Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live

TAIFA STARS KUJIPIMA NGUVU NA ETHIOPIA JIJINI ADDIS ABABA

$
0
0
Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), inatarajiwa kucheza na Ethiopia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Oktoba 8, 2016. 

Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), wameomba mchezo huo ufanyike kwao.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

JPM AMTEUA DKT ZAINAB ABDI KUWA NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI

Rais Dk.Shein akutana na Madaktari Bingwa wa Upasuaji

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Rais wa Taasisi ya Mendeleo ya Elimu inayohusiana na Mishipa ya fahamu,Uti wa Mgongo na Vichwa maji (NED) Dk.Jose Picer akiwa na Makamo wa Rais wa taasisi hiyo Dk.Mohamed Qureish walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Rais wa Taasisi ya Mendeleo ya Elimu inayohusiana na Mishipa ya fahamu,Uti wa Mgongo na Vichwa maji (NED) Dk.Jose Picer (katikati) akiwa na Makamo wa Rais wa taasisi hiyo Dk.Mohamed Qureish (kushoto) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo. Picha na Ikulu.

SIMBA YAENDELEZA UBABE LIGI KUU YA VODACOM, YAITANDIKA MAJI MAJI BAO 4-0 LEO

$
0
0
 Mshambuliaji wa Timu ya Maji Maji, Enyima Darlington akiruka sambamba na Beki wa Simba kuwania mpira wa juu katika Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
 Mshambuliaji machachari wa Timu ya Simba, Laudit Mavugo akiondoka na mpira baada ya kumtoka Beki wa Maji Maji, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
Kipa wa Timu ya Maji Maji ya Songea "Wana Lizombe", Amani Simba akiruka bila mafanikio wakati akijaribu kuudaka mpira uliopigwa kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji wa Simba, Jamal Mnyate na kuiandikia timu hiyo bao la kuongoza, katika Mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
 Mshambuliaji wa Timu ya Maji Maji, Enyima Darlington akitoa pasi nzuri ya kichwa kwa Mchezaji Mwenzake, Alex Kondo, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
 Ibrahim Ajib wa Simba akimpiga chenda maridadi, Luhanga Mapunda wa Maji Maji, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.

VIJIJI 24 WILAYANI KASULU KUPATA UMEME WA REA AWAMU YA PILI HADI MWISHONI MWA OKTOBA MWAKA HUU

$
0
0


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kulia) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe wilayani Kasulu. Kulia ni Mbunge wa Kasulu, Daniel Nsanzugwanko na kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wananchi wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter 
Muhongo akizungumza na wananchi. 

WANANCHI wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, wanataraji kuanza kufaidi umeme wa REA pindi awamu ya pili ya mradi huo itakapo kamilika mwishoni mwa  Octoba 2016.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, alipotembelea miundombinu ya Umeme wa REA katika Wilaya ya Kasulu.
Waziri Muhongo yupo katika ziara ya siku tano mkoani Kigoma kuangalia utekelezaji wa awamu ya pili ya miradi ya REA mkoani humo na Wilayani Kasulu aliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Martin Mkisi.
Prof Muhongo, akiambatana na Wahandisi wa Tanesco, REA na Wakandarasi wanaojenga miundombinu hiyo, wamezungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe na Heru Juu Wilayani Kasulu.
 Aidha katika awamu ya tatu, vijiji vipatavyo 29 vitakamilishiwa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme, kuchangamkia fursa za kufunga umeme wa bei rahisi na kujitokeza kwa wingi kwenye  mafunzo yatakayotolewa na Tanesco kuhusu umeme wa REA.
Pia amewaagiza wakandarasi kukamilisha usambazaji wa huduma hiyo ifikapo Octoba 30 mwaka huu bila kuongeza siku hata moja.

SERIKALI KUFANYA ZOEZI LA UTAMBUZI NA USAJILI KWA WATUMISHI WAKE KUANZIA OKTOBA 3

$
0
0
Na Frank Shija, MAELEZO
SERIKALI inatarajia kufanya zoezi la utambuzi na usajili wa taarifa za watumishi wa umma kuanzia tarehe 3 Oktoba ili kutoa vitambulisho vya Taifa vilivyo na taarifa zote muhimu za mtumishi husika.
Hayo yamebainisha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.

Kairuki amesema kuwa zoezi hilo la utambuzi na usajili wa wananchi ambalo linaanza na watumishi wa umma ni muhimu na litasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na kuondoa usumbufu kwa wananchi kwani taarifa zao zote muhimu zitakuwa sehemu moja hivyo kupunguza kero ya kuulizwa taarifa kila uendapo.

Waziri Kairuki amesema kuwa zoezi hilo litashirikisha Wizara yake pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ambapo taarifa zitakazotumika ni zilizilizopo katika vitambulisho vya mpiga kura.

“Kama mnavyofahamu kuwa Serikali ipo katika maboresho makubwa ya utendaji wake, hivyo ili kuendana na hali hiyo tutaanza zoezi la utambuzi na usajili wa watumishi wa umma kuanzia tarehe 3 Oktoba, zoezi litakalochukua takribani wiki mbili, zoezi hili ni muendelezo wa Serikali kukabiliana na matatizo ya kutokuwa na taarifa sahihi.” Alisema Kairuki.

Aidha Kairuki amewata watumishi wote wa umma kushiriki zaoezi hilo wakiwa na taarifa zote muhimu zinazowatambulisha ambazo ni pamoja na Cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu, kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Mzanzibar Mkazi, hati ya malipo ya Mshahara, hati ya kusafiria na kadi ya mpiga kura.

Waziri huyo ametoa wito kwa waajiri kuweka mazingira wezesha ili kufanikisha zoezi hilo ikiwemo kutenga ofisi itakayotumiwa na kwa kazi hiyo pamoja na kusisitiza waajiri wahakikishe watumishi wao wanasajiliwa bila kukusa na taarifa ya zoezi hilo iwasilishe Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawabora ndani ya siku 14 tangu zoezi hilo kukamilika kwake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro amewataka watumishi wote wa umma kulipa umuhimu mkubwa zaozi hilo na kusisitiza kuwa Serikali haita sita kucghukua hatuia za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma kwa mtumishi yeyote atakaye kaidi zoezi hilo.

Awali akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu namna zoezi hilo litakavyotekelezwa nchi znima kwa muda wa wiki mbili tu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mohammed Khamis Abdallah amesema kuwa zoezi hilo litafanikiwa kwani wanao wafanyakazi zaidi ya 460 nchini nzima ambao wapo katika Ofisi za Halmashauri.

Pia aligusia suala la vifaa na kusema kuwa tayari wamewasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo imewapa mashine za BVR kwa ajili ya kuzitumia katika zoezi hilo la utambuzi na usajili.


Zoezi la utambuzi na usajili wa wananchi hasa watumishi wa uuma kukabiliana na vyanzo vya watumishi hewa kwa kuunganisha mifumo ya utambuzi wa watu na mifumo mingine ikiwemo usimamizi wa rasilimali watu na mishahara katika utumishi wa umma ambapo kuunganishwa kwa mifumo hiyo kutawezesha mifumo hiyo kuwasiliana na kutumia taarifa zilizo kwenye kanzi data ya NIDA suala litakalokuwa limerahisisha upatikanaji wa taarifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurian Ndumbaro na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulkisho vya Taifa (NIDA), Mohammed Khamis Abdallah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba . Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Seerikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari.Picha na: Frank Shija, MAELEZO.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA SAMAKI, MAFIA, ATAKA DORIA KUZUIA UVUVI HARAMU ZIIMARISHWE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza mkuu wa wilaya ya Mafia mkoani Pwani, Bw. Shaib Nnunduma pamoja na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw. Eric Mapunda kuimarisha doria kwenye eneo la bahari ili kuzuia uvuvi haramu. 
Amesema vitendo vya uvuvi haramu vinavyoendelea katika wilaya hiyo vinapaswa kudhibitiwa haraka kwa sababu vinasababisha halmashauri hiyo kukosa mapato na kushindwa kuboresha maendeleo ya wananchi. 
Waziri mkuu ametoa agizo hilo kwa nyakati tofauti leo (Jumamosi, Septemba 24, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha Tanpesca na alipowahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kirongwe wilaya ya Mafia. 
Amesema uvuvi ndiyo shughuli kuu ya uchumi na chanzo muhimu cha mapato kwa wilaya ya Mafia na suala la uvuvi haramu linaathiri sana mapato ya halmashauri hivyo ni vema wakaimarisha doria ili kukomesha vitendo hivyo.
“Lazima jambo hili lidhibitiwe. Uvuvi wa kutumia mabomu unaharibu mazingira ya chini ya bahari hivyo samaki wanashindwa kuzaliana kwa wingi. Hakikisheni watu hao wanakamatwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuteketeza zana wanazotumia,” amesema.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Alphakrust inayomiliki kiwanda cha Tanpesca, Ganeshen Vedagiri amesema kampuni hiyo imeajiri watumishi 855 kati yake 445 ni wakazi wa wilaya ya Mafia huku wanawake wakiwa 250.
Amesema wanajumla ya mabwawa 76 ya kufugia samaki aina ya kamba na kwa sasa yanayotumika ni 30 na kila moja lina uwezo wa kuzalisha kilo 5,000 katika siku siku 150 na kufanikiwa kuvuna tani 300 kwa mwaka.
Mkurugenzi huyo amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016.2017 wanatarajia kupata wastani wa sh. bilioni 120 katika mauzo ya nje na sh. bilioni 62 kutoka katika mauzo ya ndani. Wanaltarajia kulipa kodi ya zaidi ya bilioni 15 kwa mwaka huu.
Kwa upande wake Mohamed Gomvu ambaye ni Diwani wa kata ya Kirongwe na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mafia alisema maeneo yaliyoathirika zaidi na uvuvi haramu ni vijiji vya Ndagoni (Kiega), Kifinge, Chunguruma (Tumbuju) na kisiwa cha Nyororo.
Amesema jambo linalokwamisha ukamatwaji wa uvuvi haramu ni kutokana na watumishi kukosa uamini na kuvujisha siri kwa wavuvi hao hivyo wanashindwa kuwanasa kwenye mitego yao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akitazama samaki aina ya pweza wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha TANIPESCA eneo la Kilindoni wilayani Mafia, Mkoani Pwani.  Septemba 24, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akiwa ameshika moja ya samaki aina ya pweza wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha TANIPESCA eneo la Kilindoni wilayani Mafia Septemba 24, 2016.

RATIBA FUPI YA MAZISHI YA MWANAHABARI ADOLF KIVAMWO TAREHE 25/9/2016

$
0
0



Saa 3: Mwili wa marehemu kuwasili nyumbani
Saa 3-4 Chakula
Saa 4:30: Ibada fupi
Saa 5: Safari kuelekea Leaders club
Saa 6: Kuwasili Leaders Club
Saa 6-7:Ibada ya maazishi Viwanja vya leaders
Saa 7-8 Makaburi ya Kinondoni Dar es salaam.

UJENZI WA BARABARA ZA ARUSHA KUKAMILIKA MWAKANI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi M/S Hanil Jiangsu J/V anayejenga barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 na barabara ya mchepuo (Arusha bypass) yenye urefu wa KM 42.4 kuhakikisha barabara hizo zinakamilika ifikapo mwezi Machi na Oktoba mwakani.

Profesa Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi barabara hizo na kujiridhisha na hatua iliyofikiwa kwa barabara zote.

“Meneja hakikisha ujenzi wa barabara hizi unakwenda sambamba na ujenzi wa sehemu ya barabara inayoelekea Ikulu ya mjini Arusha ili kuiunganisha vizuri barabara hiyo kwa kiwango cha lami”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akielekea kukagua kingo za Daraja la Themi linalojengwa katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha.

Amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqarro kushirikiana na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani humo kuhakikisha maji yanayopita kwenye madaraja yaliyopanuliwa kufuatia ujenzi unaoendela hayasababishi mafuriko kwenye makazi ya wananchi.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Eng. Johnny Kalupale amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara mkoani Arusha utakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

“Tumejipanga kuhakikisha barabara ya Sakina-Tengeru na ile ya mchepuo zote zitakamilika kama ilivyopangwa ili kupunguza msongamano hali itakayovutia ongezeko la watalii na hivyo kukuza uchumi wa mkoa wa Arusha”, amesema Eng. Kalupale. Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua uwanja wa ndege wa Arusha na kusisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuupanua uwanja huo ambao ni wa nne kwa uingizaji wa mapato nchini ili kuondoa msongamano uliopo sasa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkazi Shin Pil Soo wakati akikagua Daraja la Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha.

“Wakati Serikali tunajipanga kuongeza uwanja huu na nyinyi mjipange kuongeza mapato ili jitihada za Serikali ziendane na ubunifu wa watendaji”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), mkoa wa Arusha Bw. Elipid Tesha amesema uwanja huo ambao ni kitovu cha utalii katika ukanda wa Kaskazini ukiongezwa utaruhusu ndege nyingi kutua na hivyo kuuongezea mapato ambapo kwa sasa takribani miinuko 110 ya ndege hufanyika kila siku katika uwanja huo.

“Kwa sasa uwanja wa ndege wa Arusha una barabara ya kurukia yenye urefu wa KM 1.6 hali inayosababisha baadhi ya ndege kushindwa kuutumia ila mkakati wa uwanja huo ni kuuongeza uwe na urefu wa KM 2.5”, amesisitiza Bw. Tesha. Uwanja wa Ndege wa Arusha uliojengwa mwaka 1956 ikiwa ni mkakati wa kuboresha huduma za utalii katika mkoa huo uko KM 7 kutoka Arusha Mjini na una eneo la ekari 280 na uzio unaoimarisha usalama wakati wote.

Muonekano wa juu wa Daraja la Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUMUENZI MWALIMU NYERERE KWA VITENDO

$
0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butiama Musoma akiwa ameambatana na watumishi wa NEC na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT kutoka maeneo mbalimbali kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Mwitongo wilayani Butiama. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iko mkoani Mara kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi. 

Na. Aron Msigwa – NEC, Musoma.

Viongozi wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani mara baada kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.

Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani (Kushoto) akisalimiana na Msemaji Mkuu na kiongozi wa familia ya Baba wa Taifa Chifu Japhet Wanzagi (kulia) mara baada ya kuwasili eneo la Mwitongo wilayani Butiama. Wa Pili kutoka Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi. Annarose Nyamubi.

“Kupitia kumbukumbu hizi sisi watumishi wa Tume tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika, wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Amesema Kailima.

Ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa manufaa ya taifa.

“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu Nyerere kabla hajajengewa nyumba na Jeshi, kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Kailima.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama. Wengine wanaoonekana na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


Bw. Kailima amebainisha kuwa NEC itaendelea kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.

RAIS WA ZANZIBAR AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA TAASISI YA MWANAHARAKATI BIBI SITI BINTI SADI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi picha ya kuchora Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Pennyroyal Brian Thomson (kulia) iliyonadishwa na kuinunua kwa Shilingi za Kitanzania Milioni nane (8) pia akiwa amechangia Shilingi Milioni Ishirini na tano katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Sadi,hafla ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hayat Hotel Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa maelezo wakati akimkabidhi picha ya kuchora Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Pennyroyal Brian Thomson (kulia) iliyonadishwa na kuinunua kwa Shilingi za Kitanzania Milioni nane(8) pia akiwa amechangia Shilingi Miliion Ishirini na tano katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Sadi,hafla iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hayat Hotel Mjini Unguja

KUNDI LA MAKOROKOCHO TOKA TEMEKE LAIBUKA WASHINDI WA DANCE 100% 2016 CHINI YA VODACOM TANZANIA

$
0
0
 Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu ( wa pili kulia) akisaidiwa na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Matina Nkurlu, kugawa simu kwa washindi wa mashindano yaliyodhaminiwa wa Vodacom Tanzania ya Dance 100% 2016 katika viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Makorokocho waliibuka washindi wa shindano hilo kwa mwaka 2016.
Wasanii wa kundi la Makorokocho wakifanya vitu vyao kwenye fainali ya mashindano yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania ya Dance 100% 2016 katika viwanja Vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Makorokocho waliibuka washindi wa shindano hilo kwa mwaka 2016.

HIVI NDIO VIKOSI VYA YANGA NA STAND UNITED VINAVYOANZA LEO

$
0
0
Kikosi cha Yanga dhidi ya Stand united Fc

1.Ally Mustapha
2Juma Abdul
3.Haji Mwinyi
4.Vincent Bossou
5.vicent Andrew
6.Mbuyi Twite
7. Saimon Msuva
8.Thaban Kamusoko
9.Donald Ngoma
10.Amissi Tambwe
11.Deus Kaseke

Akiba

1.Deogeatius Munish Dida
2.Hassan Kessy
3.Canavaro
4.Kelvin Yondan
5.Haruna Niyonzima
6.Juma Mahadhi
7.Obrey Chirwa
1. Frank Mwamongo 30 
2. Revocatus Richard-5
3. Adeyum
4. Erick Mulilo-13
5. Ibrahim Job-4
6. Jacob Masawe-24
7. Pastor Athanas-10
8. Geremy Katura-8
9. Kelvin Sabato-3
10. Selemani Selembe-7
11. Adam Kingwande

Akiba

1. Sebastian-8
2. Frank Hamisi-21
3. Chidiebele Abasilim-9
4. Sospeter 
5. Kanyoro-11
6. Erick-28
7. Miraji-2

LUGALO GOLF CLUB BINGWA MASHINDANO YA MKUU WA MAJESHI CDF TROPHY

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda (kushoto )akimkabidhi zawadi ya Kikombe Mshindi wa Jumla wa Kombe la Mkuu wa majeshi CDF TROPHY mpiga Golf ambaye ni Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Watara mara baada ya mashindano katika Uwanja wa Golf Lugalo Jijini Dar es Salaam jana Septemba 24.
Mshindi wa Jumla wa mashindano ya CDF Trophy 2016 Mkuu wa majeshi mstaafu George Waitara (wa kwanza kulia)akipokea Mfano wa Tiketi ya Ndege aliyopewa baada ya kushinda Wapili kulia ni Mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Venance Mabeyo,watatu Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda na Wakwanza kushoto ni mwenyekiti wa Lugalo Golf Club Brig Gen Michael Luwongo.(Picha
Mshindi wa Jumla wa mashindano ya CDF Trophy 2016 Mkuu wa majeshi Mstaafu George Waitara (wa kwanza kulia)akipiga mpira wakati wa mashindano hayo katika uwanja wa Golf Lugalo Dar es Salaam wakwanza kushoto ni katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Mh Job Masima.

Promosheni ya shinda Ng'ombe na Nzagamba kanda ya ziwa

$
0
0
Meneja Masoko wa kinywaji cha Nzagamba kanda ya ziwa, Oscar Shelukindo akizungumza wakati wa droo ya kumtafuta mshindi wa Promosheni ya shinda Ng'ombe na Nzagamba kanda ya ziwa, lililofanyika katika eneo ya Magu jijini Mwanza, ambapo mwana mama Martha Peter aliibuka mshindi na kuondoka na Ng'ombe.
Sehemu ya Wakazi wa Mji wa Magu Jijini Mwanza wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye eneo la Uwanja wa Stendi kushuhudia Promosheni ya shinda Ng'ombe na Nzagamba kanda ya ziwa, iliyofanyika jana, ambapo mwana mama Martha Peter aliibuka mshindi na kuondoka na Ng'ombe.
Mmoja wa Washiriki wa Promosheni ya shinda Ng'ombe na Nzagamba kanda ya ziwa akichanganya karatasi wakati wa kuchezesha droo ya kumtafuta mshindi.

JUMLA YA WAALIMU 701 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI JIJINI ARUSHA WALIPWA STAHIKI ZAO

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Jumla ya kiasi cha shilingi 154 milion zimetolewa kwa Waalimu 701 wa shule za msingi na sekondari kutoka kwenye fedha ambazo zilitakiwa kulipa posho za nauli na simu za madiwani wa jiji la Arusha.

Akiongea na wanahabari ofisini kwake jijini hapa mkuu wa wilaya ya Arusha mjini, Gabriel Daqqaro alisema kuwa kutokana na malimbikizo ya fedha za likizo,kufiwa,nauli, uhamisho waliokuwa wanadai walimu kwa kipindi cha mda mrefu ndio maana tumeamua kuwalipa ili waweze kufanya kazi ya kufundisha watoto wetu kwa moyo.

Daqqaro alisema kuwa baada ya kikao na mkuu wa mkoa Mrisho Gambo na waalimu wa shule 48 za jiji la Arusha, na kuagizwa kuhakikisha walimu wanalipwa stahiki zao ndani ya wiki mbili na agizo hilo tumelitiza na walimu wamelipwa fedha zao zote walizokuwa wanadai.

Alisema kuwa fedha zilizolipwa waalimu hao tumezitoa kwenye fedha zilizokuwa wakijilipa madiwani posho za usafiri na posho za simu na kuzielekeza fedha hizo kutatua kero ya waalimu na mwisho wa siku vijana wetu wapate elimu stahiki bila manung'unuko kutoka kwa waalimu.

''Hapa napenda tusiingize ushabiki wa kisiasa katika hili na tuache kuzusha maneno maneno yanayaashiria uvunjifu wa amani maana tayari nimeshaanza kusikia maneno maneno yanazuka kutoka kwa madiwani, sasa nasema hivi, sisi tumeamua kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa ,na kunakili madiwani wanadai kuwa wao walikuta fedha hizi zikilipwa na ndio maana wakaendelea kupokea,hivyo nnachotaka kuesma  kama kweli walikuwa na nia njema na wananchi kwanini wasizikate mapema mpaka wasubiri mkuu wa mkoa aje aone mambo hay,na wao ndio waanze kuongea maneno maneno''alisema DC Daqqaro.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kuhakikisha wananchi walio wengi wanaondolewa kero zao kwa wakati na kuondosha kabisa kero mbali mbali ndani ya jamii ikiwemo waalimu kupewa stahiki zao kwa wakati.

Akawataka waalimu hao kuhakikisha malengo ya mkoa kuongeza ufaulu yanafikiwa kwa kufanya kazi kwa moyo mmoja huku serikali ikiendelea kumalizia malalamiko mbali mbali ya waalimu wa mkoa huo.

Malipo hayo ya waalimu 701 yametokana na agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwataka DC na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athman kihamia kuhakikisha malalamiko ya waalimu walioyatoa kwenye mkutano wao yanatekelezwa ndani ya wiki mbili .



Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake,mapema leo jijini Arusha
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa wilaya 

JWTZ KUONGEZA NGUVU UPIMAJI AFYA BURE MNAZI MMOJA,YATOA MADAKTARI WAKE NA WAUGUZI 90 KUWASAIDIA WANANCHI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza na Wananchi walio fika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kupata vipimo na kupatiwa ushauri na Madaktari kutoka Hospitali Mbalimbali Jijini Dar es Salaam,hapo jana,ambapo leo RC Makonda ameongeza Siku Mbili (2), zoezi la Upimaji Afya bure

"Awali ya yote niwapongeze wananchi wangu wa mkoa wa Dar es Salaam walioonyesha mfano mzuri wa kujali afya zao na jamaa zao kwa kuitikia fursa ya wito wangu wa kupima afya bure, lengo likiwa ni kuhakikisha tunazijua vyema na mapema hali za afya zetu ili tuwe na nafasi nzuri zaidi ya kushughulikia changamoto zozote zinazobainika ama zinazoweza kujitokeza kwa mujibu wa maelezo ya watalaamu.
"Kitakwimu, wataalamu wetu kutoka taasisi na hospitali mbalimbali ambazo ninashirikiana nazo walipokea zaidi ya wagonjwa 14,000, idadi ambayo ilitupa moyo na faraja sambamba na changamoto ndogondogo za hapa na pale kutokana na ukweli kuwa hatukuwa na matarajio ya idadi kubwa kiasi hiki, jambo ambalo kimsingi lilipelekea zoezi kushindwa kukamilika Kwa muda uliokuwa umepangwa hapo awali.
"Kwa msingi na nia yangu ile ile ya kuhakikisha kila mwananchi aliyefika viwanja vya mnazi mmoja anapatiwa huduma, nimeona ni vyema niongeze siku mbili (2) za muendelezo wa upimaji wa afya ili kumpa nafasi kila mwananchi aliyefika ktk viwanja vya mnazi mmoja kupata huduma. Pili, imenibidi niongeze nguvu kwa kumuomba waziri wetu wa ulinzi Dr. Hussein Mwinyi kutupatia madaktari na wauguzi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambaye amelipitisha ombi hilo na hivyo kutuongezea madaktari wengine pamoja na wauguzi wasiopungua 90 ambao wataungana nasi kesho, hivyo kukamilisha jumla ya madaktari na wauguzi 240, idadi ambayo nina uhakika itatuwezesha kumuhudumia kila mtu na kwa wakati.

"Mwisho ningependa kuwaomba wananchi wote hasa waliofika Mnazi mmoja kuendelea kuwa wavumilivu ili kuwapa moyo Madaktari wetu kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya. Mimi RC wenu naendelea kushirikiana nanyi bega kwa bega na sitawaacha" amsema RC Makonda.

Mkuu wa wilaya Nachingwea Mhe. Rukia Muwango ashukuru waliochangia maafa ya tetemeko Kagera

$
0
0
Mkuu wa wilaya Nachingwea Mhe. Rukia Muwango anawashukuru wale wote walioitikia wito na waliojitoa kwa hali na Mali kuchangia mkono wa pole kwa wenzetu wa Kagera waliopata maafa ya Tetemeko la ardhi, hata ambao hawakuweza kutoa chochote.
"Tunashukuru kwa maombi yao kwa kuwa tunajua walikuwa na nia njema, Tunatambua mchango wa kila mmoja kwa namna yapekee kabisa. 
"Kiasi kilichopatikana taslimu ni shilingi 5,576,000/-. Na nguo kiasi. Tutatoa taarifa ya mwisho siku ya Jumatano. Bado tunaendelea kupokea michango hadi tarehe 27, mwezi huu  saa 5 usiku. Tunashukuru kwa ushirikiano. 
"Ni imani yetu kuwa TUTAENDELEA NA MOYO HUU HASA KWA WITO WA KUCHANGIA MAENDELEO YETU WANA NACHINGWEA. Asanteni sana", alisema DC Muwango.

EXTENDED SERVICES LIMITED:WE SHIP ALL TYPES OF CARGO (SEA FREIGHT AIR CARGO) TO EAST AFRICA

$
0
0
WE SHIP ALL TYPES OF CARGO (SEA FREIGHT & AIR CARGO) TO EAST AFRICA AT UNBEATABLE RATES, i.e. BOUTIQUE STUFFS AND ACCESSORIES CONTAINERS, TRUCKS, CARS, MACHINERY ETC.

 WE ARE THE MOST AFFORDABLE AND RELIABLE SHIPPING AGENT IN U.K

*CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 850 (TILBURY/ SHERNESS PORTS)

*4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 930 (TILBURY/ SHEERNES PORTS)

*40’ CONTAINER TO DAR FROM £ 1600

*40’ CONTAINER TO MOMBASA FROM £1575 HC

*40’ CONTAINER TO ZANZIBAR FROM £ …

*20’ CONTAINER TO DAR FROM £ 1000

*20’ CONTAINER TO MOMBASA £ 970

*20’ CONTAINER TO ZNZ FROM £…

*WE ALSO HAVE A SERVICE OF TRANSPORTING ANY TYPE OF CAR (SALOON /4X4) IN A CONTAINER TO KENYA FOR £ 800, AND A VAN IN A CONTAINER FROM £ 950. THIS IS A DAILY SERVICE TO KENYA!!!!!!!

*TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2650(TILBURY PORT)

*TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2475(SOUTHAMPTOM/NEWCASTLE PORTS)

*TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM 2612.50(IMMINGHAM PORTS)

*TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2612.50 (KILLINGHAM)

*ALSO WE CAN ARRANGE PRE –SHIPMENT  INSPECTION FOR YOU TO AVOID INCONVINIENCES

*FOR MORE DETAILS PLEASE DO NOT HESITATE TO CONTACT US ON OUR CONTACTS BELOW:

EXTENDED SERVICES LIMITED, CLIPPER HOUSE, TILBURY FREEPORT, TILBURY, ESSEX, RM18 7SG

EMAIL:extendedservicesltd@gmail.com,Tel:+441375767890,mobile:+447438145815


                   















VOA: Mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa 2016

Viewing all 109935 articles
Browse latest View live




Latest Images