Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109581 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI NA POLE KAGERA KUFUATIA WATU KADHAA KUPOTEZA MAISHA NA NYUMBA KUBOMOLEWA KWA TETEMEKO LA ARDHI

0
0


Watu kadhaa wamepoteza maisha na nyumba nyingi  Mkoani Kagera zimebomoka baada ya tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.7 kipimo cha Ritcher kupita kwenye mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa.
Taarifa zinadai Mji wa Kamachumu Mkoani Kagera ndio umeathiriwa Vibaya na tetemeko hilo, ambapo nyumba nyingi zimebomolewa.

Kiasi cha watu 10 wamepoteza maisha na mamia kujeruhiwa kwa  mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollomi.

Nyumba Moja wapo ambayo imeathirika na Tetemeko hilo lililotokea Muda mfupi uliopita Mjini Bukoba.

Nyumba ikionekana kupata nyufa baada ya tetemeko la Ardhi kuutikisa Mji wa Bukoba hivi Punde

Milango ya Geti katika nyumba hiyo ikionekana kuanguka chini baada ya kukumbwa na dhoruba ya tetemeko la Ardhi, lililotikisa Mji wa Bukoba.
Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Mji wa Bukoba Zikiwa katika hali Mbaya baada ya Tetemeko la Ardhi Kupita.


Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini 

Bukoba likiwa katika harakati za Uokoaji. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

DC STAKI APIGA MARUFUKU KUFANYA BIASHARA KWA KUJAZA RUMBESA

0
0

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Wakulima wa mazao mbalimbali likiwemo zao la vitunguu wametakiwa kutofanya biashara kwa kujaza rumbesa ili kuwanufaisha wafanya biashara ambao wanajitokeza vijijini kunua mazao kwani jambo hilo linawanyonya zaidi wakulima na kuwanufaisha wafanya biashara.

Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule mara baada ya kuitisha mkutano wa wananchi katika ziara yake ya kuwahimiza kwa pamoja kujitokeza kushiriki katika zoezi la upimaji ardhi linaloendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Same.

Hata hivyo lengo mahususi la kuamua kuwapo kwa zoezi la upimaji ardhi ni kutaka kuondoa migogoro ya ardhi iliyokithiri katika maeneo mbalimbali Wilayani humo sambamba na kupinga kipimo cha Rumbesa kinachowanyonya wakulima wengi nchini.

Katika mkutano huo uliofanyika Katika Kitongoji cha Jitengeni na Mvungwe uliwahusisha pia wataalamu wa kilimo na ardhi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo sambamba na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo.

Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wakazi wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni kushiriki kikamilifu katika zoezi la upimaji ardhi hivyo kuwaarifu pia wananchi wote kujitokeza katika mashamba yao wakati wa zoezi la upimaji ili kuondoa adha inayochochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Dc Staki alisema kuwa wananchi wanapaswa kupinga kuzidisha kipimo halisi kinachokubalika kwani kutofanya hivyo ni kukubali kupunjwa na kuinyima Halmashauri mapato.

Alisema kuwa wakulima wanapaswa kujiamini kwani mazao wanayolima yana soko popote nchini hivyo kidanganywa kwa kuweka Lumbesa ni kujinyima haki yao ya msingi katika kukabiliana na wimbi la umasikini.

Aidha kabla ya mkutano na wananchi Dc Staki alitembelea mashamba ya vitunguu na kujionea jinsi ambavyo Rumbesa inavyofungwa.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya alimtaka mkuu wa Polisi Wilaya ya Same Asteriko Maiga kusimamia na kulikemea suala la Rumbesa kwenye mageti yote na endapo watawabaini wafanya biashara wanaofanya hivyo wanapaswa kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini katika kuimarisha kilimo na kujitokeza kwa wingi katika shughuli za maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akikagua magunia yaliyokutwa yakiwa yamejazwa Rumbesa
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akizungumzia unyonyaji wanaokumbana nao wananchi kutoka kwa wafanyabiashara wanaotaka magunia yaliyojazwa Rumbesa
Gari aina ya Fuso likiwa limekamatwa mara baada ya kubainika kuwa limebeba magunia ya vitunguu ambayo yamejazwa Rumbesa

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wananchi Wilayani humo

TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF)

0
0

TETEMEKO: MALINZI AWAPA POLE KANDA YA ZIWA, BURUNDI NA UGANDA

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameshitushwa na taarifa za tukio la tetemeko kubwa ardhi lenye mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 lililotokea jana Septemba 10, 2016 katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa kadhalika nchi za Burundi na Uganda.

Mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyopata athari kwa mujibu wa taarifa ni Mwanza, Mara na Kagera nchini na kuripotiwa kuua zaidi ya watu 10 na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa sambamba na kubomoa majengo mbalimbali.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini 


AFRICAN LYON V MBAO FC

African Lyon ya Dar es Salaam kesho Septemba 12, 2016 itaikaribisha Mbao FC kwenye mchezo Mchezo huo Na. 28 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru jijini. Mara baada ya mechi hiyo, raundi ya tano itafanyika mwishoni mwa wiki ijayo kadiri ya ratiba.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


ZIARA YA NAPE NA RIPOTI KAMILI YA TFF

Ripoti ya mwenendo wa mpira wa miguu Tanzania na mipango yake inayofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imemfurahisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye hivyo moja kwa moja akaupongeza uongozi wa Rais Jamal Malinzi akisema unafanya kazi kubwa.

Kutokana na ripoti hiyo, Nape ambaye ni Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, aliridhia wadau wa mpira wa miguu kusapoti timu za taifa hususani Serengeti Boys – timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambayo kwa sasa imepiga kambi Shelisheli kujiandaa kuivaa Congo-Brazzaville Jumapili ijayo.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA SIANG’A

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea taarifa za kifo Kocha wa zamani wa Simba, James Aggrey Siang’a. Taarifa kutoka Kenya zinasema amefariki leo Septemba 10, 2016 alfajiri mjini Bungoma baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Siang’a alikuwa ni miongoni mwa makocha walioheshimika Afrika Mashariki hususani Tanzania alipoingoza Simba kufanya vema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kufika hatua ya timu Nane Bora.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAWAONDOA HOFU WAZAZI

0
0
dre
Mwanafunzi  aliyeongoza masomo yote Rahma Mdea akipokea cheti cha kuhitimu darasa la  saba na zawadi yake  wakati wa mahafali ya  shule ya  Southern Highlands Mafinga

Mwanafunzi  aliyeongoza masomo yote Rahma Mdeka akipokea cheti cha kuhitimu darasa la  saba na zawadi yake  wakati wa mahafali ya  shule ya  Southern Highlands Mafingamkur
 Mkurugenzi wa shule za Southern Highlands Mafinga ,Mary  Mungai  kulia akitambulisha watumishi  wa  shule  hiyo.
………………………………….
Na MatukiodaimaBlog 

UONGOZI wa  shule ya  Southern Highlands Mafinga  wilayani  Mufindi umewataka wazazi  wa  wanafunzi zaidi ya 50 waliofanya mtihani wa Taifa  wa darasa la  saba katika shule   hiyo  kuanza  kuwa na uhakika  wa watoto wao  kufaulu mtihani   huo .


Huku ukiahidi  kutoa kuchangia sehemu ya ada kwa  wanafunzi watakajiunga na shule ya sekondari  ya  Southern Highlands Mafinga kama  sehemu ya ahsante kwa  ushirikiano  ambao  wazazi  wamekuwa  wakitoa kwa shule hizo.

Mkurugenzi mtendaji wa Southern Highlands Mafinga  Mary  Mungai  aliyasema haya jana  wakati wa mahafali ya darasa  la  saba  shuleni  hapo .


“Shule hii ilianza mwaka 1994 kama Day Care na Pre-School. Mwaka 1997 ikakuwa na kuanza shule ya msingi-Primary School mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanzawa darasa la saba wanafunzi walikuwa 17,wote walifauru vizuri na wote  walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza Katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani yasomo la kiingereza ”


Alisema kuwa matokeo mazuri ya wanafunzi wote kufaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba yamekuwa ni kawaida  kwa  shule   hiyo na  kuwa  toka kuanzishwa kwake haijapa pata  kufelisha hata  mwanafunzi  mmoja .

Hivyo kuwataka  wazazi  kutokuwa na hofu  juu ya  wanafunzi hao  waliofanya mtihani mwaka  huu kwani waanze  kujiandaa kwa kuwapeleka  sekondari.


Wakati huo   huo mkurugenzi wa familia  ya Lucy Chawe inayoishi nchini marekani na Tanzania  imepongeza jitihada za  shule  hiyo na  kuahidi kuendelea  kuiunga mkono  serikali kwa  kuhamasisha masomo ya Sayansi na Hisabati kwa  wanafunzi 

Mkurugenzi wa The Chawe Foundation Award , Kitove Mungai  alisema  kuwa  kila mwaka  wamekuwa wakitoa  zawadi kwa  wanafunzi wa Awali   hadi  darasala  saba ambao wamekuwa  wakifanya vizuri masomo ya  Hisabati na sayansi .


Aliwataja wanafunzi  ambao  wamepewa  zawadi hiyo kwa mwaka  huu kuwa ni Brayan Mgomapayo, Rahma Mdeka na Ayub Toss ambao  walifanya  vizuri katika hesabu .


Wakati katika  sayansi wanafunzi waliopewa  zawadi ni  Nimrod Nyakunga , Rahma Mdeka na Erick Mwanjelwa .

Article 5

0
0
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akizundua gati jipya la Bandari ya Pangani ambalo liligharimu zaidi ya bilioni 3 kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano wa mwisho kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA)Karim Mattaka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akiwa na viongozi mbalimbali akisoma maelekezo yaliyoandikiwa kwenye jiwe la msingi mara baada ya kufanya kuzindua gati jipya la Bandari wilayani Pangani kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Karim Mattaka kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella na PRO wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Moni Jarufu. 

Kulia ni Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)Karim Mattaka wapili kutoka kulia wakati wa uzinduzi wa gati jipya wilayani Pangani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika akifuatilia mazungumzo hayo.
WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Karim Mattaka wakati alipofanya ziara ya kuzindua gati mpya wilaya ya Pangani Mkoani Tanga katikati ni Meneja wa Tanroad Mkoani Tanga,Mhandisi Alfred Ndumbaro 


PROF.MBARAWA AZINDUA KIVUKO CHA MV .TANGA NA GATI YA BANDARI YA PANGANI

0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezindua kivuko kipya na cha kisasa cha Mv. Tanga kinachotoa huduma ya usafirishaji kati ya Pangani na Bweni na kuzindua Gati ya Bandari ya Pangani wilayani pangani mkoani Tanga.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Mbarawa amesema kuwa ujio wa kivuko hicho utafungua fursa za kibiashara na kuchochea maendeleo ya kiuchumi wilayani hapo. “Naamini ujio wa kivuko hiki utarahisisha huduma za kijamii na maendeleo ya kiuchumi wilayani hapa, hivyo naomba mkitunze vizuri kivuko hiki ili kiweze kudumu kwa muda mrefu”, amesema Prof.Mbarawa.50 242

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha huduma za kivuko zinakuwepo muda wote wilayani hapo, Serikali kupitia Wizara hiyo imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa boti ambayo itatumika kama mbadala wa usafiri wakati wa usiku katika maeneo hayo ambapo kivuko cha Mv.Tanga hakifanyi kazi.

Kuhusu ujenzi wa Gati ya bandari ya Pangani Waziri Mbarawa ameseama kuwa ujenzi wa gati hiyo utapelekea Meli kubwa kuweza kutia nanga na kurahisisha usafiri wa moja kwa moja kutoka Pangani kwenda visiwa vya Unguja na Pemba. Amefafanua kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataanzisha huduma ya boti za haraka kutoka Pangani kwenda Mkokotoni Zanzibar hivyo kufungua fursa za kibiashara na kitalii baina ya Tanga na Zanzibar.

Kwa upande wa huduma za mawasiliano ya simu wilayani hapo, Prof.Mbarawa amesema kuwa huduma hiyo itaanza mwezi Desemba mwaka huu kwa mkandarasi kufika na kuanza ujenzi wa miundombinu ya simu na hivyo kuondoa tatizo la mawasiliano wilayani hapo.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amehahidi kuanza ujenzi wa Barabara ya Tanga-Pangani-Saadani hadi Bagamoyo (KM 242) kwa kiwango cha lami ifikapo mwakani. Amefafanua kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa wa awamu ili kuweza kuharakisha kukamilika kwake ambapo awamu ya kwanza itahusisha kipande cha barabara ya Tanga- Pangani (KM 50) na kuongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utafungua fursa za kiuchumi kati ya Tanga na Pangani.

“Naahidi kujenga barabara hii ambayo ni kiungo kati ya Tanga na Pangani, naamini ukamilifu wake utalete maendeleo mkoani hapa”. Amesisitiza Prof. Mbarawa. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng.Joseph Nyamhanga amezipongeza kampuni za Songoro Marine na Alpha Logistic kwa kumaliza kwa wakati ujenzi wa kivuko na Gati ya bandari hiyo.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng.Manase Ole-kujan amesema kuwa kivuko cha Mv.Tanga kimejengwa kwa sh.bilioni nne ambapo kina uwezo wa kubeba tani 50 abiria 100 na magari madogo 6 kwa wakati mmoja.

Ujenzi wa Kivuko cha Mv. Tanga ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wilayani Pangani Mkoani Tanga.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na watendaji wa Serikali na Wizara wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko cha Mv. Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pamgani Mhe. Zainabu Abdallah Issa . 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na watendaji wa Serikali na Wizara wakizindua Gati la Bandari ya Tanga.Ukamilifu wa Gati hiyo utasaidia Meli mbalimbali kuweza kutia nanga wilayani Pangani. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akisafiri na wakazi katika Kivuko cha Mv.Tanga kutoka Pangani kwenda Bweni mara baada ya uzinduzi. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA,DKT.MAHENGE AZINDUA VODASHOP MJINI SONGEA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge(wanne kutoka kushoto)akikata utepe mwishoni mwa wiki kuashiria uzinduzi rasmi wa Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo songea mjini.Wengine katika picha ni baadhi ya wafanya kazi wa kampuni hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge,akikata keki ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo songea mjini mwishoni mwa wiki. 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge(kulia)akipokea zawadi toka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Ruvuma, Amos Vuhahula(kushoto) mara baada ya kuzindua rasmi Duka jipya la kampuni hiyo lililopo songea mjini mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge,akigonganisha glasi na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,Baada ya kuzindua rasmi Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo songea mjini mwishoni mwa wiki. 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Satano Mahenge,akisisitiza jambo wakati wa hafla fupi ya uzindua wa Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo songea mjini mwishoni mwa wiki.
Hili ndilo duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Songea mjini.

MLIMBWENDE WA OZONA MISS LAKE ZONE 2016 APATIKANA

0
0
Jumamosi Septemba 10, 2016 kuamkia leo jumapili, kinyang'anyiro kikali cha kumsaka mlimbwende wa Kanda ya Ziwa, (OZONA MISS LAKE ZONE 2016), kimefanyika ambapo Mlimbwende, Eluminatha Dominick (pichani) kutoka mkoani Geita ameibuka mshindi miongoni mwa walimbwende 17 (baada ya mmoja kujitoa) waliokuwa wakiwania taji hilo.

Ushindi wa mlimbwende huyo ulionekana kuwafurahisha mamia ya watu waliohudhuria kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye Viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza, likiwa nimeandaliwa na kampuni ya Flora Talent Promotions chini ya Mkurugenzi wake, Flora Lauwo na kudhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwemo mdhamini mkuu, kampuni ya vipodozi ya OZONA pamoja na 102.5 Lake Fm Mwanza.

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Mhe.Jeseph Linzwa Kasheku Msukuma, alisema ni furaha kubwa mkoa wa Geita kunyakua taji la Ozona Miss Lake Zone 2016 na kwamba matarajio ni kujiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua taji la Miss Tanzania 2016 ikiwa ni sawa sawa na matarajio aliyoyaeleza mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016.
Na BMG
Mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (katikati) kutoka mkoani Geita. Mshindi wa pili ni Mery Peter (Miss Mwanza 2016, kushoto) na Mshindi wa tatu ni Lucy Michael (Geita, kulia).
Mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (katikati) kutoka mkoani Geita. Mshindi wa pili ni Mery Peter (Miss Mwanza 2016, kushoto) na Mshindi wa tatu ni Lucy Michael (Geita, kulia).
Aliyekuwa Miss Lake Zone (kulia), akikabidhi taji la Miss Lake Zone mpya (kushoto)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaa ya Nyamagana, Mhe.Mary Tesha (kushoto) akimkabidhi mshindi wa Ozona Miss Lake Zone mfano wa ufunguo wa gari alilokabidhiwa kama zawadi. Mshindi wa Ozona Miss Lake Zone amewazadiwa gari lenye thamani ya shilingi Milioni 12 na kampuni ya Ozona.


WAZIRI MKUU AONGOZA WANANCHI KUAGA MIILI YA WALIOKUFA KWA TETEMEKO

0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana (Jumamosi, 10 Septemba, 2016 mkoani Kagera.

Tetemeko hilo lilitokea jana Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya athari zilizotokana na maafa hayo.

“Poleni sana tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea nchini. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Tuendelee kuwa na imani na watulivu  Serikali ipo pamoja nanyi na haitawatupa mkono,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Kamati ya Maafa ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu itakwenda wilaya za Kyerwa, Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya tathmini na kubaini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona namna ya kuwasaidia waathirika.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa mkoa huo kuchukua hatua za haraka kwa kuwatafutia eneo salama la kulala wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakato ambayo mabweni yake yote yameathirika na tetemeko hilo na hayafai kutumika.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea namna mabweni ya shule hiyo yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi kulala uwanjani.

Pia Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia kama kuna tetemeko linguine linaweza kutokea nchini ili Serikali iweze kuchukua tahadhari pamoja na kutoa elimu kwa umma namna ya kujikinga.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa wanaendelea na jukumu la kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao zimeanguka. Pia mkoa unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.

Awali Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170 wamelazwa na kutoa pole na kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na wenye matatizo ambayo yanahitaji matibabu kwenye hoispitali kubwa Serikali itahakikisha wanapelekwa huko na kuhudumiwa.

 IMETOLEWA NA:              
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI,SEPTEMBA 11, 2016
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akiwasili katika uwanja wa mpira wa Miguu wa Kaitaba mjini Bukoba mapema leo,kwa ajili ya kuwapa pole nyingi wakazi wa mji huo na kwingineko na pia kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokuwa wamekumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.

Tetemeko hilo kubwa la ardhi lenye mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea jana Septemba 10, 2016 katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa kadhalika nchi za Burundi na Uganda.Mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyopata athari kwa mujibu wa taarifa ni Mwanza, Mara na Kagera nchini na kuripotiwa kuua zaidi ya watu 15 na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa sambamba na kubomoa majengo mbalimbali.
Pichani kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu ,kabla ya kuanza sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mbunge wa jimbo la BUkoba Mjini,Mh Wilfred Lwakatare,kabla ya kuanza sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha. 

Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga wapendwa wao
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akisoma majina ya masanduku yaliyobeba miili ya marehemu,tayari kwa kuagwa kwa pamoja katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa dini wakitazama majina ya masanduku yaliyobeba miili ya marehemu,tayari kwa kuagwa kwa pamoja katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa dini wakiwa katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala ya pamoja ya kuaga miili ya marehemu waliokumbwa na tetemeko la Ardhi hapo jana mjini Bukoba mkoani Kagera.
Baadhi ya Masanduku yenye miili ya marehemu walioathiriwa na tetemeko la Ardhi hapo jana mjini Bukoba mkoani Kagera.

Rais Magufuli kuwasili Lusaka Zambia kesho kwa ziara ya siku tatu

0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 12 Septemba, 2016 anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.

Rais Magufuli anafanya ziara hii ya kwanza nchini Zambia akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Kamati hiyo inajulikana kwa jina la SADC-Troika.

Dkt. Magufuli alipokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC-Troika kutoka kwa Rais wa nne Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland tarehe 01 Septemba, 2016.

Katika Ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika watakaohudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Mashujaa Jijini Lusaka.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Lusaka



11 Septemba, 2016

Waziri Moldiline Castico ashiriki uzinduzi wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja.

0
0

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Kisiwa cha Uzi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia hiyo lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico katika viwanja vya Skuli ya Uzi.
Mc wa Mkutano huo wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi akisoma ratiba ya Uzinduzi huo katika viwanja vya Skuli ya Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Mwanachama wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi Unguja Khadija Said akisoma Quran Tukufu kabla ya Uzinduzi wa Baraza lao la Vijana la Shehia ya Uzi lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe, Moldiline Castico.
Vijana wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakicheza maigizo ya kuhamasisha Vijana kujiunga na Mabaraza ya Vijana kwa Maendeleo yao katika kujikwamua Kiuchumi.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akiwa na Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mchezo wa maigizo unaohamasisha Vijana kujiunga na Mabaraza la Vijana katika Shehia zao.,
Mwanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Salma Tunda akisoma risala yao mbele ya Mgeni rasmin wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya skuli ya uzi. 

SIMBA YALAMBA SUKARI YA MTIBWA UWANJA WA UHURU LEO, YAILAZA KWA BAO 2-0

0
0
 Wachezaji wa Timu ya Simba wakishangilia ushindi wao walioupata dhidi ya Timu ya Mtibwa Suger, katika Mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 2-0.
 Kipa wa Timu ya Mtibwa Suger, akiokota mpira wavuni baada ya kufungwa na Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo (anaeonekana nyuma ya nyavu akishangilia), katika Mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 2-0.
 Mchezaji wa Simba, Laudit Mavugo akionyesha uwezo wake mbele ya Beki wa Mtibwa Suger, Salim Abdallah, katika Mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 2-0.
 Nahodha wa Timu ya Simba, Jonas Mkude akichuana kuwania mpira na Mchezaji Kelvin Idd, katika Mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 2-0.
 Mshambuliaji wa Mtibwa Suger, Ibrahim Juma, akijaribu kutaka kumtoka Kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin, katika Mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 2-0.

CCM YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WAATHIRIWA WA TETEMEKO LA ARDHI KANDA YA ZIWA

0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za janga la tetemeko la ardhi lililotokea jana tarehe 10/09/2016 katika Mkoa wa Kagera na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza na Shinyanga.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kufuatia vifo vilivyotokana na tetemeko hilo.

Katika salamu zake Ndg Kinana amesema Chama cha Mapinduzi kinatoa pole kwa wahanga na kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika janga hilo.

Chama cha Mapinduzi kipo pamoja na wahanga, kushirikiana nao kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu.WanaCCM nchi nzima tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu pema peponi.

Amina.

Imetolewa na:-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)

MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Tarehe 11/09/2016.

WAKURUGENZI WATEULE KUWASILI DODOMA,KULA KIAPO CHA UADILIFU WA UONGOZI WA UMMA SEPTEMBA 13

0
0

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.

Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Manispaa na Wilaya, walioteuliwa siku ya Jumamosi Septemba 10, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapa.

Zoezi la uhakiki wa vyeti hivyo litakalofanyika Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika jengo la Mkapa mjini Dodoma siku ya Jumanne Septemba 13, 2016 kabla ya kuanza kwa zoezi la kuapa.

Wakurugenzi hao 13 ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa mmoja, Mkurugenzi wa Mji mmoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, wanatakiwa kuwasili Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Rebecca Kwandu, Septemba 11, 2016 inawataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanawasilisha nakala halisi ya vyeti vyao vya taaluma kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli.

Wakurugenzi hao ni Godwin Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R. Ntiruhungwa Mji waTarime, Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank Bahatui Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mwailwa Smith Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Godfrey Sanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na Yusuf Daudi Semuguruka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.

Wakurugenzi wengine ni Bakari Kasinyo Mohamed Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Juma Ally Mnweke Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Butamo Nuru Ndalahwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri Mourice Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na Fatma Omar Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Dumisheni Michezo kuongeza ufanisi katika kazi; Katibu Mkuu Kiongozi.

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
 Na Shamimu Nyaki WHUSM. 

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewataka Watumishi wa Umma kushiriki katika Michezo mbalimbali ili kuwa na afya imara itakayosaidia ufanisi katika kutekeleza kazi zao. 

Balozi Kijazi ametoa rai hiyo leo Jijini Dar es Salaam katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Lawrence Ndombaro katika Bonanza la Michezo la ufunguzi wa mashindano ya thelatini na nne yanayojulikana kama SHIMIWI lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru wa Jijini humo. 

“Michezo inasaidia mwili kuwa na afya njema na kuondoa msongo wa mawazo pamoja na kuleta nguvu na akili katika mwili vinavyosaidia katika utendaji bora wa Mtumishi kwa maendeleo ya Taifa”.Alisema Balozi Kijazi.
Aidha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi amewataka Viongozi wa Serikali na Taasisi zake kutenga muda kwa Watumishi wanamichezo wa kufanya mazoezi pamoja na kuwapatia vifaa vya michezo ili waweze kufanikiwa katika mashindano hayo. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewapongeza Watumishi wake kwa kushiriki Bonanza hilo na kuahidi kuwapa muda mzuri wa maandalizi ili wafanye vizuri katika mashindano hayo. 

Akifafanua maandalizi ya timu ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mwenyekiti wa timu hiyo Bw. John Manyika ameahidi ushindi kwa timu yake kwani wanaendelea kijiandaa vizuri katika mazoezi. 

Mashindano ya SHIMIWI yanatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu mjini Dodoma kuanzia tarehe 14 ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kmbarage Nyerere. 

Bonanza hilo lilimalizika kwa timu ya Jiji la Dar es Salaam kutwaa Kikombe kwa kuwa na wanamichezo wengi ikifuatiwa na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIJI NA VIJIJI WA NAMIBIA AFIKA NCHINI KUJIFUNZA UTAWALA WA ARDHI

0
0
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akielekezwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Mb). na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje kutumia mashine ya ATM kwa ajili ya kupata huduma katika Kituo cha Huduma kwa Mteja – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri huyo amefika nchini kujifunza Utawala wa Ardhi.
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akiwa ameambatana na ujumbe wake ndani ya Kituo cha Huduma kwa Mteja – Wizarani, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje, akipewa maelekezo na mtumishi jinsi huduma zinavyotolewa katika Kituo hicho. Waziri huyo amefika nchini kujifunza Utawala wa Ardhi. 
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akikabidhi Dola 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kurui – Kisarawe, kama pongezi kwa kijiji hicho kuwa mfano bora katika Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Ardhi. Waziri huyo amefika nchini na ujumbe wake kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akimpa mkono wa pongezi Mwenyekiti wa kijiji cha Kurui – Kisarawe, kama pongezi kwa kijiji hicho kuwa mfano bora katika Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Ardhi. Katika picha ya pamoja na Watendaji mbalimbali wa Sekta ya Ardhi na ujumbe ulioambatana na Waziri kufika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akiwa amewasili Ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, akiwa ameambatana na ujumbe wake, uliofika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi. 
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ; Angeline Mabula, kushoto kwake. Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Ardhi ; Mary Makondo na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje pamoja na wajumbe walioambatana na Waziri huyo wa Namibia, waliofika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.

BEI YA SAMAKI SOKO LA FERI JIJINI DAR ES SALAAM YASHUKA

0
0
Wachuuzi wa Samaki wakisubiri kununua kitoweo hicho katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Bei ya samaki katika soko hilo imepungua kutokana kwa kupatikana kwa wingi kwa kitoweo hicho.
Mnada wa samaki ukiendelea


Na Dotto Mwaibale

HALI ya bei ya samaki katika Soko la Kimataifa la Feri jijini Dar es alaam imeshuka kutokana na samaki kupatikana kwa wingi katika kipindi cha mwezi wa Septemba.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com jijini Dar es Salaam leo asubuhi mchuuzi wa samaki katika soko hilo Mohamed Hassan alisema katika kipindi cha wiki mbili bei ya samaki imeshuka ukilinganisha ni mwezi uliopita.

"Sasa hivi samaki aina ya King Fish, Changua wanauzwa kati ya sh.30,000 lakini kipindi ambacho wakiadimika ufikia hadi sh.35,000" alisema Hassan.Mchuuzi mwingine wa samaki katika soko hilo Shabani Shamte alisema samaki aina ya kibua, ngisi wakati huu uuzwa kati ya sh. 23,000 hadi 25,000 ambapo wakiadimika ufikia hadi sh. 30,000.

Grace Tesha ambaye uuza samaki hao maeneo ya Mabibo Loyola alisema hata wao kipindi hiki biashara yao inakwenda vizuri kutokana na kuwepo kwa samaki wengi."Samaki wakiadimika huwa inatuwia vigumu mno kibiashara kwani wateja wetu wamekuwa wakilalamia kuwauzia kwa bei kubwa" alisema Tesha.

TANZANIA SACCOS FOR WOMEN ENTREPRENEURS (TASWE - SACCOSS) WASHEHEREKEA MIAKA MIWILI TANGU KUANZISHWA KWAKE JIJINI DAR.

0
0
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna Matinde akizungumza katika hafla ya kutimiza Miaka miwili ya TASWE-Saccos jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

Alisema kuwa TASWE ipo mikoa Tofautitofauti hapa nchini Lengo kuu la hafla ya Dinner Part Gala ni kuwafikia wanawake wengi zaidi ili kutatua changamaoto zinazowakabiri hasa kwa upande wa kipato cha mwanamke.

Alisema kuwa TASWE inamatawi 14, katika matawi hayo wameona watoe elimu ya Ujasiliamali kwa wanawake wengi zaidi hapa nchini ili kupunguza ongezeko la utegemezi na waweze kuwa wanawake wajasili na wenye nguvu.
 Rais wa Chama cha wenye viwanda Biashara na Kilimo nchini (TCCIA), John Mayanja akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuwataka wanawake watumie fursa zinazojitokeza hasa kwa wale wanaotaka kusindika juisi za matunda hapa nchini kwa kuwa kuna matunda mbalimbali inapofikia msimu wake huharibika na kutupwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker, akizungumza na wanawake wakati wa kusheherekea Miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) tangu kuazishwa kwake na kuwa na wanachama wanawake wengi katika mikoa tofauti tofauti zaidi ya 10 hapa nchini. Alisema kuwa Wanawake milango imefunguka kwa benki hiyo hasa wakijiunga kwa makundi ili kupata mikopo yenye riba ya chini katika benki ya NMB hapa nchini.
 Wanawake wakiserebuka wakati wa kusherekea miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Rais wa Chama cha wenye viwanda Biashara na Kilimo nchini (TCCIA), John Mayanja atembelea baadhi ya kazi za wanawake wajasiliamali katika hafla ya Dinner Paty Gala iliyoambatana na Kusheherekea miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

MAISHA:Umuhimu wa Kusoma Vitabu

0
0
Kusoma vitabu kuna manufaa mengi kwa mtu binafsi na kwa jamii. Tunaweza kuitafakari kauli hii kwa namna nyingi. Binafsi, daima ninakumbuka usemi wa Ernest Hemingway, "There is no friend more loyal than a book," yaani hakuna rafiki wa kweli kuzidi kitabu. Ni kauli fupi na rahisi kukumbukwa, lakini ninaiona kuwa yenye ukweli kabisa.

Kitabu ni rafiki ambaye yuko kwa ajili yako muda wowote unapomhitaji. Kitabu kinaweza kuwa mshauri wako, kiongozi wako, nguzo ya kuitegemea.

Akili ya binadamu inahitaji matunzo, sawa na bustani. Bustani inahitaji kurutubishwa na kupaliliwa. Ikiachwa ivamiwe na magugu, inageuka kichaka. Kusoma vitabu ni kurutubisha akili na kuipalilia. Kama mtu anaweza, ni muhimu kusoma vitabu vya aina mbali mbali: vya siasa, saikolojia, fasihi, sayansi, maisha ya watu maarufu, falsafa, historia, uchumi, na kadhalika.

Ni makosa kudhani kuwa kusoma vitabu kunawahusu wanafunzi na waalimu pekee. Kila mtu anapaswa kusoma vitabu. Tutafakari manufaa yake kwa afya ya akili ya binadamu kama yalivyoelezwa kwa ufupi katika makala hii. 

EID MUBARAK

0
0
Timu nzima ya Kampuni ya Michuzi Media Group (MMG) inawatakiwa Wadau wake wote popote pale mlipo, sikukuu njema ya Idd el Hajj na tuisherehekee kwa amani na mapenzi tele kama ilivyolekezwa katika vitabu vitukufu vya Dini.

IDD MUBARAK
MMG TEAM
Viewing all 109581 articles
Browse latest View live




Latest Images