Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza sala wakati wa ufunguzi wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisema serikali ipo katika uhakiki wa maombi ya maeneo mapya utawala kwa kuangalia vigezo katika kuanzisha maeneo hayo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Prof. Joyce  Ndalichako akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisema serikali serikali itaendelea kuongeza udahili wa walimu wa sayansi katika vyuo vya elimu ili kuweza kukidhi mahitaji husika.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (kushoto) akimueleza jambo Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene.


UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakiwa katika mkutano Mpango wa Utekelezaji  wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi  CCM  mwaka 2015-2020 uliofanyika katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,(wa nne kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif  Ali Iddi,[Picha na Ikulu.] 13/09/2016.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika mkutano Mpango wa Utekelezaji  wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi  CCM  mwaka 2015-2020 uliofanyika katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,(kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif  Ali Iddi.
 Katibu Mkuu Baraza la Mapinduzi na Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa haji Ussi (Gavu),Mshauri wa Rais Utamaduni Mhe,Chimbeni Kheir Chimbeni na Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salmin  Juma Amour wakiwa katika mkutano wa Wizara hiyo kuhusu Mpango wa Utekelezaji  wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi  CCM  mwaka 2015-2020 uliofanyika katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,Chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakiwa katika mkutano Mpango wa Utekelezaji  wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi  CCM  mwaka 2015-2020 uliofanyika katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,Chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.]

"NATHAN MPANGALA FOUNDATION" YAMTEMBELEA PROF. NDALICHAKO DODOMA

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kifurahia jambo wakati alipokutana na Mwenyekiti wa “Nathan Mpangala Foundation (NMF),” ambaye pia ni mchora vibonzo, Nathan Mpangala (katikati) na Mkurugenzi wa “Education Improvement Trust Fund (EITF),” Joseph Chikaka, Jumamosi iliyopita mjini Dodoma. NMF yenye lengo la kuwawezesha vijana kujifunza mambo mbalimbali kupitia sanaa kwa kushiriki kwa vitendo ilitumia ziara hiyo kujifunza uzoefu na kuona ni maeneo gani programu zake zinahusiana na somo la stadi za kazi. (Picha kwa hisani ya NMF)

ZAHANATI 6 ZA NJOMBE MJINI ZAPATIWA MSAADA WA SOLAR

$
0
0
Na Hyasinta Kissima.

Halmashauri ya Mji Njombe imepokea msaada wa vifaa 06 vya umeme jua (Solar Kits) kwa ajili ya vituo 06 vya afya ndani ya Halmashauri hiyo. Vifaa hivyo vitakavyosaida utoaji wa nishati ya Mwanga hususani wakati wa kutoa huduma kwa kina mama wakati wa kujifungua zimekabidhiwa katika zahanati ya Magoda Halmashauri ya Mji Njombe.

Bi Neema Lazaro yeye ni Mratibu wa program ya Tubadili lishe kutoka shirika la CUAMM ambaye yeye amesema kuwa mchakato wa kuzitafuta Zahanati ambazo hazina chanzo chochote cha umeme ulifanyika kwa kushirikisha ngazi ya Wilaya na Mkoa hatimaye kuweza kuzitambua Zahanati hizo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya umeme wa jua (Solar Kits) Meneja wa SUMITOMO CORPORATION Ndugu Hasnein Gulamhussein amesema kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na shirika la MADAKTARI PAMOJA NA AFRIKA (CUAMM) wamesukumwa kutoa vifaa hivyo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya na kuzingatia vituo vya afya vyenye uhitaji zaidi na ambavyo havijafikiwa na umeme wa Gridi ya Taifa.

“Ni furaha yetu kuona kila Mtanzania anafikiwa na umeme popote alipo. Kwa kuzingatia umuhimu wa umeme kwenye vituo vya afya vijijini awamu hii tumeweka kipaumbele zaidi katika upatikanaji wa umeme nafuu kwenye zahanati hizi.”

Akitoa salam za shukrani  kwa niaba ya Ofisi ya Mganga Mkuu na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kibena Dkt Celine Nyoni amewaomba wafadhili mbalimbali kuendelea kuisaidi Sekta ya afya  katika zahanati zilizopo maeneo ya vijijini ambazo hazijafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa kwani zahanati hizo zimekua zinatoa huduma kwa kinamama wanaojifungua wakati wa usiku kwa kutumia vibatari, taa na tochi jambo ambalo limekua linahatarisha maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

“Tulikua kwenye shida kubwa kwa kina mama wanaojifungua kwa sababu tulikua tunatumia taa na wakati mwingine vibatari hali ambayo imekua ni changamoto kubwa kwetu. Lakini leo tumepata ufumbuzi wa mwanga kwa hiyo wakina mama watajifungua salama kabisa katika vituo hivyo vyote vilivyopatiwa msaada huu.”Alisema Dk Celina.

Anaendelea kusema “Halmashauri yetu inajumla ya Zahanati 58 zilizopo vijijini na kati ya Zahanati hizo zenye huduma ya Nishati ya umeme ni 32 tuu na leo tunaongeza idadi ya Zahanati zenye Solar kuwa 38.Hivyo bado tunaupungufu wa Zahanati 20 ambazo hazina huduma ya umeme. Hivyo wito wangu kwa wadau wote wenye mapenzi mema kuendelea kutusaidia kwa ajili ya Zahanati zilizosalia ili kuendelea kuboresha Sekta ya Afya hususani maeneo ya Vijijini.

Zahanati zilizopatiwa msaada wa vifaa hivyo vya Umeme jua (Solar Kits) katika Halmashauri ya Mji Njombe ni Zahanati ya Magoda, Idunda, Iboya, utengule, makanjaula na Lusitu. Mikoa itakayofaidika na Msaada wa vifaa hivyo vya umeme jua (Solar Kits) ni Njombe na Iringa na Jumla ya Zahanati 50 zinatarajiwa kupatiwa vifaa hivyo.
Meneja wa Sumitomo Corporation, Hasnein Gulamhussein (wa pili kushoto) akikabidhi msaada wa vifaa vya umeme jua (solar panel kits) kwa uongozi wa Zahanati ya Magoda ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuboresha sekta ya afya vijijini

YALE YALEE......

KAMANDA WA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (MOHAMED MPINGA) ATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA WA BODABODA.

$
0
0


Na: Uswege John Mwaisemba

Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, Mohammed Ramadhani Mpinga, Juzi alikuwa ni miongoni mwa Wakufunzi wa kutoa elimu ya Masuala ya Usalama Barabarani wakati wa mashindano ya Mpinga Cup 2016 yanayohusisha madereva wa Pikipiki na bajaji kwa mkoa wa Kipolisi wa Ilala jijini Dar es Salaam katika mfululizo wa michezo hiyo inayoendelea katika viwanja mbalimbali.

Katika mashindano hayo jumla ya timu 59 tayari zimefanikiwa kusonga mbele hatua ya pili ya mtoano wa mashindano haya ambayo mwishoni mwa wiki timu zilizocheza zilikuwa ni pamoja na Matunda fc dhidi ya Zahanati ambapo mashindi alikuwa ni zahanati ,alipatikana kwa njia ya penalt 5-4, wafungaji kwa upande wa Zahanati wakiwa ni Fredy Chambogo, Isaac Elisha, Musa Masho, Shiiko Rashifod , na mfungaji wa timu ya Matunda walikuwa ni Shaaban Awami, Kelvin Sweetbati, Salum MWaikimba, Yusuph Mohamed.

mchezo wa pili ulikuwa ni Kwa bibi fc aliyecheza na Chama fc na Mshindi alikuwa ni Chama Fc kwa jumla ya 1-0, mfungaji akiwa Amani kadodo dakika ya 18 kipindi cha kwanza, mchezo wa tatu ulizikutanisha timu za Tabata Bodaboda na Tabata Old Trafford na mshindi alikuwa ni timu ya Tabata Bodaboda kwa jumla ya mabao 3-1 wafungaji kwa upande wa Traffod walikuwa Abdallah Hussen dk 27 kipindi cha kwanza, Miraji Sarehe dk 36 kipindi cha kwanza na goli la tatu liliwekwa kimiani na Saidi Ngwira katika dakika za majeruhi.

Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Barakuda Kilimanjaro na Barakuda Fc ambapo mshindi alikuwa ni timu ya Barakuda Kilimanjaro kwa ushindi wa mezani baada ya wapinzani kushindwa kutokea uwanjani. Na mchezo uliofuata ulikuwa ni kati ya timu ya Liwiti fc dhidi ya Luwi Safari fc ambapo mchindi alikuwa ni timu ya Liwiti fc waliopata ushindi wa chee baada ya wapinzani kushindwa kutokea uwanjani.

Timu zilizofuatia katika ku hiyo ya jumamosi ilikuwa ni kati ya Kinyerezi Saloon waliocheza na Mbuyuni Fc ambapo matokeo katika mchezo huo timu ya mbuyuni waliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 mfungaji akiwa Kitenge Kitenge aliyefunga dakika ya 16 kipindi cha kwanza na mchezo uliofuata ulizikutanisha timu za Segerea SBG dhidi ya timu ya Segerea Sheli Bodaboda na matokeo katika mchezo huo timu ya Segerea Sheli Bodaboda waliibuka mshindi wa 1-0 mfungaji akiwa Jackson Hamadi dakika 25 kipindi cha pili.

Mashindano hayo yaliendelea tena siku ya jumapili ambapo jumla ya timu kumi na mbili zilishiriki kuwania nafasi ya kusonga mbele na mchezo wa kwanza ulikuwa ni kati ya Transpoter Fc iliyocheza na Kecha Fc na Timu ya Kecha ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mfungaji katika mchezo huo akiwa ni Mashaka Hamisi aliyefunga kwa shuti kali dakika 18 ya kipindi cha ili, huku ukifuatiwa na mchezo kati ya White Egle fc dhidi ya timu ya Migombani Fc ambapo mchezo huo timu ya White Egle iliibuka na ushindi wa mabao 8-7 baada ya kupigiana penalt kutokana na timu hizo kushindwa kutambiana kwenye dakika 90 za mchezo baada ya kumaliza zikiwa zimefungana bao 1-1.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania, mohammed Ramadhan Mpinga, akitoa elimu ya usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
Msaidizi wa Kamanda DCP Mpinga, SACP Fortunatus Muslim, akitoa elimu ya usalama bararani kwa waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 kutoka kundi E, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.
S/SGT Enock Machunde, Kitengo cha Elimu kutoka Traffic Makao Makuu Dar es Salaam, akitoa elimu ya usalama bararani kwa wachezaji wa timu zilizoshiriki kundi E ambao ni waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).

PC Abdallah Ismail, Kitengo cha Elimu kutoka Traffic Makao Makuu, akitoa elimu ya usalama bararani kwa wachezaji kabla ya kuingia Uwanjani wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 yanayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu).
Mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki kutoka mkoa wa Kipolisi Ilala, Mademla Bang’ala, akifafanua jambo kabla ya michezo hiyo kwenye michezo ya kundi (E) timu za waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakati wa mashindano ya kombe la Mpinga Cup 2016 iliyofanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule, juzi.(Picha na Traffic Makao Makuu). 

PROF. MBARAWA AKAGUA ATHARI ZA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amekagua athari za tetemeko la ardhi lililoikumba miundombinu ya barabara katika mkoa wa Kagera na kujionea athari zilizojitokeza katika mkoa huo.

Prof. Mbarawa amejionea athari za tetemeko la ardhi katika barabara ya Rwamishenye hadi Bandari ya Bukoba yenye urefu wa KM 4.6 ambayo imeathirika mita 60 na barabara ya Bukoba-Mtukula yenye urefu wa KM 80 ambayo imeathirika kwa mita 200 na kusisitiza kwamba Wizara yake itatekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza.

“Tunatoa pole kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kutokana na maafa yaliyojitokeza hivyo tutafanyia kazi maelekezo ya ukarabarati wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko kadiri tulivyoelekezwa na Waziri Mkuu”, amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa yuko mkoani Kagera kukagua athari za uharibifu wa miundombinu kufuatia tetemeko la ardhi lililopiga mikoa ya Kagera, Mara na Mwanza Septemba 10 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu takribani 16, majeruhi zaidi ya 100, uharibibifu wa nyumba takribani 800 na miundombinu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mafundi wa wanaodhibiti eneo lililoathirika na tetemeko la ardhi katika barabara ya Bukoba-Mtukula yenye urefu wa KM 80 ambayo imeathirika kwa mita 200, mkoani Kagera.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kagera Eng. Andrea Kasamwa wakati alipokagua athari za tetemeko la ardhi lililoikumba miundombinu ya barabara mkoani humo.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Rwamishenye hadi Bandari ya Bukoba yenye urefu wa KM 4.6 ambayo imeathirika mita 60 kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

MeTL Group yazindua kampeni ya “USIKATE TAMAA" jijini Dar leo.

$
0
0
     
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji akifafanua zaidi kuhusu kampeni ya USIKATE TAMAA,jijini Dar leo .
 Mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta akielezea safari yake ya muziki hadi kufika hatua aliyopo sasa, ambayo  binafsi amekiri kuwa kwake ni mafanikio makubwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji akizungumza kuhusu kampeni ya USIKATE TAMAA, Kushoto ni mwanamuziki Shetta na kulia na Kaimu Meneja Masoko wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.PICHA NA MICHUZI JR.

 kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) leo imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo imepewa jina la USIKATE TAMAA ikiwa na lengo la kuhamasisha watu waliokata tamaa kuwa nao wana nafasi ya kufanikiwa.

Akizungumzia kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuleta matumaini mapya katika jamii kwa watu ambao wamekuwa wakipoteza matumaini kutokana na hali ya ugumu wa kimaisha ambayo imekuwa ikiwakabili.

Alisema kampeni hiyo itakuwa ikitumia watu mbalimbali ambao wamefanikiwa na watakuwa wakitoa historia zao katika maeneo mbalimbali ambayo watatembelea, wakielezea jinsi walivyokuwa na maisha magumu hapo awali na sasa wamefanikiwa kimaisha.


“Kuna watu hawana uwezo na wanazungukwa na watu ambao wamekuwa wakiwaambia kuwa hawawezi kufanikiwa lakini kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA wataweza kupata matumaini kutoka kwa watu ambao walipita katika maisha magumu na baadae wakafanya vyema,” alisema Fatema.

Mkurugenzi wa masoko huyo aliongeza kuwa kampuni ya MeTL pamoja na kufanya biashara lakini pia inaijali jamii na inapenda kuona watu wakifanikiwa kimaisha hivyo kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA itaweza kusaidia watu wa aina mbalimbali waliopo katika jamii ya kitanzania wakipata matumaini mapya na kuongeza juhudi ili wafanikiwe.


“MeTL kupitia chapa yake ya MO inataka kuona watu wakiendelea kupambana na kufanikiwa, tunataka watu wafanikiwe na tuwape tuzo, tuwape sauti ya kusikika na huu ni mwanzo tu, kampeni hii itafanyika kwa muda mrefu zaidi,” alisema Fatema.

Kwa upande wa mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali (Shetta) ambaye ametumika kama mmoja wa watu ambao wamefanikiwa, alielezea safari yake ya kimuziki na kusema kuwa awali alikuwa akiishi kwa moja ya wasanii wa muziki nchini na alikuwa akifanya kazi za nyumbani kwa mtu huyo lakini akiwa na nia ya kutafuta njia ya kutoka kimuziki na juhudi alizozionyesha zimemwezesha kuwa moja ya wasanii waliofanikiwa nchini.


“Unaweza kuwa unajiamini katika kipaji chako lakini bado watu wanakudharau, mimi nimewahi kuishi na mwanamuziki mkubwa nchini lakini najijua nina kipaji lakini kwakuwa nilikuwa natafuta njia ya kutoka kimuziki ilinibidi nifanye hivyo,“Ilikuwa naosha gari lake, naosha vyombo na hata kumwogesha mdogo wake lakini nilikuwa najua nini nafanya na nini nataka, msanii yule alikuwa anafahamiana na watu wengi na mimi ikanisaidia kupata njia ya kutokea na leo kwa hatua niliyofikia nimefanikiwa,” alisema Shetta.

Ura Saccos Ltd wakabidhiwa hati miliki za viwanja vyao.

$
0
0
 Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Tatu Mfaume, akitoa neno mbele ya wanachama wa chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Usalama wa Raia Saccos URA SACCOS Ltd (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi hati miliki za viwanja kwa wanachama wake 46 walivyoviomba toka kwa kampuni ya Makazi Solution Ltd, kupitia Ura Saccos Ltd, tukio lililofanyika mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Meneja Mkuu  Ura Saccos Ltd, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Kim Mwemfula, kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi  (ACP) Innocent Mgaya, mbaye ni mjumbe wa bodi ya Ura Saccos Ltd.
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Tatu Mfaume, akimkabidhi hati miliki ya kiwanja mmoja kati ya wanachama wake 46 walioomba viwanja toka kwa kampuni ya Makazi Solution Ltd, kupitia Ura Saccos Ltd wanao shuhudia ni Meneja Mkuu Ura Saccos Ltd, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Kim Mwemfula, Mkurugenzi wa Kampuni ya makazi Solution Bw. Selemani Pazi, hafla iliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es salaam.
 Wanachama wa chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Usalama wa Raia Saccos URA SACCOS Ltd, wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi  Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Tatu Mfaume, kutoka makao makuu ya jeshi la polisi nchini, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi hati miliki za viwanja kwa wanachama wake 46 walivyoviomba toka kwa kampuni ya makazi Solution Ltd, kupitia Ura Saccos Ltd, hafla hiyo ilifanyika mwanzoni mwa  wiki hii jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya makazi solution Ltd, Bw. Seleman Pazi, akitoa neno mbele ya wanachama wa chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Usalama wa Raia Saccos URA SACCOS Ltd (hawapo pichani) wakati wa kukabidhi hati miliki za viwanja kwa wanachama wake 46 walivyoviomba toka kwa kampuni hiyo kupitia Ura Saccos Ltd.
(Picha zote na Demetrius Njimbwi-Jeshi la Polisi)

WAHITIMU WA MRADI WA UWEZESHAJI VIJANA KIUCHUMI WAIOMBA SERIKALI KUWAKUMBUKA KATIKA AJIRA.

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Kibaha.
VIJANA waishio katika mazingira magumu waliohitimu Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Pwani, chini ya Mradi wa kuwawezesha Vijana Kiuchumi (YEE) unaoratibiwa na Shirika la Plan International wameiomba Serikali kuwapatia ajira ili waweze kumudu maisha yao.

Hayo yamesemwa leo wilayani Kibaha na mmoja wa wahitimu wa mradi huo, Rajabu Kilanga alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya mafanikio na changamoto anazozipata baada ya kuhitimu mafunzo hayo.

Kilanga amesema kuwa mradi huo umemuwezesha kufahamu jinsi ya kuhifadhi fedha kwa ajili ya maisha ya baadaye pia umemnufaisha yeye pamoja na familia yake kwani kupitia fani ya umeme aliyoisomea ameweza kupata tenda ndogo ndogo ambazo zinamsaidia kuyaendesha maisha yake.
“Pamoja na faida nyingi nilizozipata kupitia mradi huu lakini ukosefu wa ajira za kudumu ni moja ya changamoto ambazo zinatukabili vijana tuliohitimu mafunzo haya hivyo, tunaiomba Serikali itusaidie kutupatia ajira ili na sisi tuweze kutimiza malengo yetu na kuchangia katika kulijenga Taifa letu”, alisema Kilanga.

Kilanga ameishukuru EU na Shirika la Plan International pamoja na wadau wengine kwa kuratibu mradi huo kwani baada ya vijana wengi kuhitimu na kuweza kujiajiri na kupata vipato kupitia mafunzo waliyoyapata chini ya mradi huo wameweza kujikwamua kutoka kwenye hatua moja ya maendeleo kwenda nyingine.

Naye muhitimu mwingine kupitia mradi huo, Simba Musa ametoa wito kwa vijana wenzie kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwani kwa kufanya hivyo wananchi wataona kazi zao hivyo kuwapelekea kupata ajira kwa urahisi.

“Nawashauri vijana wenzangu tujishughulishe, hata kama Mhe. Rais akitoa fedha hawezi kukuletea nyumbani kwa hiyo, kila mmoja kwa nafasi yake ajitume ili watu wazione kazi zake”, alisema Musa.
Aidha, ameyataja baadhi ya malengo yake yakiwemo ya kufungua duka la vifaa vya umeme pamoja na kuwafundisha vijana wenzie bila kuwatoza gharama yoyote ili nao waweze kujipatia kipato kupitia ujuzi watakaoupata.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Visigo, wilayani Kibaha, Aloisia Nyelo amesema kuwa mradi huo umewasaidia vijana kutozagaa hovyo mitaani kwani wameunda vikundi vinavyosimamiwa na watendaji wa Kata hiyo kwa ajili ya kuwapa ushauri hivyo kuwafanya wawe na adabu na heshima.

Nyelo ameongeza kuwa Kata hiyo iko mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana kupata tenda mbalimbali kwa kuwabandikia matangazo nje ya ofisi yao na kuwataka wananchi wanaohitaji wafanyakazi kusaini mkataba na vijana husika mbele ya Afisa Mtendaji ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa uhakika na wanalipwa fedha zao kama walivyokubaliana.

Mtendaji huyo alitumia fursa hiyo kuto rai kwa wananchi kuwaamini na kuwasaidia vijana hao kwa kuwapa tenda mbalimbali zinazolingana na fani walizosomea kwani wana ujuzi wa kutosha kufanya kazi hizo katika kiwango kinachotakiwa.
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Visigo, wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani Aloisia Nyelo, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mchango wa kata hiyo juu ya kuwasaidia vijana waliosomeshwa chini ya mradi wa Uwezeshaji wa Vijana Kiuchumi (YEE) kupata ajira.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi chini ya mradi wa Uwezeshaji wa Vijana Kiuchumi (YEE) unaofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya na kuratibiwa na Shirika la Plan International, Rajabu Kilanga (chini) akimshikilia kijana mwenzie George Geligoali (juu) wakati wakiendelea na kazi za kuunganisha umeme kwenye nyumba.

CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI CHATOA TAMKO KUFUATIA CHANGAMOTOKUBWA ZINAZOWAKABILI

$
0
0
Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (pichani kati),Magembe Makoye akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo mbalimbali yanayowakabili wafugaji hapa nchini,kushoto ni Mfugaji kutoka Suwambawaga,Mayunga Gamas na kulia ni Charles Mtokambati.

Bwa.Maghembe Makoye alieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji hao kuwa ni Ukosefu wa Maeneo rasmi ya malisho,Migogoro Baina ya Wakulima na Wafugaji,Migogoro kati ya Wafugaji na Idara ya Maliasili na Wanyamapori.Akaeleza kuwa kwa sasa kuna Mgogoro mkubwa kati ya Idara za Maliasili na Wanyamapori ndani ya Wizara ya maliasili na utalii na Wafugaji,akafafanua kuwa changamoto hizo zimekuwa sugu kutokana na kupanuka kwa maeneo ya Maliasili na kuchukua maeneo ya Wafugaji.

"Wafugaji wamekua wakifukuzwa kutoka kwenye maeneo hayo ambayo hapo awali walikuwa wakiyatumia kwa malisho,baada ya kuchukuliwa na maliasili na kuwa sehemu ya maeneo yaliyohifadhiwa.
Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (pichani kati),Magembe Makoye akionesha baadhi ya Nyaraka kwa waandishi wa habari,zinazoeleza kukamatwa kwa ng'ombe za wafugaji hao zaidi ya elfu moja na Wizara ya Maliasili na Utalii,ambapo mahakama iliamua kuwa Maliasili na Utalii irejeshe Ng'ombe hao kwa wafugaji,ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa ya wafugaji hao hakuna kilichofanyika mpaka sasa


BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 12/09/2016.

Muhimbili Yapeleka Wataalamu 20 Nje Kujifunza Upandikizaji Figo.

$
0
0
  Wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa wamewasili nchini India kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo. Wataalamu hao watakuwapo India kwa muda miezi mitatu na watarejea nchini Desemba 10, mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Hedwiga Swai akizungumza baada ya wataalamu hao kwenda India kwa ajili ya kujengewa uwezo wa upasuaji na upandikizaji figo.
  Mkuu wa Idara ya Urolojia katika hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro akizungumza na wenzake kabla ya kuondoka nchini.
 Baadhi ya wataalamu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Urolojia katika hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro wakati akitoa maelezo kabla ya kuanza safari ya kuelekea India wiki iliyopita.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Na John Stephen, MNH.
Dar es Salaam, Tanzania.  Wataalamu 20 wa fani mbalimbali wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameondoka nchini kwenda India kwa ajili ya kujengewa uwezo wa upandikizaji figo kwa watu wenye matatizo ya figo.

Wataalamu hao wameondoka wiki iliyopita na wakiwa huko watajengewa uwezo wa kufanya upasuaji na upandikizaji figo kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.

Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Hedwiga Swai amesema leo kwamba wataalamu mbalimbali wakiwamo madaktari bingwa wa upasuaji na upandikizaji figo, madaktari bingwa wa magonjwa ya figo, wataalamu wa maabara, madaktari wa usingizi na madaktari wa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.

Wengine ni wataalamu wa mionzi, wauguzi wa chumba cha upasuaji na chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na wataalamu wengine ambao wanakwenda kujifunza. 

“Suala la mgonjwa kupandikizwa figo ni mchakato na haliwezekani kufanywa na mtaalamu mmoja.Ni kazi inayowahusisha wataalamu wengi,” amesema Dk. Swai.
Pia, Dk. Swai amesema upandikizaji figo utapunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kuokoa fedha nyingi za serikali za kuwapeleka nje ya nchi.

Amesema kwamba wataalamu hao watakaa nje ya nchi kwa muda wa miezi mitatu na watarejea nchini Desemba 10, 2016.

“Shughuli za upasuaji na upandikizaji figo zitaanza Januari mwakani,” amesema Dk. Swai.

Nchi za Afrika zatakiwa kuzalisha wataalamu wa riadha.

$
0
0
 NCHI za Afrika wanachama wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF), zimetakiwa kuendesha kozi mbalimbali ili kuibua wataalamu wengi wa mchezo huo katika ngazi za kimataifa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo cha Kikanda cha IAAF-Nairobi, Kenya, Ibrahim Hussein, wakati wa ufungaji wa Semina ya Masoko kwa Michezo (IAAF Sports Marketing), iliyofanyika jijini humo hivi karibuni.

Ibrahim, alisema kumekuwa na uhaba mkubwa wa wataalamu mbalimbali katika mchezo wa riadha kimataifa kama Olimpiki, Mashindano ya Dunia nk. Jambo ambalo halipendezi, hivyo mashirikisho ya Riadha ya Nchi za Afrika yanapaswa kuwaandaa watu wao na Kituo chake kiko tayari kuwaendeleza katika ngazi za kimataifa.

“IAAF imekuwa ikiendesha kozi mbalimbali kama za ukocha, uamuzi, ufundishaji wa watoto na safari hii kozi ya ‘Marketing’, hivyo nendeni mkafundishe watu wenu na mimi niko tayari kuandaa mtandao na kisha kuwaendeleza katika ngazi za kimataifa,” alisema Ibrahim.

Mkurugenzi huyo, alibainisha kuwa kozi za awali ‘Level I’ ni kazi ya mashirikisho ya nchi na kuendelea ngazi ya pili ‘Level II’ na ya tatu ‘Level ‘III’ ni ya IAAF na yeye kama mkurugenzi wa Kanda ya Nairobi, yuko tayari kufanikisha katika hilo ili kuwezesha waafrika wengi zaidi kushiriki katika matukio ya riadha ya kimataifa.

Akiwazungumzia washiriki wa kozi hiyo ya masoko katika michezo, aliwataka kwenda kuyatumia vema mafunzo waliyoyapata kwa manufaa ya nchi zao na kwamba, watambue kuanzia sasa si mali ya mashirikisho ya nchi zao bali IAAF na wawe tayari kutumika sehemu yoyote watakapotakiwa.

Kwa upande wake Mkufunzi wa semina hiyo, Dk.Christoph Bertling kutoka Kitengo cha Mawasiliano na Utafiti wa Vyombo vya Habari (Instute of Communication and Media Research), Chuo Kikuu cha Michezo cha Cologne Ujerumani (German Sport University Cologne), alielezea kufurahishwa na ushirikiano ulioonyeshwa na washiriki wa semina hiyo na kuwataka kutokwenda kujifungia na ujuzi waliopata, bali wautumie kwa manufaa ya maendeleo ya mchezo wa riadha nchini mwao.

Dk. Bertling, aliwasihi washiriki hao kutosita kuendelea kuwasiliana naye kwa ushauri na kwamba hatosita kutoa msaada pale atakapoombwa.
Semina hiyo iliyofanyika hoteli ya Kasarani Sport View, ilishirikisha washiriki kutoka nchi 16 zinazozungumza lugha ya Kiingereza.

Washiriki hao ni pamoja na Stephen O. Bamiduro, Almu Umar Lambu (Nigeria), Cortex Nzima (Malawi), Phineas Mukwazo (Zimbabwe), Dk. Marc Dzradozi (Ghana), Sejanamane Maphathe (Lesotho), Bisrat A. Sileshi (Ethiopia), na Apollo B.Musherure (Uganda).

Wengine ni Tullo Stephen Chambo (Tanzania), Dennis Skrywer (Namibia), Bernard T. Kajuga, Patrick Thierry (Mauritius), Esayas Ande (Eritrea), Susan Kamau, Evans Bosire, Joseph Kipchumba, Karen Gachahi na Sally Rama (Kenya).

DC Kasesela afungua mafunzo ya Mgambo kata ya Wasa na Kihanga

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela leo amefungua mafunzo ya Mgambo Kata ya Wasa na kata ya Kihanga Wilayani humo, jumla ya wana mgambo 170 wameanza rasmi mafunzo, pamoja na mambo mengine watajifunza uzalendo, mbinu za kivita, utawala na usalama wa raia. DC Kasesela amesisitiza suala la usafi, kuacha ulevi, kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii na kuwa waaminifu. 

Akimkaribisha Mkuu wa wilaya, Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Iringa Lt. Col. Kitta alisisitiza kuwa wanao jifunza mgambo wana fursa nyingi sana za ajira hivyo basi wajitahidi wote wamalize mafunzo. Mafunzo hayo mpaka sasa katika wilaya ya Iringa yapo Kata ya Wasa, Kihanga, Mboliboli na manispaa ya Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifatilia Mafunzo hayo ya Mgambo wakati alipoyafungua leo katika Kata za Wasa na Kihanga. Kulia ni Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Iringa Lt. Col. Kitta.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akipokea taarifa ya mafunzi hayo.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza na Vijana wanaopatiwa Mafunzo ya Mgambo wa Kata za Wasa na Kihanga, Wilayani humo wakati alipoyafungua.


MBOWE, MBATIA WAWAFARIJI WANABUKOBA WALIOATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia leo wamewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Bukoba. Pia waliambatana na Mbunge  wa Viti Maalum Bi. Savelina Mwijake, Mbunge wa Bukoba Mjini, Mh. Rwakatare pamoja na Viongozi mbalimbali.
Mhe. James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ambae ni Mtaalamu wa Masuala ya Maafa amewaunga mkono Wanabukoba leo akiambatana na Mwenyekiti mwenza Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe kwenye safari ya kuwatembelea wahanga. Katika Safari hiyo wametoa misaada ya dharura kwa wahanga ikiwemo chakula, sukari, fedha na n.k, wataendelea na safari hiyo kuwatembelea Wahanga hapa Mkoani  Kagera katika sehemu mbalimbali. Leo wametembelea sehemu ya Kibeta, Hamugembe, Kashozi, Nshambya katika shule ya Ihungo iliyoathiriwa zaidi na Tetemeko hilo kubwa la Ardhi na kuwafanya wanafunzi kusimamisha masomo yao kwa wiki mbili kwa kukosa sehemu ya kusomea/Madarasa na Mabweni.
Sehemu ya Majengo katika Shule hiyo kwa sasa baada ya kutokea Tetemeko
Tetemeko likiwa limeharibu sana sehemu kubwa ya Kanisa katika Shule hiyo ya Ihungo iliyopo kilometa 8 kutoka Bukoba Mjini
Taswira ya sasa Wanafunzi wa Shule ya Ihungo wakijipanga kuondoka Majumbani mwao baada ya Tetemeko la jumamosi kuwaathiri kiasi kikubwa na kushinikizwa kufunga shule hiyo kwa wiki mbili kupisha kuangaliwa upya kwa Shule hiyo kutokana na kuathiriwa na tetemeko.

KAMPENI YA DECLUTTER AND DONATE YAZINDULIWA DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampeni ya Declutter and Donate Bi. Nasra Karl akiongea na waandishi wa habari katika mkutano jijini Dar es Salaam (kushoto) Hyacinta Ntuyeko - Mkurugenzi wa Glory Sanitary Pads (Kulia) Aunty Sadaka - Lifestyle Consultant na kushoto kabisa Bi Stella Malisha - Mkurugenzi wa IS Duke International.
 Bi Hyacinta Ntuyeko wa Glory Sanitary Pads akijibu swali kutoka mwandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Declutter and Donate iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Bi Nasra karl Mwanzilishi na Mkurugenzi ya kampeni ya Declutter and Donate na pembeni yake Aunty Sadaka Lifestyle consultant.

KAMPUNI ya Elite Organizing Services Limited imezindua kampeni inayoitwa Declutter and Donate jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa kampeni ya aina hii kuzinduliwa nchini Tanzania. Kampeni ya Declutter & Donate ni mpango wa kijamii unaohamasisha umma kugawa vitu ambavyo hawavihitaji.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampeni Bi Nasra Karl alisema “wazo la kuanzisha kampeni hii lilikuja hapo mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli alivyotamka kuwa siku ya Uhuru itasherekewa kwa kufanya usafi ila kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.  Hapo basi tulikuja na wazo yakuanza kusaidia nyumba na biashara mbali mbali kuepukana na vitu wasiyo hitaji ambayo inasaidia kukuza mazingira safi na kusaidia kuzingatia ubora katika maisha yetu ya kila siku. 

Kuwa kampuni ya uandalizi inayotoa huduma kusaidia watu binafsi na biashara mbali mbali kuepuka kuishi na vitu wasiyo viihitaji na maisha ambayo yanampangilio, ELITE ORGANIZING SERVICES LIMITED iliona haja ya kuongeza uelewa kuelimisha umma maana ya kutoa vitu visivyo na umuhimu katika maisha yao ( declutter) na ni jinsi gani vinaweza kupunguzwa katika maisha ya watu na jinsi gani inaweza kutumika kwa manufaa ya wengine.  Kama msemo maarufu  ya kingereza inayosema ‘ Taka taka ya mwanaume moja ni dhahabu kwa mwanaume mwingine’ 
Kampeni ya Declutter & Donate Campaign itaanza mwezi wa tisa Septemba na kuisha mwezi wa kumi na mbili yaani miezi mitatu. 

Katika kipindi hiki tunawaomba watu binafsi, familia na biashara mbali mbali kugawa vitu vyao ambayo zimetumika na kuuuzwa katika yard sale, mwanzoni mwa Disemba tunategemea kuwa na tukio itakayo changisha kwa ajili ya kituo inayosaida watu. (charity).

Mwishoni mwa Disemba tutakuwa na tukio ambapo tutakuwa na wataalamu wa kudeclutter wakija kuongea na wa Tanzania na kuwaeleza jinsi ya kuepeukana na vitu visivyo na muhimu katika biashara zao, nyumba zao na maeneo yanayowazunguka.  

Mwaka huu kampeni ya Declutter & Donate watasaidia watoto yatima na wanawake wanaoishi katika mazingira magumu. Mwaka huu tunapenda kusaidia wanawake wanaopata shida katika usalama ya hedhi na  ‘Mtoto anayesoma atakuwa mtu anayeweza kufikiri’ kwa watoto wanao ishi katika mazingira magumu. 

Mara nyingi tukietembelea watoto yatima na kugawa chakula, nguo na vitu vingine vya kutumia kila siku tunasahau kwamba michezo na vitabu vina jukumu kubwa katika ukuaji bora wa motto na ndio maana tumeamua kuwapa michezo na vitabu.  

Tunapokea fenicha, vifaa vya nyumbani, vitabu vya watoto na michezo ya watoto. Hivi sasa tunaishughulikia mahala pakuacha hiv vitu na tutaweza kuwajulisha hivi karibuni kupitia vyombo vya habari.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 13/09/2016.

WAKULIMA WA ZAO LA MAHINDI MKOANI RUVUMA WALALAMIKIA UTARATIBU WA KUNUNUA MAZAO HAYO.

$
0
0
Baadhi ya wakulima wa zao la Mahindi mkoani Ruvuma, wamelalamikia utaratibu wa Serikali wa kununua mahindi ya wakulima kiasi cha Tani Moja tu kwa kila Mkulima sawa na gunia Kumi na kwamba kiasi hicho ni kidogo mno ikilinganishwa na idadi kubwa ya mahindi waliyozalisha katika msimu huu.

PUMA ENERGY TANZANIA YAKABIDHI STIKA ZA WIKI YA USALAMA BARABARANI 2016 KWA JESHI LA POLISI JIJINI DAR LEO

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Tanzania,Phillipe Corsaletti akimkabidhi stika Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga ,zitakazotumika katika zoezi la ukaguzi wa magari katika juma la wiki ya usalama barabarani,inayotarajiwa kuanza hivi Karibuni.Bwa.Phillipe alisema kuwa hiyo ni sehemu ya uwekezaji wao katika masuala ya usalama barabarani ambao wanaamini ni wa muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa."Tunaamini kuwa shughuli zetu zinaweza tu kuwa salama kama jamii inayotuzunguka ipo salama",alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Tanzania,Phillipe Corsaletti pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga wakionesha baadhi ya stika mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Trafiki,jijini Dar Es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Tanzania,Phillipe Corsaletti akisoma taarifa yake kabla ya kukabidhi stika za Usalama Barabarani kwa Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama Barabarani ,mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar.Bwa.Phillipe alieleza kuwa suala la usalama barabarani linaendelea kuwa na changamoto kubwa duniani kote,amesema kuwa kwa hapa Tanzania jamii inashuhudia ajali za barabarani karibu kila siku.

"Ajali hizi zinawagusa vijana na wazee,wanataaluma,wafanyabiashara,wakulima,wanasiasa,matokeo ya ajali hizi ni vifo,majeruhi,uharibifu wa mali,upotevu wa wataalamu na mwisho kabisa mzigo mkubwa ni kwa Taifa",alifafanua Bwa,Phillipe.

Hivyo Bwa,Phillipe ameziomba mamlaka zinazohusika kuyatazama mambo hayo kwa undani na kuweka mfumo ambao utasaidia kuondoa ama kupunguza kwa kiaisi kikubwa wimbi la ajali za barabarani.Mkurugenzi huyo amesema kuwa pamoja na kuwa na wadau wakubwa wa mambo ya usalama barabarani pia wamekuwa wakitoa elimu kwenye shule mbalimbali za msingi hapa nchini na kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuzikifia shulu 30,amesema na kuongeza kuwa lengo lao kubwa ni kuzifikia shule zote za msingi za serikali hapa nchini kupitia mpango huo wa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa shule za msingi.
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images