Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1341 | 1342 | (Page 1343) | 1344 | 1345 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mnyama Faru anakiakisi Jina la Kiingereza Rhinoceros ama FARU na sio KIFARU kama wengine waitavyo. Asili ya Jina hili la kiingereza limetoholewa kwenye lugha ya Kiyunani/Greece lina mashina mawili Rhino (Pua) na Ceros (Pembe) 

  Faru ni miongoni mwa wanyama ambao ni BIG FIVE kwa Africa, wengine ni chui, simba, mbogo na tembo. Kuna takribani aina tano za faru duniani na Africa tuna aina mbili za faru ambazo ni WHITE RHINO na BLACK RHINO na aina nyingine tatu zilizobaki zinapatikana barani Asia, na kwa Tanzania sisi tuna aina moja tu ya Faru ambayo ni Black Rhino ingawa pia kuna White Rhino wanaopatikana Mkomazi ambayo ni introduced species waliochukuliwa kutoka South Africa. 
  Faru 'mweupe' ni mamalia wa pili kwa ukubwa baada ya Tembo, huku kukiwa na spishi mbili za faru wapatikanao barani Afrika ambazo ni faru mweupe na faru mweusi. Utofauti wa faru hawa ni kwenye namna ya midomo yao ilivyo kaa na sio rangi kama wengi wananyodhani. Faru wa Afrika na Sumatra (ambao ndio wadogo lakini wakali sana) wana pembe mbili huku wale wa Uhindi na Java wakiwa na pembe moja tu. 

   Kwa kawaida faru ni wanyama ambayo huishi maisha ya mmoja mmoja (Solitary ) na dume na jike hukutana tu katika msimu wao wa ujamianaji ambapo kipindi hicho hutafutana kwa njia ya harufu ambayo hutolewa na jike pale anapokuwa anamuhitaji dume. 
  Kwa bahati mbaya hivi sasa wanyama hao wamekuwa wakipungua kutokana na ongezeko la ujangili uliokithiri barani Afrika. Pembe ya Faru inasadikika kutumika kama tiba ya magongwa mbalimbali hasa Bara la Asia ambako kwa Data za karibuni wamebaki 2700 tu.....Maadui wakubwa wa faru ni BINADAMU MAJANGILI na Simba ambao huwinda watoto wao kwa ajili ya kitoweo.  Kutoweka kwa Faru kumewafanya wawekewe ulinzi wa masaa 24 na askari wa wanyama pori (Park rangers ) 

  Pembe hizo zimetengenezwa kwa keratini, protini, sawa na ile inayopatikana kwenye nywele na kucha. 

  Yasemekana pia kwamba pembe hizi hutumika kutengenezea sime/dagger pamoja na dawa maarufu ambayo hutumiwa  kuleta heshima nyumbani (VIAGRA) wakafikiri kuwa nguvu zake zinatoka kwenye hiyo PEMBE kutokana na kutumia zaidi ya dakika 40 wakati wa kujamiana, kitu ambacho kimethibitishwa na wanasayansi kwamba si kweli. Kwa nchi za Kiarabau hususan Yemen,  mwanaume huonekana tajiri na mwenye hadhi pale anapokuwa anamiliki sime iliyotengenezwa kwa maligafi ya Faru.

  Mwaka 2012 pembe ya Faru ilikuwa ikiuzwa dola 60,000 kwa kilo (Takribani milioni 130 za madafu)  kwenye soko la Dunia. 

  Faru wana uwezo mkubwa wa kusikia na kunusa, lakini uoni wao si mzuri sana........Pia Hawana kumbukumbu imara kama Tembo hivyo hawezi kulipiza kisasi.

  Anabeba ujauzito wake kwa kipindi cha miezi 18 na huwa anazaa mtoto mmoja ( Mapacha huwa ni nadra). Faru pia ni miongoni mwa wanyama wakubwa wanaopatikana nchi kavu ambapo anaweza kufikia hadi uzito wa 2000-2300KG kwa white rhino na 800-1500KG kwa black rhino. 

  Na tofauti kati ya Black rhino na White rhino ni kuwa ana mdomo mweusi uliochongoka ambao unamwezesha kula majani ya juu katika matawi ya mti (Browser) na white rhino yeye anakuwa na mdomo mpana mweupe kwa ndani ambao unamwezesha kula nyasi (Grazers), tofauti nyingine ni kwamba White rhino akiwa na mtoto huwa anatabia ya kumtanguliza mtoto mbele Kama wafanyavyo wamama wa kizungu ambao humbeba mtoto kwa mbele na kwa upande wa Black rhino yeye huwa mtoto anakaa nyuma ya mama kama wafanyavyo wamama wa kiafrica ambao huwabeba watoto wao mgongoni.
   Faru wote wana rangi ya kijivu (Grey colour ) ingawa wakati mwingine huweza kubadilika kutokana na tabia ya kufanya wallowing ( kujiwekea vumbi na matope ili kupunguza joto katika miili yao kwa sababu hawa ni hairless mammals wanyama ambao hawana nywele ) ndio maana wakati mwingine unaweza kuta rangi zao kama zina utofauti fulani.

  Kwa hapa Tanzania sehemu nzuri ya kuwaona hawa FARU ni NGORONGORO CRATER. Ni raha sana kumtazama Faru japo ana sura ya kuogofya. 

  Ni vyema tu kukumbushana kwamba si rahisi sana kuthamini hazina uliyonayo hadi inapotoweka, ikiwa wengi tulitumia simu zetu kuchukua tukioa la kupatwa kwa jua, habari gani kama utatembelea mbuga ukapiga picha wanyama kwa simu YAKO (Kanuni ya mbugani unatakiwa kuchukua PICHA tu na unatakiw kuacha nyayo tu......TAKE ONLY PHOTOS AND LEAVE ONLY FOOTPRINT......)

  ZITAFIKA NYAKATI WANYAMA KAMA HAWA TUTAWAONA AMA KUWASIMULIA KWA PICHA TU .........................yuko mtalii nilikutana naye akaniambia ni mara ya NNE anakuja kuona FARU tuuuuuuu

  ​By Geofrey Chambua toka vyanzo mbalimbali 

  0 0

  Naibu Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jafo akihutubia wadau wa kampeni ya kuchangia Madawati Mkoa wa Geita kwenye Harambee iliyofanyika Mjini Geita.
  Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila akitoa maelezo kuhusu namna Acacia ilivyoshiriki mwaka huu kuchangia kwenye zoezi la madawati.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bwana Graham Crew akiwa amenyoosha mikono kusalimia umma wa Watanzania waliongana kwenye harambee ya madawati Geita.
  Timu ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri baada ya Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila kutanga kuwa Mgodi utatoa shilingi milioni Mia Moja kwa ajili ya madawati Mkoa wa Geita.

  Na Dixon Busagaga.

  Akitangaza kiwango hicho katika hafla ya changizo iliyofanyika Desire Park Mjini Geita , Meneja Ufanisi na Mahusiano na Jamii wa Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu bwana Elias Kasitila amesema, “Bulyanhulu imebarikiwa kuwa karibu na Wilaya mbili,Halmashauri ya Msalala iliyopo Mkoa wa Shinyanga na Nyang’wale iliyopo Mkoa wa Geita. 

  “ Hivyo basi tulipopokea mwaliko kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale kuhusu kampeni ya leo ya madawati tumeamua kwamba japokuwa miradi mingine ya madawati tumeifanya mkoa wa Shinyanga tumeona kuna umuhimu wa kufanya hivyo mkoa wa Geita pia.”alisema Kasitila. 

  "Hivyo basi siku ya leo tunajitolea kuchangia Tsh100m/- kwa ajili ya kampeni za mikoa inayolenga kuondoa upungufu wa madawati 70,000.”aliongeza Kasitila. 

  Elias aliongeza kuwa, “misaada ya madawati kutoka kwenye migodi iliyoko chini ya Acacia ambayo ni, North Mara, Buzwagi and Bulyanhulu,kwa mwaka huu Acacia imetumia takriban fedha za kitanzania zaidi ya Billion Moja ambayo inakadiliwa kutengeneza zaidi ya madawati 10,000. 

  Mgeni rasmi katika hafla ya kuchangia madawati mkoa wa Geita alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi ,Utumishi na Utawala Bora, Mh.Suleiman Jafo. 

  Akiwahutubia washika dau waliokuwa Desire park Naibu Waziri Jafo alisema “Nitapeleka salamu kwa waziri mkuu kuhusiana na mwitikio ambao nimeushuhudia leo ninaagiza kamati ya Kampeni ya madawati Geita kuorodhesha washika dau wote waliochangia leo na kuwasilisha orodha hiyo kwenye ofisi ya Waziri Mkuu ili binafsi awatambue wote walioonesha kuguswa kuiondolea Geita uhaba wa madawati.” 

  Katika hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Aacacia Bulyanhulu Graham Crew binafsi alijitolea kuchangia fedha za kitanzania shilingi 750,000/- kwa ajili ya kampeni hiyo. 

  0 0

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4290 la tarehe 01 Septemba 2016, ikihusisha shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika maadhimisho ya miaka 52 ya kuzaliwa kwake na shughuli za kisiasa.

  Tunapenda  kuwataarifu wananchi kwamba kazi ya Jeshi ni kulinda na kutetea maslahi ya Taifa na mipaka ya nchi, aidha, Jeshi letu linafanya kazi kwa kufuata mila, desturi, nidhamu, kanuni na sheria za Kijeshi kwa weledi wa hali ya juu, hivyo lisihusishwe na propaganda zozote za kisiasa kwani Jeshi letu ni lenye maadili ya kitaasisi ya hali ya juu.  

  Jeshi ni taasisi ya dola wala si taasisi ya kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na wanasiasa ni wakati linapotetea na kulinda maslahi ya wananchi.  Inaombwa kuwa makini katika utoaji wa maelezo au malalamiko, iachwe mara moja vyama vya siasa kuingilia ratiba za Kijeshi.   

  Ikumbukwe kwamba tarehe 25 Julai kila mwaka ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa wetu waliolitumikia Taifa hili kwa umakini na nguvu zote kwa kuleta mafanikio tunayoyaona, na hii ilipitishwa mwaka 1979 wakati Majeshi yetu yanarudi kutoka Uganda baada ya ushindi wa vita vya Kagera.  

  Sherehe ya mapokezi hayo yalifanyika mji wa Bunazi Wilaya ya Misenye wakati huo Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ilipoanzishwa kuwa tarehe hiyo iwe siku ya Mashujaa na kupitishwa Kisheria,  ikabaki siku ya tarehe 01 Septemba kuwa ni siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, hivyo jana tulikuwa tunasherekea siku ya kuzaliwa JWTZ. Ieleweke hivyo na iachwe mara moja kuchanganya shughuli za Kijeshi na mambo ya Kisiasa, viongozi wa kisiasa wekeni kumbukumbu zenu vizuri. 

  Jeshi linasisitiza wanasiasa ni vizuri wakasoma vema historia ya nchi wanayotaka kuiongoza na wanayoongoza ili kuepusha upotoshaji, lugha na maneno yanayotolewa na viongozi wa kisiasa wenye matakwa binafsi kuhusisha shughuli za Jeshi na siasa zao yanatia ukakasi na kiungulia, awe makini kuongea vitu ambavyo haelewi na kutokuwa makini zaidi aelewe madhara yanayoweza kutokea kutokana na upotoshaji.

  Jeshi letu linafanya shughuli zake ki weredi.

  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
  Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638

  0 0
 • 09/02/16--01:00: TAARIFA YA MSIBA


 •  CLARENCE CHILUMBA ENZI ZA UHAI WAKE

  TANZIA
  MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI BI.GIMBANA EMANUEL NTAVYO,ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA AFISA HABARI NDG. CLARENCE  CHILUMBA KILICHOTOKEA LEO TAREHE 02/09/2016, NDG. CHILUMBA ALIPATA AJALI YA PIKIPIKI SIKU YA TAREHE 31/8/2016 MAJIRA YA JIONI MJINI MASASI WAKATI AKITOKEA KAZINI KUELEKEA NYUMBANI KWAKE.

  BAADA YA KUPATA AJALI ALIWAHISHWA HOSPITALINI MKOMAINDO AMBAPO ALIPATA HUDUMA YA KWANZA NA BAADAYE KUPELEKWA NDANDA. AKIWA NDANDA HALI YAKE ILIZIDI KUWA MBAYA, TAREHE 1/9/2016 ALIPATA RUFAA YA KWENDA MUHIMBILI, AMEFARIKI  AKIWA NJIANI SOMANGA O2/9/2016 MAJIRA YA SAA 8:25 USIKU.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI
  AMINA.

  TAARIFA ZA MAZISHI ZITATOLEWA BAADA YA KUWASILIANA NA NDUGU WA MAREHEMU.

  IMETOLEWA NA.
  OFISI YA MKURUGENZI WA MJI
  MASASI

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabulla (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya habari-MAELEZO Bw. Hasaan Abbasi tuzo ya ushiriki wa idara hiyo katika kisaidia kutangaza shughuli mbalimbali za makumbusho na historia nchini.Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Hassan Abbasi akiangalia tuzo aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Prof. Audax Mabulla(kushoto) ya kutambua ushiriki wa idara hiyo katika kisaidia kutangaza shughuli mbalimbali za makumbusho na historia nchini.


  0 0

  Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao wamekumbushwa kutimiza wajibu wao kwa kurejesha mikopo hiyo ili iwanufaishe watanzania wengine ambao ni wahitaji.

  Wito huo umetolewa na baadhi ya wabunge walionufaika na mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) katika hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti baada ya kumaliza kurejesha mikopo yao iliyofanyika katika ofisi za HESLB mjini Dodoma jana (Septemba 1, 2016).

  Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge wa Vwawa na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) Mhe. Japhet Hasunga alisema mahitaji ya kifedha ya Bodi ni makubwa hivyo kila mnufaika wa mikopo ana wajibu wa kurejesha ili iwanufaishe watanzania wengi wanaohitaji mikopo.

  “Mimi nilinufaika katika mwaka wangu wa mwisho wa 1995 nikiwa chuoni Mzumbe na nimeamua kulipa kwa mkupuo nikijua kuna watanzania wengi wanahitaji kusaidiwa,” alisema Hasunga katika hafla hiyo fupi na kuwaomba wabunge wenzake walionufaika na mikopo kurejesha mikopo yao.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Biharamulo Magharibi Mhe. Oscar Mukasa aliishukuru Serikali kwa mkopo uliomuwezesha kupata elimu ya juu na kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1996 na kushauri vigezo vya utoaji mikopo vitoe kipaumbele kwa watanzania waliopo katika maeneo ya pembezoni mwa nchini.

  “Na mimi nimemaliza kurejesha mkopo wote niliopewa na ninaishukuru Serikali ... lakini ninashauri vigezo vya utoaji wa mikopo vitoe kipaumbele kwa watanzania waliopo pembezoni kama Biharamulo,” alisema baada ya kukabidhiwa cheti chake na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru.

  Katika hafla hiyo, mtumishi wa Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) Bw. Richard Jafu naye alikabidhi wa cheti baada ya kurejesha kwa mkupuo mmoja kiasi cha Tshs 14.5 milioni alichokuwa anadaiwa baada ya kukopeshwa akiwa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma ambako alihitimu mwaka 2013.

  Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Bw. Jafu ambaye yupo mkoani Shinyanga kikazi, mfanyakazi mwenzake Bw. Gabriel Sikoi alisema uamuzi wa Bw. Jafu kumaliza deni lake ulisukumwa na uzalendo ili fedha hizo zitumike kuwakopesha wengine.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Bw. Badru aliwashukuru wadau hao kwa kutimiza wajibu wao na kuwasihi wanufaika wengine kujitokeza na kurejesha mikopo waliyopewa.

  “Wito wangu kwa wanufaika wote ni kujitokeza na kurejesha mikopo, ikiwezekana kwa mkupuo mmoja au miwili au mitatu kulingana na uwezo,” alisema Bw. Badru aliyeteuliwa mwezi uliopita kushika wadhifa huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw. Abdul-Razaq Badru akimkabidhi cheti cha kumaliza kurejesha mkopo wa elimu ya juu Mbunge wa Biharamulo Magharibi Mhe. Oscar Mukasa (kushoto) mjini Dodoma jana (Septemba 1, 2016). Kulia ni Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga ambaye naye alikabidhiwa cheti baada ya kumaliza kurejesha mkopo wa elimu ya juu.
  Mbunge wa Biharamulo Magharibi Mhe. Oscar Mukasa akizungumza katika mkutano na wanahabari mjini Dodoma jana (Septemba 1, 2016) baada ya kukabidhiwa cheti cha kumaliza kurejesha mkopo wa elimu ya juu. Wengine ni Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (kulia) ambaye naye alikabidhiwa cheti baada ya kumaliza kurejesha mkopo wa elimu ya juu na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw. Abdul-Razaq Badru aliyekabidhi vyeti hivyo.

  0 0
 • 09/02/16--02:38: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  MKURUGENZI wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani nyumba takribani tano za wasanii wake wa kundi la Yamoto Band na kuwataka wananchi waelewe kuwa msanii anahitaji nyumba na sio magari.

  Nyumba hizo zilizojengwa nje ya mji kidogo, Katika kata ya Kisewe amesema kuwa hiyo ni moja ya maendeleo kwa wasanii ,kwani hii si mara ya kwanza kuwazawadia nyumba wasanii wake.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa ameamua kuziweka wazi hasa baada ya kusikia maneno mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa Yamoto Band hawafaidiki na Muziki wanaoufanya.

  Fella amesema kuwa nyumba hizo mpaka sasa hajajua thamani yake ila zitakapokamilika ataita watu wa tathmini kwa ajili ya kuziangalia ili kujua zimetumika kiasi gani kwenye ujenzi huo.

  Ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi kubwa sana alizozifanya katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua wasanii. Na katika nyumba hizo zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.

  Meneja wa Mkubwa na Wanawe, Amani Temba 'Mh. Temba' amesema kuwa hizi nyumba zimejengwa kwa fedha za wasanii wenyewe wanazozipata kwenye shoo za muziki wanazozifanya na sio kama hela zinazotoka mfukoni mwa kiongozi yoyote.

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka amefurahishwa na hatua hii kwani ni mara chache sana kwa viongozi wa muziki kuchukua dhamana ya kuwajengea nyumba vijana hawa wadogo na amewataka wasanii kutokufanya mzaha kwenye tasnia hii.

  Fella amezindua pia nguo aina mbalimbali zenye nembo y Yamoto Band na wamezilipia Brela,COSOTA kwa hiyo yoyote atakayejaribu kunakili watamshughulikia.

  Nyumba za Wasanii wa Yamoto Band zikionekana kwa muonekano wa nje.
  Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.

  Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.

  Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akikagua nyumba ambazo zipo kwenye hatua ya mwisho ya umaliziaji.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akionyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo ya Yamoto Band zitakazopatikana nchi nzima

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Vodacom Afrika Bw. Shameel Joosub (kushoto),ambaye aliongozana na Viongozi wengine wa Vodacom Tanzania na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam
    Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Vodacom Afrika Bw. Shameel Joosub (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania Balozi Mwanaidi Sinare Majaar (kushoto) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Vodacom Afrika Shameel Joosub.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dkt. Agness Kijazi akizungumza katika warsha ya siku moja kwa Waandishi wa Habari juu ya Masuala ya Utabiri wa Hali ya Hewa kwa Msimu huu, inayofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Kituo hicho, Ubungo Plaza, Jijini Dar es salaam.
  Meneja wa Kituo cha Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Samuel Mbuya akitoa mafunzo kwa baadhi ya Waandishi wa Habari juu ya Hali ya Hewa kwa Msimu wa Mwaka 2016, inayofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Kituo hicho, Ubungo Plaza, Jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Hamza Kabelwa akifafanua jambo wakati akijibu maswali, katika warsha ya siku moja kwa Waandishi wa Habari juu ya Masuala ya Utabiri wa Hali ya Hewa kwa Msimu huu, inayofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Kituo hicho, Ubungo Plaza, Jijini Dar es salaam.
  Meneja wa Kituo cha Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Samuel Mbuya akifafanua jambo wakati wa Warsha hiyo.
  Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a akielezea jambo kwa Waandishi wa Habari, wakati wa warsha ya siku moja kwa Waandishi wa Habari juu ya Masuala ya Utabiri wa Hali ya Hewa kwa Msimu huu, inayofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Kituo hicho, Ubungo Plaza, Jijini Dar es salaam.

  0 0  Serikali ya Tanzania na Iran zakubaliana kuanzishwa kwa wiki ya Utamaduni itakayowezesha kujifunza namna ya kuukuza ,kuulinda na kuendeleza sekta hiyo.

  Makubaliano hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Tanzania na Iran.

  Waziri Nnauye alisema kuwa amekubaliana na wazo la kuanzishwa kwa wiki ya Utamaduni kati ya Tanzania na Iran na ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwao namna ya kuukuza, kuulinda na kuuendeleza utamaduni wa mtanzania.

  “Utamaduni ni silaha ya upendo na nimefurahia wazo la kuanzisha wiki ya Utamaduni na tuko tayari kujifunza kutoka kwenu na hakika tumelipokea na tunaamini fursa hii italeta mafanikio makubwa katika sekta hii”, alisema Mhe. Nnauye.

  Kwa upande wa Naibu Waziri wa Utamaduni Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa wataendelea kushirikiana katika masuala ya Utamaduni na kuendelea kujifunza kutoka kwa watanzania namna bora ya kuenzi,kuendeleza na kuutunza Utamaduni.

  Naibu Waziri huyo wa Iran aliendelea kusema serikali yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika uandaaji wa Filamu na kubadilishana uzoefu katika masuala ya filamu kati ya nchi hizo mbili.

  Hata hivyo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nnauye alipata mwaliko kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni Iran Mhe. Turkaman kwenda nchini Iran kujionea vivutio vya utamaduni.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (wa tatu kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam walipokutana kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa pili kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai na kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Iran Bw. Ali Bagiri. 
  Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (wa tatu kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman akielezea azma yake ya kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Utamaduni kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Septemba 2,2016 wa pili kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai na kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Iran Bw. Ali Bagiri.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2,2016 kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya kiutamaduni kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiangalia kitabu cha Utamaduni kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai. 
  Picha/Habari na Raymond Mushumbusi .

  0 0  TIMU ya wasichana ya New Generation imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Star, Zanzibar, baada ya kuifunga Women Fighter kwa mabao 2-1 katika fainali iliyochezwa visiwani humo jana.

  Mchezo huo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Fuoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar na kuvuta hisia za mashibiki wengi wa soka wanawake na wanaume, hasa kwa vile timu hizo zina upinzani wa jadi.

  Mabao ya New Generation yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza ambapo bao la kwanza lilifungwa na Warda Mwinyi katika dakika ya 10 wakati bao la pili lilifungwa mnamo dakika ya 16 wakati bao la kufutia machozi la Women Fighter lilifungwa na Khadija Hassan dakika ya 27.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi kombe kwa washindi afisa habari wa chama cha soka Zanzibar ZFA Ali Bakari Cheupe kwa niaba ya rais wa chama hicho, aliipongeza kampuni ya Airtel kwa uamuzi wake wa kudhamini michuano hiyo ambayo imeweza kuleta hamasa kubwa kwa wananchi wa Zanzibar.

  Alisema kabla ya michuano hiyo Zanzibar ilikuwa nyuma katika soka la wanawake lakini kupata udhamini huo ari imeongezeka zaidi na tayari wanawake wengi wamehamasika kutaka kucheza mpira wa miguu.

  Naye Meneja Mauzo wa Airtel Muhidin Mikidad alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia michezo hiyo kadri ya hali itavyokuwa, ambapo amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuwaunga mkono

  Jijini Mbeya, timu ya wavulana ya Mbaspo Academy imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi baada ya baada ya kuifunga Uyole Alliance 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

  Mchezo huo uliamuliwa kwa penati kufuatia timu hizo kutoka sare ya kufungana 3-3 katika muda wa kawaida wa dakika 90.

  Katika mchezo huo ulipigwa juzi katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ulishuhudia vijana wa Uyole Alliance kutoka nje kidogo ya jiji la Mbeya wakijipatia goli la kuongoza katika dakika ya saba baada ya Daniel Shaban kufunga kwa penati baada mchezaji wa timu hiyo kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

  Mbaspo walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha katika dakika ya 20 kupitia kwa Albinus Haule kabla ya Claud Alex wa Uyole Alliance kuandika bao la pili timu yake dakika ya 42.

  Mabao mengine kwenye mchezo huo yalipatikana dakika 82 kwa upande wa Mbaspo mfungaji Shadraki Sape,wakati bao la Uyole Alliance lilipatikana dakika ya 88 mfungaji ni Claud Casto.

  Wachezaji wa timu ya New Generation wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa baada ya kuifunga Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar, zilizochezwa kwenye uwanja wa Fuoni Alhamisi 25 Agosti 2016

  Nahodha wa timu ya New Generation Amina Hali Abdallah (nyekundu) akikabidhiwa kombe na Afisa Habari wa ZFA Ali Bakari baada ya kuichapa timu ya Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar Jana 25 Agosti 2016. New Generation ilishinda 2-1.

  Naodha wa timu ya Mbaspo Academy Mbeya, Biva Steven akipokea kikombe kutoka kwa mgeni rasmi Katibu Tawala wa mkoa huo Alone Mbinga baada ya timu yake kuifunga Uyole Alois Academy Penati 4-3 katika mchezo wa fainali ya Airtel Rising stars ngazi ya mkoa uli0pigwa katika dimba la uwanja Sokoine juzi. 
  Wachezaji wa timu ya New Generation wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa baada ya kuifunga Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar, zilizochezwa kwenye uwanja wa Fuoni Alhamisi 25 Agosti 2016.

  0 0
 • 09/02/16--03:45: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto), akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto), akiangalia video inayoonyesha jinsi ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia kamera maalum, wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
  Mtaalamu wa mifumo ya Komputa , Boris Derygin akitoa maelezo kuhusu mada inayohusiana na udhibiti wa uhalifu wa mitandao wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Gabriel Mukungu. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
  Mtaalamu wa mifumo ya Komputa, Boris Derygin ,akionyesha karatasi inayoelekeza jinsi ya kuitambua gari iliyofanya uhalifu wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.
  Kamishna Msaidizi , SACP Gabriel Mukungu wa Jeshi la Polisi la Tanzania, akielekezwa na Kapteni Vasily Gerasimov wa Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, namna ya kudhibiti uhalifu katika majengo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya nchi hizo. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na mkewe mama Janeth,wakisalimiana na wenyeji wao mara baada ya kuwasili Pemba mapema leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili visiwani humo,ambapo hapo baadae ataelekea Unguja kuendelea na ziara yake ya kikazi .
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na mkewe mama Janeth,na ujumbe mwingine aliofuatana nao wakitazama kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili Pemba mapema leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili visiwani humo,ambapo hapo baadae ataelekea Unguja kuendelea na ziara yake ya kikazi.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hayati Dk.Omar Ali Juma lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
  Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli akiomba dua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hayati Dkt.Omar Ali Juma lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa ameambatana na Mkewe,Janeth Magufuli (hawaonekani pichani) wakisubiri kuweka mashada ya maua na kuomba dua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hayati Dkt.Omar Ali Juma lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba.

  0 0


  0 0

  Msaragambo Neno msaragambo linamaanisha mfumo uliokubaliwa na jamii katika kitongoji, kijiji au kata wa kushirikiana katika kufanya kazi zenye faida kwa watu wote, maarufu kwa kazi za ujenzi wa taifa. Kwa kazi hizi ni za ridhaa zilipaswa kwanza zikubaliwe na wengi vinginevyo haikuwa rahisi mtu mmoja kuitisha wito wa kazi fulani na watu wengine kuja kuifanya.

  Kazi hizi ambazo hata serikali ya awamu ya kwanza ilizikazania sana mara baada ya Tanganyika kupata uhuru, ni pamoja na ujenzi wa mashule, kuchimba visima vya maji, kuchimba barabara na kadhalika.
  Upo ushahidi wa kutosha kuhusu Wapare walivyotumia mfumo huu na kupata maendeleo makubwa Wilayani mwao. Zipo barabara za Mwanga hadi Ugweno na Usangi; Ndungu hadi Mamba na Vunta; Hedaru hadi Mwala; Makanya hadi Chome,Mpirani hadi Bombo Song’ana,Gonja Maore hadi Vuje naVudee hadi Mbaga.
  Hata hivyo, si barabara tu lakini zahanati, na shule nyingi zimejengwa na wapare wa wilaya za Same na Mwanga na kuinua kiwango cha maendeleo yao. Nakumbuka watu hawa si watu wapenda misaada ya mteremko ndiyo maana pamoja na kukabiliana na hali mbaya ya uhaba wa mvua mara kwa mara wamekuwa si watu wa kupiga yowe haraka. Kazi zilizofanywa kupitia utaratibu huu wa msaragambo ziliufanya Mkoa huu wa Kilimanjaro uongoze kwa maendeleo ya barabara nzuri, ujenzi wa shule nyingi hadi katika vitongoji.
  Hivyo basi nashauri, ili kukabiliana vyema na maandamano yasiyo na tija kwa taifa ni heri kwa Serikali kuitisha Msaragambo tarehe ambazo wale wasiopenda maendeleo watakuwa wakiandamana. Serikali ibuni shughuli za maendeleo ambazo siku hiyo viongozi na wananchi watashirikiana kuzitimiza.
  Watakaotaka kwenda kwenye maandamano waachwe waende na wapenda maendeleo wakachape kazi. Wakitoka kwenye maandamano watakuta maendeleo. Tena ingefaa kwa wale Wabunge wa Chama Tawala siku hiyo kila mmoja awe jimboni mwake na kufanya msaragambo. Kwa yale majimbo ya upinzani, mwenyekiti wa chama tawala na wale wagombea wanaolitaka jimbo wawe mstari wa mbele ili kuwaonyesha wananchi kwamba hapa ni kazi tu.

  Mdau,
  Theophani Celestine Ishika

  0 0

  Huko  Ujerumani, hususan katika makao ya Kiongozi mkuu wa Ngoma Africa band nyumbani kwa Kamanda Ras Makunja hali imekuwa si shwari baada ya mbwa aina ya Bulldog mwenye jina la sajent Domo Baya (juu) mlinzi namba moja wa Ras Makunja ametioweka lindoni kwa muda wa siku tatu sasa na kikosi cha kuangalia wanyama cha mji wa Oldenburg kinamtafuta mbwa huyo mwenye umri wa miaka 14 ambaye mara nyingi ni mwenye vituko pale anapochoka kulinda.
  Mmiliki wa mbwa huyo kamanda Ras Makunja amekaririwa  akimlalamikia mlinzi wake huyo kwa kudai kuwa "kama kachoka kazi atamfuta" Mwanamuziki huyo anamlalamikia Domo Baya kwa visa na kwamba siku hizi ana tabia za uzembe sana .
  "Kishanigombanisha na jirani baada ya kuvamia swimming pool yao bila idhini ya wenyewe", anasema  Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni. Lakini wakati msako ukiendelea hebu sikiliza kazi zao at www.ngoma-africa.com
  Kiongozi mkuu wa Ngoma Africa band Ras Makunja

  0 0

  Prof. Idris A. Rai (left), the Vice Chancellor of the State University of Zanzibar (SUZA) talks with Ms. Cornelia Jesse, the World Bank (WB) Senior Education Specialist on various issues of mutual benefit between their institutions. They met on Friday 2nd September, 2016.
  Ms. Jesse and Mr. Kaboko Nkahiga, another WB official then paid a visit to the SUZA Digital Television studio which is supported by the WB, the studio which will mainly produce educational programmes will be inaugurated in the very near future.  

older | 1 | .... | 1341 | 1342 | (Page 1343) | 1344 | 1345 | .... | 3272 | newer