Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Serikali yapiga marufuku usafirishaji wanyama nje ya nchi

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa serikali imepiga marufuku biashara ya kusafirisha wanyama hai nje ya nchi mpaka pale itakapowekwa misingi mizuri ili nchi iweze kunufaika na biashara hiyo.

Prof. Maghembe ameyasmea hayo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC 1 ambapo alisema Serikali iliamua kuangalia upya utaratibu huo wa kuuza wanyama hai na kuamua kusitisha biashara hiyo hadi pale taratibu na misingi mizuri ya biashara hiyo itakapowekwa.

“Ni kweli kulikuwa na utaratibu wa kuuza wanyama hai nje ya nchi bila kuiwezesha nchi kupata faida yoyote ile, hivyo kwa sasa kama nchi tumeamua kupiga marufuku biashara kwa maslahi ya taifa”.

“Haiwezekani uuze wanyama hai nje halafu anayenufaika ni yule anayenunua na kuiacha nchi bila faida yoyote ya uwepo wa maliasili hiyo, hivyo kama nchi tumeamua kupiga marufuku biashara hiyo hadi pale misingi mizuri ya kibiashara itakapowekwa na kuiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake, na nisisitize kwa sasa hata Chawa wa Tanzania hataweza kusafirishwa nje ya nchi”. Alisema Prof. Maghembe.

Aidha, Prof. Maghembe alisema kuwa kwa sasa Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na ujangili wa wanyama pori kama Tembo na Faru ikiwemo kukamata watu wote wanaohusika katika biashara hiyo na mpaka sasa wameshakamata  baadhi ya watu akiwamo mwanamama anayejiita malikia wa pembe za ndovu ambaye alikuwa kinara katika biashara hiyo.

Prof. Maghembe aliongeza kuwa hatua hiyo imeonesha mafanikio kwani kwa kipindi cha hivi karibuni soko la mauzo ya pembe za ndovu nje nchi hasa bara la Asia ambao ndio walikuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa hizo yameshuka na hatua hiyo inatokana na mikakati iliyowekwa na Serikali.

Akizungumzia wizi katika mazao ya misitu Prof. Maghembe alisema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kupambana na wizi wa mazao ya misitu na imekubaliwa kuwa iwapo gari litakamatwa likiwa na mazao hayo bila kuwa na kibali, Serikali itataifisha gari hilo na wahusika watashtakiwa kama wahujumu uchumi.

Pia Prof. Maghembe alisema kuwa kwa sasa utawekwa utaratibu wa magari yote yanayobeba mazao ya misitu kusafiri mchana kwenye gari lililo wazi ili kurahisisha ufuatiliaji na udhibiti wa wizi huo.

Serikali imeahidi kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki kwenye vijiji vilivyo pembezoni mwa misitu ili kuweza kudhibiti uchomaji moto kwenye kwenye maeneo hayo hali itakayowezesha pia utunzaji wa mazingira. Na Hassan Silayo, MAELEZO

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd, Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipeana mkono wa shukurani na Nd,Hassan Khatib Hassan,baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshughulikia Idara Maalum za SMZ,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

LEO KATIKA KIPINDI CHA "TUNATEKELEZA" NDANI YA TBC1 ATAKUWEPO WAZIRI WA ULINZI NA JKT, DKT. MWINYI

EALA SWEARS IN NEW EX-OFFICIO MEMBER

0
0
The Minister for State, of East African Affairs, Republic of Uganda, Hon Julius Wandera Maganda, this afternoon took Oath of Allegiance as an Ex-Officio Member of the Assembly.

Hon Maganda was sworn in by the Clerk to the Assembly at a brief ceremony witnessed by the Speaker and Members of EALA in line with the Rule 5 of the Rules and Procedures of the Assembly. The Rule 5(4) of the Rules of Procedure says in part that: “No Member can sit or participate in the proceedings of the House until the Oath or Affirmation of Allegiance to the Treaty is taken”.

Rule 5(5) specifically states that “when a Member first attends to take his or her seat other than at the first Sitting of a new House, he or she shall be brought to the table by two Members and presented by them to the Speaker who shall then administer the Oath or Affirmation of Allegiance”.

Hon Maganda was ushered in to the House by EALA Members, Hon Nusura Tiperu, Hon Dora Byamukama and Hon Chris Opoka.Hon Maganda was appointed to Cabinet by H.E. Yoweri Kaguta Museveni on June 6 2016. He replaces Hon Shem Bageine.

Prior to the appointment as Minister for State, East African Affairs, Hon. Maganda was the Member of Parliament of Samia Bugwe County South, a position he still holds to date.Hon Maganda has served on various Committees in the Parliament of Uganda including that of Education and another on Rules, Discipline and Privileges. Others are the Trade and Tourism Committee and the Committee on National Economy.

Hon Maganda holds a Bachelor of Public Administration degree from the Islamic University of Uganda, a Certificate in Legal Practice from the Law Development Centre in Uganda and a Post Graduate Diploma in Management from the Uganda Management Centre.
Hon Maganda Julius Wandera takes the oath of allegiance. Looking on from left is Hon Dora Byamukama, Hon Chris Opoka and Hon Nusura Tiperu. On right is Senior Clerk Assistant, Stephen Mugume.
Hon Maganda Julius Wandera takes the Oath of Allegiance administered by Stephen Mugume, Senior Clerk Assistant, EALA. Looking on is Hon Nusura Tiperu.

TCRA CCC YAKABIDHI VYETI NA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUANDIKA INSHA NA MAKALA

0
0
Baraza la Ushauri kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania ( TCRA CCC) leo limekabidhi vyeti na zawadi kwa washindi walioshiriki katika shindano la uandishi wa insha kwa shule za msingi na sekondari na makala kwa vyuo vya elimu ya juu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Mashindano hayo yalihusisha washiriki kuandika insha na makala juu ya haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano hapa nchini.

Akikabidhi vyeti na zawadi hizo kwa washindi mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano DK. Maria Sasabo amesema amehamasika kuona vijana wameshiriki katika mashindano hayo na kutoa maoni juu ya faida, changamoto na mbinu mbali mbali za kukabiliana na changamoto hizo katika kuboresha utoaji wa huduma kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano.

Aidha, Dr. Sasabo ametoa rai kwa vijana kutumia fursa mbali mbali zitokanazo na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano kukuza vipaji, kujielimisha na pia kupata ajira.Pia, amewaasa vijana kutumia huduma mbali mbali za mawasiliano kwa kufuata sheria na kanuni za nchi kwa ustawi wa wao kielimu, kijamii na kiuchumi.
Regani Yudos kutoka shule ya Msingi Mbuyuni akipokea cheti na zawadi ya mshindi wa pili katika shindano la kuandika insha kwa shule za msingi
Jane Michael Andrew wa Mbuyuni mshindi wa kwanza katika shindano la kuandika insha kwa shule za msingi akipokea cheti na zawadi kutoka kwa mgeni.
Felician Crispin Kapama kutoka Zanaki Sekondari mshindi wa pili shindano la kuandika insha kwa shule za sekondari.
Omary Abas Mdungu mshindi wa kwanza makala kwa vyuo vya elimu ya juu.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA TAASISI YA AFRICA MATTER LIMITED YA UINGEREZA MHE. LYNDA CHALKER

0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimkaribisha kuketi  Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimsindikiza Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya  mzungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016. 
  "Hapa kazi tu..." anaonekana kusema Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya  mzungumzo yake na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016

Rais Magufuli amteua Bw. James Dotto kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Doto M.James aliyeteuliwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.

DIRA YA DUNIA JUMATANO 31.08.2016


Mjue Msanii Wako: Diamond Platnumz akiwa Kenya!

0
0

Courtesy of Citizen TV Kenya

Article 22

Mbeya City kuifuata Mbao Fc Jijini Mwanza

0
0
IKIWA inaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc  uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mbeya City fc  inataraji kuondoka mjini Shinyanga   ijumaa hii kuelekea jijini Mwanza  tayari kwa  kuikabili timu hiyo  iliyopanda daraja  kwa ‘mtereko’ tiketi ya mezani.

Wakiwa kwenye uwanja wa Kambarage  wakati wa mazoezi ya asubuhi  afisa habari wa kikosi hiki, Dismas Ten,  amesema kuwa  Mbeya City  itaondoka  mjini Shinyanga  ijumaa  jioni kuelekea  jijini Mwanza  ikiwa na lengo moja tu la kuvuna  pointi tatu zingine  kwenye uwanja wa CCM Kirumba  kama  ilivyokuwa kwenye mchezo wa juma lililopita dhidi ya wenyeji Toto Africans.

“Tumekuwa hapa Shinyanga  toka siku ya jumatatu, kwa ajili  ya mazoezi na matayarisho ya mchezo wa jumamosi,Mwalimu alichagua  kufanya mazoezi Kambarage  kwa lengo moja tu la kupata utulivu na kuandaa kikosi vizuri ili kuhakikisha tuanshinda  na kupata pointi tatu kwenye siku nzuri ya Septemba 3 , kikosi chetu kiko sawa, pasipo majeruhi yeyote na tunakwenda Mwanza kucheza kwenye uwanja ambao  siku zote tumekuwa na bahati nao”. alisema

Akiendelea  zaidi Ten aliweka wazi kuwa kiungo Geoffrey Mlawa  na mshambuliaji Omary Ramadhani waliyopata majeraha  kwenye mchezo uliopita  dhidi ya Toto Africans wamerejea kwenye hali  nzuri  na anaweza kuwa  sehemu ya mchezo huo wa jumamosi endapo Mwalimu Kinnah Phiri  atapenda kuwatumia.

“Dakika 90 zilizopita tulizihitimisha kwa kupata majeruhi wawili kwa Omary Ramadhani na Geoffrey Mlawa, jopo la madaktari  wamethibitisha kuwa  wachezaji hao wako sawa na wanaweza kucheza kwenye mchezo wa jumamosi ingawa jambo hilo  litategemea  na  maamuzi ya mwalimu, kuwepo kwao kikosini  kutaongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji ambalo ni muhimu kwenye kusaka pointi tatu,hasa ukizingatia kiwango kizuri walichokionyesha kwenye mechi dhidi ya Toto Africans” alimaliza.

RITA YATOA MAFUNZO KUHUSU MPANGO MPYA WA USAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO MKOA WA IRINGA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wake kuhusu kusimamia kikamilifu Mpango mpya wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bila ya malipo Kwa watoto wenye Umri chini ya miaka mitano katika Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa VETA Mjini Iringa, ambapo utekelezaji wake utaanza hivi karibuni katika Mikoa ya Iringa na Njombe. kulia kwake ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson, anayemfuatia kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela na Mwingine ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Nuhu Mwasumilwe.
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia Hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza kuhusu usimamizi na ufuatiliaji wa Mpango mpya wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bila ya malipo Kwa watoto wenye Umri chini ya miaka mitano pindi utakapoanza kutekelezwa katika Halmashauri na Wilaya zote za Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri za Iringa, Kilolo na Mufindi.

TRL YATANGAZA NAULI MPYA TRENI YA PUGU

0
0

NAULI ya abiria wa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu jijini Dar es Salaam, imepanda kutoka Sh 400 ya awali hadi 600.
Tozo hiyo ya nauli mpya inatarajiwa kuanza rasmi Septemba mosi, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Ng’hwani Kudema, alisema viwango hivyo vya nauli vilivyokokotolewa na Mamlaka ya Majini na Nchi Kavu (Sumatra), vimepanda kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu.
“Baada ya siku 14 nauli hizi zitaanza kutozwa kwa mujibu wa utaratibu na hili tutabandika matangazo. 
Hadi kufikia Septemba 13, mwaka huu nauli itakayokuwa inatozwa ni shilingi 600 kwa mtu mzima na shilingi 100 kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,” alisema Kudema
Alisema wakati wa majaribio ya treni hiyo Agosti mosi mwaka huu, walikuwa na mabehewa 10 lakini kutokana na mahitaji ya usafiri huo kuwa mkubwa, walilazimika kuongeza mabehewa ambayo kwa sasa yamefika 18.

TTCL yasogeza huduma na bidhaa anuai kwa wadau TCRA

0
0
Maneja Usambazaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Robert Noel (kulia) akionesha kwa mmoja wa wateja baadhi ya bidhaa za mawasiliano ya intaneti zinazotolewa na kampuni hiyo katika maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za TTCL, kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wateja waliotembelea maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akihudumiwa kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam. Kikosi cha wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kilichofanya maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo kwa wadau kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam. Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akitoa ufafanuzi kwenye maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo kwa wadau kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya kikosi cha wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kilichofanya maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo kwa wadau kwenye Jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam kikiwa katika picha.

RC ARUSHA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI

0
0


Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mrisho Gambo(katikati)akizungumza na Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto)  alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo nae akiwa ameambata na Mbunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki(Eala)Mheshimiwa Angela Kizigha.

Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia)  baada ya mazungumzo yao.

Na Nteghenjwa Hosseah – Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameendelea  na  ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa dini  ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi  baada ya kuteuliwa kushika  wadhifa huo hivi karibuni.

Mh.Gambo amekutana na  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Mchungaji  Solomon Masangwa , Askofu wa  Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi  na Askofu  Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount  Kilimanjaro.

Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.

Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph  Magufuli kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani  halmashauri zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya  mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali  zitakazowawezesha kufanya  shughuli za uzalishaji mali.

Amewataka  wawajulishe waumini wa dini zote na serikali iko tayari  kupanga utaratibu wa

maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa  elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala kisiasa.

Askofu Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Aidha alishauri  kutokana na idadi ya watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo  ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.

Mh. Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili  watoe mawazo yao katika kuiboresha na  kuifanya itekelezeke   kwa wepesi zaidi.




CHADEMA YAAHIRISHA MAANDAMANO YA UKUTA

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mhe.Freeman Mbowe amesitisha shughuli za maandamano na mikutano  zilizokuwa zimepewa jina la UKUTA  na zilizopangwa  kufanyika Septemba 1, 2016 kwa kile alichodai hatua hii imekuja baada ya kuombwa na viongozi wa Dini na taasisi mbalimbali kufanya hivyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya CHADEMA Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,  Freeman Mbowe amesema  Viongozi hao wakuu wa kidini wamewaomba na kuwasihi katika vikao mbalimbali walivyokaa pamoja nao na kusema tunaheshimu viongozi hao. 
Mbowe amesema wanawapa muda wa wiki mbili au tatu ili waonane na Rais Magufuli kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huu wa kisiasa na kuliepusha taifa na machafuko ya kisiasa. 
Pia amesema Viongozi wa Taasisi za kiraia kama vile Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Jukwaa la Wahariri na Jukwaa la Katiba nao wamewasihi kuahirisha UKUTA kwa muda ili kutoa fursa kwa jitihada za mazungumzo na majadiliano kufanyika. 
"Sisi CHADEMA tunatambua na kujali haki zetu za kisiasa kama zilivyofafanuliwa katika Katiba na Sheria za nchi yetu. 
"Hata hivyo tunajali na kuheshimu kwa kiasi kikubwa zaidi haki za Watanzania ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yao" amesema Mbowe".
Amewatangazia viongozi wote  wa ngazi zote CHADEMA, pamoja na wanchama,wafuasi na Watanzania wote kuahirisha  mikutano na maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia kesho Septemba Mosi.

MAGAZETINI LEO

EXECUTIVE OFFICE SPACE FOR RENT (HUGO HOUSE, KINONDONI)

0
0
A spacious office space is available for rent at Hugo House Kinondoni (Plot no 22).

It has 5 rooms which are well partitioned and suitable for any executive office setting with space of 72 SQM. 
The office is fully carpeted and has Split units air conditioners.
Available for immediate occupancy.

For inquiry please contact 0713 465 336 or 0713 274 535 

BancABC YASHINDA TUZO YA KUONGOZA KATIKA MIAMALA MITANDAONI TANZANIA

0
0

Mkuu wa Kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC Silas Matoi akifafanua kuhusu matumizi ya kadi ya benki hiyo ya ‘Visa travel Money’ inayomwezesha mteja kufanya malipo mitandaoni kwa urahisi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini.
(Toka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini, Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi Silas Matoi wakionyesha tuzo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliyopewa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania. Mkutano na waandishi wa habari umefanyika katika makao makuu ya benki hiyo mapema leo jijini Dar es salaam.
(Toka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini, Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi Silas Matoi wakionyesha Tangazo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) lenye maelezo kamili kuhusiana na tuzo ya Visa waliyopewa hivi karibuni baada ya benki yao kuongoza katika miamala mitandao
Jitihada za BancABC katika ubunifu,kuendeleza na kufanikisha usalama wa miamala  matandaoni nchini Tanzania, imetambuliwa kwa tuzo ya Visa kuthibitisha ubora wa huduma yake mitandaoni.
Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo, Bi. Joyce Malai alithibitisha taarifa hiyo alipozungumza na vyombo vya habari mapema leo katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.

“Tunafurahi kupokea tuzo hii licha ya ushindani wa masoko uliopo, hii inaonyesha ni jinsi gani tumejidhatiti kuhudumia wateja wetu na kuwarahisishia kufanya miamala ya kifedha,” alisema Bi. Malai.

Aliongeza kuwa katika jitihada hizi za kuboresha miamala salama mitandaoni,  mtu yeyote anaweza kumiliki  kadi hii  ya Visa bila kujali kama anayo akaunti ya BancABC au la. Bi. Malai alifafanua kwamba kadi ya Visa ya BancABC ni rahisi kutumia kwani humhakikishia mteja ulinzi wa fedha zake na pia huondoa usumbufu wa kutembea na pesa taslimu.

Kadi hii inaweza kutumika kufanyia miamala mbalimbali ya kifedha kama vile kulipia tiketi za ndege pia kulipa posho na mishahara kwa wafanyakazi, kulipa ada za shule na kujikimu kwa wanafunzi, mikopo na misaada kwa serikali na mengineyo.ili kupata kadi hii mteja anahitajika kuwa na  kitambulisho halisi na kisha kujaza fomu zinazopatikana katika tawi lolote la benki hii.

Aliongeza kwamba wateja wanaweza kuweka fedha kwenye kadi hiyo kwa kutumia huduma mbalimbali za kutuma pesa kama vile TIGOPESA, AIRTELMONEY au M-PESA pamoja na benki zingine zilizopo Tanzania.

“Tunaamini kwamba upekee wa huduma hii ndicho kilichowavutia wateja na hivyo kusababisha ushindi wa tuzo ya Visa,” alisema. Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Bi. Upendo Nkini alisema, kadi hiyo inaweza kutumika pia kwa fedha za mataifa mbalimbali kama Shilingi ya Tanzania, Dola ya Kimarekani, Euro na Randi ya Afrika Kusini.

“Licha ya kuwawezesha wateja kufanya biashara mitandaoni, Mteja anaweza kutumia pesa zake kwenye Visa ATM Zaidi ya 400 nchini au Visa ATM Zaidi ya 1.3milioni duniani kote.

 Zaidi ya hapo Visa inamawakala Zaidi ya 1000 Tanzania na mawakala Zaidi ya 35 milioni duniani kote. Kupata kadi hii tutumie barua pepe customercaretz@bancabc. com.
 
Atlas Mara iliinunua BancABC Juni 2014 huku ikizidi kujitanua Tanzania, Botswana, Mozambique, Zambia na Msumbiji. Baada ya hapo ilinunua benki mbili nchini Rwanda (BR Commercial na BPR ambazo zinaendelea kukamilisha mchakato wa kuungana).

Atlas Mara iliorodheshwa katika Soko la Hisa London, mwezi Desemba 2013. Ndoto za kampuni hii ni kuanzisha taasisi kubwa ya kifedha Kusini mwa Sahara kupitia uzoefu wake, umahiri na upatikanaji wa mitaji, ukwasi na uzalishaji fedha. Malengo yakiwa ni kujumuisha ujuzi wa taasisi za dunia nzima na mitazamo ya kina ndani ya Afrika, hivyo kusaidia kukuza uchumi katika nchi zinazo hudumiwa na Kampuni hii.

NEWS ALERT: TANZANIA DAIMA YATUPIWA VIRAGO NJE NA MADALALI WA NHC LEO

0
0
Mapema asubuhi ya leo, watu wanaodaiwa kuwa ni Madalali wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) wamefika ofisi za Gazeti la kila siku la Tanzania Daima zilitopo katika makutano ya Mtaa wa Mkwepu na Indraghand na kuwatolea vyombo vyote nje kufuatia deni la muda mrefu la kodi ya pango wanalodaiwa bila kulipwa. Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Neville Meena amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wako kwenye Msukosuko mkubwa sana sasa ila wanafanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unaendelea kufanyika kama kawaida. 
Sehemu ya Wafanyakazi wa Gazeti hilo wakiwa nje ya Ofisi huku wakitafakari namna ya kufanya.
Vyombo vya Ofisi hiyo vikiwa nje.

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images