Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiingia kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuendesha mkutano wa nne(4) wa bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma. 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai Akiwaongoza Wabunge wa kuimba wimbo wa Taifa wakati wa mkutano wa nne(4) wa bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika ukumbi wa bunge wakati wa mkutano wa nne(4) wa bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa mkutano wa nne(4) wa Bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Selemani Said Jafo (MB) akieleza mpango wa kuendelea kuimarisha hospitali za Serikali Nchini.
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akiwaeleza jambo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju na Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana,Wazee na Wenye Ulemavu wakati wa mkutano wa nne(4) wa bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BILIONI 3 KUSAIDIA WATOTO WA KIKE KURUDI SHULE.

0
0

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akizungumza kuhusu mradi ambao una malengo ya kurejesha watoto wa kike shuleni. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Hashina Begum na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi akizungumza kuhusu mipango ya serikali kukabiliana na tatizo la watoto wa kike kukatishwa masomo.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watu Duniani (UNFPA), Maria Karadenizli akielezea takwimu za watoto wa kike ambao hawapo shuleni.

Na Mwandishi wetu.
Katika kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa shuleni na hatimaye kumaliza masomo yao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetenga Dola 1,605,000 ambazo ni zaidi ya Bilioni 3 za Kitanzania ambayo zitatumika kuwasaidia watoto wa kike nchini kurejea katika shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo.

Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodriguez alisema kuwa Tanzania bado inaonekana kuwa na tatizo la watoto wa kike kuachishwa masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo kupata mimba za utoto na ndoa za utotoni hivyo kupitia mradi huo wataweza kuwasaidia watoto hao kuendelea na masomo.

Bi. Rodriguez alisema UNESCO imeamua kushirikiana na serikali ili kuwasaidia watoto wa kike kurejea masomoni na utafanyika kwa uhakika bila kumwacha mtoto yoyote na wana matumaini utaweza kusaidia watoto wa kike ambao wamekatishwa ndoto zao kimaisha kutokana na kukatishwa masomo.

“Tanzania kuna tatizo la watoto wa kike kusahaulika katika elimu na UNESCO imejitoa kushirikiana na serikali ya Tanzania ili kusaidia kukuza elimu ya watoto wa kike, “Baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kuchangia ni pamoja na mambo ya asili, wamekuwa wakiwaozesha ndoa za utotoni na na watoto wengine wamekuwa wakipata mimba za utoto na hivyo kuacha masomo … mradi huu ni wa uhakika na utasaidia kukuza elimu,” alisema Bi. Rodriguez.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi alisema serikali inafahamu kuwepo kwa changamoto hizo na imekuwa ikifanya jitihada ili kuhakikisha kuwa matatizo ya watoto wa kike kukatishwa masomo yakimalizika.

Alisema kuwa makabila mengi ya Tanzania yamekuwa yakiwaona watoto wa kike kama watu wa kukaa nyumbani na kulea watoto lakini kama jamii ikiwa na mtizamo tofauti na kuwawezesha watoto wa kike basi wanaweza kusaidia nchi kukuza uchumi.

“Tumeona kazi ambayo wameifanya UNESCO hata machifu huko Ngorongoro wameanza kuelewa umuhimu wa watoto wa kike kuwa shuleni na kwa mpango huu matarajio ya serikali ni kumaliza changamoto iliyokuwepo awali.

“Serikali inafahamu kuna changamoto nyingi ambazo zinawakuta watoto wa kike na sio katika elimu pekee bali ni maeneo mengi … serikali inataka kukuza thamani ya elimu kwa watoto wa kike ambao wengi wao wanakatishwa kwa sababu ya mimba na ndoa za utotoni,” alisema Bi. Tarishi.


Nae Afisa Mradi wa Maswala ya Afya ya Uzazi kwa Vijana (UNFPA), Fatina Kiruviya alisema mradi una malengo ya kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa shuleni na kwa kuanza wanataraji kufanya mradi Ngorongoro, Pemba, Geita na Sengerema.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO

UCHAMBUZI WA HABARI MAGAZETINI LEO.

Benki ya TIB Corporate sasa kutoa huduma zake kupitia Benki ya Posta.

0
0

Benki ya TIB Corporate imeingia mkataba wa ubia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) utaoiwezesha benki hiyo (TIB Corporate) kutoa huduma zake kupitia matawi makubwa na madogo zaidi ya 60 ya benki ya Posta yaliyopo kote nchini.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana , Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate Bw Frank Nyabundege alisema ushirikiano huo wa kimkakati unalenga kuwaongezea wigo wa kibiashara wateja wake kupitia zaidi ya matawi makubwa 30 na mengine madogo 30 ya TPB yaliyopo kote nchini.

"Ushirikiano baina yetu unakwenda sambamba na mtazamo na malengo ya benki yetu kuhakikisha tunawafikia wateja kwa ukaribu kadiri tuwezavyo. Umuhimu wa aina hii ya ushirikiano unaonekana kuwa na tija zaidi kwa sasa kwa kuwa nchi yetu inaelekea kujikita kwenye uchumi wa viwanda hivyo kama taasisi ya fedha tunawajibu wa kuwa karibu zaidi na wateja wetu,’’ alisema Bw Nyabundege.

Alisema ushirikiano huo utahusisha huduma zote muhimu zinazotolewa na benki yake sambamba na kuhakikisha suala la usalama katika mihamala ya wateja wa benki hizo kwa kuwa masuala ya uhamisho wa fedha hayatahusisha ubebaji wa fedha kwenye mifuko huku pia suala la kutunza siri za wateja likizingatiwa zaidi.

“Hivyo basi iwapo mteja wetu ataweka pesa zake kupitia benki ya Posta, kiasi hicho cha pesa kitaingia kwenye akaunti yake benki ya TIB Corporate mara moja,’’ alibainisha. Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw Sabasaba Moshingi, alipongeza ushirikiano huo huku akibainisha kwamba wateja wa benki yake pia watanufaika na mpango huo.

"Baadhi ya wateja wetu wamekuwa wakifanya biashara na wenzao wenye akaunti za benki ya TIB Corporate hivyo kupitia ushirikiano huu wateja wetu watakuwa wamerahisishiwa shughuli zao za kibiashara. Kwa sasa benki yetu ina matawi makubwa zaidi ya 30 na mengine madogo 30 kote nchini, hivyo ni wazi kwamba ushirikiano huu una tija kubwa katika kipindi hiki cha kujenga Tanzania ya viwanda ,’’ alibainisha.

Zaidi Bw Moshingi alitoa wito kwa wateja wa benki zote mbili kuutumia vyema ushirikiano huo ili uwe na tija zaidi katika shughuli zao za kibiashara.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate Bw Frank Nyabundege (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Bw Sabasaba Moshingi (kulia) wakibadilishana mkataba wa ubia utaoiwezesha benki ya TIB Corporate kutoa huduma zake kupitia matawi 32 ya benki ya Posta Tanzania yaliyopo kote nchini wakati wa hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Jaffer Machano (wa kwanza kulia),Mkurugenzi wa Teknolojia na Uendeshaji wa TPB Bw Jema Msuya (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya TIB Rasilimali, Bi Antoinette Tesha-Ntlemo (wa kwanza kushoto)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate Bw Frank Nyabundege (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Bw Sabasaba Moshingi (kulia) wakibadilishana mkataba wa ubia utaoiwezesha benki ya TIB Corporate kutoa huduma zake kupitia matawi makubwa na madogo zaidi ya 60 ya benki ya Posta Tanzania yaliyopo kote nchini wakati wa hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Charles Singili (wa pili kulia), akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa benki ya TIB Rasilimali, Bi Antoinette Tesha-Ntlemo ( kushoto) akizungumza wakati wa hafla hiyo.

MZEE SENGA NDANI YA KIPINDI CHA THE AVENUE CHA TBC1

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKANUSA TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII

0
0
  

YAH: KUKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE
MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII

Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.

Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.

Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais



Dar es Salaam

MATUKIO YA BUNGENI MJINI DODOMA LEO.

0
0
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiingia kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuendesha mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai Akiwaongoza Wabunge wa kuimba wimbo wa Taifa wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika ukumbi wa bunge wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wakati wa mkutano wa nne(4) wa  bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

Shule za msingi 50 jijini Dar zachuana shindano la kutamka herufi.

0
0
 Mwanafunzi wa shule ya msingi Genesis, Andrelia Muga (kushoto),
akichuana na wanafunzi wenzake ili kumpata mshindi    katika shindano
la kutamka herufi lililodhaminiwa na kampuni ya Saruji Tanga ambalo
zaidi ya shule 50 za jijini Dar es Salaam zilishiriki.
 Mwanafunzi wa shule ya msingi Genesis,Aggrey Marealle (kushoto),
akichuana na wanafunzi wenzake ili kumpata mshindi    katika shindano
la kutamka herufi lililodhaminiwa na kampuni ya Saruji Tanga ambalo
zaidi ya shule 50 za jijini Dar es Salaam zilishiriki jijini humo
juzi.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Genesis wakishangilia baada ya shule
yao kuibuka kidedea katika shindano la kutamka herufi lililodhaminiwa
na kampuni ya Saruji Tanga ambalo zaidi ya shule 50 za jijini Dar es
Salaam zilishiriki.

 Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Saruji Tanga, Hellen
Maleko (kushoto), akikabidhi kikombe kwa wanafunzi wa shule ya msingi
Genesis, baada ya shule yao kuibuka washindi wa jumla wa shindano la
kutamka herufi lililodhaminiwa na kampuni ya Saruji Tanga ambalo zaidi
ya shule 50  Dar es Salaam zilishiriki jijini humo jana.

JPM akagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam asubuhi hii

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kukakagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam asubuhi hii,Rais Magufuli aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh,Paul Makonda pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako .

 Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akizungumza jambo wakati Rais Dkt Magufuli alipokwenda kukagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam asubuhi hii,Rais Magufuli aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh,Paul Makonda pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

BEI YA MADAFU LEO.

WANAFUNZI 3918 WACHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO KWA AWAMU YA PILI.

0
0
WANAFUNZI 3,918 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano awamu ya pili kujaza nafasi zilizokuwa wazi kutokana na ufinyu wa nafasi na baadhi ya wanafunzi kutoripoti kwa wakati.

Taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe ilisema kati ya wanafunzi hao wasichana ni 2,413 na wavulana 1,505.

“Kuchaguliwa kwa wanafunzi hao kumefuatia kuwapo kwa nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni tangu kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano katika awamu ya kwanza” alisema Mhandisi Iyombe. 

Aidha Mhandisi Iyombe alibainisha kuwa kati ya wanafunzi 1,864 sawa na asilimia 47.58 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo kati yao   wasichana 1,099 na wavulana 765.

Mhandisi Iyombe aliongeza kuwa katika masomo ya Sanaa na Biashara wanafunzi takribani 2,054 (52.42%) wamechaguliwa kujiunga na masomo hayo, ambapo kati yao wasichana ni 1,314 na wavulana 740. 

“Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii” alisema Mhandisi Iyombe.
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz. 

REPUBLIC OF S. SUDAN DEPOSITS INSTRUMENTS OF RATIFICATION ON THE ACCESSION TO THE TREATY FOR THE ESTABLISHMENT OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY TO THE SECRETARY GENERAL

0
0
The Republic of South Sudan today deposited the instrument of ratification on the Accession to the Treaty for the Establishment of the East African Community to the Secretary General of the East African Community (EAC) Amb. Liberat Mfumukeko at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

Depositing the instrument of ratification with the Secretary General of the East African Community means the Republic of South Sudan is now a new family member of the East African Community with full and equal rights, obligations and privileges.

‘’I would, therefore, like to seize this opportunity to commend President Salva Kiir, the Government and the entire people of the Republic of South Sudan for their tireless efforts and commitment that enabled them to achieve this important milestone”,  the Secretary General said at a short ceremony attended by the Chair of the EAC Council of Ministers and Tanzania’s Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation, Amb. Dr. Augustine Mahiga; Kenya’s Cabinet Secretary, Ministry of East African Community, Labour and Social Protection, Hon. Phyllis Kandie; Burundi’s Minister of Foreign Affairs, Hon. Alain Aime Nyamitwe, and the one in the Office of the President responsible for EAC Affairs, Hon. Leontine Nzeyimana; Permanent Secretaries/ Principal Secretaries from Partner States, EAC Deputy Secretaries Generals, Counsel to the Community and members of media.
Chair of the EAC Council of Ministers, Amb. Dr. Augustine Mahiga receives document of instrument of ratification from H. E. Hon. Aggrey Tisa Sabuni.

In addition, on the Republic of South Sudan were Secretary General, South Sudan EAC Secretariat, Mou Mou Athian Kuol, South Sudan Ambassador to Tanzania, Mariano Deng Ngor, Director of East African Community, Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Amb. Agnes Oswaha and Legal Counsel, Ministry of Justice and Constitutional Affairs, Juba, South Sudan,Lawrence Loro Kamilo.

Amb. Mfumukeko disclosed  that now that South Sudan have taken a step further, the Secretariat will seek guidance from the Council of Ministers on developing a detailed roadmap for integrating the Republic of South Sudan into the ongoing EAC projects and programmes.“We shall be informing the Leardership in Juba of every step we shall be taking in this regard”.

The EAC Chief called upon the media to fully participate in integrating the Republic of South Sudan in the EAC by reporting objectively on the issues at hand. He said EAC  attaches great importance to the role of the Media in promoting awareness, discourse and involvement of the broad range of stakeholders in the East African regional integration process.
 
Secretary General of the East African Community (EAC) Amb. Liberat Mfumukeko displays document of instrument of ratification from S.Sudan.

The EAC Secretary General also reiterated to  both  national, regional and International media on their role to get the region and the new Partner State to embrace regional integration with passion, dedication and commitment for the benefit of the present and future generations of the Community.

On his part, the Presidential Envoy of the Republic of South Sudan, H. E. Hon. Aggrey Tisa Sabuni said membership in EAC for Republic of South Sudan will henceforth mean that the country will never be the same again. “The EAC integration process is important for South Sudan. Currently, the EAC is the most advanced Regional bloc on the African Continent”.

He noted that South Sudan’s membership in the EAC is likely to provide concrete benefits to the country and the region as a whole, adding that “deep regional integration programmes that South Sudan shall soon undertake are likely to enhance overall EAC competitiveness which will lead to higher economic growth, employment creation and poverty reduction”.

Notes to Editors

Republic of South Sudan applied to join the East African Community on 10th June, 2011. A Verification Committee from the EAC visited the Republic of South Sudan from 15th to 31st July, 2012 with the aim of establishing the Republic of South Sudan‘s level of conformity with the criteria for admission of foreign countries into the East African Community as provided under Article 3 of the EAC Treaty.
Presidential Envoy of the Republic of South Sudan, H. E. Hon. Aggrey Tisa SabunI having chat with Amb. Liberat Mfumukeko.

Based on recommendation of the report by the Verification Committee, the EAC Heads of State Summit in November, 2012 directed the Council of Ministers to negotiate the admission of South Sudan putting into consideration the provision of the EAC Treaty on the criteria of joining the Community.

As a result, the EAC Council of Ministers established a High Level Negotiation Team and negotiation process with the Republic of South Sudan commenced. To initiate this process on the side of South Sudan, His Excellency Salva Kiir Mayardit also appointed a High Level Committee on 13th March, 2014 to oversee South Sudan’s accession to the EAC.

Negotiations between the EAC and the Republic of South Sudan went smoothly culminating in its admission to the EAC by the 17th EAC Heads of State Summit held on 2nd March, 2016 in Arusha, Tanzania. At that Summit, the Heads of State designated the Chairperson of the Summmit, H. E. President Dr. John Pombe Joseph Magufuli to sign the Treaty of Accession with the Republic of South Sudan.
A group photo opportunity, delegation from South Sudan, EAC Partners States Ministers, EAC Executives and other officials.

In this regard, H. E. President Salva Kiir and H. E. President Dr. John Pombe Joseph Magufuli signed the Treaty of Accession on 15th April this year in Dar es Salaam, Tanzania. The Republic of South Sudan was given up to 30th of September, 2016 to deposit the instrument of ratification with the Secretary General of the East African Community in Arusha.

SERIKALI KUTOA RUZUKU KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI.

0
0
Wachimbaji Wadogo Wadogo


Na Daudi Manongi-MAELEZO-Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imepanga kuwapatia ruzuku wachimbaji wadogo wa madini ili kuongeza mchango wa madini katika pato la taifa kutoka asilimia 3.5 ya sasa hadi 10.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha Tunatekeleza kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Taifa(TBC).

“Sekta ya Madini inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa,lakini dhamira yetu ni kwamba wakati tunaingia kuwa nchi ya kipato cha kati madini yanapaswa kuchangia si chini ya asilimia kumi”

Aidha aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025, hivyo adhma ya Wizara yake ni kuongeza kasi ya pato linalotokana na sekta ya madini na 

Aliongeza kuwa ili mafanikio hayo yafikiwe Serikali imekusudia kupandisha hadhi ya wachimbaji wadogo ili wafikie ngazi ya kuwa wachimbaji wa kati na hivyo sekta hii itachangia pato la Taifa kwa kiasi kikubwa.

Aidha Waziri Muhongo alisema kuwa Serikali imepokea pesa mkopo wa Tsh. Bilioni 3 kutoka Benki ya Dunia na imepanga kutoa ruzuku ya vifaa kwa wachimbaji hao wakati wowote kuanzia sasa.

“Serikali imeshaanza kutoa maeneo na kufikia tarehe 15 septemba tutaanza kutoa ruzuku kwa wachimbaji hao” alisema Prof. Muhongo.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuzuia utoroshaji wa madini nje ya nchi Profesa Muhongo alisema kuwa tangu mwaka 2012 Wizara yake iliweka madawati ya ukaguzi wa madini katika viwanja vya ndege vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam,Kilimanjaro na Mwanza na wakafanikiwa kukamata madini zaidi ya tani kumi. 

BALOZI KIJAZI KUWA MGENI RASMI UFUNGUZI WA BONANZA LA SHIMIWI

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi
Na May Simba-MAELEZO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Bonanza la Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambalo litafanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shimiwi. Bw. Moshi Makuka, bonanza hilo litafanyika tarehe 10, Septemba mwaka huu katika uwanja wa Taifa (Uhuru) kuanzia saa 12:30 asubuhi.

“Bonanza litawashirikisha watumishi wote wa Serikali kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salam” alisema ndugu Makuka.

Aidha Bw. Makuka alisema kwamba bonanza hilo ni maandalizi ya michezo ya Shimiwi ambayo yamepangwa kufanyika Mkoani Dodoma kuanzia tarehe 14 mpaka 27 Octoba mwaka huu.

Michezo ya mwaka huu ina lengo la kuunga mkono agizo la Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli la kuhamishia Makao Makuu yake mkoani Dodoma.

Mbali na hayo Bw. Makuka alisema michezo hiyo itawapa fursa watumishi wa umma kufahamu mazingira na kufanya maandalizi muhimu kwa ajili ya kuhamia mkoani humo

Bw. Makuka aliongeza kwamba walipanga michezo hiyo kuanza Octoba 14 ili kuadhimisha kumbukumbu muhimu ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere na kuenzi agizo lake la Serikali kuhamia Dodoma linalotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

“Michezo ya mwaka huu itaanza na ibada maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa na kumtakia afya njema Mhe. Rais Dkt. John Magufuli sanjari na kushiriki upandaji miti katika maeneo yatakayopendekezwa na Serikali ya mkoa”aliongezaBw. Makuka.

Michezo ya Shimiwi hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwaunganisha wafanyakazi wote na kuimarisha afya zao ili kuepuka maradhi ya mara kwa mara.

BENKI YA CRDB YAZINDUA KADI ya Kimataifa ya ‘TembocardVisa Infinite’

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), akimkabidhi Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kadi ya kimataifa ya ‘TembocardVisa Infinite’, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo uliokwenda sambamba na kituo cha kutolea huduma ‘Premier Club’ jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma "Premier Club" pamoja na Kadi ya Kimataifa ya TemboCardVisa Infinite uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza wakati wa uzinduzi wa TemboCard Visa Infinite pamoja na uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja Wakubwa cha Premier Club.
Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.

MSAADA WA MATIBABU KWA MGONJWA DANIEL MANOTA.

0
0
Daniel Manota ni mhitimu wa mafunzo ya ualimu Ilonga Tc mwaka 2015.anasumbuliwa na maradhi ya FIGO tangu mwezi wa 10/2015, kwa sasa yuko Muhimbili hospitali, hari yake inazidi kuwa mbaya kwa kukosa pesa za kununua dawa, hivyo kama ndugu, jamaa na rafiki unaombwa kumchangia ili aweze kununua dawa zake zinazogharimu kiasi cha sh.milion 1 kwa wiki.

 Tunaomba tumuunge mkono kijana mwenzetu ambaye anapata maumivu makali. 
MUNGU HUMBARIKI ATOAYE KWA MOYO WA UKUNJUFU.
Tuma mchango kupitia namba hii, tuunganishe nguvu zetu kwa lengo la kuokoa maisha yake.
hii.
0659656970. NEEMA URASA
076818874 .DANIEL MANOTA.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIWA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO.

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na wabunge kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6,2016. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwenye jengo la Utawala  la Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DAS BAGAMOYO AWATAKA WATENDAJI KUACHA NA TABIA YA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA RUSHWA

0
0
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

WATUMISHI wa umma Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani  wametkakiwa kuachana na vitendo vya kuwa na tamaa, ya kupokea rusha au kutoa kwa lengo la kuweza kuuza viwanja kiholela bila ya kuzingatia sheria na utaratibu kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha  kuwepo migogoro ya ardhi ya mara kwa mara kwa wananchi.   

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Erica Yegella kikao maalumu cha mafunzo ya kazi kilichoandaliwa  kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuweza kutimiza majukumu  yao ipasavyo wajumbe wa mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya kata zilizopo  katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Yegella alisema kwamba watendaji wa ngazi zote kwa kushirikiana na wajumbe wa mabaraza wanapaswa kuitambua vizuri sheria ya ardhi ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa  katika kutatua migogoro ambayo imedumu kwa kipindi cha muda mrefu  ikiwa sambamaba na kutenda haki bila ya kuwa na upendeleo wowote ili kuepukana na vurugu ambazo zinapelekea uvunjifu wa amani.

“Jamani nyinyi ni watendaji hivyo ni lazima kuhakikisha mnafanya kazi kwa misingi ambayo inatakiwa kitendo cha kuuza mashamba au vinnja ni kinyume kabisa na sheria, na kingine tuache tama kabisa ya kufanya mambo bila kuangalia madhara yake kwani baadhi ya maeneo migogoro ya ardhi inachangiwa na baaadhi yetu,”alisema Yegella.

Aidha alisema kwamba ana imani baada ya watendaji hao kupatiwa mafunzo hayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kutatua migogoro ya ardhi ambayo wakati mwingine inapelekea kuwepo kwa vurugu kutokana na kugombania viwanja.

 Naye Afisa kutoka tume ya maadili ya viongozi wa umma  kanda ya Mashariki Seleman Shaban amewataka watendaji nawatumishi wa umma kuhakikisha wanazingatia maadili na taraibu zote  za kazi zao ili kuepukana na suala la kutoa au kupokea rushwa kwani ni kinyume kabisa  na sheria za nchi.

Jerome Njiwa ni Mwenyekiti wa baraza la ardhi katika Wilaya ya Kibaha ambaye alihudhuria katika kikao hicho na hapa anafafanua zaidi kuhusina na migogoro mingi ambayo imekuwa ikijitokeza katika mabaraza ya ardhi ya kata na nyumba kutokana na kutozifahamu sheria vizuri.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya  kata  na nyumba warioshiriki katika mafunzo hayo  akiwemo Mwinyikondo Asia, Mariamu Swala pamoja na Hassan Ally wamesema kwamba walikuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi katika ufanya maamuzi kutokana na kutozijua vizuri sheria za ardhi.

Mafunzo hayo  ya kuwajengea uwezo wamewashirikisha wajumbe mbali mbali kutoka katika mabaraza ya ardhi ya kata  zilizopo  katika Wilaya ya Bagamoyo  Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kupunguza kero na migogoro ya aradhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara na kusababisha vurugu kwa wananchi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Erica Yegella akizungumza na wajumbe wa mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya kata hawapo pichani katika ufunguzi wa kikao kazi maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao katika kutatua migogoro ya ardhi kilichofanyika katika shule ya sekondari Lugoba.

NHC YAVAMIA WADAIWA SUGU UPANGA NA KUWATOLEA VYOMBO NJE

0
0
Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Mzizima Auction Mart wakitoa vyombo vya Winfrida Nkungu Mpangaji wa shirika la nyumba NHC nyumba namba 838 Mtaa wa Senegal Upanga jijini Dar es salaam kutokana na kudaiwagharama ya Pango miezi tisa kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tatu 2,300,000. Shirika la Numba la Taifa NHC liko kwenye kampeni kubwa ya kukusanya madeni yake maeneo mbalimbali nchini.
Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Mzizima Auction Mart wakikusanya nguo na vitu mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwenye nyumba hiyo.
Wakiewndelea kutoa vyombo nje.
Vyombo vikiwa nje baada ya kampuni hiyo kukamilisha kazi ya kutoa vyombo hivyo nje.
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images