Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LILILOKUWA NA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA, AONGEA NA WAAKAZI WAKE.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi Mhe John Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Ali Hapi na viongozi wengine akitembelea eneo lililokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  alipotembelea na kuongea na wakaazi wa  Magomeni Kota wilaya ya Kinondoni  jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
 Wananchi wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi  wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
 Kiongozi wa wakazi wa  nyumba za Magomeni Kota Bi Mwajuma  Sama akiongea machache na kuomba dua  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli   alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016. 
PICHA NA IKULU.

INTRODUCING: QS INTERNATIONAL MUSIC BAND - Acha Nibangaize

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIXMUND BEGASHE

$
0
0

USIKOSE KUUNGANA NA MR SIXMUND BEGASHE TAREHE  10 SEPTEMBA 2016  ASUBUHI KATIKA KUMEPAMBAZUKA YA ITV ILI AKUJUZE VYEMA JUU YA MUSEUM ART EXPLOSION KWA UHAI WA SANAA NA UTAMADUNI NCHINI. 


KUMBUKA MAONESHO YANAYOFUATA YA PROGRAM YA M.A.E ni Tar 22 Sept Saa 11 jioni Ufunguzi wa maonesho ya Sanaa za Ufundi na Tar 23 Sept Saa moja kamili hadi saa 3:30 jioni Maonesho ya Jukwaani.

MAGAZETINI LEO JUMATANO SEPTEMBA 07

TSSA YATOA TAARIFA KWA SERIKALI JUU UKUZAJI UCHUMI NA UJEZI WA VIWANDA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Viajana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Mkutano wa kupokea taarifa ya Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), Meshach Bandawe akizungumza  wakati wa Mkutano wa kutoa taarifa kwa Serikali  juu ya hatua iliyofikiwa na Shirikisho hilo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara ambaye pia ni Mjumbe wa Shirikisho hilo, akichangia mada katika Mkutano wa kupokea taarifa ya Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.

Statement by the Deputy Minister for Health, Dr. Hamisi Kigwangalla, MP., on Homosexuality in Tanzania After a Meeting with Dr. Pierre Somse, UNAIDS Country Director for Eastern and Southern Afric

$
0
0
Yesterday I was visited by Dr. Pierre Somse, UNAIDS Deputy Director for Eastern and Southern Africa. We had a long meeting. Among other things, he was keen to learn my position regarding speculations among the donor countries as well as the international community that Tanzania is ‘harassing and discriminating Lesbian, Gay, Bisexual, Transgender and Intersex (LGBTI) people’, and that we are ‘banning HIV/AIDS programmes targeting HIV/AIDS interventions on these people and we are de-registering all NGOs with interventions on LGBTI’. He reported that there is an environment of fear and uncertainty in the HIV/AIDS programming work.

He said these speculations followed an intervention by our Minister where ‘she ordered no more distribution of lubricants until further notice’ and my visit to an NGO named CHESA which was purportedly accused of carrying out programmes on LGBTI and that ‘I ordered arrest of their officials etc.’

I responded as: 

1.Tanzania is a country built on the strong foundation of respect for human rights, dignity, personal freedom, democracy and rule of law. 
2.The Tanzanian government recognizes, respects and highly regards efforts and support by various stakeholders, including international NGOs, donor countries, local NGOs and the general community, in the HIV/AIDS response.
3.Tanzania upholds professionalism and has been using best practices emanating from scientifically proven and rigorous research and HIV/AIDS programmes used in the HIV/AIDS response.
4.Tanzania has its own constitution, laws, regulations, guidelines and modes of operation; our country takes very seriously our national values and beliefs, customs and traditions, and we will, always, protect them.
5.Tanzania assures our friends, partners and the donor community of our continued collaboration and my office is open for any dialogue when there is any uncertainty. Let it be known that I operate on an ‘open-door’ policy.   
6.Despite the fact that we have been insisting that the most important of the key and vulnerable populations for us is the ‘adolescent girls and young women group’, I can not deny the presence of LGBTI people in our society, and the risk they pose in fueling the spread of HIV/AIDS in the society, and I understand that is why our Ministry, before even I was appointed to this position, had its own ‘National Guideline for Comprehensive Package of HIV Interventions for Key Populations’, which I am aware that it provided authority for programmes to distribute ‘lubricants’ to LGBT etc. 
7.Let all be aware that, before I came to this office, the government had de-registered NGOs such as ‘Sisi Kwa Sisi’ and banned a number of programmes which violated the requirements of the laws of our land, customs and traditions, with respect to issues around LGBTI people. This task is a continuation of the same as well improve working relationship between the government and partners. 
8.We have information that some NGOs have been implementing programmes ‘in the name of HIV/AIDS response in the LGBTI people’ and went beyond their scope, in fact they have been promoting homosexuality. Some NGOs have been implementing programmes in jurisdictions without LGBTI people; I have vivid complaints by villagers in various areas of Tabora and Shinyanga where some programmes have been distributing ‘lubricants’ and educating them on how to use them! NB: we all know that some of these communities are even skeptical when it comes to taking and or receiving education about  ‘condoms’ and how to use them, what is of ‘lubricants’? We have evidence that some NGOs have been defaulting their mandatory returns; some have been withholding, against the law that registers NGOs, information regarding their various programmes and their various sources of funding. A good example is CHESA, which omitted to provide reports regarding their programmes and donors, and when asked to do so, mis-reported and under-reported – they had funds from JHPIEGO which they received but purposively omitted to report, while JHPIEGO was honest enough as to report the work that they were doing in partnership with CHESA! 
9.Despite the presence of LGBTI people in our country, we do not subscribe to the assertion that ‘there is a gender continuum’, we still recognize the two traditional sexes, i.e. Male and Female, and there is nothing in between or beyond! So any effort to claim otherwise is not allowed in Tanzania. 
10.Tanzania does not allow activist groups carrying out campaigns that promote homosexuality and the assertion that there is a ‘gender continuum’ that must be recognized and protected. 
11.Any ‘act or attempt to commit unnatural offences’ is illegal and severely punished by law (refer Cap 16 of the Laws of Tanzania, The Penal Code, Sect. 154 and 155.)  
12.We, so far, have not de-registered any NGO that carries programmes on LGBTI, we are investigating those which have been reported to have broken the law. The various state organs are working on the matter keenly and closely. If there will be found any violation of the laws, customs and traditions, appropriate actions shall be taken in accordance to the laws and regulations of our country. 
13.Our technical team is looking into the technical aspects of carrying out implementation of programmes using the ‘public health approach’ without breaking the laws, regulations, customs and traditions. The government will publicize its way forward when consensus is reached regarding our position and approach on LGBTI programming. 

Meanwhile, 

(i)I demand the team that is carrying out the ‘Mapping and enumeration study for Intravenous drug users (IDUs), Men having sex with men (MSMs) and female sex workers (FSWs)’ to never share their findings with any one within or outside the country, without permission of the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children. 
(ii)We will collaborate with the Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS), - the Civil Society Desk, in embarking on a vetting task for NGOs and enlist credible NGOs in their website as well as our website. We further advise international NGOs and partners interested to work with credible NGOs to contact the government for a letter of clearance so that programmes brought in our country in good faith shall not be tarnished by irresponsible and unprofessional people carrying out illegal activities.
(iii)The government shall use its machinery to properly vet all NGOs in terms of programme activities, funding sources and other motives.
(iv)The government requires all NGOs working with our Regional Secretariats and Local Government Authorities to revisit our national guidelines on how to work in partnership with these authorities, where they would be reminded of community entry/exit steps, community mobilization strategies, procedures for behavior change communications, procedures for supportive supervisions, requirements of sharing their implementation plans, research results, progress reports and summative programme reports. 
(v)Whenever you are not sure if you have crossed the line, visit the office of the Director of NGOs at the Ministry for clarity and guidance. 

By

Dr. Hamisi Kigwangalla, MP.
Deputy Minister – Health, Community Development, Gender, Elderly and Children.

APOKEA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS SALVA KIIR NA KUTOKA KWA RAIS NKURUNZIZA.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit amemtumia ujumbe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akimuarifu kuwa hali ya usalama katika nchi hiyo imeanza kutengemaa.
Rais Salva Kiir Mayardit amewasilisha ujumbe huo kupitia kwa Mjumbe wake Maalum Mhe. Aggrey Tisa Sabuni ambaye pamoja na kuwasilisha ujumbe huo amesema Sudani Kusini imekamilisha nyaraka za azimio la kuridia mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao umewasilishwa  tarehe 05 Septemba, 2016 katika makao makuu ya Jumuiya Jijini Arusha. 

Mhe. Aggrey Tisa Sabuni amesema Sudan Kusini ipo tayari kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala mbalimbali yenye manufaa kwa wananchi ikiwemo biashara na uwekezaji na kwamba ni matumaini yake kuwa itapata ushirikiano mzuri.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na taarifa za kutengemaa kwa hali ya amani nchini humo na kwamba ni matarajio yake kuwa Sudan Kusini itajikita katika maendeleo ya wananchi wananchi wake.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza ulioletwa na Mjumbe Maalum wa Rais huyo Mhe. Aime Laurentine Kanyana.

Katika ujumbe huo Rais Nkurunziza amesema hali ya Burundi ni shwari na kwamba wananchi wa Burundi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Tanzania yenye wakimbizi takribani 200,000 wa kutoka Burundi inafurahishwa na taarifa za kuwepo hali ya amani nchini humo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Septemba, 2016.

WENYE MAJINA HAPO CHINI WAHITAJIKA KUPATA TAARIFA MHIMU.-MAHAKAMA.

$
0
0
Tunaomba kutoa taarifa kuwa, wenye majina na anuani hapo chini ambao ni watumishi/walikuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanahitajika kupata taarifa muhimu na maalum juu ya masuala yahusuyo Utumishi wao: Wafike na kuonana na Bibi. Agatha Ng’ingo – Mkurugenzi Msaidizi- Idara ya Utawala na Utumishi, namba ya simu (0673 – 001 773) ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.

S/N

JINA KAMILI

CHEO

KITUO CHA KAZI

C/N

1

BW. ROBERT WILLIAM CHAGAKA

DEREVA II

MAHAKAMA YA WILAYA IRAMBA

111824992

2

BW. GODLISTEN MOSES MWANRI

DEREVA II

MAHAKAMA YA WILAYA KISHAPU

111827839

3

BI. AGNES AUDAX RWEGOSHORA

HAKIMU MKAZI II

MAHAKAMA YA MWANZO UJIJI KIGOMA

111838464

4

BI. HAPPINESS ELIAS MISHWARO

HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO MWANDAMIZI

MAHAKAMA YA WILAYA MBARALI

10915901

5

BW. BARAKA JAFARI MUKAMA

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA YA WILAYA ILALA

9927780

6

BW. RAMADHANI MOHAMED KILYOUSUNGU

MLINZI

MAHAKAMA YA WILAYA RUFIJI

9496501

7

BI. REHEMA SAMWEL PANDAPANDA

HAKIMU MKAZI II

MAHAKAMA YA WILAYA MPWAPWA

9927919

8

BI. HAWA GODREY MKUMBO

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA YA WILAYA KASULU

8203232

9

BW.CHRISTINA JOHN MAYILA

MSAIDIZI WA OFISI MWANDAMIZI

MAHAKAMA YA WILAYA KAHAMA

7758540

10

BW. YASSINI WAZIRI MASELE

MLINZI

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SINGIDA

111400187

11

BW. JOSEPH FRANCIS BOMA

MLINZI

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SINGIDA

111397724

12

BW. BRUTON RABIEL KIMARO

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MANYARA

7203497

13

ABIHUDI GILLIARD MASEU

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA KUU ARUSHA

5187924

14

HUSSEIN HASSAN BACHOO

AFISA UGAVI I

DAR ES SALAAM

5529186

15

ASHA MAGOMBA ABDALLAH

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II

MAHAKAMA YA WILAYA MONDULI

111827925

16

BW. AMRI MUSSA RASHIDI

MLINZI

MAHAKAMA YA WILA

YA TANDAHIMBA

9544435

Imetolewa na,
MTENDAJI MKUU.

Benki ya TIB Corporate yatoa msaada wa Sh 10 million kwa taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

$
0
0
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya TIB Corporate Bw Frank Nyabundege (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi y ash milioni 10 kwa Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dk. Julius Mwaiselage (kulia) kuiwezesha taasisi hiyo kukabiliana na mahitaji mbalimbali katika matibabu ya wagonjwa wa saratani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Charles Singili (wa pili kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Charles Singili (kushoto) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 
Benki ya TIB Corporate imetoa msaada wa sh mil 10/- kwa taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ikilenga kuiwezesha taasisi hiyo kukabiliana na mahitaji mbalimbali katika matibabu ya wagonjwa wa saratani.Msaada huo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo katika kuisaidia jamii kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mteandaji wa benki hiyo Bw Frank Nyabundege alisema taasisi hiyo ina uhuru wa kuchagua mahali inapoweza kuelekeza matumizi ya pesa hizo kulingana na vipaumbele vyake.

“Tunaunga mkono jitihada zinazofanywa na ORCI katika kukabiliana na saratani hapa nchini na ndio maana na sisi tukaona tuna wajibu wa kuunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia kiasi hiki cha pesa ili kisaidie kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili taasisi hii muhimu zikiwemo,’’ alibainisha Bw Nyabundege.

Alisema uwepo wa taasisi hiyo ni fahari kwa taifa kwa kuwa imekuwa ikisaidi mapambano dhidi nya ugonjwa huo ambao umekuwa kikwazo katika uzalishaji kwa kuwa umekuwa ukishambulia nguvu kazi ya taifa.

“Matibabu ya ugonjwa huu pia yamekuwa yakihusisha gharama kubwa na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi katika ngazi za kifamilia,’’ aliongeza.Alitoa wito kwa watu binafsi na mashirika mengine kujitokeza na kusaidia taasisi hiyo ya Serikali kwa kiasi chochote.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage alisema kwa sasa taasisi yake inakabiliwa na ongezeko la wagonjwa huku akikabiliwa na uhaba wa miundombinu na dawa na vifaa tiba vinavyoendana na ongezeko hilo na hivyo kutoa wito kwa mashirika, taasisi na watu binafsi kuisaidia taasisi hiyo.

“Kwa takwimu za mwaka jana tulipokea wagonjwa zaidi ya elfu tano ikilinganishwa na wagonjwa 1500 kwa mwaka tuliokuwa tukiwapokea miaka ya nyuma wakati taasisi inaanza,’’ alisema huku akitaja baadhi ya sababu za ongezeko la ugonjwa kuwa ni pamoja na aina ya vyakula vinavyoliwa na kwa sasa, matumzi ya tumbaku na ukosefu wa mazoezi miongoni mwa wana jamii.

BENKI YA CRDB YAZINDUA KADI ya Kimataifa ya ‘TembocardVisa Infinite’

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma "Premier Club" pamoja na Kadi ya Kimataifa ya TemboCardVisa Infinite uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza wakati wa uzinduzi wa TemboCard Visa  Infinite pamoja na uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja Wakubwa cha Premier Club.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), akimkabidhi Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kadi ya kimataifa ya ‘TembocardVisa Infinite’, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo uliokwenda sambamba na kituo cha kutolea huduma ‘Premier Club’ jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi Kadi ya TemboCard Visa  Infinite Naibu Spika Dk. Tulia Ackson.


CLIMATE OUTLOOK FOR TANZANIA OCTOBER – DECEMBER, 2016 VULI RAINFALL SEASON

MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA TANZANIA KIPINDI CHA OKTOBA - DESEMBA 2016

MAKAMU WA RAIS AZINDUA HOTEL YA NYOTA TANO KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la funguzi wa hotel ya Ramada Encore  yenye hadhi ya nyota 5 jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo Bw. Abdul Ismail.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa hoteli ya Ramada Encore iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli Ramada Encore  Bw. Abdul Ismail wakati wa halfa fupi wa uzinduzi wa Hotel ya Ramada Encore jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua hoteli ya nyota 5 ya Ramada Encore katikati ya jiji la Dar es salaam.

Kikosi cha Young Africans leo dhidi ya Ndanda FC.

$
0
0
Kikosi cha Young Africans leo dhidi ya Ndanda FC.
1. Ali Mustafa 
2. Juma Abdul 
3. Haji Mwinyi
4. Andrew Vicent 
5. Nadir Haroub 
6. Thabani Kamusoko 
7. Saimoni Msuva
8. Amisi Tambwe
9. Donald Ngoma
10. Obrey Chirwa 
11. Deusi Kaseke

Akiba:
- Beno Kakolanya 
- Hassani Kessy
- Oscar Joshua
- Kelvin Yondani
- Juma Mahadhi
- Mateo Antony
- Yussuf Mhilu.

TASWIRA MBALIMBALI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitoa wito kwa waajiri nchini kuwasilisha nyaraka za wastaafu kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii miezi mitatu hadi sita kabla ya kustaafu kwa wateja wao ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba Leo Bungeni Mjini Dodoma.

BEI YA MADAFU LEO.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 06/09/2016

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA MSUMBIJI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Bibi, Monica Patricio Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais leo,(katikati) Balozi Mdogo wa Msumbiji anyefanyia kazi zake Zanzibae Bw. Jorge Augusto Menezes.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio  mara  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio (wa pili kulia) akiwa na ujumbe aliofuatana nao mara  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
[Picha na Ikulu.]

WIZARA YA AFYA NA UNDP KUJA NA MRADI WA KUPUNGUZA TAKA HATARISHI.

$
0
0
Na Ally Daud – Maelezo.
HOSPITALI  za Muhimbili, Amana, Mwananyamala na  Kairuki za Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuwekwa kwenye mradi maalum wa kudhibiti taka hatarishi ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha usafi wa mazingira katika huduma za afya nchini.

Mradi huo wa kudhibiti taka hatarishi ikiwemo sindano, gloves, nyembe na bandeji unasimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mazingira uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma ya Afya na Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Neema Rusibawengile  alisema kuwa lengo la mradi huo  una lengo la kukabiliana na magonjwa ya maambukizi katika maeneo ya hospitali nchini. 

“Mkutano huu umelenga kuandaa na  mradi utaodhibiti taka hatarishi amabao utanza kufanya kazi katika hospitali za Muhimbili,Amana,Mwananyamala kairuki na baadaye kuendelea nchi nzima” alisema Dkt Rusibawengile. 

Dkt. Rusibawengile alisema kuwa  mkutano huo pia umewakutanisha wadau mbalimbali wa Maendeleo na Mazingira watakaojadili   mbinu mpya za kutunza mazingira kwa ajili ya kupeuka magonjwa ya maambukizi nchini yanayotokana na taka hatarishi.

Kwa mujibu wa Dkt Rusibawengile alisema  mkutano pia huo unalenga kupata njia mbadala za kupunguza uzalishaji wa mekyuri katika hospitali, zahanati na vituo vya afya ili kuondoa utumiaji wa vifaa vyenye nishati hiyo.

Kwa upande wa mratibu wa udhibiti wa taka hatarishi za Hospitali Dkt. Honest Anicetus alisema  wadau wa mkutano huo pia wamepanga kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili  sekta ya afya katika utunzaji wa mazingira.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images