Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1340 | 1341 | (Page 1342) | 1343 | 1344 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakiwa wamekusanyika kwenye eneo linakotarajiwa kutokea tukio adhimu la kupatwa kwa Jua tayari kwa kushuhudia tukio hilo, ambalo litaonekana vizuri kwenye eneo hilo lililopo Rujewa, Mbalali Mkoani Mbeya kuda wowote kutokea sasa.  Globu ya Jamii imeweka kambi katika eneo hilo, na itakuletea kila kilichojiri huko kupitia hapa hapa Libenekeni. hivyo usicheze mbali.
  Watu wakiwa tayari tayari kushuhudia tukio hilo.
  Mabanda ya Makampuni mbalimbali ya Utalii yakiwa tayari kutoa huduma hiyo.
  Kina mama ntilie nao hawachezi mbali na eneo la tukio, kwani watu wengi huitaji huduma yao.

  0 0

  Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia  wakazi wa jiji la Dar-es-salaam na  Mji wa Kibaha mkoan Pwani kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa wastani wa Saa 14, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 05:00 usiku, siku ya Ijumaa tarehe 02/09/2016.

  Sababu ya kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Juu ni kuruhusu usafishaji wa bomba jipya na kufanya majaribio ya sehemu ya mtambo mpya wa Maji wa Ruvu Juu, Zoezi hili linaashiria hatua za mwisho za upanuzi wa mtambo huo, ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu.

  Kuzimwa Kwa mtambo wa Ruvu Juu kutapelekea maeneo yafuatayo kukosa Maji:

  MLANDIZI MJINI, RUVU DARAJANI, VIKURUTI, DISUNYARA, KILANGALANGA, JANGA, MBAGALA, VISIGA, MAILI 35, ZOGOWALE, MISUGUSUGU, TANITA, KIBONDENI, KWA MATHIAS, NYUMBU, MSANGANI, KWA MBONDE, PICHA YA NDEGE, SOFU, LULINZI, GOGONI, KIBAMBA, KIBAMBA NJIA PANDA SHULE KIBWEGERE, MLOGANZIRA, KWEMBE, KIBAMBA HOSPITALI, KWA MKINGA, NA LUGURUNI.
  WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA

  DAWASCO INAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

  Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE).
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA UHUSIANO
  DAWASCO-MAKAO MAKUU


  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amesema kuwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Rais aliyesubiriwa kwa muda mrefu tangu kuanza kwa Uhuru.

  Cheyo ameyasema hayo jana alipokuwa akielezea juu ya utendaji wa Rais Magufuli tangu ameingia madarakani Novemba, 2015.

  “Utendaji wa Rais Magufuli umewashtusha watu wengi kwani hawakutegemea kwa muda mfupi aliokuwa madarakani kama angeweza kuchukua hatua kubwa kama vile kupambana na mafisadi, jambo ambalo limekuwa likiongelewa na viongozi waliopita lakini kulikuwa hakuna matunda ya moja kwa moja,” alifafanua Cheyo. 

  Ameendelea kwa kusema kuwa Rais Magufuli amekuwa na adhima ya kupambana na Mafisadi na kutatua kero za Taifa tangu akiwa kwenye kampeni huku akisimamia kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

  Vile vile Cheyo amesema kuwa kero ambazo amekuwa akizitatua Rais Magufuli zikiwemo ufisadi, uchumi tegemezi, mapato madogo na ukosefu wa vifaa mahospitalini ni kero ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na kambi ya upinzani kwa muda mrefu.

  Hivyo kuingia kwa Rais Magufuli madarakani kumeleta utatuzi mkubwa kwa kero hizo ambazo zimekosa utatuzi kwa muda mrefu kutokana na viongozi waliopita kutozichukulia uzito mfano Rais Magufuli alivyoweza kutatua tatizo la vitanda hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kipindi kifupi ambapo hivi sasa hakuna mgonjwa anayelala nchini katika hospitali hiyo. 

  Akielezea suala la ufisadi nchini, Cheyo amesema kuwa ufisadi ni ugonjwa wa muda mrefu ambao umepoteza fedha nyingi za nchi kutokana na mikataba mibovu iliyokuwa ikisainiwa na viongozi wa juu. 

  Aidha amempongeza Mhe. Rais kwa kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na kuona tatizo hilo lishughulikiwe kisheria na kwa njia maalum ili kukomesha ufisadi nchini.

  Cheyo amewataka watanzania kugeuza mawazo yao na kuchukia rushwa kwa kukataa kupokea na kutoa rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na inarudisha nyuma maendeleo ya nchi. 

  0 0


  0 0  0 0

   Jua jinsi linavyoonekana kwa kutumia karatasi maalumu ambayo unaweza kuona jua katika madhari mbalimbali.
   Kikundi cha ngoma wakitumbuiza katika eneo ambapo kupatwa kwa jua kumetokea na kuonekana kwa kutumia kifaa maalumu Rujewa Mkoani Mbeya.
  Biashara zikiendela katika eneo la Rujewa Mkoani Mbeya kama ijulikanavyo Mkoa wa Mbeya kwa Kulima Mpunga hapo biashara ya Mchele ikiendelea.
  Mamalishe nao hawakusita kuona fursa iliyojitokeza katika eneo Rujewa Mkoani Mbeya kuhudumia wananchi wanaoenda kutazama kupatwa kwa jua.
  Mwananchi akijiandaa kuanalia jua kwa kutumia karatasi maalumu.
  Picha na Fadhili Atick na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Kanali Mstaafu Chiku Galawa pamoja na Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) , Pascal Shelutete wakiangalia tukio la kupatwa kwa Jua kutumia vifaa maalum muda huu, katika eneo la Mpunga Relini, Mbarali mkoani Mbeya. Tukio hilo limeonekana vizuri zaidi katika eneo hilo kuliko maeneo mengine nchini. Watu kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia wako katika eneo hilo, kushuhudia kwa uzuri tukio la kupatwa kwa Jua.
  Hivi ndivyo jua lilivyoanza kuonekana baada ya kupatwa, Hapo ni eneo la Mpunga Relini, Mbarali mkoani Mbeya, eneo lililotengwa kwa ajili ya kutizamia tukio hilo kwa uzuri zaidi.
  Na hata kina sie huku Mjini Dar es salaam tumelishuhudia tukio, japo tulitandwa na wingu zito. ila si haba tumebadatika kuiona kwa namna hii.

  0 0

  Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali umemalizika katika mjini Mbabane Swaziland ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi muhimu na nyeti ya Siasa, Ulinzi na USalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC- (SADC Organ On Politisc, Defence and Security Cooperation) ambapo nchi ya Angola imeteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa asasi hiyo.


  Jukumu kubwa la asasi hiyo litakuwa ni kuangalia masuala yote yanahusiana na Siasa, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC huku changamoto kubwa ikiwa ni namna ya kutafuta suluhu ya kudumu hususani katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Lesotho.

  Akizungumzia mambo muhimu yaliyojiri kwenye Mkutano huo wa 36 wa SADC mjini Mbabane - Swaziland, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia  Suluhu Hassan ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa na amehimiza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa nchi wanachama wa SADC kwa sasa zinatakiwa kuongeza juhudi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi haraka kama hatua ya kujenga ustawi bora wa wananchi wa kanda hiyo.

  Kuhusu Mpango wa Mfalme wa Swaziland wa III wa kujenga Chuo Kikuu cha SADC nchini mwake kabla ya mkutano ujao wa SADC hapo mwakani chuo ambacho kwa kuanzia kitatoa ufadhili wa masomo ya Sayansi,Ugunduzi na Utafiti kwa wanafunzi wanaotoka kwenye nchi wanachama wa SADC, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema mpango huo ni mzuri na utasaidia kutoa wataalamu wengi hasa wanasayansi katika ukanda wa SADC na serikali ya Tanzania inaunga mkono mkakati huo.

  Kuhusu Tanzania kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa nchi za SADC, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga amesema Tanzania itahudumu katika asasi hiyo kwa mwaka MMOJA na anaimani kuwa changamoto za kisiasa zilizopo katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Lesotho zipatiwa ufumbuzi.

  Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC pia umeiteua nchi ya Swaziland kuwa mwenyekiti wa SADC na Jamhuri ya Afrika Kusini imeteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC.

  Katika mkutano huo wakuu wa nchi na serikali wametia saini rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali ya jumuiya hiyo ikiwemo mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Mbabane
  Swaziland
  1-Sep-16

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akikagua paredi ya vijana 1140 wa operesheni Magufuli kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha 825 KJ kilichopo Mtabila katika Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma.

  Na Abel Daud, Globu ya Jamii, Kigoma

  Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya operesheni Magufuli (kwa mujibu wa sheria) kutoka wilayani hapo kwenda kutekeleza falsafa ya hapa kazi tu.

  Hayo ameyasema alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana 1140 operesheni Magufuli kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha 825 KJ kilichopo Mtabila katika Wilaya ya Kasulu na kuwataka kwenda kuungana na watanzania wengine wote katika kuiamini kuitekeleza na kuiishi falsafa ya hapa kazi tu kwa vitendo.

  Akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi, Mkuu wa kambi ya 825 KJ, Meja George Kazaula amesema kikosi kimefanikiwa kutengeneza madawati 1074 ikiwa ni agizo la Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli.

  Pia ameelezea changamoto zinazoikabili kambi hiyo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa umeme wa gridi ya taifa pamoja na miundombinu ya barabara kuwa mibovu hali inayopelekea matumizi makubwa ya uendeshaji wa umeme wa genereta pamoja na matengenezo ya mara kwa mara ya magari ya kikosi.

  Nae mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa hapa nchini Luten col. Philipo Mahende amewataka vijana hao kuwa wazalendo wa kweli ambao watakuwa tayari kulilinda taifa kwa gharama yoyote ile ili amani,umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania unakuwa endelevu, na kuwaomba kujiepusha na kutokuwa miongoni mwa watanzania wachache wanaoshabikia mgawanyiko miongoni mwetu kwa misingi ya itikadi za kisiasa,kidini au mahali anapotoka mtu.

  Akisoma lisara kwa mgeni rasmi mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ameiomba serikali kuiongeza bajeti Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa ili vijana wengi wapate nafasi kujiunga na mafunzo ya JKT ili waweze kujifunza uzalendo na shughuli za uzalishaji mali ili kuwatengenezea uwezo wa kujiajiri wenyewe pasipo kuitegemea Serikali.
  Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akitoa zawadi kwa baadhi ya vijana waliofanya vizuri katika mafunzo hayo
  Vijana hao Wakipita kwa mwendo wa haraka.
  Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akipokea heshema ya kijeshi kutoka kwa vijana wanaohitimu.


  0 0  0 0

  Meza Kuu,Pichani tatu kushoto ni Rais Dkt John Pombe Magufuli akishiriki kama Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 14 ya Wahandisi,yaliyofanyika leo Mlimani City,jijini Dar,

  Baadhi ya Wahandisi wakiwa kwenye maadhimisho ya 14 ya siku ya Wahandisi, kwenye ukumbi wa MlimaniCity jijini Dar es Salaam asubuhi hii.Rais John Pombe Magufulindiye mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayoambao kauli mbiu yake ni "Kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda"  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli Mkutano akisalimiana na  Maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye maonesho yanayoenda sambamba na  Mkuu wa 14 wa Wahandisi unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kitengo cha mauzo (katikati) wakiwahudumia wateja kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao. Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kitengo cha mauzo (katikati) wakiwahudumia wateja kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao. Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.  Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.Baadhi ya wakandarasi wakitembelea mabanda anuai kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao. Baadhi ya wakandarasi wakitembelea mabanda anuai kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi ambapo mbali na mkutano huo kampuni kadhaa ikiwemo TTCL zilipata fursa ya kuonesha baadhi ya bidhaa zao.Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.  Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wateja juu ya bidhaa za TTCL kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo. Kampuni ya TTCL imepeleka bidhaa zao na huduma kuwaonesha wakandarasi.

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Septemba, 2016 amemuapisha Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Bw. Doto M. James aliteuliwa kushika wadhifa huo jana tarehe 31 Agosti, 2016 na amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Servacius Likwelile ambaye atapangiwa kazi nyingine.
  Kabla ya uteuzi huo, Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).
  Hafla ya kuapishwa kwa Bw. Doto M. James imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
  Aidha, Bw. Doto M. James amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma, zoezi ambalo limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.

   Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es salaam
  01 Septemba, 2016 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Doto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango Doto James mara baada ya kuapishwa.PICHA NA IKULU

  0 0

  Maelfu ya Watu kotoka Sehemu Mbalimbali Duniani walijitokeza kwa wingi kushuhudia tukio kubwa la Kihistoria Duniani la kupatwa kwa Jua lililo onekana vyema katika Eneo la Rujewa Relini Wilayani Mbalari Mkoani Mbeya ni Mara baada ya Miaka Mingi tukio hili kutokea Duniani, wengi wafarijika kushuhudia tukio hilo la Kihistoria la kupatwa kwa Jua.
  Baadhi ya Wanasayansi kutoka nje ya Nchi ya Tanzania wakipata Taswira ya tukio hilo la kupatwa kwa Jua tukio lililo onekana vyema Eneo la Rujewa Mbalari Mkoani Mbeya.
  Taswira ya Muonekano wa Jua likipatwa.
  Mkuu wa mkoa wa mbeya kulia Mh.Amos Makalla akizungumza jambo na Mdau Kutoka Katika Eneo la Tukio Rujewa Mbalari Mkoani Mbeya.

  Mitambo Ikiwekwa sawa.
  PICHA ZOTE NA MR.PENGO WA MMG RUJEWA.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Septemba 1, 2016
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Septemba 1, 2016
    Wahandisi wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Septemba 1, 2016. Picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  Kamanda wa mkoa wa Njombe wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkaguzi Joseph Mwasabeja akitoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Njombe. (PICHA ZOTE NA FC GODFREY PETER)

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa ameambatana na viongozi waandamizi wa Jeshi hilo wakikagua moja ya kisima (Fire Hydrant) kinachoweza kutoa msaada wa maji katika matukio pindi magari ya zimamoto yanapoishiwa maji.


  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa ameambatana na viongozi waandamizi wa Jeshi hilo wakikagua moja ya kisima (Fire Hydrant) kinachoweza kutoa msaada wa maji katika matukio pindi magari ya zimamoto yanapoishiwa maji.
  Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionyesha jinsi ya uzimaji moto na kiasi cha maji yanayotumika (Pressure) wakati wa matukio.

  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na kufanya kazi chini ya sheria namba 14 ya mwaka 2007 “FIRE AND RESCUE FORCE ACT”. Majukumu makubwa ya Jeshi ni kuzima moto na  kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengineyo.
  HUDUMA YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI INATOLEWA.
  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii. Hivyo basi mtu yeyote anastahili kupata huduma hiyo kwa kupiga namba ya simu 114. Pia kuna huduma nyingine zitolewazo na Idara.
  HUDUMA ZITOLEWAZO NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.
  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linajukumu kubwa la kutoa huduma kwa jamii katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Kuokoa maisha ya watu na mali zao, Kuzima moto, Kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga moto, Kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya  moto, Kusoma ramani za majengo na kutoa ushauri, Kutoa huduma ya kwanza katika majanga na ajali barabarani, Kutoa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto, Kufanya uchunguzi kwenye majanga ya moto na Kutoa huduma za kibinadamu.
  KUFIKA KWENYE TUKIO BILA YA VITENDEA KAZI (MAJI)
  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wote huwa limejiandaa kwa magari yake kuwa na vitendea kazi vya kuzimia moto na kufanyia maokozi pia magari huwa yamejazwa maji wakati wote yanapokuwa vituoni yakisubiri matukio. Changamoto iliyopo ni wananchi wengi kuwa na dhana kuwa magari ya Zimamoto huenda kwenye matukio bila maji.
  AINA YA GARI LA ZIMAMOTO, VIFAA, UWEZO WA KUBEBA MAJI (UJAZO), NA JINSI YA UFANYAJI KAZI   
  Gari la Zimamoto linapofika kwenye tukio hufanya kazi kama mtambo wa kuzimamoto, magari hayo yanamatanki ya maji yenye ujazo kuanzia lita 1,500 hadi lita 7,000 (kuna moja linabeba lita 16,000) ili maji hayo yatoke kwa nguvu na kuweza kuzimamoto, magari ya Zimamoto yamefungwa pampu zenye uwezo wakusukuma lita 2,000 hadi lita 6,000 kwa dakika.
  Kwa kawaida tunapofika kwenye tukio hutumia mipira yenye kipenyo cha milimeta 70  na kufunga kifaa cha kumwagia maji (branch pipe) chenye kipenyo cha milimeta 20 na pampu husukuma maji kwa nguvu ya  bar 7, kwa vipimo hivyo huwa tunamwaga lita 1,000 kwa dakika kwa njia moja ya kutolea maji hivyo kwa gari lililobeba lita 7,000 maji yatakwisha ndani ya dakika saba, kwa kawaida tunatumia njia mbili za kutolea maji hivyo huwa tunamwaga lita 2,000 kwa dakika, na gari lililobeba lita 7,000 maji yatakwisha baada ya dakika 3½ nasisi hulazimika kuondoka eneo la tukio kwenda kutafuta maji.
  Huku nyuma wanaweza kuja waandishi wa habari na kuwauliza wananchi mbona moto unawakana Zimamoto hawapo? Wananchi hujibu kuwa wamekuja lakini baada ya muda mfupi wameondoka na kusema kuwa wanakwenda kuchukua maji,  hapo ndipo dhana ya Zimamoto wamekuja kuangalia  kwanza ukubwa wa moto na sasa ndio wamekwenda kuchukua maji hujengeka. Ki uhalisia si kweli kuwa magari ya Zimamoto hufika kwenye tukio bila ya maji.
  Maji yanayobebwa na magari ya Zimamoto husaidia kuanzia kazi, kabla maji ya kwenye gari kwisha gari la Zimamoto hutegemea kupata maji kutoka kwenye vituo maalum vya maji kwa ajili ya Zimamoto (Fire Hydrants) ambazo katika miji yetu mingi huwa hazifanyi kazi kutokana na sababu zifuatazo:-
  1. Kutokuwa na maji
  2. Kufukiwa na vifusi au mchanga au kufunikwa kutokana na ukarabati wa mitaa au barabara.
  3. Kung’olewa na kubadilishwa matumizi.
  4. Kung’olewa kwa alama za utambulisho (H sign)
  5. Kuibiwa kwa mifuniko kutokana na biashara ya chuma cha kavu.
  6. Miradi mingi ya maji katika miji kutoshirikisha ufungwaji wa vituo vya maji (Fire Hydrants).

  0 0
 • 09/01/16--20:00: IN LOVING MEMORY
 • THE LATE MAMA JOYCELINE MKAMSURI SAWAYA MAWALLA MAREALLE

  31 st DECEMBER 1940 - 2 ND SEPTEMBER 2010

  You were a wonderful woman, a caring mother to your children, a mother- inlaw who never stopped supportive and most of all a grandmother we will always keep in memory. Things have not been and will never be the same now that you are no not with us. Even though it has been 6 years since you left, we still miss your presence amongst us.

  We are looking forward to meeting you again. You will always be loved by your children: Emmy Marealle and Leonard Marealle, Daughter- inlaw: Caroline Marealle, granddaughters: Vanessa Benne, Joyceline Marealle and Eve Marealle and the rest of Sawaya, Mawalla & Marealle family.

  0 0


   Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata picha ya  pamoja na Wanajeshi wa JWTZ Kikosi cha Anga 603 KJ Majumba Sita Ukonga jijini Dar es salaam  alikotembelea kuwapongeza kwa kusherehekea miaka 52 ya Jeshi la Wananchi leo Septemba 1, 2016


  Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwaunga mkono na kuwatumia wahandisi wa ndani wenye ujuzi mbalimbali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, reli, barabara na miundombinu mingine.
  Hayo yamesema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, alipokuwa akifungua Mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 01 Septemba, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
  Dkt. Magufuli amesema atafurahi kuona miradi inayohusisha kazi za kihandisi na hasa wakati huu ambapo nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda inatekelezwa kwa kutumia wahandisi wa ndani na hivyo amewataka kujipanga sawasawa ili kukabiliana na changamoto hiyo.

  "Nyinyi wahandisi mkiamua nchi hii iende kwenye uchumi wa kati tutafika, mkiamua nchi hii iende kwenye uchumi wa viwanda tutafika, na msipoamua hatutafika. 
  "Sasa hivi kuna ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) kwani nyinyi mnashindwa kujenga?" Amehoji Rais Magufuli huku akisisitiza kuwa Serikali yake ipo tayari kuwaunga mkono pale watakapohitaji msaada.
  Hata hivyo Dkt. Magufuli amewakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa ubora, ushirikiano na upendo miongoni mwao huku akielezea kusikitishwa kwake na baadhi ya wahandisi ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo kushirikiana na wakandarasi na wazabuni kuzidisha viwango vya makadirio ya gharama za miradi na manunuzi ya Serikali ili kujipatia fedha isivyo halali na kupitisha miradi iliyojenga chini ya viwango.
  Rais Magufuli ameongeza kuwa Serikali yake itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wote wanaotumia vibaya fedha za umma na amesisitiza kuwa hatua zaidi za kuhakikisha kunakuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha za Serikali zitachukuliwa.
  "Kuna watu wanasema mzunguko wa pesa umepungua na hali imekuwa ngumu, hizo pesa zilizokuwa zinachezewa huko mitaani zilikuwa pesa za Serikali, mimi nataka pesa ziende kwenye miradi ya maendeleo na ndio maana bajeti ya maendeleo tumeongeza kutoka asilimia 26 hadi asilimia 40" Amesisitiza Rais Magufuli.
  Katika tukio jingine, Rais Magufuli amewatembelea Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 603 (Air Wing) kilichopo Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuwapongeza kwa kuadhimisha miaka 52 ya tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo. 
  Katika kuadhimisha miaka 52 ya JWTZ Askari wa Jeshi hilo wamefanya usafi katika maeneo mbalimbali.
  Pamoja na pongezi hizo Rais Magufuli amekagua baadhi ya ndege zinazotumiwa na Jeshi hilo na amewahakikishia Wanajeshi kuwa Serikali yake itaendelea kuliimarisha Jeshi hilo kwa vifaa na maslai ya Askari ili kuendelea kuwa na Jeshi bora, la kisasa na lililo tayari kuilinda nchi wakati wote. 
  Gerson Msigwa 
  Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU 
  Dar es Salaam 
  01 Septemba, 2016

  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
  0 0


older | 1 | .... | 1340 | 1341 | (Page 1342) | 1343 | 1344 | .... | 3285 | newer