Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1309 | 1310 | (Page 1311) | 1312 | 1313 | .... | 3353 | newer

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akiwa na baadhi viongozi wa vijiji wakielekea eneo lengine kukutana na wananchi na kuyasikiliza na kutatua matatizo yao kwa namna moja ama nyingine wilayani Mkuranga,mkoa wa Pwani
   Mbunge Abdallah Ulega akijionea hali halisi ya miundombinu ya usafiri kwa wananchi wake wa Mkuranga mkoani Pwani
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na  wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata shungubweni wilayani Mkuranga katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
   Shabani Omary  akiuliza swali kwa mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega leo mkoani Pwani
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na walimu wa shule ya  msingi  kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya shungubweni  leo mkoani Pwani.

  wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata shungubweni wilayani Mkuranga wameshauliwa kuchukua shamba lenye ukubwa wa hekari 66.6 ambalo alipewa mwekezaji Salim tangu mwaka 1988 na kushindwa kuliendeleza,ili walitumie Kwa shughuli za kuzalisha mali.

  Ushauri huo ulitolewa wilayani humo na Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega mara baada ya kupokea malalamiko Kutoka Kwa wananchi wake akiwa katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.

  Ulega alisema haiwezikani watu wanajimilikisha mashamba makubwa miaka hadi miaka alafu wanashindwa kuyaendelea huku wananchi wakipata shida ya kukosa maeneo hata ya kulima kilimo cha mbogamboga vijana.

  "Nasema kuwa kama shamba hilo limekaa miaka yote hiyo haliendelezwi, napia huyo mwekezaji haonikani sasa mnasubiri nini kulichukua na kufanya uendelezaji,nashauri litwaeni alafu tutapambana nayo huko mbele"

  Pia Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa siasa imekwisha na kilichobaki ni watu kufanya Kazi Kwa nguvu zote na kwamba atakuwa bega Kwa bega katika kuhakikisha maendeleo wanayapata Kwa haraka.

  Awali wananchi wa kijini cha Kurutu walimweleza mbunge kuwa wanashamba kubwa ambalo alipewa mwekezaji miaka mingi iliyopita tena kienyeji lakini hadi leo ameshindwa kuliendeleza hivyo awasaidie walipate ili vijana wa eneo hilo wazalishe chumvi.

  Mbunge huyo bado anaendelea na ziara zake za kutembelea kijiji hadi kijiji kwa lengo la kuwashukuru na kuhimiza shughuli za maendeleo ambapo anawataka kujituma katika kufanya kazi kwani wilaya hiyo imechelewa kimaendeleo.


  0 0  Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Maiko Lekule Laiser ,akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda, aliyepo kushoto kwa mkuu huyo ni mwenyekiti wa Taso kanda ya Kaskazini ndugu Athar Kitonga Shayo wakiwa katika uzinduzi wa maonyeho hayo ya wakulima na wafugaji katika viwanja vya Taso Themi nanenane Njiro Jijini Arusha.


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda amewataka Wakurugenzi wote wa Mikoa yote mitatu iliyopo Kanda ya Kaskazini ,wabadilishe mabanda yao na wajenge ya kisasa zaidi kwaajili ya maonyesho ya wakulima na wafugaji ambayo yatakuwa na mvuto zaidi.

  Aliyasema hayo alipokuwa kifungua maonyesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vyaThemi nanenane Njiro Jijini Arusha,huku akiwataka Taso washirikiane na Jiji pamoja na viongozi wa mikoa yote ili waweze kutengeneza ukumbi mkubwa wa kisasa.

  Aidha alisema kumekuwa na changamotoya wananchi.kutoielewa kauli mbiu ya maonyesho ya nanenane mwaka huu hivyo basi amewaagiza wakulima na wafugaji waweze kuingia.kwenye mafunzo ya shamba darasa na kwenye mabanda ili waweze kupata elimu zaidi.

  Aliwaagiza washiriki wenye mabanda yenye technolojia za kilimo waandae taarifa fupi ambayo mwananchi atakwenda nayo nyumbani na zitakazo waletea mabadiliko katika maeneo wanayotokea.

  Sambamba na hayo aliwataka Taso kuangalia sheria viwanja vya maonyesho ambayo inapiga marufuku ongezeko la makazi ndani ya viwanja vya maonyesho,pia amewataka washiriki wote wa maonyesho watoe ushirikiano kwa vyombo vyabulinzi na Usalama na katika maeneo yao.

  Vijana wa JKT Oljoro wakiwa wanatoa burudani siku ya uzinduzi wa maonyesho ya wakulima na wafugai ya nayandelea katika vianja vya Taso Themi nanenane mi njiro Arusha.
  Meya wa Jiji la.Arusha wa pili kutoka kulia ndugu Calist Lazaro a
  kiteta jambo na diwani wa kata ya Themi Melance .E.Kinabo wa kwanza kulia katika maonyesho yanayoendelea katika maonysho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.
  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo akiwa anatoa utambulisho.kwa.viongozi mbalimbali waliohudhuria sikubyaufunguzi wa.maonusho ya wakulima na wafugaji yanayondelea katika viwanja vya Themi Njiro.

  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imekusanya sh.Trioni 1.055 kwa mwezi julai sawa na asilimia 95.6 ya lengo la kukusanya sh.trioni 1.103 iliypangiwa na serikali kwa mwezi huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa Kodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Richard Kayombo amesema kuwa ukusanyaji huo huo umetokana na mwitikio kwa wananchi juu ya ulipaji kodi na kufanya kuongezeka kila mwezi.

  Amesema kipindi cha mwezi Julai 2015 TRA ilikusanya sh. Bilioni 914 sawa na asilimia 15.43.

  Kayombo amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017 mamlaka hiyo imepewa lengo la kukusanyanya sh.Trioni 15.1 ikilinganishwa na lengo la kukusanya sh.Trioni 13 .32 ya mwaka wa fedha 2015/2016.

  Amesema mikakati iliyopo kwa mamlaka hiyo kuhakikisha walipakodi wapya wanasajiliwa zaidi pamoja na kuhuisha taarifa za walipakodi kwa kuhakikisha namba za utambulisho wa mlipakodi (TIN) na ambazo hazitumiki zitafutwa katika mfumo wa TRA.

  Kayombo amesema kuwa hadi sasa waliochukua mashine za kieletroniki EFD ni 2700 na wengine walikuwa wanazitaka mashine lakini wamekosa sifa.

  Aidha amesema kuwa katika mkakati mwingine ni ukusanyaji wa mapato ya kodi za nyumba ambapo watatembea nyumba hadi nyumba na kutaka wapangaji kutoa ushirikiano.
   Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mampato Tanzania(TRA), Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa ukusanyaji huo huo umetokana na mwitikio kwa wananchi juu ya ulipaji kodi na kufanya kuongezeka kila mwezi.

  Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Makao Mamkuu, Gabriel Mwangozi akifafanua jambo kuhusina na namna Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) walivyojizatiti katika mpango wa kutembea nyumba zenye wapangaji kwaajili ya kuwahamasisha kulipa kodi katika Mamlaka hiyo kwa kila mkoa hapa nchini. Kushoto ni Meneja huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Honesta Ndunguru.
   Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mampato Tanzania(TRA), Richard Kayombo(Mbele) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0

  Halmashauri ya wilaya ya Mufundi Mkoani Iringa imefanikiwa kutekeleza agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, baada ya kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 4.7 sawa na asilimia 82.7 kati ya bilioni 5.6 ilizopanga kukusanya katika mwaka wa Fedha 2015-2016.

  Taarifa ya kitengo cha habari na mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imetanabaisha kuwa, mafanikio hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO MGINA kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichoketi mjini Mafinga.

  MGINA amesema, mafanikio hayo ni matokeo ya ufuatiliaji na usimamizi mzuri wa vyanzo vya mapato vya halmashauri kama vile mapato yatokanayo na usafirishaji wa mbao na Magogo, kuuzwa kwa sehemu ya msitu wa halmashauri sanjari na ushuru unaokusanywa kwa wafanyabiashara wadogo katika halmashauri hiyo.

  Aidha, Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa, pamoja na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kila halmashauri kukusanya mapato kwa asilimia 80 na kuendelea, kikwazo kikubwa cha kutofikia asilimia 100 ni kuzaliwa kwa halmashauri ya mji wa Mafinga jambo amabalo lilisababisha kugawana vyanzo vya mapato .

  Mgina, ametaja mkakati wa kufidia vyanzo hivyo kwa mwaka mpya wa Fedha 2016-2017 kuwa ni pamoja na kuanzisha stendi katika miji midogo ya Igowole na Nyololo, kuimarisha doria nyakati za usiku kwa wafanyabishara wanaotumia njia za panya kusafirisha mbao na Magogo hususani nyakati za usiku sanjari na kuongeza vizuio katika vijiji.
  Madiwani katika kikao cha baraza wakifuatilia kwa umakini.
  Mkururugenzi mtendaji wa Halmashauri Dk. Riziki Shemdoe, akizungumza kama katibu wa kikao cha baraza.
  Mwenyekiti wa halmashauri, Festo Mgina akizungumzia mafanikio ya ukusanyaji wa mapato.

  0 0

  Na Woinde Shizza ,Arusha.
   
  Rais Wa bendi ya FM Academia Nyoshi El Sadat amewahidi wakazi Wa jiji la Arusha kuwapa burudani ya nguvu katika onyesho la kumsaka Miss Kanda ya kaskazini.

  Akiongea na waandishi Wa habari jijini hapa, Mwanamuziki huyo alisema kuwa bendi hiyo imejipanga vya kutosha kuwapa burudana wapenzi na mashabiki wake.Alisema kuwa katika shoo hiyo ya Usiku Wa kumpata mrembo Wa kanda ya kaskazini amekuja na wanamuziki wote pamoja na wacheza show wa bendi ya Fm Academia .

  "Tunawapa burudani ya kufa mtu tunamastaili mapya ,pia yule mnenguaji ambae walimmiss kwa muda mrefu Qeen Suzy atakuwepo katika onyesho hilo"alisema Nyoshi .

  Naye mwandaaji wa onyesho hilo Faustine Mwandago alisema kuwa katika show hii atahakikisha washabiki wote wanaifurahia show hiyo . Alisema show hiyo itafanyika kesho jumamosi July sita itaanza kuanzia tatu kamili Usiku na kiingilio kawaida itakuwa kawaida 10000 huku V.I.P 30000.

  Picha ikionyesha warembo wanaoshiriki shindano la miss kanda ya kaskazini wakiwa wanafanya mazoezi kwa ajili ya shindano linalofanyika jumamosi hii July 6 katika viwanja vya ukumbi Wa triple A .

  0 0


  Na  Ally Daud-Maelezo.
  SERIKALI nchini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea msaada wa shilingi bilioni 142.23 kutoka  nchi washiriki Canada, Denmark, Uswizi na Korea Kusini ili kusaidia kuinua vituo vya afya nchini.

  Akizungumza mara baada ya kusaini msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa msaada huo wataupeleka moja kwa moja katika Zahanati za vijiji,Hospitali za  Wilaya na mkoa ikiwa pamoja na vituo vya afya nchi nzima.

  “Tumepokea msaada huo kwa furaha kubwa na kuhaidi kupeleka fedha hizo hizo mahali panapohitajika kwa matumizi ya kukuza na kuboresha vituo vya afya katika zahanati na hospitali nchi nzima ili kuokoa maisha ya watanzania” alisema Dkt. Ulisubisya.

  Aidha Dkt. Ulisabisya anaishukuru Benki ya Dunia kwa kuimarisha na kusaidia mfuko wa maendeleo ya afya nchini kwa kuwakutanisha na wahisani kutoka nchi mbalimbali.

  Mbali na hayo Dkt.Ulisabisya amewaomba Benki ya Dunia na nchi wahisani wasichoke na kushindwa kuisaidia Tanzania katika sekta ya Afya ili kutokomeza maradhi kwa kiwango kikubwa  na kupambana kwa ajili ya kukuza uchumi wan chi.
   Wadau wa Nchi washiriki kutoka Canada,Uswizi, Denmark na Korea kusini wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya katikati mara baada ya kusaini msaada wa Bilioni 142.23 kwa ajili ya kuinua vituo vya afya nchini.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na wadau wa Nchi washiriki kutoka Canada,Uswizi, Denmark na Korea kusini hawapo pichani wakati wa kusaini msaada wa Bilioni 142.23 kwa ajili ya kuinua vituo vya afya nchini.
  Wafanyakazi wa Common Wealth war Graves Commision wakisafisha sanamu la askari liliopo katikati ya mji wa Dar es salaam ili kuwaenzi mashujaa waliopigana vita kuiletea Uhuru nchi yetu.
  Picha Na Ally Daud-Maelezo. 

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KUELEKEA Mkutano Mkuu wa wanachama wa Yanga ulioitishwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji , Uongozi wa Yanga kupitia kwa mratibu wa Matawi na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Omary Kaya  amezitaja ajenda kuu zitakazotumika kwenye mkutano huo huku suala la Mabadiliko ya Katiba ya Yanga yakipewa kipaumbele. Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kesho siku ya Jumamosi unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama wanaotaka kufahamu mwenendi mzima wa timu ya yao.

  Amesema katika mkutano huo ajenda zitakazojadiliwa ni ushiriki wa timu yao katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua waliyofika katika mashindano ya Kombe la Shirikisho, pili suala linguine ni  ushirikiano mdogo wanaoupata kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Nchini(TFF) na kipi kifanyike ili kukuza uhusino mzuri na shirikisho hilo huku ajenda ya tatu ikibeba katiba ya klabu pamoja na maboresho yanayotakiwa kufanyika ili kupata katiba bora.

  Mapato na matumizi yatakuwa katika ajenda namba tano pamoja na kuto shukrani kwa uongozi uliopita kwa kazi kubwa waliyoifanya na kukaribisha uongozi mpya. Kingine ni maendeleo ya klabu hiyo pamoja na kuangalia mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu yao ili kuhakikisha inapata maendeleo zaidi ya yaliyofanyika kipindi cha nyuma na endapo wanachama watakubaliana na jambo hilo litaanza utekelezaji haraka.

  "Endapo tutakubalia kuingia katika mfumo wa kampuni basi tutaami huko na wanachama wanatakiwa kielewa kuwa hatujakurupuka katika jambo hili bali tumefanya utafiti wa kutosha" amesema Kaya. Wanachama wanatakiwa kuhudhuria kwa wingi ili kuleta maendeleo na mabadiliko ya pamoja ndani ya klabu hiyo kongwe hapa nchini. Baada ya kumalizika kwa mkutano huo Yanga itashuka dimbani kuvaana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa ndani ya uwanja wa Taifa na kiingilio cha mchezo huo kitakuwa 5,000 huku pia mchezo huo ukiwa sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya Mo Bejaia.

  Mabingwa hao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara  msimu uliopita, timu ya Yanga imegoma kutumia jezi mpya zilizotolewa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo juzi. Kaya amesema kuwa jezi yake ya ugenini inafanana na ile waliyotumia msimu uliopita hivyo hawatapata faida katika mauzo ya jezi hizo.

  Pia wamesema kuwa hawakushirikishwa katika mchakato wa kuandaa jezi hizo ambazo zimetengenezwa kwa kiwango cha chini sana. Yanga haina hadhi ya kuvaa jezi zisizo na bora na kiwango kisichoridhisha kama kilichotumika kutengenezeanjezi hizo.   "Sisi ni klabu na tunajiendesh kibiashara tutauza vipi jezi zetu na kupata faida kama zinafanana na zile za mwaka jana pia timu yetu haiwezi kuvaa jezi zisizo na ubora kama hizi zilizotolewa na wadhamini wetu", amesema Kaya.

  Amesema kikubwa watakachokifanya ni kuhakikisha wanafuata na kuheshimu nembo ya mdhanimi katika jezi watakazotumia msimu ujao wa ligi kuu.

  0 0

  Ikiwa na ari, nguvu na kujaa hamasa na matumaini ya kushinda, timu ya mpira wa miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, kesho Jumamosi Agosti 6, 2016 itaingia Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Magharibi mwa Mji wa Johannesburg, Afrika Kusini kucheza na wenyeji katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zitakazofanyika Madagascar hapo mwakani.

  “Tutaifunga Afrika Kusini hapa kwao,” ni maneno ya Mchawi Mweusi - Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, alipozungumzia mchezo huo utakaoanza saa 9.00 alasiri kwa saa za Afrika Kusini wakati huko Tanzania itakuwa ni saa 10.00 jioni katika uwanja ambao hutumiwa na timu ya Moroka Swallows ambayo kwa sasa imeshuka daraja hadi la pili.

  Afrika Kusini ambayo Serengeti Boys inacheza nayo kesho ni mtihani wa kwanza kati ya miwili kabla ya kutinga Madagacar. Mchezo wa kwanza unafanyika hapa Afrika Kusini, kabla ya kurudiana Agosti 21, 2016 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi-nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Mchawi Mweusi ambaye jina lake halisi ni Bakari Nyundo Shime, amesema: “Kwa jinsi tulivyojiandaa. Sina wasiwasi na timu yangu.”

  Shime amesisistiza: “Najua Afrika Kusini watataka kutumbia mbinu za nyumbani. Lakini sina wasiwasi. Nimelenga kushinda michezo yote iliyo mbele yangu. Si kwamba napigania kufuzu kwenda Madagascar tu kwenye fainali za Afrika, la hasha, nataka timu hii niipeleke Kombe la Dunia.”

  Shime ambaye alianza na timu hiyo mwaka mmoja uliopita, amerudia maneno yake: “Sioni kama itakuwa kikwazo kuifanikisha kufika fainali za Kombe la Dunia. Namuomba Mungu atunyooshee mkono wake, nawaombea viongozi wa TFF wazidi kuihudumia timu hii, lakini pia wadau wengine waisapoti timu hii bila kuangalia au kuchagua mtu anayeongoza TFF. Hii ni timu ya Watanzania wote.”

  Shime alishukuru mipango na ahadi ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kugharamia kambi ya siku 10 iliyoyofanyika Madagascar akisema: “Ilikuwsa ni kambi bora. Kwa sasa kikosi changu kinahitaji kulipam deni la Watanzania na ahadi ya Rais Malinzi.”

  Kikosi tarajiwa kesho ni Ramadhani Awm Kabwili atakayecheza golini, Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Vitalis Nkosi, Dickson Nickson Job, Shaban Zuberi Ada, Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Mohammed Abdallah Rashid Ibrahim Abdallah Ali na  Syprian Benedictor Mtesigwa.

  Ili kufika hapo, Serengeti iliifunga Shelisheli jumla ya mabao 9-0 katika mechi mbili za Tanzania na Shelisheli.

  Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.

  0 0

  Wafanyakazi wa bandari ya Zanzibar wakishusha madeski yaliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar.
  Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania Salim Hassan Turky akimkabidhi sehemu ya madeski hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya kuchangia madeski Zanzibar Haroun Ali Suleiman Bandarini Zanzibar.
  Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania Salim Hassan Turky akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madawati hayo wakati wa makabidhiano bandarini Zanzibar.
  Picha na Mkame Mshenga -Maelezo Zanzibar.

  Na Mwashungi Tahir, Maelezo Zanzibar.
  JUMLA ya madawati  5,500 ikiwa ni mgao wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  yamewasili  Zanzibar  kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wa skuli za Unguja na Pemba.

  Akipokea madawati hayo  bandarini  Zanzibar, Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya madawati  Zanzibar  Haroun Ali Suleiman amesema mgao huo utapunguza tatizo kubwa la madawati linalozikabili skuli nyingi hapa nchini.

  Amesema kupatikana kwa madawati hayo  kutaleta faraja kwa wanafunzi na kuongeza hamasa na ari katika kujipatia elimu.

  “Msaada huu utapunguza usumbufu wa wanafunzi kukaa chini kwa muda mrefu na utaongeza ufanisi kwa walimu na wanafunzi katika kusomesha na kujifunza, “alisema Mwenyekiti huyo.

  Nae  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki  Pembe Juma amewashukuru Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia kupatikana madawati hayo na ameeleza matumaini yake ya kupatikana msaada zaidi wa madeski.

   Amewaomba wasamaria wema kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na tatizo la madawati kwa kutoa michango yao kupitia Kamati ya Taifa ya Madawati ya Zanzibar.  

  Aidha  amewaomba walimu wakuu wa skuli zitakazopata madeski hayo kuwapa elimu wanafunzi  jinsi ya kuyatunza  ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.

  Sambamba na hayo Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zuberi Ali Maulid alisema kupatikana kwa madeski hayo  ni faraja  kwa baraza hilo kwani suala hilo linazungumzwa sana na tumeanza kuona mafanikio  yake.

  Amesema kupatikana kwa msaada huo ni jambo la kupigiwa mfano kwa wabunge kwani wabunge  waliopita  hawajawahi kufanya jambo kama hilo. 

  Makamo Mwenyekiti wa wa Bunge Salim Hassan Turky ambae ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae kwa niaba ya wabunge wenziwe amesema  madawati hayo ni mchango   wa bunge  uliotokana na pesa za bajeti zilizobakia katika  bajeti iliyopita.

  Jumla ya shilingi billion sita zimetumika kununulia madawati hayo  ambayo ni kila jimbo lilitarajiwa  kupata  madeski 300 na  kwa kuanzia kila jimbo limetapatiwa madeski 100 na mengine yatafuatia baadae.

  Aidha amemshukuru Rais  wa Jamhuri ya Muungano Mh. John Pombe Magufuli kwa kutoa wazo la kutumia fedha zilizobaki za bunge  bajeti iliyopita kwa kununulia madeski hayo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Agosti 5, 2016 amekutana na Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam na kuzungumza nao maswala mbalimbali ya kiusalama kwa Mkoa wa Dar es salaam, huku akiwapongeza Askari hao kwa uzalendo wao kwa Taifa.

  "Hakuna wafanyakazi wazalendo nchini kama Askari, kwani wako tayari kufa ili taifa la Tanzania liwe salama, Pia uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu" alisema Makonda.

  Makonda amewaahidi Askari hao kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba waimarishe usalama wa Jiji la Dar es salaam, ili iwe kama Dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta, kwani Jiji hili linapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa.

  Makonda amewahakikishia askari hao kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt. John Magufuli, ombi la Makonda lilikua ni juu ya asilimia 20% ya faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa ni pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika kwenye eneo la tukio bila kuchelewa.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katika Mkutano wake huo na Askari Polisi wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza jambo na baadhi ya Askari Polisi wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam.

  0 0
 • 08/05/16--07:50: Article 11


 • 0 0


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akiwa nje ya Jengo la Kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kufuatia mmiliki wa kituo hicho Tabibu Juma Mwaka kuendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa kwa siri pia kujitangaza kwenye vyombo vya habari licha ya agizo la Serikali la Julai 11, 2016 la kumtaka asitishe kutoa huduma zake kutokana na kukosa vigezo vya kisheria vya kumruhusu kutoa tiba nchini. 
  Baadhi ya Wagonjwa waliokutwa wakisubiri Tiba katika kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopigwa marufuku na Serikali kutoa huduma zake nchini.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akizungumzwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED waliokuwa wakitoa huduma licha ya kituo hicho kupigwa marufuku na Serikali kutoa huduma zake nchini.Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri Dkt. Hamis Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata ndani ya saa 24 na kumfikisha Mahakamani Mmiliki wa Kituo hicho tabibu Juma Mwaka kwa kukiuka agizo la Serikali na kutoa huduma kinyume cha Sheria. 
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia), Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dk. Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) kwa pamoja wakipitia kwa makini baadhi ya nyaraka zilizokutwa ndani ya kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuchukua vielelezo kama ushahidi wa Tabibu Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  0 0  0 0


  0 0


  0 0

  Ankal,
  Nimeona nijitokeze ili kumuhakikishia mdau wa BLOG yetu pendwa aliyeomba mijadala yenye tija irudi hapa kwa manufaa ya kuelimishana.

  Ni kweli wadau nikiri nilikutana na John Mashaka hivi majuzi (12/07/2016) katika uwanja wa ndege wa JK Nyerere na kati ya mazungumzo yetu kwa pamoja yalikuwa ni kwa namna gani tutashirikiana na wadau wa Globu hii ya Jamii kutoa mada zenye mshiko wa wafuatiliaji wa mambo mbali mbali yanayohusu Tanzania yetu.

  Niwahakikishie kuwa muda si mrefu mtaanza kupata mijadala itayokuwa inaendana na “mwendo kasi” Tupo pamoja, niko Tanzania, na ninawashauri wale ambao mngependa kujua “utamu wa ngoma” njooni tuicheze wote.


  Mdau
  Hildebrand Shayo.

  PS: Nashukuru sana Dr. Hildebrand Shayo na mdau John Mashaka kwa kujibu haraka matakwa ya wadau. Hii inaonesha ni jinsi gani Globu ya Jamii, inayotimiza miaka 11 ifikapo mwezi Septemba, inavyoendeleza Libeneke kwa kasi ile ile ya kuanzia kuzaliwa kwake kule Finlandia Hall, Helsinki, Finland. Sina cha kusema zaidi ya kuwakaribisha tena magwiji wa mijadala Dr. Shayo na mdau Mashaka. Mbarikiwe sana kwa kuendelea kuamini kwamba Globu ya Jamii iko pale pale na wadau wake.
  - Ankal

  0 0  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye afanya ziara Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kwa kumtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dk. Ayoub Rioba ili kujifunza na kukuza mahusiano kati ya Taasisi hiyo na Jeshi hilo.

  Katika ziara hiyo Kamisha Jenerali, alitembelea ofisi za Shirika hilo zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam, mapema leo asubuhi na  alipata fursa ya kujifunza jinsi gani shirika hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kuwa na mazungumzo ya kina na mkurugenzi huyo. “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana na shirika hili ili tuweze kuelimisha umma” alisema Kamishna Jenerali.

  Akiwasilisha taarifa ya uendeshaji wa Jeshi hilo Kamishna Jenerali alimueleza changamoto zinazolikabili Jeshi hilo na nia ya yeye kutembelea ofisi hiyo ni kudumisha mahusiano ambayo yatakuwa chachu kwa taasisi hizo kwa manufaa ya umma.

  Mkurugenzi wa shirika hilo naye alisisitiza kuwa nivema sasa Jeshi hilo likashirikiana na Shirika hilo ili kutekeleza dhima ya kuokoa maisha na mali, kwa kutumia chombo hicho pamoja na kuwa bajeti ya serikali ni finyu. “Kituo chetu ni cha umma na kwakuwa kazi zetu ni kuisaidia umma wa watanzania tupo tayari kushirikiana”, alisema Mkurugenzi mkuu wa TBC.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba akimkabizi kitabu ta wageni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea ofisi za Shirika hilo mikocheni mapema leo asubuhi. 
   Mkurugenzi wa Matukio wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Bi Martha Swai (wa kwanza kulia) akitoa maelezo jinsi ya upokeaji wa habari za matukio mbalimbali kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (katikati) alipotembelea ofisi hizo mapema leo asubuhi (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Dk. Ayoub Rioba .
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  Thobias  Andengenye aliyesimama mbele, akimsomea taarifa ya Jeshi hilo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba alipotembelea ofisi za Shirika hilo mapema leo asubuhi

   Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (katikati) akipokea maelezo jinsi ya chumba cha matangazo kinavyofanya kazi (Studio) kutoka kwa Mtangazaji Bi Anna Mwasioke hayupo pichani, (kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa TBC Taifa Dk. Ayoub Rioba. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 08/05/16--13:30: MEM-WEEKLY-BULLETIN-131


older | 1 | .... | 1309 | 1310 | (Page 1311) | 1312 | 1313 | .... | 3353 | newer