Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 133 | 134 | (Page 135) | 136 | 137 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Wito umetolewa kwa serikali za Afrika kutoa msaada kwa wakulima wanawake kama bara hilo linataka kufikia maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi.

  Akihutubia kongamano kubwa la kikanda la kilimo la muungano wa umoja wa vyama vya kilimo kusini mwa Afrika (SACAU) jana jijini Dar es Salaam, waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Nigeria, Dkt. Akinwumi Adesina alisema ni muhimu serikali na wadau wengine wanaosaidia maendeleo ya kilimo wakajua kuwa wakulima wengi katika bara hilo ni wanawake.

  “Bila wakulima wanawake, bara la Afrika haliwezi kufikia malengo yake katika sekta hii ya kilimo,” alisema. Kongamano hilo litakaloangalia kwa undani swala la jinsi ya kuhudumia kifedha kilimo cha Afrika linatayarishwa na Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) kwa kushirikiana na SACAU.

  “Wakulima wanawake wanahitaji kupata mikopo nafuu, uhakika wa ardhi, na teknolojia,” alisema, na kuongeza kuwa mustakabali wa sekta ya kilimo katika bara la Afrika sio wa uhakika kama wanawake wakulima watawekwa pembezoni na mipango ya maendeleo yanayohusu sekta hiyo.

  Kongamano hilo linaloangalia kwa undani swala la jinsi ya kuhudumia kifedha kilimo cha Afrika linatayarishwa na Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) kwa kushirikiana na SACAU.

  Waziri huyo alisema kuwa hakuna sababu ya bara la Afrika kuagiza chakula toka nje wakati zaidi ya asilimia 60 ya ardhi inayofaa kwa kilimo na ambayo bado haijatumika iko katika bara hilo.

  “Kwa raslimali ya maji, ardhi na nguvu kazi ya kutosha tuliyonayo, tunatakiwa kulisha dunia,” alisema. Kwa upande wake, afisa mtendaji mkuu wa SACAU, Bw. Ishmael Sunga alisema kuwa wakulima wa Afrika hawawezi kuendelea kwa haraka na kuwa wakubwa kama hawataweza kupata huduma za uhakika za kifedha.

  “Tusiishie kuona chakula kinapatikana katika ngazi ya familia tu, bali tuendeleze sekta hii, wakulima na kuongeza uzalishaji,” alisema. Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao toka wizara ya Kilimo, Usalama wa Chakula na Ushirika, Dkt. Mshindo Msolla alisema ni muhimu kwa serikali za Afrika zikajitahidi kuwa na usalama wa chakula katika kila nchi kabla ya kufanya lolote.

  “Ni muhimu tukazalisha kwanza chakula cha kutosha katika maeneo yetu Afrika kabla ya kufikiria kitu kingine kwanza,” alisisitiza. Akizungumza kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Dkt. Msolla alisema kuwa serikali ya Tanzania inafanya juhudi kubwa sana kufikia mapinduzi ya kilimo kupitia mipango mbalimbali kama vili Kilimo Kwanza na mpango maalum wa kuendeleza kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

  Washiriki zaidi ya 200 kutoka nchi 14 za kusini mwa Afrika pamoja na wawakilishi wa vyama vya wakulima kutoka maeneo mengine ya Afrika wanashiriki kongamano hilo la siku tatu. Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utaangalia ushirikiano kati ya SADC/COMESA/EAC katika maswala ya kilimo. Pia mkutano huo utaangalia makisio ya mahitaji ya bidhaa za kilimo duniani na kuona fursa na tishio lake kwa wakulima.

  Pia washiriki hao wataangalia kama mfumo wa kifedha uliopo sasa unaweza au hauwezi kuendeleza sekta ya kilimo katika siku zijazo. Inatarajiwa kwamba Rais Jakaya Kikwete atahutubia mkutano huo leo (Jumanne).

  0 0


  0 0


  0 0
 • 05/14/13--01:45: Article 22


 • 0 0

    Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi akionesha ripoti na machapicho aliyozindua, wengine wanaoshuhudia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donan Mmbando
   Waziri wa Afya Dkt. Hussein Mwinyi akihutubia wakati wa uzinduzi huo
    Mkurugenzi Mkuu TFDA, Hiiti Sillo, akiwasilisha maelezo ya utangulizi katika uzinduzi wa taarifa ya ufuatiliaji wa dawa za ALu na machapisho mbalimbali

  Mwakilishi wa WHO, Dkt. Rufaro Chatora akiwasilisha salamu za WHO katika uzinduzi huo

  =========  ========= ==========

  TFDA YAZINDUA RIPOTI YA UFUATILIAJI WA KARIBU WA DAWA YA MALARIA AINA YA ALu KATIKA KUFUATILIA MADHARA YA DAWA
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Hussein A. Mwinyi  amezindua ripoti ya ufuatiliaji wa usalama wa dawa  mseto ya Malaria aina ya Artemether + Lumefantrine (ALu)  na  kusema kwamba imethibitika kisayansi ni salama na haina madhara makubwa  (adverse reactions) na badala yake ina madhara madogo yanayovumilika (side effects).  Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa  (TFDA) kupitia mpango wa Ufuatiliaji wa karibu wa madhara ya dawa ya ALu, imezinduliwa mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini.
  Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Hussein Mwinyi amewataka wananchi waliokuwa na wasiwasi juu ya dawa hii  kuendelea kuitumia dawa mseto ya Malaria aina ya ALu kwa kuwa ni salama.
  Sambamba na uzinduzi huo, Waziri pia amezindua machapisho yanayotumika katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wagonjwa kwa lengo la kufuatilia usalama wa dawa nchini. Machapisho hayo ni vitendea kazi katika mfumo wa ufuatiliaji wa karibu wa madhara ya dawa ambao unawezesha kukusanya taarifa nyingi zaidi na kuweza kufanya tathmini ya kisayansi ya uhusiano wa dawa na madhara yake.
  Kufuatia uzinduzi huo, Waziri amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutumia machapisho husika kama ilivyokusudiwa kwa lengo la ufuatiliaji wa madhara ya dawa kwa kuhakikisha fomu husika zinajazwa na kuwasilishwa TFDA kwa wakati.
  Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Rufaro Chatora, ameahidi kuendelea kuisaidia TFDA katika kuhakikisha kuwa usalama wa dawa unaendelea kudumishwa nchini.
  Wakati huohuo, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, amesema kuwa TFDA ipo katika hatua ya kukamilisha maandalizi ya ufuatiliaji wa karibu wa usalama wa dawa za kupunguza makali ya Ugonjwa wa UKIMWI (ARVs) katika mwaka wa fedha 2013/2014.
  Mfumo wa ufuatiliaji wa madhara ya dawa ya Malaria unaojulikana kitaalamu kama Cohort Event Monitoring (CEM) ulianza kutekelezwa nchini mwaka 2009 kufuatia mafunzo yaliyotolewa na WHO nchini Ghana ambapo TFDA ilishiriki.

  0 0
 • 05/14/13--02:22: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

 • 0 0


  Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini, Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusheherekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

  Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
  207 w Hampton Pl, 
  Capitol Height, MD

  Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, Mitindo ya mavazi kutoka Tanzania na hapa Marekani, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani na hapa Marekani yote ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili

  TEGA SIKIO, HABARI ZAIDI ZITAFUATA
  -------------------------------------------------------
  kwa wajasiliamali ambao wangepenga kudhamini na kuijipatia meza ya kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613 5165, 301 661 6696 na 301 792 8562 mwisho ni June 1, 2013 Asante


  NO COVER CHARGE, FREE DINNER

  0 0
 • 05/14/13--03:16: Article 18


 • 0 0

  Maofisa wa Jeshi kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Ghana, wakitembelea Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, kwa lengo la kujenga ushirikiano katika nyanja za Sayansi, Teknolojia, Kiuchumi na Kijamii.Maofisa wanaosoma katika chuo hicho wanatoka Afrika Kusini, Nigeria, Ivory Coast, Togo, Rwanda na Ghana.
   Meneja Uhusiano wa TBL, Doris Malulu (kulia) akitoa maelezo kwa maofisa hao kuhusu shughuli mbalimbali za kampuni hiyo.
  Maofisa wa Jeshi wakitembelea kiwanda hicho


  0 0

   Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka (R) hands over sports kits to TFF football development officer Salum Madadi for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.
   Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka addresses the media at a ceremony where Coca-Cola Tanzania handed over balls and bibs for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.
  TFF football development officer Salum Madadi speaks to the media at a ceremony where Coca-Cola Tanzania handed over balls and bibs for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.

  0 0

  WajumbewaBodiya SSRA wakiwa katika viwanja vya monyesho vya Nyerere Square mjini Dodoma kutoka kushoto ni Juma Muhimbi, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Jayne Nyimbo na Kabeho Solo.
   Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji cha SSRA, Sara Kibonde akifurahia jambo na Wakuu wa Mifuko ya GEPF, Daud Msangi na mfuko wa LAPF, Eliud Sanga.
   Meneja wa Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele akimkaribisha mjumbe wa bodi ya SSRA, Kabeho Solo katika banda la PPF.
     Meneja Masoko wa GEP, Aloyce Ntukamazi akitoa maelezo ya shughuli na faida wazipatazo wanachama wa GEPF kwa wajumbe wa bodi ya SSRA
   Ofisa wa Uwekezaji wa PSPF, Hamidu Ngororo akiwaeleza wajumbe wa SSRA mradi wa nyumba za bei nafuu za wanachama zilizopo Dar es salaam, Mtwara, Tanga, Shinyanga na Morogoro.

  0 0

  Amani masue akipokea cheti cha kuhitimu shahada yake ya pili ya (Masters of financial management)
  Picha ya pamoja wa wahitimu kutoka nchi mbali mbali zipatao 50 wakiwemo watanzania zaidi ya 40 waliohitimu katika shahada mbali mbali

  Picha ya pamoja ya baadhi ya watanzania waliohitimu

  pamoja na marafiki  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI ADMISSION OPEN FOR ACADEMIC  2013/14 UNIVERSITY OF MYSORE INDIA.  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akiongea na Watumishi hawapo picha Juu ya uboreshaji wa Mahakama nchini Katika suala zima la utoaji haki, kushoto kwa Jaji Mkuu ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, kulia ni Jaji Wa Mahakama Kuu, Mhe. Jaji Kaluwa.
  Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Aron Lyamuya (kushoto) akiwa na Mahakimu Wakazi wa Mkoa wa Mbeya Katika Mkutano Kati ya Jaji Mkuu na Watumishi wa Mahakama Mbeya.
  Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Mbeya wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu alipokuwa akiongea nao Leo. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).

  0 0
 • 05/14/13--07:20: Article 12

 • 0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa kuzungumzia Mustakabali wa maendeleo ya Wakulima Barani Afrika uliofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam leo.mkutano huo umeandaliwa na asasi ya(The southern African Confederation of Agriculktural Unions(SACAU).Wapili kushoto ni Kaimu Rais wa SACAU Bwana Ishmael Sunga na Watatu kushoto ni Waziri wa Kilimo Christopher Chiza.
  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Mkutano utakaojadili Mustakabali wa Maendeleo ya Wakulima Barani Afrika uliofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam ambao umendaliwa na asasi ya SACAU(The Southern African Confederation of Agricultural Unions).(picha na Freddy Maro).

  0 0
 • 05/14/13--07:51: Redd's Miss Ubungo 2013
 • Baadhi ya washiriki wa Shindano la Redd's Miss Ubungo 2013 wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao jana. Warembo hao wanataraji kupanda jukwaani Ijumaa ya Mei 17, mwaka huu katika Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza jijini Dar es Salaam na kusindikizwa na kundi zima la FM Academia wazee wa Ngwasuma.(Picha na Mpigapicha wetu).

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza hesabu za Serekali (P.A.C) Omar Ali Shehe akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wandishi wa habari kwa lengo la kupata mashirikino na ufanisi katika utendaji wa kazi zao. Kikao hicho kilifanyika Baraza la Wawakilishi Mbweni.
  Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee Ibrahim akichangia katika kikao cha Wadau mbalimbali wakiwemo wandishi wa habari wa vyombo tofauti kwa lengo la kupata mashirikino na ufanisi katika utendaji wa kazi zao, (kulia) Mhasibu Mkuu wa Serekali Omar Hassan, huko Baraza la Wawakilishi Mbweni.
  Mwandishi Salum Vuai, akitoa mchango wake kuhusu majukumu ya kamati ya kuchunguza hesabu za Serekali. Kikao hicho kilifanyika Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  Ramadhani Ali-Maelezo Zanzibar

  Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee Ibrahim amesema Serikali inawajibu wa kuyafanyia uchunguzi wa kina mapendekezo ya Kamati za Baraza la Wawakilishi na haipaswi kuwachukulia hatua moja kwa moja watu waliotajwa ndani ya taarifa kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma.

  Mkurugenzi huyo ameeleza hayo leo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa pamoja kati ya Kamati ya Uchunguzi wa Mahesabu ya Serikali na Mashirika (PAC) na wadau wa Kamati hiyo kwenye Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani.

  Amesema katika kuyapitia na kuyafanyia uchunguzi mapendekezo ya kamati, wahusika wanaotajwa hupewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuyatolea uamuzi na kazi hiyo huchukua muda kukamilika.

  “Serikali haiwezi kuyachukulia hatua mapendekezo yote yanayotolewa na Kamati ya Baraza bila ya kuwapa nafasi ya kujitetea watuhumiwa na kubaini wanaostahiki ili kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wengine kupelekwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa Umma”, alieleza Ibrahim Mzee.

  Ameitaka Kamati ya PAC kuelewa kwamba kuna mchakato mkubwa unaotekelezwa na Serikali kabla ya kuchukua hatua zinazostahiki kwa wahusika na haipaswi kupewa shinikizo na chombo chochote.

  Amesema kazi ya Kamati ya PAC ni kuchunguza na kuishauri Serikali bila ya kutumia vitisho wala kutoa hukumu na kuipa muda Serikali kufanya wajibu unaostahiki ikiwa ni pamoja na kuwachukuliwa hatua waliobanika na makosa.

  Mkurugenzi wa Mashtka alieleza kwamba kumekuwa na muingiliano wa kazi kati ya kamati moja ya Baraza la Wawakilishi na Kamati nyengine na hivyo kupelekea kamati mbili kuhoji jambo moja.

  “Kamati mbili ama zaidi kuhoji kitu kimoja ni kasoro kubwa hivyo inafaa mujipange vizuri ili kila kamati ijuwe wajibu wake”, alisisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka.

  Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Khamis Mussa Omar ameitaka kamati ya PAC wanapowasilisha taarifa katika Baraza kupunguza hamasa kwani mara nyingi hujenga picha kwa jamii kuwa wahusika ni wizi na mafisadi.

  Akiwashukuru wadau wa PAC Mwenyekiti wa Kamati hiyo Omar Ali Shehe ameomba kujenga mashirikiano ya karibu kati yao na wadau wengine ili kufanikisha majukumu yao yao ya kazi.

  Amewahakikisha wadau hao kwamba Kamati ya PAC haina nia ya kumuonea Mtendaji yeyote wa Serikali lakini kubwa wanalofanya ni kuhakikisha rasilimali chache zilizopo Nchini zinawanufaisha Wananchi wote kwa mujibu wa nafasi zao.

  Wadau walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa mahesabu ya Serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Muhasibu Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka na Vyombo vya Habari.

  0 0

   Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Uhusiano wa Microsoft Africa, Louis Otieno,  Louis Onyango Otieno akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mihayo Wilmore na Mkurugenzi wa Utambuzi COSTECH, Faith Shimba.

  DAR ES SALAAM, Tanzania

  KAMPUNI za Microsoft na Uhuru One, wameanza mpango wa majaribio wa utoaji wa elimu ya Teknolojia ya Mawasiliano (Tehama) kwa kutumia mkongo wa Taifa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu lengo likiwa kuibua uvumbuzi mpya katika sekta hiyo.

  Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Uhusiano wa Microsoft Africa, Louis Otieno alisema mpango huo utachukua miezi sita hadi mwaka mmoja.


  Alisema mpango huo umewalenga wanafunzi kwa kuwa ndio kundi kubwa ambalo linaingia katika shughuli za uzalishaji ikiwa ni pamoja na ajira, ujasiriamali na ukweli kuwa ngazi ya elimu ya juu ndipo ambapo wanafunzi wanakuwa katika hali ya kuweza kubadilika.


  "Tumeangalia ngazi ya vyuo kwa kuwa ndio ambapo wanafunzi wanabadilika na hata kuweza kufanya uvumbuzi" alisema na kuongeza kuwa Tanzania ina vipaji vngi ambavyo vimeweza kufanya uvumbuzi katika eneo jingine lakini sio katika Teknohama.


  Awali akizungumza katika mkutano huo, Mtendaji wa wadau wa Uhuru One, Mihayo Wilmore alisema mpango huo umelenga watu kuweza kuutumia mkongo wa Taifa katika shughuli za habari na mawasiliano hususan maeneo ya vijijini.


  Alisema mkongo wa Taifa umefika hadi katika ngazi ya wilaya lakini lakini umekuwa hautumiki hali ambayo alisema chini ya makubaliano hayo yana lengo la kuhakikisha hali inakuwa tofauti na majaribio yanayofanyika ni endelevu na wadau zaidi wanakaribishwa.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) hapa nchini, Bw. Emmanuel Kalenzi alipofika Wizarani leo. Katika mazungumzo yao walizungumzia kuhusu maendeleo ya viwanda hapa nchini ikiwa ni pamoja na juhudi zinazofanywa na UNIDO kwa kushirikiana na SIDO katika kuendeleza viwanda vidogo vidogo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
  Bw. Kalenzi akifafanua jambo kwa Balozi Mushy wakati wa mazungumzo yao.
  Balozi Mushy (katikati) akiendelea na mazungumzo na Bw. Kalenzi huku Bi. Jubilata Shao, Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo hayo.
  Balozi Mushy akiagana na Bw. Kalenzi mara baada ya mazungumzo yao.

  0 0

  MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) leo katika ukumbi wa White House mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na wengine kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu imemteua mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chambani, Pemba Mattr Said .(Picha na Bashir Nkoromo).

older | 1 | .... | 133 | 134 | (Page 135) | 136 | 137 | .... | 3285 | newer