Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

INTRODUCING: Uncle Amri - Kwa Mungu Kutamu Prd Kimambo Touches


INTRODUCING: Meddy Music ft Mr. Sholla - Ni Wewe

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 09/09/2016

RAIS DKT MAGUFULI ALIPOONGEA NA WAKAAZI WA MAGOMENI KOTA

introducing "MZURI PESA" by King Crazy GK

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO

TASWIRA MBALIMBALI ZA SHINDANO LA MISS ILALA 2016, MREMBO JUDITH KABETE ATWAA TAJI

$
0
0
Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Miss Ilala 2016, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akingumza na kutoa nasaha zake kwa Warembo wao ambao pia ni Mabalozi wazuri wa utunzaji wa Mazingira katika Wilaya Ilala. Mh. Mjema amewapongeza Warembo hao kwa kujitoa kwao katika shunguli mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusaidia wasiojiweza, amesema huo ni mfano wa kuigwa na wengine pia. Alieibuka Mshindi na kuwa Miss Ilala 2016, ni Judith Kabete (13), Mshindi wa Pili ni Nuru Kondo (9) pamoja na Grace Marikita (4) alieshika nafasi ya tatu.
 Baadhi wa Warembo hao wakiwa na bango la kuonyesha juhudi zao za kupiga vita uchafuzi wa Mazingira katika Wilaya ya Ilala.
 Warembo wakitoa bururani ya ufunguzi.
 Baandi ya Warembo wakipita na mavazi ya Ubunifu.


MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA KIWANDA CHA KOROSHO CHA AMAMA NA KUHUTUBIA WANANCHI WA TANDAHIMBA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemaliza ziara yake ya siku NNE mkoani Mtwara kwa kuwahakikishia mamia ya wakazi wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kuwa serikali imetenga zaidi ya bilioni 170 kwa ajili ya utekeleza wa mradi mkubwa wa maji katika wilaya hiyo ili kuondoa tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi wa Tandahimba.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Tandahimba na wakati amesimamishwa njiani na wananchi wa vijiji vya Kitama I na Kitama II ambao walitaka kumsalimia akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais amesema mkakati wa serikali wa sasa unalenga kuhakikisha wananchi wa Tandahimba na wa maeneo mengine nchini wanapata maji safi na salama hali ambayo itaondoa usumbufu wa wananchi kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Amesema anaimani kubwa kuwa mradi huo wa maji utakapokamilika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara utakuwa ni suluhu ya kudumu ya uhaba wa maji kwa wananchi hao wa Tandahimba.

Kuhusu usafirishaji wa korosho kwa njia ya magendo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonya kuwa serikali kamwe haiwezi kuwavulia watu wanaofanya vitendo hivyo na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.

Makamu wa Rais amesema kuwa biashara ya magendo ya korosho inainyima serikali mapato mengi ambayo yangesaidia shughuli za maendeleo za wananchi hivyo ameuagiza uongozi wa mkoa wa Mtwara uchukue hatua za kukomesha biashara hiyo haramu ambavyo ameifananisha na uhujumu uchumi kwa serikali.

Kuhusu ubovu wa barabara kutoka mjini Mtwara hadi wilaya ya Tandahimba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itajenga kilomita 50 za awali kwa kiwango cha lami katika barabara hiyo ili kuimarisha shughuli za usafiri na usafirishaji kati ya Mtwara mjini na wilaya ya Tandahimba.

Makamu wa Rais pia ameuagiza uongozi wa mkoa wa Mtwara kukutana haraka na Watendaji wa Wakala wa Barabara wa mkoa wa Mtwara ili kujadiliana kuhusu namna gani ujenzi huo utakavyotekelezwa.

Akiwa mjini Tandahimba, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika zoezi la utoaji wa zawadi mbalimbali kwa uongozi wa shule ya sekondari ya Tandahimba kwa kuingia katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya Kidato cha Sita ambapo Kampuni ya Startimes imetoa hundi ya shilingi milioni Mbili kwajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wilayani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Kitema I wilayani Tandahimba  waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili kwenye wilaya hiyo ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa kwa burudani ya ngoma wakati akiwasili kwenye makao makuu ya wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa wilaya ya Tandahimba  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kiwanda cha kubangua korosho cha AMAMA kilichopo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi na Mdhibiti wa ubora wa bidhaa Bw. Karim Hassan (kushoto) ya hatua mbali mbali ambazo korosho hupitia wakati wa kubanguliwa kwenye kiwanda cha AMAMA kilichopo Tandahimba mkoani Mtwara.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

DKT. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA (SMZ)

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo

MKUU WA MKOA WA MWANZA AKABIDHI VYAKULA KWA NIABA YA RAIS MAGUFULI KWENYE KITUO CHA WAZEE BUKUMBI KWA AJILI YA IDD EL HAJJ

$
0
0
Katika kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj siku ya Jumatatu Septemba 12, 2016, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, ametoa msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi laki saba na elfu themanini (780,000), kwa ajili ya Kituo cha kulelea Wazee na Walemavu wasiojiweza cha Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Akikabidhi msaada huo jana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliuhimiza uongozi wa kituo hicho kusimamia vyema ugawaji wa vyakula hivyo li kuwafikia walengwa, ikizingatiwa kwamba kumekuwa kukiibuka malalamiko kutoka kwa wazee wanaoishi katika kituo hicho kwamba misaada ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali imekuwa haiwafikii yote.

Hata hivyo Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Georgina Kwesigabo, alitanabaisha kwamba vyakula na misaana ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali kituoni hapo, yote imekuwa ikiwafikia walengwa wote isipokuwa kuna changamoto ya baadhi yao kuuza misaada wanayopatiwa ikiwemo vyakula, jambo ambalo linaulazimu uongozi wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kusimamia misaada hiyo hususani kuwapikia chakula wanaoishi kituoni hapo badala ya kuwagawia chakula ili wajipikie wenyewe.

Wazee wanaoishi kituoni hapo waliishukuru serikali kwa msaada huo ambapo walisema wanaendelea kumuombea Rais Magufuli na Serikali yake ili iendelee kuboresha kituo hicho ikiweo kuwekewa uzio ili kuondokana na hofu ya kiusalama waliyonayo kwani wakati mwingine wamekuwa wakiibiwa mali zao ikiwemo kuku ambazo wamekuwa wakizifuga.

Vyakula vilitolewa na Mhe.Rais Magufuli ni, mchele gunia sita (kila gunia kilo 50), mafuta ya kupikia madumu manne (kila dumu lita 20) pamoja na mbuzi wawili.
Baadhi ya wazee wanaoishi kwenye Kituo cha Bukumbi, wakifurahia mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya Rais Magufuli kuwapatia msaada wa vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj, itakayofanyika kesho kutwa jumatatu.

NEWZ ALERT: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Katibu Tawala Songwe na Wakurugenzi wa Halmashauri 13

$
0
0

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2016 amemteua Bw. Eliya Mtinangi Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo.

Bw. Eliya Mtinangi Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa jana tarehe 09 Septemba, 2016 ambao ni Ado Steven Mapunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na Bw. Tixon Tuliangine Nzunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

1.      Godwin Emmanuel Kunambi - Manispaa ya Dodoma
2.      Elias R. Ntiruhungwa             - Mji wa Tarime
3.      Mwantumu Dau                     - Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
4.      Frank Bahati                          - Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
5.      Hudson Stanley Kamoga        - Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
6.      Mwailwa Smith Pangani         - Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
7.      Godfrey Sanga                       - Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
8.      Yusuf Daudi Semuguruka      - Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
9.      Bakari Kasinyo Mohamed     - Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
10.   Juma Ally Mnwele                 - Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
11.   Butamo Nuru Ndalahwa       - Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
12.   Waziri Mourice                    - Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
13.   Fatma Omar Latu                 - Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo


Wakurugenzi wa halmashauri wote 13 walioteuliwa wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkoani Dodoma siku ya Jumanne tarehe 13 Septemba, 2016 kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam



10 Septemba, 2016

YANGA YAICHAPA MAJI MAJI BAO 3-0 UWANJA WA UHURU LEO

$
0
0
 Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko akiwania mpira na Beki wa Maji Maji, Selemani Kibuta wakati wa Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akionyesha uwezo wa kuuchukua mpira kwa adui yake, wakati wa Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
 Amis Tambwe wa Yanga, akimpiga tobo maridadi, beki wa Maji Maji, Ernest Raphael, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
 Chenga ya mwili: Mchezaji wa Yanga, Simon Msuva akimkwepa Beki wa Maji Maji, Hamad Kibopile, wakati wa Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Timu ya Maji Maji ya Songea, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 3-0.
 Mchezaji wa Yanga, Deus Kaseke akiipatia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Maji Maji.
Donald Ngoma wa Yanga, akichuana vikali na Beki wa Maji Maji, Bahati Yussuf.

SWALA YA EID KUSWALIWA BAKWATA MAKAO MAKUU KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laureana Ndumbaro azindua Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi jijini Dar es salaam

$
0
0
 Watumishi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika mistari tayari kwa kuanza mazoezi wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.
 Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (watatu kulia) na Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo (wa tatu kushoto) wakiongoza watumishi kutoka Wizara na Taasisi za Umma kufanya mazoezi wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.

  Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean  Ndumbaro (watatu kulia) akiwa bega kwa bega na  Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo akiwaongoza watumishi kutoka Wizara na Taasisi za Umma kufanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.
 Watumishi wa Umma kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Umma wakihitimisha mazoezi ya kupasha mwili huku wakiongozwa na Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (watatu kulia) akiwa na  Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo  wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.
 Watumishi wa Umma kutoka Wizara na Taasisi wakifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.

Mgeni rasmi Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru. Nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

UVCCM WATOA POLE KWA WAATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI

$
0
0
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umetuma salamu za pole wananchi wa mkoa wa Kagera kutokana na vifo vya zaidi ya watu 11 vilivyosababisha na tetemeko la ardhi lililotokea juzi.

Katika salamu hizo zilizotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVVCM, Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya umoja huo, alisema wamepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya vifo hivyo.

Alisema tetemeko hilo ni pigo kwa UVCCM na taifa kwa ujumla kwa kuwa limesababisha vifo vya watu ambao ni nguvu kazi ya taifa pia kusababisha hasara kutokana na uharibifu wa mali mbalimbali na makazi.

"UVCCM tumepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo kubwa na zito ambalo limesababisha maafa na hasara kwa taifa,"alisema.

Alisema umoja huo unawaombea marehemu wa tukio hilo wapate pumziko la milele peponi na kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurudi kwenye shughuli zao za kawaida.

"Katika kipindi hiki kigumu Jumuia yetu inaungana na Watanzania wengine kuzipa mkono wa pole familia zote zilizopoteza ndugu zao na pia tukiwafariji wote waliopata hasara ya kuharibikiwa nyumba zao na kupoteza mali,"alisema.

Alisema janga hilo ni limemgusa kila mtanzania mwerevu mwenye upendo na uzalendo hivyo linapaswa kuwaweka pamoja Watanzania wote ili kufarijiana na kukabiliana na magumu yaliyotokea.

Aidha, Shaka alisema wanatoa mkono wa pole kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kutokana na vifo hivyo na kasara iliyopatikana.

Shaka aliwashukuru na kuwakupongeza viongozi wa umoja huo walioko mkoani humo wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Yahya Kateme, kwa ushirikiano walioendelea kuutoa baada ya kutokea kwa tukio huilo.

Huu si wakati wa siasa bali ni kipindi kigumu cha kukabili yale yote yaliotokea na kudhuru au kuharibu taaswira iliokuwepo awali ya ustawi wa maisha ya wenzetu ambao wamepatwa na janga hilo.

Kila kijana mzalendo ni vyema akaenda kuripoti kwa viongozi wa maeneo husika aidha wakuu wa wilaya au mkoa ili kupewa maelekezo na miongozo katika kila hatua ya kusaidiana kwa hali na mali wakati wote hadi hali itakaporejea kama kawaida.

KAMPUNI YA MIKAELA PROFESSIONAL TAILORS KULITAMBULISHA JIJI LA MWANZA KWENYE UBUNIFU WA MAVAZI

$
0
0
Ofisi za Mikaela Professional Tailors zinapatikana Ghana Green View, barabara ya Airpot Jijini Mwanza. Wapigie kwa nambari 0767 68 28 88 ili wakuhudumie kwa wakati na kwa ubora.

Tofauti na ilivyo katika majiji mengine nchini kama vile Jijini Dar es salaam, Jiji la Mwanza halina mwamko mkubwa katika ubunifu wa mavazi.
Ni kutokana na hali hiyo, Wataalamu na Mabingwa wa Ushonaji wa mavazi ya aina mbalimbali (Kike na Kiume) Jijini Mwanza, Mikalela Professional Tailors, wameahidi kulitambulisha Jiji hilo katika ubunifu wa mavazi ili kuendana na kasi iliyopo katika majiji mengine.
"Awali nilikuwa nateseka sana. Nguo zangu nilikuwa nikishea Jijini Dar au Arusha na nikizivaa watu wengi wakawa wanauliza niliposhonea na kutamani niwapeleke. Nikaona kumbe Mwanza kuna uhitaji mkubwa wa ubunifu na ushonaji wa mavazi hivyo nikaamua kuanzisha kampuni ya ubunifu na ushonaji wa mavazi ya Mikaela Professional Tailor ili kukata kiu hiyo.

INTRODUCING "NI WEWE" BY NGOVI & PINORDY, 5 ONE RECORDS

back to school “Big Bash” and end of summer event on September 17 in Calgary – Alberta.

$
0
0
Friends of Calgary in collaboration with the Calgary Tanzanian Community in Canada are organizing  a back to school “Big Bash” and  end of  summer event on September 17 in Calgary – Alberta. 
This will include a soccer game between Calgary Vs Edmonton (Watani wa Jadi). In addition,  other activities such as volleyball, basketball and tennis  games will be  fielded - capped  by  a tongue-twisting  BBQ. 
You don’t wanna miss it...Wallahi tena!
Location:- South Calgary Park, Calgary, AB
Wote Mnakaribishwa!!!
By Team Calgary

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara ya kikazi Pemba

$
0
0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo  akitokea Unguja kwa ziara kikazi kisiwani humo akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwemma Shein

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na MkeweMama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo  kwa ziara maalum kisiwani humo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa KMKM Pemba wakati alipofika katika kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba kuangalia karafuu zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni  Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,alipofanya ziara maalum leo,(wa pili kulia) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Bi.Amina Salum Ali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mdhamini wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Nd,Abdalla Ali Ussi (kushoto) alipotembelea kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba kuangalia karafuu zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni  Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba leo alipofanya ziara maalum
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Bi.Amina Salum Ali (katikati) wakati alipotembelea kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba baada ya kuangalia karafuu zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni  Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kikazi kisiwani humo,(kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Nd,Bakari Haji Bakari
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma (wa pili kushoto) wakati alipotembelea Uwanja wa Mpira wa Gombani kuangalia matengenezo makubwa yaliyomalizika kwa utiaji wa (Tatan) ambapo sasa Uwanja huo utaweza kutumika kwa shuhuli mbali mbali za michezo ikiwemo Riadha,(kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu. 
Picha na Ikulu.


Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images