Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1337 | 1338 | (Page 1339) | 1340 | 1341 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Agosti 22, 2016 Umoja wa Vijana wa CCM tuliutangazia umma na dunia kwamba ifikapo Agosti 31 mwaka huu tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwa utendaji wenye tija, ufanisi na uliorudisha imani na matumaini kwa wananchi.

  Msimamo na dhamira ya kufanya maandamano hayo ya amani yenye maudhui na kusudio hilo, bado uko pale pale ingawaje si kwa tarehe tuliopanga na kutangaza awali yaani Agosti 31 mwaka huu.

  Jumuiya yetu kama mjuavyo ni ya Vijana wa CCM, (UVCCM) inapata malezi kwa karibu mno na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Wiki ya jana Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Nd. Abdallah Bulembo alikutana na waandishi wa habari akitutaka UVCCM tuahirishe maandamano ya Agosti 31 mwaka huu hadi wakati mwingine.

  Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi ndiyo Msimamizi wa Malezi, Maadili na Adabu kwa Vijana wote nchini, sisi UVCCM tunaamini kuwa sikio halishindani na kichwa, mtoto ni mtoto kwa Wazazi wake hakui, hana jeuri wala ubishi.

  Mtoto au watoto wanaokaidi amri, ushauri au maelekezo ya Wazazi wao huitwa watukutu, wenye viburi, manunda na wasioambilika. UVCCM si watukutu, hatukufunzwa tuwe wabishi, wakaidi na wenye viburi. Tumezingatia kutii maelekezo, makatazo na maonyo , tumeambiwa tuahirishe maandamano yetu nasi tumekubali na kuheshimu mambo tuliyoaswa.

  Sambamba na hilo tumepata majibu ya barua yetu tuliyomwandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernes Mangu) inayotutaka tuache kufanya maandamano yetu kwa sababu Polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa na maandamano nchi nzima.

  Jambo jingine ambalo limetufanya pia tuahirishe maandamano yetu ya Amani ni taarifa ya kintelejinsia iliowasilishwa na Kamati yetu ya Usalama na Maadili ya UVCCM mbele ya kikao cha Sekreteriet yetu, nayo ilipendekeza  suala hilo liahirishwe kwa wakati huu hadi muda mwingine.

  Pia jambo jingine ambalo limefanya maandamano hayo tuyabatilishe ni kulipisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambalo litakuwa katika shughuli za maadhimisho miaka 52 tokea kuanzishwa kwake. 

  Wanajeshi wetu watakuwa katika kazi mbalimbali za kijeshi kwenye kambi zao na mitaani kufanya usafi wa mazingira, hivyo isingependeza na wala si heshima wakati sisi tukiandamana, wao wakifanya kazi muhimu kila mmoja wetu zinazomgusa badala yake ni vyema kuwaunga mkono jambo wanalolifanya la usafi wa mazingira. 

  UVCCM tumekubali, hatutaki kuingia katika uvunjaji wa sheria hasa baaada ya kutakiwa kuahirisha na mamlaka za Kisheria hadi wakati mwingine muafaka na si wakati huu.

  Tunaelewa kwamba uamuzi wetu wa awali wa kutaka kuandamana kwa amani hata kama tungenyimwa kibali ungetugharimu, ungetusababishia madhara na pengine hasara, kwa wakati huu na kuona jambo lenyewe ni la kuipa Ari serikali katika kuhimiza Uwajibikaji, Utendaji na Usimamizi bora wa Uendeshaji wa masuala ya kiutawala.

  Tulishusha maagizo kwa Makatibu wetu wote wa Mikoa yote 32 na Wilaya 171 ya Kichama tukiwataka waandike barua katika Ofisi za Ma RPC na OCD, washirikiane ili kuratibu maandamano na kuyafanikisha kama tulivyokusudia.

  Watendaji wetu wa ngazi husika wamefuata maelekezo, wametii taratibu zetu za kiutendaji na leo tumewajulisha tena wasitishe maandamano hadi tutakapowapa tena maelekezo mengine. Tunawahimiza na kuwataka ni vyema kutii mamlaka za Kikanuni na Kisheria.

  UVCCM kwa wakati huu tumeamua kuachana na maandamano badala yake tunajikita katika matayarisho ya kuwapeleka Vijana wetu wakashiriki katika Mafunzo ya Siasa, Utawala, Uongozi, Ufundi na Ujasiriamali yatakayoanza kufanyika katika Chuo chetu kilichopo huko Ihemi Mkoani Iringa ambapo kitakuwa kielelezo na alama nzuri ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa vitendo.

  Tumewataka Makatibu wetu wa Mikoa na Wilaya kuendelea na zoezi la Uratibu na Uhakiki kwa Vijana ambao watateuliwa kushiriki Mafunzo hayo huko Ihemi.

  UVCCM tunarejea kusema tena kwamba dhamira ya maandamano yetu ya kusifu Utendaji wa Serikali ya awamu ya tano iko pale pale ila tutapanga tarehe nyingine katika wakati ujao badala ya kufanyika Agosti 31 mwaka huu kama tulivyotangaza hapo awali.

  UVCCM tunawataka Vijana wote kuendelea kuheshimu Tunu ya Amani Umoja na Mshikamo wetu kwa Taifa.


  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
  Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
  KAIMU KATIBU MKUU.

  0 0

  Shirika la ndege la Rwanda (Rwandair) linataraji kuingiza ndege zake mbili mpya aina ya Airbus A330 zenye uwezo wa kubeba abiria 276. akizungumza ofisini kwake jijini Dar es salaam, Meneja mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Ibrahim Bukenya amesema kuwa ndege hizo zitaanza safari zake kuelekea miji ya Bombay nchini India na Guanghzou nchini China zikitokea Mjini Kigali Rwanda. ndege hizo zitawasili kabla ya mwisho wa mwaka huu.

  0 0

  Ofisa Mafunzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS, Ashura Kassim (kulia) akimuandikisha Bi. Azina Ramadhani mmoja wa watu  waliofika katika banda lao wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mafuzo Idara ya Uendeshaji, Doris Mlenge na wa pili kulia ni Ofisa Masoko na Uhusiano, Waziri Ramadhani.
  Ofisa Masoko na Uhusiano, Waziri Ramadhani (kushoto), akitoa elimu juu ya  Uwekezaji wa Pamoja kwa mmoja wa watu waliotembelea banda lao.
  Wananchi wakijiandikisha katika Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS.
  Ofisa Mafunzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS, Ashura Kassim akitoa maelekezo kwa mmoja wa watu waliotembelea banda la UTT-AMIS.


  0 0

  Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar, Wanamkurukumbi wakiteta jambo leo kwenye Uwanja wa Kaitaba kwa mara ya kwanza Tangu Uwanja huo ukamilike hivi karibuni. Na sasa ukiwa tayari kwa Michezo mbalimbali ikiwemo Mitanange ya Ligi Kuu Vodacom. Kagera Sugar wanajifua kujiandaa kwa Mchezo wao wa tarehe 3 Septemba, 2016 dhidi ya Mwadui kutoka Shinyanga ambapo nmchezo huo utapigwa katika Uwanja huo ambao umejengwa tayari kwa Viwango vya Fifa. ‘Wanankurukumbi’ walipambana hadi siku ya mwisho kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu uliopita wakiwa na kocha wao Adolf Rishard na sasa wakiwa na Kocha mpya msimu huu mpya 2016/2017 Mecky Mexime ambao pia wamefanya usajili wakiwemo makipa. Leo wameanza kujifua kwenye Uwanja wao kwa ajili ya kuhakikisha hawakumbwi na gharika iliyowakosa msimu uliopita na hatimae kufanya vyema kwa msimu huu ambao umeanza kwa aina yake wakianzia ugenini mechi zao mbili za mwanzo.
  Wakiomba kabla ya kufanya Mazoezi leo hii jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.
  Mwenyekiti wa kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama ambaye pia ni Katibu wa KRFA (katikati) kulia ni Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), WALLACE KARIA nao walikuwepo Uwanjani hapo kujionea Uwanja huo ambao umemalizika kwa kusuasua. 
  Mecky Meximeakitoa maelekezo kwa wachezaji wake leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba, Wakijiandaa kuikaribisha Timu ya Mwadui hivi karibuni.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Bashir Yakub.

  Kampuni ya umma ndio huitwa public company kwa kiingereza. Kampuni hii hutofautishwa na kampuni binafsi (private company). Zote ni kampuni kwa ajili ya biashara na mara zote hutegemea unahitaji kufanya nini ili ujue ni kampuni ipi uunde.

  1.JE KAMPUNI YA UMMA INAWEZA KUMILIKIWA NA WATU BINAFSI.

  Ndio inawezekana. Watu wengi hudhani kwa kuwa jina la kampuni hii ni UMMA basi hudhani ni kampuni ambazo huundwa na serikali. Neno umma ni jina na limetokana na namna muundo wa kampuni yenyewe ulivyo , yumkini halina uhusiano wowote na kampuni za namna hii kumilikiwa na serikali.

  Hivyo yafaa ifahamike kuwa hata wewe mtu binafsi mjasiriamali wa kawaida waweza kuunda kampuni ya namna hii pengine kutokana na faida zinazotokana na kampuni ya aina hii.

  2.KWANINI UUNDE KAMPUNI YA UMMA BADALA YA KAMPUNI BINAFSI.

  ( a ) Uhuru wa wanahisa. Kampuni ya umma imetoa uhuru mkubwa kwa wanahisa. Wakati kampuni binafsi inaruhusu kuwa na wanahisa mwisho 50 kampuni ya umma haina ukomo wa idadi ya wanahisa.

  Hii ina maana waweza kuwa na wanahisa hata milioni na zaidi. Hakuna ukomo wa kiwango cha mwisho isipokuwa kuna ukomo wa kiwango cha chini. Kiwango cha chini yalazimu wanahisa kuanzia wawili.

  ( b ) Uhuru wa kuuza na kununua hisa. Katika kampuni binafsi hakuna uhuru wa kununua na kuuza hisa. Katika kampuni binafsi yatakiwa kabla hujauza hisa zako kwa mtu mwingine upate ridhaa ya wanahisa wenzako. Wakikataa huwezi kuuza.

  Lakini pia huwezi kumuuzia hisa mtu ambaye wanahisa wengine hawampendi. Yule wanayempenda na kumridhia ndiye huyo unayeweza kumuuzia tu na si vinginevyo.


  0 0

  Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia Dk Bernald Achiula akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo wakati akishukuru wanafunzi wa chuo hicho kwa michango yao waliyochanga ili kumsaidia mwanafuzni mwenzao Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ana matatizo ya kusikia, wanafunzi hao wamechanga Fedha na kumnunulia mwenzao Vifaa vya kumsaidia kusikia vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano, Kulia ni Mwanafuzni Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ameelezewa kuwa ana uwezo mkubwa katika masomo yake darasani pamoja na kutokuwa na uwezo wa kusikia, na Katikati ni Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.
  Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia akielezea kwa waandishi wa habari kuwa kitu kilichowafanya wanafunzi wa chuo hicho kumchangia mwanafunzi mwenzao Shinuna Salum Kulia ni kutokana na uwezo wake katika masomo pamoja kuwa tatizo la usikivu linalomkabili.
  Mwanafuzni huyo Shinuna Salum Nyamkokwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea kuhusu msaada wa vifaa hivyo ambapo amesema awali kichwa kilikuwa kinamuuma sana lakini kwa sasa hakiumi tena.
  Gordian Kilave Mkuu wa Idara ya Lugha Chuo cha Diplomasia akielezea matatizo yaliyokuwa yakimkuba na kumsumbua mwanafunzi Shinuna Salum kabla ya kupatiwa vifaa hivyo ambavyo ninamsaidia kusikia kwa sasa.

  0 0

  Na Mathias Canal, Singida

  Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Mkoa wa Singida wamekabidhiwa jumla ya madawati 90 kwa kila Halmashauri ili kuondoa adha waliyokuwa wanakumbana nayo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipowaagiza wakuu wa mikoa yote nchini wakati akiwaapisha Ikulu, jijini Dar es Salaam Machi 15, 2016.
  Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa chini wakiwa darasani.
   Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba na wadau wa maendeleo Mkoani humo.


  0 0

  Profesa Julius Nyang'oro ni Mwalimu, mtaalam wa sayansi ya siasa na mwanasheria.
  Amekuwa mwalimu tangu mwaka 1977 nchini Tanzania na hapa nchini Marekani.
  Ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 14, vingi vikiigusia Tanzania kwa namna moja ama nyingine. Moja ya vitabu alivyoandika, na ambavyo vilimtambulisha zaidi kwa jamii ya waTanznia, ni kumhusu Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete. Ambapo ameandika vitabu viwili kumhusu.
  Prof Nyang'oro alikuwa mkarimu sana kuungana nasi kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu ya Agosti 29, 2016 kuzungumzia mambo mbalimbali kuihusu Tanzania akiwa mwandishi, mwalimu, mtaalamu wa mausala ya siasa na mwanasheria
  KARIBU

  0 0

   Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw . Mohamed Seif kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume hiyo akikabidhi kwa Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog, Bw. John Bukuku Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mgahawa wa Mokka City Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog, Bw. John Bukuku akiwa na Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015 mara baada ya kukabidhiwa rasmi.

  Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog, Bw. John Bukuku akionesha
   Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015

  0 0

  New Upcoming artist goes by the name Topazz Millenium release his first Rnb video song called " SIJIWEZI" produced by AM Records, The video was directed by pdk films studios.

  0 0


  0 0

  Meneja Msimamizi wa masuala ya Usalama wa Vodacom Tanzania, James Wawenje (kulia) na Ofisa Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Jehud Ngola (kushoto),wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati) akiwasilina na Hassan Mfaume Mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambaye aliibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 5/- katika droo ya wiki ya promosheni ya ‘Kamata Mpunga’inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Jumla ya washindi 224 wamepatikana tangu kuanza kwa promosheni hiyo.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya.

  Na Mathias Canal, Singida
  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru katika kituo cha Afya cha Mlali kilichopo Katika Kata ya Mlali Wilayani humo kusikiliza kero wanazokumbana nazo wakati wanapofika hospitalini kupatiwa tiba.
  Huu ni muendelezo wa ziara za kusikiliza kero za wananchi nakuzitatua kwa dhamira ya kupunguza na kuziondoa kabisa kero ndogo ndogo ambazo zimesababishwa na wananchi wenyewe ama watendaji wa serikali katika maeneo yote ya Wilaya hususani sekta ya Afya.
  Mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha Afya alitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo majengo mbalimbali, wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo kiasi cha kupelekea kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.

  Licha ya jengo hilo kujengwa chini ya kiwango chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhudumu katika Wilaya hiyo.
  Hata hivyo kufuatia kadhia hiyo Mhe Ndejembi ameagiza Mkandarasi kutafutwa haraka iwezekanavyo ili aweze kuhakikisha jengo hilo linarekebiswa upwa kwa kutumia gharama zake mwenyewe.
  Dc Ndejembi amemtaka mganga mkuu wa Kituo cha afya Mlali  kuhakikisha anasimamia vyema Mali na majengo ya umma ili kuendelea kutoa huduma nzuri na zenye ufanisi kwa kila Mtanzania anayefika katika Zahanati hiyo.

  Kwa upande wa wananchi waliofika kupatiwa huduma kutoka katika Kijiji cha Mlale na maeneo Jirani wamesema kuwa huduma zinazotolewa katika Kituo hicho cha Afya zina ahueni kubwa huku changamoto kubwa ikiwa ni uduni katika huduma za chanjo kwa watoto kwani hawapati huduma hiyo kwa wakati.
  Sambamba na hayo Dc Ndejembi ameagiza kusimamiwa haraka na kutatuliwa kwa kadhia hiyo ili wananchi wafurahie huduma bora zitolewazo katika vituo vya Afya sawia na kuimarisha Afya zao ili kufanya Kazi kwa salama na kuitikia dhana ya HapaKaziTu kwa vitendo.

  Dc Ndejembi alipotembelea wodi wa wagojwa 
  Dc Ndejembi akisisitiza jambo kabla ya kuondoka katika kituo cha afya Mlali


  0 0

  Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake.

  Familia ya marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo (pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi, kwa ajali ya gari.

  Familia inapenda kuwashukuru kipekee Wakwe wa marehemu - familia ya Mzee Edriss Mavura;  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Prof Elifas T. Bisanda pamoja na uongozi wa chuo na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT); 

  Uongozi na wafanyakazi wote wa Shirika la Afya duniani (WHO) Uganda na Tanzania; Dr Harvinder Palaha wa Aga Khan Hospital, na madaktari wenzie, wauguzi na wafanyakazi wote wa Aga Khan Hospitali kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU); 

  Mzee wetu Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi; Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania na Bw. Ziya Kaharan, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki; Prof. Fatmahan Atalar, Mkurugenzi wa MUHAS Genetic Laboratory ya Chuo Kikuu cha Muhimbili; Wanajumuiya wa Ikungi Development Association (IDEA); Umoja wa Wanafunzi waliosoma Uturuki, Masheikh wa Dar es Salaam na Ikungi; na Majirani wote wa Dar es Salaam na Singida.

  Kwa kuwa si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja, tunaomba wote mlioguswa na msiba huu mpokee shukrani zetu za dhati.

  Tunapenda kuwataarifu kuwa Dua ya arobaini (40) ya marehemu itasomwa Jumamosi, tarehe 03 Septemba 2016, Makiungu-Ikungi, Singida, saa 5 asubuhi Wote mnakaribishwa.
  INNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUUN.

  0 0

   Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote jijini Dar es Salaam leo.

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kumi na nne ya Siku ya Wahandisi yatakayofanyika Septemba mosi hadi pili jijini Dar es Salaam.

  Maadhimisho hayo ya siku mbili yanatarajiwa kukutanisha zaidi ya wahandisi elfu mbili kutoka ndani na nje ya nchi ili kupata fursa ya kufanya majadiliano ya kitaaluma, kufanya maonesho ya kiufundi na kibiashara, kuwatambua na kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo yao ya mwisho na kuwaapisha wahandisi waliokidhi vigezo.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote amesema mada kuu katika maadhimisho hayo itakuwa ni “TANZANIA KUELEKEA KUWA NCHI YA UCHUMI WA KATI NA KUWA NCHI YA VIWANDA: NINI JUKUMU LA WAHANDISI”.
  “Tumejipanga Siku ya Wahandisi mwaka huu iwe na mvuto wa pekee kwa sababu mada yake ni ya kitaifa ikiangalia Dira ya Maendeleo ya Taifa na mwelekeo wa nchi kuwa nchi ya viwanda” amesema Eng. Mlote.


  Maadhimisho ya wahandisi Tanzania yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2013, lengo likiwa ni kuiwezesha jumuiya ya wahandisi nchini kuionesha jamii kile ambacho wahandisi wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo ya nchi.

  Takribani wahandisi elfu 17 wanakadiriwa kuwepo nchini katika sekta mbalimbali, lengo likiwa ni kuwa na wahandisi elfu 83 ili kukidhi mahitaji ya nchi kuwa ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  JIJI la Dar es Salaam linatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa awamu ya nne wa hoteli za Africa ambapo wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wapatao 200 wanatarajiwa kuhudhuria kuzugumzia masuala muhimu katika sekta ya ukarimu.

  Mkutano huu umeandaliwa na kuratibiwa na kampuni ya kimataifa ya LNoppen na HD Partnership ambapo wameingia katika makubaliano ya kuandaa mkutano huu. Wadau na wamiliki wa hoteli wanaweza kuhudhuria katika mkutano huu kwa kujiandikisha kabla ya tarehe 6 Septemba kupitia tovuti ya africa.hotelandresortsummit.com.

  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya LNoppen Group amesema, “ Tanzania ni nchi iliyo juu kwa kutembelewa na wageni mbalimbali kutoka barani Afrika na mataifa mengine. Kampuni nyingi za kimataifa zimewekeza nchini Tanzania na nchi inazidi kuimarika katika kanda ya Afrika. Tumeona ni vyema mkutano wa mwaka huu tuufanye nchini Tanzania kutokana na fursa zilizopo hapa hasa katika sekta ya Utalii na Ukarimu”.

  Nchi zilizoandaa mkutano huu katika miaka iliyopita ni Ghana 2014, Sengal 2015 na Nigeria Januari 2016.
  Katika siku mbili za mkutano huu mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya ukarimu na utalii yatajadiliwa ikiwa pamoja na usimamizi wa mapato, marejesho ya mtaji, rasimali watu na ajira, huduma bora kwa wateja na ushindani katika sekta ya Utalii Afrika. Majadiliano yatafanyika katika paneli ambapo tafiti zitajadiliwa kwa kina. Mkutano utafunguliwa na Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye atatoa utambuzi wa sera za serikali na vichocheo kwa wawekezaji nchini Tanzania.

  Akiongelea umuhimu wa Mkutano huu, Meelis Kuuskler, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa HD Partnership amesema, “ Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa namna hii, mkutano huu hautatangaza Tanzania kama kitovu cha Utalii peke yake bali utatangaza nchi kwa wawekezaji na jumuiya ya maendeleo kwamba Tanzania ipo wazi kwa biashara''
  Wadau mbalimbali wa sketa ya Utalii na Ukarimu wanasisitiziwa kuwa watapata fursa ya kuhudhuria mkutano kwa kujiandikisha kabla ya tarehe 6 Septemba 2016. Kujiandikisha na kupata taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya africa.hotelandresortsummit.com.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, ACP Sida Mohammed Himid ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ anayeshughulikia Idara maalum za SMZ.

  Ndugu Hassan Khatib Hassan ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto anayeshughulikia masuala ya Wazee, vijana, wanawake na Watoto.

  Dkt. Ali Salim Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja katika Wizara ya Afya.

  Uteuzi huo umeanza leo tarehe 30 Agosti, 2016.
  Bw. Mohammed Kheir Mtumwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuanzia tarehe 28 Agosti, 2016.
  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  MBUNGE wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amechangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha daraja litakalounganisha kata ya pangani iliyopo halmashauri ya mji Kibaha Mkoa wa Pwani na mpiji magoe iliyopo kata ya kibamba manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

  Daraja hilo ambalo linatarajia kujengwa kwa ushirikinao wa Jeshi la wanachi Tanzania (JWTZ) litakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya Kibaha pamoja na wale wanaotoka katika kata ya kibamba sambaamba na kuwasaidia wanafunzi pamoja na wakinamama ambao walikuwa wanashindwa kuvuka wakati wa masika.

  Akizungumza katika halfa ya fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kufanya harambee wa daraja hilo Koka amesema litagharimu milioni 36 na kwamba JWTZ tayari wameshakubali kusaidia ujenzi huo ambapo ukikamilika utaweza kutoa fursa mbali mbali za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo lake pamoja na kuondokana na kero ya kuvuka nyakati za masika.

  “Mimi kama mbunge wenu hii changamoto ya wananchi wangu naifahamu kwani wamekuwa wakipata tabu sana wakati wa kuvuka hasa katika kipindi cha mvua ukizingatia daraja hii lilolopo kwa sasa linahatarisha masiha ya watu kutokana limejengwa kwa miti,lakini hili ambalo litajengwa na JWTZ litaweza kusaidia na kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa panagani na maneo mengine,”alisema Koka.

  Aidha Koka aliongeza kuwa katika kuhakikisha daraja hilo linajengwa ataendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo ikiwemo wawekezaji ambao wamewekeza katika kata ya pangani ili waeze kusaidiana nao na kuweza kutimiza malengo ambayo wamejiwekea ya kuwaletea mabadiiko chanya ya kimaendeleo.

  Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kata ya pangani akiwemo Musa Maige pamoja na Hamisi Ugo Wananchi wanapata shida kubwa ya kufuata huduma za afya kwani wanatembea zaidi ya umbali wa kilometa 11 mpaka maili moja na kupelekea wakati mwingine baadhi ya wakinamama wajawazito kujifungulia njiani wakati wakwenda kupatiwa matibabu.

  Mmoja wa wakinamama aliyejtambuisha kwa jina la Subira Ally hapa anaelezea jinsi wanavyopata shida hasa wakati wa kujifungua, pamoja na watoto wao ambao wanasoma shule wanavyopata shida katika kipindi cha masika kwani daraja linajaa maji na kujikuta wanashindwa kuvuka katika mto huo.

  Nae Diwani wa Kata ya Pangani Augustino Mdachi alisema kwamba kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutaweza kuwasaidia wananchi wake ambao walikuwa wanateseka kwa kipindi cha muda mrefu kuweza kuvuka kwa urahisi na kuendelea kufanya shughuli za mbali mbali za uzalishaji na kuleta maendeleo.

  Awali akisoma risala katika hafla hiyo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Pangani Abdlah Ngulengule hapa anabainisha changamoto ambazo zinakwamisha kuanza kwa ujenzi huo wa daraja pamoja na mikakati waliyojiwekea ili kufanikisha zoezi hilo.

  KIVUKO cha awali ambacho walikuwa wanakitumia ni cha miti hivyo wakati wa mvua inaponyesha kinafunikwa na maji hivyo kuwapa wakati mgumu wananchi hao na kuwalazimu kutumia usafiri wa pikipiki kwenda maili moja kwa ajili ya kufuata huduma ambapo nauli ni kati y sh.20000 hadi 30000.
  Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwa na wananchi wa kata ya pangani pamoja na viongozi wengine wa serikali kwenda katika kuangalia sehemu amabyo itajemgwa daraja hilo la Pangani.
  Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka wa katikati akikagua sehemu ambayo itajengwa daraja hilo la pangani, ambalo litagharimu kiasi cha shilingi milioni 36, ambapo daraja hilo linatarajiwa kujengwa chini ya usimamizi wa JWTZ.PICHA NA VICTOR MASANGU

  0 0

  Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA ya sasa na ile tuitakayo.
  Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kutoa maoni kulingana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania na ukuaji wa Demokrasia ya nchi yetu.
  KARIBU

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KLABU ya Simba imekubali mwaliko wa kwenda kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Polisi Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kuhamia Mkoani Dodoma.

  Mwaliko huo umeletwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mulamu Nghambi ambaye amesema kuwa wao kwa pamoja wanaunga mkono juhudi za Rais za kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani kwao kwani zitaleta maendeleo makubwa.

  Nghambi amesema, walituma maombi yao kwa uongozi wa klabu ya Simba wa Kuonesha nia ya kushirikiana katika harakati hizo kwani mkoa wa Dodoma una mashabiki wengi wa timu ya Simba na mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 03 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamefurahi kupata mwaliko huo na kwa kuwa hakuna ratiba ya ligi wikiend hii nawaahidi mashabiki wa Simba mkoani Dodoma kusubiri ujio wetu kwa shangwe zote.

  "Katika kuhakikisha tunaunga mkono hoja za Rais John Pombe Magufuli za kuhamishia makao makuu ya nchi Mkoani Dodoma na Chama cha Mpira wa Miguu mkoani humo kutupatia mwaliko tumeupokea kwa mikono miwili na tunawataka wanachama na mashabiki wa timu ya Simba kuja kushuhudia mchezo wetu na Polisi Dodoma siku ya Jumamosi Septemba tatu mwaka huu,"amesema Manara.

  Kikosi cha Simba kitaondoka Alhamisi wakiwa na wachezaji wao wote waliosalia baada ya wengine kuwepo kwenye majukumu ya timu zao za Taifa.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) Mulamu Nghambi akizungumza na waandishi wa habari akielezea kuhusiana na kuunga mkono juhudi za Mheshima Raisi John Magufuli za kuhamishia makao makuu mkoa wa Dodoma Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Haji Manara.
  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Haji Manara akizungumza na Waandishi wa habari leo kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli za kuhamia Dodoma na kuridhia timu yake kwenda kucheza mechi ya kirafiki na Polisi Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dodoma (DOREFA) Mulamu Nghambi.

older | 1 | .... | 1337 | 1338 | (Page 1339) | 1340 | 1341 | .... | 3286 | newer