Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1369 | 1370 | (Page 1371) | 1372 | 1373 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (wapilikulia), akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango mkubwa wa  wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia), wakati wa uzinduzi wahafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanjawa Kalangala la mkoani Geita, na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Geita Ezekiel Kyunga (kushoto) na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Kamanda Mohamed Mpinga.
   Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani, Mheshimi wa Hamad Masauni amesema kuwa bado kuna matukio mengi ya ajali za barabarani nchini zinaso sababisha vifo vya wananchi wengi hivyo kuna haja ya kuongeza nguvu katika kampeni za Usalama barabarani ili kupunguza tatizohili.Wasanii wa maigizo wa Futuhi wa kitumbuiza kwenye viwanjawa Kalangalala mkoani Geita, wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, yenye kauli mbiu” Hatuta kiajali,tunataka kuishi”.
  NAIBUWaziri Masauni aliyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa mkoani Geita ambapo pia alitumia fursahiyo kuyapongeza makampuni ya kibiashara na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayosaidiana na serikali kupitia Jeshi la Polisi kufadhili na kuendesha kampeni za Usalama barabarani.
  “Pamoja na kuwepo na matukio mengi ya ajali serikali inafarijika kuona yapo makampuni ya kibiashara na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanashirikiana kwa karibu na serikali kupitia Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani kuendesha kampeni za Usalama barabarani kwa jamiii kiwemo kufadhili shughuli za uhamasishaji Usalama katika Wiki hii ya Nenda kwa Usalama barabarani”.Alisema Mh.Masauni.
  Aliongeza kuwa jukumu hili  la kutoa elimu ya Usalama barabarani sio la Jeshi la polisi pekee bali kunahitajika ushirikiano kutoka  kwa wananchi wote kwa kuwa kila mmoja ni mtumiaji wa barabara na vyombo vya usafiri na aliwataka madereva kuzingatia sheria na kanuni za Usalama barabarani.
  Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha kampeni za Usalama barabarani kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Usalama barabarani na Kikosi cha jeshi la  polisi cha Usalama barabarani.
  Katika miaka mitatu mfululizo Vodacom imekuwa ikifadhili Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani ambapo mwaka huu imetumia zaidi ya shilingi milioni 48 kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza matukio ya ajali nchini katika uhamasishaji wa usalama katika kipindi hiki. 
  pia imekuwa ikiendesha kampeni za usalama kwa madereva na makundi mbalimbali ya jamii kwa kushirikiana na wadau wengine wa masuala ya  usalama barabarani. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia,amesema kuwa Vodacom itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza matukio ya ajali nchini. 
  “Kama Kampuni ya mawasiliano tumekuwa tukiendesha kampeni inayojulikana kama ‘Wait to Send’ ambayo imekuwa ikihamasisha madereva kutotumia simu za mkononi wakati wanaendesha vyombo vya moto ikiwemo kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi”.Alisema Mworia.
  Mworia pia alisema kuwa kampuni imekuja na mkakati wa kuhakikisha elimu ya usalama barabarani inawafikia wanafunzi wa shule za msingi ili wawe wakiwa na uelewa wa umuhimu wa kuzingatia kanuni za usalama barabarani ambapo kwa kushirikianana Jeshi la Polisi imekuwa ikiendesha mafunzo kwa wanafunzi wa shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini.

  0 0

  Waziri nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, uratibu, bunge, vijana na watu wenye ulemavu) Mhe  Jenister Mhagama ametoa siku saba kwa taasisi za serikali, wizara,makampuni na watu binafsi kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)

  Vilevile Waziri Mhagama imeiagiza Bodi za wadhamini za mifuko mingine ya hifadhi ya jamii kuhakikisha wanawasukuma wadeni wao kulipa madeni yote wanayodaiwa ili kuiwezesha mifuko hiyo kujiendesha kwa ufanisi zaidi.

  Waziri Mhagama alitoa tamko hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni huku akitumia fursa hiyo kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, Bw Erick Shitindi  kuhakikisha uongozi wa mifuko hiyo unampatia ripoti ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wote walioshindwa kulipa madeni yao.

  “Ninafahamu fika kuna mikataba ambayo ilisainiwa na pande zote mbili kabla ya kutolewa kwa hiyo mikopo na makubaliano mengine hivyo naomba basi mikataba hiyo itumike kufanikisha agizo hili,’’ alisema.

  Pia alimuagiza  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe kuhakikisha kwamba anampatia ripoti muafaka  ya utekezaji wa agizo hilo.
  "Kwa niaba ya serikali, ninataka kuona kwamba wadaiwa wote wa mifuko hii bila kujali nafasi zao kiuchumi au kisiasa wanalipa madeni wanayodaiwa…hii lazima ijumuishe makampuni, wawekezaji na taasisi za serikali,’’ alisema.
  Awali,Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema licha ya mfuko wake kufanikisha utekelezeaji wa miradi mbalimbali ikiwemo majengo bado wateja wake wengi hawajalipa madeni wanayodaiwa na mfuko huo ikiwemo watu binafsi, taasisi za serikali na zile binafsi wakiwemo pia wale walionunua nyumba za shirikal hilo.
  Kwa mujibu wa Prof. Kahyarara, shirika hilo bado linadai takribani sh bilioni 20 kutoka kwa wa wapangaji wake, deni linalohusisha pia dola za kimarekani milioni 1.2.Kiasi kingine cha bilioni 86 kinadaiwa kama adhabu kutoka kwa waajiri walioshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao.
  Madeni mengine ni pamoja na deni la sh milioni 42 na Dola za kimarekani milioni 35.9 ambazo zilitolewa  kama mikopo kwa sekta binafsi mbalimbali huku mkopo mwingine  wa sh bilioni 38 ulitolewa kupitia SACCOS na bado hazijarejeshwa.
  “Hata hivyo tumeanza kuchukua hatua mahususi kwa kulingana na matakwa ya sheria kuhakikisha kwamba madeni yote yanalipwa,’’ alibainisha Prof Kahyarara.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu huo kufuatia mikopo hiyo shirika litachukua hatua dhidi  wadeni wake hatua iliyosababisha baadhi ya wadaiwa hao kwenda mahakamani kupinga huku uamuzi wa mahakama kuhusu suala hilo ulitarajiwa kutolewa leo (Jumatatu).
  Akiwa kwenye miradi ya shirika hilo Waziri Mhagama alionyesha kuridhishwa na miradi hiyo iliyoanza mwaka 2014 na inatarajiwa kukamilika mwisho mwa mwaka 2016 ukihusisha ujenzo wa nyumba 439 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu zikiwemo zile ambazo zitapangishwa. 
   Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu   Mhe. Jenister Mhagama akizungumza na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe.
   Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Mhe. Jenister Mhagama akiwa ameambatana na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe. (kushoto) akizungumza mbele ya Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Mhe. Jenister Mhagama wakati waziri huyo alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia). 
   Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia) akizungumza mbele ya Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu Mhe.  Jenister Mhagama wakati waziri huyo alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe (kushoto).

  0 0

  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatumia fursa hii kufafanua kwamba, msimamo alioutoa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji  Francis Mutungi (pichani) kuhusu mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF una maana kwamba, kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa kwake  na pande mbili zinazosigana na kwa mujibu wa Katiba ya CUF toleo la 2014, Msajili alijiridhisha kwamba, Profesa Lipumba bado ni Mwenyekiti halali wa Taifa wa chama cha CUF, kwa sababu alitengua barua yake ya kujiuzulu kabla haijakubaliwa na mamlaka yake ya uteuzi, kama inavyoelekeza ibara ya 117(2). 


  Aidha, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaviasa vyombo vya habari kufanya jitihada za kuelewa msimamo wa Msajili wa Vyama vya Siasa, badala ya kuandika habari au makala zinazopotosha umma. 


  Hivyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatumia fursa hii pia, kukanusha taarifa zinazoenezwa katika vyombo vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii kwamba, "Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kuwa, hakumrudishia Profesa Lipumba Uenyekiti wa Taifa wa CUF, bali Profesa Lipumba kajirudisha mwenyewe kinyemela". 

  Habari hiyo siyo ya kweli, imepotoshwa kwa makusudi. Watanzania wanapaswa kuipuuza.

  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inawaasa viongozi wa kitaifa wa chama cha CUF, kusoma kwa makini msimamo uliotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kuuheshimu, kwani kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, Msajili wa Vyama vya Siasa anao wajibu wa kujiridhisha kwamba, mabadiliko yoyote yaliyofanywa katika uongozi wa taifa wa chama cha siasa, ni halali na yamefanywa na mamlaka halali kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika.


                                                          Sisty L. Nyahoza                           

                                               Kny: MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA               

   26 Septemba, 2016   0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dkt. Othman  Kiloloma akimuonyesha mkuu wa wilaya  ya Arusha
  Mhe. Gabriel Daqarro sehemu ambayo mtoto amefanyiwa upasuaji wa kichwa


   kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma akiwa anampa mkuu wa wilaya ya Arusha maelekezo ya picha inayoonyesha jinsi mtoto alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji
   mkuu wa wilaya ya Arusha mjini akimkabidhi pampas moja ya mama mzazi wa mtoto ambaye amefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa ikiwa ni moja ya zawadi walizopatiwa na GSM Foundation

   mkuu wa wilaya ya Arusha akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa kikubwa


  Na Woinde Shizza, Arusha

  Jumla ya watoto 4,000 wanazaliwa kila mwaka na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi na kati ya hao ni watoto 500 tu ndio wanafikishwa hospitalini kwa ajili ya upasuaji huku wengine 3500 haijulikani wanapopelekwa.


  Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu  Muhimbili (MOI) Dkt. Othman  Kiloloma wakati akiongea na waandishi Wa Habari Mkoani hapa.

  Alisema kuwa  wao kama taasisi ya MOI  walikaa chini na kuona kuna watoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya garama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho amesema si kweli.

  Alibainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 ambayo ni awamu ya kwanza na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.

  "Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 atujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma

  Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji Wa kichwa Nasson Daniel 17 aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman 17aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.

  Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada .

  "Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa mud a mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto ,tusisikilize dhihaka za watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa kinaendelea kupungua ,tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.

  Naye Mkuu wa wilaya ya Arusha  Mhe. Gabriel Daqarro alitoa wito kwa jamii hususan  wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto anapona kabisa .

  Aliwashukuru madaktari hawa walioibua na kuangalia namna gani wanaweza kusaidia watoto  hawa pamoja na shirika la GSM foundation ambao ndio waliothamini Huduma hii ya upasuaji bure  ambapo alisema kwa upande wa Arusha jumla ya watoto 35 wameonwa huku watoto sita wakiwa wamekishwa fanyiwa upasuaji.

  0 0

  Vijana wa Bukoba Mpya wampongeza Profesa  Anna Tibaijuka kwa ushindi wa Tuzo ya 'HRH Prince Khalifa Bin Salman Al Khalifa Award for Suitanable Development' Sherehe za utoaji wa tuzo hizo umefanyika juzi katika viwanja vya makao makuu ya umoja wa mataifa  jijini New York, Marekani, na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali duniani wakiwemo mabalozi, mawaziri  na viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa.
  Bi Happiness Essau,Katibu, Vijana wa Bukoba Mpya akimpongeza Mama Anna Tibaijukakatika kongamano la Bumudeco lililofanyika  mjini Bukoba Desemba  27, 2015 


  Salaam za pongezi kwa 
  Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka

  Tumepokea kwa furaha isiyo kifani taarifa ya ushindi wako wa Tuzo ya 'His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award for Sustainable Development'. Ushindi huu ni uthibitisho mwingine juu ya kutambulika kwa juhudi na kuthaminiwa kwa jitihada zako katika kuendeleza makazi.
  Tunaona fahari kwa kazi kubwa uliyoifanya kuubadilisha Mtaa wa Kibera nchini Kenya na kwa hakika, halitafutika jina la Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka kwenye miradi mikubwa ya makazi na mazingira inayoendelea kutekelezwa katika nchi za maziwa makuu (Nile Basin Initiatives, Land Reform and Urban Planning, Lake Victoria Environmental Management Programme, n.k).
  Toka uhuru, ukiachilia mradi wa SADELIN, Kagera haina kumbukumbu ya kuletewa mradi mkubwa kwa nguvu na jitihada za Serikali. Lakini upo ushahidi usiofutika juu ya jinsi ushawishi wako kwenye ashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na UNDP ulivyoisaidia Kagera kufikiriwa pamoja na mikoa mingine na hatimaye kupata miradi ya maendeleo.
  Nahau za mfumo‐dume husema ‘Omwatani Takweeta Mushaija’ na iko hivyo pia katika maandishi ya Vitabu vitakatifu kwamba ‘Nabii Hakubaliki Nyumbani Kwake na Kwa Watu Wake’ Tunasikitika kwamba haya yote yamekuwa kweli hata kwako pia. Kama tulivyoeleza katika kitubio chetu kwenye mkutano wa BUMUDECO, vijana wa Bukoba Mpya tunajutia zaidi kwamba nasi tulishiriki kukusurubisha pasipo kutafuta kuujua ukweli. Tulipelekwa na upepo wa matukio na tukajinyima nafasi ya kutathmini malengo ya matukio. Tunazidi kukuomba msamaha na kuwaombea wengine wote ambao ukweli haujafunuliwa kwao ikiwemo watakaotusi pongezi hizi. Tunakuahidi kuwa watakao baki katika fikra za zamani ni wale wasiokuwa wetu lakini sisi vijana wa Bukoba Mpya tutasimama daima na watu wetu ikiwemo wewe.
  Pamoja na pongezi hizi za jumla, tunaomba mara urejeapo nchini na upatapo muda, ujumuike na uwakilishi wa Bukoba Mpya‐Tawi la Dar es Salaam kwa hafla fupi ya kukupongeza.

  Imetolewa na
  Happiness Essau
  Katibu, Vijana wa Bukoba Mpya


  0 0

  BENKI ya NMB imeendelea kutoa elimu kwa viongozi wa Halmashauri, Manispaa, Majiji na wananchi wa kada mbalimbali juu ya huduma za kibenki ambazo wamekuwa wakizitoa kupitia mkutano mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala na Serikali za Mitaa (ALAT) unaofanyika kitaifa mjini Musoma mkoani Mara ambapo wajumbe zaidi ya 500 wanahudhuria mkutano huo. 
  Benki hii imetoa elimu kwa viongozi wa Halmashauri, Manispaa, Majiji na wananchi wa kada mbalimbali juu ya huduma za kibenki katika Mkutano mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala na Serikali za Mitaa (ALAT) unaofanyika kitaifa mjini Musoma mkoani Mara ambapo wajumbe zaidi ya 500 wanahudhuria mkutano huo.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akisalimiana na meneja wa NMB tawi la Musoma, Sebastian Kayanga alipokuwa anaingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwembeni Complex kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa mwaka wa ALAT Taifa. NMB imedhamini mkutano wa ALAT Taifa kwa shilingi Milioni 206 ikiwa ni gharama za mkutano na zawadi kwa ajili ya Meya bora wa Mwaka. Pichani kulia ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Amos Mubusi.
  Kupitia mkutano huo NMB imeelezea jinsi ilivyounganisha mfumo wake wa kibenki na mfumo wa serikali za mitaa (LGRCIS) kufanikisha ukusanyaji mapato ya kwa wakati na bila kupotea na kuandaa vituo vya makusanyo ya fedha kusaidia serikali katika makusano.Akitoa mada kwenye mkutano huo ulioingia siku ya 2 hii leo,Afisa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa (NMB) Augustino Mbogella,amesema licha ya kusaidia serikali katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, benki hiyo pia imesaidia miradi ya maendeleo ya jamii ikilenga zaidi katika utoaji wa misaada katika sekta ya elimu  na afya.

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) George Simbachawene,akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la NMB kwenye maonyesho ya ALAT.

  Mkaguzi Mkuu wa ndani wa (NMB) Augustino Mbogella (pichani),amesema licha ya kusaidia serikali katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, benki hiyo pia imesaidia miradi ya maendeleo ya jamii ikilenga zaidi katika utoaji wa misaada katika sekta ya elimu  na afya.

  Mbogella amesema mwaka 2015 pekee zaidi ya shule 140 za msingi na sekondari zilipata zaidi ya madawati 7,000 kwa Tanzania nzima katika mpango wa kuendelea kutatua tatizo la madawati mpaka kufikia septemba 2016 tayari wametumia zaidi ya milioni 900. “Upande wa afya tumetoa vifaa mbalimbali kwenye hospitali 50 za serikali pamoja na vituo vya afya ambapo kiasi cha fedha takribani shilingi milioni 200 zilitumika” alimalizia Augustino Mbogella. 
  Wakati huo, viongozi na wananchi wameombwa kutembelea banda la NMB ili kuweza kupata elimu zaidi likiwemo pia suala la ufunguaji wa akaunti mbambali kwenye benki hiyo ambazo zina manufaa makubwa.


  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR – ZNZ.
  Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran imeahidi kuendelea kutoa fursa zaidi ya Mafunzo ya Elimu ya juu kwa wanafunzi wa Zanzibar katika mpango wake wa kuimarisha uhusiano uliopo kati yake na Zanzibar uliodumu kwa muda mrefu sasa.  
  Fursa hizo zitazingatiwa zaidi katika fani ya Uhandisi kwa vile Visiwa vya Zanzibar tayari viko katika maandalizi ya utafiti wa mafuta na gesi ikijiandaa kuelekea katika uimarishaji wa Sekta ya nishati itakayosaidia kubadilisha uchumi wa Zanzibar katika miaka michache ijayo.
  Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Balozi Hussein Mollale Abdullahi alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Balozi Hussein alisema Iran kwa vile imebarikiwa kuwa na rasilmali nyingi zilizopelekea kuongoza nafasi ya Pili katika uzalishaji wa mafuta na Gesi Duniani imejitolea kuunga mkono Mataifa Rafiki katika azma ya  Mataifa hayo kujenga uwezo zaidi wa kujitegemea.
  Akizungumzia miradi ya kujitegemea Balozi Hussein alisema Taifa lake lilioko Mashariki ya Kati tarayi limeshatoa msaada mkubwa wa Vifaa na mashine kwa ajili ya chuo cha Amali kiliopo Mkokotoni ili kuwajengea uwezo vijana wanaopata mafunzo ya ujasiri amali kwenye chuo hicho.
  Alisema Mafunzo ya Amali yanayojumuisha fani za ufundi, biashara pamoja na ujasiri amali ndio njia sahihi ya kumuandaa kijana mara amalizapo masomo yake ili apate uwezo mkubwa utakaomuwezesha  kujitegemea katika kuendesha maisha yake ya kila siku.
  Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran kwa msaada wake mkubwa iliyotowa kwa Chuo cha Amali Mkokoni msaada ambao utaleta ukombozi mkubwa kwa kundi kubwa la Vijana kuweza kuwanyooshea njia ya kujitegemea wenyewe binafsi.
  Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliamua kuanzisha vyuo vya  Amali Unguja na Pemba lengo likiwa kupunguza wimbi kubwa la ukosefu wa ajira ambalo Serikali Kuu pekee haina uwezo wa kuajiri vijana wote wanaomaliza masomo yao.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  aliiomba Serikali ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia Mkurugenzi Mkuu huyo kutoka Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Balozi Husseid kuendelea kuisaidia pia Zanzibar katika Sekta ya Afya.
  Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya tayari imeshaanza matayarisho wa ujenzi wa Vitengo vya kutibu Maradhi ya Saratani pamoja na Moyo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mambo ambayo Iran inaweza kusaidia utaalamu na Madaktari kwa vile imeshapiga hatua kubwa katika fani  hiyo.
   Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Balozi Hussein Mollale Abdullahi akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Jengo la Baraza la Wawakilishi lilipo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Balozi Hussein Mollale mara baada ya mazungumzo yao. Wa kwanza kutoka Kulia ni Katibu wa kwanza Msaidizi wa Ubalozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Mjini Dar es salaam bwana Mohammad Dehghani. 
  Picha na OMPR – ZNZ.

  0 0
 • 09/26/16--11:03: Article 10


 • 0 0

  img-20160925-wa0172Mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wa Shield our Watoto(SOW) Bhoke Kirigiti kushoto na mumewe Peter Kirigiti katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya taasisi hiyo ya kulinda watoto dhidi ya ukatili na ghasia za kingono iliyofanyika Jumamosi Septemba 24 jijini Columbus Ohio. img-20160925-wa0012Bhoke Kirigiti akizungumza. img-20160925-wa0010Jummy Olawale mzungumzaji mkuu akitoa hotuba. img-20160925-wa0007Jackie Mapigano akitoa sala ya Ufunguzi. 

  0 0
  0 0

   Na Bodi ya Filamu
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nnape Nnauye amesisitiza kuwa wasambazaji wote wa filamu kutoka nje lazima waingie mikataba na wazalishaji wa filamu watakazotaka kuzisambaza nchini. Kauli hiyo ya Waziri Nnape ameitoa kwenye kikao baina ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na jumuiya ya wasambazaji wa filamu kutoka nje kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Waziri Nnape amesema “kuingia mikataba na wazalishaji wa filamu ni takwa la kisheria lisiloepukika”. Aliendelea kusisitiza kwamba kazi ya serikali ni kuhakikisha inasimamia sheria hata kama sheria hizo zitakuwa haziwafurahishi walio wengi.
  Kikao hicho baina ya Waziri Nnape na wasambazaji wa filamu kutoka nje ni mwendelezo wa vikao vya kurasimisha tasnia ya filamu nchini. Awali Waziri Nnape aliwaagiza watendaji wa wizara yake pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kwa pamoja na jumuiya ya wasambazaji wa filamu kutoka nje kuunda kamati ndogo ambayo itakuwa na kazi ya kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wasambazaji wa filamu za nje na kuzitolea ufumbuzi.
  Ikumbukwe mwezi Julai Waziri Nnape pamoja na Bodi ya Filamu Tanzania walifanya operesheni ya kukamata kazi bandia za wasanii. Kwenye zoezi hilo mitambo ya kudurufu kazi za wasanii na zaidi ya santuri(CD na DVD) 600,000 zilikamatwa. Baada ya zoezi hilo wasambazaji wa filamu kutoka nje kupitia jumuiya yao na mbunge wa Ilala Mussa Azzan waliomba kukutana na uongozi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Baada ya kikao kufanyika Waziri Nnape aliagiza iundwe kamati ndogo itakayoshughulikia changamoto zinazowakabili wasambazaji wa filamu za nje chini ya uenyekiti wa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania.
  Kwa upande wake Mbunge wa Ilala Mussa Azzan (zungu) amewataka wasambazaji hao kuheshimu maazimio waliyoyafikia baina yao na serikali kupitia kamati ndogo iliyoundwa na Mheshimiwa Nnape.
  WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE AKISISITIZA JAMBO KWENYE KIKAO NA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE. MHESHIMIWA NNAPE AMEWAASA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE KUHAKIKISHA WANAINGIA MIKATABA NA WAZALISHAJI WA FILAMU WANAZOTAKA KUZISAMBAZA HAPA NCHINI KWANI NI TAKWA LA KISHERIA LISILOEPUKIKA.

   1.MBUNGE WA ILALA MHESHIMIWA MUSSA AZZAN (ZUNGU) AKIZUNGUMZA NA WASAMBAZAJI WA FILAMU KUTOKA NJE(HAWAPO PICHANI) AMBAO WALIHUDHURIA KIKAO BAINA YA JUMUIYA YA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE NA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO. KWENYE NASAHA ZAKE MHESHIMIWA ZUNGU ALIWAASA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE KUTEKELEZA MAAZIMIO YALIYOFIKIWA.

  1.BAADHI YA WASAMBAZAJI WA FILAMU KUTOKA NJE WAKIMSIKILIZA WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NNAPE NNAUYE WAKATI WA KIKAO CHA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WASAMBAZAJI HAO.


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Azam Marine Hotel Abubakar Aziz Salim wakati alipotembelea ujenzi wa Hoteli ya Kisasa ya Azame marine iliyopo Mtoni Unguja leo akiwa  katika ziara maalum (wa tatu kushoto) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Azam Marine Hotel Abubakar Aziz Salim (katikati) wakati alipotembelea ujenzi wa Hoteli ya Kisasa ya Azame Marine iliyopo Mtoni Unguja. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akiagana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa, baada ya kumaliza ziara yake kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko Fumba Wilaya ya Magharibi na Ujenzi wa Hoteli ya Azam Marine  iliyopo Mtoni Unguja 

  0 0

   Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(kulia ) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud.
   Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa(kulia) wakati alipotembelea Mtambo wa  kutengenezea lami katika Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group leo wakati  alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi (wa pili kulia) Mtaam wa Mtambo N.P.Singh.
  [Picha na Ikulu.]26/09/2016. 

  0 0

  WAZIRI MKUUkuu  Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji. 
  Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.  baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na sita licha ya kuwa na shule. 
  "Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji.",alisema Waziri Mkuu. 
  Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira. 
   "Hivi sasa serikali inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa. 
  Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa. 
   Alisema wenyeviti wa vijiji wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria. 
   "Hatuwezi kuendelea kuwa na watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima"alisema Waziri Mkuu. 
   Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji, Utete, Waziri Mkuu aliahidi kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo litatengewa fedha kuwa ajili ya kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama yake kabla ya kutangaza zabuni ya ujenzi. 
   Kuhusu utengenezaji wa madawati, Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30, mwaka huu kila wilaya nchini inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo kwenye shule nchini. 
   Aidha, alisema ipo miradi mingi inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo mradi wa Bonde la Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa, hivyo wamepeleka timu ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe hatua.
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majliwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Rufiji  baada ya kuwasili mjini Utete kwa ziara ya siku moja wilayani humo  leo Septemba 26, 2016. 


   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipokea magodoro 10 kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mendeleo ya Wananchi cha Kibiti, Bi.  Cecilia Mfuko ukiwa ni mchango uliotolewa na Chuo hicho kwa Hospitali ya Kibiti. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa michezo mjini Kibiti 
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiingia  kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti wilayani  Rufiji ambapo Waziri Mkuu alihutubia mkutano wa hadhara , Septemba 26, 2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo. 
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee Abadallah Ngwele  baada ya kupokea madawati 10 yaliyotolewa  na wazee wa Kibiti katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti, Septemba 26, 2016.  Kushoto ni mkewe Mama Mary Majaliwa  na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo

  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimuagiza Mkuu wa wilaya ya Rufiji Mhe. Juma Njwayo kuhakikisha  anachukuwa hatua za haraka dhidi ya watumishi wa hospitali ya wilaya hiyo ambao hawazingatii maadili ya kazi zao na wamegeuka kuwa kero kwa wananchi. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Zainabu Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Zainabu Chaula mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


  0 0


  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari ya Dar es salaam leo akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi  Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo  kuangalia sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa   Kampuni ya Ushushaji Mizigo Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016. 
   


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Jijini Dar es salaam juu ya uwepo wa Kongamano la Uwekezaji litakalofanyika Mkoani Morogoro Septemba 29-10, 2016 lenye lengo la kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Mkoani humo, kwani umejaaliwa kuwa na mazingira mazuni na uwepo wa rasilimali nyingi ambazo bado hazitumika ipasavyo, pia amewataka vijana wa kitanzania kuacha kukimbilia mijini na badala yake wajikite kwenye fursa ya uwekezaji wa kilimo na ufugaji. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari akifafanua jambo katika Mkutano huo na Waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam juu ya uwepo wa Kongamano la Uwekezaji Mkoani Morogoro litakalofanyika Septemba 29-10, 2016 , ambapo amesema kuwa Kongamano hilo litasaidia kuutangaza Mkoa wa Morogoro kama miongoni mwa maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kibiashara kwa Makampuni ya ndani na nje ya nchi.
  Mkutano huo ukiendelea.

  0 0
 • 09/27/16--03:53: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

  Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mh. Geum-Young Song amemtembelea Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kubadilishana mawazo na uzoefu katika sekta ya Sheria nchini na kuona jinsi wanavyoweza kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara na Jamhuri ya Korea ili kuiendeleza Sekta ya Sheria nchini.

  Akizungumza katika kikao na ugeni huo Prof. Mchome ameelezea kufurahishwa kwake na Jamhuri ya Korea juu ya dhamira yake ya kuisaidia Wizara na Sekta ya Sheria nchini hadi kukubaliana kuwepo na makubaliano kati ya Wizara na nchi hiyo yatakayowezesha Wizara kupata misaada na kujifunza kutoka Korea. Pia amemueleza Mhe. Balozi Song kwamba wizara iko tayari kutekeleza makubaliano watakayokubaliana ili kuimarisha sekta ya sheria nchini na kuishukuru nchi hiyo kwa mpango wake wa kuisaida wizara.
  Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome  akizunumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mh. Geum-Young Song jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutembelewa na ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

    Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome  akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mh. Geum-Young Song.

older | 1 | .... | 1369 | 1370 | (Page 1371) | 1372 | 1373 | .... | 3286 | newer