Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1352 | 1353 | (Page 1354) | 1355 | 1356 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) itaanza kutoa Vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini kwa wananchi wote waliokamilisha taratibu za usajili na utambuzi na kuchukuliwa alama za kibaiolojia (Alama za vidole, Picha, Saini ya Kielektroniki).

  Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew Massawe; utekelezaji wa zoezi hilo utaanza rasmi Jumanne tarehe 14 Septemba 2016 katika ofisi zote za NIDA zikiwemo ofisi za Wilaya zilizoanza usajili Tanzania Zanzibar na mikoa ya Dar-es-salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, na Ruvuma) pamoja na waheshimiwa Wabunge Dodoma.

  Waombaji wote ambao Vitambulisho vyao viko tayari watatumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) katika simu zao za kiganjani (mkononi) kufahamishwa kufika katika vituo vya Usajili kuchukua Vitambulisho vyao.

  Kuhusu wananchi ambao tayari wana Vitambulisho visivyo na saini; Bw. Massawe amesema…. “ Mamlaka inakusudia kubadilisha vitambulisho vyote vya zamani visivyo na saini, ila kwa sasa vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika sambamba na vipya wakati taratibu za kuendelea kuvibadilisha zikiendelea” alisisitiza.
  Amesema kutokana na uwepo wa njia nyingi na salama za kusoma taarifa za mwombaji zilizomo ndani ya kifaa maalumu kilichofichwa kwenye kadi ya mtumiaji (chip); ndiyo maana vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika katika huduma mbalimbali zinazohitaji kumtambua mtumiaji kabla ya kupata huduma.

  Akizungumzia wananchi ambao hawakuwahi kusajiliwa, Bw. Massawe amesisitiza kwamba wananchi wote ambao hawakuwahi kusajiliwa na wana umri wa miaka 18 na kuendelea; kwa mikoa ambayo tayari kuna ofisi za usajili, kuendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kupata Vitambulisho vya Taifa kwani zoezi la usajili ni endelevu.
  “Kwa wale wananchi ambao walisajiliwa kupitia Daftari la Mpiga kura NEC; NIDA iko mbioni kuanza kutoa nambari za utambulisho wakati tukiendelea kukamilisha taratibu za usajili ili kupata utambulisho kamili na kuanza kunufaika na matumizi mapana ya Utambulisho wa Taifa wakati taratibu za uzalishaji wa Vitambulisho zikiendelea”.


  Wananchi wanakumbushwa kutunza vizuri Vitambulisho vyao ili kuepuka gharama kwani kitambulisho cha Taifa kwa mara ya kwanza kitatolewa bure na iwapo kitapotea, ili kupata kingine lazima mtumiaji akilipie.

  Kwa sasa vitambulisho vya Taifa vimeanza kutumika katika baadhi ya huduma nchini hususani kwenye mabenki kwa ajili ya kufungua akaunti na kuthibitisha taarifa za mtu kabla ya kupatiwa huduma.  Taratibu za kupanua wigo wa matumizi ya Vitambulisho kielektroniki kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zinaendelea.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijumuika na waumini wengine wa kiislam katika swala ya Idd El Hajj iliyoswaliwa kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam leo asubuhi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake katika swala ya Idd El Hajj iliyoswaliwa kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam leo asubuhi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na waumini wengine wa kiislam wakisikiliza maswaidha wakati wa swala ya Idd El Hajj iliyoswaliwa kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam leo asubuhi.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa DKT.John Pombe Magufuli ameahirisha ziara yake nchini Zambia ili ashughulikie tatizo la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16,mamia kujeruhiwa na nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera.


  0 0

   
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana (Jumamosi, 10 Septemba, 2016 mkoani Kagera.
   
  Tetemeko hilo lilitokea jana Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.
   
  Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya athari zilizotokana na maafa hayo.
   
  “Poleni sana tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea nchini. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Tuendelee kuwa na imani na watulivu  Serikali ipo pamoja nanyi na haitawatupa mkono,” amesema.
   
  Waziri Mkuu amesema Kamati ya Maafa ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu itakwenda wilaya za Kyerwa, Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya tathmini na kubaini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona namna ya kuwasaidia waathirika.
   
  Wakati huo huo Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa mkoa huo kuchukua hatua za haraka kwa kuwatafutia eneo salama la kulala wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakato ambayo mabweni yake yote yameathirika na tetemeko hilo na hayafai kutumika.
   
  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea namna mabweni ya shule hiyo yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi kulala uwanjani.
   
  Pia Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia kama kuna tetemeko linguine linaweza kutokea nchini ili Serikali iweze kuchukua tahadhari pamoja na kutoa elimu kwa umma namna ya kujikinga.
   
  Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa wanaendelea na jukumu la kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao zimeanguka. Pia mkoa unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.
   
  Awali Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170 wamelazwa na kutoa pole na kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na wenye matatizo ambayo yanahitaji matibabu kwenye hoispitali kubwa Serikali itahakikisha wanapelekwa huko na kuhudumiwa.
   
  (mwisho)
   IMETOLEWA NA:              
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI,SEPTEMBA 11, 2016

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (wa pili kushoto) wakati akiwasili katika Uwanja wa Karume kuhitimisha mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star Septemba 11, 2016 kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wanamichezo, wadau wa michezo na wanahabari kabla ya kushuhudia fainali ya mashindano hayo yiliyohitimisha mashindano hayo kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 Airtel Rising Star katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua wachezaji wa timu ya Morogoro Boys kabla ya kuanza kwa fainali kati yao na timu ya Ilala iliyofanyika katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikabidhi kikombe kwa nahodha wa Timu ya wasichana ya Temeke walioibuka washindi wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wasichana katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.


  0 0


  Mkurugenzi wa kiwanda cha ukamuaji na usafishaji wa mafuta ya alizeti cha Mukta Agro-Proccesing Co Ltd cha mjini Babati Mkoani Manyara, Bakari Mukta akishika mwenge wa uhuru ulipofika kuzindua kiwanda hicho.
  Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu George Mbijima, akipokea zawadi ya mafuta toka kwa mkurugenzi wa kiwanda cha ukamuaji na usafishaji wa mafuta ya alizeti cha Mukta Agro-Proccesing Co Ltd Bakari Mukta, mjini Babati Mkoani Manyara.

  0 0

   
    Viongozi wapya wa KIDIFA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege
   Mwenyekiti wa KIFIDA aliyemaliza muda wake, Hassan Ngubege akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa chama hicho Jesse John katiba ya chama hicho.
   
   
  Na Mwandishi Wetu,Kisarawe
  MTANGAZAJI nguli wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jesse John amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA) katika uchaguzi uliofanyika jana.
  Jesse ambaye aliupata uongozi huo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa aliibuka kidedea baada ya kupata kura 32 na kumshinda mpinzani wake Karim Wenge aliyepata kura 21.
  Katika uchaguzi huo Mohamed Lubondo alichaguliwa kuwa Katibu baada ya kupata kura 30 na kumshinda Francis Mkamba aliyepata kura 27.Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Amosi Kisebengo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa Abdul Mogella.
  Wasimamizi wa uchaguzi huo kutoka Chama Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), Mweka Hazina wa KIDIFA alichaguliwa Iddo Mtangaze na Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa kuwa Sadiki Nasoro.
  Mwakilishi wa klabu kutoka Tarafa ya Mzenga alichaguliwa kuwa Suleiman Mahenge, kutoka Tarafa ya Sungwi alichaguliwa Abdallah Kuga na Mwakilishi wa klabu alichaguliwa kuwa Ally Madega na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa mkoa alichaguliwa kuwa Mohamed Masenga.
  Mwenyekiti wa KIDIFA aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege akimkarisha Jesse kushukuru wajumbe aliwataka viongozi wapya kufufua matumaini ya vipaji vya vijana katika soka wilaya ya Kisarawe kwa kuanzisha mashindano mbalimbali yenye lengo la kutafuta vipaji.
  Jesse akiwashukuru wajumbe hao aliahidi kushirikiana na wadau wa soka ndani na nje ya wilaya hiyo kupata timu ya wilaya itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kama timu nyingine zinashiriki mashindano hayo.
  Mwenyekiti Jesse alisema wilaya ya Kisarawe ambako yeye ni mzaliwa wa asili alisema anaamini vijana wengi hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hivyo atatumia miaka minne ya uongozi kuzalisha vijana wazuri katika soka.

  0 0  Arusha. Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) zimetwaa ubingwa wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.

  Taswa FC na Taswa Queens ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) zilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika bonanza hilo la kusisimua na waandishi kushindana katika michezo mbalimbali mbali ya soka na netiboli.

  Timu ya Wazee Club ambao ilishika nafasi ya pili, ndiyo pekee iliyonusurika na kichapo katika bonanza hilo aada ya kuambulia sare ya mabao 2-2. Hata hivyo, timu hiyo ilibidi ifanya kazi ya ziada baada ya kusawazisha mabao mawili katika dakika sita za mwisho. Timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji cha AJTC kilishika nafasi ya tatu na timu ya mwisho ni Redio Sunrise.

  aswa FC ilianza kwa kasi na kufunga mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Saidi Seifu akipokea pasi safi za Majuto “Dr Regret” Omary. Martin Shila, Edrward Mbaga, Muhidin Sufiani, Zahoro Mlanzi, Salum Jaba na kipa wao, Mwarami Seifu walikuwa kizingiti kikubwa katika mechi zote.

  Katika mechi ya pili, Taswa FC ilishinda mabao 4-0n dhidi ya Sunriseb Redio , bao la kwanza likifungwa na kapteni, Wilbert Molandi kwa kuunganisha kona ya Hare Temba na baadaye Saidi Seifu akifunga mabao matatu kufutia pasi ya Athumani Jabir na Majuto Omary ambaye alitoa pasi ya bao la tatu na la nne.

  Katika mchezo wa mwisho, Taswa FC iliibuka na ushindi wa ba 1-0 dhidi ya AJTC, bao la dakika za majeruhi lilifungwa na Ali “Maradona” Salum kufuatia kona safi ya Majuto.Timu ya netiboli ya Taswa Queens ilifanya ‘mauaji’ kufuatia ushindi wa mabao 30-2 dhidi ya AJTC. Mabao ya Taswa Queens yalifungwa na Sharifa Mustapha aliyefunga mabao 22 na Rose Michael aliyefunga mabao nane.

  Taswa Queens ilitawala sana mchezo huo kupitiaa wachezajia wake, Zuhura Abdinoor, Johari William, Elizabeth Mbasa, Tatu, Mage na Vicky Godfrey.
  Timu zote hizo zilizawadiwa kitita cha sh 100,000 kila moja na kombe. Kwa upande wa kukimbiza Kuku, Taswa Queens pia walifanikiwa kuibuka na ushindi wakifuatiwa na Sunrise Radio ambao wote waliondoka na kuku kila mmoja.

  Mgeni rasmi katika bonanza hilo la 11 lillilofanyika katika viwanja vya General Tyre alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ambaye alisema kuwa waandishi wa habari ni muhimu kushiriki michezo ya aina mbalimbali ili kuiweka miili vizuri.

  Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Bonanza la 11 nahodha wa timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini(Taswa FC),Wilbert Molandi katika fainali la Bonanza la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha kwenye uwanja wa General Tyre jumapili,kulia ni Mwenyekiti wa Taswa FC,Majuto Omary na kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo,Mussa Juma.

  Nahodha wa timu ya Netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC)Zuhura Abdulnoor na mchezaji mkongwe wa Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini,(Taswa FC),Muhidin Sufiani(kulia)wakifurahia ushindi.

  Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akizungumza katika Bonanza la 11 la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha.  
  Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na waratibu wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha. 

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
   Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la maua  mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka.
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga   mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu  Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga   akipokea heshima mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka
    Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe Grace Mujuma akiwa na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Mhe Judith  Kapijimpanga wakifurahia wakati ndege iliyomchukua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ilipotua katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka.

  PICHA NA IKULU.

  0 0


   Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania wakimkabidhi nahodha wa Temeke wasichana Shamimu Hamisi kombe la ubigwa wa Airtel Rising Stars 2016.  Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
   Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye akimkabidhi nahodha wa Temeke wasichana Shamimu Hamisi kombe la ubigwa wa Airtel Rising Stars 2016.  Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
   Timu ya Morogoro wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016 kwa upande wa wavulana. Morogoro iliifunga Ilala 1-0 katika fainali iliyopigwa kwenye uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.
  Temeke wasichana wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016. Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.

  Goli pekee lililofungwa na mshambuliaji hatari Tepesi Evans wa Morogoro lilitosha kuifanya timu hiyo kuwa mabingwa wa michuano ya vijana chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 kwa kuwafunga Ilala 1-0. Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kuvutiwa yenye upinzani mkali ilishuhudiwa na mamia ya mashabiki akiwepo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.

  Baada ya kosa kosa nyingi, Evans aliachia shuti kali mnamo dakika 77 ya mchezo, shuti ambalo lilienda moja kwa moja na kuamsha shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki. Juhudi za Ilala kuzawashisha hazikuzaa matunda mpaka mchezo unamalizika.

  Mchezo huo ulikuwa ni kama marudio ya mechi ya Alhamisi ambapo timu hizo zilikutana kwenye hatua ya makundi huku Ilala ikitoka kichwa chini kwa kukubali kichapo cha 2-0.

  Akifunga michuano hiyo ya kila mwaka, Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na wadhamini. ‘Kwa kuwapa fursa wasichana na wavulana hawa kuonyesha vipaji vyao, ni kusaidia kubadilisha maisha yao kwani mpira wa soka ni zaidi ya burundani – ni kufahamiana, kupata uzoefu na zaidi, ni ajira’, alisema Nnauye.

  Naye Mkurungenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kampuni yake inajivunia mafanikio ya Airtel Rising Stars yaliyopatikana miaka tano iliyopita. ‘Wachezaji ambao waliisaidia Uganda kufuzu kwenye michuano ya AFCON 2017 Gabon ni uzao wa Airtel Rising Stars na ni uhakika hayo yatatokea Tanzania hivi karibuni’. Alisema Colaso huku akiongeza kuwa Airtel mpaka sasa ishawekeza Tshs2.4 billioni kwenye michuano hiyo.

  Kwa upande wake Raisi wa TFF Jamal Malinzi alielezea michuano ya Airtel Rising Stars kama michuano ya kutumainiwa katika kuibua vipaji. ‘Serengeti Boys na timu ya Taifa ya Wanawake ni ushuhuda tosha wa mafainikio ya michuano hii’, alisema Malinzi.
  Timu bora, wachezaji bora, waamuzi pamoja na makocha walipewa tuzo wakati wa fainali za michuano hiyo.

  Timu ya Temeke wasichana walishinda ubingwa wa michuano hiyo kwa penati 5-4 baada ya kwenda sare ya 2-2 kwenye muda wa kawaida.

  Wakati huo huo, timu ya Temeke wavulana walishinda nafasi ya tatu ya michuano hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati ya 5-4 dhidi ya Kinondoni baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye muda wa kawaida.

  Kinondoni wasichana walipata nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuwafunga wenzao Arusha 2-0. Magoli yote ya Kinondoni yalifungwa na Veronica Mapunda.

  0 0

  Wafanyabiashara wa Biashara Ndogondogo Maarufu kwa Jina la Machinga waanza kunufaika na Soko kuu la Kimataifa la Mwanjelwa lililopo Jijini Mbeya mara baada ya Serikali kuwaruhusu kuingia katika Soko hilo na kuwapiga marufuku kufanya tena Biashara zao nje ya Soko hilo na kuzingatia Utaratibu na Sheria za Soko hilo la Mwanjelwa Jijini Mbeya.
  Moja kati ya Wafanyabiashara hao akijipatia Taswira kwenye moja ya kijieneo alicho Kibuni kwajili ya kufanyia Biashara zake katika Soko hilo la Mwanjwelwa Jijini Mbeya.
  Kikundi cha Wafanyabiashara hao  ya umachinga wakidhadhiana Jambo ndani ya wigo wa Soko hilo mara baada ya kuruhusiwa kufanya Biashara zao ndani ya Soko hilo la Mwanjelwa.

  Moja ya Barabara Iliyo kuwa ikitumika na Wafanya Biashara hao katika Eneo la Mwanjelwa sasa Shwarii kabisaa hakuna anaeuza Nje ya Wigo wa Soko hilo.
  PICHA ZOTE NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Majagina wa muziki wa Afrika Mashariki na washindi wa tuzo kibao, Sauti Sol (Kenya) wameachia video ya wimbo wao unaofanya vizuri, KULIKO JANA, uliopo kwenye santuri yao ya tatu: Live and Die in Afrika. Bien wa Sauti Sol anaelezea maana ya wimbo huo, “Unamaanisha kuwa uaminifu wa Mungu haukomi kamwe. Huruma yake haiishi – kila uchao ni vipya.” Wakimshirikisha Redfourth Chorus (Upper Hill School), wimbo huo mtamu lakini wenye ujumbe mzito, umezikwea chati na kuwagusa mashabiki barani Afrika na zaidi.

  Video maarufu ya Sauti Sol wakiimba akapela ya wimbo huo wakiwa na Redfourth Chorus, ulivutia masikio ya watu mashuhuri duniani na kwenye vyombo vya habari hadi kumfanya Amber Riley, nyota wa kipindi kilichoshinda tuzo za Emmy, Glee, kuandika kwenye Instagram, “Sielewi wanachokisema lakini najua ni kizuri. Inasikika kimalaika, kuna yeyote anayejua kama kuna video?” Mastaa wengine waliowahi kuiweka video hiyo kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja Master P, Anthony Hamilton, Jb Smoove na  WorldstarHipHop, miongoni mwa tovuti zingine za habari za kimataifa.

  Katika video mpya iliyotoka yenye rangi nyeusi na nyeupe ya KULIKO JANA, Sauti Sol wameungana na chipukizi lakini mweye kipawa cha hali ya juu, Redfourth Chorus kwa maajabu ya kimuziki. Sauti Sol wamesema kwenye taarifa yao, “KULIKO JANA ni wimbo maalum sana kwetu. Ulihamasishwa na safari yetu na rehema zisizoisha, mapenzi na baraka ambazo Mungu ametuonesha muda wote licha ya udhaifu wetu.”

  Video ya KULIKO JANA imetayarishwa na Fulfillment Limited, na kufanyika Kenya na waongozaji wakiwa Tim Mwaura na Joash Omondi.  Wimbo umeandikwa na kutayarishwa na Sauti Sol.  Kipande cha akapela kilipangwa na Philip Tuju na Redfourth Chorus.


  0 0

  Hatimaye mvutano wa baadhi ya wanasiasa na wananchi kuhusu kuirejesha tena stendi kuu ya Mabasi kati kati ya mji wa Songea badala ya kuendelea kuwepo eneo la Msamala umefikia kikomo, Ni baada ya Kamati ya wataalamu mbalimbali wa Manispaa ya Songea kutoa ripoti yao ya utafiti na kupendekeza stendi ya Msamala kuwa kituo kikuu cha Mabasi.


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania, Dr. Stephen Nindi akizungumza jambo juu ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa pamoja kuhakikisha maeneo yanapimwa na kuweka mpango mzuri wa Matumizi Bora ya Ardhi.
  Mkutano ukiendelea
  Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
  Katika kupanga matumizi bora ya ardhi nchini Tanzania ikiwa na lengo la jamii kutumia rasilimali hiyo vizuri kwa matumizi ya kawaida, Serikali imesema kuwa hadi sasa imefikia takribani vijiji 1645 na Wilaya 40 nchi nzima. Kutokana na ufinyu wa bajeti na kasi ndogo ya upimaji bado kuna vijiji 11,393 ambavyo havijafikiwa.

  Akizungumza Mkoani Morogoro ,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Ardhi,Dkt Stephen Nindi wakati wa Mkutano wa  Kikosi kazi cha kuanda mpango kazi wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa maendeleo ya Ardhi nchini.
  Pia Mkutano huo ulijadili kuhusu migogoro ya ardhi inayoendelea nchini na mipango ya matumizi ya ardhi kama inaweza kusaidia kupunguza migogoro hiyo,uliowakutanisha  wadau mbalimbali kutoka Serikalini ,taasisi na Mashirika mbalimbali yanayosimamia masuala ya ardhi.

  Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanashirikiana kwa pamoja kuhakikisha maeneo yanapimwa na kuweka mpango mzuri wa matumizi ya ardhi kwa matumizi yaliyokusudiwa katika kujadiliana ni namna gani wataona njia zinazofaa kutumika kukamilisha zoezi hilo la upimaji kwa vijiji vingine ikiwemo kuwepo kwa teknolojia mpya ya upimaji na kuwepo kwa bajeti ya kutosha.

  Aliongeza kuwa lengo la  kupima,kumilikisha na Kupanga kila kipande cha ardhi ni pamoja na kuhakikisha ardhi inakuwa na matumizi mazuri katika nchi.

   Dkt.Nindi alisema tayari serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametoa elimu katika timu za wilaya 100 kuwawezesha kujua  kupima,kupanga,kumilikisha ,kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi .

  Kwa upande wake Mratibu wa Programu ya Mradi ya Ardhi yetu kutoka Shirika la Kimataifa la CARE nchini Tanzania ,Mary Ndaro alisema mpaka sasa ni miaka mingi tangu nchi ipate uhuru kasi ya upimaji wa maeneo imekua ndogo .

  Alisema kama nchi inajiandaa kuwa na wawekezaji wengi zaidi inatakiwa kuhakikisha inakuwa na mipango bora ya  matumizi ya ardhi ambayo baadae haitaweza kuleta mgogoro wowote kati ya wanakijiji na muwekezaji.Aliongeza kuwa kwa sasa kati ya vijiji 12,545 nchi nzima ni vijiji 1645 ndiyo tayari vina mipango ya matumizi ya ardhi mpaka sasa. 

  Vijiji vingi bado havina mipango kutokana na ufinyu wa bajeti na kuwepo kwa kasi ndogo ya upangaji.Ndaro alisema lengo la mkutano huo wa wadau ni kuona ni namna gani  vijiji   vilivyobaki kati ya vijiji 12,545  vinapangiwa matumizi ya ardhi, kunakuwa na ushirikiano wa karibu wa wadau na namna vipi wanashirikiana kutatua migogoro ya ardhi ambayo inazidi kuongezeka.

  “Pamoja na kuwepo kwa kasi ndogo ya upangaji matumizi  ya ardhi, bado kuna changamoto ya kutoheshimu mipango ya matumizi ya ardhi iliyokwishaandaliwa ambapo  utakuta kijiji tayari kimepangwa lakini kinakuja kukatwa katikati na kuwa vijiji viwili au zaidi,”alisema  Alisema serikali inapaswa kuweka mipango ya matumizi ya ardhi ipasavyo ili kuweza kudhibiti hali ya migogoro ya ardhi kati ya watumiaji mbalimbali, mfano baina ya wawekezaji na wanavijiji kwa kupanga matumizi ya ardhi.“Serikali inapoita wawekezaji nchini inapaswa pia kuhakikisha mpango ya matumizi bora ya ardhi inayoeleweka kwa lengo la manufaa ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,”alisema

  0 0

  Wananchi wa Zambia wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye Uwanja wa Mashujaa Jijini Lusaka tayari kwa Shamrashamra za kuapishwa Rais Edgar Lungu wa nchini hiyo muda huu. Makamu wa Rais, Mh. Samira Suluhu Hassan atamwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Sherehe hiyo.
  Wengi wajitokeza kushuhudia Rais wao akiapishwa.


  0 0

  Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo, tulizungumzia janga kuu la Tetemeko la ardhi nchini Tanzania.
  Wadau Baraka Galiatano wa BukobaWadau Blog na Erick Kimasha walijiunga nasi kwa njia ya Skype kutoka Tanzania kutupa taswira ya nini kilitokea, vipi kilipokelewa na maendeleo tangu Sept 10 na hali ilivyo hivi sasa mjini humo.
  Pia tuliungana na mmoja wa wanaharakati ambao wameanzisha mfuko maalum kuchangia wahanga wa tetemeko hilo Agnetta .

  Ungana nasi kuanzia saa 11 kamili jioni majira ya Marekani Mashariki (5:00pm ET) kupitia www.kwanzaproduction.com ama kupitia TuneIn tun.in/sfeLX
  Kwa walio Marekani na Canada piga 240 454 0093
  Karibuni

  0 0


  0 0

   Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Happiness Mgalula akitoa hotuba wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma mjini Dodoma, Kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo, dkt. John Mduma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla kutoka Tume ya Mipango dkt. Lorah Madete.
   Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma.

  Na Adili Mhina, Dodoma.
  Tume ya Mipango imewashauri maofisa wa serikali wenye dhamana ya kusimamia miradi ya umma kuhakikisha wanatumia mbinu za kisasa katika kuchambua, kuchagua, kutekeleza na kusimamia miradi ya serikali ili kuhakikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo yanafikiwa kwa wakati.

  Ushauri huo umetolewa jana mjini Dodoma na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma, Mhandisi Happiness Mgalula alipokutana na maofisa mipango wa Ofisi za  Mikoa na Halmashauri za kanda ya kati iliyojumuisha Mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara kwa lengo la kutoa elimu katika kuandaa, kusimamia, na kutekeleza miradi ya Umma.

  Alisema kuwa Serikali ilifanya tathmini na kugundua kuwa hakuna vigezo vinavyofanana katika kuandaa na kuchagua miradi ya umma katika taasisi mbalimbali za Serikali kitu kinachorudisha nyuma juhudi za kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

  “Dira ya Taifa ya Maendeleo inaelekeza kuwa hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania inatakiwa iwe inchi ya uchumi wa kati na kwa vile tumedhamiria kwa dhati kifikia hapo ni lazima tujipange upya na kutumia utaalamu wa kisasa na vigezo vinavyofanana katika kuchagua miradi yenye uwezo wa kulifikisha taifa huko,” alisema Mgalula.

  Kukosekana kwa vigezo vinavyofanana kumesababisha upungufu mkubwa katika  miradi ya umma huku  ikipelekea miradi mingine kukosa mikopo katika soko la mitaji la ndani au la kimataifa kutokana na kuwa na maandiko yasiyokidhi vigezo vinavyohitajika.
  Mgalula aliongeza kuwa ili kuwekeza katika miradi yenye tija itakayoharakisha Tanzania kuingia katika nchi za uchumi wa kati, Tume ya Mipango imedhamiria kuendelea na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa walengwa nchi nzima ili kuongeza utaalam katika kuweka vipaumbele vichache vyenye ufanisi kwa kila mwaka wa bajeti kuliko kuwa na miradi mingi isiyokamilika.

  Na kwa upande wa maafisa wanaopata elimu hiyo wanakiri kuwepo kwa changamoto nyingi katika maandalizi ya miradi ya umma kutokana kukosekana kwa mfumo unaofanana katika uwekezaji wa miradi ya umma.

  “Tayari tumeanza kuelekezwa namna ya kuandaa miradi kwa kuzingatia vigezo vya kisasa viliyoainishwa katika mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa miradi ya serikali, hii itatusaidia kuwa na utaratibu mmoja na unaoeleweka  tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo kila mradi mpya ulikuwa na mfumo wake” Alisema Bwana Mkama kutoka Dodoma.

  Naye Afisa Mipango kutoka Halmashauri ya Babati Bw. Godlisten Geofray alieleza kuwa kuwepo kwa mfumo wa kisasa kutasaidia kuweka kumbukumbu sahihi za miradi hata ile ambayo haitafanikiwa kupata fedha kwa mwaka husika pale mfumo wa kanzidata utakapoanzishwa ambao utahifadhi kubukumbu za miradi yote nchini.

  Washiriki wa mafunzo hayo wameonesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Tume ya Mipango katika kutoa elimu hiyo katika ngazi mbalimbali huku wakieleza kuwa utaratibu huo utasaidia kuimarisha mawasiliano kwenye bajeti ya miradi kati ya serikali kuu na serikali za mitaa.

  Wataalamu hao wamesisitiziwa kuwa miradi yote itakayohitaji fedha za Serikali katika Bajeti italazimu kufuata utaratibu uliobainishwa katika Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma ili kuweza kuimarisha ufanisi na kupata thamani ya fedha.

  0 0
 • 09/13/16--02:45: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa orodha ya makundi manne na timu zitakazoshiriki Ligi Daraja la Poli ((SDL) inayotarajiwa kuanza baadaye, mwaka huu.

  Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi (TPLB), chombo maalumu cha kusimamia michezon inayoendeshwa na TFF makundi na timu hizo ni kama ifuatavyo.

  Kundi A.
  Bulyanhulu FC- Shinyanga
  Geita Gold SC- Geita
  Mashujaa FC- Kigoma
  Milambo SC- Tabora
  Polisi Tabora FC- Tabora
  Transit Camp FC- Shinyanga
  Kundi B
  AFC- Arusha
  Green Warriors- Dar es Salaam
  JKT Oljoro- Arusha
  Kitayosa- Kilimanjaro
  Madini SC- Arusha
  Pepsi- Arusha
  Kundi C
  Abajalo SC- Dar es Salaam
  CDA- Dodoma
  Changanyikeni- Dar es Salaam
  Cosmopolitan- Dar es Salaam
  Kariakoo FC- Lindi
  Burkina FC- Morogoro
  Kundi D
  Namungo FC- Lindi
  Mawenzi Market- Morogoro
  Mkamba Rangers- Morogoro
  Sabasaba United- Morogoro
  The Mighty Elephant- Ruvuma
  Wenda FC- Mbeya.

older | 1 | .... | 1352 | 1353 | (Page 1354) | 1355 | 1356 | .... | 3353 | newer