Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

PINK RIBBON KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUFANYA UCHUNGUZI NA TIBA YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

0
0


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Pink Red Ribbon toka nchini Marekani Bi.Celina Schocken,shirika hilo limeahidi kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mazima ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ili kuwezesha huduma kuwa endelevu,kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS Dkt.Warren Naamara
Waziri Ummy Mwalimu akizungumza kwenye kikao hicho,kushoto ni mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha afya na mtoto-wizara ya afya dkt.Georgina Msemo .
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Pink Ribon Red Itinerary Bi. Celina Schocken.

RAIS DKT MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU NNE MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Mdini Mhe. Dkt Medard Kalemani baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na madiwani na viongozi wa Katoro na Buseresere baada ya kuhutubia wananchi wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsabahi mtoto Shabani Kalemani (miezi 8) na mama yake Asha Simon baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa kwa furaha kijijini Bwanga wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia wananchi kijijini Bwanga wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016

SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA GGM

0
0

Na Veronica Simba - GEITA

Serikali imetoa siku 30 kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwalipa fidia wananchi wanaoishi ndani ya eneo la leseni ya Mgodi huo au kuwaruhusu rasmi waendelee kuishi humo na kufanya shughuli za kiuchumi.

Sambamba na agizo hilo, pia Serikali imeupa Mgodi huo siku 14 kuziba Tuta lililopasuka ambalo huzuia maji machafu kutoka Mgodini yasiende katika makazi ya wananchi.

Aidha, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na timu ya wataalam wa mitetemo kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), baada ya kukamilisha kazi waliyopewa kutafiti chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wananchi na majengo mbalimbali yaliyo jirani na Mgodi wa GGM, Serikali imeagiza timu hiyo kufanya tathmini maalum ya idadi ya waathirika.

Iliagizwa kazi hiyo ifanyike kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Maafa na Kitengo cha Mazingira pamoja na uongozi kuanzia ngazi za vijiji mpaka madiwani na wabunge husika kwa muda wa siku Saba tu kuanzia tarehe 29 mwezi huu na kuiwasilisha serikalini ili hatua stahiki zichukuliwe.

Maagizo hayo yalitolewa hivi karibuni mjini Geita na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani katika kikao chake kilichomshirikisha Mkuu wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani.

Dkt Kalemani alisema kuwa maagizo hayo ni kufuatia maelekezo aliyoyatoa mapema mwezi Februari mwaka huu alipotembelea mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi wa vitongoji vya Katoma na Nyamalembo. Alisema maagizo hayo yasipotekelezwa ipasavyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa, chini ya sheria ya madini na sheria nyingine za nchi.


Afisa Madini wa Geita, Fabian Mshai (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), namna ambavyo Ofisi yake ilitekeleza maagizo aliyoyatoa kwao kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) likiwemo suala la mipasuko ya nyumba zao. Wengine pichani ni maafisa kutoka Wizarani.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi kuhusu ripoti ya wataalam wa mipasuko kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) juu ya chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba na majengo yaliyo karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani kuhusu uamuzi wa Serikali kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwa shughuli zinazoendeshwa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna .

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI NA BALOZI WA ITALIA WAKIKAGUA RAMANI YA BARABARA

0
0
BEN2 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
BEN3 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
BEN4 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama.
BEN1 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga kushoto  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia. 

JPM amaliza mgogoro wa makazi Magomeni Kota

0
0
Na Jonas Kamaleki, MAELEZO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemaliza mgogoro wa makazi wa Magomeni Kota uliodumu kwa kipindi kirefu.Hayo yamesbainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati akiongea na Kamati ya Mgogoro wa Makazi ya Magomeni Kota mbele ya waandishi wa habari.

“Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefuta hati na mikataba yote inayohusiana na ardhi ya yaliyokuwa makazi ya Magomeni Kota, Dar es Salaam”,alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi Rais ameondoa umiliki wa eneo hilo toka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kumilikisha Serikali Kuu ambayo ndiyo itakayosimamia ujenzi wa nyumba 644 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.

“Tutajenga nyumba 644 na kuwauzia kwa bei ya jengo na siyo ya ardhi ili kuwapeni unafuu katika kununua,”alisema Lukuvi huku akishangiliwa na baadhi ya wakazi wa Magomeni.Aidha, Lukuvi amesema kuwa anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kumaliza mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ameagiza timu ya wataalamu wa Wizara kupima na kuchora michoro kwa ajili ya ujenzi.

Lukuvi amesema katika eneo hilo zitajengwa nyumba za heshima ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu ili kukidhi mahitaji ya kifamilia kwani watu hawa wamekaa kwa miaka takribani 50 hadi wameshapata wajukuu. Ameongeza kuwa kila mmiliki wa nyumba hiyo atapewa hati yake hata kama nyumba hiyo itakuwa kwenye ghorofa.

Lukuvi amesema kuwa Rais ameagiza maeneo kama ya Magomeni Kota katika mikoa ishirini ya Tanzania Bara nayo yatakuwa katika mfumo huo wa Magomeni. Kwa mujibu wa Lukuvi wazee ambao wanakaa kwenye nyumba kama hizo sehemu nyingine wasiondolewe kwani hao walikuwa watumishi wa umma hivyo Rais amesema wasibughudhiwe.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mgogoro wa Makazi Magomeni Kota, George Abel ameshukur Mhe Rais Magufuli na Wazir Lukuvi kwa kutatua mgogoro huo ambao anadai umewasumbua sana.

Ameahidi kutoa ushirikiana kwa Serikali pindi suala la ujenzi litakapokuwa linaendelea ili kuhakikishaujenzi unaenda haraka.Naye Wakili ambaye alikuwa akiendesha kesi hiyo kabla ya Mhe. Rais kuingilia kati, Mhe. Twaha Tasilima ameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.

“Rais Dkt Magufuli na Mhe. Waziri Lukuvi ni watu wa vitendo na si maneno na kweli wanawajali wanyonge, nawashukuru sana,”alisema Tasilima.Uamuzi wa kurudisha eneo hilo kwenye Serikali Kuu umetolewa na Rais Magufuli tarehe 10/7/ 2016.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa Magomeni Kota kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa makazi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto Ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula na Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Yamungu Kayandabila.
Wakazi wa Magomeni Kota wakimsikiliza Waziri Lukuvi akitoa taarifa ya kumalizika kwa mgogoro wa makazi ya eneo hilo leo jijini Dar es Salaam.

TIMU ZA OLIMPIKI ZAKABIDHIWA BENDERA, DSTV WAIPA SHAVU.

0
0
Baadhi ya wadau wa michezo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi akizungumza kabla ya kukabidhi bendera na kuwaaga  kwa wanaokwenda katika mashindano ya Olimpiki Rio De Jeneiro nchini Brazil.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura akiwakabidhi wachezaji bendera ya Taifa kwaajili ya kwenda kupeperusha huko Rio De Jeneiro nchini Brazil wanaokwenda kushiriki mashindano Olimpiki.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura  akiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa mashindano ya Olimpiki wanaoenda nchini Brazil

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura amewataka washiriki wanaoenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu Rio De Jeneiro nchini Brazil kujituma na kuhakikisha wanafanya vizuri ili kurudi na medali, hayo ameyasema wakati wa kukabidhi bendera kwa timu za kuogelea, judo na riadha leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Wambura amesema kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa macho na masikio ya watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa wamevaa medali zao. " Mnakwenda katika mashindano ya Olimpiki na macho yote ya watanzania yapo kwenu tunategemea mkiwa mnarudi basi tutakuja kuwapokea mkiwa na medali zeni kifuani na hilo linawezekana kama mtajituma mkiwa na ari ya ushindi".

Akiwa anawakabidhi bendera hiyo, Wambura amewaasa wanamichezo hao kutumia fursa nyingine ya kujifunza zaidi kwani kama wataenda kukutana na mataifa mengine mbalimbali. Naye moja ya wadhamini wa safaru hiyo kampuni ya Multichoice Africa, imewataka washiriki hao kujituma zaidi kwani watanzania wote watakuwa wanawaangalia kupitia chaneli zao zinazopatikana kwenye kisimbuzi cha DSTV.

Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande amesema mwaka huu mashindano yote yatakuwa yanakuja moja kwa moja kupitia channeli za Super Sport na itawapa fursa watanzania kuwashuhudia.wawakilishi wao kwenye mashindano hayo makubwa duniani. Mbali na hilo watakapokuwa huko waitangaze nchi yetu kwa vivutio vilivyopo nchini ili kuzidi kupata watalii mbalimbali kutoka.kote duniani hayo yamesemwa na Godfrey Tengeneza mkurugenzi wa utalii nchini.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi amesema kuwa kwa mwaka huu washiriki wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na wengine wakiwa nje ya nchi na hilo.limefanikisha kuweza kujifua vyema ili kuweza kurejesha ushindi nyumbani. Hilal ameweza kuweka kambi nchini Dubai, Magdalena alikuwa nchini Australia. Andrew aliweka kambi chuo cha polisi Moshi na wanariadha waliweka kambi mkoa wa Arusha.

Washiriki kwa upande wa riadha ni Alphonce Simbu, Said Makula l, Fabian Naasi na Sarah Makela. Timu ya kuogelea inawakilishwa na Hilal Hilal na Magdalena Moshi na Judo ni Andrew Mlungu. Huku timu ya kwanza ikitarajiwa kuondoka alfajiri ya leo wakiambatana na daktari wa timu Nasoro Matuzya.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA NANENANE MOROROGORO

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Banda la Maonyesho la wilaya ya Temeke kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidha mbalimbali zinazotokana na zao la mronge zikiwema, dawa, mafuta na sabuni wakati alipoembelea meza ya Bibi Salome Kaiza (kulia) kwenye banda la wilaya ya Tameke katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro, Agosti, 1, 2016. Kulia kwake ni Mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva wakati alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Monyesho ya Wakulima Nane mjini Morogoro Agosti 1, 2016, Kushoto ni mkewe Mary. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia kwake)wakitazama kilimo cha mbogamboga kwa mtindo wa kilimo kichuguu wakati walipotembelea banda la Chuo Kikuucha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye maonyeshoya Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016.

Mrema akutana na Madereva Bodaboda wa Kinondoni.

0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati)akisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenekiti wa Waendesha Bodaboda na Bajaj wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede na kushoto ni Katibu wake Bw. George Mbwale.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema ( Mwenye Kofia Katikati) akisisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.
Baadhi ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani) alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa.Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo

Ilala yawataka wafanyabiashara kuzingatia muda wa usafi

0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaaam imewataka wafanyabiashara kuzingatia muda uliopangwa na Serikali kwa ajili ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi unaofanywa kila ifikapo siku ya jumamosi.

Muda uliowekwa kwa ajili ya zoezi hilo ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:30 asubuhi, ambapo wafanyabiashara wote watapaswa kufungua maduka na masoko yao mara baada ya zoezi hilo kukamilika.

Hayo yamesemwa leo na Afisa wa Manispaa hiyo, David Langa wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii kuhusu mwitikio wa wananchi juu ya zoezi la usafi wa mazingira unaofanyika kila jumamosi na kila mwisho wa mwezi.

“Nawaomba Wafanyabiashara wenye tabia ya kujichelewesha ili wafike baada ya muda wa usafi pamoja na wale wanaofungua biashara kabla ya muda uliopangwa na Serikali kuacha mara moja kwani lengo la kubadili muda wa kufungua biashara ni kwa ajili ya kufanya usafi” alisema Langa.

Akifafanua zaidi Langa aliwatahadharisha wananchi wanaopenda kutupa taka hovyo kuacha mara moja kwani sheria ya afya na sheria ya mazingira inapinga suala hilo na kwa mujibu wa sheria hizo adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miaka 6.

Kwa mujibu wa Langa alisema kuwa, suala la usafi sio suala la Serikali pekee bali wananchi wanatakiwa walifanye kuwa ni sehemu ya kulinda afya zao, hivyo kila mmoja anapaswa kuzingatia usafi kwenye maeneo yanayomzunguka. Aidha Langa alisema kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzie kwani zoezi la kulipishwa faini bado ni endelevu, mtu atakaemkamata mwenzie anatupa taka atapewa shilingi elfu 20 na aliyekamatwa atatoa faini ya shilingi elfu 70

Naibu Waziri Anastazia Wambura akagua eneo la ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Leo Jijini Dar es Salaam.

0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura eneo eneo la ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura na Katibu Mkuu Wizara ya hiyo Prof Elisante Ole Gabriel kuhusu ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016 Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

MBUNGE ULEGA AKUTANA NA WANANCHI WAKE VIJIWE VYA KAHAWA

0
0

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega wa tatu kutoka kushoto akiwa sambamba na Wazee wa Mkuranga katika eneo la stendi kwenye kijiwe cha kahawa akipata kikombe cha kahawa pamoja ambapo pia walibadilishana mawazo juu ya maendeleo ya wilaya yao leo mkoani Mpwani. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

Mrisho Mpoto ndani ya Kipindi cha The Avenue

WAZIRI MKUU AITAKA WIZARA KUWEKA MIKAKATI YA KUENDELEZA UVUVI KATIKA KINA KIREFU CHA BAHARI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuweka mikakati endelevu ya kuwawezesha wananchi kuvua katika maji ya kina kirefu cha bahari kwa kutumia meli kubwa na za kisasa ili Taifa liweze kunufaika na rasilimali hiyo ambayo imekuwa ikichukuliwa na wavuvi wenye vyombo vya kisasa kutoka nje ya nchi.

Aidha, amezitaka halmashauri zote nchini ziweke mikakati na mipango ya kuifanya mito na maziwa mbalimbali nchini kuwa na uvuvi endelevu kwa kufuatilia kwa karibu shughuli za wavuvi na kuwaadhibu wote watakaovua kinyume na sheria.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Agosti 01, 2016) wakati akifungua maadhimisho ya 23 ya sherehe za maonesho ya wakulima Kanda ya Mashariki katika Uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere yanayofanyika katika mkoa wa Morogoro ambapo amesema bado nchi haijaweza kutumia rasilimali hiyo kikamilifu.

Amesema halmashauri zinatakiwa zihamasishe vijana kuunda vikundi vya kuanzisha miradi ya kufuga samaki katika maeneo yao na wewezeshwe kupata teknolojia ya ufugaji huo.

Akizungumzia vikundi vya wajasiariamali wanaovua katika maeneo ya bahari na maziwa alishauri waelimishwe kuhusu namna ya kupata mikopo ya kununulia zana bora za kisasa za uvuvi ili shughuli zao ziwe na tija.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema wakulima wanatakiwa  kuzingatia matumizi ya kanuni bora za kilimo ikiwemo matumizi sahihi ya zana za kisasa, pembejeo na viuatilifu vilivyopendekezwa na wataalam ili kufanikisha mapinduzi ya kilimo kuelekea kilimo cha biashara.

Akizungumzia kuhusu suala la usindikaji alisema wakati anatembelea mabanda mbalimbali alipata fursa ya kuona teknolojia zinazoweza kutumiwa na wakulima, wafugaji na wavuvi katika kuongeza uzalishaji bora wenye tija.

Amesema amefurahi kuona wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wa mazao, pembejeo na zana za kilimo wana ari kubwa ya kushiriki katika kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na kasi ya Serikali ya kuifanya nchi kujitosheleza kwa chakula na kuendeleza uchumi wa viwanda.

“Naamini kuwa pamoja na lengo la kujitosheleza kwa chakula, wakulima, wafugaji na wavuvi wataongeza ari ya uzalishaji kwa kushirikiana na sekta za umma na binafsi katika kuvipatia viwanda vyetu malighafi na kuongeza thamani ya mazao,” alisema.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu aliziagiza halmashauri zote kuhamasisha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vidogo vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kushirikisha taasisi za umma na binafsi, mashirika na vikundi vya ujasiriamali katika maeneo yao.

Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi watahamishiwa katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa na wenye mifugo michache watatengewa maeneo katika vijiji.

Awali Waziri Mkuu alitembelea baadhi ya mabanda na maeneo ya vipando vya mazao mbali mbali yaliyoko katika viwanja hivyo ambapo alisema ameridhishwa na juhudi zilizofanyika katika maandalizi ya maonesho ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa uwanja huo.

“Napenda kutoa pongezi za dhati kwa kujenga miundombinu na nyumba za kudumu za kufanyia maonesho. Aidha, natoa shukrani za pekee kwa Halmashauri zetu, Mashirika yetu ya Umma na binafsi; na watu binafsi ambao wamejenga na wanaendelea kujenga majengo mazuri na ya kudumu,” alisema.

Pia alizindua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na kusema kuwa uboreshaji wa viwanja hivyo unaonesha jinsi wadau wote katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na ushirika wanavyotambua umuhimu wa maonesho hayo kama njia ya kuongeza maarifa na kumuenzi mkulima, mfugaji na mvuvi kwa kutambua mchango wao katika uchumi wa Taifa.

Kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa mwaka huu ni kilimo, mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo: vijana shiriki kikamilifu   (“HAPA KAZI TU”)         
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, AGOSTI 01, 2016. 

WADAU WA SEKTA YA AFYA KANDA YA KASKAZINI WADAU WAKUBALIANA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA.

0
0
 Wadau wakiwa katika picha ya pamoja. 
  Meneja Masoko wa AAR Insurance Tanzania, Tabia Masoud akitambulisha wafanyakazi wenzake kwa wadau wa sekta ya afya wa mkoa kanda ya Kaskazini wakati wa mkutano wa kampuni hiyo na wadau hao kujadiliana namna ya kuboresha huduma za afya jana jijini Arusha.
  Meneja Maendeleo ya Biashara wa AAR Insurance Tanzania, Hamida Nassor akijadiliana jambo na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano kati ya kampuni hiyo na wadau wa sekta ya afya kanda ya kaskazini kujadiliana namna ya kuboresha huduma za afya jana jijini Arusha

Ikiwa ni sehemu ya jitihada zake kuimarisha utoaji huduma za afya nchini, kampuni ya bima ya AAR Insurance Tanzania pamoja na wadau wake waliopo Kanda ya Kaskazini wamekubaliana kuhakikisha huduma zitolewazo kwa wateja wake zinakuwa za ubora wa hali ya juu na za kuridhisha. Maazimio hayo yamefikiwa baada ya wadau hao kukutana jijini Arusha mwishoni mwa wiki ambapo walijadiliana mikakati na changamoto za kiutendaji zinazokabili utoaji huduma za afya.

Akiongea katika mkusanyiko huo uliojumuisha wadau kutoka hospitali mbalimbali, vituo vya afya, zahanati, kliniki na maduka ya dawa kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, Mkuu wa Operesheni wa AAR Insurance Tanzania, Wilfred Rono alisema ubora wa huduma ya afya unaweza kuboreshwa na uongozi bora, kuwa na mipango mizuri, elimu na mafunzo, upatikanaji wa rasilimali, menejimenti thabiti ya rasilimali, wafanyakazi, na ushirikiano miongoni mwa wadau na akaongeza kuwa ni muhimu kwa wadau hao kukutana na kuweka mikakati.

Wilfred Rono pia aliongeza kwamba dhumuni la tukio hilo lilikuwa ni kuimarisha uhusiano kati ya kampuni hiyo kubwa zaidi ya bima ya afya na wadau wake huku na kuongeza kuwa mkutano huo umetumika kuelimisha wadau juu ya bidhaa na huduma za bima ya afya.

AAR Insurance Tanzania ni sehemu ya AAR Insurance Holdings ambayo ndio kampuni kubwa zaidi ya bima za afya kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

YALE YALEEE.....


MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AKABIDHI MADAWATI 537 NA VITABU KWA UONGOZI WA HALMASHAURI

0
0
Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Juma wa kulia akimkabidhi madawati 537 Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibaha vijijini Mansouri Kisebengo katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya sekondari kilanga langa.

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya uhaba wa madawati na viti na kusababisha baadhi yao kuwa tabia ya utoro kwa sasa wameanza kunufaika na agizo la Rais Dr.John Magufuli la kutaka wanafunzi wote nchini kuhakikisha wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati.

Agizo hilo la Rais limetekelezwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa kupitia kupitia fedha ambazo zimepatikana kutokana na kubana matumizi yasiyo ya lazima katika ofisi yake kwa lengo la kuweza kusaidia katika kuboresha sekta ya elimu.

Akikabidhi jumla ya madawati 537 Mbunge wa Jimbo hilo kwa uongozi wa halmashauri ya kibaha vijijini katika halfa fupi zilizofanyika katika shule ya sekondari kilangalanga iliyopo Mlandizi, amesema kwamba ametoa madawati hao pamoja na vitabu kwa lengo la kuweza kupunguza kero na kuondokana na adha ambayo walikuwa wanaipata wanafunzi wa jimbo lake katika siku za nyuma.
Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Jumaa akitoa taarifa fupi kabla ya kukabidhi madawati 537 pamoja na vitabu kwa uongozi wa halmashauri hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa kwa nchi nzima la kila mwanafunzi anatakiwa asome akiwa kwenye dawati na sio kukaa chini.

Kwa upande wake Afisa elimu katika halmashauri ya kibaha vijijini Coskansia Mafuru amebainisha kwamba awali kabla ya agizo la Rais walikuwa wana upungufu wa madawati 1923 kwa shule za msingi, hivyo msaada huo utaweza kumaliza changamoto zilizokuwa zikiwakabili na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MISS EASTERN ZONE 2016 KUPATIKANA AGOSTI 06, NASHERA HOTEL MOROGORO

MAREHEMU JOSEHPH SENGA APUMZISHWA KWA AMANI KIJIJINI KWAO SHUSHU, KWIMBA JIJINI MWANZA

0
0
Waombolezaji wakilishusha jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Marehemu Senga alifariki wiki iliyopita nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya moyo. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi AMIN.
Mjane wa Marehemu Joseph Senga, Bi. Winfrida Senga akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mumewe, wakati wa mazishi yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti hili, marehemu Joseph Senga wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza. 
Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa akiweka shada la Maua.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ambaye pia ni Mmiliki wa Kampuni ya FreeMedia wachapishaji wa Gazeti la Tanzania Daima alikokuwa akifanya Kazi Marehemu Joseph Senga, akitoa salamu za Rambirambi, wakati wa Mazishi yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza.
Ibada ya Mazishi ikiendelea.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiweka shada la maua kaburini.

WASHIRIKI WA MICHUANO YA OLYMPIC WAAGWA RASMI

INTRODUCING Rogers Lucas feat Josee Mtambo - siri ya maumivu

Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images