Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 132 | 133 | (Page 134) | 135 | 136 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Airtel Bw Sunil Colaso akiongea na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.
  Mkurugezi wa mauzo na masoko wa Airtel bw Mustafa Kapasi (kushoto) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo Afisa mauzo kanda ya dar es salaam Airtel John Gondwe baada ya kuhitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji ya muda wa miaka miwili yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU). Wafanyakazi 56 kutoka katika mikoa mbalimbali walihitimu mafunzo hayo, akishuhudia katikati ni Mkurugenzi Rasilimali watu Patrick Foya akifatiwa na Melvin Joel Meneja wa Centum Learning Makao Makuu.
  Meneja Mauzo wa Airtel Bw Stratory Mushi (katikati) akiwa katika picha ya pomaja na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.
  wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakikata keki kwa pamoja wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Bw. Juma Kasim Tindwa akizungumza katika majadiliano ya ushirikiano kwa manufaa ya wote(Smart Partnership Dialogue) kwa watu wa kada mbalimbali kisiwani humo, (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utwala kutoka Baraza la Taifa la Biashara ( TNBC),Bi. Oliva Vegulla (kulia mwisho) ni Mfanyabishara Bw. Ali Bakari na (katikati) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara Zanzibar (ZBC), Mr Ali Vuai Haji.


  0 0

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (katikati mwenye suti nyeusi) akipokea sehemu ya msaada wa mifuko 200 kutoka kwa Meneja Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza, iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Arusha mwishoni mwa wiki.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (katikati mwenye suti nyeusi) akimshukuru Meneja Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza, baada ya kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (kulia) akizungumza baada ya kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Twiga Cement kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni. Kulia kwake ni Meneja Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (aliyeshika kamba kulia) akisaidia maandalizi ya ujenzi wa daraja sehemu iliyoharibiwa na mafuriko katika hafla ambayo kampuni ya Twiga Cement ilikabodhi msaada wa saruji kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni.

  0 0


  Kwa usajili wa tuzo za muziki za rfi ambazo hufanyika kila mwaka na kuwashirikisha wanamuziki mbalimbali katika bara la Afrika bonyeza hapo chini rfi music award registration.

  0 0

  Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka addresses the media at a ceremony where Coca-Cola Tanzania handed over balls and bibs for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.
  TFF football development officer Salum Madadi speaks to the media at a ceremony where Coca-Cola Tanzania handed over balls and bibs for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.
  Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka (R) hands over sports kits to TFF football development officer Salum Madadi for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.

  Coca-Cola has handed over balls and bibs to the Tanzania Football Federation (TFF) for youth teams taking part in this year’s Copa Coca-Cola football tournament which has now moved from U-17 to U-15 in order harness and expose talent from a younger age giving players a better chance of being picked up by local football academies and clubs.

  The first batch of the sports kits which caters for the district level phase of the tournament was received on behalf of TFF by football development officer Mr. Salum Madadi who called on all regional football association to observe rules and regulations governing the tournament. The presentation ceremony was held at Coca-Cola Tanzania offices over the weekend.

  He said that some of the districts had already started matches and urged the rest to begin the tournament as soon as possible now that the balls and bibs are available.

  Earlier in his remarks, Coca-Cola Tanzania Brand Manager Tanzania Maurice Njowoka underscored Coca-Cola’s commitment and obligation to continue supporting the championships which has played a significant role in identification of football talents in the country.

  “Our move from U-17 to U-15 gives COPA players the opportunity to develop their football skills and gain experience early, thus putting them at an advantage over their peers,” said Njowoka.

  In Africa, the Coca-Cola COPA tournament is run in over 20 countries giving more than 50,000 young players the opportunity to display their talent. Over the years, bona fide professional stars have emerged from the tournament including Zambian national team goalkeeper Kennedy Mweene and his teammates Nathan Sinkala and Stophila Sunzu; Ugandan international defender Timothy Batabaire; Nigeria FC Porto midfielder Mikel Agu; Kenyan midfielder McDonald Mariga; Tanzanian striker Thomas Ulimwengu; and South African duo Mandla Masango and Happy Jele among others.

  “We have many heroes born from the COPA Coca-Cola tournament each year,” said Njowoka. “The professional players who have made it big and inspire us all are heroes. Our players who work hard and support one another are heroes. The parents who offer support and guidance to our players are heroes. 

  The coaches who pour their hearts and souls into their teams are heroes. Even the fans who come out to cheer their teams are heroes and every day, we see new heroes emerge. This formed the thinking behind our new slogan ‘Where Heroes Are Born’ which you will see on all marketing materials going forward,” he added.

  This year’s tournament follows a successful campaign last season where the tournament was activated in over 20 markets across Africa with 134 players from Sub-Sahara Africa selected for a two-week international boot camp in Pretoria, South Africa.

  0 0

  Katibu Tawala msaidizi wa Serikali za Mitaa mkoa wa Lindi,Abdul Dachi akitoa elimu kwa Madiwani ikiwemo wajibu na majukumu yao katika semina ya uelimishaji kwa madiwani ikiwemo kupitia mpango wa maendeleo ya wilaya hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Addoh Mapunda akitoa taarifa kwa Madiwani kuhusu Mpango wa Uboreshaji wa Wilaya ya Kilwa ikiwemo Upimaji wa Viwanja katika semina kwa Madiwani na kufuatiwa na kikao Maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kupitisha mpango wa maendeleo.
  Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa wakiwa katika kikao maalum ili kujadiliana na kupitisha mpango wa maendeleo ya wilaya hiyo.
  Jumba la Maendeleo Wilayani kilwa jengo ambalo linatumika sasa katika kuendeshea vikao mbalimbali ikiwemo Baraza la Madiwani na hafla mbalimbali kama sherehe za Ndoa na burudani zingine na kupitia mpango huo Halmashauri itajenga ukumbi wa kisasa utakaogharimu tshs 3.5 Bilion.

  Na Abdulaziz Video. 

  Baraza la madiwani ktk halmashauri ya wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, limepitisha kwa kauli moja Mpango wa kuboresha maendeleo ya halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa dhamana wa Taifa (UNIT TRUST OF TANZANIA}.

  Mpango huo uliopitishwa, unajumuisha miradi miwili mikubwa ya upimaji wa zaidi ya viwanja 6,000 ktk mji mdogo wa Kilwa Masoko, mji mkongwe wa Kivinje na Nangurukuru pamoja na ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa Katika Mji mdogo wa Kilwa Masoko.

  Taarifa ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kilwa Adoh Mapunda kwa wajumbe wa Baraza hilo, imebainisha kuwa zoezi zima la utekelezaji wa mradi huo linategemewa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 8 ambapo shilingi bilioni 4.5 zitatumika kwenye upimaji wa viwanja na ujenzi wa ukumbi utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.5.

  Akizungumzia juu ya tatizo sugu la upimaji wa viwanja katika halmashauri hiyo mkurugenzi huyo amesema kwa zaidi ya miaka 20 sasa kuna viwanja 200 tu vilivyopimwa na kuthibitishwa ktk mji wa Masoko na hivyo kusababisha upungufu mkubwa wa viwanja na kuwafanya baadhi ya watu kujenga kiholela au kulazimika kutoa rushwa kwa wafanyakazi wa idara ya ardhi ili kupimiwa viwanja.

  0 0

  Rais wa zamani wa Nigeria,Chief Olusegun Obasanjo akiongea katika uzindunzi wa Jengo la utafkiri wa kisayansi wa kilimo katika nchi za tropiki lililopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  picha zaidi zitawajia baadae kidogo

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
  Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chifu Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo pamoja na Rais Mstaafu,Mh. Benjamin Mkapa wakizindua rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI  0 0

  Mechi ya Fainali kugombea kombe la Mbuzi na jezi kati ya Manunda FC na G-West iliyofanyika kwenye Uwanja wa Msisiri A Jana 12/5/2013 Mwananyamala DSM ilikua na vimbwanga vya aina yake ambapo moja ya tukio la kukumbukwa ni pale timu hizo zilipokataa katakata kubadili jezi zilizokuwa zikilandana kwa madai kwamba tayari zilishapitia kwa "Babu" Licha ya Jitihada ya mwamuzi na watu wenye ushawishi, hakuna timu iliyokubali na hivyo mwamuzi akalazimika kuchezesha mechi hiyo ya mchangani kwa matakwa ya timu hizo
  Mechi hiyo iliishia kwa G West kuibuka mabingwa kwa njia ya Penalty 4-2 baada ya dakika za kawaida kuisha kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1, wafungaji wakiwa na Msimbe kwa Manunda dk ya 43 na Mome dk ya 81

  Matukio mengine yaliyogubika mechi hizo ni wachezaji wawili wa G-West kuanguka uwanjani kwa imani za kuzidiwa na majini, pamoja na washabiki kuvunja nazi na mayai kwa imani za ushirikina na G-West kunyweshwa maji yaliyochanganywa na majani mithili ya Alovera badala ya maji ya kawaida  


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akifungua kongamano la tatu la waandishi wa habari na wadau wa habari mkoa wa Kilimanjaro lilifanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkoa.
  Mkuu wa wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi akizungumza na wadau wa habari wakati wa kongamano la wadau na wanahabari lililofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
  Watoa mada katika kongamano la wadau wa habari na wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro linaloendelea katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.kutoka kushoto ni afisa mtendaji utawala wa kiwanda cha sukari TPC,Jafary Ally ,meneja wa kituo cha Radio cha Kibo fm ,Abdalah Husein na mhadhiri wa chuo kikuu cha mtakatifu Stephano Moshi ,SMMUCO,Gasper Mpehongwa. Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Annacleti Kashuliza akifungua mafunzo ya wiki 3 ya Vijana 40 waliohitimu masomo ya elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana kazi leo jijini Dar es salaam .Mafunzo hayo kwa vijana yanalenga kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi ya maendeleo na kuwafanya waweze kuajiri vijana wengine pamoja na kusaidiwa kupata fedha benki kwa ajili ya kuanzisha biashara kutokana na michanganuo watakayoiwasilisha.
  Sehemu ya Vijana 40 waliohitimu katika chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana ajira wakiwa katika mafunzo ya wiki 3 ya kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi itakayowajengea uwezo wa kuajiri vijana wengine. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Biashara yameandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) na Kituo cha masuala ya Biashara na uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDEC) ikiwa ni moja ya mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wa vyuo vikuu nchini. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM kata ya Themi,Petro Ndarivoi akirudisha kadi ya chama cha mapinduzi kwa mwenyekiti wa chama cha CUF halmashauri ya jiji la Arusha,Hamza Mustaph kwenye makao makuu ya chama hicho jana jioni.
  Mgombea udiwani kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF kata ya Themi kwenye uchaguzi utakaoanza wiki ijayo Petro Ndarivoi akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya CUF halmashauri ya jiji la Arusha jana jioni wakati aliporudisha rasmi kadi ya ccm na kuchuwa kadi ya CUF mbele ya mgombea udiwani kwenye kata ya ELERAI John Bayo na mwenyekiti wa CUF wilaya ya Arusha Hamza Mustaph.(picha na mahmoud ahmad arusha).

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Mohamed Chande Othman akisalimiana na mmoja wa Maafisa wa Mahakama Mara alipowasili Katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya leo, katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Jaji Noel Chocha.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi waliokuja kumpokea Katika Uwanja wa Ndege wa Songwe jijini Mbeya, Mhe Jaji Mkuu amewasili mkoani Mbeya Katika ziara ya kikazi ya kutembelea Mahakama mkoani Mbeya. Picha na Mary Gwera

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akitoa mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo uliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha, mwishoni mwa wiki. 
  Mmoja wa wajumbe wa mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa CRDB akiwa katika maandalizia ya kuingia katika ukumbi wa  mikutano wa AICC jijini Arusha.
   Mtangazaji Mkongwe, SalimMbonde (kulia) akifuatilia Mkutano Mkuu wa  18 wa Wanahisa wa CRDB uliofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
   Wanahisa wa mkutano huo.
   Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Arusha.
   Mwanahisa akitoa mada.
   Mwenyekiti wa Mkutano huo akisoma majina ya wajumbe waliochaguliwa kuingia katika Bodi ya Wakurugenzi.
   Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kushoto) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo pamoja na mmoja wa wanahisa (wa pili kulia). 
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyadhiyay akiwa na mke wake pamoja na mjumbe wa bodi ya CRDB, Kai. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.

   Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei.
   Wanahisa.
  Charles Itembe akitoa mada kuhusu fursa za uwekezaji na upatikanaji mitaji katika masoko ya fedha wakati wa semina ya wanahisa wa benki ya CRDB iliyofanyika mjini Arusha.

  0 0
 • 05/13/13--09:07: Article 6


 • 0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda na kitaifa. Katika Mkutano huo Mhe. Membe alifafanua juu ya hali ya kisiasa nchini Madagascar na Zimbabwe na kutoa taarifa za kuwasili kwa vikosi vya kulinda amani vya Tanzania huko Mashariki mwa DRC. Kuhusu masuala ya kitaifa Mhe. Membe alilitolea ufafanuzi suala la shambulio la bomu lilitokea hivi karibuni huko Arusha ambapo alisema kuwa Serikali inaendelea na uchunguzi  na kwa ujumla hali nchini ni tulivu. Wengine katika picha ni Bw. John Haule (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe.Khalfan  Juma Mpango (kulia), Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Mei, 2013.


  Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (wa pili kushoto) kwa pamoja na baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza mhe. Waziri Membe (hayupo pichani) wakati alipozungumza na Mabalozi hao.


  Mabalozi wengine na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

  Sehemu nyingine ya Mabalozi wakati Mhe. Membe alipozungumza nao.


  Balozi Mpango akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake mara baada ya Mhe. Membe kumaliza mazungumzo nao.  Picha zaidi za mkutano huo wa Mhe. Membe na Mabalozi.


  Mhe. Membe akizungumza na Waandishii wa Vyombo mbalimbali vya Habari juu ya mazungumzo yake  na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hao hapa nchini.

  0 0

  THE COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLGY (COSTECH) IS RUNNING A TRAINING OF CAPACITY BUILDING WORKSHOP FOR HIGHER LEARNING INSTITUTIONS AND TECHNICAL SCHOOLS ON THE AREA OF OIL AND GAS AT MILLENIUM RESORT BAGAMOYO ON 13-16 MAY 2013

  Mr Halard Arnt Friisk from Norway presenting about the Sub Sea Production System to the members during the training of capacity building on the area of oil and gas    A section of participants from the higher leaning and technical institutions listening carefully to the presentations organized by COSTECH
  Prof Jostein Pettersen from Norway University of Science and Technology (NTNU) giving his presentation


  A group photo of the participants

  Group discussions

  0 0  0 0


  The department of Statistics of the University of Dodoma is announcing short course training on hypothesis testing that is going to be conducted on May 18 – 19, 2013. Apart from other things the training will cover hypothesis testing in correlation and regression.

  Venue: MRL 2 (Social Science Masters Class)

  Training Fee: TZS 50,000/= for UDOM students and TZS 150,000/= for others.

  Mode of payment:     All payments should be done through;
  Account Name: College of Natural and Mathematical Sciences; Account no: 0150221567000
  Bank: CRDB.

  Mode of Registration: Send message or email indicating your name after making payment
  using contact below. All participants will be required to present bank    deposit slip.

  Participants are required to come with their laptops.

  For more information, please contact; Josephat Peter,
  Mobile: 0718 453 773


  NB: We invite requests from various interested groups to communicate with us for the training
         to be conducted in their respective places.

  0 0

  WASANII wa Muziki wa Kizazi kipya Naseeb Abdul 'Diamond Platinam' na Ney wa mitego wanatarajia kupanda jukwaa moja kumtafuta nani mkali katika uzinduzi wa video ya Muziki gani itakayozinduliwa Mei 18 mwaka huu katika ukumbi wa Dar LIVE mbagala, Dar ers Salaam.

  Uzinduzi wa Video hiyo ambao umeandaliwa na Kampuni ya Yuneda Entertainment inayohusika na masuala ya burudani itawapambanisha wasanii hao ambao kutatafutwa nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva ambapo nyimbo hiyo ya muziki gani inamahadhi ya kubishana kati ya miziki hiyo.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati wa kutambulisha uzinduzi huo, Mratibu wa onesho hilo Kahabi Mwendesha alisema uzinduzi huo utasindikizwa na wasanii wa Hip Hop na Bongo Fleva na kuwataka mashabiki wa fike kwa wingi ili kushuhudia wababe hao.

  "Onesho hili litakuwa ni la kumtafuta nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva ambapo kupitia uzinduzi wa video hii utadhihirisha nani mkali kati ya muziki wa bongo fleva na hip hop,"alisema Mwendesha.

  Alisema mara baada ya video hiyo kuzinduliwa Mei 18 Dar LIVE uzinduzi huo utahahamia katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza, na baadaye Arusha na kuwataka mashabiki wa mikoa hiyo kukaa tayari kwa ajili ya burudani hiyo.

  Alisema viingilio katika onesho hilo vitakuwa ni sh. 10,000 huku akisisitiza ulinzi kuimarishwa ambapo pia alisema kwa mashabiki wa burudani ambao hawatakuwa na viingilio kwa ajili ya mechi ya Simba na Yanga wafike katika ukumbi huo kwa kuwa mechi ya watani hao wa jadi itaoneshwa LIVE kupitia televisheni kubwa zilizipo ukumbini hapo.

older | 1 | .... | 132 | 133 | (Page 134) | 135 | 136 | .... | 3270 | newer