Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WASOMI: JPM NA LOWASSA WAMEONYESHA KUWA MAZUNGUMZO YATALETA MUAFAKA.

$
0
0
Na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salaam

Wasomi na Wanazuoni mbalimbali wamepongeza hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu zamani Edward Lowassa kushikana mikono na kusalimiana wakati wa Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa na Anna Mkapa.

Wanazuoni hao wametoa kauli hiyo leo katika mahojiano maalum na Idara ya Habari iliyokuwa ikitaka kupata maoni yao kuhusu kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao kwa jamii.Profesa Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa huo ndio Utanzania ulivyo wa kutofautiana bila kugombana.
Amesema kuwa kitendo hicho kimewaonyesha wananchi kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa ya kuondoa tofauti zilizopo kuliko kutumia njia nyingine kama vile maandamano na mabavu katika kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya matatizo.“Kukutana kwa viongozi hao na kupeana mikono wakati wa kusalimiana kunakumbusha utamaduni wetu uliojingekea toka siku nyingi wa kutatua matatizo yetu kwa mazungumzo bila kugombana au kutumia mabavu,”alisema Profesa Mkumbo.
Kwa upande wa Profesa Joseph Semboja amesema kuwa amefurahishwa sana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao kwani kimeuonyesha ulimwengu kuwa Watanzania ni watu wenye Amani na upendo.Amesema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa Watanzania wanaweza kuwa na tofauti lakini wakaendelea kuishi pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa lao.
Profesa Semboja amewataka wananchi kujifunza kutokana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao ambao wameonyesha kuwa ni lazima wakae pamoja kwa ajili kushughulikia mambo muhimu ya maendeleo ya wananchi badala kuendeleza tofauti ambazo hazina manufaa kwa Watanzania.
Amesema kuwa ipo haja ya kwenda zaidi ya hapo kwa kuweka utaratibu wa kukaa pamoja na kujadiliana ili kutatua vyanzo vya migogoro kwa ajili ya mustakabali mzuri wa Taifa hili.Profesa amesema kuwa sio sahihi kutumia mfumo wa jino kwa jino kwani utaratibu huo ndio unaoweza kusababisha kukua zaidi kwa migogoro na wakati mwingine unasababisha umaskini kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwani muda mwingi wananchi hawana muda wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa sababu ya migogoro.
Naye Profesa Samwel Wangwe amesema kuwa hatua ya viongozi hao kukutana na kupeana mikonop ni ishara kwa Watanzania kujifunza kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa katika kuleta muafaka mgogoro wowote kuliko kutunishiana misuli.
Amesema kuwa mazungumzo yana nguvu kubwa katika kultea upatanishi katika migogoro mbalimbali inatokea katika jamii kuliko kutumia njia nyingine ambazo zinaweza kusababisha vurugu na uharibifu wa mali za watu na upotevu wa maisha ya watu.

WAZIRI JENISTA ATOA SOMO KWA MABENKI.

$
0
0
 Waziri Jinista Mhagama akizungumza na wawanyaakazi wa FINCA.
SEKTA za kifedha zinazohusika na utoaji wa mikopo nchini zimetakiwa kutenga utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wa wadogo, kati na wakubwa ili kuleta unafuu wa masharti ya ukopaji. Hayo yalisemwa katika kilele cha mafunzo ya Wiki ya Huduma ya Kifedha na Uwekezaji na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira  na Walemavu Jenista Mhagama alipokuwa anafunga siku ya mwisho ya mafunzo hayo Agosti 27.

Mhagama alisema kuwa mafunzo kwa wajasiriamali yamekuwa yakitolewa mara kwa mara ila kikwazo kimekuwa ni mkopo hususani kwa wajasiriamali wanaoenda kukopa masharti wanashindwa yakiwemo uwekaji wa hati ya nyumba kama dhamana na riba kubwa.

“Tanzania kuna takribani wajasiriamali milioni tano, ila wengi wao wanashindwa kupiga hatua kutokana na masharti mazito ya mikopo, mfano mama anauza vitumbua unamwamabia alete hati ya nyumba na wakati kapanga chumba kimoja” Alisema Mhagama.

Alieleza kuwa banki na wadau wote wa maendeleo wakutane ili kujadili ni namna gani wanavyoweza kupunguza masharti kwa wajasiriamali wadogo ili kuwakomboa na kupunguza tatizo la ajira na umasikini nchini. Mhagama ambae pia ni Mbunge wa Peramiho alisema kuwa Serikali itakuwa tayari kufanya majadiliano kuona namna ya kumsaidia mjasiriamali mdogo na wa kati huku akiwapongeza Banki ya Finca kwa kupunguza gharama za ukopaji kwa wananchi.

Meneja Masoko na Afisa Mahusiano wa Bank ya Finca, S pacio Aboubakar alisema walijitahidi kufatilia vikwazo vyote vinavyowakwamisha wajasiriamali na kuvifanyia kazi na kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa masharti kwa mkopaji na ulipaji wa riba. Banki ya Finca imekuwa mkombozi kwa wajasiriamali nchini katika maonyesho hayo walifanikiwa kusajili zaidi ya wajasiriamali 4000 wapya.

Katika mafunzo hayo wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali vilishiriki ikiwemo Vikoba pia washindi walikabidhiwa fedha taslimu laki tano ili kuwapa motisha wajasiriamali wengine kushiriki miaka inayofata. Nuru Salim ni mmoja wa washindi wa zoezi lililofanywa na banki ya Finca na kuibuka mshindi alisema wamama wajitokeze kwa wingi kujifunza na kupata elimu ya uwekezaji na ujasiriamali ili kuepukana na tatizo la kuwa tegemezi.

“Mimi najihusisha na uuzaji wa nguo za wanawake Kariakoo, ila hapohapo nauza vitafunwa ninavyotengeza mwenyewe kama vitumbua ila nimekuja hapa kuongeza vitu vipya” Aleleza Nuru.

Maonyesho hayo yalikuwa ya tano na huwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta za banki, bima na uwekezaji kutoa elimu kwa wajasiriamali zaidi ya 20,000 na muitikio mkubwa ulikuwa wa wamama kuliko vijana na wanaume
Mwandishi: Muyonga Jumanne (Mwananchi)

KIFAHAMU KIPINDI KIPYA CHA 'CHUKUA HATUA' KINACHOHUSU VIJANA MKOANI DODOMA

$
0
0
Mohammed Hammie na Happy Balisidya wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kufahamu watakuwa wakiendesha kipindi cha CHUKUA HATUA.
 Watangazaji wa kipindi kipya cha CHUKUA HATUA Happy Balisidya na Mohammed Hammie, siku ya kwanza walipokutana wakati wa maandalizi ya kutengeneza kipindi hicho.

Chukua Hatua ni kipindi kipya cha radio kitakachowashirikisha vijana, wakizungumza na kujadili kwa pamoja masuala yanayowahusu hasa ya kujikwamua na maendeleo mkoani Dodoma na maeneo jirani.

Hiki ni kipindi ambacho kinatarajiwa kujadili kwa kina changamoto za ajira kwa vijana kupata mwelekeo wa maendeleo kwa vijana wa kike na kiume.
Lengo kuu la kipindi hiki ni kutoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia vijana kuondokana na ukosefu wa ajira na changamoto wanazokutana nazo katika mihangaiko yao, kipindi kitapaza sauti za vijana ambazo hazikupata nafasi ya kusikika hapo kabla.

Si kipindi tu, bali pia ni jukwaa kwa ajili ya kubadilishana ujuzi, mawazo, uzoefu na pia kujifunza kutoka kwa wengine, ni mahala pekee ambapo kijana atayaona matarajio na uzoefu kutoka fani na taaluma mbalimbali.
Kipindi pia kinatarajiwa kuimarisha ujuzi na kuelekeza upya akili za vijana kufanya kazi na kuchangamkia fursa za ajira kwa ujasiriamali, kujiajiri na kuukwepa umaskini uliokithiri miongoni mwao.

Kipindi kitaanza kuruka hewani siku ya Alhamisi ya tarehe 01/09/2016 kupitia kituo cha RASI FM RADIO inayopatika masafa ya 103.7 Dodoma.
Pia kipindi kitakuwa kinapatikana kupitia mtandao wa Youtube ukurasa wa CHUKUA HATUA, pia mijadala itakuwa inaendelea kupitia ukurasa wetu wa facebook ambao ni CHUKUA HATUA, Instagram ni KIJANA CHUKUA HATUA, na Twitter ni CHUKUA HATUA1.

Kipindi hiki kimewezeshwa na mpango wa pamoja wa ajira kwa vijana wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kazi Duniani (ILO) kwa udhamini wa SIDA.

MSEKWA:WATANZANIA WAACHE KUFUATA MKUMBO

$
0
0


Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa

Na Fatma Salum na Sheila Simba, MAELEZO

Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa amewaasa watanzania kuacha kufuata mkumbo wa kisiasa badala yake watii mamlaka ili kuepuka kuvunja sheria na kuleta madhara kwao binafsi na taifa kwa ujumla.

Msekwa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia masuala mbalimbali kuhusu mwenendo wa siasa za hapa nchini na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Alieleza kuwa watu wengi wana hulka ya kufuata mkumbo kwenye mambo fulani bila ya kuchunguza na kufahamu ukweli wake kabla ya kushabikia.

“Ni hulka ya watanzania kushabikia mambo wasiyoyafahamu ilimradi tu yanawafurahisha masikioni au machoni mwao kwani hata huko mitaani wanakimbilia ngoma bila ya kujua inatokea wapi au inaelekea wapi, hivyo nawasihi wajaribu kuwa makini na mbinu za siasa zinazotumiwa na baadhi ya vyama kwa kuwa nyingine zina madhara ndani yake.” Alisema Msekwa.

Akifafanua mwenendo wa siasa za hapa nchini, Mzee Msekwa alisema kuwa bado wanasiasa wengi hawafuati kanuni za ushindani wa kisiasa katika kutafuta madaraka badala yake wanatumia mbinu ambazo zinavunja sheria za nchi na hatimaye wanapambana na mamlaka.

“Ushindani wa kisiasa ni jambo la kawaida na linalokubalika ingawa ushindani huo ni lazima ufuate sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kufikia lengo, hivyo kubuni vitu ambavyo vinachochea utovu wa nidhamu na uvunjifu wa amani sio jambo zuri, ' alisisitiza.

Aidha, Msekwa alieleza kuwa utendaji wa Mhe. John Magufuli ni wa kuridhisha na wa aina yake kwa kuwa amekusudia kuleta mabadiliko chanya kwa watanzania na kuondoa mfumo wa utendaji kazi kwa mazoea jambo ambalo limesaidia kurudisha nidhamu kwa watumishi wa Serikali.

Akizungumzia uzoefu wake katika masuala ya kuongoza Bunge, alieleza kuwa tofauti ya Bunge la zamani ni kwamba lilikuwa na nidhamu kubwa na linaheshimika lakini Bunge la sasa halina utii na hicho ndio chanzo cha malumbano yanayojitokeza mara kwa mara katika vikao vya Bunge.

Aliongeza kuwa tangu awali wapinzani kazi yao ni kuipinga Serikali iliyo madarakani lakini kwenye Bunge la uongozi wake walikuwa wakipinga kwa kutumia hoja na kufuata kanuni bila ya kudharau mamlaka ya Spika wala Serikali iliyoko madarakani.

“Kanuni zinatoa nafasi kwa mbunge asiyeridhika na maamuzi ya Spika kushitaki kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge, na kamati hiyo itasikiliza na kutoa uamuzi kama mahakama inavyosikiliza lakini wabunge wa sasa hawataki kutumia utaratibu bali hutumia mbinu za tofauti ili waweze kupata sifa ambazo hazina tija kwa wananchi waliowachagua,” alisema.

Msekwa pia amewaasa vyama vya upinzani kutumia mbinu nzuri katika kutafuta madaraka bila ya kuvunja sheria au kuhatarisha amani ya nchi kwani waliowachagua wanategemea zaidi matokeo ya kazi waliyoahidi kuwatumikia kuliko malumbano yasiyo na tija kwa ustawi wao na taifa.

Executives meet for the 2 nd Edition of Mikono Speakers International Executive Breakfast Meeting in Dare salaam

$
0
0
More than 150 Business owners and finance personnel met on the 26th of August for an Executive Breakfast Meeting hosted by Mikono Speakers in Dare salaam and discussed as to which is the best way for financing the expansion of one’s business.

This was focused more on expanding businesses with a turnover of Tsh500million into a billion Tsh turnover, as well as businesses which turnover is above Tsh20 billion and is looking forward to expand into a regional level to countries like DRC Congo,Burundi,Rwanda,Uganda,Kenya and other nations. The Executive breakfast panelists were experts who had a wealth of knowledge on both debt and equity as ways of financing their businesses.
The 2nd edition of the Mikono Speakers International Executive Breakfast Meeting, was attended by executives and experts from the financial sector, different senior people and elites from the business community, financial institutions and academia, for discussions on the topic: ‘Expanding your business: equity or debt’ at a breakfast meeting organized Mikono speakers International, and supported by Tanzania Financial services Expo, My Staff check, Dun and Bradstreet credit Bureau.

The panelists included; Adebowale Atobatele General Manager Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Ltd ,Sanjay Rughani C.E.O; Standard Chartered Bank,Patrick Mususa: Manager: Projects & Business Development at Dar es Salaam Stock Exchange and Oswald Urassa:Chief Finance Officer at Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) and Moderated by Ambrose Nshala .

Different experts from the Panel were of the opinion that delegates may choose either equity or debt or even both depending on the nature of one’s business. Equity is not a very common method of financing business in Tanzania because it’s still a new concept for most Tanzanians as we used to be in a closed economy and the DSE was opened late in 1990’s so it emphases for Business to opt for this new concept here in Tanzania. Panelists were of the opinion that most people have been opting for dept part of debt as means of financing their businesses without losing ownership of the business and what is needed is people to have good credit profile and people to become ethical and trustworthy.
Mr Adebowale Atobatele commented that ‘’One reason as to why most people fail to repay loans is because they are borrowing more to finance their Life style rather than to expand their businesses.’’

Equity is when an investor or another business institution buys into the operations of a business, making the former a part owner of the entity. The money invested through the partnership can then be used to support the operations and expansions of the entity for the two to share profits as well as risks.

Mr Partick Mususa Urged that ‘’To list your company with DSE is one of the best and easiest way to finance the Expansion of your Business as for the DSE requirement only 25% shares of your company need to be sold to the public. We have great examples such as the Mwalimu commercial bank plc and many others who succeed because of IPO with more than 200,000 subscribers and their capital is increasing so fast through DSE. This is a great opportunity for other SMEs and Startup companies looking for ways to finance the expansion of their Business’’

Debt on the other hand is when a business entity borrows at an agreed interest rate from financial institutions to support its operations and according to Mr. Sanjay Rughani-The C.E.O of Standard Chartered Bank Tanzania as Tanzanians we need to change our culture, we need adopt good values such as transparency and compliance, to avoid borrowing without discipline and without insurance.

Also in the case of the judiciary we need cases on loan payment defaults to be sorted out quickly as the value of money changes over a period of time. We are really optimistic as for the reforms in the judiciary and some cases have already taken the fast track. Also the new regime is emphasizing more on these values and has waged a clear war on lack of transparency and corruption. This will create a more conducive environment for lenders and borrowers to work together.
While debt is repayable, mostly with interest and within a specified period of time, equity makes the investor a part of the business, with the option to exit at an agreed time.

Mr. Yacine Faqir Director General @D&B Credit Bureau Morocco aired his views that there is one underline denominator which is Trust, if you want to build a strong company you need to build trust with your staff, the same way if you want to build a great relationship with lenders you need to build trust by keeping your part of bargain, thus paying, and what is going on in Africa especially where i come from thus Morocco SME's need to build trust with Lenders.

One reason as to why interest rates are high is lack of trust as most people have been defaulting in paying, once this is changed even the central bank will want to calm down the situation as most Banks keep high interest rates because of fear of losing their money, so we need to build trust between Banks and SME's.

The theme, of 2nd Executive Breakfast Meeting which was full sponsored by Tanzania Financial services Expo 2016, was to expose participants and the entire business community to the advantages and disadvantages of the two sources of funding available to businesses in the country.

Waziri Kairuki awasisitiza watumishi wa Umma kufahamu kanuni za utumishi

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amewasisitiza watumishi wa Umma kufahamu kanuni za kudumu za utumishi wa umma ili kutambua haki zao na kuepuka kunyanyaswa na waajiri wao.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri huyo alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mipango na mikakati iliyowekwa na wizara yake katika kipindi cha uongozi wa awamu ya tano.

Waziri Kairuki amesema kuwa ni muhimu kwa watumishi wa Umma kufahamu kwa undani maadili yaliyowekwa na Serikali kwa ajili yao kwa kuwa yatawasaidia kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu.

“Inawezekana maafisa utumishi walikuwa wakizishikilia kanuni za utumishi wa umma na kuona kama ni za kwao kana kwamba mtu mwingine hatakiwi kuzifahamu lakini napenda kutoa rai kwa watumishi wote kuwa kanuni hizi ni za kwetu wote hivyo ni muhimu kuzifahamu”, alisema Mhe. Kairuki.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa kanuni za utumishi za mwaka 1994 zilirekebishwa na kwa sasa kanuni zinazotumika ni za mwaka 2009 ambazo zinapatikana katika tovuti za wizara mbalimbali hivyo upatikanaji wake umerahisishwa tofauti na zamani.

Pia amewataka watumishi kufuatilia waraka mbalimbali wa maendeleo ya kiutumishi inayotolewa na wizara hiyo kwa kuwa itawasaidia kufahamu miundo mipya ya utumishi inayotolewa, endapo mtumishi hatofahamu mabadiliko hayo atakosa taarifa muhimu.

Aidha, Waziri huyo amewakumbusha Maafisa Utumishi kuwa kazi hiyo wamesomea na watumishi ndiyo wadau wao wakubwa hivyo kwa namna moja ama nyingine kazi yao kubwa ni kuwasimamia na kuwahudumia vyema watumishi hao katika maeneo yao ya kazi.

“Napenda kutoa agizo kwa Maafisa Utumishi wote kufanya kazi zenu kwa umakini kulingana na kanuni za utumishi, kwa kuwa kazi hiyo mmeisomea basi ni lazima muwahudumie vizuri watumishi ili nao waweze kupata ufanisi zaidi wa kutekeleza majukumu yao”, alimalizia Mhe. Kairuki.

Wadau wa Michezo washauriwa kuwekeza katika Viwanda.

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi - WHUSM 

Wadau wa Michezo nchini wameshauriwa kujenga viwanda kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya michezo ili kuleta maendeleo katika sekta hiyo.

Ushauri huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizindua channeli mbili za Michezo za Kampuni ya king’amuzi cha TING.

Naibu Waziri Anastazia alisema kuwa kwa kupitia uwekezaji huo kutasaidia kuinua sekta ya michezo nchini pamoja na kuondokana na changa moto ya vifaa vya michezo jezi za michezo,mipira na vifaa vinginevyo.

“Tuunge mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuwekeza katika viwanda vitakavyotengeneza vifaa vya michezo” alisema Mhe. Anastazia

Aidha, Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa kuwepo kwa viwanda hivyo kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa vifaa vya michezo nchini kwani vifaa vingi vya vinatoka nje ya Tanzania hivyo huuzwa kwa bei ya juu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt. Veron Frenandes ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali wa Michezo nchini katika kukuza na kuendeleza sekta hiyo.

Chaneli za Michezo zilizozinduliwa katika Kingamuzi hicho ni ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 ambazo zitakuwa zikionesha michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.    

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikata utepe kuashiria uzindua wa Channeli mbili za michezo ambazo ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Said Kiganja akionesha zawadi ya King’amuzi aliyopewa na Kampuni ya TING wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni hiyo Agosti 28,2016.


aibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa Michezoalipokuwa akizindua uzinduzi wa Channeli mpya za Michezo kutoka kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt .Veron Fernandez akielezea kuhusu faida za channeli mbili mpya za michezo kutoka katika kampuni yake zitakavyosaidia kukuza Michezo nchini Agosti 28,2016.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt. Veron Fernandez wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.Picha na 
Raymond Mushumbusi - WHUSM
 

Serikali yaahidi kutoa ushirikiano kwa TECC

$
0
0
Serikali imeahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) inastawi na kufaidisha wananchi kwa kupitia miradi yake mbalimbali kwa maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.

Akizungumza hayo katika uzinduzi rasmi wa TECC Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa watendelea kuwa pamoja na Taasisi hiyo ili kufikia malengo ya watanzania kiuchumi.

“Kwa niaba ya serikali natambua mchango wa wajasiriamali hivyo tupo pamoja na TECC kwa kila jambo watalofanya kwa ajili ya kusapoti uchumi wa nchi kupitia ujasiriamali katika kuelekea uchumi wa viwanda.” Alisema Mhe. Jenista

Mbali na hayo Mhe. Jenista amesema kuwa malengo ya TECC ni kuimarisha ubunifu na ushindani wa biashara ndogo na za kati za Tanzania kwa kuwavuta wajasiriamali waliopo ndani ya sekta isiyo rasmi, wahitimu wa vyuo na wengine wenye kutaka kuanzisha biashara zinazoongeza thamani kwa mazao na kutengeneza bidhaa nchini.

Aidha Mhe. Jenista amesema kuwa Biashara zikianzishwa nyingi na nyingi zikijipanua kiushandi ndivyo na serikali itapata mapato zaidi kupitia kodi hivyo uzalishaji uongezeke zaidi na zaidi kwa maendeleo ya nchi.

“Natoa wito kwa taasisi mbalimbali kuiunga mkono TECC,” alisema, akiongeza kuwa fursa za kusaidia ziko nyingi kama kuwajengea uwezo kina mama wajasiriamali, wazee wanaostaafu, au kupanua programu ya Kijana Jiajiri katika mikoa mingine ya Tanzania.

Mbali na hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TECC, Bi. Beng’i Issa alisema tangu kuanza kazi miaka miwili iliyopita, kwa kutumia rasilimali chache, taasisi hiyo imeweza kujipanga na kuonyesha mafanikio makubwa katika kujenga uwezo wa wananchi kumiliki uchumi.

“Tunahitaji kufanya zaidi ya hapa na uwezo huo tunao kama tutaungwa mkono na Serikali kikamilifu ili kuweza kutekeleza wajibu wa sera yetu katika kunyanyua wajasiriamali kwa maendeleo ya taifa,” alisema Bi. Beng’i

Aidha Bi. Beng’i amesema kuwa mpaka sasa TECC imeshatekeleza miradi miwili muhimu ambayo ni mradi wa Kijana Jiajiri ambao unatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Uingereza la Youth Business International (YBI) na kufadhiliwa na umoja wa makampuni yanayochimba gesi na mafuta katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Bi. Beng’i amesema kuwa Kupitia mradi wa Kijana Jiajiri na ufadhili wa shirika la International Youth Foundation ambalo limepata fedha kutoka Master Card Foundation vijana 1,250 watajengewa uwezo katika mikoa ya Mtwara, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma kuanzia mwezi ujao wa Tisa.

Kwa mujibu wa Bi. Beng’i, mradi wa pili ambao TECC imeufanya ni kwa kushirikiana na mradi wa BEST-Dialogue wa kufanya utafiti wa maoni ya wamiliki wa biashara ili kupata changamoto ambazo zinazuia ushindani kibiashara katika mradi wa Business Leaders Perception.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua na Meneja wa Ofisi wa TECC, Bi. Mwasiti Mkembe (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (kushoto) akimkabidhi kitabu cha Mpango Kazi wa miaka miwili cha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya taasisi hiyo, Bi. Beng’i Issa wakati wa uzinduzi rasmi wa TECC mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Bi. Beng’i pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC), Bi. Beng’i Issa (wa pili kulia); mjumbe wa bodi hiyo, Dkt. Hassan Mshinda (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua (kushoto) wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Bi. Issa pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wakati Dkt. Mshinda pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Sehemu ya wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  

AIRTEL MONEY TIMIZA YAFANYA SEMINA NA MAWAKALA MKOA WA MWANZA

$
0
0

Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitia msisitizo zaidi katika semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.
Mawakala toka viunga mbalimbali ndani ya jiji la Mwanza wamekusanyika hapa ndani ya ukumbi wa Gold Crest Hotel kwa nia ya kupata mafunzo.
Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitoa semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.

Serikali yawataka Watanzania kuwapa Moyo Wanamichezo nchini

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewataka Watanzania kujifunza kuwatia moyo Wanamichezo wanaposhiriki katika michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Wito huo ameutoa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa Hafla ya kuwapongeza na kupokea bendera ya Taifa toka kwa Wanamichezo ambao walishiriki katika Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, nchini Brazil. Mhe. Nnauye alisema kwamba, Watanzania ni vizuri wakajifunza kusema maneno mazuri kwa wanamichezo pindi wanaporejea toka katika Mashindano mbalimbali ili kuwapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri wanamichezo hao huku akisisitiza kuwa, ni vema ukosoaji ukaendana na ushauri mzuri wenye kujenga badala ya kulaumu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (kulia) akimkabidhi cheti Mwanariadha Alphonce Simbu baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya tano katika Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.

Aliongeza kuwa, Wanahabari nchini wanapaswa kuandika mazuri yanayofanywa na wanamichezo kwani yana manufaa kwa Taifa badala ya kutafuta maneno yasiyo na tija ya kukosoa mara kwa mara kwani kuna wavunja moyo wanamichezo. “Tukijifunza kuandika na kusema mabaya tu ya kuvunja moyo kwa wanamichezo wetu hii sio sawa sawa, tujifunze kuwatia moyo, na hii ni hatua ya kwanza na wito wangu kwa Watanzania wote”, alisema Mhe. Nnauye

Alisisitiza kwamba, Watanzania wanapaswa kujifunza kujivunia vitu vya kwao kwa njia hiyo itakuwa ikiongeza hamasa kwa wanamichezo katika kujituma kwa manufaa yao na ya Taifa.

Aidha, alisisitiza kuwepo na maandalizi ya mapema kwa Wanamichezo nchini ili waweze kufanya vizuri zaidi huku akishauri uwekezaji wa kutosha katika sekta hiyo na kuyataka Makampuni kuwa na tabia ya kuwatumia Wanamichezo nchini katika kutangaza utalii wa nchi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (kulia) akimkabidhi King'amuzi cha Kampuni ya DSTV Mwanariadha Alphonce Simbu baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya tano katika Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.

Ametoa wito kwa Viongozi wazembe ambao watashindwa kufikia malengo mazuri katika tasnia hiyo ni bora wakaachia ngazi zao ili kuwapa nafasi watu wengine wenye uwezo kutekeleza kazi hiyo.

“Nadhani sasa tuanze kukabana kwenye Vyama, ukichaguliwa na kukawa na mashindano kama haya, ukashindwa kupeleka hata mchezaji mmoja, kazi yako ya kwanza nadhani ni kijiuzulu”, alisema Mhe. Nnauye.

Awali akitoa taarifa ya Wanamichezo walioshiriki katika Mashindano hayo, Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Gulam Rashid alisema kwamba, Tanzania ilishiriki mashindano hayo ikiwa na Wanamichezo saba, walimu wa tatu wa michezO ya kuogelea, Judo na riadha ambapo kati yao wachezaji wa nne walipata nafasi ya upendeleo (Universality).
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mataka akiongea na baadhi ya Viongozi, wageni waalikwa pamoja na Wanamichezo (hawapo pichani) walioshiriki katika Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.

Alifafanua kuwa, wachezaji wa nne waliofanikiwa kupata nafasi ya upendeleo ni wale ambao walishiriki katika michezo mbalimbali katika kusaka viwango, lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kufikia viwango vinavyowaruhusu wao kushiriki katika mashindano hayo, hivyo kulingana na Sera na itikadi za Olimpiki zilitaka kila nchi Duniani ambayo ni Mwanachama wa Mashindano hayo kutoa watu wake, hivyo walitoa nafasi hiyo kwa wale waliokosa kufikia viwango kuweza kushiriki.

“Nchi ambayo haikuwa na wachezaji waliofikia viwango vya Olimpiki walipewa nafasi ya upendeleo kwa wanamichezo kuweza kushiriki na kwa Tanzania tulikuwa na Waogeleaji wa tatu, mchezaji wa Judo na mchezaji wa kike wa mbio (Marathon) kwa hiyo, huo ndiyo upendeleo ambao wengi hawauelewi ni upendeleo upi”, alisema Bw. Gulam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki (TOC) Bw. Filbert Bayi akiongea na baadhi ya Viongozi, wageni waalikwa pamoja na Wanamichezo (hawapo pichani) walioshiriki katika Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.

Aidha, katika hafla hiyo, mbali na kukabidhiwa Bendera ya Taifa toka kwa kikosi hicho cha Wanamichezo walioshiriki katika Olimpiki 2016mjini Rio-Brazil, Mhe. Nnauye kwa niaba ya Makampuni ya TTCL na DSTV-Multi Choice aliwapatia zawadi mbalimbali washiriki hao zikiwemo fedha taslimu ambapo kwa nafasi ya kipekee Mwanariadha Alphonce Simbu ambaye aliibuka katika nafasi ya tano katika Mashindano hayo amepatiwa Mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa Balozi wa DSTV ambapo kila mwezi atakuwa akilipwa kiasi cha Shilingi milioni moja pamoja na king’amuzi maalum, huku washiriki wengine wakipewa ving’amuzi na fedha.

JUMUIYA YA WATANZANIA WALIOSOMA CHINA YAPATA UONGOZI MPYA

$
0
0

Jumuiya ya watanzania waliosoma China – CAAT wameishauri serikali kuwatumia wasomi hao katika kuhakikisha inanufaika na mikataba na masuala mbalimbali yahusuyo TANZANIA na CHINA. 


Wakizungumza katika mkutano mkuu wa kuchagua uongozi mpya wa jumuiya hiyo wanachama wa CAAT wameeleza kuwa Watanzania waliosoma China wanaijua nchi hiyo vizuri, tabia za wachina na lugha yao hivyo wakishirikishwa kabla ya kusainiwa kwa mikataba au kuingia makubaliano yeyote wanaweza kuwa chachu ya nchi kunufaika zaidi.

Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya hiyo Dk.Mhame Paulo aliyeenda kusoma china miaka ya 80 amesema, sera ya Tanzania ya viwanda inaweza kutimia ndani ya miaka mitano kwakuwa Tanzania inauwezo wa kuzalisha na kuuza katika soko la China akitolea mfano uwezo wa Tanzania kutengeneza dawa za kutibu ugonjwa na pumu na kuziuza katika soko la China na dunia kwa ujumla.

Mwenyekiti mpya wa CAAT, Dk.Liggyle Vumilia akishukuru baada ya kuchaguliwa amesema wanachama wa jumuiya hiyo wakitumika Tanzania itapata manufaa kwakuwa wanachama wake wanajua kuongea kichina, wanajua tabia za wachina na wanaielewa china vyema kiasi cha kujua kitu gani kinapatikana wapi hivyo serikali ikiwatumia itaepuka udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa wazalendo.

Uchaguzi wa jumuiya wa watanzania waliosoma China umewaweka madarakani viongozi wa masuala mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti, katibu, mwekahazina, mkurugenzi wa masuala ya bisahara na uwekezaji, mkurugenzi wa sanaa, utamaduni na utalii, mkurugenzi wa masuala ya elimu na Tehama pamoja na mkurugenzi wa takwimu , habari na mawasiliano.

Uhusiano wa Tanzania na China una zaidi ya miaka hamsini na watanzania wamenufaika na uhusiano huo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kwenda kusoma china na idadi yao kuzidi kuongezeka kila mwaka hali iliyopelekea kuundwa jumuiya watanzania waliosoma China. Tayari jumuiya hiyo ya watanzania waliosoma China imekwishapata usajili katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi tangu mwezi wa Juni 2016.

mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dk. Mahame Paulo akizungumza na wanajumuiya ya CAAT
Wanachama wa CAAT wakiwasikiliza viongozi wao wa mpito
Gustavu Sanga Gustavu Sanga mwenyekiti wa uchaguzi CAAT akitoa maelekezo kwa wajumbe wa CAAT

ATE WAZINDUA TUZO YA MWAJIRI BORA 2016.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua Tuzo ya Mwajiri bora wa mwaka 2016 ambayo itakuwa ikihamasisha na kuendeleza rasilimali watu ili kuleta maendeleo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa NHO, Joyce Nangai.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa NHO, Joyce Nangai.Baadhi ya wafanyakazi na waandishi waki msikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Aggrey Mlimuka.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE) wazindua Tuzo ya Mwajiri bora wa 2016 ambayo itakuwa ikihamasisha na kuendeleza rasilimali watu ili kuleta maendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania(ATE), Aggrey Mlimuka amesema kuwa kwa mwaka huu hafla ya tuzo hiyo itafanyika Desemba.

Mlimuka amesema kuwa lengo la tuzo hiyo ni kutambua wanachama wenye sera nzuri za usimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na makampuni mbalimbali mwanachama hapa nchini.

Amesema kuwa tuzo hiyo itafuata mbinu za Kisayansi na kitaalamu ili kuangalia umuhimu wa Rasilimali watu katika makampuni ya Kibiashara makubwa na madogo na yale ya kati ili kuinua ujuzi wa wafanyakazi wanaofanya kazi kwa kujituma sehemu zao za kazi.

Amesema tukio lakutafuta msihindi wa tunzo hiyo limegawanyika katika makundi mawili ambapo wataanza kufanya utafiti kwa kutumia Mshauri mwelekezi pamoja na kuwa na hafla ya tuzo itakayo fanyika Desemba mwaka huu.

Amesema kuwa kwa tunzo ya mwajiri bora mwaka huu wataangalia kipengele cha ushirikishaji wa watu wenye ulemavu pamoja na hali ya kujali wafanyakazi katika sehemu za kazi.

Mlimuka amesema kuwa tuzo hio pia itajikita zaidi katika kuangalia maeneo muhimu ya rasilimali watu, uongozi,utawala, usimamizi wa Rasilimali watu, kusaidia jamii pamoja na kuwajibika katika jamii, ubora na uzalishaji, amesema kuwa wanachama ashiriki kujaza kwa mkono dodoso kwaajili ya kushiriki.

BEI YA MADAFU LEO.

TAMASHA LA UHONDO WA ZANTEL LAKONGA NYOYO ZA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Meneja Habari na Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel,Winnes Lyaro (kulia)  akitoa maelezo kwa  baadhi ya wakazi wa Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la  Dares Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu huduma mpya zitolewazo na kampuni hiyo ikiwa ni moja ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya katika kuboresha bidhaa zake  na kutoa huduma bora kwa wateja. Ilikuwa ni katika tamasha lililopewa jina la Uhondo wa Zantel lililodhaminiwa na kampuni hiyo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetesa na wimbo wake maarufu wa ‘Unanitega Shemeji’, Selemani Jabil ‘MsagaSumu’ akifanya vitu vyake wakati wa tamasha la ‘Uhondowa Zantel’ lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Zantel.
 Meneja Habari na Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia)  akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa maswali ya papo kwa papo wakati wa tamasha la ‘Uhondo wa Zantel’ lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Tamasha hilo lililodhaminiwa na Zantel kama sehemu ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya katika kuboresha bidhaa zake na kutoa huduma bora kwa wateja.

MSANII NIGERIA ATOA MSAADA KWA KITUO CHA KULELEA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU CHA KIGAMBONI COMMUNITY CENTER

$
0
0


Na Sheila Simba

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Omo Alhaji,Jagabana maarufu YCEE,ametoa msaada wa shilling million 1,kwa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Kigamboni Community Center(KCC).

Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo jijini Dar es salaam mratibu wa ujio wa msanii huyo bi Salha Kibwana amesema kuwa msanii YCEE ametoa msaaada huo katika kituo hicho kwa lengo la kusaidia watoto hao ili kujipatia mahitaji maalum ya kila siku wawapo kituoni hapo.

“Ametoa msaada huo kutokana na faaida anayopata katika kazi zake usanii ili kukuza vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu wa elimu kwa jamii hasa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,”alisema Salha

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa kituo hicho Mbwana Msangule,amesema kuwa kituo chake kinalea watoto hao ili kuwasaidia kuondokana na maisha magumu yanayowakabili.

“msaada huu utasaidia sana kwasababu kituo kina watoto 14 wanaoishi kituoni hapo na wengine wanakuja na kurudi makwao,na nashukuru sana kwa msaada huu kwani ni sanii wa kwanza kutoka msaada,nawaomba pia wasanii wa ndani kijitokeza kutoa msaada”alisema Mbwana

Kwa upande msanii huyo amesema kuwa amekuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuonana na wasanii wengine wakubwa wa Tanzania huku akiwataja Diamond na Ali Kiba,ameongeza kuwa amefurahi pia kuktana na mashabiki wake ambao amekua wakichati kupitia mitanzandao ya kijamii.
 
Msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE kutoka Nigeria akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule(kushoto) leo Jijini Dar es Salaam Katikati ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.Msanii hyo yupo nchini kufuatia ziara yake kwa Vyombo vya Habari inayoratibiwa na Kampuni ya Mahusiano ya Umma ya LAS Consultancy. Picha na Frank Shija .


Mwanzilishi wa Kampuni ya Mahusiano ya Umma, LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt na Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tinny Entertainment kutoka Nigeria Arokodare Timilehin akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE (wa tatu kutoka kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt. 
Msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE kutoka Nigeria akizungumza na  waandishi wa habari kuhusu ziara yake katika Vyombo vya Habari inayoratibiwa na Kampuni ya Uhusiano wa Umma ya LAS Consultancy ya Jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto ni Mwanzilishi wa Kampuni ya LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana, Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina ya uongozi wa LAS Consultancy walipokuwa wakimtambulisha msanii kutoka Nigeria Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE ambaye yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kutembelea Vyombo vya Habari.

Wananchi wa Kanda ya Ziwa zaidi ya 750 wapata mafunzo Kilimo Biashara jijini Mwanza.

$
0
0
Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akitoa salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani).

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumzia malengo ya Kongamano la Kilimo Biashara kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) kufungua rasmi.
Mwezeshaji ambaye pia ni Rais wa vijana wajasiriamali na wataalamu wa miradi ya maendeleo mkoa wa Singida, Philemon Kiemi akitoa mafunzo ya ufugaji kuku wa kisasa kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

BREAKING: SERIKALI YAVIFUNGIA VITUO VIWILI VYA REDIO LEO JIJINI DAR

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amezifungia radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi ambavyo vimerushwa hewani vinavyoashiria uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Nape amesema kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baada ya kujirdhisha kuwa kipindi cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016 muda wa saa 2 usiku hadi saa 3 na kituo cha utangazji cha Radio 5 pamoja na kipindi cha Morning Magic katika kipengele cha Kupaka Rangi Agosti 17 vilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa Amani.

Nape amesema kuwa kufuatia hilo amevifungia kwa muda usiojulikana kwani wamekiuka masharti ya kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.

Wakati vituo hivyo vikifungiwa kwa muda usiojulikana kamati ya maudhui imepewa jukuu la kuviita na kusikiliza kwa kina Zaidi utetezi wao na ni hatua gani zaidi ya kuchukua dhidi yao kwa mujibu wa kanuni ya huduma za utangazaji.

Nape ameendelea kuvitahadhalisha vyombo mbalimbali vya habari kutoshawishika kuvunja sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ili kulinda heshima ya tasnia yetu na wakati huo kuhakikisha nchi inabaki na Amani, Mshikamano na Umoja. 
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, wakati akitangaza kuzifungia radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi na kuvirusha hewani ambavyo vinaashiria uchochezi. 

Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akitoa  ufafanuzi alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Wanahabari,wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kivifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi vyenye maudhui yenye viashiria vya uchochezi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUHARIBIIKA KWA MASHINE YA MRI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inapenda kuujulisha umma kwamba mashine ya MRI itasimama kwa muda kufanya kazi baada ya kuharibika. Mashine hii iliharibiika tarehe 24/08/2016 baada ya kutokea hitilafu ya umeme.

Baada ya kuharibiika, tarehe hiyo (24/08/2016) mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wetu walianza kutafuta athari baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.

Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi.
Hospitali ya Taifa Muhimbili inawaomba radhi wananchi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Imetolewa na:

                                                                                        John Stephen, Ofisa                                                                                                      Uhusiano,
                                                                                            Kitengo cha Mawasiliano ya                                                                                                                             Umma                                                                                                                      na Huduma kwa Wateja,
                                                                                         Hospitali ya Taifa Muhimbili 
                                                                                     Tarehe 29/08/2016.

TEASER JOTO LA ASUBUHI AUGUST 30 JUMANNE

MAGAZETINI LEO JUMANNE AGOSTI 30

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live


Latest Images