Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

KIVUTIO CHA KIMONDO KUENDELA KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI

0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI inaendelea kutangaza Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya ikiwa ni kivutio muhimu na adimu nchini na duniani kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Kamani leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Vwawa  Mhe. Japhet Hasungu lililohusu mpango wa Serikali katika kuhamasisha watalii wa ndani na nje kuja kuangalia Kimondo hicho. 

Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali imekuwa inaendelea kuhamasisha kwa kukitangaza Kimondo hicho kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo vipindi vya runinga na nakala za machapisho mbalimbali.

“Uhamasishaji umefanyika kwa kutumia njia mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na vipindi vya runinga vya ZAMADAMU na Utalii wa ndani na kutumia machapisho ya Tanzania ya “The land of great Heritage Sites” na “Tanzania Cultural Heritage Resources” ambapo nakala zake husambazwa katika maonesho mbalimbali na Balozi zetu pamoja na jarida la “Ifahamu Idara ya mambo ya kale”” na jarida la Maliasili,” alifafanua Naibu Waziri huyo.

Aidha, Mhandisi Kamani aliongeza kuwa juhudi hizo limepelekea ongezeko la idadi ya watalii na mapato ambapo kati ya mwaka 2012/2013 na 2014/2015 watalii waliongezeka kutoka 990 hadi 1,681 pamoja na mapato kuongezeka kutoka shilingi 811,000 hadi 2,426,00.

Mbali na hayo, Mhandisi Kamani alitoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na wadau wengine kujitokeza kuboresha mazingira na miundombinu ya eneo la kimondo hicho ili kuweza kuzidi kuvutia watalii wengi na kuongeza pato la taifa.
Kimondo hicho kinaendelea kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia katika masuala ya utalii ambapo kinaaminiwa kuwa ni kati ya vimondo nane vikubwa zaidi duniani kinachokadiriwa kuwa na uzito wa tani 12, urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA MAKAZI YAKE MAPYA DODOMA

0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia  kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (kushoto)  wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kuhusu ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu, kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Badhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. Katikati ni mkewe Mary.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na masuala ya uchumi katika kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe mijini Dodoma aliyetaka kujua hali ya uchumi ilivyo kwa sasa hapa nchini.

Waziri Mkuu amesema kuwa lengo kuu la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha uchumi wa nchi unaongezeka kupitia nyanja tofauti kwa kushirikiana na taasisi za fedha zilizopo ili kufikia uchumi wa kati kama ilivyoanishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi Akizungumza kuhusu suala la midororo wa upokeaji wa mizigo katika bandari nchini, Waziri Mkuu amesema kuwa mdororo huo umetokana na kupungua kwa kiasi cha mizigo na kushuka kwa uchumi duniani.

Katika suala ya mauaji yaliyotokea Tanga, Mwanza na Vikindu, Waziri Mkuu amesema kuwa usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali ikiahidi kupambana vitendo vya mauaji kwa raia na askari katika maeneo mbali mbali nchini.

“Serikali imesikitika sana na jambo hili la mauaji hivyo itahakikisha wauaji hao wanawekwa katika mikono ya Sheria na kuongeza ulinzi kwa maeneo yote nchini kwa kuanzia ngazi ya vitongoji” alifafanua Waziri Mkuu.

Mbali na hayo Waziri Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuthibiti matukio hayo.

Kuhusu suala la uwepo wa tozo katika zao la korosho swali limeibuliwa na Mbunge wa viti maalumu Mhe.Riziki Lulida (CUF), Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia uondoaji wa Tozo zisizo na maana katika zao la korosho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania Bungeni na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) akimuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alimhakikishia kuwa Serikali ipo imara katika kusimamia ipasavyo uchumi wa nchi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akiwashukuru wabunge mara baada ya kumaliza kujibu maswali wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma.

AJALI MBAYA ENEO LA PALM BEACH JIJINI DAR LEO

0
0
 Salaam Ankal, 
Leo nimepita maeneo ya Palm Beach wakati nikitokea mjini muda wa SAA 12:15 asubuhi Nimeikuta gari hii aina ya Altezza au Subaru (maana haieleweki kutokana na ilivyoumia) likiwa halitamaniki, inaelezwa kuwa limegonga nguzo ya taa za barabarani. Haijafahamika kulikuwa na watu wangapi na hali zao zikoje mpaka sasa.

DC WA HANDENI GODWIN GONDWE ASULUHUSHA MGOGORO WA MPAKA ULIODUMU KWA MUDA MREFU

0
0
 Mkuu wa wilaya ya Handeni wa kwanzakushoto  akisoma ramani ya mwaka 2007 akiwa na  viongozi na wananchi ili kujua mpaka upo sehemu gani.DC Gondwe  amefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa mpaka uliodumu kwa muda mrefu akiwa ameambatana na Wakurugenzi wa halmashauri zote mbili uliohusisha Kijiji cha Kweditilibe cha Handeni vijijini na kitongoji cha makinda kilichopo Handeni Mji.

RAMANI YA 2007  ndiyo iliyotumika kusuluhisha mgogoro huo ambapo aliwaeleza wananchi kuwa ramani hiyo ndiyo iliyotumika kuweka mipaka ya maeneo husika Tanzania nzima na hakuna mwenye mamalaka ya kuibadili isipokua Raisi mwenye mamalaka ya Ardhi ya Tanzania nzima.
Mkuu wa wilaya Mh. Godwin Gondwe akisalimiana na mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Handeni kabla ya zoezi la kutatua mgogoro wa mpaka.

BENKI KUU YAIBUKA KIDEDEA

IGP KUKABIDHIWA UENYEKITI WA SARPCCO MKOANI ARUSHA

0
0
Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu anatarajia kukabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) katika mkutano unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Septemba, 2016 jijini Arusha. IGP Mangu atakabidhiwa uenyekiti huo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi ya Msumbiji ambapo atadumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa kamati tendaji za SARPCCO amabazo zitakutana Septemba 14 na 15 mwaka huu ili kuandaa ajenda na mapendekezo ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa wakuu wa Polisi ambao unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katika mkutano huo mambo mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu yatajadiliwa ikiwemo uhalifu wa kuvuka mipaka, pamoja na kuweka mikakati na maazimio ya kufanya Oparesheni za pamoja zinazojumuisha nchi zinazounda shirikisho hilo.

Vilevile, mkutano huo utajadili kwa kina utekelezaji wa maazimio mbalimbali kupitia kamati tendaji za wakurugenzi wa upelelezi, kamati tendaji ya sheria, kamati tendaji ya mafunzo na kamati tendaji ya mtandao wa Polisi wanawake.

Aidha, suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo litajadiliwa katika mkutano huo.

SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika katika kukabiliana na uhalifu. Mpaka hivi sasa umoja huo unaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Seychelles.

Imetolewa na:-
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA MKUTANO WA 17 WA DHARULA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha ndani kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa dharula wa wakuu wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa dharula wa wakuu wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya Bw. Liberat Mfumukeko muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa dharula wa wakuu wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016.


DKT REGINALD MENGI MGENI RASMI TASWE SACCOS

0
0
TASWE SACCOS INAZIDI KUKULETEA FURSA.

TASWE inapenda kuwakaribisha katika halfa ya chakula cha jioni tarehe 10/09/2016 saa 11 jioni ukumbi wa Cardinal Rugambwa. 

Madhumuni ni kusherehekea mafanikio yetu waalikwa zaidi ya 300 watakuwepo pamoja na Balozi mbalimbali, makampuni alikadhalika na banks. Mgeni rasmi katika shughuli hii ni Dr. Reginald Mengi. Meza za biashara zitakuwepo ili uweze kuonyesha na kuuza biashara yako na fursa nyingine kibao.

Tiketi zinapatikana kwenye ofisi  za TASWE zilizopo oysterbay au piga namba 0655 629 400
Wahi sasa jipatie tiketi yako!!!!!

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR LATOLEA UFAFANUZI TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO JUU YA KUKAMATWA WATU WANAOKUWA KWENYE NYUMBA ZA WAGENI

0
0

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani  kupuuza  taarifa za sauti  zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni. 


Taarifa hizo za uvumi  zinazoendelea kuzagaa  kwenye mitandao ya Kijamii kama WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba Askari Polisi wanawakamata watu  ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni  kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA NI KAZI TU’.

Kimsingi niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na oparesheni za kuwasaka watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba za kulala wageni kinyume cha sheria (guest bubu), majambazi na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

 Aidha taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa, hivyo Jeshi la Polisi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata wahalifu.
Niwajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, Hoteli, migahawa, Vilabu vya vileo,  kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria, hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa. Sheria ya Mwenendo ya makosa ya jinai kifungu cha 60(1) (sura ya 77 iliyofanyiwa marekebisho 2002) kinampa nguvu askari kufanya ukaguzi wa maeneo yote yaliyotajwa hapo juu na kumkamata mtu yeyote anayetiliwa shaka akienda kinyume na utaratibu wa biashara hizo. 

Sambamba na hayo nawatahadharisha wafanyabiashara wote wa nyumba za kulala wageni wafuate taratibu za kupokea wageni kwa kuandika kwenye vitabu, kuandika namba za vitambulisho vyao na sehemu wanayotoka, na pale watakapomtilia mashaka mteja yeyote watoe taarifa kituo chochote cha polisi. 

Pia wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wanawajibika kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki ili kuimarisha usalama katika jiji letu la  Dar Es salaam.

DAR ES SALAAM BILA UHALIFU INAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUISAFISHA JIJI LETU

S.N.SIRRO - CP
 KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

VIONGOZI NA WATUMISHI WA UMMA KUCHUKULIWA HATUA KALI IWAPO WATABAINIKA KUKIUKA TARATIBU ZA KAZI-MAMA SAMIA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nchi kuchunguza na kuwachukulia hatua kisheria na za kinidhamu viongozi na watumishi wa umma ambao wanakiuka taratibu za kazi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 8-Sep-2016 mjini Mtwara wakati anafungua jengo la sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini ambalo ujenzi wake umegharimu takribani shilingi bilioni MBILI.

Makamu wa Rais amesema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma hali ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni watendaji hao.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuiimarisha sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini kwa kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha kwa kadri hali ya uchumi itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Makamu wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kuthamini na wahakikishe walinda maslahi ya umma wakati wote wa utendaji wao wa kazi ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.

Makamu wa Rais amesema ni jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia mienendo ya viongozi wa umma na kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla hawaleta madhara kwa serikali na jamii kwa ujumla.

Makamu wa Rais pia ametoa rai maalum kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuitumia ofisi hiyo mpya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini kwa kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi wanaokiuka maadili ya umma katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki amesisitiza kuwa kazi ya kuhakiki mali na madeni ya viongozi wa umma itaendelea kwa kasi nchini na mwaka huu sekretarieti hiyo itahakiki mali za viongozi wapatao 500 kote nchini.

Naye Jaji Mstaafu na Kamishna wa Maadili Nchini Salome Kaganda akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo ameiomba serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kwa nchi nzima.

Imetolewa na 
Ofisi ya Makamu wa Rais 
Mtwara.
8-Sep-2016.

RC ARUSHA,MRISHO GAMBO ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UTUME –KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO - ARUSHA

0
0


Rais Magufuli, Viongozi wa dini hamasisheni wananchi walipe kodi.

Viongozi wa dini nchini wameombwa kuhamasisha waumini wao kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi ili kuongeza kasi ya kuleta maendeleo katika Taifa la Tanzania na pia wametakiwa kuhamasisha waumini wao kuhakikisha wanadai risiti kila wanapoenda kununua bidhaa au kupata huduma mbalimbali.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr John Joseph Pombe Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.

Akizungumza na waumini na viongozi wa Kanisa hilo lililopo Burka mjini hapa, Mkuu wa Mkoa Arusha Gambo alisema, Watanzania wanalojukumu la kufanya kazi kwani hata Vitabu vya Dini vimeelekeza kuwa mtu asiyefanya kazi na asile na mafundisho hayo ya dini yanaendana na falsafa ya hapa kazi tu.

Mhe. Gambo aliendelea kusisitiza kwamba kutokana na maelekezo hayo ya vitabu vya dini ni wazi kwamba kila mtu anatakiwa kufanya kazi kwa kadiri ya uwezo aliopewa na Muumba ili apate riziki hatua itakayowezesha pia kupunguza wategemezi katika Taifa letu.

Akizungumza katika maadhimisho hayo RC Gambo kwa niaba ya Rais Magufuli alisisitiza kuwa ni vyema kwa kila mmoja wetu kufanya kazi na kulipa Kodi.

"Kwa yule ambaye hatalipa Kodi ajue kwamba anaikosesha nchi yake mapato ambayo yangeweza kutumika kuendesha shughuli mbalimbali za maendeleo, pia tutambue kwamba huduma zote ni gharama na zinatokana na kodi tunazolipa. Hivyo katika Serikali ya Awamu ya Tano asiyefanya kazi na asile na zaidi ya hapo asiyelipa kodi ni vyema akafahamau kwamba analirudisha taifa lake nyuma. Niwaombeni sana viongozi wa Dini muhamasishe waumini walipe kodi kwa mustakabali wa Taifa letu"

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni Mch. Geofrey Mbwana akitoa somo fupi wakati wa maadhimisho hayo alisema amefurahishwa sana na uteuzi wa Mhe. Gambo na ana imani na vijana kwa sababu vijana wakati wao ni sasa na pia ni Taifa la leo hivyo wakipewa nafasi kama hii hudhihirisha vipawa vilivyomo ndani yao na bila shaka Mkoa wa Arusha utakua Mkoa kielelezo kwa Taifa hili.

Kanisa hili la Sabato katika Tanzania lilianzishwa Katika kijiji cha Giti kilichopo Mamba Miamba huko Same mnamo mwaka 1903 na kuendelea kukua katika Mji wa Shirati Mara na kisha kufika Arusha na kuanzisha Kanisa la Burka mwaka 1966 likiwa na Jengo moja dogo na waumini nane tu.

Hivi sasa Kanisa hili lina majimbo mawili na waumini zaidi ya 500,000 Tanzania. Kanisa hili pia wanamiliko Chuo Kikuu kimoja, Shule za Sekondari 17, Msingi 11 na shule za awali 11. Pia Kanisa hili lina Hospital moja, Kituo cha Afya kimoja na Zahanati 28.

RC Gambo aliendelea kuwaomba viongozi mbalimbali wa dini wazidi kumuombea na kumtia Moyo Mhe. Rais katika kazi yake ngumu na kubwa anayoifanya kwa maslahi ya Taifa haswa kusaidia wanyonge ambao kwa muda mrefu hawakuwa sehemu ya Agenda kubwa ya Serikali. Pia waendelee kuwasisitiza wanasiasa watambue kuwa wakati wa Siasa umekwisha ni vyema Mhe. Rais akapewa nafasi ya kuwatumikia watanzania kwa yale aliyoyaahidi kupitia utekelezaji wa ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI na watakutana tena kwenye siasa mwaka 2019 - 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(Katikati) akikata utepe kama ishara ya maadhimisho ya maiaka 50 ya Utume Burka,kushoto ni Mch. Mchungaji Eliasi Ijiko na kulia ni Askofu Godwin Godwin Lekundayo.Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwasilisha hotuba ya Mgeni Rasmi kwa viongozi wa kanisa na waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato. 
Katika picha ya pamoja ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(katikati) na viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Kutoka kulia ni Mchungaji Eliasi Ijiko akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo vitabu na majarida mbalimbali yanayochapishwa na Taasisi za kanisa la wasabato Tanzania 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(Kushoto) akiendelea kutembelea mabanda ya maonyesho katika maadhimsho ya miaka 50 ya Kanisa la Wasabato, burka. 



Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(Katikati) akiongozwa na vijana wakubwa wa Skauti kwenda kukagua mabanda ya Taasisi za kanisa la waadventista wa sabato Tanzania 

MASWALI NA MAJIBU KWA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA LEO SEPTEMBA 8, 2016

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO LA SEKRETARIETTI YA MAADILI YA UMMA KANDA YA KUSINI

0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
Jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kagandaakihutubia kwenye hafla hiyo
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akihutubia kwenye hafla hiyo.
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda mara baada ya kuwasili kwenye halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara

SERIKALI HAIJASHINDWA KUONGOZA NCHI-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo macho, haijalala na haijashindwa kuongoza nchi bali imejipanga kuliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa.

"Serikali haijashindwa kuongoza nchi. Nataka niwahakikishie waheshimiwa Wabunge na wananchi wote kwamba tutaongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa na kazi hiyo imeanza kwa marekebisho makubwa kwa maeneo ambayo tunadhani yatafanya Taifa hili liweze kupata mafanikio makubwa,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2016) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe, ambaye alitaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kunusuru mdororo wa uchumi uliopo nchini.

Bw. Mbowe alidai kwamba hali ya uchumi imeshuka na kwa mujibu wa taarifa za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) uagizaji wa bidhaa kutoka nje umepungua, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na sekta ya ujenzi imesimama hali inayoashiria kudorora kwa uchumi.

Kuhusu suala la kupungua kwa mizigo katika bandari na vituo vya forodha, Waziri Mkuu amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bahari umeshuka duniani kote kwa sababu ya kushuka kwa hali ya uchumi kutokana na kuporomoka kwa bei ya mafuta na gesi.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema tayari wafanyabiashara wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wameihakikishia Serikali kwamba mizigo yao yote itakuwa inapitia Bandari ya Dar es Salaam hasa kwa mkakati wa pamoja wa ujenzi wa reli ya standard gauge inayoanzia Dar es Salaam-Tabora - Isaka.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuimarisha amani na ulinzi kwenye maeneo yote nchini na kwamba vyombo vya dola viko macho. “Watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu yakiwemo mauaji watakamatwa popote walipo na kuchukuliwa hatua za kisheria,; amesema.

Amesema hatua hiyo inatokana na matukio ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni ambapo raia wasiokuwa na hatia na askari waliuawa katika maeneo ya Vikindu mkoani Pwani, Tanga na Mwanza. Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani

Katika swali lake, Bw. Ngonyani alitaka kujua ya Serikali kuhusu kukomesha mauaji hayo, yanayotokea kwa watu wasio na hatia pamoja na askari, ambapo Waziri Mkuu, alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi na familia, ambazo ndugu zao walipoteza maisha katika mauaji hayo.

Pia ametoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha wanawafichua watu ambao wanawatilia shaka na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili waweze kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA. JUMATANO, SEPTEMBA 8, 2016

PARTY CONTINUES THE LEGEND SPECIAL EDITION FEATURING GUEST DJ - DJ ASH FROM THE UK

Mbeya yaichapa Temeke bao 2-0 michuano ya Airtel Rising Stars.

0
0
 Mchezaji wa timu ya Temeke Ismail Kovu (no 4) akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Mbeya Pius Griton (no 15) wakati wa mashindano yanaoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Mbeya ilishinda 1-0. 
 Mchezaji wa timu ya Temeke Ismail Kovu (nyeupe) akitafuta jinsi ya kuwatoka mabeki wa timu ya Mbeya wakati wa mashindano yanaoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Mbeya ilishinda 1-0.
Beki wa timu ya  Temeke Ismail Kovu (nyeupe) akichuana na kiungo wa timu ya Mbeya Salum Luhinda wakati wa mashindano yanaoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Mbeya ilishinda 1-0.

Kinondoni yaipunguza kasi Arusha.
Timu ya Temeke ya wavulana imeshindwa kutamba mbele ya Mbeya baada ya kumkubali kichapo cha 2-0 kwenye mashindano yanayoendelea ya Airtel Rising Stars fainali za taifa zinazochezwa kwenye uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

Kwenye mechi ya kwanza ya michuano hiyo iliyochezwa leo, Jumatano 7 Septemba – timu ya wasichana ya Kinondoni iliifunga Arusha 4-0. Kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa jana Jumanne 6 Septemba, Arusha waliwafunga Lindi 2-0. Magoli ya Kinondoni yalifungwa na Anna Audela dakika ya 35 kwa njia ya penati. La pili likifungwa na Maimuna Abasi dakika 39, la tatu Aisha Juma dakika ya 41 na la nne likifungwa na Vaileth Tadeo dakika ya 60.

Kwenye mechi ya Mbeya na Temeke, timu ya Temeke ndio walianza na kasi baada ya kuwa wameshinda mchezo wa kwanza 4-1 dhidi ya Kinondoni, lakini mabeki wa Mbeya walisimama imara na kudhiti washambualiaji wa Temeke. Kwa dakika takribani 20 za kipindi cha kwanza, timu ya Temeke waliweza kuwadhiti vizuri Mbeya na hivyo kusababisha mpira kuchezwa nusu ya uwanja.

Hata hivyo, kadri muda ulivyokuwa unaenda, timu ya Mbeya iliweza kuanza mashambulizi taratibu na ilipofika dakika ya 45, Mbeya waliweza kuonana vizuri na kucheza pasi za uhakika ambapo Lameck Juma alitoa pasi nzuri kwa Ernest Kamange ambaye alimpiga beki wa Temeke na kuachia shuti lililomshindwa mlinda mlango wa Temeke na hivyo kuiandikia timu yake bao la kwanza. Timu zilienda mapumziko Mbeya ikiwa inaongeza 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Temeke wakitafuta bao la kuzawazisha. Hata hivyo kwenye dakika ya Ernest Kamange alifanyiwa madhambi kwenye nje kidogo na eneo la penati ambapo mwamuzi wa mchezo aliamuru ipingwe foul. Alikuwa na Lameck Juma ambaye alienda kucheza hiyo foul ambapo aliachia shuti lililoenda moja kwa moja hadi kimiani. Baada ya bao hilo, Temeke waliendeleza mashambulizi lakini yote yaliishia au kwa mabeki au kwa mlinda mlango ambaye alionyesha mpira wa kuvutiwa. Mpaka dakika ya 90 Temeke 0 Mbeya 2.

Fainali za Airtel Rising Stars 2016 zilifunguliwa jana Jumanne 6 Septemba na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mkuu huyo wa Ilala alitoa Shukrani kwa kampuni ya Airtel Tanzania kuweza kuwekeza kwenye soka la vijana. ‘ Nataka nitoe pongezi za dhati kwa wenzetu wa Airtel kwa kudhamini mashindano haya. Hii inasaidia vijana kuweza kujipatia ajira kwani kwa wale watakaofanya vizuri watachanguliwa kujiunga na timu yetu ya vijana ya Serengeti Boys pamoja na Twiga stars, alisema Mjema.  Aliongeza kuwa Wazazi wanatakiwa wawape watoto uhuru wa kuchangua fani zao na kusimamia bega kwa bega kuwaunga mkono.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema huu ni mwaka kwa Airtel kudhamini mashindano ya Airtel Rising Stars hapa nchini na kuhaidi kuendeleza udhamini huo.

SIKU YA KUSOMA DUNIANI: ROOM TO READ WADHAMIRIA KUONDOA UJINGA KWA VITENDO

0
0
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Room to Read, Peter Mwakabwale akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea siku ya kusoma dunia ambapo kilele chake ni Kesho Septemba 9.
Hapa kila mmoja anaelewa anacho kisoma hii ni kutokana na kuwa na walimu ambao wamewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo wamekuwa wanaweza kusoma na kuandika vizuri.

ZANTEL WATOA MBUZI 100 KWAAJILI YA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA VILIVYO CHINI YA BAKWATA JIJINI DAR ES LEO.

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akikabidhi Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzani, Sheihk Ally Ngeruko Mbuzi 100 kwajiili ya vituo vya  kulelea watoto yatima vilivyo chini ya BAKWATA vya jijini Dar es Salaam.

 Msaada huo umekabidhiwa kwaajili ya sikukuu ya Kuchinja ya Idd el –Adha ambayo ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza mara baada ya kukabidhi Mbuzi kwa mwakilishi wa Mufti wa Tanzania ili aweze kugawa kwenye vituo vilivyo chini ya BAKWATA hapa nchini.
Amesema Zantel wameona sikukuu hiyo ya Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.

Mbuzi 400 watatolewa kwa wateja wa Zantel wenye matumizi zaidi kuliko wengine na ambao watakuwa wamejisajili katika kampeni kwa kupitia *149*15# na kuchagua  “Jibwage na Mbuzi”. Kujisajili katika promosheni hii ni bure kwa wateja wote wa Zantel. Kila siku wateja 40 watakaokuwa wametumia muda zaidi watajizawadia mbuzi.

“Hii si bahati nasibu, wale wateja wa juu watakaokuwa wametumia dakika nyingi bila kuchezeshwa mchezo wa bahati watakuwa wamejizawadia moja kwa moja hivyo natumia fursa hii kuwahamasisha wateja wetu kujisajili ili kupata mbuzi na kusambaza furaha ya Eid katika familia zao” amesema  Benoit

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YAWAMFANO WA KUIGWA KWA KUENDESHA UCHAGUZI WA HURU NA HAKI.

0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Msaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada walipotoka kwenye mkutano wa 18 wa Tume za Uchaguzi katika nchi zilizo Kusini Mwa Jangwa la Sahara (SADC), uliofanyika Mjini Gaborone-Botswana. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Clerence Nanyaro.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ni moja ya Tume kati ya tume za Afrika ambayo imekuwa mfano wa kuifwa katika uchaguzi kutokana kila unapofanyika uchaguzi umekuwa wa huru na haki.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuonekana kwa tume hiyo ni katika mkutano wa 18 wa Tume za Uchaguzi katika nchi zilizo Kusini Mwa Jangwa la Sahara (SADC), uliofanyika Mjini Gaborone-Botswana,  amesema katika mkutano huo Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika usimamizi wa uchaguzi na kufanya nchi zingine zifanye mfumo huo.

Lubuva amesema kuwa Tume za Uchaguzi katika nchi za SADC zimekuwa zikifanya kwa kutumia vitambulisho vya taifa tofauti na Tanzania kutumia kitambulisho cha mpiga kura lakini uandikishaji wa muda mfupi.

Amesema kuwa Tanzania ziliwakilishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kwa pamoja zimeonekana kuendesha uchaguzi wa haki na amani.

Aidha amesema kuwa katika mkutano huo nchi za Afrika  zimeonekana kila uchaguzi ukiisha walioshindwa huwa hawakubali matokeo katika chaguzi mbalimbali.

Lubuva amesema kuwa vitambulisho vya taifa vikikamilika kwa kila mtanzania kuwa na kitambulisho kuangalia namna ya kutumia katika chaguzi zijazo.

Hata hivyo amesema mkutano huo Tanzania kupitia NEC zimeweza kujifunza baadhi ya vitu katika uendeshaji wa uchaguzi na wataendelea kufanyia kazi katika kuboresha chaguzi zijazo.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images