Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

TIMU YA MAJESHI YAKABIDHIWA BENDERA TAYARI KWA KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita, Meja Generali Issa Nassoro (kushoto) akimkabidhi Bendera Mkuu wa Msafara wa timu teule za Jeshi, Brigedia Generali, Jairos Mwaseba, atakayeongoza timu itakayoshiriki mashindano ya Afrika Mashariki yanayoanza Agosti 5 hadi 18 Kigali Rwanda. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Agosti 3. 2016. (Picha na Seleman Semunyu, JWTZ).


BANDA LA NSSF LAVUTIA WENGI KWENYE MAONESHO YA NANENANE LINDI

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linashiriki kwenye maonesho ya nanenane ambayo yanafanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Katika maonesho hayo NSSF inatoa huduma mbalimali zikiwemo kutoa taarifa za michango za wanachama, kuandikisha wanachama wapya na kutoa kadi mpya kwa wanachama wa zamani, kutoa maelezo juu ya uuzaji wa nyumba za mtoni kijichi phase 3 na Viwanja vya Kiluvya na pia kutoa elimu ya mafao na huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF.

NSSF inapenda kuwakaribisha wananchi wa Lindi na Mtwara kutembelea banda lao lililopo kwenye viwanja hivyo vya Ngongo.
Afisa wa NSSF mkoa wa Lindi, Saad Juma akitoa maelezo kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi waliotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya Nanenane mkoani humo.
Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Lindi, Adam Mbena akimwandikisha kujiunga na NSSF mmoja wa wakazi wa Lindi aliyetembelea kwenye maonesho ya Nanenane.
Afisa Mifumo ya Kompyuta Rukia Penza akimuelezea mwanachama taarifa yake ya Michango alipotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya nanenane Lindi.
Afisa Masoko Muandamizi Amina Mmbaga akiwapa maelezo wakazi wa Lindi waliotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya nanenane anayoendelea mkoani Lindi.

JAMII YATAKIWA KUWAPA USHIRIKIANO WASICHANA WANAOSHIRIKI MASHINDANO YA UREMBO

$
0
0


Warembo wanaoshiriki shindano la miss kanda ya kaskazini kutoka katika mikoa ya Arusha,Manyara,Tanga na Kilimanjaro wakiwa nje ya hotel ya Clous view sehemu ambayo wanafanyia mazoezi kwa ajili ya shindano hilo linalofanyika july 6 katika viwanja vya ukumbi wa Triple A fm.


Na Woinde Shizza,Arusha

Jamii imetakiwa kuwapa ushirikiano wa kutosha wasichana wanaoshiriki mashindano ya urembo kwani mashindano hayo ni kazi kama vile kazi zingine.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka mrembo wa kanda ya kaskazini (Miss Kanda ya kaskazini ) wakati walipokuwa wakiongea kwa nyakati tofauti na Ripota wa Globu ya Jamii ndani ya hotel ambayo warembo hao wameweka kambi kwa ajii ya shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mapema jumamosi Julai 6 katika ukumbi wa Triple A uliopo jijini Arusha
warembo hao wakiwa katika pozi 



Mmoja wa washiriki hao aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Mohmed (18) Mshiriki kutoka mkoa wa Manyara alisema kuwa wazazi wengi hususani ndugu wamekuwa wakichukulia shindano hili kama ni sehemu ya uhuni kitu ambacho sio cha kweli



Alibainisha kuwa shindano hili ni zuri na linatoa ajira kwa vijana wengi na mbali na ajira pia linasaidia vijana wengi ambao ni wasichana kujiajiri wenyewe na wengine kuajiriwa katika sehemu mbalimbali.
Kwa upande wake mshiriki kutoka mkoani Tanga Rukaiya Hassan (20) alisema kuwa kuingia katika urembo sio uhuni wala si umalaya kwani, mtu kuwa na tabia chafu kama hizo ni hulka yake mwenyewe na sio mashindano haya ndio yanasababisha mshiriki au mshindi kuwa muhuni
Aidha pia aliongeza kuwa kwa upande wake anaamini kabisa atashinda katika kinyaganyiro hicho kwani anajiamini na aliwasihi wenzake iwapo itatokea mtu akitolewa nje asibahatike kuingia katika hatua ya tano bora asikate tamaa kwani anaweza pia kushiriki katika mambo mengine ikiwa ni pamoja na uwanamitindo.

Kwa upande wake muaandaaji wa shindano hilo Mkurugenzi wa Mwandago Ivestiment, Faustine Mwandago alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yameshakamilika wanasubiri tu siku ya tukio ifike kwani warembo wamepikwa wakapikia vya kutosha . 

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AWAAGIZA WACHIMBAJI MADINI KUPELEKA ORODHA YA WACHIMBAJI WADOGOWADOGO MADINI YA JASI NA MAKAA YA MAWE.

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo akizungumza na wadau mbalimbali wa uchimabji wa madini ya Jasi (Gypsum) na Makaa ya mawe nchini leo Jijini Dar es salaam na kuwaagiza wawakilishi wa wachimbaji wa madini ya Jasi (Gypsum) kutoka kanda zote hapa nchini kufikia Agosti 10-11 kupeleka orodha kamili ya majina ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya Jasi (Gypsum) na makaa ya mawe katika wizara ya Nishati na madini.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa uchimbaji wa madini jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa orodha ya majina  wachimbaji wa madini ikipelekwa watafanya marekebisho ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Mhandisi wa madini ya Jasi(Gypsum) kutoka kanda ya kusini Benjamin Mchwapaka akielezea changamoto zinazopatikana ukanda wao wa Kusini ambazo zinawafanya kufikia maleno yao ya kusambaza madini hayo kwenye viwanda tofauti hapa nchini.

amesema  kuwa mpaka sasa kuna leseni 1,115 zilizosajiliwa na maeneo yanayopatikana ni Kilwa Makaganga, Hoteli Tatu na Nondwa ambapo kuanzia 2009 uchimbaji umeongezeka na kuongeza upatikanaji wa jasi. Katika leseni hizo 7 ni za uchimbaji mkubwa , 22 ni za utafutaji wa ligi huku 1086 zikiwa ni za wachimbaji wadogo na kati ya hizo 306 uchimbaji unafanyika. 

Changamoto kubwa inayosababisha kushindwa kufikia maleni hayo ni pamoja na vifaa ikiwemo na ukosefu wa mitaji kwa wachimbaji hao huku wakiwa na mikataba isiyokuwa na tija kutoka kwa viwanda vinayochukua madini hayo kwani wanapatiwa miakatab ya siku 28 na malipo yanachelewa kufikia miezi 2 hadi 4. Ukiachilia hilo pia miundo mbinu imekuwa shida hasa kipindi cha masika wanshindwa kuchimba, ukosefu wa taarifa za kutosha  pia kina kirefu cha madini hayo ikiwemo na tozo zinazokera.
Mjiolojia na Mkuu wa Kitengo cha Kanzi Data (Database) Nchini,Masota Magigita akitolea ufafanuzi kuhusiana na masuala ya upatikanaji wa madini ya Makaa ya mawe mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo leo Jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wadau mbalimbali wa uchimbaji madini hapa nchini wakimsikiliza waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo jijini Dar es Salaam leo. Picha na Yasri Adam, Globu ya Jamii.

DC WA ILALA MH SOPHIA MJEMA AKABIDHIWA MSAADA WA MADAWATI KWA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO WENYE ASILI YA CHINA JIJINI DAR LEO

$
0
0


Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akimkabidhi moja ya dawati kati ya 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Karikoo wenye asili ya China ,kwa Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema mapema leo jijini Dar.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 200 kutoka kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya China leo jijini Dar,kwa ajili ya shule ya msingi Maghorofani iliyopo Gongolamboto,jijini Dar Es Salaam.Wafanyabiashara hao waliahidi kumkabidhi Mh.DC Mjema Madawati 200 lakini leo wamekabidhi nusu ya madawati hayo (100),huku mengine yakiendelea kutengenezwa.Shule hiyo ya Maghorofani ilikuwa na uhitaji wa madawati 525,yakapatikana madawati 250 na kupungukiwa madawati 275.
Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akizungumza kwa ufupi mbele ya Waalimu,wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),kabla ya kukabidhi madawati 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariako wenye asili ya China jijini Dar,pichani kulia ni Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema. 
Baadhi ya Wanafunzi wa shule hiyo ya Maghorofani wakiwa wamekalia baadhi ya madawati yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya China jijini Dar. 
Wakiwa katika picha ya pamoja .PICHA NA MICHUZI JR.

VYUO 5 VYAFUTIWA USAJILI, 175 VYAPEWA NOTISI YA KUSHUSHWA HADHI.

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mhandisi Steven Mlote(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,wakati wa alipokuwa akitoa tamko la baraza hilo juu ya kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati ya 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja ,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini,Katikati Kaimu wa baraza hilo Dkt. Adolf Rutayuga na Mkurugenzi wa Udhibiti,Ufuatiliaji na Tathimini Bi. Agness Ponera.
Baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwa kwenye mkutano wakati Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi Steven Mlote(hayupo pichani)alipokuwa akiongea na waandishi habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na tamko la baraza hilo kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati hivyo 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini. 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kuwa vyuo 5 vimefungwa kuendesha mafunzo na kufutwa kwenye rejista ya vyuo vya ufundi nchini.
Pia Baraza limetangaza kuwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vimepewa muda wa wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Vilevile, vibali vya  usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati  vyuo 57 vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati, imetangazwa jana.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza (NACTE), Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) Bw Edwin Rutageruka atembelea mabanda ya nane nane lindi

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) Bw Edwin Rutageruka akipata naelezo kutoka kwa Bw John Julius juu ya uzalishaji wa mafuta ya ufuta katika banda la halmashauri ya Masasi kwenye maonesho ya 88 mkoani Lindi. Mafuta ya ufuta yanasoko kubwa sana nje ya Afrika hasa nchi ya Japan na ni mafuta ya pili yenye ubora baada ya olive oil. 
Lengo kuu tasisi hii kushiriki maonesho haya ni kuunganisha wazalishaji na masoko ya ndani na nje ya nchi. Hivo imekuwa ikipita kwa wazalishaji mbalimbali kuangalia fursa za kuwaungaisha na masoko mbalimbali ili kukuza uchumi wa nchi yetu na pia kualika wawekezaji katika nchi yetu na kuifanya Tanzania yenye viwanda. Tantrade imeshirik katika maonesho haya maarufu kama 88 kwenye kanda tano ambazo ni Lindi, Morogoro, Mwanza, Mbeya na Arusha na kila mkoa wazalishaji hutofautiana kutokana na aina za uzalishaji wa bidhaa za kila mkoa.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0


SIMU.TV: Serikali imetoa tani 100 kwa ajili ya kaya 850 zilizokumbwa na njaa baada ya vyakula vyao kuharibiwa na mafuriko wilayani Ludewa mkoani Njombe;https://youtu.be/yNk4dIlAOVs

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Tanga limefanikiwa kuwauwa watu 2 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi huku likiwasaka wengine 2 waliokimbia; https://youtu.be/Pk-V_dM99Tc

SIMU.TV: Naibu waziri wa kilimo, uvuvi na ufugaji William Ole Nasha, ametoa agizo kwa mrajisi wa vyama vya ushirika kwenda kuchunguza mkoani Mtwara ili kubaini kama kuna wizi wa fedha umefanyika; https://youtu.be/F_A1626ogzc

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Prof Makame Mbarawa, ameagiza kuvunjwa kwa nyumba na majengo yote yaliyojengwa katika hifadhi ya reli Tazara;https://youtu.be/zEmdNrfznls

SIMU.TV: Benki ya NMB imetenga zaidi ya Bilioni 500 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wakulima na wafanyabiashara ili kukuza sekta ya kilimo; https://youtu.be/tuumQyZGK3M

SIMU.TV: Serikali imeanza kutoa mafunzo ya sheria ya VAT ili kuleta uwiano sawa kwa wananchi na kuepusha sintofahamu kama ilivyotokea hapo awali;https://youtu.be/0ZknjHLnXaM

SIMU.TV: Kampuni ya Yono Auction Mart imefanikiwa  kushinda tuzo ya kimataifa kutokana na utendaji kazi wake mzuri uliotukuka; https://youtu.be/6wOZ6XRbr2g

SIMU.TV: Timu ya jeshi la Tanzania hii leo imekabidhiwa bendera ya taifa tayari kwenda kuipeperusha kwenye mashindano yanayohusisha majeshi nchini Rwanda ;https://youtu.be/pQs7itbLuwI

SIMU.TV: Shirikisho la soka nchini TFF kwa kushirikiana na FIFA, limeandaa kozi maalumu kwa ajili ya makocha wa magolikipa ili kuwaongezea uwezo walinda milango nchini;https://youtu.be/AUaEi-GK6-o

SIMU.TV: Katika muendelezo wa kuzichambua timu mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara, leo hii tutakuwa na timu ya Stand United kutoka mkoani Shinyanga;https://youtu.be/Nw4isbf4g9g

SIMU.TV: Timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles, imechelewa kuwasili kwa wakati kwenye michuano ya Olimpiki nchini Brazil kwa kile kinachodaiwa ukosefu wa nauli; https://youtu.be/Zpy6WZvhmp4

KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

INTRODUCING NEW VIDEO BY SIMAO FT. MONI "MADE IT" Directed by: Nicklass

TV 1 YAWAKUMBUKA WAPENZI WA SOKA NCHINI, SASA KURUSHA MECHI ZA LIGI KUU YA UINGEREZA

$
0
0
Dkt. Licky Abdallah ambaye ni Mchambuzi nguli wa masuala ya Soka nchinia kizungumza na waandishi wa habari kuhusiana  na  uzinduzi wa kuonyesha Mechi za ligi kuu za Uingereza zitakazokuwa zinaonyeshwa na kituo cha TV 1 kuanzia msimu huu.
Joseph Sayi Mkurugenzi mkuu wa TV 1 akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kuonesha mechi za ligi kuu ya Uingereza  zitakazooneshwa kituo cha televisheni cha TV 1 inayopatikana kwenye king'amuzi cha Startimes
 Gillian Rugumamu Meneja masoko wa TV 1 akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kituo cha televisheni cha TV 1 kilivyojipanga kuonesha mechi za ligi kuu ya Uingereza itakayoaanza wiki ijayo.
Meneja wa Uzalishaji wa Vipindi wa TV1, Mukhsin Mambo  akionesha waandishi wa habari sehemu ya itakayotumika kurushia matangazo ya mechi za ligi ya Uingereza zitakazorushwa kupitia kituo cha Televisheni cha TV 1

Huduma ya usafiri wa Treni ya Pugu kutolewa bure mpaka Ijumaa Agosti 05, 2016

$
0
0
Taarifa kutoka makao makuu ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), inaeleza kuwa huduma ya treni ya Pugu itaendelea kuwa ya majaribio hadi Ijumaa Agosti 5, 2016. Hivyo ndiyo kusema abiria wataendelea kujinafasi kwa huduma hiyo ya bure hadi siku hiyo. 
Kuanza rasmi kwa huduma hiyo kutategemea idhini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra). Leo Jumatano Agosti 3, 2016 Wataalamu wa Sumatra walisafiri na treni hiyo na kutoa maagizo maalum ya kurekebisha mabehewa ya treni hiyo, na TRL imeshajiandaa kufanya marekebisho hayo kwa wakati muafaka. Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ikiwa tayari kwa safari yake ya Jiji kuanzia Stesheni  kwenda Pugu huduma ambayo imeanza kutolewa huku ikiwapa abiria nafasi ya kusafiri bure hadi Ijumaa Agosti 5, 2016 .

WAZIRI MKUU ATOA SIKU MOJA KWA MANISPAA YA MOROGORO KUTANGAZA MAENEO KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA WADOGO

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na kuyatangaza kesho.
“Mbali na kutenga maeneo pia nawaagiza muwasaidie wafanyabiashara hawa kuunda vikundi kulingana na aina ya biashara wanazozifanya ili kuwawezesha kupata mikopo kwa urahisi kutoka katika taasisi za fedha” alisema.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo leo (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Msamvu unaojengwa kwa ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Awamu ya kwanza ya mradi huo inatarajiwa kufunguliwa Agosti 12 mwaka huu utakuwa ni kituo cha mabasi cha kwanza cha kisasa Tanzania ambapo Waziri Mkuu amezitaka halmashauri zote zilizoko makao makuu ya mikoa nchini kuiga mfano huo.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kulipongeza Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro na LAPF kwa kubuni mradi huo wa kisasa utawezesha abiria kupata taarifa ya basi lilipo na muda litakapowasili kituoni hapo hivyo kupunguza udanganyifu kutoka kwa mawakala wasiokuwa waaminifu.
Kwa upande wake Meneja wa mradi huo Stanley Mhapa alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 40 ambapo Manispaa inamiliki asilimia 40 ya hisa na mfuko wa LAPF unamiliki asilimia 60.
“Mafanikio ya mradi huu ni pamoja na kuiwezesha Manispaa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka sh 350,000 kwa siku hadi kufikia sh. milioni 1.7 kwa siku,” alisema.
Mhapa alisema mradi huo utakapokamilika utatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kibenki, vibanda vya biashara, sehemu za chakula, ofisi na sehemu ya mapumziko ya abiria na vibanda vya kukatia tiketi.

Mwanamitindo mstaafu wa kimataifa Tausi Likokola aja kivingine

$
0
0

 Mwanamitindo mstaafu wa kimataifa Tausi Likokola, ambaye yupo hapa nchini, ana miradi mbalimbali  inayoendelea, kwa sasa anazindua kipindi chake cha Television, chenye malengo ya kuwainua wasichana na wanamitindo kwa jumla kwa kutumia ulimbwende, fasheni na uanamitindo kama mwamvuli.  

Tausi ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kukuza vipawa vya wasichana ulimwenguni kote kwa kutumia uzoefu wake katika fasheni, mitindo uandishi wa vitabu na ujasiriamali, anasema ni wakati sasa wa kufanya hayo hapa nyumbani kwao mwenyewe.
Kipindi kinaitwa ‘TAUSI LIKOKOLA’S AFRICAN PRINCESS MODEL SEARCH’ ambacho kimetokana na wazo lililobebwa katika vitabu vyake viwili, T’he African Princess’ na kingine cha ‘Beautiful You’. 
Kipindi hicho cha kwanza na cha aina yake, kitaanza kurushwa katika kituo cha televisheni cha TV1 kuanzia IJumaa ya Agosti 5, 2016 saa 10:00 jioni na kurejewa tena Jumapili asubuhi.
Tausi anaamini kwamba wasichana wanahitaji kufundishwa na kutiwa moyo kuelekea katika ndoto zao, na kipindi hiki kitaonesha vipengele tofauti tofauti katika maisha kuanzia maadili, ulimbwende, nidhamu na mambo mengine, hiki ni kipindi kwa familia nzima.
Lengo kuu la Tausi Likokola’s African Princess Model Search ni kukuza na kuongeza uwezo wa msichana mmoja mmoja katika stadi za uongozi na uwezo katika kujitambua, kujikubali, kujiamini na kuwa na mawazo chanya na kujifunza stadi za mawasiliano mazuri ambayo hatimaye yatafanya washindani kufanikiwa sana katika maisha yao ya baadaye katika ulimwengu wa ushindani wa fasheni.
Tausi aliyezindua bidhaa kadhaa za urembo na maisha kupitia kampuni yake ilipo Tanzania,ijulikanayo kama ‘Tausi Dreams Ltd. Tausi anayeishi Marekani bado, yupo hapa nchini kwa sasa kuendeleza miradi mbalimbali ikiwepo bidhaa zake zilizoanshishwa hivi karibuni ikiwemo pafyumu yake inayoitwa Tausi Dreams ikiwemo nywele za binadamu zinazoitwa Tausi Beautiful You Hair.

Tausi aliyekulia katika ulimwengu wa fasheni kimataifa katika miaka ya 90, amefanya kazi na makampuni makubwa ya mitindo kama Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Tommy Hillfger, Escada na wengine wengi, na sura na kazi zake kupamba kurasa za mbele na za ndani katika magazeti na majarida kadhaa ya mitindo na maisha ya kimataifa na hapa nyumbani, amekuwa akiwatia moyo wanamitindo wengi hapa nchini na wengine duniani kote. 

Tausi amefanikiwa sana kulitumia jina na kipawa chake kuwasaidia watu wake wa Tanzania katika elimu, kutambua UKIMWI, mahitaji ya jamii, na ameweza kuchangia katika kukua kwa utalii katika nchi yake ya kuzaliwa (Tanzania), kibiashara na kukuza maliasili. Tausi ana mpango wa kusimamia kazi kadhaa za kujitolea kupitia kampuni yake ya ‘Tausi and Friends for Life’
Tausi alipumzika kujitokeza katika uanamitindo ili kupata muda mzuri wa kukaa na familia. Wakati wa kazi za mitindo Tausi ametembelea nchini nyingi za Afrika, Ulaya, Asia, Australia na kwa sasa akiwa anaishi Marekani. Tausi ameandika vitabu vinne hadi sasa akitumia uzoefu wake uliopata toka mataifa mbalimbali akifanya kazi na wasichana toka ulimwenguni kote kuwasaidia kwa hali na mali. Vitabu alivyotoa hadi sasa ni; The Art of the Beauty and Health’,  The African Princess,’ ‘The Touch of an Angel’ na ‘Beautiful You’.



Kipindi Maalum cha Rais Magufuli alipohutubia Mkutano wa hadhara Kahama

NYANDA WA KUTUMAINIWA KATIKA CHAMA LA NANIHII

$
0
0
Nyanda nambari wani wa Chama la Nanihii,Ankal akiruka kwa umaridadi kabisha kunyaka mpira ulioelekezwa langoni mwa timu yake ya Timu ya Upinzani, katika mtanange wa Kombe la nanihii uliopigwa jana katika Dimba la Kimataifa la nanihii, Mjini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu TIC akutana na Waziri wa zamani wa Uingereza wa maswala ya Afrika na maendeleo ya Kimataifa

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari akiwa pamoja na Waziri wa zamani wa Uingereza wa maswala ya Afrika na maendeleo ya Kimataifa, Baroness Lynda Chalker walipokutana ili kuzungumzia mazingira ya uwekezaji nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa TIC alimuhakikishia Mgeni wake huyo kuwa TIC itajitahidi kuhakikisha uwekezaji nchini unakuwa ni ule wenye manufaa na mazingira yake kuwa bora.

VIONGOZI WA DINI WAOMBEA JENGO LA TATU LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akiomba dua  kuombea uwanja wa ndege wa Terminal III unaoendelea kujengwa leo jijini Dar es Salaam uliopo katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA)jijini Dar es Salaam. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Dini.
Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam na kiongozi wa Kanisa la Anglikana, Mchungaji John Solom(aliyeshika kipaza Sauti) akisali kuombea uwanja wa ndege wa Terminal III unaoendelea kujengwa leo jijini Dar es Salaam uliopo katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam. 
Katibu wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA), wakili Ramadhani Maleta (mwenye tai nyekundu) akitoa neno la Shukrani mara baada ya kumaliza ziara ya viongozi mbalimbali wa dini waliotembelea katika uwanja wa ndege unaoendelea kugengwa wa Terminal III jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mradi wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA), Mhandisi, Mohamed Millanga akitoa maelekezo kwa viongozi mbalimbali wa dini jijini Dar es Salaam leo walipotembelea na kuombea kiwanja cha ndege cha Terminal III kilichopo katika uwanja wa ndege wa Malimu Julius Nyerere (JNIA).
Picha na Yasir Adam, Globu ya Jamii.

UTT-PID NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI ZASHIRIKI PAMOJA MAONESHO YA KILIMO YA NANENANE, LINDI

$
0
0
  Maofisa wa Taasisi ya miradi ya UTT wakiwa pamoja na watumishi wa Halmshauri ya Manispaa ya Lindi katika Maonesho hayo ya Nanenane.  
Moja ya Miradi mikubwa iliyofanywa na ubia huu ni upimaji wa viwanja katika eneo la Mabano na Mmongo, uuzaji na uwekaji wa Miundombinu ya barabara. Kwa muendelezo wa ubia huo na mafanikio ya awamu ya kwanza ubia huo kati ya Taasisi hizo mbili za Serikali wataingia utekelezaji wa awamu ya pili ya upimaji na uuzaji wa viwanja katika maeneo tofauti ndani ya Manispaa ya Lindi. Kupitia ubia huu na mapato Manispaa ya Lindi iliyopata iliwezesha wakazi wa halmashauri kunufaika na vitu vingi ikiwemo: - Ujenzi wa maabara kwa shule za Sekondari. - Ujenzi wa nyumba za walimu. - Ujenzi wa nyumba za waauguzi. 

 - Ununuzi wa magari pikipiki na boti kama vyombo vya usafiri. - Ununuzi wa trekta ya manispaa. - Ukarabati na ununuzi wa fenicha ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri. - Ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule zote za sekondari za halmashauri.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 03/08/2016

Vodacom yakabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi kuu(VPL).

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella(mwenye miwani)na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa klabu mbalimbali wakati wa hafla ya ukabidhi vifaa kwa timu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Jijini Dar es Salaam leo.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura akitoa neno la shukurani kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Hafla hiyo iliandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 Vijana waliovyalia jezi za nyumbani na ugenini za timu ya Simba kwa msimu wa ligi ya Vodacom Tanzania bara 2016/17 wakizinesha jezi hizo wakati wa hafla iliyoandaliwa na wadhamini wakuu ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali kwa timu zitakazoshiriki ligi hiyo.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura(kulia)

TIMU zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vina thamani ya shilingi milioni 514,208,400 /=.

Akikabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha  Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Nandi Mwiyombella ,alisema kuwa  kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi  vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika.

“Tunajisikia furaha  kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza  matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi  wa 2016/2017”Alisema Mwiyombella.

Mwiyombella alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake  wanapata burudani ya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote,ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.

Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha  zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza  maslahi kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu  kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanzia ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa ”Alisema Mwiyombella.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,Boniface Wambura aliishukuru hiyo,  na kuzitaka klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechi za ligi.
“Ninatoa mwito kwa klabu zote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”alisema.

Aliongeza kuwa  TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini  kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.

Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote  kukamilika mapema pia timu zitazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images