Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Barua kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dkt. Abdallah Kigoda : Pendezo kuhusu kuzuia Unyonyaji Dhidi ya Wasanii wa Tanzania katika Biashara ya Miito(Ring back tones)

$
0
0

Kwenda kwa:        DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara

Kuhusu:             BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)

Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRIna UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.

USIRI
Biashara hii ya “Ring Back Tones” (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao nao huingia mikataba na Wasanii (Content Creators). Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo “Network providers” na “Content Providers” kuwa watu pekee wenye taarifa zote za biashara hii. Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au ‘content’ nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii. Wachuuzi (Content Providers) nao hawatoi taarifa za mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa wasanii kuwasainisha mikataba inayowanyonya. Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasi cha asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake. Hivi sasa biashara hii inathamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.

Suluhisho: Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimisha makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito ya simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules). Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa taarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)

UNYONYAJI
Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii wamekuwa wakinyonywa kimapato. Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake (wimbo) katika mwezi (downloads).

Lakini mapato yatokanayo na “subscriptions” ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku msanii hapati chochote. Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za ‘downloads’ na ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa na Kampuni za Simu.

Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public Performances) na hivyo “copyright Association” ya Marekani imeweka kiwango cha chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa. Marekani msanii hulipwa asilimia 10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.

SULUHISHO
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi za wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama ‘performance’ na kwamba Kampuni za simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya mapato ghafi, ambapo asimilia 10% itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi na Ulinzi wa kazi za Wasanii.

HITIMISHO
Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya ‘Ring Back Tones’ na mgawo wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloleta tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni (Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013

Kabwe Z. Zitto, Mb
Kigoma Kaskazini
Dodoma, 13 Mei 2013.

Redd's Miss Ustawi wa Jamii kufanyika Mei 17

$
0
0
 Walimbwende wanaowania taji la Redd's Miss Uswawi wa Jamii 2013,wakiwa wameweka pozi kwenye picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na shindano lao hilo linalotarajia kufanyika Ijumaa hii (mei 17,2013) katika Ukumbi wa SunSirro,Sinza jijini Dar es Salaam huku wakisindikizwa na Malkia wa Mipasho Tanzania,Bi. Khadija Kopa na Msanii wa Bongo Fleva,Barnaba.

Article 3

$
0
0
To make Fid Q the BEST HIP HOP ARTIST send AH1 to 15345 and to make him the BEST LYRICIST send AW1 to 15345 and to make SIHITAJI MARAFIKI the BEST HIP HOP SINGLE send BT5 and to make the BEST COLLABORATION SINGLE send BR4. Support real Hip Hop from TONGWE RECORDS by sending AW1, BR4 and BT5 to 15345 to make this hardcore MC walk away head high with the Kili awards. You can also vote online via ktma@innovexdc.com

UTEUZI WA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI NA UMOJA WA FALME ZA KIARABU

kutoka maktaba ya globu ya jamii

$
0
0
 Januari 24, 2005: Ankal akiwa katika benchi la Serengeti Boys katika uwanja wa Barbourfields jijini  Bulawayo, Zimbabwe, wakati wa mpambano wa timu hiyo na timu ya Taifa ya Zimbabwe ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 chini ya kocha Abdallah 'King' Kibaden (wa pili kulia). 
Chini Serengeti Boys wakipiga jalamba kabla ya mchezo huo ambao vijana hao wa Tanzania walishinda kwa bao 1-0 na kufanikiwa kuvuka kuingia fainali ya kombe la Vijana wa Afrika zilizofanyika nchini Gambia. 
Bao la ushindi lilifungwa na Nizar Khalfani dakika ya 36 na kuwapa ushindi wa mabao 4-1 kufuatia mechi yao ya awali wiki mbili zilizopita uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam waliyoshinda bao 3-1

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
BUSHOKE FT K-LYNN - NALIA KWA FURAHA

GSMA ESTABLISHES OFFICE IN NAIROBI TO SUPPORT BURGEONING AFRICAN TELECOMS MARKET

$
0
0
The GSMA today announced that it has opened a permanent office in Nairobi, Kenya. 
The office will be based in Nairobi's Innovation Hub (iHub) and will enable the GSMA to work more closely with its members and other industry stakeholders to extend the reach and socio-economic benefits of mobile throughout Africa. 
The rapid increase of mobile connections has attracted GSMA to the region. Mobile connections in Sub-Saharan Africa increased by 20 per cent to 500 million in 2013 and are expected to increase by an additional 50 per cent by 2018. 
The GSMA’s permanent presence in Kenya will enable the organisation to work closely with its members to put the conditions in place that will facilitate the expansion of mobile, bringing important connectivity and services to all in the region.

iHub is Nairobi's Innovation Hub for the technology community, which is an open space for the technologists, investors, tech companies and hackers in the area. This space is a tech community facility with a focus on young entrepreneurs, web and mobile phone programmers, designers and researchers. It is part open community workspace (co-working), part vector for investors and VCs and part incubator.
 More information can be found here:http://www.ihub.co.ke/about

About the GSMA
The GSMA represents the interests of mobile operators worldwide. Spanning more than 220 countries, the GSMA unites nearly 800 of the world’s mobile operators with more than 230 companies in the broader mobile ecosystem, including handset makers, software companies, equipment providers and Internet companies, as well as organisations in industry sectors such as financial services, healthcare, media, transport and utilities. The GSMA also produces industry-leading events such as the Mobile World Congress and Mobile Asia Expo. 


For more information, please visit the GSMA corporate website at www.gsma.com or Mobile World Live, the online portal for the mobile communications industry, at www.mobileworldlive.com.


Mhe ole naiko akabidhiwa dhamana kuwa balozi wa heshima wa botswana nchini tanzania

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (kulia) akimkabidhi dhamana Mhe. Emmanuel Ole Naiko aliyeteuliwa na serikali ya Botswana kuwa balozi wake wa heshima hapa nchini.  

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI SPECIAL OFFER TO EAST AFRICA

$
0
0


40' CONTAINER TO DAR/MOMBASA NOW £1,800
IT CAN'T GET BETTER THAN THIS!
SAVE OVER £700!
BEI ZETU NI CHINI SANA KULIKO SEHEMU YOYOTE

AIR CARGO TO NAIROBI 
£2.80 per KILO! INCLUSIVE CLEARANCE
ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN KENYA
UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA TU KENDA HOUSE
TOM MBOYA STREET NAIROBI
FLIGHTS EVERY WEEK
TO COLLECT CARGO FROM LONDON £25 
TO COLLECT CARGO FROM OUTSIDE LONDON £50
KAMA UNA MZIGO MKUBWA COLLECTION NI FREE! FROM LONDON
MINIMUM WEIGHT IS 35K
CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243

MSAADA TUTANI- MDAU ANATAFUTA UFUTA

$
0
0

kAKA MICHUZI.
 MIMI NI MFANYA BIASHARA NATAFUTA WAUZAJI WANAOWEZA KUNIUZIA UFUTA UKIWA DAR-ES-SALAAM NAMBARI YANGU NI0717001199 AU 0786642858 AU MAIL ; swahilinet.com@gmail.com

NATAFUTA UFUTA MWEUPE AMA KWA KIZUNGU "WHITE SESAME"  MZIGO  WA KUANZIA TANI 10 HADI 100 ILA BAADA YA HAPO NITACHUKUA MZIGO WOWOTE UTAKAOPATIKANA HATA UKIWA MWINGI KIASI GANI.

bei ya madafu leo

Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii yaendelea kutoa elimu kwa waheshimiwa wabunge pamoja na waandishi wa habari katika maonesho ya wiki ya hifadhi ya jamii mjini Dodoma

$
0
0
 Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka akifungua rasmi semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na SSRA na Mifuko ya Hifadhi ya jamii 
  Mkurugenzi Mkuu wa SSRA BI Irene Isaka akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari. Pembeni yake ni waziri wa kazi na ajira Bi Gaudentia Kabaka pamoja na naibu waziri Dr Milton Makongoro Mahanga
 Mmoja wa waandishi wa habari akichangia mada katika semina ya waandishi wa habari
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi Irene Isaka akiwasilisha mada kuhusu sekta ya hifadhi ya jamii kwa waheshimiwa wabunge
Picha 6: Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw Daud Msangi akiwasilisha mada juu ya mchango wa GEPF katika kuendeleza sekta ya hifadhi ya jamii

 Mhe Juma Nkamia Kondoa akishiriki katika mada.
Naibu Spika Mh Job Ndugai akifungua rasmi semina maalum ya waheshimiwa wabunge iliyoandaliwa na SSRA na Mifuko ya Hifadhi ya jamii mjini Dodoma.

Mh. Anna Abdallah akiuliza swali juu ya shughuli za Mifuko ya Hifadhi ya jamii.

IKULU YAMSHUSHUA PROFESA LIPUMBA

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba amekaririwa na Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatano, Mei 15, 2013 akisema kuwa “amenasa taarifa za siri za kuwepo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani”.

Katika habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, “Lipumba: Kuna njama za kumwongezea JK muda” Mheshimiwa Lipumba anadai kuwa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete “ itakaa madarakani hadi mwaka 2017” kwa sababu kuna “wasiwasi kuwa mchakato wa sasa wa kupata Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014.”

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa taarifa hiyo ya Mheshimiwa Prof. Lipumba ni uzushi mtupu na ni upotoshaji usiokuwa na msingi.  Rais Kikwete hafahamu kuwepo mipango hiyo.  Ni vyema Mheshimiwa Lipumba aisaidie jamii kusema nani anafanya mpango huo ili ukweli ujulikane.  Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na Watanzania kwa ujumla kuacha tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea muda Watanzania kufikiria mambo yasiyokuwepo.

Ukweli ni kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi, ni matarajio ya Rais Kikwete kuwa mchakato wa Katiba utakamilika mwaka 2014 na kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika chini ya Katiba Mpya kama inavyotarajiwa na kumpa nafasi ya kustaafu mwisho wa kipindi chake cha uongozi wa taifa letu. 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

15 Mei, 2013

Jaji Warioba: Jukwaa la Katiba Ruksa kwenda Mahakamani

$
0
0

Na Mwandishi Wetu
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema haimzuii mwananchi, asasi au taasisi yoyote kufungua kesi Mahakamani kupinga au kuzuia mchakato unaoendelea wa Katiba Mpya.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba ametoa ufafanuzi huo kwa baadhi ya waandishi wa habari waliofika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Mei 15, 2013) kutaka ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyotolewa na Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salaam jana (Jumanne, Mei 14, 2013).
Katika tamko lake, Jukwaa la Katiba lilieleza nia ya asasi yake kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania ndani ya siku saba ili kusimamisha mchakato wa katiba Mpya kutokana kile ilichodai ni kasoro zinazojitokeza katika mchakato wa katiba unaoendelea.
Ruksa kwenda Mahakamani
Hata hivyo, akiongea na baadhi ya waandishi wa habari waliofika leo ofisini kwake leo, Jaji Warioba alisema Tume yake haina tatizo na mtu au asasi kwenda Mahakamani kwa kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba.
“Nimesoma tamko lao na niseme tu halina jipya. Hii si mara ya kwanza kusikia hili (la kwenda Mahakamani), na jibu letu lilikuwa waende na ndio jibu letu hadi sasa,” alisema Jaji Warioba anayeongoza Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 2 mwaka jana.
“Mimi nasema waende ili tujue Jukwaa haswa ni nani, kwa sababu ninafahamu ni mkusanyiko wa asasi mbalimbali na baadhi ya asasi hizohizo zimetuletea maombi ya kuunda Mabaraza ya Katiba ya Taasisi na Asasi… sasa jukwaa hili ni nani haswa?,” alisema Jaji Warioba.
Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
Kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba amesema kuwa ingawa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba sio jukumu la Tume, wanafahamu kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kurekebisha sheria hiyo kama ilivyoahidiwa.
“Hili la marekebisho ya sheria ingawa sio jukumu letu, lakini nalo sio jipya. Wote tulimsikia Waziri Mkuu hivi karibuni kule Bungeni akisema kuwa Serikali inaandaa marekebisho ya Sheria hiyo yatakayowasilishwa Bungeni … sasa hawa wanataka nini?,” alihoji Jaji Warioba.
Tume ina watu wenye weledi na uadilifu mkubwa
Kuhusu, mchakato wa Katiba kukosa uongozi madhubuti, Mwenyekiti huyo amesema kuwa Tume yake imeundwa na watu wenye sifa, weledi na uadilifu mkubwa ambao wametokana na mapendekezo ya wadau mbalimbali yakiwemo makundi, vyama, asasi mbalimbali za kijamii na kiraia.
“Mimi najivunia kuongoza Tume yenye watu wenye weledi na uadilifu mkubwa na wananchi wanalifahamu hili na kwa kweli wanatuunga mkono,” alifafanua Jaji Warioba. 
Muda wa kutolewa Rasimu ya Katiba
Katika mahojiano hayo, Jaji Warioba pia alifafanua kuhusu muda ambao Tume yake inatarajia kutoa Rasimu ya Katiba kwa lengo la kujadiliwa na kutolewa maoni katika Mabaraza ya Katiba.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, hivi sasa Tume inaendelea kuandaa Rasimu ya Katiba na wananchi watapata muda wa kutosha kuijadili na kutoa maoni yao.
“Mpango wa Tume ni kukamilisha kazi zake ndani ya muda uliopangwa na sheria... tutatoa Rasimu ya Katiba katika muda ambao utatosha kuwafanya wananchi na wajumbe wa Mabaraza ya Katiba kuisoma,” alifafanua Jaji Warioba.
Jaji Warioba pia ameelezea kushangazwa kwake na kauli za wadau mbalimbali kuhusu utendaji kazi wa Tume na kusisitiza kuwa wananchi na wadau wengine wasubiri Rasimu ya Katiba itolewe na Tume ndipo watoe maoni.
“Nadhani itakua ‘fair’ (sawa), tukishatoa rasimu ndiyo watu watuhukumu,” alifafanua Mwenyekiti huyo ambaye pia alishawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Tusiwabeze Wananchi
Kuhusu madai kuwa wananchi waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya hawana uwezo na weledi wa kujadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba, Jaji Warioba amesema madai hayo hayana msingi na yanabeza maamuzi ya wananchi.
Mwenyekiti huyu ameongeza kuwa uamuzi wa Tume kushirikisha wananchi kuanzia ngazi ya mitaa, vijiji, vitongoji na shehia ulilenga kuwapa wananchi hao fursa ya kuchaguana na kuongeza kuwa wananchi walitumia fursa hiyo vizuri.
“Wanaosema haya wanawabeza wananchi waliowachagua hao wajumbe,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa taarifa ambazo Tume yake imezipata zinaonyesha kuwa katika wajumbe hao kuna wananchi wasomi na wenye weledi wa kutosha kujadili rasimu ya katiba.

MSANII DIPO AJIUNGA KWENYE MASUMBWI

$
0
0
Kocha wa mchezo wa masumbwi Klabu ya Amana CCM ,Kondo Nassoro (Kushoto) akimwelekeza msanii wa michezo ya kuigiza kwenye Luninga, Haruna Mussa 'Dipo' wa Dar es salaam jana jinsi ya kutupa makonde alipokwenda kufanya mazoezi ya ngumi kwa ajili ya kujiweka sawa sawa katika kuakikisha anafanya vizuri kwenye fani yake

Vodacom na Samsung zazindua S4 nchini Tanzania

$
0
0

Picture

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Sylvester Manyar (kushoto) akimuonesha mwandishi wa habari wa clouds media Bi.Esther Machangu moja ya teknologia iliyopo kwenye simu aina ya Samsung Galax S4 yenye teknolojia mbalimbali za kisasa ,wakati wa uzinduzi wa simu hizo wateja watakaonunua simu hizo watapata huduma ya bure ya Intaneti ya (5GB) kwa muda wa siku 30 sambamba na waranti ya mwaka mmoja ya matengezo, uzinduzi huo ulifanyika Vodashop Oysterbay jijini Dar es Salaam, Wanaoshuhudia watatu toka kushoto ni Afisa Masoko wa Vodacom Ibrahim Kingozi, Elihuruma Ngowi, Meneja wa Samsung nchini Kishor Kumar.

Picture

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Samsung wakiwazijaribu simu aina ya Samsung Galax S4 iliyosheheni teknolojia mbalimbali za kisasa ,wakati wa uzinduzi wa simu hizo ambapo wateja watakaonunua aina ya simu hizo watapata huduma ya bure ya Intaneti ya (5GB) kwa muda wa siku 30 sambamba na waranti ya mwaka mmoja wa matengezo,simu hizo zitakazokuwa zikipatikana kwenye maduka ya Vodacom nchini.Uzinduzi huo ulifanyika katika duka la Vodacom eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Ziara ya Mhe Pandu Ameir Kificho Spika wa Baraza la Wawakilishi Ziarani Uholanzi

$
0
0
 Mhe Spika wa Baraza la Wawakilishi  Mhe Pandu Ameir Kificho (mwenye shati jeupe) akiwa na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Balozi Dr. Diodorus Kamala (mwenye tai) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe uliofuatana na Mhe Spika na Uongozi wa kampuni ya Damen ya Uholanzi. Mhe Spika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wako kwenye ziara siku nne nchini Uholanzi.

Mhe. Pandu Ameir Kificho Spika wa Baraza la Wawakilishi akiwa na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Kamala (mwenye tai) wakiwa ndani ya Boat iendayo kasi iliyotengezwa na kampuni ya Damen. Kushoto kwa Mhe Spika ni Mhe Omar Yusuph Mzee waziri wa Fedha Zanzibar. Na kulia kwa Dr. Kamala ni Mhe. Mohamed Abdala Mohamed Mkurugenzi  wa Nishati Zanzibar. Ujumbe wa Zanzibar unaendelea na ziara ya kikazi nchini Uholanzi

PSPF yang'ara katika wiki ya hifadhi ya jamii mjini dodoma‏

$
0
0
 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa hiari wa PSPF Bi. Zuhura Lwamo akipokea fomu ya usajili ya Mpango huo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA ndugu Irene Isaka baada ya Mkurugenzi huyo kujisajili katika Mfuko huo.
 Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni PSPF Ndugu Gabriel Silayo akielimisha wabunge juu ya shughuli mbalimbali za Mfuko wa PSPF katika Semina iliyofanyika bungeni, Dodoma. 
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakiwa bandani pao Dodoma.

Kitabu cha Mwakalebela hadharani siku ya mechi ya watani wa Jadi

$
0
0

KITABU cha kwanza nchini kinachozungumzia soka la Tanzania kijulikanacho kwa jina la “Soka la Tanzania” kitaanza kuuzwa siku ya mechi ya watani wa Jadi, Yanga na Simba iliyopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mtunzi wa kitabu hicho, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na yamedhaminiwa  na kampuni TSN Group kupitia kinywaji chake cha kuongeza nguvu Chilly Willy, Events World, Vannedrick Tanzania Limited na  Inbox Pub.
Wadhamini wengine ni Clouds FM, Times FM na Street Soul kwa mujibu wa Mwakalebela. Alisema kuwa kwa sasa ametoa nakala 10,000 kwa ajili ya kuuzwa Tanzania nzima. Alisema kuwa kitabu hicho kimezungumzia historia ya soka la Tanzania katika Nyanja za vijana, wanawake na wanaume, ligi kuu ya Tanzania Bara, Taifa Cup, Timu ya Taifa na Utawala Bora.
Mbali ya hayo, kitabu hicho kimezungumzia ujio wa kocha Marcio Maximo, mchango wa serikali katika kuinua mpira wa miguu, wadhamini, uhusiano kati ya waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira wa miguu Tanzania.
“Pia nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar Tenga kwa kipindi cha miaka mine nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka kwa makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa kwanza  Juni 15, 2006,” alisema Mwakalebela.
Alisema kuwa kitabu hichi ni muhimu sana kwa wana-habari, wachezaji, makocha, waamuzi na wadau wengine wa mchezo huo kwani kuna kumbukumbu zote za mechi za timu ya Taifa ikiwa mabao ya kufunga, wafungaji, vikosi tofauti vya timu za taifa na mambo mengine.

hoja ya haja: Nini Kinachofuata Baada Ya Mabadiliko Ya Katiba Mpya

$
0
0

Tanzania ipo katika kipindi cha mpito cha mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania baada ya serikali kuitika mwito wa vyama mbalimbali vya upinzani na wananchi kwa ujumla. Naishukuru serikali kwa jitihada zake za kuanzisha mchakato huu wa kidemokrasia wa mabadiliko ya katiba mpya chini ya uongozi wa rais wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Tukiwa wote ni mashahidi, bila ya shaka serikali imejitahidi kwa kuchukua hatua zote za kutekeleza suala hili kuanzia ngazi za mitaa, kata, wilaya, vijijini na mikoa yote kwa malengo ya kuhusisha wananchi na asasi na vyama mbalimbali hapa nchini kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia ya kuwakilishwa kimantiki. Naam, na tumeona changamoto mbalimbali katika mchakato huu na kama tunavyojua au na kama tunayoomba mwisho wa yote haya yachukuliwe yale mapendekezo ya wananchi na mapendekezo ya asasi mbalimbali na vyama mbalimbali yatakayojenga taifa letu kuwa imara, kuwa na amani na kutuwezesha kuwa wamoja bila ya kuangalia itikadi yoyote yenye kuvunja amani na umoja wa taifa letu.
 
Kutokana na mipango ya tume ya mabadiliko ya katiba ilivyojipanga, rasimu ya katiba ipo njiani kutokana na muda wa sheria uliotolewa na bila ya shaka itafika wakati wake muwafaka katiba kuwekwa hadharani. Pamoja na yote haya yanayofanywa na serikali kuridhisha wananchi na vyama na asasi mbalimbali kwa kulitakia kheri taifa lake, suala la kujiuliza ni, Serikali imejipanga vipi au imeweka mikakati gani ya kuchukua hatua mara mchakato wa katiba utakapokwisha na katiba kuwekwa hadharani ili kuzuia watu wachache wasije wakaunda majeshi bila ya silaha ili kutuvunjia utulivu na amani nchini kwetu kwa kutaka kuitikisa serikali?
 
Ushauri Wangu:
 
Kama serikali ilivyoanza kupokea na kuridhia mabadiliko ya katiba mpya kwa kuhusisha vyama na asasi mbalimbali nchini na mpaka kuunda tume ya mabadiliko ya katiba mpya inayoongozwa na Mheshimiwa jaji Joseph Warioba (ambaye ni mmoja wa hazina ya taifa letu) na kushirikiana na watu wenye weledi na uadilifu mkubwa katika tume hiyo, ushauri wangu ni kuwa, chombo au idara au tume nyingine mpya ya kudumu iundwe 'maalum na hususan' ya kulinda amani wakati na baada ya katiba mpya kutolewa hadharani ambayo tume hiyo ihusishe au/na iwakilishwe na vyama na asasi mbalimbali na iwe na wanachama huru wasiofungamana na upande wowote wa asasi au vyama vya kisiasa, ambao wanachama hao wawe na nguvu ya kuchukulia hatua za kisheria asasi au chama chochote chenye uchochezi wa kuvunja amani nchini. Tume hii ishirikiane pamoja na serikali katika kulinda amani mara baada ya kipindi cha rasimu ya katiba itakapowekwa hadharani na baada ya kipindi cha katiba kukamilika na kupitishwa, na kwa yeyote iwe ni asasi au chama kisichotaka kujihusisha na kushirikiana na mchango wa tume hii ya kuweka amani baada ya katiba itakapotolewa iwe kipindi cha rasimu au kipindi cha mwisho wa kutolewa katiba, hapa ndipo tutamjua mzuri nani na mbaya nani katika taifa letu lenye usalama na amani ambalo watu wake hawakuangalia, hawaangalii na nataraji hawatoangalia itikadi za kidini, kisiasa au za kikabila kama tulivyorithishwa na wazee wetu na tuendelee hivyo hivyo ili kuendeleza usalama na amani kwa vizazi vijavyo vya Tanzania. Usalama na Amani siyo jukumu la serikali peke yake, ni jukumu la kila Mtanzania, na tukumbuke kuwa mbegu tunayoipanda sasa hivi ndio tutaivuna baadae.
 
Ushauri wangu tume hii yenye nguvu ya kulinda amani nchini ipatiwe kipengele au vipengele katika katiba yetu mpya ili kusiwe na walakini huko tunapokwenda, au inawezwa ikaundwa huru kama asasi au idara mojawapo ya serikali ya kulinda amani kwa yoyote mwenye kuleta utata juu ya katiba ili tuilinde katiba yetu adhimu.
 
Huu ni mchango na ushauri wangu tu katika katiba mpya na nataraji suala hili litaangaliwa.
 
Nini Kinachofuata Baada Ya Katiba Mpya?
 
Serikali kama ilivyojipanga kwenye mabadiliko ya katiba mpya, vilevile ijipange kwa mabadiliko ya 'Kiuchumi' ya kunufaisha wananchi wa Tanzania kwa ujumla, kwani ikiwa tutasahau tunapotoka na kilichotufikisha hapa kazi yetu itakuwa haijakwisha na matokeo ya baadaye yatakuwa si mazuri.
 
Wakati huu huu wa kipindi cha mabadiliko ya katiba, serikali iandae njia ya kuonesha wananchi wa Tanzania 'A clear roadmap' ya kuwa mabadiliko ya katiba yanaenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi ya taifa letu na mabadiliko ya kiuchumi ya kuwawezesha Watanzania. Hapana! naona bado hujanifahamu. Mabadiliko haya ya uchumi ninayosema mimi siyo mabadiliko ya kujenga barabara za lami tu na magorofa makubwa mjini, mabadiliko ya kila Mtanzania kuwezeshwa kihali ili kupiga vita ufukara kwa kuwekewa ngazi na fursa mbalimbali za kihalali, za kimaadili na za kiutamaduni wa Kitanzania ili kuupiga vita ufukara. Wananchi wawekewe wazi ni muda gani na tutafika wapi, kwa mfano malengo ya miaka 10 (kumi) ya kuwawezesha wananchi, ingawa wote tunakubali kuwa siyo rahisi kuondoa ufukara wa watu zaidi ya milioni arubaini ndani ya miaka kumi, lakini angalau kuwe na malengo ya kufikia ngazi fulani, na malengo hayo yawekwe wazi kwa wananchi ili wajue serikali ina malengo gani kwao. Kufanya hivi ndiyo demokrasia inavyotutaka tufanye na ni njia mojawapo ya kuepusha vurugu na ni njia ya kuleta amani na usalama si Tanzania tu bali popote pale katika dunia hii ya leo. Njia hii (roadmap) ya kuwawezesha wananchi iwekwe wazi kwa wananchi katika njia zote za habari na hata kwa vipeperushi kikampeni lakini si kwa kampeni za kisiasa bali kwa malengo ya kutimiza majukumu hayo ya msingi. Baada ya haya, iwapo kutakuwa na vurugu zisizo na msingi kutoka kwa watu wachache wanaotaka kutugawa na kuvunja amani nchini kwetu, itabidi sheria ichukue mkondo wake kwa watu hawa.
 
Ningependa kutoa ushauri au mchango wangu mdogo kutokana na ninavyoona dunia hivi sasa inapoelekea. Kutokana na mtazamo wangu, demokrasia ya karne ya 21 (ishirini na moja) iwe ni demokrasia ya Kiuchumi ya kuwasaidia wananchi kutokana na 'Utandawazi' ambao tulioukubali kuupokea katika kipindi hiki cha karne mpya ya kizazi kipya. Demokrasia ya Kiuchumi ni mbali na demokrasia ya Kisiasa ambayo kama ilivyokuwa ikitumika katika zama za miaka na karne zilizopita, ingawa demokrasia ya Kisiasa itabaki kuwepo na inaweza kutumika kama ni chombo cha kupelekea mafanikio ya uchumi kwa Watanzania (lakini kama tukiwa makini) na kwa maridhiano na wadau. Mengi yanayotokea tunayoyaona sasa ni kuwa tumejisahau kuwa dunia inabadilika lakini sisi wenyewe hatujibadilishi na hiyo ndiyo hatari kubwa ya tunapoelekea.
 
Serikali ya awamu ya nne imefanya mengi mazuri ambayo tunayaona wazi ya kimaendeleo, lakini kutokana na mabadiliko haya ya utandawazi ambao unaelekea kutanda kwenye kila ngazi ya jamii lazima serikali ijipange tena kwa kuonesha njia ya kuwawezesha wananchi kikampeni ambayo isiyo ya kisiasa na ioneshe mifano ya kutekeleza malengo hayo katika kuwezesha watu wake Kiuchumi ili kuondoa au kupunguza umaskini wa wananchi. Rais wa zamani wa Marekani, Thomas Jefferson, amesema, "That government is best which governs the least, because its people discipline themselves."
 
Baada ya yote haya ningependa kumaliza kwa kusema ukilinda Utamaduni wa taifa umelinda amani ya taifa.
 
Huu ni mchango wangu wa katiba na samahani kama nimekosea.
 
Ndugu yenu,
 
Saleh Jaber.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images