Mashindano ya kusaka vipaji vya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars Jumamosi, Julai 30 yameanza rasmi kutimua vumbia katika ngazi ya mkoa jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Jamali Malizi amewataka vijana kujituma ili kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji nyota.
Malinzi pia ameziomba klabu zinazoshiriki Ligi Kuu pamoja na Ligi Daraja ya Kwanza kutumia fursa ya Airtel Rising Stars kwa ajili ya manufaa yao. ‘ Michuano hii inatoa nafasi nzuri kwa klabu zetu kuja na kutambua vipaji vinavyoibukia na kuwasajili kwenye timu zao’, alisema Malinzi.
Aliongeza kuwa, michuano hii ni sehemu bora ya kutambua vipaji, kwani ni fursa kwa wavulana na wasichana wanaoshiriki michuano kujitambua kwao kimaisha.
Akihutubia wachezaji wa Mikoa ya Kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke, Malinzi alisema kuwa, wachezaji kufanya vizuri kwenye michuano hii ni kujitengenezea nafasi ya ajira . Aliwakumbusha jinsi soka limeweza kubadili maisha ya mchezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, huku akisisitiza kwamba soka inatoa ajira kwa mamilioni ya wachezaji ulimwenguni kote.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo, Mkurungenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso aliwashukuru wadau wa soka kwa kusaidia na kushiriki kwao kwenye michuano ya Airtel Rising Stars kwa miaka mitano na kuwaomba makocha kuwachangua wachezaji wenye vipaji kwa ajili ya kuandaa timu ya kushiriki michuano ya taifa.
‘Tunajivunia uhusiano wetu mzuri na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Afrika kwa ujumla na tunayo furaha kuwa Klabu na Timu za Taifa zinafaidika na matunda ya Airtel Rising Stars’, alisema Colaso na kuongeza kuwa Airtel itaendelea kuthamini na kukuza soka la Tanzania.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi waliwapongeza Airtel kwa program hii huku akisema imesaidia kutafuta na kukuza vipaji vya soka nchini.
Michuano ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa ikishirikisha Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Lindi, Zanzibar na Arusha itafikia tamati wakati wa fainali za taifa zitakapofanyika kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam tarehe 6 mpaka 11 Septemba mwaka huu.
Mkurungenzi Mtendaji Airtel Sunil Colaso na Rais wa TFF Jamal Malinzi wakikagua timu wakati wa ufunguzi wa michuao ya Airtel Rising Stars 2016 Mkoa wa Dar es Salaam kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam Jumamosi 30 Julai 2016.
Mkurungenzi Mtendaji Airtel Sunil Colaso akikangua timu wakati wa ufunguzi wa michuao ya Airtel Rising Stars 2016 Mkoa wa Dar es Salaam kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam Jumamosi 30 Julai 2016.