaumu kumbe ni kutofahamu namna ambavyo taasisi zenu zinafanya kazi aliongeza.

  “Katika Wilaya hii ukizungumzia Taasisi kubwa za Serikali kuna Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Baraza la wafugaji pamoja na Halmashauri ambao wanapata Fedha nyingi kwa ajili ya kuleta maendeleo lakin bado kasi ya maendeleo kwa kweli hairidhishi kabisa, ni vyema basi kwa pamoja tutafute majawabu ya matatizo yanayoikabili Ngorongoro”, alisema Gambo.

  Baada ya Taasisi zote kuwasilisha taarifa zao iligundulika kwamba kuna mgogoro wa Ardhi ambao sasa umekua wa muda mrefu kati ya Vijiji vya Sukenya, Soitsambu, Mondorosi na Muwekezaji wa Kampuni ya Thompson.

  Rc Gambo alisema ni wakati sasa wa kuketi meza moja na makundi yote kuona namna ambavyo tunaweza kutatua mgogoro huu ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao na Muwekezaji afanye kazi zake kwa amani katika eneo hilo na kupitia kikao hiki nimepata kufahamu vitu vingi ambavyo ntakuja kuvifanyia kazi wakati wa Ziara yangu.

  Ziara hii ya Kikazi Wilayani Ngorongoro itakua ya pili tangu Mhe. Gambo alipochaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema mwezi Agosti 2016.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akifuatilia na kunakili hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau wa taasisi zisizo za Kiserikali zinazofanya shughuli zake katika Wilaya ya Ngorongoro wakati wa Kikao kilichofanyika katika Ofisi yake. 
  Mkurugenzi wa Taasisi ya PWC Bi. Manda Ngoitiko(aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya NGO anayoiongoza wakati wa kikao maalum na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama. 
  Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Arusha wakifuatilia kikao wakati wa uwasilishaji wa taarifa za Taasisi na Kampuni zisizo za Kiserikali zinazofanya kazi katika Wilaya ya Ngorongoro 
  Wadau toka kwenye Kampuni na Taasisi mbalimbali kutoka Ngorongoro walioshiriki katika Kikao maalumu kilichoitihswa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha 
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega wakati wa Kikao na NGO’S NA Kampuni zinazoendehsa shughuli zake katika Wilaya ya Ngorongoro. 
  Mkurugenzi wa taasisi ya PWC Bi. Manda Ngoitiko (kushoto) pamoja na Manger wa Kampuni ya Thompson Safaris (kulia) kila mmoja akielezea namna ambavyo mgogoro wa ardhi uliopo unavyoathiri shughuli zao za kila siku. 

  0 0  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu (kushoto) kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme kwenye makao makuu ya nchi Dodoma wakati alipotembelea Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2, 2016. Wengine Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Christina Mndeme.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu (katikati) wakati alipotembelea Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 1376 | 1377 | (Page 1378) | 1379 | 1380 | .... | 3272 | newer