Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 135 | 136 | (Page 137) | 138 | 139 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Baadhi ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za SADC wakiimba wimbo wa umoja huo katika mkutano wa mwaka wa  kumi na nane wa shirikisho la Wakuu wa polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka.
   Baadhi ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za SADC wakiimba wimbo wa umoja huo katika mkutano wa mwaka wa  kumi na nane wa shirikisho la Wakuu wa polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema akizungumza katika mkutano wa mwaka wa  kumi na nane wa shirikisho la Wakuu wa polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka
  Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil akizungumza katika hafla fupi ya kufungua mkutano wa mwaka wa  kumi na nane wa shirikisho la Wakuu wa polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka.
  Picha zote na Frank Geofary wa Jeshi la Polisi

  0 0

  Ubao  wa matangazo  ukionyesha namna  ambavyo kila Nchi ilivyopiga  Kura yake   Azimio  Kuhusu hali ya  Syria,  upigaji kura huo ulifanyika wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokutana siku ya Jumatano. Azimio hilo lilipitishwa kwa kura za ndiyo 107,  za hapana 12 na 59 za kutofungamana na upande wowote.  Madhumuni ya  Azimio hilo ni kuchagiza usitishaji wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchi humo. Ingawa Azimio hilo limepita lakini limelalamikiwa  kwamba mchakato wake haukuwa wazi, shirikishi,  halikuzingatia ushauri wa wajumbe wengine na  lilikuwa limeegema upande mmoja.

  0 0

  Mbinu hii imefanikiwa kuthibiti wizi wa mfuniko wa barabarani kwa asilimia mia moja sasa kwani yapata mwezi sasa mfuniko huu uliopo mtaa wa Jamhuri jijini Dar es salaam una mwezi na ushee hivi haujachapwa.
  Pongezi kwa waliobuni mbinu hii ambayo pia inatumika kama kip-lefti kwenye barabara hiyo nyembamba

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete welcomes to the State House Joint Special Representative of the African Union-Unite Nations Hybrid operation in Darfur(UNAMID) and Joint Chief Mediator Dr. Mohamed Ibn Chambas when the later paid a courtesy call on him in Dar es Salaam Wednesday.

  0 0

  Washindi watatu wa promosheni ya shinda tiketi na Western Union wameondoka kwa shamra shamra Dar es Salaam juzi usiku  kwenda kushuhudia fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Chelsea FC na SL Benfica iliyochezwa usiku wa kuamkia leo jijini Amsterdam. 
  Akizungumza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, mmoja wa washindi hao Bw. Quraish Shindo, amesema kwamba amefurahia sana nafasi aliyoipata kutoka kwa Western Union kwenda kuona mchezo huo laivu tofauti na pale alipokuwa amezoea kushuhudia kabumbu kwenye luninga. 
  “Unajua mi ni mshabiki mkubwa sana wa mpira wa miguu, kwahiyo nilivyoona promosheni hii, nikasema ngoja nijaribu bahati yangu. Mungu si Athumani, katika siku ya droo nikaibuka mmoja ya washindi na sasa niko hapa nikielekea Amsterdam kwa shauku kubwa,” Shindo alisema. 
  Aidha, Meneja Masoko wa Benki ya Posta (TPB) Bw. Andrew Chimazi amesema kwamba benki yao inaheshima kubwa sana katika kutoa huduma za Western Union na amefurahishwa sana na mshindi aliyepatikana kutoka benki kwake.
   “Nawatakia safari njema washindi wote, pili napenda kuwahakikishia umma na watanzania kwamba bado promosheni hii inaendelea na zawadi mbali mbali bado zipo zakushindaniwa zikiwemo ving’amuzi kutoka Star Times,” Shimazi aliongeza. 
  Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya Diamond Trust (DTB) Bi. Chandni Jiwa, alitoa rai kwa wateja mbali mbali wa benki hiyo kuendelea kutuma na kupokea fedha kupitia huduma yao ya Western Union ili waweze kujishindia zawadi zingine bwelele zilizobaki. 
   “Nawatakia safari njema na natumai washindi watafurahia fainali hiyo na mji wa Amsterdam Uholanzi kwa ujumla,” aliongeza Bi. Jiwa. 
  Washindi wengine wa Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyodhaminiwa na Western Union ni Flora Mbuya na Mzee Patropa Ndanshau. 
   Mbali na kutazama mechi, wakiwa jijini Amsterdam, washindi hao watatu watatembezwa katika vivutio mbali mbali vya utalii pamoja nakuhudhuria tafrija maalum ya ‘Western Union Experience’ itakayowakutanisha na washindi wengine kutoka nchi mbali mbali duniani. Washindi wa Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya wanatarijwa kurejea tarehe Mei 17, 2013, baada ya kushuhudia fainali hiyo kali baina ya timu ya Uingereza Chelsea FC na SL Benfica kutoka Ureno.

     Kutoka kushoto katika picha ya pamoja ni Meneja Masoko wa Benki ya Posta (TPB) Bw. Andrew Chimazi, Quraish Shindo (mshindi), Flora Mbuya (mshindi), Mratibu wa promosheni hiyo kutoka 24D Brand Communications Bi. Farida Makame, Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya Diamond Trust (DTB) Bi. Chandni Jiwa na Bw. Patropa Ndanshau (mshindi) wakiwa uwanjani JNIA.      Mmoja wa washindi wa tiketi kuona fainali ya ligi ya mabingwa iliyodhaminiwa na Western Union Bw. Quraish Shindo akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu ushindi wake na safari ya kwenda kushuhudia fainali kati ya Chelsea FC na SL Benfica huko Amsterdam, Uholanzi       Meneja Masoko wa Benki ya Posta (TPB) Bw. Andrew Chimazi akisisitiza jambo kwa waandishi wa  habari kuhusu huduma na promosheni za Western Union alipofika uwanja wa JNIA kuwatakia safari njema washindi.      Washindi wa Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) Flora Mbuya (kulia) na mwenzake Quraish Shindo wakiwa katika wakati wa furaha kabla ya kukwea kuelekea jijini Amsterdam kushuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Chelsea FC na SL Benfica 


        Safari ndo imeiva: Mzee Patropa Ndanshau, ambaye ni msanifu maarufu wa majengo (architect)  wa kampuni ya Plan Associates ya Dar es salaam, akielekea katika mstari wa kukaguliwa uwanjani JNIA tayari kwa safari ya Amsterdam. Mzee Patropa alitabiria ushindi wa Chelsea FC dhidi ya SL Benfica. 


  0 0

  On a dramatic evening in Amsterdam on Wednesday, the Blues lifted the Europa League trophy with a 2-1 victory over Benfica and in so doing, became just the fourth club in history to take a European Grand Slam.

  0 0

   Mfalme wa muziki wa asili nchini Costa siboka 'Mfalme' anatarajia kuanza ziara yake ya utambulisho wa nyimbo mpya hivi karibuni.Siboka wiki ijayo atakuwa jiji la Mwanza na kuzunguka visiwa vyake vyote vinavyozunguka jiji hilo.Ikiwemo visiwa vya ukerewe,kisiwa cha ukara,kisiwa cha Ghana na kumalizia mjini Geita.
  Baada ya hapo ataelekea Mjini Mbeya na Tunduma kwa ajili ya kutambulisha nyimbo mpya inayoitwa TWISILE aloimba kwa Lugha ya kinyakyusa.Siboka Mfalme anadhaminiwa na KONYAGI, CXC Africa na Michuzi Blog.
  Vilevile ameanza muziki huu wa asili kwa kudhaminiwa na Balimi Extra Lager. Siboka anaomba wadhamini wengine wajitokeze kumpiga tafu. Halikadhalika, anasema Mfalme Siboka,  katika ziara hiyo atatangaza AMANI kwa Watanzania wote.
   Juu na chini ni Siboka Mfalme akiwa katika zaiara za mikoani siku za nyuma  0 0


  Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 wakiwa katika Picha ya Pamoja

  Baada ya shamlashamla na mapokezi makubwa ya Miss Utalii Tanzania walipo ingia Mkoani Tanga na kupokelewa na umati mkubwa wa watu, warembo hao wapo kambini tayari kwa maandalizi ya Fainali hizo.

  Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania zitafanyika Tarehe 19.05.2013 Mkoani Tanga ambapo warembo zaidi ya 30 watapanda Jukwaani kuwania Taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013 ndani ya Mkwakwani.

  Sambamba na Fainali hizo za Miss Utalii , kutakuwa na Burudani ya Kukata na shoka ambayo itasindikizwa na Bendi kongwe ya Muziki Msondo Ngoma kutoka Dar es salaam, Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao, Majuto Arts Group, Mdumange, vikundi vya ngoma na Sarakasi.

  Fainali za Taifa zitaanza kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 jioni Ambapo viingilio kwa watoto itakuwa 2,000 na wakubwa 5,000 Baada ya hapo kuanzia saa 1 usiku hadi Majogoo viti Maalum itakuwa ni 20,000 na kawaida itakuwa 10,000 

  Mpaka sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini ,wanajiandaa vizuri  kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.

  0 0

  Msanii maarufu wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya CPwaa ateuliwa na kampuni ya bia Heineken Tanzania kusimamia michuano ya mpira wa mezani (Foosball) pamoja na kutangaza na kuhamasisha mchezo huo wakati wa mashindano ambayo ni endelevu.Mpango huo ulikamilishwa kati ya kampuni ya Brainstormmusic & Media Co. Ltd na Heineken Tanzania Limited
   Cpwaa, msanii maarufu na wakimataifa wa Bongoflava akisaini mkataba wa kuteuliwa kuwa  msimamizi na MC wa michuano ya mpira wa mezani (Foosball) nchini Tanzania, pamoja naye ni Caroline Kakwezi meneja masoko wa Heineken Tanzania na Uche Unigwe Mkurugenzi wa Heineken Tanzania
  Sharon Mariwa Meneja Muenezi Biashara Brainstormusic, Caroline Kakwezi, Meneja Masoko wa Heineken Tanzania na Uche Unigwe – Mkurugenzi Mkuu na Cpwaa msanii maarufu wakishikana mikono na Mkurugenzi wa Heineken Tanzania baada ya kusaini mkataba wa kuteuliwa kuwa msimamizi na MC wa michuano ya mpira wa mezani (Foosball) kulia ni Ronald Louis Meneja Opereshini wa Brainstormusic.

  0 0


  0 0
 • 05/15/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ngoma ya 'Mama Ntilie' ya AT na Ray C inapendeza....

  0 0

  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Jaji Sambo akimkaribisha Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania kuongea na Watumishi wa Mahakama ya Sumbawanga mapema leo Katika jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.
  Jaji Mfawidhi Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo (aliyenyosha mkono) akimuelekeza baadhi ya maeneo Mhe. Jaji Mkuu na ujumbe wake alipotembelea jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mhe Jaji Mkuu yupo mkoani humo kwa lengo la kujionea Hali ya utoaji haki Katika Mkoa huo.
  Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman ( wa nne kutoka kulia) akiwa Katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa alipotembelea Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mapema Leo, lengo likiwa ni kujionea hali ya utoaji haki Katika Mkoa huo.(Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).


  Na Elizabeth Ntambala
  Sumbawanga
  JAJI mkuu wa Tanzania Mohamed Chande  amesema kuwa mahakama  kuu Tanzania inaendelea na mkakati endelevu wa miaka 2 utakao husisha unoreshajki wa miundombinu ya mahakama za ngazi zote nchini kutoa elimu ya kujiendeleza kwa watumishi wake na pia kuzitolea uamuzi kesi zote zilizochukua mda mrefu.

  Jaji mkuu  Mohamed Chande  aliyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya siku ya kwanza ya kukagua maendeleo ya utendaji haki kwa mahakam ya mikoa ya Rukwa na Katavi.

  Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed alisema kuwa utekelezaji wa mkakati huo ni moja ya miundombinu za kuondoa usumbufu wanaoupata wananchi wakati wa uendeshaji wa kesi zao na pia kuondoa lawama za muda mrefu za uwajibikaji mdogo na vitendo vya rushwa.

  Akiongea na watumishi wa mahakama hizo za hakimu mkazi wilaya na mkoa na baadae watumishi wa mahakama kuu kanda ya sumbawanga alidai kuwa zaidi ya shilingi bilioni 10 zinategemewa ku[itishwa katika mwaka huu wa fedha wa utekelezaji mkakati.

  Kwa upande wake hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Manase Goroba alisema kumekuwepo na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo hasa ya wapiga chapa ikiwamo ya uchakavu wa majengo mengi ambayo yanahitaji ukarabati mkubwa katika mahakama .

  Alisema kuwa kumekuwepo na mahakama mpya ambazo ni zilijengwa kwa nguvu za wananchi na bado majengo hayo hajakamilika hivyo kunahitaji fedha kwa ajili ya umaliziaji wa majengo hayo.
  Mustafa sijani ni hakimu wa mwanzo wa wilaya walimweleza jaji mkuu kuwa adha zinazowakabili watumishi wa mahakama katika utendaji wa kazi ni pamoja na uhaba wa watumishi vitendea kazi.  0 0

  Mgeni rasmi Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi viongozi wakuu wa TAPSEA pamoja na waratibu wa Kongamano hilo la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.
  Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda akimkaribisha Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda alipokuwa akiwasili  mapema leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu akimkabidhi zawadi ya kinyago mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mh.Mama Tunu Pinda ,shoto kwake ni Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda wakati wa Kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania.
  Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mh.Mama Tunu Pinda akifungua Kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania,lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC ..
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania,lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

  Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mh.Sofia Simba akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kwenye
  mkutano wa Kongamano  la  tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania,uliofanyika mapema leo  kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

  Sehemu ya meza kuu ndani ya mkutano wa kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC,kutoka kushoto ni  Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mh.Sofia Simba,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu,Mgeni rasmi wa Kongamano hilo la TAPSEA,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda pamoja na Naibu Waziri wa katiba na sheria ambaye pia ni Mshauri wa masuala ya sheria na kazi waTAPSEA,Bi.Angella Kairuki.
  Pichani ni sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.

  0 0


   MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amewaasa Makatibu Muhtasi na kuwataka wazingatie maadili ya taaluma yao ya uhazili ili kuongeza ufanisi wa majukumu ya kazi zao.


  Ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Mei 16, 2013) wakati akifungua Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.


  Kongamano hilo la siku mbili, limehudhuriwa na Makatibu Muhtasi zaidi ya 1,500 kutoka mikoa yote nchini, na baadhi ya wawezeshaji kutoka Kenya, Uganda na Rwanda.


  “Umuhimu wa taaluma ya uhazili katika taasisi tunazofanyia kazi unatokana na nafasi  kubwa ya makatibu muhtasi kama wasimamizi wa ofisi na wasaidizi wa watendaji wakuu. Nafasi yenu inawapa fursa ya kuandaa na kutunza nyaraka mbalimbali za kiofisi zinazohusu menejimenti ya taasisi hizo. Niwaombe makatibu muhtasi wote mzingatie maadili ya kazi ya uhazili katika kutekeleza majukumu yenu,” alisisitiza.


  Aliwataka waongeze jitihada za kukimarisha Chama cheo ili hatimaye TAPSEA iweze kuenea Mikoa yote na kuwa Chombo kitakachosimamia miiko na maadili ya fani ya Uhazili.


  Alisema majukumu ya makatibu muhtasi siyo kupiga chapa pekee na kuongeza kwamba, kama chama cha kitaaluma, TAPSEA lazima iendeleze jitihada za kubadili mtazamo huo ili jamii iweze kutambua umuhimu wa nafasi ya makatibu muhtasi katika taasisi mbalimbali za umma na za sekta binafsi.


  “Hata hivyo, napenda ieleweke kwamba kazi ya kuleta mabadiliko ya kimtazamo inaanzia kwa katibu muhtasi mwenyewe. Nawashauri wanachama wote wa TAPSEA wawe mstari wa mbele katika kubadilika kifikra na kujiendeleza kila wakati ili kujijengea uwezo wa kuzikabili ipasavyo changamoto za taaluma ya uhazili katika mazingira ya sasa,” alisema.


  Mama Tunu Pinda alisema kuwekeza katika teknolojia ni jambo muhimu lakini teknolojia pekee haiwezi kuleta mabadiliko chanya katika kuboresha huduma na kuongeza tija. “Jambo hili ni lazima liende sambamba na uwekezaji katika rasilimali watu kwa watumishi kusoma zaidi na kupatiwa fursa za mafunzo zaidi ndani na nje ya nchi,” alisisitiza.


  Mama Tunu Pinda pia alizindua TAPSEA SACCOS na kuwataka makatibu muhtasi hao wajiunge kwa wingi ili kutunisha mfuko wa chama chao.


  Mapema, akimkaribisha kuzungumza na washiriki wa mkutano, Mlezi wa TAPSEA Dk. Mary Nagu ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Uwekezaji na Uwezeshaji aliwataka wawe waaminifu katika kuijenga TAPSEA SACCOS ili hatimaye ifikie hatua ya kuwa benki yao maalum kama ilivyo kwa Chama cha Walimu nchini.


  Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Angela Kairuki ambaye pia mshauri wa Kisheria wa TAPSEA aliwataka washiriki wa kongamano hilo kuzingatia maadili kwa kutunza siri za ofisi wanazozitumikia.


  “Inasikitisha kuona kila mara kunakuwa na taarifa ambazo zinavuja lakini ukifuatilia wapi taarifa hizo zimetokea utabaini kuwa chanzo ni makatibu muhtasi... ninawaomba sana mjitahidi kutunza siri za taasisi zenu,” alisisitiza.  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  ALHAMISI, MEI 16, 2013.

  0 0


   BMW Z3 - 1998, 6gear AUTO, Convertible, RHD, Imported & registered in January 2013 for sale.  Original Germany made. 
  Serious buyers (no middlemen) call  +255684860860
   


  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi anayeshuhulikia mashirikiano ya nchi mbili wa Denmark Charlotte Slente,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo mchana akiwa na ujumbe aliofuatana nao,akiwemo Balozi wa Denmark nchini Johnny Flento.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi anayeshuhulikia Mashirikiano ya nchi mbili wa Denmark Charlotte Slente,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo mchana akiwa na ujumbe aliofuatana nao,akiwemo Balozi wa Denmark nchini Johnny Flento,(kushoto) [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0


  Ili kuondoa mkanganyiko ambao umeanza kujitokeza, Wizara inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tamko lililotolewa na Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. 

  Aidha, kama ilivyoelezwa katika taarifa mbalimbali za umma zilizokwisha kutolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na  TFDA  kuhusiana na suala hili, bado inasisitizwa kwamba kampuni ya TPI Ltd iliiuzia Bohari  ya Dawa (MSD) dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo.

  Tunapenda kusisitiza kwamba, Mhe. Waziri katika hotuba yake hakukanusha kuwa kampuni ya TPI Ltd iliiuzia MSD dawa bandia bali alieleza kwamba uchunguzi wa awali katika kiwanda cha kampuni hiyo haukuonesha dawa hiyo ilizalishwa na TPI Ltd  bali vifungashio ni vya TPI Ltd na nyaraka zinaonesha TPI Ltd kuiuzia MSD dawa hizo bandia.

  Aidha, alieleza kuwa vyombo vya usalama bado vinaendelea kulichunguza suala hilo ili kubaini chanzo na wahusika wakuu wa dawa hizo bandia.

  Kwa kuzingatia unyeti wa suala hili, Wizara inatoa wito kwa vyombo vya habari kusubiri hatma ya uchunguzi unaofanywa na vyombo vya usalama na kuepuka kutoa taarifa ambazo zinaweza kupotosha umma na jitihada kubwa za Serikali katika kupambana na dawa bandia nchini.

  Imetolewa na:

  N. Mwamwaja

  MSEMAJI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

  16 Mei, 2013


  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi za bendera ya taifa) akiwa na Mratibu wa Tanzania wa Taasisi ya Wataalam Waandamizi wa Uholanzi(PUM) Mhe. Samuel Goldfinger. Balozi Kamala amemtembelea Mratibu huyo ofisini kwake mjini the Hague na kumuomba Taasisi yake ikubali kushirikiana na Tanzania kuandaa mpango wa kuwezesha vijana wa Kitanzania kupata ujuzi wa kuwawezesha kujiajiri na kuajiriwa. (Skills Development). PUM wamekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuandaa mpango huo.

  0 0


  Tanzania's most celebrated pugilist  Francis Boniface Cheka  (pictured) is shopping for an opponent from outside the African continent for his optional defense of his title for the fourth time. Cheka’s desire for foreign boxers derived from the dismal performances exhibited by Africa boxers he had met so far. 

  “I have yet to see any African boxer who has challenged me aggressively” says Cheka, the IBF Continental Africa Super Middleweight King” .

  Francis Cheka won the IBF Continental Africa Super Welterweight Title  for the first time in 2005 and vacated it the following year  for other “less colorful titles” only to recapture it in 2011 and has since defended it successfully! He is the most celebrated boxer in Tanzania and the whole of East & Central African region.

  His metaphor of the country’s name and status out pass that of many sportsmen and women before him as he has accumulated a lot of respects from various quarters within African boxing fraternity! This is one boxer who enjoys boxing and when he is the ring his body language connect with that of the spectators in the venue as they sing and cheers him throughout the fight punch after punch to victory!

  Born in Dar es salaam and raised in Morogoro, Francis Boniface Cheka is a great boxing entrepreneur who know how to tilt the sport to his favor. He is so popular in Tanzania that youths emulate how he dresses and walk. Francis Boniface Cheka is larger than life as far as boxing in Tanzania and East Africa is concerned. He epitomizes glory and the success which come with  prize fighting!

  Cheka's investments portfolio calls for admiration in that very few sportsmen/women in Tanzania have invested to so many enterprises without proper formal education!  He runs  a string of business enterprises springing from plastic recycling factories to environment management! He is the role model to many young people in Tanzania.

  And now, he is shopping for a pound to pound boxer from outside Africa to match his boxing caliber, saying that he is above the level of many opponents from the Continent! If you happen to hear him speaking for the first time you would compare him with a professor lecturing students. He is so organized in his life as well as in the ring.
                                                                                                                                                              
  Cheka is the only boxer who cannot take a fight if he is not well prepared not matter what the price can be. When preparing for a fight he secludes himself from all luxuries in the world, including staying away from his beloved wife saying that sex and wine are the greatest destruction for sportsmen/women!

older | 1 | .... | 135 | 136 | (Page 137) | 138 | 139 | .... | 3285 | newer