Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1368 | 1369 | (Page 1370) | 1371 | 1372 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu
  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.


  Serikali imesema gharama za kujenga upya shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ni Sh. Bilioni 60 hadi kukamilika miundombinu yake ambayo itakayoruhusu wanafunzi kupata elimu kama kawaida. 
  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu leo mjini Bukoba alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo. 
  Katika kukamilisha ujenzi wa shule hizo, Mkuu wa mkoa amesema kuwa hatua ya kuvunja majengo yote imeshaanza ambapo tayari Kampuni ya CHICO ya Wachina inaendelea na uvunjaji wa majengo yote ili kazi ya ujenzi uanze.. 
  “Wataalam wote wa ujenzi kutoka idara mbalimbali za Serikali wanaendelea na uchambuzi yakinifu wa majengo mapya ya shule hizo utakaozingatia viwango vya ujenzi ambapo ghrama za awali kwa tathmini iliyotolewa na wataalamu hao ni Sh. bilioni 30 kwa shule za Ihungo na Nyakato” alisema Meja Jenerali Mstaafu Kijuu.


  Uamuzi wa kuzijenga shule hizo upya zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi, ulipelekea Serikali kuzifunga na kuwahamisha wanafunzi waliokuwa wanasomea katika shule za Sekondari Ihungo na Nyakato ili waweze kuendelea na masomo wakati shule zao zinajengwa upya. 
  Wanafunzi wa shule hizo tayari wamepangiwa shule watakazoenda ili kuendelea na masomo kulinhgana na mihula ya mwaka na ratiba za vipindi vya masomo kila siku. 
  Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amesma kuwa katika kuhakikisha ujenzi wa majengo ya taasisi za Serikali na wananchi yanakuwa imara na salama, wataalam wa Wakala wa Jiolojia Tanzania ndio watatoa ushauri wao kabla ya ujenzi mpya haujaanza ili ujenzi wa majengo mapya ufanyike sehemu sahihi. 
  Kuhusu misaada inayotolewa na Serikali, nchi rafiki, wadau na wananchi, Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Kamati ya Maafa katika kukabiliana na athari za tetemeko kwa wananchi walioathirika tayari imetoa mahitaji mbalimbali kwa waathirika wa tetemeko hilo. 
  Mahitaji yaliyotolewa kwa wananchi ni pamoja na unga wa sembe kilo 3,450, sukari mifuko 410, mchele kilo 3,150, maharage kilo 5,753, maji katoni 850, sabuni katoni 24, mashuka 90, mablanketi ya watu wazima na watoto 2,020, vyandarua 1,274, sare za wananfunzi 570, magodoro 694, mahema 127 na matrubali 2,760. 
  Aidha, mkuu huyo wa mkoa amezitaka Kamati za Maafa za Wilaya zikarabati miundombinu ya kutolea huduma za kijamii ikiwemo shule za sekondari na msingi, vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoharibiwa na tetemeko la ardhi ili huduma hizo muhimu ziweze kurejea mara moja na kutoa huduma kwa wananchi.

  Hadi sasa wamebaki jumla ya majeruhi 13 ambapo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wamebakia majeruhi tisa, Hospitali ya Mugana majeruhi wawili na Hospitali ya Rufaa ya Bugando majeruhi wawili ambao wanaendelea kupata huduma za matibabu na hali zao zinaendelea vizuri. 
  Tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, 2016 Mkoani Kagera lilisababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, majeruhi 427 tayari wametibiwa na kuruhusiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa na vituo mbalibali vya afya kwenye mkoa.
  0 0

  Kutoka Shoto ni muwakilishi wa Timu ya Zalagoza Fc akipokea Zawadi ya kombe kutoka kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Mh.David Mwasilindi Mara Baada ya timu hiyo kuibuka mshindi katika ligi ya Mobisol Cub ligi iliyo andaliwa na kusimamiwa na kampuni ya kuzalisha Nishati ya Umeme wa Jua Mobisol ambao kwa sasa wanahudumia mikoa 17 Tanzania Kusambaza nishati ya Umeme wa Jua na kwa yeyote atakaye hitaji taarifa zaidi kuhusu Mobisol anaweza kupiga simu kituo cha huduma kwa wateja 0800 755 000 Bure.
  Burudani ikitolewa na Vijana Wa Mobisol kampuni Inayozalisha umeme bora na wenyekiwango wakitoa burudani katika Fainali ya Mobisol Cup kwa mwaka huu iliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya Hivi karibuni.
  Mchezaji wa Timu ya Mbeya City B akijiribu kuwatoka wachezaji wa Timu ya Zalagoza Fc waliopigilia uzi mweupe Katika Fainali ya Mobisol Cup ambapo Timu ya Zalagoza Fc Ilibuka Mshindi na kupewa KItita cha shilingi milioni tatu, Mshindi wa pili ni Mbeya City B ambao nao walilamba kitita cha shilingi Milioni Moja Ikifuatiwa na Mshindi wa Tatu Fellaly Fc ambao nao walichukuwa kitita cha Shilingi Laki Tano kama mshindi watatu kutoka katika Kampuni ya Kuzalisha nishati ya Umeme  Bora na Salama wa Jua Tanzania Mobisol.
  Baadhi ya Kikosi kazi cha Timu ya Mobisol Katika Picha Ya Pamoja ambao waliwachapa Vilivyo Timu ya Wanahabari wa Meya Gori Tatu kwa Moja Katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

  0 0

  Na Shamimu Nyaki-WHUSM  
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura ametoa agizo kwa wasanii nchini kuhakikisha wanasajili kazi zao katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili watambulike kwa mujibu wa Sheria.

  Agizo hilo amelitoa jana Jijini Dar es Salaam  alipokuwa anazindua Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA) ambapo amewaahidi wasanii kuwa wakijisajili watatambulika  na itakuwa rahisi kwa Serikali kujua changamoto wanazozipata na kuzitatua kwa urahisi.

  “Napenda mtambue kwamba suala la Urasimishaji linakwenda sambamba na uwepo wa Haki Miliki ya kazi za ubunifu, nawashauri mtunze Haki Miliki zenu na msiziuze na wale wabunifu  wapya na ambao hamjasajili kazi zenu nawaomba mfanye hivyo ili kuepuka uharamia”.Alisisitiza Mhe. Anastazia.

  Aidha Mhe.Naibu Waziri amewaomba wadau wote wa Sanaa kutoa maoni yao katika kuboresha tasnia hii yenye kubeba maeneo kama Muziki, Filamu, Maonyesho, Ususi, na Uchoraji ili kuwezesha tasnia hii kujulikana na  kuboresha mapato ya Wasanii.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza amewataka Wasanii kutunza vibali wanavyopatiwa na Baraza hilo kwani ndio utambulisho wao popote wanapokuwa na inakuwa rahisi wao kusaidiwa wanapopata changamoto.

  “Wengi wenu mmejisajili lakini wale wachache ambao bado naomba mfanye hivyo ili sisi tuwatambue na Sheria ya  Haki Miliki pia iwatambue”.Aliongeza Bw.Muingereza.

  Naye Msanii wa Uchongaji Bibi Hapiness Mmbaga amewashauri wanawake kupenda fani hiyo na kuacha dhana inayosema kuwa kazi hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu kwani ulimwengu wa sasa umebadilika hakuna tena kuchagua aina ya kazi ya kufanya.

  Tamasha la siku ya Msanii duniani linaadhimishwa kwa mara tatu mfululizo ambalo linalenga kuthamini mchango wa kazi za Sanaa hapa nchini ambao kauli mbiu yake  ni “Nguvu ya Sanaa”na kilele chake itakuwa ni tarehe 26 mwezi oktoba mwaka huu.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akizungumza na Wasanii kuhusu umuhimu wa kusajili kazi zao wakati wa uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza laTaifa la Sanaa (BASATA) pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production  lililofanyika  Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.   Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza akitoa maelezo mafupi kuhusu siku ya Msanii Duniani wakati wa uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza hilo pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production lililofanyika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Haak Neel Production Bw. Emmanueli Maendeka akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa Kampuni yake katika uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa  pamoja na Kampuni yake lililofayika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akiangalia baadhi ya kazi za Sanaa kutoka kwa Wasanii wakati wa  uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production  lililofanyika  Septemba 24 Jijini Dar es Salaam
   Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akiangalia baadhi ya kazi za Sanaa kutoka kwa Wasanii wakati wa  uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani


  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akimkabidhi Cheti cha ushiriki  Bw.Adrian Nyangamale Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi katika uzinduzi wa  Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza laTaifa la Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production  lililofanyika  Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.


  0 0  0 0  0 0

   Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
  Shirika la Kiristo la Kuhudumia Wakimbizi Tanganyika (TCRS) limechangia vifaa vyenye jumla ya Sh. milioni 60.92 ikiwa ni mchango wao wa kuwafuta machozi wanakagera baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi. 
  Katika kuhakikisha hali za wananchi na ttaasisi za kutolea huduma za kijamii  zinaimarika na kurudi kwenye hali ya kawaida, wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi bado michango yao inahitajika. 
  Akikabidhi mchango huo, Mratibu wa Miradi inayoendeshwa na TCRS Oscar Rutenge pamoja na Jasmine Gwamsy wametaja mchanganuo wa msaada huo kuwa ni pamoja na blanketi, 1680, mashuka 840, ndoo za kutumia 840, nguo za kutumia kwawanawake, wanaume na watoto box 50, sabuni katoni 1680 pamoja na vifaa vingine 2250. 
  Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amemelishukuru shirika hilo kwa mchango wao huo kwani ni wa thamani hasa baada ya tetemeko hilo kuwaaathiri wananchi wa mkoa huo. 
  Aidha, Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewakaribisha na kuwataka wadau wengine waguswe kwa namna ya kipekee na waendelee kutoa michango yao waweze kuwasaidia wananchi na kurudisha hali yao  na kuendelea na shughuli zao za kijamii na kimaendeleo.

  Mkuu wa msafara wa Shirika la Kiristo la Kuhudumia Wakimbizi Tanganyika (TCRS) Jasmine Gwamsy akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu vifaa vyenye thamani ya jumla ya Sh. milioni 60.92 ikiwa ni mchango wao wa kuwafuta machozi wanakagera baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi.

  0 0

  Na Mwandishi Maalum,New York
  Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amasema, Afrika itandelea kubaki nyuma kielimu ikiwa jitihada za makusudi hazitafanyika kuwekeza katika elimu.
  Ametoa kauli hiyo jana jumamosi mbele ya maelfu kwa mamia ya wakazi wa Jiji la New York waliofurika Central Park kuhudhuria tamasha maarufu lijulikanalo kama Global Citizen Festival.
  Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka huwaleta pamoja viongozi kwa kada mbalimbali, wanaharakati na idadi kubwa ya waungaji mkono wa juhudi za kuutokomeza umaskini uliokidhiri na limeandalia na mtandao wa Uraia wa Kimataifa ( Global Citizen) kwa pamoja na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Elimu ( Global Partnership for Education) .
  Rais Mstafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni  Kamishna wa Kamisheni ya Kimataifa kuhusu elimu akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa jiji la New York katika tamasha la Global Citizen Festival lililofanyika Central Park. Kupitia tamasha hilo, Mhe.Kikwete aliichagiza jumuiya ya kimataifa kuchangia na kuwekeza katika elimu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho. Pamoja naye ni Makamishna wenzie, Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Australia Julia Gillad.
  Aidha fedha zinazopatika kupitia tamasha hilo hutumika katika kusaidia masuala ya kimandeleo kama yakiwamo ya afya, elimu, mazingira, usalama wa chakula pamoja na masuala yanayohusu wanawake na watoto wa kike.

  Ni katika tamasha hilo ambalo mwaka huu limelenga pamoja na masuala mengine, fursa ya elimu kwa watoto wote ambapo, Rais Mstaafu Kikwete ambaye pia ni Kamishna katika Kamisheni ya Kimataifa kuhusu Elimu, ameitaka jumuiya ya kimataifa kupitia hadhara hiyo kusaidia na kuwekeza katika eneo hilo muhimu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho.
  Umati wa wakazi wa jiji na New York waliojitokeza katika tamasha hilo fedha zinazopatikana kipitia tamasha hilo hupelekwa kusaidia masuala mbalimbali ya kijamii. Tamasha hilo lilitumbuizwa na wanamziki maafuru akiwamo Rihanna ambaye ametangazwa kuwa Balozi wa Elimu.

  “ Afrika yangu, itakuwa makazi ya vijana bilioni moja ifikapo mwaka 2050, na tayari ipo nyuma kielimu” akasema Kikwete na kuongeza. “Kama hatutawawezesha vijana wote sasa kwa kuwapatia ujuzi na maarifa , uchumi utapoteza kiasi cha dola 1.8 trilioni na watoto 800 milioni hawata kuwa shuleni ifikapo mwaka 2030. 
  Na hii ni gharama ya kutoelimisha sasa” Rais Mstaafu aliyezungumza na halaiki hiyo kwa pamoja na Makamishna wenzie, Waziri Mkuu wa Norway Bi. Erna Solberg na Waziri Mkuu wa zamani wa Australia, Bi. Julia Gillard ambaye ni pia ni Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Kimataifaka kuhusu Elimu ( GPE).Amesisitiza kwamba “ Ni lazima tujenge kizazi kinachojifunza kwa kuogeza fedha kiasi cha dola 3 trilioni ifikapo mwaka 2030. Washirika wa maendeleo ni lazima waungane nasi katika misheni yetu hii, na sehemu kubwa ya fedha lazima zitoke katika vyanzo vya mapato vya ndani”.
  Rais Mstaafu akibadilishana mawili matatu na Waziri wa Mazingira wa Nigeria Amina Mohammed ambaye naye alikuwa mmoja wazungumzaji katika tamasha hilo.

  Katika harakati hizo za kuwafikishia fursa ya elimu watoto wote wa kike na kiume, Global Partnership for Education and Global Citizen, wamemtangaza mwanamziki maarufu wa Marekani Rihanna kuwa Balozi wa Elimu ambapo kupitia Taasisi yake ya Clara Lionel watafanya kampeni ya pamoja na Global Partinship for education na Global Citizen kuhakikisha kwamba watoto wote wa kike na wa kiume wanapa fursa ya elimu bora.
  Jukumu jingine la mwanamsiki huyo ni pamoja na kuwahamasisha viongozi wa dunia kuunga mkono uwekezaji katika elimu nchini mwao.
  Rihanna na wanamziki wengine maarufu walitumbuiza katika tamasha hilo.
  Rais Mstaafu Kikwete akisalimiana na Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power walipokutana kwenye tamasha hilo.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu
  WAKATI Serikali ya Tanzania ikiwa imenunua ndege mbili za aina ya Bombardier Dash8 Q400 kutoka Canada, imebainika na kusisitizwa kuwa ndege hizo zina usalama mkubwa, zinatumia mafuta kidogo na kutabiriwa kuwa nguzo muhimu kwa usafiri wa bei chee wa ndani ya nchi mbalimbali.

  Hayo yamo katika makala iliyoandikwa na kuchapishwa na jarida mashuhuri duniani la Forbes ikiwa na anuani “Can Bombardier’s Q400 Save Regional  Air Service in the US?” ambapo mwandishi anafafanua faida za ndege hizo ikilinganishwa na nyingine zinazofanya usafiri wa ndani Marekani.“Bombadia ina kasi nzuri na ya kutosheleza mahitaji ya safari za ndani kwa kiwango cha kuwa na faida zaidi kibiashara ikilinganishwa na ndege nyingine za aina yake kama ATR,” linaandika Forbes.
  Faida nyingine inayotajwa ya Bombardier ni matumizi ya mafuta. Forbes wanaandika kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutumia mafuta kidogo sana kiasi kwamba hata bei ya tiketi zake itakuwa chini na kuwasaidia abiria wengi wa ndani.“Kutumia kwake mafuta kiasi kunaifanya Bombardier kuwa na ufanisi wa asilimia kati ya 48 mpaka 50 za kuwa bora zaidi ya ndege nyingine za ukanda huu,” linaandika Forbes.
  Forbes wanasisitiza kuwa kutokana na gharama za matengenezo kupanda, na gharama nyingine za uendeshaji ikiwemo mishahara mizuri kwa marubani, kuna uwezekano mkubwa kwa Bombardier kuendeshwa kwa bei rahisi na ikauza tiketi kwa bei rahisi zaidi kuliko ndege nyingine.
  “Kwa sasa tunakadiria kuwa ndege aina ya Bombardia ndio zitakuwa mbadala na zitashika njia nyingi za ndani (Marekani) kwa kiasi cha asilimia 50 hadi 60 na zitasaidia kurejesha usafiri uliositishwa (kutokana na gharama kubwa kwa ndege nyingine) katika viwanja takribani 20,” linaandika zaidi Forbes.Akikaririwa katika makala hiyo,  Mike Arcamone, Rais wa Masuala ya Biashara wa Bombardier anasema wasiwasi wa awali wa abiria kuhusu ndege hizo kutumia mfumo wa turbo sasa umeondoka kwa kuwa injini na dizaini ya kisasa ya ndege hizo inaifanya isiwe na kelele kama ilivyodhaniwa.
  “Wanunuzi wengi wa ndege hizi wamebaini kuwa hazina kelele na watumiaji wengi wanaamini kuwa zinaweza kuwa mbadala wa ndege nyingine za bei nafuu,” anasema afisa huyo kauli inayokubaliwa na wachambuzi wa Forbes.
  Tayari Serikali ya Tanzania imeahidi kuleta ndege nyingine ya pili wiki hii baada ya ile ya kwanza kuwasili nchini wiki iliyopita ukiwa ni mkakati na utekelezaji wa ahadi ya Rais John Pombe Magufuli ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
  Kuwasili kwa ndege hizo kunaashiria mengi lakini muhimu ni uthabiti wa ahadi za Dkt. Magufuli akiwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake, ambapo mambo mengi makubwa ambayo ameyaahidi ameanza kuyafanyiakazi na kuwakuna wengi nchini na nje ya nchi.  0 0


  0 0

   WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia uwanjani kukagua timu ya Wabunge mashabiki wa Yanga na wabunge mashabiki wa Simba katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo wakati mchezwa hisani ya kuchangishafedha kwa ajili wahanga watetemeko la ardhi, mkoani Kagera.Yanga walishinda bao 5-2

   WAZIR Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi wengine na timu wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza mechi ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Wabunge mashabiki ya Yanga na wabunge mashabiki wa Simba. Yanga walishinda bao 5-2

   WAZIR Mkuu Kassim Majaliwaakikagua timu kabla ya kuanza mechi ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Wabunge mashabiki ya Yanga na wabunge mashabiki wa Simba. Yanga walishinda bao 5-2
   Mshambuliaji wa timu ya wabunge mashabiki wa Yanga,Ridhiwan Kikwete akiwatoka wachezaji  wabunge mashabiki wa Simba. Yanga walishinda bao 5-2

  Mshambuliaji wa timu ya wabunge mashabiki wa Yanga akiwa,Mwigulu Nchemba akiwapiga chenga wabunge mashabiki wa Simba. Yanga walishinda bao 5-2. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii


  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Padri Jackson Sosthenes (kushoto) na Padri Johnson Lameck wakati alipowasili katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam kushiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. 
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia waumini wa  kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam baada ya  Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  0 0


  Waombolezaji wa kipeleka jene nyumbani kwa marehemu, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam le tayari kwa shughuli ya kuagwa na hatimaye viwanja vya Leaders Club ambapo mwili wa marehemu ulikwenda kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam leo.
  Mwandishi wa Habari, Grace Nackso akimfariji mjane Frigeria Adolf Kivamwo wakati wa ibada fupi ya kuaga mwili wa marehemu Adolf Saimon Kivamwo nyumbani kwake Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam leo.

  Waombolezaji wakiwa katika shughuli hiyo. 


  0 0

  Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, wakipatiwa maelezo na Mtendaji Mkuu wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari, juu ya fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Dodoma, wakati wa Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Dunia kanda ya Afrika uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda hivi karibuni. Mkutano huo uliandaliwa na COMESA kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda.
  Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, wakimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari, alipokuwa akiwaelezea juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Mkoani Dodoma, wakati wa Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Dunia kanda ya Afrika uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda hivi karibuni. 

  0 0  Mwandishi wetu, Mwanza

  Chacha Masinde kutoka mkoani Mara ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jana jijini Mwanza baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:03:00, akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya David Kilimo aliyetumia muda wa saa 01:04:40

  Mbio hizo za kilomita 21 zilianzia Uwanja wa CCM Kirumba kupitia Barabara ya ikulu ndogo hadi mzunguko wa samaki na kuelekea Buzuruga kisha kutokea barabara ya pasiansi na kumalizikia uwanjani Kirumba huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella akishiriki kukimbia mbio za km 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.

  Nafasi ya tatu upande wa wanaume ilichukuliwa na Mkenya Moris Mosima aliyetumia muda wa saa 01:04:57, ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.

  Akizungumzia siri ya ushindi wake, Chacha siri ya mafanikio hayo ni kujituma kwake zaidi katika kufanya mazoezi maalum kwa ajili ya mashindano hayo ili kuhakikisha kwamba mwaka huu mshindi wa kwanza katika mbio hizo anatoka nchini Tanzania tofauti na miaka ya nyuma ambapo washindi walikuwa wakitoka nchini Kenya.

  “Niliweka nadhiri nikasema mwaka huu lazima mshindi atoke Tanzania zaidi niwe mimi na ninashukuru nimetimiza adhama yangu. Pamoja na hilo maandalizi ya mwaka huu yamekuwa mazuri zaidi mahitaji yote muhimu yakiwemo maji tukiwa njiani yamesaidia mafanakinio hayo licha ya washiriki kuwa zaidi mwaka huu hatua ambayo iliongeza changamoto kwetu zaidi,’’ alisema.

  Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mtanzania pia Faimina Abdi kutoka mkoani Arusha aliyetumia muda wa saa 01:13:12 akifuatiwa na mwenzake kutoka mkoani Arusha Angelina Daniel aliyetumia saa 01:14:38 huku Mkenya Dorifine Omary akishika nafasi ya tatu akitumia saa 01:16:54

  Washindi wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya nane jijini Mwanza waliibuka na kitita cha Sh1.5 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh900,000 na washindi watatu Sh700,000.

  Mashindano hayo ya kila mwaka yaliyokatika kalenda ya RT yaliandaliwa na Kampuni ya Capital Plus kwa udhamini kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB, New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door.

  Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi kwa washindi na washiriki wa wa mbio hizo Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella ambae pia alishiriki mbio hizo kwa kukimbia mbio za km 5 alisema mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kuirudishia nchi heshima yake katika mchezo huo.

  “Ndio maana tumekuwa tukisisitiza wadhamini waendelee kujitokeza kusaidia mbio hizi ili ziendelee kuwa bora zaidi,’’ aliongeza.

  Akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba kwa niaba ya Katibu tawala jana, Afisa michezo mkoa waMwanza James William alisema mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha wetu nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kuirudishia nchi yetu heshima ya kipekee katika mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

  Alisema: “Tanzania inaweza kurejea katika ramani ya dunia kwenye michezo kama tukijikita katika maandalizi mazuri ya kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wetu nchini hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi.”

  Naye Mbunge wa jimbo la Ilemema ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Ntumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula alipongeza waandaaji wambio hizo na kutoa wito kwa washiriki walioshindwa kufanya vizuri kwenye mbio hizo kutokata tama bali wajiandae na mashindano yajayo ili waweze kufanya vizuri.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema mbio hizo zimeweza kufanyika kwa mafaniko makubwa na ushirikiano walioupata kutoka uongozi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani huku pongezi pia zikielekezwa kwa jeshi la polisi kwa kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama .
  Chacha Masinde kutoka mkoani Mara akimaliza Rock City Marathon na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mbio hizo zilizofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana . Chacha alitumia muda wa saa 01:03:00 kumaliza mbio hizo akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya David Kilimo aliyetumia muda wa saa 01:04:40.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw John Mongella sambamba na maofisa kutoka benki ya NMB wakishiriki mbio za za km 5.
  Washiriki wa mbio za km 21 wakiondoka Uwanja wa CCM Kirumba kuanza safari ndefu.
  Ushindani ulikuwa ni mkubwa!  0 0

   Ashara Mubaraka are the first 10 days of Moharram, that mark the martyrdom of Imam HusainAS, grandson of Prophet MohammedSAW, that took place fourteen centuries ago. This is a very important religious and spiritual event in the Dawoodi Bohra Calendar.  Each year, Dawoodi Bohras across the world observe Ashara Mubaraka by attending religious sermons, mourning the tragedy of Karbala and remembering the supreme sacrifice of Imam HusainAS.   

  Imam HusainAS refused to pledge allegiance to Yazeed, a tyrannical ruler who had transgressed all that Islam stood for and had established a reign of oppression after coming to power. In the battle of Karbala, Imam HusainAS along with seventy two of his followers including his family fought bravely on the scorching sands of Karbala and acquired martyrdom.  The oppressors had totally denied them food and water for 3 consecutive days and even Imam HusainAS’s six month old son was martyred in the battlefield of Karbala.  Imam HusainAS made this supreme sacrifice so that truth may prevail, tyranny be exterminated and the cherished human values of righteousness, piety and virtue may ever remain supreme and uncompromised.

  Following the footsteps of his predecessors, each year, 53rd al-Dai al-Mutlaq, His Holiness Dr. Syedna Mufaddal SaifuddinTUS,on receiving requests and invitations from his followers from different towns and cities, chooses a venue for delivering sermons during Ashara Mubaraka.  In this Islamic year, 1438 H, the city of Dar es Salaam is blessed to have been chosen as the venue for Ashara Mubaraka, which will be from the 2nd to the 11th of October, 2016.  
  With the encouragement and blessings of His Holiness’ predecessors, a few Dawoodi Bohras made their homes in Tanzania more than two centuries ago. They came here principally to carry on business and trade. Finding the country a land of opportunities and experiencing the welcoming nature of the Tanzanians, they subsequently settled and made their homes in Tanzania.  The Dawoodi Bohras of Tanzania and those of Dar es Salaam, in particular feel extremely privileged to host this event and expect to host about 30,000 guests from all over the world including East Africa.

  During Ashara Mubaraka sermons, His Holiness Dr. Syedna Mufaddal SaifuddinTUS will narrate the tragic events of Karbala and shower pearls of wisdom upon his followers, mentoring them on the noble teachings of Islam and the principles of humanity that Imam HusainAS sacrificed his life for.  During these auspicious days, His Holiness will pray for the victims of the earthquake in Kagera region. His Holiness and his followers, the Dawoodi Bohra community, offer support and help to the efforts of the Government of Tanzania in rebuilding and providing relief to the victims of the earthquake in Kagera region.  It is also the intention and desire of Anjuman-e-Saifee (Dar es Salaam) to launch a scheme for the support of those affected by the calamity.

  Wherever he travels, His Holiness reminds his loyal followers of the noble teachings of Islam that “love for the land of abode is an essential part of the faith” and that “religion is not just prayer and fast but also to strive for betterment in this world and hereafter”.  He guides them to strive for the betterment of their neighbours and for the common good of all the people of their country.  His Holiness guides and directs his followers to invest in trade and industry in Tanzania and has dedicated resources to assist them to work hand in hand with other members of the society and for the country at large.  Following the guidance and directions of His Holiness, the Dawoodi Bohras residing in Tanzania continue to contribute to the growth and development of their country.  

  The anticipated arrival of His Holiness to Dar es Salaam is on Tuesday, 27th September at 1300 Hrs.

  0 0   

  Tanzania has registered ten (10) entries under nine (9) categories in the World nominations 2016 for the World Travel Awards organized by the World Travel Awards that will take place on 2nd December 2016 at the Olhuveli Beach & Spa Resort in the Republic of Maldives. Under the  Africa nominations 2016, thirty two (32) entries for Tanzania have been recorded under 17 categories. 

  The winner of this competition will be decided by votes. Voting for the World and Travel Technology nominations opens online on Friday, 23rd September 2016 and will end on Monday, 24th October 2016. The voters will be travel professionals and consumers with a vote cast by qualifying travel professionals carrying a weighting of two votes.
  “We are delighted to inform you of your nomination in the 23rd annual World Travel Awards and I congratulate your achievement” says Graham Cooke, the President of World Travel Awards.

  Tanzania’s ten entries with their categories in brackets are:  Tanzania (World’s Leading Safari Destination 2016); Zanzibar-Tanzania (World’s Leading Dive Destination 2016); Zanzibar - Tanzania (World Leading Island Destination); and Mt. Kilimanjaro-Tanzania (World’s Leading tourist attraction).

  Others are: Diamond La Gemma dell’Est Zanzibar -Tanzania (World’s Leading Beach resorts 2016); Essque Zalu Zanzibar - Tanzania (World’s Honeymoon Resort 2016); &Beyond Mnemba Island Lodge-Tanzania and Singita Sasakwa Lodge – Tanzania (World’s Leading Luxury Lodge 2016); &Beyond Mnembo Island Lodge Zanzibar – Tanzania (World’s Leading Private Island Resort 2016) and Chumbe Island Coral Park – Tanzania (World’s Leading Conservation Company).

  This comes five months after Mount Kilimanjaro which is the highest mountain in Africa, and the highest free-standing mountain in the world, being declared Africa’s leading tourist attraction in 2016 during the World Travel Awards Africa and Indian Ocean Gala Ceremony held in Zanziba Tanzania on 9th April 2016. 

  The World Travel Awards was founded in 1993 to recognize, acknowledge and reward excellence in the travel, tourism and hospitality industry worldwide. This year’s World Travel Awards is celebrating its 23rd anniversary. Its brand is now recognized globally as the hallmark of quality, with winners setting the benchmark to which all others aspire.

  Issued by:

  PUBLIC RELATIONS OFFICE
  TANZANIA TOURIST BOARD
  Sept 26, 2016.

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheri kushoto akiwa pamoja na Makamo Mwenyekiti Maryam Ishau Abdalla wakionesha vyeti vyao walivyopatiwa baada ya kuchaguliwa na kuzungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
  kil1
  Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Maryam Ishau akisisitiza jambo alipozungumza na Waandishi wa Habari kuelezea mikakati walioiweka baada ya kuchaguliwa,katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
  kil2
  Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa Mwenyekiti pamoja na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar kuelezea mikakati walioiweka baada ya kuchaguliwa,katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
  kil3
  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheri akifafanua baadhi ya maswala yalioulizwa na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa kuelezea mikakati yao walioiweka baada ya kuchaguliwa,katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
   

  PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Maofisa Misitu wanne na kusimamisha shughuli za uvunaji wa mazao ya misitu wilayani Rufiji kwa muda usiojulikana baada ya kutoridhishwa na usimamizi wake.

  Maofisa waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Dk. Paul Ligonja, Ofisa Misitu wilaya Gaudens Tarimo, Ofisa Misitu Yonas Nyambuya na Ofisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wa wilaya Seleman Bulenga.

  Waziri Mkuu amefanya uamuzi huo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Rufiji kwenye ukumbi wa halmashauri kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanya jumba la maendeleo wilayani Rufiji.

  Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Njwayo kukusanya magogo yoye yaliyoko msituni na kuyapiga mnada na kuitaka  wizara ya Maliasili na Utalii kwenda wilayani Rufiji kufanya uchunguzi wa leseni za uvunaji walizozitoa kwa wilaya hiyo.

  Waziri Mkuu amebainisha kwamba wilaya ya Rufiji ni moja kati ya wilaya inayoongoza kwa uvunaji wa mazao ya misitu bila ya kufuata taratibu licha ya kuwa na maofisa misitu.

  “Hakuna mafanikio katika sekta ya misitu kwenye wilaya hii ya Rufiji. Nasimamisha shughuli zote za uvunaji wa mazao ya misitu pamoja na watendaji wake kwa sababu hatuwezi kuacha watu wanakata magogo bila ya kufuata taratibu,”

  “Haiwezekani Rufiji iwe shamba la bibi, nimesimamisha uvunaji wa magogo hata kwa wenye leseni hadi tuzichunguze zimetoka wapi. Hatuwezi kuruhusu maofisa wanashiriki vitendo vya hujuma kwa kuvuna misitu Rufiji na kugonga mihuli ya Kilwa kisha fedha wanatia mifukoni,” amesema.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Rashid Salum kufuatilia maagizo aliyoyatoa kuhusu kizuizi cha Ikwiriri kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipokutana na watumishi wa wizara hiyo.

  Julai 18 mwaka huu Waziri Mkuu alikutana na watumishi wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam  na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea kuwa na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji.

  Waziri Mkuu aliitaka wizara hiyo kupunguza idadi ya vizuizi vya ukaguzi wa mazao ya misitu kwenye  barababara  mbalimbali baada ya kukosa tija, alitoa mfano wa barabara ya kwenda mikoa ya kusini  kuanzia Dar es Salaam yenye vizuizi visivyopungua sita na kila kizuizi kinatumika kwa ajili ya kukagua mazao ya misitu na maliasili inayotoka kuvunwa.

  Awali mbunge wa Rufiji Mohammed Mchengelwa alilalamikia vitendo vya dharau vinavyofanywa na watumishi wa sekta mbalimbali katika wilaya hiyo jambo linalosababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao. 

  0 0

   Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) na Naibu Spika wa Baraza hilo  Mhe Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea.
   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu toka kulia) akifuatilia kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati alipowatembelea. Wapili kulia ni Spika wa Baraza hilo Mhe Zuberi Ali Maulid na wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (kulia) na Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma (kushoto).
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  WAKATI Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania akishikilia msimamo kuwa nchi yake haitasaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) na Jumuiya ya Ulaya (EU) mpaka dosari kadhaa zitakaporekebishwa, baadhi ya wabunge wa EU wamemuunga mkono na kutahadharisha mkataba wa sasa utaua viwanda vya ndani.

  Siku kadhaa zilizopita, msimamo wa Tanzania na Burundi ulilazimisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kukubaliana kusogeza mbele makubaliano ya ama zote zisaini mkataba huo au la ili kuruhusu uchambuzi zaidi.
  Tayari nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zimekubaliana na mkataba huo wa EPA huku Tanzania na Burundi zikitoa sababu nzito za kiuchumi zinazolenga kuhakikisha kuwa kabla ya kusaini mkataba huo ni vyema suala la ulinzi wa viwanda vya ndani likazingatiwa. Mkataba huo unapaswa kusainiwa na nchi zote ili uanze kutumika katika ukanda mzima

  Chini ya mkataba huo ambao majadiliano yake yalianza tangu mwaka 2007 EU inaahidi kuzipatia bidhaa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki soko kwa kutotozwa kodi zinapopelekwa kwa nchi wanachama wa Ulaya lakini na yenyewe italeta bidhaa zake katika soko la ukanda bila kutozwa kodi.

  Hata hivyo, msimamo wa Tanzania umesimama katika ulinzi wa viwanda vya ndani hasa wakati huu Serikali ikijikita zaidi katika uchumi wa viwanda. Msimamo huo sasa unaungwa mkono na wabunge wawili wa EU Marie Arena na Julie Ward, ambao wanashauri Afrika Mashairiki isisaini mkataba huo wa ubia kwa namna ulivyo sasa.

  Katika mahojiano yao maalum na mwandishi wa mtandao wa jarida mashuhuri la The New Times, wabunge hao wanasema bayana kuwa uamuzi wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wa kuahirisha kusaini ubia huo hadi mwakani ili watafakari zaidi uko sahihi.

  “Tunaamini mkataba huu kwa namna ulivyo sasa hauko sawa. Ulaya inaitumia Kenya ambayo ndiyo yenye maslahi zaidi katika mkataba huu kuwa kama ngao yao. Wakati Kenya ilishaendelea kiviwanda, hali sio kama hivyo kwa Tanzania, Uganda na Burundi ambazo hazitafaidika.

  “Iwapo bidhaa za Ulaya zitaruhusiwa kuingia tu katika ukanda wa Afrika Mashariki italeta ushindani usio wa haki na zaidi nchi hizo zitapoteza kodi katika baadhi ya bidhaa na pia baadhi ya viwanda vitashindwa ushindani na kufa,” wanasema wabunge hao.

  Wabunge hao wananukuliwa wakisisitiza kuwa kutokana na hali hiyo wamejitolea kuzisaidia nchi kama Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kuzishinikiza nchi za Ulaya zipitie upya ubia huo na kuanzisha mfumo mpya wenye manufaa kwa pande zote.

  “Tunadhani nchi hizi zinapaswa kusubiri mpaka zote zitakapoingia katika uchumi wa kipato cha kati ndipo zinaweza kuingia mikataba kama hii yenye kuleta ushindani wa kibiashara. Kwa Rwanda na nchi zingine za EAC sisi tunaona kwa sasa wangeimarisha kwanza soko lao la ndani katika ukanda huo,” wanaongeza wabunge hao.

  Wabunge hao wanafafanua kuwa kwa sasa Kenya ambayo imeshaingia katika uchumi wa kipato cha kati inaweza kufaidika lakini wanaonya nchi nyingine hazitafaidika na EPA mpaka hapo watakapofikia uchumi wa kati.

  Walipoulizwa ni kwa nini wakiwa wabunge wa Ulaya bado wanapingana na mkataba huo utakaoipa faida za kiuchumi jumuiya yao, wabunge hao walijibu:

  “Hoja yetu sio kupinga biashara na Afrika Mashariki, tunachotaka ni kuona ubia huu unanufaisha pande zote. Tunazo taarifa nyingi za kitafiti hata kutoka Kituo cha Kimataifa cha Biashara zinazoonesha kuwa mkataba huu utakuwa na hasara kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

  Wabunge hao wanazidi kufafanua kuwa mikataba mibovu inayoingiwa na Ulaya na Afrika inaathari nyingi ikiwemo kusababisha umaskini Afrika na matokeo yake kuleta athari mbaya kwa Ulaya ikiwemo kuongezeka kwa wahamiaji haramu.


older | 1 | .... | 1368 | 1369 | (Page 1370) | 1371 | 1372 | .... | 3284 | newer