Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110009 articles
Browse latest View live

KATIBU MKUU WA CCM, KINANA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA CNDD-FDD CHA BURUNDI, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Kataibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD, Evariste Ndayishimiye, leo Oktoba 1, 2016, katika Ofis Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwa na mazungumzo baina ya viongozi hao kuhusu uhusiano wa vyama hivyo ya CCM na CNDD-FDD. Kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa CNDD-FDD, Gelase Ndabirabe.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya maofisa katika ujumbe wa Burundi uliofuatana na Katibu Mkuu wa Chama cha  CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam. 

PICHA ZAIDI/BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 Oktoba 2016 ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam.


Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya Kilwa – Kurasini katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora katika utunzaji wa Manzingira.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.

Amesema kuwa jitihada za kupanda miti nchini zinatakiwa kuimarishwa maradufu kwani zitasaidia katika uhifadhi wa mazingira hususani katika suala zima la kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Makamu wa Rais katika hotuba yake ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuongezeka hewa ya ukaa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi kuwa ya watu hivyo jitihada za pamoja kati ya serikali,taasisi binafsi,asasi za kiraia na wananchi zinahitajika katika kutunza mazingira na kupanda miti.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia amepongeza jitihada za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji na uimarishaji wa mifumo ya maji katika barabara itakayosaidia kurahisisha umwagiliaji wa miti iliyopandwa.

Amesema anafaraja na matumaini makubwa kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.

Baada ya kuzindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ambaye aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan Mwinyi itakayotumika kumwagilia miti iliyopandwa pamoja na kuongeza na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Gymkana.


Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo katika mti alioupanda eneo la JKT Mgulani Barabara ya kilwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la JKT Mgulani ambapo shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam zilifanyika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiunga na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
................................... 
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SERIKALI IPO PAMOJA NA WANAKAGERA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU-RAIS DKT MAGUFULI

$
0
0
Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kagera.

RAIS John Pombe Magufuli amesema kuwa serekali ipo pamoja na wanakagera katika kipindi hiki ambacho  wamekumbwa na tetemeko la ardhi na lililopelekea kuleta maafa na kupoteza makazi.

 Magufuli aliyasema hayo jana kwenye viwanja vya seminari ya Rubya wakati wa ibada ya misa ya uzinduzi wa jubilei ya miaka 150 uinjilishaji na 100 ya upadre Tanzania.

Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji,Mh Charles Mwijage  aliyasema hayo kwa niaba ya Rais, alisema kuwa Rais amemtuma kuwapa pole nyingi wana kagera walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea september 10 mwaka huu.

 Magufuli alisema kuwa serekali yake inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu mbalimbali kwa haraka kama vile shule,zahanati,nyumba za ibada na barabara ili huduma za kijamii ziwe kurudi katika hali yake ya kawaida.

 Aliwapongeza wanakagera kwa uvumilivu waliounyesha katika kipindi hiki walichokumbwa na tetemeko la ardhi ambapo hawajayumba kiimani wameendelea kusimama imara.8

 " Sasa hivi mataifa mbalimbali na Dunia kwa ujumla pamoja na Serekali yangu ipo bega kwa bega na wanakagera katika kuhakikisha miundo mbinu iliyo haribiwa na tetemeko ina rudi haraka katika hali yake ya awali"alisema Magufuli.

 Pia Rais Magufuli alilipongeza kanisa katoliki kwa mchango wake mkubwa katika huduma za kijamii kama vile elimu,afya pamoja na huduma zingine  xa kijamii wamekuwa wakifanya vizuri na serekali inautambua mchango wao.

 Naye Askofu mkuu wa jimbo la Mwanza Thadeus Rweiche kwaniaba ya Rais wa baraza la maaskofu Tanzania(TEC) Talicusis Ngaralekumtwa aliwataka wanakagera kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito na kuwataka mapdre wasivunje moyo katika kazi zao za unjilishaji.

Alisema huduma za kiroho zinatolewa katika mazingira mazuri kwasababu serekali inatoa ushirikiano wa bega kwa bega na viongozi wa dini pamoja na waumini.

 Askofu Rweiche alisema semenari ya Rubya ni chimbuko la mapdre kwa Afrika mashariki.
 Waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage akitoa salamu za Rais John Magufuli kwenye ibada ya misa ya uzinduzi wa Jubilei ya miaka 150 ya uinjilishaji na miaka 100 ya upadre Tanzania iliyofanyika kwenye viwanja vya semenary ya Rubya Wilayani Muleba
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akitoa salam za Mkoa kwenye ibada ya misa ya uzinduzi wa jubilei ya miaka 150 ya unjilishaji na 100 ya upadre Tanzania
 Katibu mkuu wa baraza la maaskofu Tanzania (TEC)Padre Raymond Saba akitoa neno la shukrani 
 Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la  Bukoba Method Kilaini akitoa shukrani kwa niaba ya Askofu mkuu wa Jimbo la katoliki Bukoba Askofu Desderius Rwoma kwa wageni na waumi.wote waliohudhuria ibada hiyo
 Baadhi ya maaskofu kutoka majimbp yote Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya ibada
 Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania waliohudhuria ibada hiyo.

Waziri Nnauye azindua Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali zikiwemo za Sanaa na Utamaduni umekuwa chachu kubwa katika kuwajengea uwezo wasanii wetu na kutekeleza shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na wataalamu kutoka pande hizi mbili.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akizindua wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China katika Ukumbi wa Utamaduni wa watu wa China leo jijini Dar es Salaam.


 “Kwa miaka mingi Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano uliotoa fursa kwa watu wake kujifunza shughuli za sanaa na kiutamaduni zilizoko katika kila nchi hivyo kuendeleza na kuuenzi ushirikiano uliopo katika sekta za Sanaa na Stamaduni” amesema Mhe. Nnauye


Mhe. Nnauye amesema kuwa ushirikiano wa nchi hizi mbili umeweza kukua, kuboresha na kuendeleza wasanii wetu hasa katika kipindi hiki cha maonyesho ambapo hutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali ya kiutamaduni na kuwapa wasanii wa hapa nchini fursa ya kufanya maonyesho kama haya nchini China.


Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong amesema kuwa Maonyesho ya Utamaduni wa China hapa nchini yanatoa fursa nzuri kwa wananchi wa Tanzania kuelewa na kujifunza utamaduni na sanaa ya China, kuimarisha ushirikiano wa utamaduni wa China na Tanzania pamoja na kukuza urafiki wan chi hizi mbili.


Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin amesema kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu kwa sekta ya Sanaa na Utamaduni na kujifunza mambo mapya ili kuendeleza Utamaduni, ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.


Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China itakuwa na maonyesho mbalimbali kama vile maonyesho ya sarakasi ya Kichina, maonyesho ya picha, hadhara za opera za China, Udaktari wa kijadi wa China na Utamaduni wa mazoezi maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. (katikati mbele) ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong.

 Kikundi cha Utamaduni na Sanaa cha Jiangxi kikionyesha sarakasi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.

DC DAQARRO AWEKA MAZINGIRA KUHAKIKISHA USALAMA WA CHAKULA

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA

Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro mwishoni mwa wiki hii amekutana na Maafisa Watendaji wa Kata zote za Jiji la Arusha kuzungumzia kuhusu masuala mbalimbali muhimu yanayotakiwa kupewa kipaumbele katika Wialaya hiii. 

Katika Kikao hicho Dc Daqarro ametilia mkazo masuala ya Usalama wa Chakula katika Mitaa yote, Ulinzi na usalama, usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na utoaji wa taarifa za matukio yasiyo ya kawaida yanayotokea katika kila Kata.

Akizungumza katika kikao hicho alisema “nahitaji kupata takwimu sahihi kutoka katika kila Kata ya mahitaji ya Chakula, kiasi kilichopo na namna ambavyo mmejipanga kukabiliana na upungufu endapo utatokea, kila afisa ugani wa eneo husika ahakikishe anatoa elimu ya kutosha na kufuatilia kuhusu usalama wa chakula katika eneo lake na kuwasilisha taariha hizo katika Ofisi yangu. Sitamuelewa mtendaji ambaye kwa kutokuwajibika kwake kutasababisha njaa ama upungufu wa chakula kwa namna yeyote ile.

Aidha alisisitiza kusimamia miradi ipasavyo ili iwe na ubora na iweze kudumu muda mrefu, kusimamia Usalama wa Kata kwa kutoa taarifa za kila tukio lisilo la kawaida linalotokea kila siku na kudhibiti uingiaji wa wageni kutoka nje ya nchi wanaofika katika Kata. 

“Wageni wote wa Nje ya Nchi lazima taarifa zao zifikishwe kwa Afisa uhamiaji wa Wilaya ili kujiridhisha kwamba wameingia nchini kihalali na kuwa na shughuli maalumu iliyowaleta katika maeneo yenu aliongeza”.

Sambamba na hilo alisema si ruhusa kwa Mtendaji wa Kata kutoa mihutasarti kwa ajili ya kumilisha upatikanji wa silaha kwa sababu hivi sasa zoezi hilo limesitishwa mpaka pale Uhakiki wa silaha utakapokamilka hivyo kwa kuwa muombaji ni lazima aanzie kwenye ngazi ya kata si ruksa kwa vikao husika kutoa mihutasari ya aina hiyo.

Mwenyekiti wa Watendaji wa Kata katika Jiji la Arusha Ndg. Suleimani Kikingo alisema kwa umoja watahakikisha kwamba maagizo yote yaliyotolewa wanayatekeleza kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko ya haraka na kutoa hudma bora kwa wakazi wa Jiji hili.
      Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro akizungumza na Maafisa watendaji wa Kata wa Jiji la Arusha (Hawapo Pichani) wakati wa kikao maalumu na watendaji hao kilichofanyika miwshoni mwa juma jijini hapa.

 Mwenyekiti wa Maafisa watendaji wa Kata na Mtendaji wa Kata ya Kati Ndg. Suleimani Kikingo akichangia wakati wa Kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arusha
      Maafisa Watendaji wa Kata waliohudhuria Kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arusha

    Afisa Mtendaji wa Kata ya Levolosi Easter Maganza akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali wakati wa kikao


     Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro(kushoto) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposya wakati wa kikao na watendaji wa Kata.

Serikali yajipanga kukuza ujuzi wa nguvu kazi kwa vijana takribani 15,000 ifikapo 2017

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Serikali ya awamu ya tano imejipanga kukuza ujuzi wa nguvu kazi kwa vijana takribani 15,000 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuwaongezea uzoefu wa kazi na kuongeza fursa za upatikanaji wa ajira.

Ujuzi wa nguvu kazi nchini utatolewa kupitia programu maalum ya mafunzo kazini kwa njia ya Uanagenzi (Apprenticeship), mafunzo kwa vitendo  kwa wahitimu (Internships) pamoja na urasimishaji  wa ujuzi uliopatikana kwa mfumo usio rasmi (Recognition of Prior Learning).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ajira, Ally Msacky alipokuwa akimuwakilisha Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde wakati wa mahafali ya mwisho ya vijana waishio katika mazingira magumu waliohitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World.

Mhe. Mavunde amesema kuwa maendeleo ya nchi yoyote yanategemea nguvu kazi ambayo kwa asilimia kubwa inatoka kwa vijana kwahiyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha vijana wanapatiwa elimu na mafunzo ili waweze kujiajiri au kuajiriwa na hatimaye kupunguza utegemezi na kuongeza pato la Taifa.

“Napenda nitumie fursa hii kuwataarifu kuwa Serikali yetu imetoa kipaumbele cha juu katika kujenga ujuzi wa nguvu kazi, takribani vijana 15,000 watafaidika na programu hiyo kwa mwaka huu wa fedha kwani tayari tumeanza kutekeleza kwa kuingia mikataba na Makampuni ya kutoa mafunzo kwa vitendo katika maeneo ya kazi”, alisema Mhe. Mavunde.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kusimamia Sera ya Taifa ya Ajira na Sera ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa lengo la kuweka msisitizo katika kuweka mazingira na kutoa elimu ya ufundi stadi kwa ngazi mbalimbali ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira na hatimaye kuongeza fursa za ajira nchini.

Aidha Mhe. Mavunde amehaidi kuendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa ukuzaji wa ajira kwa vijana unapewa kipaumbele pia ameahidi kusaidia kuimarisha utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao unawasaidia vijana kupata mikopo kwa masharti nafuu.


Mradi huu wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi - Dar es Salaam (DYEE) kupitia mafunzo ya stadi za kujiajiri (BEST Model) unafadhiliwa na Benki ya NBC na kuratibiwa na Shirika la Plan International, umetekelezwa katika kipindi cha miaka 3 na umetoa mafunzo kwa jumla ya vijana 1,225.


Mkurugenzi wa Ajira, Ally Msacky akisoma hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde alipoenda kumuwakilisha katika mahafali ya mwisho ya vijana waliopo chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi – Dar es Salaaam (DYEE) waliohitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World, kushoto ni Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Plan International – Tanzania, Bi. Gwynneth Wong na kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Robert Mkolla. Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya NBC na kuratibiwa na Shirika la Plan International.  


Mmoja wa vijana waliopo chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi – Dar es Salaaam (DYEE) waliohitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World, Hamis Abdallah akimuonyesha Mkurugenzi wa Ajira - Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Ally Msacky jinsi ya kuchanganya vinywaji na kupata kinywaji kimoja (cocktail) katika siku ya mahafali yao. Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya NBC na kuratibiwa na Shirika la Plan International.

 Mkurugenzi wa Ajira - Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Ally Msacky akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi katika Chuo cha Future World chini ya mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi – Dar es Salaaam (DYEE). Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya NBC na kuratibiwa na Shirika la Plan International.

BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU (NBAA) YAFANYA MAHAFALI YA 38.

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kulia, akiwahutubia wahitimu na jumuiya ya Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) (Hawako Pichani), wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo, yaliyofanyika katika Kituo cha Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Bw. Pius Maneno na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Mafunzo wa Bodi hiyo, Bi. Anne Mbughuni.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akimkabidhi cheti cha kufanya vizuri katika masomo ya taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T), Bi. Happiness Ngowi, wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akitangaza kuwatunuku vyeti wahitimu wa taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T) waliofanya vizuri katika masomo yao, wakati wa mahafali ya 38 ya NBAA, yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Wahitimu waliofanya vizuri katika masomo ya NBAA, baada ya kupokea vyeti vya kutambua umahili wao katika masomo pamoja na kupewa zawadi za fedha taslimu zilizotolewa na wadhamini mbalimbali wa Bodi hiyo, wakati wa Mahafali ya 38 yaliyofanyika katika Kituo cha NBAA, kilichoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, (aliyeketi nafasi ya saba kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi pamoja na wadhamini wa tuzo mbalimbali zilizotolewa kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao, tukio lililofanyika katika kituo cha NBAA, kilichoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto), akisalimiana na Msajili wa Hazina Bw. Laurance Mafuru, baada ya kumalizika kwa mahafali ya 38 ya Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA), yaliyofanyika katika kituo cha Bodi hiyo, Nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
(Picha zote na Wizara ya Fedha) 
 
 

UZALENDO wawapa Ajira za Jeshi wanamgambo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Askari Mgambo walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mara baada ya kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya JWT jana. 
 Askari Mgambo  na wanajeshi walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mara baada ya kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya JWT jana. 


Na: Frank Shija, MAELEZO
UZALENDO umewapatia ajira takribani vijana 70 baada ya Amiri Jeshi Mkuu,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufurahishwa na namna ambavyo washiriki wa zoezi la Amphibia Landing walivyoonyesha umahiri wao.
Hayo yamebainika jana katika fukwe za kijiji cha Baatani, wilayani Bagamoyo, wakati wa hafla kufunga mazoezi hayo ambapo Mhe. Rais Magufuli alisema kuwa kutokana na alivyojionea mazoezi hayo na amearifiwa kuwa kati ya washiriki wa mazoezi hayo wamo mgambo 30 na JKT 40 aliagiza wote waingizwe kwenye orodha ya waajiriwa wapya wa JWTZ.
“Katibu Mkuu Kiongozi nakuagiza Kufanya utaratibu waku waingiza kwenye ajira hawa vijana 30 wa mgambo na 40 wa JKT kwani wameonyesha moyo wa uzalendo kwelikweli, tena ikiwezekana ata kesho waingie kwenye orodha ya waajiriwa wapya”. Alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange kuangalia namna ya kuwapa motishi wote walioshiriki kufanikisha zoezi hilo ili kuwaongezea morali ya kuwajibika.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Majeshi kushirikia hususan katika eneo la unzanzishaji wa viwanda ili kutoa mchango wao katika hasma ya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
“Ni lazima sasa tujipange nataka Majeshi yetu muwekeze katika viwanda iwe kwa kuunganishwa nguvu pamoja ama mmoja mmoja naamini hatushindwi, leteni mpango Serikali itasaidia”. Alisema Rais Magufuli.
Alitolea mfano wa Jeshi la Magereza kuwa na kiwanda cha viatu katika Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro, kushangaa kuona majeshi mengine yananunua viatu kutoka nje ya nchini. Aliwaagiza washirikiane katika kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na viwanda.
Alisema kuwa Jeshi letu limekuwa na mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu yake ambayo aliyataja kuwa ni ulinzi wa mipaka ya nchi, kulinda katiba ya nchi, kufundisha wananchi masuala ya ulinzi wa Taifa, uokoaji na utoaji wa misaada katika maafa, kutoa elimu ya kujitegemea pamoja na ulinzi wa amani na ukumbozi.
Nakuongeza kuwa limeweza kulinda mipaka ya nchi, na kulinda amani iliyopo pamoja na kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kulinda amani katika baadhi ya maeneo ikiwemo Sudan Kusini na DRC Congo.
Septemba Mosi mwaka huu JWTZ walitimiza miaka 52 ya uhai wake,ambapo ilianza kuadhimsha miaka hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile usafi, huduma za upimaji wa Afya Bure na zoezi hili la Amphibia Landing ni muendelezo wa maadhimisho hayo.
Ambapo katika zoezi hilo vifaa kama Meli Vita, Vifaru vinavyo tembea nchi kavu na majini, milipuko pamoja na Ndege vita vilitumika. 

WAZIRI MKUU ASHANGAZWA NA KODI KUBWA SOKO LA DODOMA

$
0
0
*Aagiza Baraza la Madiwani lipitie upya na kumpa majibu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Baraza la Madiwani la Manispaa ya Dodoma lifanye marekebisho ya kodi inayotozwa kwenye soko la Majengo ambayo imepandishwa kutoka sh. 20,000 hadi sh. 150,000 kwa mwezi.
 Amesema anatambua maamuzi ya Baraza ni ya kikao halali lakini hakubaliani na ongezeko hilo ambalo ni sawa na asilimia 650 kwani linawaumiza wananchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba Mosi, 2016) wakati alipotembelea soko hilo akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.

Amesema soko hilo linatakiwa lifanyiwe mapitio ili liwekwe kwenye hali nzuri na Manispaa ihakikishe maboresho hayo yanafanyika bila ya kuwaumiza wafanyabiashara.

“Kwa kuwa uamuzi wa kupandisha kodi ulifanyika kisheria na kupitishwa na baraza la Madiwani, sitaki kuvunja sheria. Nawaagiza mkazungumze tena katika baraza na muangalie namna ya kupunguza gharama hizo,” amesema.

“Hali hii haiwezekani kuachwa iendelee, huku ni kuwaumiza wananchi. Mkurugenzi wa Manispaa nenda kaitishe tena kikao, mfanye mazungumzo upya kwenye baraza lenu na mje mnieleze mmekubaliana nini” amesisitiza.

Pia ameitaka Manispaa hiyo ihakikishe makusanyo yote ya fedha katika soko hilo yanakusanywa kwa njia ya kielektroniki ili fedha hizo ziweze kuleta tija na kuwataka Mkuu wa mkoa na wilaya kuwachukulia hatua wotewatakaobainika kuiba fedha hizo.

Amesema Manispaa hiyo inatakiwa kupanua masoko kwa kujenga masoko mapya makubwa katika maeneo ya Nkuhungu, Kisasa, Mlimwa na Barabara ya Iringa ili huduma hizo zisambazwe.

Mapema akisoma risala yake, Mwenyekiti wa soko hilo, Bw. Godson Rugazama alimueleza Waziri Mkuu changamoto zinazolikabili soko hilo kuwa ni pamoja na ongezeko la kodi isiyozingatia uhalisia wa maisha na shughuli za wajasiriamali sokoni hapo. “Kodi imeongezeka kutoka sh. 20,000 hadi 150,000 kwa mwezi,” alisema.

Mwenyekiti huyo alitaja changamoto nyingine ni uchakavu wa mifereji ya maji machafu, kuvuja kwa paa la soko, bidhaa kuuzwa katika maeneo yasiyokuwa rasmi na kusababisha wateja kutoingia sokoni.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu ametembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma na kukagua maeneo mbalimbali zikiwemo wodi za wagonjwa, jengo la wazazi na jengo jipya la wagonjwa wa Bima ya Afya (NHIF).

Akiwa hospitalini hapo, pia alizungumza na watumishi wa sekta ya afya na kuwataka wawahimize wananchi wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao unawawezesha mtu kulipia bima ya matibabu kwa ajili ya mhusika, mwenza wake na watoto/watemezi wanne na serikali inajazia kiasi kile kile alichochangia.

Akizungumzia miundombinu ya afya mkoani humo, Waziri Mkuu alisema mkoa wa Dodoma hauna shida ya matibabu au utoaji wa huduma ya afya kutokana na miundombinu iliyopo hivi sasa.

Aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu na uaminifu na kuongeza tija katika utendaji kazi wao huku wakitanguliza utunzaji wa mali ya umma.

“Ninawasihi mjenge tabia ya huruma kwa wagonjwa huku mkitambua unyeti wa kazi mliyonayo. Ninaamini mtatunza vifaa mlivyonavyo na siyo kuvichukua na kuvipeleka kwenye zahanati zenu au maduka yenu binafsi ya dawa,” alionya.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAMOSI, OKTOBA MOSI, 2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wafanyabiashara wa soko Kuu la manispaa ya Dodoma la Majengo wakati alipolitembela Oktoba 1, 2016.
 Kama kawaida ya watanzania wengi siku hizi suala la matumizi ya mbango kama njia ya kuwasilisha ujumbe wao kwa viongozi  wafanyabiashara  hawakuzubaa  wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea soko kuu la manispaa ya Dodoma la majengo Oktoba 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa   akitembelea soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo 
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa   akitembelea soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo 
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa   akitembelea soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo 
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Jordan Rugimbana akimkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na wafanyabiashara wa soko kuu la Manispaa ya Dodoma la Majengo baada ya kulitembelea Oktoba 1, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko kuu la Dodoma la Majengo  wakati alipotembelea soko hilo Oktoba 1, 2016. 


UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA SOKONI, MBEYA

$
0
0
* Aagiza Halmashauri kuwapatia mikopo wanawake wajasiriamali waliopo stand ya Kabwe.* Awataka wazazi na walezi kuhakikisha wanasimamia malezi ya watoto wao.

Na Erasto Ching’oro- Msemaji wa Wizara, Mbeya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) amefanya ziara ya kushtukiza katika Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya kwa ajili ya kuongea na wanawake wajasiriamali wanaofanya biashara katika stendi hiyo ili kufuatilia utekelezaji wa Ilani kuhusu Halmashauri kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake. Akiongea na Wanawake hao Waziri Ummy Mwalimu amewataka kujiunga katika vikundi ili kuwawezesha kukopesheka na kupata fursa mbalimbali za biashara ikiwemo mafunzo na masoko.

Mhe. Ummy, alieleza kuwa Serikali itahakikisha inawapa mikopo yenye riba nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, na pia kuweka mazingira wezeshi ya kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zao katika mazingira salama. Hivyo amewasisitizia kuwa ni muhimu wajiunge katika vikundi ili waweze kufikiwa na fursa za huduma za masoko na mikopo kwa kwa wepesi zaidi. 

Kwa upande wao, wanawake wajasiriamali hao katika stendi ya Kabwe walisema changamoto kubwa waliyonayo ni kukosa mitaji na masoko hali ambayo ilimlazimu Waziri Ummy kumuagiza Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha anawapatia mikopo wanawake wa Standi ya Kabwe ndani ya mwaka huu wa fedha wa 2016/17.

Pia akiwa katika soko hilo, Waziri Ummy ameeleza kufurahishwa na jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe William Paul Ntinika kwa kuwahamasisha wajasiriamali hao kufanya biashara zao katika mazingira ya usafi kwa kufanikisha matumizi ya meza za kufanyia biashara katika eneo hilo. Mhe. 

Waziri Ummy alitoa rai kwa Halmashauri nyingine kuiga mpango wa kufanya biashara katika mazingira ya usafi ili kuhakikisha tunadumisha usafi wa miji yetu na mazingira ya maeneo ya wafanyabiashara wadogowadogo. 

Aidha, akiwa Mkoani Mbeya Waziri Ummy alitembelea Mahabusu ya Watoto iliyopo katika Jiji la Mbeya. Akiongea na watoto takribani 16 waliopo katika Mahabusu hiyo Waziri alieleza kuwa Serikali itahakikisha watoto waliopo mahabusu wanapata haki zao zote za msingi hususan haki ya kupata elimu kwa maendeleo na ustawi wao. 

Hata hivyo, Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto wote nchini kuhakikisha wanawalea watoto wao katika misingi bora itakayo wawezesha kuwa na tabia njema. Hii itasaidia kupunguza idadi ya watoto wanaokinzana na sheria na kupelekea kufikishwa katika mahabusu za watoto. 

Waziri alionya kuwa makosa mengi yanayowakumba watoto waliopo mahabusu msingi wake mkubwa ni malezi mabaya yanayo pelekea watoto kukosa maadili ambayo hujikuta wamehusishwa na makosa ya mauaji, wizi, ubakaji na ulawiti. Hivyo kila mzazi ano wajibu wa kulea watoto katika maadili na tabia njema ili kuepuka migogoro ya kisheria. 

Aidha, Watoto hao waliopo mahabusu ya watoto Mbeya walimuomba Waziri Ummy kusaidia kuharakisha kusikilizwa kwa mashauri ya kesi zinazowakabili zilizopo mahakamani ili waweze kurudi nyumbani, wakiwa huru na kuendelea na masomo.

Waziri Ummy yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya Kazi ya siku 2 ambapo pia tarehe 01 Oktoba 2016 atakuwa Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kitaifa eneo la Rujewa, Wilayani Mbarali.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb.) akikagua usafi wa eneo la soko la wanawake wajasiriamali, alipofanya ziara ya kushitukiza katika soko lililoko Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya tarehe 30/9/2016. 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb.) akiongea na wanawake wajasiriamali, alipofanya ziara ya kushitukiza katika soko lililoko Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya ili kufuatilia utekelezaji wa Halmashauri kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake. (30/9/2016)

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb.) akiongea na wanawake wajasiriamali, alipofanya ziara ya kushitukiza katika soko lililoko Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya ili kufuatilia utekelezaji wa Halmashauri kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake. 

HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD: IMPORTANT NOTICE TO LOAN APPLICANTS FOR 2016/2017

$
0
0
During the exercise of processing 2016/2017loan application forms, the Board has come across loan applications which are missing some vital information such as applicant’s and guarantor’s signatures. For that reason, the Board would like to inform loan applicants with such incompleteness to visit HESLB offices in Dar es Salaam.
Loan applicants and/or their guarantors who have not signed their documents are required to physically visit HESLB offices on Plot No. 8, Block No. 46 Sam Nujoma Road, Mwenge, Dar es Salaam to append signatures to their loan applications from Monday 3rd October 2016.
Loan applicants who did not attach applicant’s photo, guarantor’s photo (to their application forms) or who attached uncertified photocopies of birth certificates, academic certificates, guarantor’s particulars such as photocopy of Passport or voter’s registration cards; should send the missing particulars with covering letters indicating their full names and form four index numbers with year of completion e.g. S0143.0012.2013 via EMS through the following address:

The Executive Director,
Higher Education Students’ Loans Board,
P. O. Box 76068,
DAR ES SALAAM.



The deadline for correction of the shortcomings is Friday 7th October 2016.


All attachments must be certified by a Commissioner of Oaths.

NB:    The Board is:
•    Cautioning loan applicants to be careful with some unscrupulous individuals who might take advantage of this opportunity to make financial demands.
•    Reminding loan applicants that correction of missing items is not a guarantee to be awarded loans.
•    Incomplete application forms will not be considered for further processing until the missing information is provided within specified time.



This notice is also available in the HESLB’s website (www.heslb.go.tz) 

TICTS YASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI KTI SHULE YA SEKONDARI KURASINI JIJINI DAR

$
0
0
 KAMPUNI ya TICTS inayojishughulisha na kazi ya uendeshaji wa huduma za bandari, Dar es salaam imeendelea na kampeni ya yake ya "Go GREEN" kwa kupanda miti katika eneo la Shule ya Sekondari Mivinjeni, Wilayani Temeke.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti jijini hapa, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa alisema ili Tanzania ifikie lengo la kuwa na uchumi wa kati kufikia mwaka 2015, suala la upandaji miti ni lazima kufanyika ili kuenda sambamba mkakati huo.

"Tukiwa na miti michache au miti iliyotoweka, tutaangamia kama taifa na ikiwa tutakuwa na miti mingi, hapo hatuna cha kupoteza, ila tukiruhusu ukataji miti uendelee katika nchi yetu bila kupanda mingine, tutaishia kuwa ombaomba kama si kufa kwa njaa" alisema Talawa.

Pia alitoa wito kwa makampuni mengine yanayofanya biashara hapa nchini, kuisaidia Serikali kuhamasisha masuala yenye manufaa kwa taifa kama hilo la kupanda miti.
 Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa akishiriki kupanda Mti katika eneo la Shule ya Sekondari Kurasini, kupitia Kampeni yao ya "Go GREEN" yenye kuhamasisha jamii umuhimu wa kupanda miti. 
 Meneja wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari wa Kampuni ya TICTS, Hassan Mageta (kati) akimwagilia maji mti wake muda mfupi baada ya kuupanda katika eneo la Shule ya Sekondari Kurasini, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2016.
 Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya TICTS, Caroline Owenya (kushoto) akishirikiana kupanda mti na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kurasini, Mwl. Marcelino Fussi (katikati) pamoja na mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2016.
Wafanyakazi wa Kampuni ya TICTS wakipanda miti.

SERIKALI IMEUNDA TIMU YA WATAALAMU - WAZIRI MKUU

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeunda timu ya wataalamu ambao watatoa ushauri juu ya suala zima la kuhamishia makao makuu Dodoma.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Oktoba 1, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa Serikali wa mkoa wa Dodoma, wazee wa mkoa huo, wafanyabiashara pamoja na viongozi mbalimbali kwenye ukumbi wa mikutano wa Dodoma (Dodoma Convention Centre).

“Tumeunda timu ya watu 10 ambao ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa miji mikuu, hawa wana uzoefu wa kuangalia makao Makuu ya nchi yanafananaje. Watakuja Dodoma, wapitie master plan na kisha watapita kwenye maeneo kadhaa ya mji ili waone hali halisi ikoje ndipo watupe maoni yao,” amesema.

“Tunataka tusirudie kosa la Jiji la Dar es Salaam la kulazimika kubomoa makazi ya watu kila inapolazimu kufanya uboreshaji wa miundombinu. Hawa watu watatuambia wapi tunatakiwa tuweke njia nne au sita za magari, wapi tuweke bustani au wapi tujenge nyumba za ghorofa moja, mbili, tatu au zaidi,” ameongeza.

Akifafanua kuhusu miundombinu, Waziri Mkuu amesema timu hiyo pia itatakiwa kutoa ushauri juu ya wapi ijengwe njia ya malori tu au mahali gani zinahitajika kujengwa barabara za juu (flyovers) ili kuepusha msongamano katikati ya mji wa Dodoma.

Bila kutaja majina ya wajumbe wa timu hiyo, Waziri Mkuu amesema timu hiyo itaongezewa wataalamu kutoka China na Malaysia ambao nchi zao tayari zina uzoefu wa kuhamisha makao makuu ya nchi zao zaidi ya mara moja.

Alitumia fursa hiyo kuwaeleza watumishi juu ya uwepo wa Tume ya Kuboresha Maslahi ya Wafanyakazi ambayo imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka jana. “Kuna vikao vimekuwa vinafanyika tangu mwaka jana baina ya Serikali na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kwa lengo la kujadili uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi, na jambo hili linaendelea vizuri,” amesema.

Kuhusu madeni ya watumishi wa umma, Waziri Mkuu amewasihi watumishi wawe na imani na Serikali yao kuhusu madeni hayo na kwamba ikimaliza uhakiki unaofanyika hivi sasa, kila mwenye stahili zake atalipwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ihakikishe inakamilisha upimaji wa viwanja 100,000 kama ilivyojipangia ili watumishi hao pamoja na wananchi waweze kupatiwa viwanja haraka iwezekanavyo.

“Nimearifiwa kuwa mna mpango wa kupima viwanja 100,000 kwa ajili ya kuwapatia wananchi na watumishi. Kamilisheni utaratibu huo haraka ili watumishi wapewe viwanja na waweze kujenga nyumba zao za kuishi,” amesema huku akishangiliwa.

Natambua kuwa mmekubaliana kuanzisha utaratibu wa kuingiza viwanja kwenye mfumo wa kompyuta ili kuepuka double allocation. Harakisheni zoezi hilo ili kama itawezekana, kabla ya Novemba kazi hiyo iwe tayari na watu wapatiwe viwanja chini ya mfumo huo mpya,” amesisitiza.

Kuhusu huduma za kijamii kama elimu, umeme, maji na masoko, Waziri Mkuu amewahakikishia watumishi hao kwamba Serikali imeangalia kila eneo na kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa ili kuboresha utoaji wa huduma hizo. Amewataka watumishi hao wabadilike na wawe tayari kuwapokea watumishi wenzao watakaowasili kwa awamu kuanzia mwezi huu.
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA
JUMAMOSI, OKTOBA MOSI, 2016.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa serikali na Taasisi zake mjini Dodoma Oktoba 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa serikali na Taasisi zake wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao mjini Dodoma Oktoba 1, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)


VOA Swahili: Wamarekani wasema Clinton amemshinda Trump kwenye Mdahalo

CHEF ISSA APEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KATIKA SHEREHE YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 25 YA CHUO CHA KIMATAIFA CHA UTALII SWITZERLAND (IMI )

$
0
0
Tarehe 28/9/2016 Ilikua ni siku ya heshima kubwa sana kwa Mtanzania mzalendo Issa Kapande maarufu kama chef Issa kupata mualiko wa kujumuika katika chakula maalumu cha jioni  kilichoandaliwa Hotel National Luzern Switzerland maalumu kwa Alumni (wahitimu) 50 tu bora waliofanikiwa kitaaluma na kifani katika biashara au ajira toka pande zote za dunia kuanzia chuo kilipoanzishwa miaka 25 iliyopita.
Tarehe 29/10/2016 Ilikua ni siku maalumu ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa chuo cha IMI miaka 25 iliyopita,  chuo hiki ni moja ya vyuo bora vya fani ya hotel na utalii nchini Switzerland. Sherehe ziliudhuliwa na watu mbali mbali toka mataifa 30 duniani.
Kwa ufupi Chef Issa ni mpishi wa kimataifa mzalendo anaeipeperusha vyema bendera ya taifa letu la Tanzania kwa kushinda tuzo mbali mbali katika mashindano mbali mbali duniani. Chef Issa ni mmiliki wa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika balani Ulaya ujulikanao kwa jina Tanzanian Restaurant. 
Pia chef Issa amekua akifundisha mpishi kwa njia ya blog www.activechef.blogspot.com hapo utaweza pata mafunzo ya mapishi ya kila aina. 

Kwa kupata taarifa zaidi za unaweza like Facebook page hii:
Habari nzuri kwa Watanzania ni kwamba Chef Issa ameweza kupigania na kupata nafasi za upendeleo kwa Mtanzania yeyote yule atakaependa kwenda kusoma fani ya hotel na utalii chuo cha IMI international Hotel Management Institute Switzerland atapewa nafuu ya ada na chuo kitamsimamia kupata leaving and work permit kipindi chote atakachokua masimoni. 
Kama una mwanao au ndugu yako basi wasiliana na Chef issa kwa email active.chef@yahoo.com 

GOLI LA KUSAWAZISHA LA SIMBA DHIDI YA YANGA

SIMBA NA YANGA ZATOKA SARE 1-1, MASHABIKI WANG'OA VITI, MABOMU YARINDIMA

$
0
0
 HAKUNA mbabe, ule mtanange uliokuwa unasuburiwa kwa hamu kubwa uliohusisha mahasimu wawili Yanga na Simba umemalizika jioni ya leo kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.
Katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa kwa kila upande, Yanga walifanikiwa kupata goli dakika ya 26, baada ya Amisi Tambwe kumzidi mbinu beki Novat Lufungo wa Simba na kuandika goli la kuongoza huku nahodha Jonas Mkude akipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwamuzi kwa kudai kuwa Tambwe aliushika mpira kwa mkono.
Mpira ulisimama kwa dakika takribani tano kutokana na  vurugu kutokea ikiwemo mashabiki wa Simba kuanza kung'oa viti na kuvirusha uwanjani, hali iliyopelekea Jeshi la Polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia iliyojitokeza uwanjani hapo.
 Mpaka ilipofika mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa goli 1-0, lakini kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Kelvin Yondan aliyekuwa na kadi ya njano na kuingia Andrew Vicent "Dante", Saimon Msuva akachukua nafasi ya Juma Mahadhi, Haruna Niyonzima akiingia baada ya Deus Kaseke, Simba wakimtoa Laudit Mavugo na kuingia Fredrick Blagnon, Ibrahim Ajib na kuingia Mohamed Ibrahim na Novat Lufungo na kuingia Jurko Murshid.
Mchezo uliokuwa wa kasi kwa kila upande huku Yanga wakitafuta goli la kuongoza na Simba wakisaka la kusawazisha, ambapo dakika ya 89 Shiza Kichuya anawainua mashabiki wa Simba baada ya kupiga kona iliyoenda moja kwa moja wavuni na kusawazisha na kudumu mpaka dakika 90. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

Beki wa Yanga, Juma Abdul akimchezea rafu kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (Mchezo wa Watani wa Jadi), uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam leo. Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. 
Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya akishangia baada ya kuipatia timu yake goli la kusawazishi dhidi ya Watani wao wa Jadi, Yanga ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiipatia timu yake goli, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
 Mabomu ya machozi yarindima jukwaa la mashabiki wa Simba ili kutuliza ghasia iliyojitokeza uwanjani hapo.
Mshabiki akipiga mateke viti vilivyong'olewa na kurushwa uwanjani 

Extended services limited

YALE YALEEEEEE.... MASHABIKI WA SIMBA WALIPOHUJUMU UWANJA WA TAIFA BAADA YA YANGA KUPATA BAO...

$
0
0

 Afisa habari wa Simba SC Haji Sunday Manara akikimbilia upande wanaokaa mashabiki wao kujaribu kutuliza jazba zilizopelekea kung'olewa kwa viti na kutupwa uwanjani baada ya Yanga kupata bao 
 Afisa habari wa Simba SC Haji Sunday Manara akijaribu bila mafanikio kutuliza jazba za mashabiki wa timu yake waliokuja juu baada ya Yanga kupata bao na wao kupinga kwa kuwa mfungaji alinawa.

 Mshabiki akipiga mateke viti vilivyorushwa uwanjani kwa jazba
Askari polisi akiangalia wakati mshabiki wa Simba SC akijaribu kumtuliza mwenzie mwenye jazba.

TASWIRA ZA AMIRI JESHI MKUU RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOFUNGA MAFUNZO YA MEDANI YA KIVITA

$
0
0


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani mkoa wa Pwani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa akiwa  na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA.



Viewing all 110009 articles
Browse latest View live




Latest Images