Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live

Msaada Tutani...John Mashaka Yuko Wapi ?

0
0
Ankal,
Natumai unaendelea vizuri katika zama hizi za mwendo kasi. Ankal, kwa kifupi ni kwamba, mimi ni mfuasi na mdau mkubwa wa blogu ya jamii tangu 2007. Ambapo hadi leo sijakosa hata siku moja kulichungulia globu letu. Nilinogewa na hii blogu yetu enzi za wakina John Mashaka (pichani) , Hildebrand Shayo na US Blogger waliokuwa wakizua mijadala mizito ya maana yaliyoenda shule. Kwa wanaofahamu historia ya blogu hii, John Mashaka, ni jina mashuhuri kutokana na upeo wa mada zake ambazo zilizogusa watanzania kila pembe ya dunia. 
Ombi langu Ankal kwa leo ni kwamba, tumebakia kama mayatima kwa kutokuwepo kwa hawa magwiji na wataalamu wetu. John Mashaka, US Blogger , na Hildebrand Shayo Tunaomba re-union ya miaka kumi.  Ndugu yetu John Mashaka atushushie nondo hata moja tu. Kwani mijadala yao ilikuwa ni kivutio kikubwa sana kwa wasomaji wa rika zote. Tunaobeba maboxi ughaibuni, stress zote za kazi ziliisha pale tulipoinamishwa vichwa vyetu kwenye computer kusoma mada za ndugu Mashaka na kisha majibu ya Gwiji US-Blogger. 
Ankal, tukoshe roho japo kidogo. Tunaomba ile mijadala irudi hata kwa wiki moja tu, washabiki wa globu hatuna raha kabisa. Kama hataki kushiriki, basi atuandikie hata kibarua sisi wafuasi wake
Wake mtiifu, Mdau
Manchester, UK

NEWS ALERT: TUNDU LISSU AACHIWA KWA DHAMANA

0
0
                                              Na Mwene Saidi wa  
                                                 Globu ya Jamii
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu  (pichani) ambaye leo amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam na kupandishwa kizimbani dhidi ya mashtaka matatu ikiwamo kuidharau mahakama na kusababisha chuki kwa watanzania dhidi ya Rais John Magufuli na serikali yake ameachiwa kwa dhamana.
Lissu alipandishwa kizimbani  na kusomewa mashtaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Cyprian Mkeha, katika kesi iliyoanza saa 9.26 mchana hadi saa 2.25 usiku. 
Hakimu alitupilia mbali kiapo cha Jamhuri cha pingamizi la dhamana kwa kuwa hakikuonesha tarehe iliyotolewa. 
Kisha Hakimu akamtaka mshtakiwa kujidhamini mwenyewe kwa kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 10. Akafanya hivyona kuachiwa.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi, akisaidiana na Wakili Serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi, Mawakili wa Serikali Simon Wankyo na Paul Kadushi.

Wakili Kadushi alidai kuwa Agost 2,2016 akiwa na nia ya kujenga chuki dhidi ya Rais Dk John Magufuli kwamba ni dikteta uchwara. 
Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza mshtakiwa akiwa na nia ya kuleta dharau katika mfumo wa mahakama nchini alitamka kwam a "Kesi    ya kipuuzi na mashtaka yamekaa kimagufuligufuli "alinukuliwa mshtakiwa.
Shitaka la tatu linadai kuwa siku na eneo la tukio la kwanza mshtakiwa baada ya kutoka kusikiliza kesi zake mbili tofauti zinazomkabili katika mahakama hiyo akiwa na lengo la kudharau mahakama alitamka "Siwezi kufungwa mashtaka yenyewe ya kipuuzi yamekaa kimagufuligufuli" alinukuu Wakili Kadushi.
Lissu alidai kuwa maneno anayodaiwa kuyatamka katika hati ya mashtaka ni ya kweli lakini siyo ya uchochezi hivyo alikana mashtaka hayo.
Hata hivyo Wakili Nchimbi alidai kuwa upande waJamhuri unapinga dhamana dhidi ya mshtakiwa kupitia hati ya kiapo iliyowasilishwa na Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala ( RCO) kwamba mshtakiwa akipewa dhamana atarudia kufanya makosa hayo kinyume cha sheria.
Pia Wakili Nchimbi aliwasilisha pingamizi la kumkataa wakili kiongozi wa utetezi Peter Kibatala kwamba ametoa maelezo polisi na kwamba anatarajiwa kuwa shahidi wa Jamhuri dhidi ya mshtakiwa.
kuhusu uwakili Kibatala alidai kuwa hakuna sheria inayomzuia kumtetea mteja wake na kwamba ni njama za upande wa Jamhuri kwa kuwa wanamhofia.
Kutokana na pingamizi la dhamana, Lissu alilazimika kujibu hoja mwenyewe baada ya upande wa Jamhuri kusisitiza kwamba Kibatala haruhusiwi kumtetea mshtakiwa hadi mahakama itakapoamua vinginevyo.
Alidai kuwa hoja za Jamhuri hazina mashiko ya kuzuia dhamana yake kwa kuwa hajatiwa hatiani na kwamba chini ya kifungu cha 148 kidogo cha (5)a hakijaanisha sababu zilizotolewa na Jamhuri kuzuia dhamana yake.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

NAIBU WAZIRI WA AFYA ALIPOZITEMBELEA HOSPITALI ZA MUHIMBILI NA MWANANYAMALA JIJINI DAR

0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto) akipitia kwa makini jalada (file) la matibabu Bi. Kuluthumu Kasongo (aliyelala kitandani) anayesumbuliwa na ugonjwa wa Seli Mundu (Sicle Cell) kujiridhisha juu ya matibabu yake kufuatia taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii leo kuwa mgonjwa huyo ametelekezwa bila kupatiwa matibabu na kulazwa chini katika wodi hiyo jambo ambalo sio la kweli.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla (kushoto) akiwa ameongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Delila Moshi kufuatilia ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo jijini Dar es salaam kuangalia ubora wa huduma za Afya zinazotolewa na hospitali hiyo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Delila Moshi (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) juu ya huduma za Tiba alipotembelea wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla (kulia) akizungumza na akina mama wenye watoto waliokuwa katika wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo.Amewahakikishia akina mama hao kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma za Afya katika hospitali zake.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akimsalimia mtoto aliyekuwa amelala na akina mama wenye watoto aliowakuta katika wodi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo kukagua ubora wa huduma za Afya.

Waziri wa Mambo ya Ndani auagiza uongozi wa Magereza ya mkoa wa Iringa kuanza mchakato wa kuhamisha magereza ya Manispaa ya Iringa

0
0
WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameagiza uongozi wa Magereza ya mkoa wa Iringa kuanza mchakato wa kuhamisha magereza ya Manispaa ya Iringa ili eneo hilo kutumika kupanua Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.


Nchemba ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea eneo hilo ambalo limekuwa likiombwa kwa muda mrefu na viongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa ili litumike kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Iringa .

Akizungumza baada ya kutembelea eneo la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa alisema kuwa amekubaliana na maombi ya viongozi wa mkoa wa Iringa ya kuomba gereza hilo kuhamishiwa katika eneo la Mlolo nje kidogo na Manispaa ya Iringa huku eneo hilo la Magereza litumike kupanua majengo ya Hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

“ Kwa kawaida kati ya Hospitali na magereza kinachotakiwa kuwepo mjini ni Hospitali na sio magereza hivyo hivyo kati ya mgonjwa na mfungwa ama mahabusu anayeweza kufanya kazi ya kufyatua tofari za ujenzi ni mahabusu ama mfungwa na sio mgonjwa , hivyo naagiza mtaalam wa ujenzi wa magereza kuanza kuandaa vifaa vya kufyatualia tofari na kwa kufuata taratibu za magereza waorodheshwe wale ambao watakuwa tayari kujitolea kufanya kazi ya ujenzi ili kazi hiyo ianze” 

Hata hivyo waziri huyo alisema kuwa kuanzia leo anataka kupata orodha ya wafungwa waliopo gerezani hapo ambao wanauwezo wa kufanya kazi.

Pia alisema suala la kuhamishwa kwa gereza hilo litafanyika kwa awamu na kuwa wakati gereza linajengwa na baadhi ya nyumba za watumishi bado askari wataendelea kuishi katika eneo hilo huku majengo yao likiwemo jengo la Ghorofa utawekwa utaratibu wa kujengewa jingine ili hilo linalotumiwa na magereza litumike kwa ajili ya madaktari.


 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimiana na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi (kulia) baada ya kukutana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, leo.

 
Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi (katikati)  akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, wakati walipokutana leo nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Waziri Simbachawene avutiwa na Banda la SSRA katika Maonyesho ya Nane Nane, Kanda ya Kusini

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene akipokea vipeperushi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika mara baada kupata Maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo, wakati akikagua baadhi mabanda ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kitaifa Kanda ya Kusini Lindi na Mtwara.
Picha ya pamoja kati ya watumishi wa SSRA na Baadhi ya wadau waliotembelea Banda hilo ikiwemo wakulima waliotembea kujifunza jinsi Mifuko ya Jamii inavyojiendesha chini ya usimamizi wa Mamlaka hiyo.
Mmoja wa Wanachama wa Mifuko ya Jamii ambae alijitambulisha kama Mstaafu Mtarajiwa akipokea vipeperushi vya Mamlaka hiyo oka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika.
Afisa Uhusiano na Uhamasishaji SSRA, Ally Masaninga akikabidhi zawadi kwa Bi. Saida, Afisa Vijana Mkoa wa Lindi alietembelea Banda la Mamlaka Hiyo katika Viwanja Vya Ngongo Lindi Manispaa.

Serikali Zanzibar yatilia mkazo soka la wanawake

0
0
Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar pamoja imewahasa wazazi nchini kutoa uhuru kwa watoto wao wa kike kucheza mpira wa miguu ili kuifikisha nchi katika Mashindano ya Kimataifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, Hassan Mitawi alipokuwa akifungua mashindano ya Airtel Rising Stars yaliyofanyika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Alisema bila ya michezo Zanzibar haiwezi kujulikana hivyo ni vyema kwa wazazi na walezi kuwapa motisha watoto wao wa kike kushiriki katika michezo hasa mpira wa miguu.

Alisema mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wenye kutoa ajira kama ilivyo kwa wanaume lakini tabia ya baadhi ya wazazi kuwakataza watoto wao wa kike kujiingiza katika soka kunawakosesha fursa zinazotokana na mpira ikiwemo afya bora, ajira pamoja na kuchangia katika kukuza soka la wanawake nchini.

Mitawi alisema watu wanazaliwa na vipaji na vipaji hivyo vinapaswa kuendelezwa hasa kwa upande wa Zanzibar wanawake washirikiane kudumisha michezo.

Aidha aliishukuru Airtel kuzidi kukuza na kusaidia michezo nchini na kuwataka kuendelea kuwekeza katika michezo hususani soka la wanawake.

Awali Mwenyekiti wa soka la wanawake Hatima Mwalimu alisema mashindano hayo yatasaidia kuinua vipaji vitakavyoisaidia Zanzibar kushiriki katika mashindano mbalimbali.

Nae Meneja Mauzo wa Airtel Zanzibar Muhidin Mikadadi alisema “Tunajisikia fahari kusaidia mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 hapa nchini na tumejipanga kuibua vipaji vya vijana kupitia program hii. Tunafurahi kuona vijana wengi wanajitokeza kushiriki mashindano hayo na tunawashukuru ZFA na Wizara ya Michezo kuwaunga mkono katika kusaidia na kukuza michezo nchini”.

Huu ni msimu wa sita kwa mashindano ya Airtel Rising Star nchini kwa mwaka humu Zanzibar impeta nafasi ya kushiriki, jumla ya timu sita zinashiriki katika mashindano haya ni pamoja na Mwenge kutoka Wilaya ya Kusini, Kidimni Kutoka Wilaya ya Kati,New Generation Kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi, Jumbi Women kutoka Wilaya ya Kati na Bungi Sisters kutoka Wilaya ya Kati.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamanduni na Michezo Zanzibar Hassan Mitawi akikangua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar Ijumaa 5 Agosti 2016.
Mchezaji wa Bungi Sister FC Agatha Peter (nyekundu) akichuana na beki wa Jumbi Woman Fighter Arafa Mbaraka wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji wa Bungi FC Suzan Francis (nyekundu) akichuana na Agnes Andrew wa Jumbi Woman Fighter wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.

DIWANI ASWEKWA NDANI KWA KUKIUKA MAADHIMIO YA BARAZA LA MADIWANI WILAYANI IKUNGI

0
0
Na Mathias Canal, Singida

Jeshi la polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida limemtia nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke  Emmanuely Njingu (CHADEMA) kwa kosa la kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali kufanya kazi yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha awali kabla ya kuwekwa nguvuni na jeshi la polisi alivuliwa ujumbe wa kamati hiyo kutokana na kukiuka taratibu na makubaliano ya baraza la madiwani jambo ambalo limepelekea kuhamishiwa katika kamati nyingine.

Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa diwani huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Irisia Ally Juma Mwanga amesema kuwa Diwani huyo amekamatwa kwa mujibu wa sheria hivyo yeye kama mwenyekiti hawezi kuingilia taratibu, sheria,na kanuni za serikali.
Kutoka Kushoto ni Eng Sadick Chakka Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga, na Kulia ni Abel Suri Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Mwanga amesema kuwa tarehe 19 mwezi Julai moja ya maadhimio ya kamati ya fedha na vikao vya baraza ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri lakini diwani huyo amekiuka makubaliano hayo kwa kung’oa mageti ya vizuizi vya barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa mazao jambo ambalo limepelekea kuzorota kwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.

Ameongeza kuwa Mjumbe yeyote anayekiuka maazimio wanayokubaliana na kutoa siri za kamati adhabu yake kisheriani kupoteza sifa ya kuwa mjumbe wa kamati husika. Amesema diwani huyo ameondoshwa katika nafasi hiyo baada ya maridhiano ya kamati hiyo na kukubaliana kumuhamishia katika kamati nyingine ya huduma za uchumi.

“Jambo mkishakubaliana kisheria tena kwenye vikao vya kisheria maana yake linakuwa ni sheria hivyo kwa kiongozi yeyote akikiuka taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake, kanuni za Halmashauri ni za watu wote hazichagui upande mmoja” Alisema Mwanga

Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alihutubia Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mara yake ya mwanzo kabisa tangu alipochaguliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na kuzungumzia kuwepo kwa changemoto ya uhaba wa maabara, afya duni na miundombinu pia alizungumzia kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato jambo ambalo linairudisha nyuma Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Bajeti ya Wilaya ya Ikungi kwa Mwaka 2013/2014 ilikuwa na Shilingi 509,701,044 namakusanyoyakeyakawa ni 338,325,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kuwa na upungufuwa shilingi 171,376,044.

Mwaka 2014/2015 ilipangwa bajeti ya shilingi 631,455,000 lakini makusanyo yake yakawa ni shilingi 457,555,172 ambapo mwaka ulimalizika kwa kukusanya 173,899,828.

Mwaka wa bajeti 2015/2016 bajeti ya Halmashauri iliyopangwa ilikuwa ni shilingi 1,127,030,000 makusanyo yalikuwa ni 679,283,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kwa kuwa na upungufu wa shilingi 450,747,000 hivyo kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji.

Mwanga amesema kuwa Kutofikiwa malengo hayo kumesababishwa na kutopewa ushirikiano watendaji katika ukusanyaji wa mapato hii ikiwa ni kufuatia kauli za mazuio zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.

Hata hivyo ametoa Mwito kwa viongozi wa serikali, wanasiasa, taasisi za dini na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo ya kuifanya Ikungi kukua kiuchumi .

ROTALY CLUB OF SONGEA YAKARABATI CHOO CHA SHULE YA SEKONDARI BOMBAMBILI, MKOANI RUVUMA

0
0
Rais aliyemaliza muda wake wa Rotaly Club tawi la Songea mkoani Ruvuma Michael Sinienga (kushoto) akikabidhi hati na kumbukumbu mbalimbali za ofisi kwa Rais mpya wa club hiyo Albert Kessy (kulia) kabla ya kuzindua mradi wa ukarabati wa choo katika shule ya sekondari Bombambili mkoani Ruvuma jana,  ambapo club hiyo imeanza ukarabati wa choo hicho kwa gharama ya shilingi milioni 4 ili kuwanusuru wanafunzi wa kiume ambao wanatumia choo kimoja kilichoazimwa kwa wanafunzi wa kike.
Rais mpya wa Rotaly Club of Songea mkoani Ruvuma Albert Kessy kulia akichanganya udongo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa choo cha wavulana katika shule ya sekondari Bombambili katika Manispaa ya Songea mkiani Ruvuma ambacho hadi kukamilika itagharimu kiasi cha shilingi milioni 4,kushoto ni Rais wa club hiyo aliyemaliza muda wake Michael Sinienga.
Baadhi ya wanachama wa Rotaly club of Songea mkoani Ruvuma,wakiangalia jana choo cha wavulana katika shule ya sekondari Bombambili kata ya Bombambili katika manispoaa ya Songea ambayo imeharibika na wanafunzi wa kiume 620 wa shule hiyo kujisaidia katika choo kimoja cha wasichana chenye matundu 6,ambapo Rotaly club of Songea iliamua kufanya ukarabati mkubwa wa choo hicho ili kuwanusuru watoto hao.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bombambili kata ya Bombambili katika manispaa ya Songea wakimsikiliza jana Rais wa Club ya Rotaly tawi la Songea mkoani Ruvuma Albert Kessy(hayupo pichani) kabla ya Rais huyo kuzindua mradi wa ukarabati wa choo cha wavulana shuleni hapo ili kuwanusuru wanafunzi 620 wa kiume wanaolazimika kutumia choo kimoja chenye matundu 6 ambacho kinatumika kwa ajili ya wanafunzi wa kike.
Rais wa Club ya Rotaly tawi la Songea mkoani Ruvuma Alibert Kessy akizungumza jana na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Bombambili kata ya Bombambili katika manispaa ya Songea kabla ya kuzindua mradi wa ukarabati wa ujenzi wa choo cha wavulana shuleni hapo ili kuwanusuru wanafunzi 620 ambao wanajisaidia choo kimoja ambacho ni cha wanafunzi wa kike kufuatia choo chao kuharibika na mvua miaka miwili iliyopita. Picha na Muhidin Amri

Halmashauri zinazodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa sasa kubanwa

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.George Simbachawene akikata utepe kuzindua rasmi gati ya kisasa katika kisiwa cha Songosongo jana. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Godfrey Zambi na nyuma ya Mkuu wa mkoa ni Mhandisi Gilbert Mwoga, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.

Na Mathew Kwembe, Lindi

Serikali imesema kuwa halmashauri zinazodaiwa na bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa na ambazo zimeshindwa kurejesha malimbikizo ya madeni inayodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa hazitaruhusiwa kukopa katika taasisi nyingine za kifedha hadi zikamilishe kwanza deni llinalodaiwa na Bodi hiyo.

Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.George Simbachawene wakati alipotembelea maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayofanyika kitaifa mkoani Lindi.

Waziri Simbachawene alisema kuwa halmashauri zote zinazodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa hataziruhusu kuomba mkopo wa fedha kutoka taasisi nyingine zozote hadi kwanza zikamilishe deni walilokopa kutoka katika Bodi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.George Simbachawene akiangalia bustani ya mbogamboga inayomilikiwa na Shirika la SUMA JKT.

Waziri Simbachawene alisema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha kuwa fedha zote zilizokopwa na halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo zinarejeshwa ili mfuko huo uwe endelevu na kuzipa fursa halmashauri nyingine kukopa fedha kutoka kwenye Bodi hiyo.

Aidha Waziri Simbachawene ameitaka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kuandaa utaratibu maalum utakaoziwezesha halmashauri zinazokopa fedha kupitia taasisi hiyo zinarejesha fedha zake moja kwa moja benki bila ya kukumbushwa mara kwa mara.

Hatua hiyo ya Waziri Simbachawene inafuatia maelezo ya Mhasibu wa Bodi hiyo Bwana Mourice Kobalogira kumweleza Waziri kuwa Halmashauri nyingi zilizokopa fedha kupitia Bodi hiyo zimekuwa zikikwepa kurejesha fedha kwa visingizio mbalimbali hali inayosababisha chombo hicho kushindwa kuzikopesha halmashauri nyingine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.George Simbachawene akifurahia baada ya kushuhudia bustani ya mboga mboga aina ya bilinganya ambayo imestawi vyema katika eneo la maonyesho ya Nanenane mkoani Lindi. Bustani hiyo inamilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa kupitia shirika lake la SUMA JKT.

Bwana Kobalogira alimweleza Waziri Simbachawene kuwa hali ya urejeshaji mikopo imekuwa ya kusua sua mno ambapo hadi kufikia sasa maombi mapya ya halmashauri zinazotaka kukopa kupitia bodi hiyo yamefikia bilioni 49 lakini Bodi imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni tisa tu.

“Tatizo Mhe.Waziri ni kuwa halmashauri hazizingatii urejeshaji kulingana na mikataba yao waliyoombea mikopo, mfano mtu kama aliomba mkopo kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikuu cha Mabasi, basi fedha za urejeshaji zitoke katika mapato ya stendi, au kama halmashauri iliomba mkopo kwa ajili ya ujenzi wa soko, fedha za urejeshaji zitokane na mradi huo, lakini halmashauri nyingi zimekuwa hazifanyi hivyo,” alisema bwana Kobalogira.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Simbachawene aliiagiza Bodi hiyo kuhakikisha kuwa inaweka kipengele katika mkataba wa mkopo utakaozibana halmashauri hizo kurejesha fedha ilizoombea mkopo kulingana na masharti yaliyowekwa na bodi hiyo, tofauti na ilivyo sasa ambavyo halmashauri nyingi zilizopewa mkopo zimekuwa zikikwepa kutekeleza suala la marejesho.
Mhasibu kutoka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa Bwana Mourice Kobalogira akimweleza waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.George Simbachawene wakati alipotembelea banda la Ofisi katika Maonyesho ya Nane nane yanayofanyika kitaifa mkoani Lindi.

BAADA YA KUKAA KWA ZAIDI YA MIAKA 10, SASA WAKAZI WA SALASALA WAPATA NEEMA YA MAJI

0
0
WANANCHI zaidi ya 265 wa mtaa wa Upendo, Mbezi Salasala wilayani Kinondoni wamelishukuru Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), kwa kuwafikishia huduma ya Majisafi waliyoipatia shida kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja wa serikali za mitaa na DAWASCO, Mjumbe wa mtaa wa Upendo Bw. Robert Massawe amepongeza juhudi zilizofanywa na Dawasco za kuwapatia huduma ya Maji wananchi wa eneo lake na kwamba juhudi hizo zinaendana na kauli ya serikali ya awamu ya tano inayosema hapa kazi tu.

Akieleza historia fupi ya eneo hilo Bw. Massawe alisema tangu watu waanze kuhamia eneo hilo huduma ya Maji ilikuwa ni ya kununua kutoka mtaa mwingine wa mbali ambao ulikuwa umefikiwa na huduma hiyo ya Maji.

“Ilifikia kipindi gharama ya kununua Maji ni kubwa kuliko gharama ya chakula, na wananchi wengi walikuwa wakitumia muda wao mwingi kuhangaika kutafuta Maji jambo ambalo lilikuwa likikwamisha kutekeleza majukumu mengine ya kujenga nchi” alisema Massawe.

Nae mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Bi. Sofia alisema; “Kweli DAWASCO imemtua mama ndoo ya Maji kichwani, sisi akina mama ndio tuliokuwa tukiteseka zaidi na suala la Maji, lakini akina mama wa mtaa huu tulijitoa ili kupambana na janga la Maji ambalo lilikuwa likitukabili, na hatimaye tumefanikiwa kupata huduma ya Maji”

Kwa upande wa Dawasco, Meneja wa Mkoa wa Tegeta, Bw. Alpha Ambokile amewataka wakazi wa mtaa huo kujitokeza kwa wingi kufanya maombi ya kuungiwa huduma ya Maji kwa kuwa tayari huduma hiyo imefika katika makazi yao, baada ya kuhangaika kwa muda mrefu wakisaka huduma hiyo, na ameahidi kuwaunganishia huduma Maji mapema na kwa uharaka zaidi, mara tu baada ya kupokea maombi yao ya kuungiwa huduma.

“Ninawaomba mjitokeze kwa wingi ili kwa pamoja tuweze kuwaunganishia huduma ya Maji, nitawatengea siku yenu maalum ambayo timu yangu ya ufundi itakuja kuwafanyia maunganisho ya Maji, ambao bado hamjafanya maombi, fanyeni haraka ili tuweze kuwaunganishia wote kwa pamoja huduma ya Maji” alisema Ambokile.
Sehemu ya wakazi wa mtaa wa Upendo, Mbezi salasala wakiwa na Mjumbe wa mtaa huo, Bw. Robert Massawe (aliyevaa shati ya bluu), wakisikiliza kwa makini katika kikao cha pamoja na uongozi wa Shirika la Maji safi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) kutoka mkoa wa Tegeta, baada ya mtaa huo kufikiwa na huduma ya Majisafi na salama kwa mara ya kwanza tangu waanze kuhamia katika makazi hayo, jijini Dar es salaam.

KUMALIZIA MICHUANO YA ICC: LIVERPOOL KUKIPIGA NA BARCELONA LEO

0
0
KUELEKEA ukingoni mwa Michuano ya kirafiki ya Kimataifa (ICC), Jioni ya leo ndani ya dimba la Wembley jijini London, takribani watazamaji 90,000 wanadhamiwa kukaa vitini kuutazama mtanange mkali wa kukata na shoka kati ya majogoo wa jiji Liverpool na mabingwa wa Laliga Fc Barcelona. Mpambano huu unawakutanisha mabingwa wa Ulaya mara 5 kila moja. 

Timu hizi mbili zimewahi kukutana katika mchezo wa kirafiki kama huu takribani miaka 40 iliyopita, zilikutana mwaka 1977 ndani ya dimba la Olympic Stadium, Amsterdam huko Uholanzi ambapo Liverpool wakiwa chini ya kocha Bob Paisley, walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na David Johnson.

Baada ya hapo timu hizi zimewahi kukutana tena mara sita katika mashindano ya Ulaya tangu mwaka 2001-2007, ambapo kila timu iliweza kupata ushindi mara mbili, kupoteza mara mbili na kutoka sare mara mbili. 
Tarehe 5/4/2001 timu hizi zilikumbana katika michuano ya Uefa Cup, Nou Camp, Barca wakiwa na magwiji kama Luis Enrique kocha wa sasa wa timu hiyo, Pep Guardiola, Patrick Kluivert na Rivaldo, huku Liver ikiwa na nyota kama Robbie Fowler, Steve Gerard na Michael Owen. Timu hizi hazikuweza kufungana.

Tarehe 19/4/2001, kwenye Uefa Cup huko Anfield Liverpool wakapata ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Gary McAllister. Lakini mwaka huo huo 2001 November 20 katika uwanja wa Nou Camp Barcelona wakailaza Liverpool kwa mabao 3-1, Liver walianza kwa bao la Michael Owen lakini Barca wakapata mabao yao kupitia kwa Kluivert, Overmass na Rochemback. 2002, March13, kwenye Champions league huko Nou Camp timu hizi hazikuweza kufungana.

Februari 21-2007 katika michuano ya Champions League ndani ya dimba la Camp Nou wenyeji Barcelona walilala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Liverpool kwa mabao ya Craig Bellamy na John Arne Riise huku Deco akiifungia Barcelona bao la kufutia machozi.
Mwisho ilikuwa 2007, March 6, katika uwanja wa Anfield kwenye michuano ya Champions League Liverpool ililala dhidi ya Barcelona kwa bao 1-0, goli ambalo lilifungwa na Eidur Gudjohnsen. Wakati huo Barcelona walikuwa wamesheheni wakali kama vile Samwel Eto'o, Ronaldinho na Lionel Messi.

Kivutio kikubwa katika mchezo huu ni urejeo wa mchezaji Luis Suarez alijiunga na Barcelona akitokea Liverpool huku akiwa ni kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo, swali ni je atapokewa vipi?

TAASISI YA VIJANA YA TYVA YAADHIMISHA MIAKA 16 YA KUUNDWA KWAKE

0
0
Katibu tawala wa Manispaa ya  Ilala, Mh.Edward Mpogolo(wa pili kutoka Kulia) akikata keki na Mwenyekiti wa TYVA, Nuria Mshare wakati wa maadhimisho ya miaka 16 ya taasisi ya Vijana ya TYVA  iliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council. wa kwanza kulia ni Afisa vijana wa Jiji la Dar es Salaam, Masalida Zephania Njashi na wa kwanza kutoka kushoto ni Zulekha Ibrahim. (Picha na Geofrey Adroph)
Pia mgeni rasmi alizindua kitabu cha mtazamo wa Vijana Bajeti ya mwaka wa fedha ya 2016/2017 kilichoandikwa na Taasisi la Vijana la TYVA pamoja na kuzindua Dokumentari ya Video ya Binti Jitambue.

Katibu tawala wa Manispaa ya  Ilala, Mh. Edward Mpogolo akuzungumza na vijana wa shirika lisilo la kiserikali la TYVA waliofika katika maadhimisho ya miaka 16 ya shirika hilokatika ukumbi wa British Council leo jijini Dar.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

AFRICAN SPEAKERS LOBBY FOR A STRONGER CONTINENTAL ASSEMBLY -WANT AU MEMBER STATES TO RATIFY MALABO PROTOCOL

0
0
East African Legislative Assembly, Midrand, South Africa: August 5, 2016: The 8th Annual Conference of Speakers has opened in Midrand, South Africa.  In attendance at the two-day Conference whose theme is from “Adoption of the African Union Treaties in particular the new Protocol of the PAP” are over 30 Speakers from the National Assemblies and Regional Parliaments in the continent.

The Prime Minister of Lesotho, Rt Hon Bethel Pakalita Mosisili opened the two-day conference.

In his remarks, the Prime Minister reiterated the importance of ratifying the Constitutive Act of the African Union relating to the Pan-African Parliament that empowers the continental Assembly to execute its mandate to accord credence to the AU Policies and programmes. 
A section of the African Speakers in attendance

“African States are urged to sign and ratify the Malabo Protocol.   In addition, a balance of legislative powers must be struck between the National Parliaments and the Continental Assembly (PAP) to ensure acceptability as we move towards continental free trade area and continental integration” the Premier said.

The Prime Minister called for popular participation and engagement of citizens in the processes. “It is absolutely critical that we carry our people along.  It cannot and must not be a leaders’ or a Governments’ issue alone.  Our people must fully comprehend, accept and own the process.  The need for concerted education on the matter cannot be overemphasized.  This is so as to avoid a repeat of what happened in Europe – Brexit”, he added.

EALA Speaker, Rt Hon Daniel F. Kidega re-affirmed the need for African Governments to speed up the ratification process of the revised Protocol of the Pan African Parliament.  The Protocol among other things, aims at giving PAP opportunity to develop model laws and elections of Members through universal suffrage once the electoral code is in place.
The Prime Minister of Lesotho, Rt Hon Bethuel Pakalitha Mosisili opens the 8th Conference of Annual Speakers at the PAP headquarters in Midrand, South Africa.

Making key note remarks while presenting a paper entitled; “Plan of Action for PAP to achieve Legislative Powers, Rt Hon Kidega said legislation was a key function of any legislature and called for the harmonious balancing of power and interaction between the Parliament, the Executive and the Judiciary.

Wanaolewa kwa Fedha za TASAF kuondolewa kwenye Mpango huo

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akimkabidhi fedha Bw. Methesela Mrobi wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III ,katika kijiji cha Mwamgoba, Wilaya ya Busega Mkoani humo.

Na Stella Kalinga

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kata na vijiji kuwabaini wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya TASAF III (PSSN) wanaojihusisha na ulevi na kuwaondoa katika orodha ya wanufaika wa mpango huo.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega katika zoezi la uhawilishaji fedha za TASAF III PSSN, ambapo jumla ya shilingi 2,976,000 zimegawiwa kwa wanufaika 82 kijijini hapo.

Mtaka amesema lengo la mpango wa TASAF III ni kuwatoa watanzania katika hali ya umaskini kwa kuwapa ruzuku itakayowasadia kupata huduma muhimu ikiwa ni pamoja huduma za afya, kuwasaidia watoto wao waweze kwenda shule lakini baadhi ya wanufaika wamekuwa wakitumia fedha hizo kulewa badala ya kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku, mbuzi na kondoo pamoja na kilimo ili miradi hiyo iwasaidie kuwaongezea kipato.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.

“Hatuwezi kuleta fedha tukifikiri zitawasaidia kujikwamua katika Umaskini lakini mnashinda baa na vilabuni kulewa , wengine mnaongeza wake, tukiwabaini mtaondolewa kwenye huu mpango” , alisema Mtaka.


MASAUNI AWATAKA ASKARI WA USALAMA BARABARANI KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA AJALI KWA KUFUATA SHERIA

0
0
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Edwin Ngonyani, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Serikali ya Brazil yaonyesha nia ya kufanikisha azma ya Rais. Dkt. Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda

0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente, wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (Kushoto), akisaini Kitabu cha Wageni ofisini kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), alipomtembelea Waziri na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika uwekezaji kwenye sekta ya nishati.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (Kulia), wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala ya uwekezaji katika sekta za nishati na madini. Wengine pichani ni Maafisa wa Wizara waliohudhuria mkutano huo.

Na Veronica Simba

Serikali ya Brazil imeonesha nia kuwekeza katika sekta ya nishati nchini hususan katika kuzalisha umeme kwa kutumia maji na mabaki ya miwa. Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente, alipomtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake na kufanya mazungumzo naye.

Balozi Puente alimweleza Profesa Muhongo kuwa nchi yake inao ujuzi na uzoefu wa kutosha katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali hususan maji.

Alisema, Brazil ingependa kuchangia kufanikisha azma ya Rais John Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

“Kutekeleza mchakato wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda, unahitaji umeme mwingi unaotokana na vyanzo mbalimbali. Ni bahati nzuri kwamba Tanzania inazo njia za kufanikisha azma hiyo,” alisema.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Friedkin Conservation Fund na African Wildlife Trust wadhamini Rock City Marathon

0
0

IKIWA ni sehemu ya mkakati wa kupambana na ujangili pamoja na kutangaza utalii wa ndani kampuni za Uhifadhi za Friedkin Conservation Fund (FCF) na African Wildlife Trust (AWT) zimeamua kudhamini Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika Septemba 25 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na udhamini huo wa miaka mitatu, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hizo Bw Pratik Patel alisema kampuni mzake zitatumia mbio hizo kuzindua kampeni yao inayofahamika “*Okoa Wanyama Wetu*; *Kataa Ujangili”*

“Tutatumia Rock City Marathon kutangaza kampeni yetu ya kupinga ujangili
itakayofanyika katika baadhi ya majiji ulimwenguni.,’’ alibainisha Pratik. Alisema kampeni hiyo ya “*Okoa Wanyama Wetu*; *Kataa Ujangili”* itaanza nanmatembezi yatakayofanyika Septemba 24 mwaka huu jijini Arusha, Moshi na Dar es Salaam yakifuatiwa na mbio hizo Septemba 25, Uwanja wa CCM Kirumba.

“Tuliamua kudhamini Rock City Maratahon kwa kuwa lengo la mbio hizi ni
kutangaza utalii wa ndani na sisi tuliona kwamba huo utalii unaotangazwa
ili uwe na tija zaidi unategemea uwepo wa maliasili. Na ni wazi kwamba
uwepo wa maliasili hizi unategemea sana jitihada za kweli katika uhifadhi
wake! Na hapo ndipo hasa utatukuta sisi ,’’ alisema.

Wakizungumza kwenye uzinduzi wa mbio hizo jijini Mwanza hivi karibuni, Mkuu wa mkoa huo John Mongella na Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambae pia ni Rais wa chama cha riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka walipongeza wadhamini wa mbio hizo zikiwemo kampuni za Friedkin Conservation Fund (FCF) na African Wildlife Trust (AWT) kwa kuunga mkono jitahada za serikali  katika kutangaza utalii wa ndani pamoja na kupambana na ujangili hapa nchini.

Pamoja na pongezi hizo pia viongozi hao wa walikuwa wa kwanza kujisajili
kushiriki Rock City Marathon huku wakiahidi kuhakikisha kwamba mbio
zinapata washiriki wa kutosha sambamba na wadhamini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mbali na kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife
Trust,wadhamini wengine wa mbio hizo ni pamoja na  Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR
Solutions na kampuni ya Fabec.

Akizungumzia mbio hizo Mratibu kutoka kampuni ya Capital Plus Bw Mathew Kasonta alisema Rock City Marathon zitahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, kilomita 3 kwa ajili ya walemavu na zile za wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19.

Pia litoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani kujisajili kwa
kuchukua fomu katika vituo kadhaa vikiwemo Ofisi za michezo wilaya zote za
mkoa wa Mwanza, Ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na
Shinyanga,   Uwanja wa Nyamagana,  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino  Mwanza, Kituo cha michezo Malya na Shule ya Kimataifa ya Isamilo,

“Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu jengo la ATC, jijini Dar es, Salaam na vituo vingine vitaendelea kutangazwa hivi
karibuni,” alihitimisha.

SERENGETI BOYS ILIVYOWADINDIA WASAUZI

0
0
Ikicheza mbele ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Naibu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Rosemary Chambe Jairo, timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys leo imegoma kupoteza mchezo dhidi ya wenyeji Afrika Kusini baada ya kuibana Amajimbos na kutoka sare bya bao 1-1.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini –Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti kwa kila upande. Afrika Kusini walianza kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa na Linamandlia Mchilizeli kabla ya Ally Msingi kuisawazishia Serengeti Boys katika dakika ya 70.

Penalti ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys kumfanyia madhambi Mchilizeli  wa Amajimbos ndani ya eneo la hatari wakati ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos kunawa mpira eneo la hatari.

Afrika Kusini iliyoanza kwa kasi dakika 10 za mwanzo wa mchezo huo, ilipotea dakika zote 30 za kipindi cha kwanza ambao kukosa bahati na umakini kidogo tu kwa nyota wa Serengeti Boys kulisababisha kukosa mabao matano yakiwamo mawili yaliyogonga mwamba hivyo kuwatia hasira Serengeti Boys ambao walionyesha kuwa na njaa ya mabao.

Kubanwa katika kipindi cha kwanza, kulisababisha Kocha Mkuu wa Amajimbos kufanya mabadiliko ya wachezaji wote watatu kipindi cha pili, wakati Bakari Shime kwa upande wake alimpumzisha Ibrahim na nafasi yake kuchukuliwa na Muhsin ambaye alisaidia kuendedlea kuwabana Afrika Kusini waliokjuwa wanawategemea nyota kama na Mswati Mavuso na Lethabo Mazibuko.
Shukrani za pekee zinaweza kwenda kwa Kipa Ramadhani Kabwili aliyeokoa hatari nyingi ikiwamo mpira uliokuwa unakwenda golini uliotokana na adhabu ndogo. Kadhalika Msengi aliyekuwa nyota wa mchezo huo akimiliki vema idarta ya ulinzi akishirikiaana nDickson Job.

Shime maarufu kama Mchawi Mweusi alisema: “Nashukuru kwa matokeo haya. Si mabaya kwangu. Tunarudi nyumbani kujipanga. Afrika Kusini ilikuwa inanitia hofu ndio maana nilisema mechi itakuwa ngumu.”

Kwa upande wake, Naibu Balozi Rosemary alisema: “Ahsanteni vijana (Serengeti Boys) kwa kulinda heshima yangu,” wakati Malinzi alisema: “Sina mengi. Mkiwafunga Afrika Kusini Agosti 21, 2016 kambi inapigwa tena nje ya nchi. Sijui ni nchi gani, lakini mtakwenda kujiandaa nje ya nchi.”

Katika mchezo huo, Kikosi cha Serengeti kilikuwa: Ramadhani Kbawili, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Ally Msengi, Dickson Job, Shaban Ada, Kelvin Naftal, Ally Ng’anzi, Ibrahim Abdallah/Muhsin Makame (Dakika ya 72), Asad Juma na Mohammed Rashid.

Afrika Kusini: Glen Tumelo, Mswati Mavuso, Luke Donn, Sechaba Makoena, Kwenzokuhle Shinga, Mjabulise Mkhize, Bonga Dladla, Linamandla Mchilizeli, Luke Gareth, James Monyane na Siphamandla Ntuli.

UCHAMBUZI WA MAGAZETI LEO

Viewing all 109594 articles
Browse latest View live




Latest Images