Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1308 | 1309 | (Page 1310) | 1311 | 1312 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Captain Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Captain Sadick Muze kwa kosa la  kuchagua rubani mmoja ambaye hajakidhi vigezo anavyotakiwa kuwa navyo marubani wanaotarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Canada kwa  ajili ya mafunzo  ya kurusha ndege mpya mbili zinazotarajiwa kuwasili nchini katikati ya mwezi Septemba.

  Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Kyela, Mkoani Mbeya Prof. Mbarawa amesema baada ya kukamilisha malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya kwa ajili ya ATCL  alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo kuwachagua marubani watano wenye vigezo ambavyo vinahitajika kwa ajili ya mafunzo hayo jambo ambalo amebaini mmojawapo wa waliochaguliwa hajatimiza vigezo na hivyo kuamua kumsimamisha kazi kwa kosa la uzembe.
  Waziri  Mbarawa amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha kila mtumishi  wa umma anatekeleza wajibu  wake kwa kufuata sheria kanuni na taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo huo Serikali haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu.
  Shirika la Ndege Tanzania katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege tatu.

  0 0
 • 08/04/16--07:06: Serengeti Boys yatua sauzi
 • Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini wakitokea Antananarivo, Madagascar walikoweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. 
  Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys na viongozi walipowasili Hoteli ya Garden Court Milapark ambako imepiga kambi kabla ya kuivaa Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)

  0 0

  Na Greyson Mwase, Shinyanga

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ameitaka kampuni ya Pangea Minerals Ltd ya Canada inayofanya shughuli za utafutaji wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Mwakitolyo Mkoani Shinyanga kuachia sehemu ya Leseni yake ili eneo hilo litengwe na kumilikishwa Wachimbaji Wadogo.

  Akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Shinyanga pamoja na Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Pangea Minerals Ltd mkoani Shinyanga, aliitaka kampuni hiyo ambayo imeanza mazungumzo ya kuuza eneo hilo kwa kampuni ya Busolwa Mining Ltd, kuachia sehemu ya leseni yake yenye namba PL 5044/2008 ambayo kwa sasa wananchi wanaokadiriwa kufikia 3000 wanajishughulisha na uchimbaji mdogo wa dhahabu katika eneo hilo tangu mwaka 2011.

  Alifafanua kuwa ili kuepuka mgogoro huo ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya kampuni hiyo na wananchi hao, ni vyema kampuni hiyo itoe ushirikiano kwa kijiji hicho kwa kuachia sehemu ya leseni yake ili wananchi nao wapate maeneo ya kufanyia shughuli za uchimbaji wa madini.

  Dk. Kalemani aliitaka kampuni hiyo kuachia eneo hilo kwa Kamishna wa Madini ifikapo Agosti 17, 2016 ambapo eneo hilo litaanza kugawanywa kwa wananchi kuanzia Septemba 2, 2016.

  Wakati huohuo Naibu Waziri Kalemani aliwataka wachimbaji wadogo kuheshimu sheria za nchi na kukubali kuhamia eneo litakalotengwa kwa ajili yao ifikapo tarehe 2 Septemba, 2016.

  Naye Mwakilishi na Mkurugenzi kutoka kampuni ya Pangea Minerals Limited Ltd, Deo Mwanyika alikubali maamuzi hayo na kueleza kuwa kampuni ipo tayari kukabidhi sehemu ya leseni hiyo ili iweze kutumiwa na wananchi.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliipongeza serikali kwa mikakati yake ya kusaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapatia maeneo ya kujiajiri kwa ajili ya kujiongezea kipato.

  Aliwataka Wachimbaji Wadogo kutojihusisha na vitendo vya kiharakati na kuwarubuni baadhi ya wachimbaji na kupinga juhudi za Serikali kwa kuchochea vurugu migodini badala yake wayatumie maeneo hayo waliyotengewa kwa shughuli za kiuchumi.

  Eneo la Mwakitolyo ni kati ya maeneo yenge utajiri wa dhahabu hapa nchini yanayomilikiwa na kampuni ya Acacia kupitia kampuni yake tanzu ya Pangea Minerals Ltd.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akisisitiza jambo katika moja ya vikao vyake.

  0 0

  MTU mmoja amefariki dunia jana  baada ya kugongwa na geti la lango la kuingilia treni Stesheni jijini Dar es Salaam, Ajali hiyo imetokea baada ya   Marehemu kunining’inia nje ya behewa wakati wa treni ya Pugu ilivyokuwa  ikitoka eneo la  stesheni majira ya jioni.

  Katika Taarifa ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) iliyotolewa na na Afisa ya Uhusiano Kwa niaba ya  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Focus Makoye Sahani  imeeleza kuwa  tofauti ya usafiri wa basi ni kuwa na kondakta anaweza kusimamisha basi ili kumshusha mtu anayening’inia nje lakini kwa treni jinsi ilivyo ndefu  hilo haliwezekani.

  Pia ametoa wito kwa wasafiri  na wananchi kwa jumla wanaotumia usafiri huo  kufuata masharti ya usafiri ili kuepuka maafa yaliyomkuta mwenzetu.

  Taarifa hiyo imeeleza kuwa kikosi kazi cha TRL hapo kesho Agosti 5, 2016 kitaanza kampeni za kuwahamasisha wananchi wanaofanya shughuli  katika maeneo  ndani ya mita 15 za tuta la reli kuhama kwa hiyari. 

  Hatua hiyo inachukuliwa ili kuwaepusha wananchi hao na uwezekano wa kupata madhara endapo ajali ya treni kuacha njia itatokea na pia kulinda tuta la reli dhidi ya mmonyoko unaosababishwa na shughuli za kibinadamu za kila siku . Kikosi kazi hicho kitahusishwa Idara ya Usalama na Ulizni wa reli na Kikosi cha Polisi TRL.

  Watumiaji wa huduma za usafri wa treni za abiria za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wametakiwa  kuzingatia  sheria za matumizi ya usafiri huo ili kuepuka adhabu ya kufungwa jela miezi sita.

  Nae   Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Polisi TRL ACP Mary Lugola amesema matumizi ya usafri wa abiria unasimamiwa na sheria , kanuni ,taratibu na masharti maalum. Mojawapo amelitaja ni kutodandia mabehewa baada ya milango kufungwa.

  ‘Endapo mtu atafanya kosa hilo atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita”.Alisisitiza Afande Lugola.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza kwa unyenyekevu mbele ya Wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakati alipokutana nao ili kujitambulisha na kufahamiana nao baada ya kuanza kazi kama mkuu wa wilaya hiyo, Aliwaomba wazee hao kushirikiana naye bega kwa bega na kumpa ushauri wa kila mara ili aweze kutekeleza majukumbu yake ya kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo na kufanikisha mipango ya Rais Mh. Dk John Pombe Magufuli ili kutekeleza kwa ufanisi ilani ya uchaguzi ya CCM, Katika picha kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Asaa Simba , Mkutano huo ulifanyika kwenye ofisi za CCM wilaya ya Ilala.
  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Asaa Simba akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema ili kuongea na wazee wa CCM wilaya ya Ilala.
  Baadhi ya wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakiwa katika mkutano huo uliowakutanisha na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.
  Baadhi ya wazee wa CCM wilaya ya Ilala wakiwa katika mkutano huo uliowakutanisha na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akikagua timu wakati wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars mkoani humo. Ameambatana na mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Mwanza (MZFA) Jackson Songora.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akipiga penati kufungua rasmi michuano ya Airtel Rissing Stars mkoani humo

  Mwanza. 
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mheshimiwa John Mongella leo amefungua mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoani humo na kuwataka vijana kuzingatia nidhamu na taratibu zinazoongoza mchezo huo maarufu duniani.

  “Hata ukiwa na kipaji cha aina gani bila kuwa na nidhamu kamwe huwezi kutimiza ndoto yako ya kuwa mchezaji nyota wa mpira wa miguu kwa sababu, kama ilivyo kwenye nyanja nyingine yoyote, mchezo wa soka unaongozwa na kanuni na sheria ambazo kila mchezaji lazima azifuate”, alisema.

  Alisema kuwa binafsi anaifurahia sana programu ya Airtel Rising Stars kwa kuwa inakwenda sanjali na mikakati ya serikali ya kuwawezesha vijana. “Wote tunafahamu kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni chanzo cha ajira ya kuaminika kwa vijana duniani. Mnaweza kupata kipato na kuboresha maisha yenu kupitia mpira”, alisema Mongella na kuipongeza kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuwekeza katika soka kupitia programu hii ya vijana.

  Alisema michuano ya Airtel Rising Stars inasaidia kubaini wachezaji wenye vipaji kutoka sehemu mbalimbali ambao bila mashindano haya wangeweza kupotea hivi hivi. Aliwataka viongozi wa soka mkoa humo kushirikiana na shirikisho la soka nchini (TFF) kuwalea na kuwaendeleza vijana wanaopatikana kupitia Airtel Rising Stars.

  Akiongea katika hafla hiyo ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Mwanza (MZFA) Jackson Songora alisema kuwa Airtel Rising Stars imetoa hamasa kwa vijana wengi mkoani Mwanza kucheza soka na kuonyesha vipaji vyao. “Tunajivunia kuweza kutoa mfungaji bora na mchezaji bora katika fainali za mwaka jana. Aliwataja wachezaji hao kuwa ni David Richard na Cypria Mtesigwa.

  Songora pia alisema kuwa mkoa wa Mwanza umetoa wachezaji wa kutegemea katika timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Serengeti Boys. Aliwataja wachezaji hao walioibuliwa kupitia Airtel Rising Stars kuwa ni Arish Suleiman, Cypria Mtesigwa, Ally Ng’anzi na Ally Hussein Msengi.

  Kwa upande wake, Meneja wa kanda ya ziwa wa Airtel Tanzania Emmanuel Raphael alisema kuwa kampuni yake inajivunia kuweza kutoa mchango katika soka la Tanzania. “Airtel Rising Stars imekuwa chanzo cha kutumainiwa kwa klabu na timu za Taifa kupata vijana chipukizi wenye vipaji. Tunaona fahari kuweza kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Raphael.

  Hafla hiyo ya ufunguzi ilishuhudia mchezo wa ufunguzi kati ya Barass Sports Centre na Alliance Academy ambapo Barass Sports Centre waliwaduwaza wapinzani wao kwa kuwatandika 4-1. Mshambuliaji Frank Osoro alikuwa moto wa kuotea mbali na kufanikiwa kufunga magoli huku goli la nne likifungwa na mlinzi wa Alliance aliyejifunga mwenyewe katika juhudi za kuutoa mpira katika hatari. Alliance Sports walipata goli la kufutia machozi kwa njia ya penati iliyofungwa na Rashid Hamis


  0 0

  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akimkabidhi nyenzo za kazi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt. Ben Moses kushoto wakati wa Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) Bw. Hiiti Sillo wa pili kushoto akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Ushauri TFDA wakati wa Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam.

  Na Ally Daud 

  Serikali imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje zipatikane nchini.

  Akizungumza hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga hatua katika uchumi wa viwanda.

  “Serikali kupitia wizara yangu tumetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa kutumia viwanda”.alisema Mhe. Ummy.

  Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa kushirikiana na Serikali wanapaswa kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye ubora kwa matumizi ya binadamu ili kupunguza magonjwa yanayotokana na sumu za kemikali zitokananzo na dawa hizo.

  Mhe. Ummy ameongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane na Taasisi ya viwango nchini (TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi viwango na ubora unaopaswa kutumiwa na Watanzania.

  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili kuwawezesha watanzania kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu .

  Mbali na hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa ikusanye mapato kwa wingi zaidi ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga hatua kiuchumi ili isaidie wananchi katika shughuli za maendeleo.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt.Ben Moses amesema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri na watayafanyia kazi kwa haraka na ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA KAZI TU”.

  “Tumepokea maagizo ya Mhe. Waziri na nataka kumuhakikishia kwamba tutaendelea na kasi yetu ili kuifikisha nchi yetu kwenye kilele cha maendeleo na Afya bora” alisisitiza Dkt. Moses.

  0 0

  At first glance, we may seem worlds apart – two women from different countries and different generations. We met for the first time under the Olympic flame, and discovered that we are not that different: we share the burning hope of a world where gender equality is not a luxury, but the norm. When we walked side by side, sharing the great honor of carrying the Olympic Torch through the streets of Rio de Janeiro, Brazil, we represented more than just ourselves. We were there representing all women and girls – half the world’s population.

  Historically, the Olympic Flame represents the value of purity and the runners who carry the Olympic Flame convey a message of peace on their journey. While carrying the flame, at this time of widespread conflict in the world, we thought of how important it is that women contribute to peace processes. We know that when women are present at the peace table it is considerably more likely that agreements will be signed and that peace will last.

  We also know that making peace is more complex than ending war. True peace comes to life through the right to live free from fear of violence, free from discrimination, fulfilling our full potential, in our families, communities, schools, work places, or sport fields. With every step we took under that flame, we carried the Torch forward, and with it the message of Gender Equality.

  In that brief walk we followed pioneering women such as sailor Hélène de Pourtalès, first female Olympic champion (1900); Enriqueta Basilio, first woman to light the Olympic Cauldron at the Olympic Games in Mexico City (1968), and Flor Isava Fonseca, the first woman to serve on the International Olympic Committee’s Executive Board (1990).

  We carried the Olympic Flame cheering for the thousands of women athletes who will be part of the Rio Games and who, with their swiftness and endurance in the sports arena, increase women’s visibility as top-achieving sports icons, strategic thinkers, role models and leaders. We also raised the flame for all the young women and girls in even the furthest- flung villages who are fighting against all odds to play sport, stay on the field, and reap its benefits of broader freedoms.

  Since women’s first participation in the Olympics in 1900 they have brought down gender barriers and reduced discrimination. Today, at the Rio Games, we are just under parity in terms of participants and events. Yet outside, entrenched obstacles remain to full equality.

  In Brazil, as in many other places around the world, adolescent girls and young women are often pressured to conform to traditions and social stereotypes. They enjoy less autonomy over their bodies, and often lack an environment that helps them develop sports skills. By contrast their male counterparts enjoy new privileges as they grow up that are reserved for men, including autonomy, mobility, and power. Globally, only one in five parliamentarians is a woman; one in three women worldwide experiences violence against her, and without change in the present rate of progress, it will take another eight decades for women to achieve equality in work.

  But change is coming from all directions, with international movements like UN Women’s “HeForShe” where men take the initiative to stop discrimination and reshape expectations, with the building of “Equal Pay’ campaign, and local programs like ‘One Win Leads to Another’ in Brazil, where under-privileged girls in Rio de Janeiro will develop leadership skills through sport, improving their ability to influence decisions that impact their lives at all levels.

  As we walked through Rio’s cheering crowds, we witnessed how sport unites people from all walks of life with the power to rise above differences of sex, race, religion, and nationality. We dared to hope that this flame will spread, and that the determination to achieve gender equality will transcend all obstacles.

  0 0


  0 0

  Panapo majaliwa kama tutafanikiwa kuiona siku ya Tarehe 6/8/2016 tambua kuwa Kwenye yale mambo yetu ya Fashion Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin kutoka Tanzania pamoja na wanamitindo wengine watatimua vumbu katika onesho kubwa la Mitindo "Kenya Woman Reunion" linalo tarajia kufanyika huko Dallas Texas. Kama wewe ni mmoja kati ya wadau wa Tasnia ya mitindo endelea ku-Suport Mitindo ya Tanzania.


  0 0

  Na Mwene Saidi
  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa madai ya kutoa lugha ya uchochezi na kwamba mapema kesho anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

  Akizungumza na Blogu ya Jamii kwa njia ya simu ,Wakili wa Lissu, Peter Kibatala alisema mteja wake alikamatwa jana mkoani Singida.
  "Alikamatwa jana saa 12 jioni mkoani Singida wakaanza safari akiwa chini ya ulinzi hadi Kituo cha Polisi Chamwino Mkoani Dodoma

  "Leo mchana waliwasili Kituo Kikuu Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam...walianza kumhoji saa 9 hadi 9;30 Mahojiano yalihusu kujihusisha na matamshi ya uchochezi katika viwanja vya mahakama ya Kisutu" alisema Kibatala.

  Aidha alisema kwa mujibu wa sheria hadi kufika kesho asubhi Lissu atakuwa amekaa chini ya ulinzi wa polisi kwa masaa 36 kwa hiyo inatakiwa apelekwe mahakamani ama kuachiwa kwa dhamana.

  0 0

  CD cover iliyobeba nyimbo na video zililizoimbwa na Mh Dr Rehema Nchimbi (RC) akishirikiana na Kamanda Joyce Mwaikofu, kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa watanzania wote kupitia Sanaa ya Uimbaji.
  “Video ipo tayari na Muda si mrefu itaanza kusamba kwenye vyombo vya habari, na kazi hii haitauzwa ni bure hivyo vyombo vyote vya habari vinaombwa kushiriki katika kuwafikishia ujumbe huu wa Tanzania ili kuifanya Tanzania  yetu iendelee kuwa ya Amani na Upendo kwa minaji ya kuwapa watu nafasi ya kufanya kazi za ujenzi wa Taifa kama anavyo tuasa Rais wetu wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli” Amesema Mtoto wa Mh Dr Rehema Nchimbi,  Bw. Sixmund Nchimbi.


  0 0

   Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada  Kikosi ya mazoezi kwenye viwanja vya mazoezi ya Uwanja wa FNB, Johannesburg Afrika Kusini. 
  Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys wakiwa na furaha ya aina yake mara baada  Kikosi ya mazoezi kwenye viwanja vya mazoezi ya Uwanja wa FNB, Johannesburg Afrika Kusini. 

  Mmoja wa makipa wa Serengeti Boys, Kelvin Kayego akinolewa na Kocha, Juma Kaseja.(Picha na Alfred Lucas wa TFF).  0 0


  SIMU.TV: Serikali imeazimia kuvilinda viwanda vya ndani ili viweze kuzalisha bidhaa zinazoweza kushindana na bidhaa zinazotoka nje ya nchi. https://youtu.be/4t4ry8opqzk

  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda ametoa kiasi cha laki moja na nusu kwa ajili ya matibabu ya mkazi wa Temeke jijini Dar es salaam.https://youtu.be/x06ZDLBIHzs

  SIMU.TV: Kamati ya usalama barabarani imekuja na utaratibu wa kuweka alama kwenye leseni za madereva watakaosababisha ajali barabarani. https://youtu.be/pa7yiwAH2Tc

  SIMU.TV: Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee, watoto na walemavu Ummy Mwalimu, ameitaka mamlaka ya uthibiti wa dawa na chakula kuthibiti dawa zote feki zinazoingia nchini. https://youtu.be/0550oV3Shq4

  SIMU.TV: Maonesho ya nane nane yameendelea kuwa chachu ya wananchi kuelimika na kupata fursa ya kujua miradi ya maendeleo inayofanywa na serikali.https://youtu.be/0Cp12JKWpQ8

  SIMU.TV: Serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kubaini gharama halisi zilizotumika kujenga jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe.https://youtu.be/WIxASSdZQu4

  SIMU.TV: Serikali imesema itaendelea kuzisaidia na kuziunga mkono taasisi za fedha zilizojikita katika kuinua wananchi wahali ya nchini kiuchumi.https://youtu.be/ZOMbWGMwS2w

  SIMU.TV: Naibu waziri ofisi ya rais TAMISEMI amewataka wananchi wanaosubiri ajira mpya na watumishi wanaosubiri kupandishwa vyeo kuwa na subira, maana serikali inakaribia kumaliza zoezi la uhakiki wa watumishi. https://youtu.be/HiVR2K-UN70

  SIMU.TV: Wananchi katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wamelalamikia wafugaji kuvamia mashamba yao na kuwatishia maisha yao. https://youtu.be/p6y-GwJ1OVA

  SIMU.TV: Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU imethibitisha kumkamata rais wa klabu ya Simba Evance Aveva kwa tuhuma za rushwa.https://youtu.be/2M5dGtrNXYg

  SIMU.TV: Mabingwa wa soka Tanzania bara timu ya Yanga pamoja na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu zimekabidhiwa vifaa vya michezo na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom. https://youtu.be/KcdOcLkCUzw

  SIMU.TV: Timu ya Serngeti boys imewasili nchini Afrika Kusini ikitokea nchini Madagascar ilikokuwa imeweka kambi kwa ajili ya mchezo wake na timu ya vijana ya Afrika Kusini.https://youtu.be/h5v0O_OKgt4

  0 0

  Wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani wameshauliwa kuchukua shamba lenye ukubwa wa hekeri 66.6 ambalo alipewa mwekezaji tangu mwaka 1988 na kushindwa kuliendeleza,ili walitumie Kwa shughuli za kuzalisha mali.
     Ushauri huo ulitolewa wilayani humo na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kupokea malalamiko kutoka Kwa wananchi wake  akiwa katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
  Ulega alisema haiwezikani watu wanajimilikisha mashamba makubwa miaka hadi miaka alafu wanashindwa kuyaendeleza huku wananchi wakipata shida ya kukosa maeneo hata ya kulima kilimo cha mbogamboga vijana.
   "Nasema kuwa kama shamba hilo limekaa miaka yote hiyo haliendelezwi, na pia huyo mwekezaji haonekani sasa mnasubiri nini kulichukua na kufanya uendelezaji. Nashauri litwaeni alafu tutapambana nayo huko mbele"
  Pia Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa siasa imekwisha na kilichobaki ni watu kufanya Kazi Kwa nguvu zote na kwamba  atakuwa bega Kwa bega  katika kuhakikisha maendeleo  wanayapata Kwa haraka.
  Awali wananchi  wa kijiji cha Kurutu walimweleza mbunge kuwa wanavshamba kubwa ambalo alipewa mwekezaji miaka mingi iliyopita tena kienyeji lakini hadi leo ameshindwa kuliendeleza hivyo awasaidie walipate ili vijana wa eneo hilo wazalishe chumvi.
   Mbunge huyo bado anaendelea na ziara zake za kutembelea kijiji hadi kijiji kwa lengo la kuwashukuru na kuhimiza shughuli za maendeleo ambapo anawataka kujituma katika kufanya kazi kwani wilaya hiyo imechelewa kimaendeleo.
   Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mhe Abdallah Ulega akielekea kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani kwa mtumbwi.
   Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akikagua daraja
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na walimu wa shule ya  msingi  ya kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni 
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na  wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata shungubweni wilayani Mkuranga katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
  Mwanakijiji Shabani Omary  akiuliza swali kwa mbunge wa jimbo la mkuranga Mhe. Abdallah Ulega. Habari na picha na Emmanuel Masaka wa Globu ya Jamii

  0 0
  0 0
 • 08/04/16--20:30: KUMBUKUMBU
 • Leo tarehe 5/8/2016 ni mwaka ,mmoja tangu ututoke ghafla mpendwa Baba, Kaka, Babu, Mjomba Rogers Thomas Maeda.  Tunakumbuka upendo wako, hekima,  busara  na ushauri wako kwetu.  Unakumbukwa daima na mkeo Miriam, Baba yako Thomas Maeda,  Wanao: Ruth, Rehema, Cathy, Leah, Thomas, Clinton na little Rogers, Kaka yako Humphrey Maeda, Dada zako: Flora, Loveness, Faustina, Haika na Martha, Wapwa zako: Hosea, Thomas T, Lilian, Neema, Emma, Germanus, Gadios, Ruth, Koku, Tumaini, Neema, Mwajabu, Thomas M, Victoria, Veronica, Irene, Godbless, Suzan, Whynjones pamoja na mjukuu wako Brian. Wote tunakukumbuka na tuna imani umepumzika mahali pema peponi  pamoja na Mama Ruth, Dada Ida na Dada Mage. Tulikupenda sana lakini Mungu kakupenda zaidi, BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA – JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
  *Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie – upumzike kwa Amani*. 
  AMEN.

  0 0

  Shirika la ndege la RwandAir linategemea kupokea ndege mpya mbili aina ya Airbus zenye uwezo wa kubeba abiria 274 ifikapo mwezi Septemba 2016, ikiwa na Business class viti 30, Premium Economy Class viti 20 na Economy viti 224. Meneja mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Ibrahim Bukenya amesema ujio wa ndege hizo utaanzisha safari mpya za Bombay nchini India na Guangzhou nchini China. Aliendelea kusema kuwa Shirika hilo litaanzisha safari zake zingine kuelekea Abidjan, Harare, Durban, Abuja, Cotonou na Khartoum.
  Meneja mkazi wa Shirika la ndege la RwandAir, Ibrahim Bukenya. 

  0 0

  Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Maiko Lekule Laiser ,akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda, aliyepo kushoto kwa mkuu huyo ni mwenyekiti wa Taso kanda ya Kaskazini ndugu Athar Kitonga Shayo wakiwa katika uzinduzi wa maonyeho hayo ya wakulima na wafugaji katika viwanja vya Taso Themi nanenane Njiro Jijini Arusha. 


  Na Woinde Shizza,Arusha.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda amewataka Wakurugenzi wote wa Mikoa yote mitatu iliyopo Kanda ya Kaskazini,wabadilishe mabanda yao na wajenge ya kisasa zaidi kwaajili ya maonyesho ya wakulima na wafugaji ambayo yatakuwa na mvuto zaidi.

  Aliyasema hayo alipokuwa kifungua maonyesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vyaThemi nanenane Njiro Jijini Arusha,huku akiwataka Taso washirikiane na Jiji pamoja na viongozi wa mikoa yote ili waweze kutengeneza ukumbi mkubwa wa kisasa.

  Aidha alisema kumekuwa na changamotoya wananchi.kutoielewa kauli mbiu ya maonyesho ya nanenane mwaka huu hivyo basi amewaagiza wakulima na wafugaji waweze kuingia.kwenye mafunzo ya shamba darasa na kwenye mabanda ili waweze kupata elimu zaidi.

  Aliwaagiza washiriki wenye mabanda yenye technolojia za kilimo waandae taarifa fupi ambayo mwananchi atakwenda nayo nyumbani na zitakazo waletea mabadiliko katika maeneo wanayotokea.

  Sambamba na hayo aliwataka Taso kuangalia sheria viwanja vya maonyesho ambayo inapiga marufuku ongezeko la makazi ndani ya viwanja vya maonyesho,pia amewataka washiriki wote wa maonyesho watoe ushirikiano kwa vyombo vyabulinzi na Usalama na katika maeneo yao.
  Vijanana wa JKT Oljoro wakiwa wanatoa burudani siku ya uzinduzi wa maonyesho ya wakulima na wafugai ya nayandelea katika vianja vya Taso Themi nanenane mi njiro Arusha.
  Meya wa Jiji la.Arusha wa pili kutoka kulia ndugu Calist Lazaro akiwa wakiteta jambo na diwani wa kata ya Themi Melance  Kinabo wa kwanza kulia katika maonyesho yanayoendelea katika maonysho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.

  0 0

  RAIA wawili wa Kigeni wakamatwa jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuishi hapa nchini bila kibali na kuwa watumishi wa Serikali.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule amesema kuwa  Raia hao ni Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo  na Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi.

  Amesema kuwa Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo ambaye anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kinyume na sheria za nchi, na Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi ambaye alikuwa Mganga Mkuu katika kituo cha Afya Mburahati anatuhumiwa kufanya kazi Serikalini wakati si raia wa Tanzania.
  Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wawili wa Serikali ambao sio raia wa Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Watuhumiwa ambao sio raia wa Tanzania waliokuwa wakifanya kazi serikalini wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa Uhamiaji, kushoto ni Bw. Bahilanya Milingita aliyekuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)na kulia ni Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba ambaye alikuwa Mganga Mkuu Kituo cha Afya Mburahati.
  Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo.

older | 1 | .... | 1308 | 1309 | (Page 1310) | 1311 | 1312 | .... | 3353 | newer