Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA YATUPILIA MBALI SHAURI LA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA PANGANI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso katika akipongezwa na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kutangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kuwa mshindi halali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau.
Mbunge Aweso Jumaa akiwa amebebwa juu juu na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kesi iliyofunguliwa dhidi ya mpinzania wake wa CUF Amina Mwidau ya kupinga matokeo ya uchaguzi kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso (wa tatu toka kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani "Proffesa Maji Marefu " wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Tanga wakisuburia kuanzwa kwa kesi hiyo hata hivyo hukumu hiyo ilimpa ushindi halali Mbunge Aweso katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga jana ili tupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Pangani lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia tiketi ya CUF Amina Mwindau dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Hamidu Aweso CCM na kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo. 

Akizungumza wakati akitoa huduma ya Shauri hilo,Jaji Patricia Fikirini alisema mlalamikaji Amina Mwindau CUF ameonekana kushindwa katika shauri hilo dhidi ya mlalamikiwa Jumaa Aweso katika upingaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika oct 25 mwaka jana. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO

MWANAFUNZI WA KITANZANIA ASHINDA SHINDANO LA INSHA LA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Mogens Lykketoft akiwazungumza washindi 60 wa Insha kuhusu Lugha Nyingi, Dunia Moja, miongoni mwa washindi hao ni mwanafunzi wa Kitanzania Amani Alfred Naburi anayesoma Chuo Kikuu cha African Leadership kilichopo nchini Mauritius wengine katika picha ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma ya Umoja wa Mataifa, Bi. Cristina Gallach.
Amani Alfred Naburi akisoma sehemu ya Insha yake aliyoiandika kwa lugha ya kiingereza ambayo ilizungumzia lengo namba kumi na moja la maendeleo endelevu ambalo linahusu Miji jumuishi, salama na endelevu. Hafla hii ilifanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya wanafunzi wa Insha kuhusu Lugha Nyingi, Dunia Moja wakiwa katika ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa..Hafla hii ilikuwa ni sehemu ya Kongamano la Kimataifa la Vijana.
Naburi anaonekana katika mstari wa tatu akishangilia jambo na wanafunzi wenzie kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao walikusanyika siku ya Ijumaa baada ya kushinda uandishi wa Insha kwa kutumia lugha sita rasmi zinazotumika katika Mikutano ya Umoja wa Mataifa.

Na Mwandishi Maalum, New York

Mwanafunzi wa Kitanzania, Amani Alfred Naburi, ni mmoja wa kati ya wanafunzi 60 kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali duniani ambao wameshinda shindano la Insha ijulikanayo kama “Lugha nyingi, Dunia Moja” ( Many languages, One World) lililoandaliwa kwa ushirikiano baina ya United Nations Academic Impact ( UNAI) na ELS Educational Services, Inc.

Jumla ya wanafunzi 3,600 kutoka mataifa 165 walijitokeza kuwania shindano hilo ambalo hatimaye majaji waliwaibua wanafunzi 60 kutoka mataifa 36 kama washindi wa shindano hilo.

Amani Alfred Naburi ni mtanzania anayesoma Chuo Kikuu cha African Leadership University, huko Mauritius. Baadhi ya masharti ya kuingia shindano hilo lilitaka mshiriki lazima awe ni mwanafunzi aliye.

Washindi hao 60 walipata fursa ya kusoma sehemu ya Insha yao mbele ya washindi wenzao na washiriki wengine waliokuwa wakihudhuria kongamano la vijana, katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mbali ya washindi hao 60 kuzungumza, wazungumzaji wakuu wengine walikuwa ni ambayo Rais wa Baraza Kuu Bw. Mogens Lykketoft na Bi Cristina Galach Naibu Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayesimamia idara ya Mawasiliano ya Umma ya Umoja wa Mataifa na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kuhusi Vijana Bw. Ahmad Alhendawi aliwasilisha Salamu za Katibu Mkuu Ban Ki Moon.

Washindani wa Insha hiyo walitakiwa kuandisha Insha juu ya namna watakavyochangia katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( Agenda (2030). Ambapo kila moja wapo alitakiwa kuiandika insha hiyo yenye maneno yasiyozidi 2,000 kwa lugha nje ya lugha yake ya asili ya nchi anayotoka.

Tafsri yake ni kuwa walitakiwa kuandika kwa lugha sita ambazo ni rasmi na zinazotambuliwa na kutumika na Umoja wa Mataifa. Lugha hizo ni Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi.

Malengo waliyopewa washindani hao kuyandikia maoni hayo ni lengo namba kumi na mbili linalozungumzia Matumizi na Uzalishaji Bora ( Ensure Sustainable consumption and production ) lililowasilishwa kwa lugha ya Kifaransa, lengo namba kumi na sita ambalo linazungumzia kuhusu Amani, Haki na Taasisi Imara ( Promote just, peaceful and inclusive societies) lilowasilishwa kwa Kirusi, lengo namba kumi na tano linaluhusu Uhai juu ya Ardhi( Sustainably manage forests, combat desertification, halt and reverse land degradation, halt biodiversity loss ) lilowasilishwa kwa Kispanishi.

Malengo mengine ni lengo namba kumi na tatu kuhusu kuchukua hatua kwa mbadiliko ya Tabia nchi na athari zake ( Take urgent action to combat climate change and its impacts), lengo namba tisa kuhusu Viwanda, Ubunifu na Miundo Mbinu ( Build resilient infrastructure, promote sustainable industrialization and foster innovation), lengo namba kumi na moja kuhusu kuifanya miji kuwa jumuishi, salama, na endelevu ( make cities Inclusive, safe, resilient and sustainable). Lengo hilo ndilo ambalo Mwanafunzi Amani Naburi aliliandika insha kwa lugha ya kiingereza kiasi cha kukoga nyonyo za majaj.

Lengo kuu la uandishi wa insha kwa lugha sita rasmi zinazotumika katika umoja wa Mataifa ni pamona na mambo mengine, kuwawezesha wanafunzi kujifunza lugha na tamaduni za nchi nyingine , kupanua wigo na fursa ya kujifunza mambo na changamoto zinazoikabili dunia na kujaribu kutoa mawazo yao yatakayoweza kusaidia katika kuzikabili changamoto hizo. Lengo jingine ni kuwawezesha wanafunzi kutambua uwezo na vipaji vyao kama njia moja wapo ya kuwaandaa kuwa viongozi wa taifa la kesho.

KIWANDA MAARUFU CHA DANGOTE CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 15 KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

$
0
0
Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza simenti cha Dagonte Industry limited kilichopo mjini Mtwara kusini mwa Tanzania, kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Katika siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara Imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani hapo, kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na makondakta wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji wa eneo hilo.

Kwa Mujibu wa Naibu waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.

Kwa upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria ya mazingira.

Naibu waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na kukisifu kwa utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.

Ziara ya Mhe. Mpina pia ilihisisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ( katikati), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Khatib Kizinga (kushoto) wakipata maelezo toka kwa Bw. Sultani Pwaga wa kiwanda cha Gas cha Madiba Mjini Mtwara wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mpina kiwandani hapo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (kushoto) akipata maelezo kuhusu uchimbaji wa malighafi ya kutengeneza gypsum toka kwa bwana Hamisi Juma meneja kiwanda cha Dangote.
Eneo ya fukwe ya mnazibay Mjini mtwara inavyooneka kuathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababisha sunami mwaka 2015 february..Naibu Waziri Mpina Alitembelea eneo hilo kujionea athari za mabadiliko ya tabia nchi.(Picha na Evelyn Mkokoi)

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI LAFANYA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU SALAMA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye awaongoza viongozi waandamizi, maafisa, askari na watumishi wote wa Jeshi hilo katika zoezi la uchangiaji damu salama ili kutimiza dhima ya kuokoa maisha ya watu wanaopoteza maisha kwa ajali za moto, ajali za barabarani, vifo vya mama wajawazito wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua na magonjwa mbalimbali kama vile ukimwi, malaria, anaemia na kansa.

zoezi hili limefanyika katika viwanja vya kituo cha jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa ilala kwa kushirikiana na taasisi ya mpango wa damu salama ulio chini ya wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia watoto na wazee.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto mstari wa mbele) akiwaongoza Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo kuelekea katika viwanja vya kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala eneo lililotengwa kwa ajili ya zoezi la uchangiaji damu salama mara baada ya kuwasili kituoni hapo mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akihutubia Maafisa, Askari na watumishi wote wa Jeshi hilo wakati akifungua zoezi la uchangiaji damu salama ambalo lilishirikisha vituo vyote vya Zimamoto mikoani, ufunguzi huo ulifanyika katika viwanjwa vya Zimamoto na uokoaji mkoa wa Ilala mapema leo asubuhi.
Maafisa, Askari na watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka katika vituo vya Zimamoto Makao Makuu, Chuo, Ilala, Kinondoni, Temeke na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakimsikiliza Kamishna Jenerali (hayupo pichani )wakati akihutubia katika ufunguzi wa zoezi la uchangiaji Damu salama lililofanyika katika viwanja vya Zimamoto mkoa wa Ilala.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akichangia damu katika zoezi lililofanyika viwanja vya kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala zoezi lililoshirikisha vituo vyote vya Zimamoto mkoa wa Dar es Salaam mapema leo.
Askari na watumishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakichangia damu katika zoezi hilo mapema leo asubuhi. (PICHA ZOTE NA FC GODFREY PETER)

Wafanyakazi Muhimbili Waongeza Mapato Hadi Kufikia Sh 4.8 Bilioni

$
0
0

Na John Stephen, MNH .

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kuongeza mapato kutoka Sh 2.3 bilioni yaliyokuwa yakikusanywa Desemba mwaka jana hadi kufikia Sh 4.8 bilioni Mei mwaka huu. 

Hayo yamesemwa LEO na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru wakati hafla ya kutunuku vyeti kwa wafanyakazi bora wa hospitali hiyo.
Hospitali hiyo imefanikiwa kuongeza mapato kutokana na juhudi za wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwa ari kubwa ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa. 
Pia, wafanyakazi wamehamasika kutokana na mkurugenzi huyo kuwajali wafanyakazi na kusikiliza kero na kuzitatua kwa wakati kwa mfano hivi karibuni alilipa malimbikizo ya wafanyakazi. Profesa Museru amesema mapato hayo yameongezeka kutokana na juhudi za wafanyakazi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na hivyo kusababisha mapato hayo kufikia Sh 4.8 bilioni. 

“Mafanikio haya yametokana na juhudi za wafanyakazi. Mwaka jana niliwaomba wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii, na wao walikubali. Imani yangu ni kwamba posho kwa wafanyakazi wangu zitaanza kulipwa baada ya bodi kupitisha ombi la kuwaongezea. Nafikiri tukiwaeleza vizuri bodi watatuelewa na hivyo wafanyakazi watapata kile tulichowaahidi,” amesema Profesa Museru. 

Mkurugenzi huyo amesema kwamba hospitali imepata mafanikio makubwa yakiwamo kuongeza huduma za afya kwa mfano kuanzishwa kwa huduma ya kusafisha figo, kuongeza wodi kwa wagonjwa wanaohitaji uangali maalumu, huduma za matumbo na kuboreshwa kwa mazingira ya kutolea huduma. 

Amesema hospitali hiyo inajitahidi kuongeza mapato zaidi ili iweze kulipia huduma za umeme, huduma za simu, ankra za maji pamoja na kudi za majengo.
“Sisi hatufanyi biashara bali tunatoa huduma kwa wagonjwa, tunapaswa kuongeza mapato ili kulipia huduma kutoka kwa washirika wetu akiwamo Tanesco, kulipia maji na huduma za simu,” amesema Kaimu Mkurugenzi huyo. 

Akizungumzia changamoto, Profesa Museru amesema sehemu zinazotumika kutoa huduma zinatakiwa kukarabatiwa. Amesema miundombinu inapaswa kukarabatiwa kwa kuwa imekuwa ikichakaa kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa hospitali hapo.
“ Majengo ya hospitali hayajakarabatiwa karibu miaka 20, hivyo tunapaswa kukarabati sasa,” amesema. 

Pia Profesa Museru amewapongeza wafanyakazi bora ambao wametunukiwa vyeti baada ya kuibuka kuwa wafanyakazi bora. 

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika hafla ya kuwatunukia vyeti wafanyakazi bora 54. Hafla hiyo imefanyika katika hospitali hiyo. Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakimsikiliza Profesa Museru Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege akisoma risala kwa mgeni rasmi, Profesa Museru katika hafla ya kuwakabidhi vyeti wafanyakazi bora Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa TUGHE, Mziwanda Chimwege. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA   

Mtanzania mkazi wa UK Karrima Carter na wahisani wenzie kutoka Norwich watoa misaada Tanzania

$
0
0

Kundi la watoto yatima wanaotunzwa na Karrima na wahisani wenzake Waingereza kutoka Norwich hapa Uingereza
Baadhi ya wahisani kutoka Norwich wakiwa katika halfa ya utoaji misaada kwa kituo cha kulea yatima, Bagamoyo


Mwanadada wa Kitanzania, Karrima Carter, mwenye makazi yake Norwich, hapa Uingereza, wiki hii ameshirikiana na wahisani wenzake kutoka Uingereza kutoa misaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima huko Bagamoyo na uzinduzi wa vyoo vilivyokarabatiwa kwa uhisani wa dada huyo na wahisani wenzake kutoka Uingereza.
Tukio la kwanza lilifanyika Jumapili iliyopita na kuhudhuriwa na baadhi ya wasanii mbalimbali kama vile Gabo na Faiza Ally (ambao walialikwa rasmi kwa minajili ya kuwapa tabasamu watoto yatima), na tukio la pili lilifanyika Jumatatu iliyopita.
Picha na maelezo ya tukio la tatu la kukabidhi madawati zitawajia kesho. Awali, Karrima alisita kuhusu wazo la ku-blogu kuhusu matukio haya akisema kwamba asingependa 'publicity' lakini mie binafsi nilimshauri kuwa kuweka hadharani habari hizi kunaweza kusaidia kuwahamasisha Watanzania kuhusu utamaduni wa kutoa misaada kwa wenzetu wenye uhitaji, eneo ambalo ni maarufu hapa Uingereza lakini ni geni kwa nchi nyingi za Afrika.
Karrima amekuwa akijibidiisha katika sekta hiyo ya misaada kwa wenye uhitaji kwa kitambo sasa. na amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kwa wakazi wenzie wa Norwich.

Karrima n wahisani wenzake kutoka Norwich, uingereza, mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa hafla mbalimbali za utoaji misaada.
Hafla ya kuzindua vyoo katika Shule ya Msingi Ilala, ambavyo vilifanyiwa ukarabati kwa uhisani wa Karrima na wenzie kutoka Norwich, Uingereza

Karrima na wahisani wenzie kutoka Norwich wakiwa shuleni Ilala.

WAKURUGENZI MKOANI SIMIYU WAAGIZWA KUTENGA BAJETI ZA MAAFISA KILIMO

$
0
0

Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa kilimo wa Vijiji,Kata na Wilaya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ambacho kilihudhuriwa na Wakuu wa wilaya,Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi na Makatibu Tawala Wilaya kutoka katika wilaya zote tano za mkoa huo.

Mtaka amesema Maafisa Kilimo wanapaswa kuwezeshwa kwa kupewa vyombo vya usafiri kama pikipiki na magari pamoja na mafuta, ili waweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao kwa ajili ya kuwapa ushauri wa kitaalam kila wanapowahitaji katika kuendeleza kilimo bora na chenye tija.

“Mwaka huu kilimo kwa mkoa wetu ni kipaumbele cha pili na Halmashauri za Mkoa huu zinategemea kilimo kwa takribani asilimia 90 ya mapato yake ya ndani, ipo haja kuwawezesha maafisa kilimo kwa kuwa wana mchango kubwa katika mapato ya Halmashauri. Ningependa kuona mwaka 2016/2017 hadhi ya Maafisa Kilimo inapanda, Wakurugenzi muwathamini hawa wataalam ndiyo wanaowasaidia kupata hayo mapato katika pamba, choroko, dengu, mpunga na mazao mengine”, alisema Mtaka.

Aidha, kufuatia makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na India yaliyofanywa hivi karibuni kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa India juu ya biashara ya mazao ya jamii ya mikunde kama choroko, dengu na mbaazi takribani tani milioni sita, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unayo fursa kubwa ya kuzalisha mazao haya kwa takribani asilimia 60 kama ilivyo katika zao la pamba, kwa kuwa kuna ardhi yenye rutuba na wananchi wanalima mazao hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na Viongozi  na Maafisa Kilimo wa mkoa huo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah .
Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa(hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kutoka  kushoto), Mhe. Tano Mwera (Busega),Mhe. Joseph Chilongani(Meatu), Mhe. Benson Kilangi (Itilima ) na Mhe. Seif Shekalaghe.Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa waSimiyu, Ndg. Jeremia Shigala akichangia katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu .
Viongozi na Maafisa kilimo wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu.


AfDB YAAHIDI KUENDELEA KUIPIGA JEKI TANZANIA KUKUZA UCHUMI WAKE

$
0
0

Na Benny Mwaipaja,MoFP

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leautier, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo ameishukuru Benki hiyo kuwa mojawapo ya mashirika ya kimataifa yanayoisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Benki hiyo imewekeza hapa nchini kiasi cha dola Bilioni 2 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 4.4 kama ruzuku na mikopo yenye riba nafuu ili kuendeleza sekta mbalimbali ikiwemo barabara, elimu, kilimo, nishati ya umeme, na viwanda.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Dkt. Mpango, ameelezea kufurahishwa kwake na Dira ya AfDB ambayo inafanana na vipaumbele vya serikali, kupitia Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano ambao umelenga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Dira ya Benki hiyo imejikita katika malengo matano ambayo ni kuwekeza katika nishati ya umeme, uzalishaji wa chakula, kuendeleza viwanda, kuiunganisha Afrika kwa mtandao wa barabara na kuboresha maisha ya watu.

Mhe. Dkt. Mpango, amesema kuwa uwekezaji katika sekta hizo utasaidia mpango mkubwa wa uboreshaji wa miundombinu kama vile kujenga viwanda kwa kuhusisha sekta ya umma na binafsi-PPP, umeme wa kutosha kuendesha viwanda, barabara ambazo zitaunganisha nchi zote za Afrika.

“AfDB wametusaidia sana katika ujenzi wa barabara nyingi nchini Tanzania ikiwemo barabara ya kutoka Tanga kwenda Horohoro, ambayo imerahisisha usafiri wa kwenda nchini Kenya. Barabara nyingine zitajengwa kutoka mpakani Kagera kupitia Kigoma kwenda Katavi, Dodoma hadi Iringa. Hili ni jambo kubwa” Alisema Dkt. Mpango
.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) akiwa kwenye majadiliano na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leutier (katikati) na Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie Leutier, kulia kwa Dkt. Leutier, ni Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero na watendaji wa Wizara.
Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango. Kutoka kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie Leutier, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (anayeandika).

SIA PIUS AIBUKA NA TAJI LA MISS SINZA 2016

$
0
0

Windhoek Draught Miss Sinza 2016, Sia Pius (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Listoni (kushoto) na mshindi wa tatu Hafsa Mahamood baada ya kutangazwa mshindi Hoteli ya Defrance lilikofanyika shindano hilo jana usiku kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia kinywaji wa Windhoek.

Warembo walioingia tano bora. Kutoka kulia ni Catherine Listone, Sia Pius, Hafsa Mahamood, Saida Khalifa na Faith Msuya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabidhi mshindi wa kwanza wa shindano hilo kitita cha sh.500,000.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabishi mshindi huyo moja ya katoni ya windhoek kati ya tano zilizotolewa na kampuni hiyo kwa mshindi huyo ambapo pia mshindi wa pili na watatu walikabidhiwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Miss Sinza 2016 imemtangaza Sia Pius kuwa mshindi wa Windhoek Draught Miss Sinza 2016 baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Defrance iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana usiku.

Pius aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake tisa waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Catherine Listoni huku ya tatu ikichukuliwa na Hafsa Mahamood.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spiritis kupitia bia ya Windhoek pamoja na wadhamini wengine.Mshindi wa kwanza wa shindano hilo alizawadiwa sh.500,000 wakati wa pili akijipatia sh.300,000 na watatu akiondoka na kitita cha sh.200,000 huku washiriki wengine wakiondoka na kifuta jasho cha sh.100,000 kila mmoja.

Washindi hao watatu wataingia moja kwa moja katika shindano la kumsaka Miss Kinondoni 2016 litakalofanyika mwezi ujao.
 

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAWASILI DAR, KUAGWA KESHO VIWANJA VYA SINZA-UZURI

$
0
0


Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India. 
 
MarehemuSenga alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA NA K0-VIS MEDIA/Khalfan Said) .

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo.

Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
 
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili.

JUMUIYA YA KANGA MATERNITY TRUST YA ZANZIBAR YAFANYA SEMINA KWA WATAFITI WAZALENDO

$
0
0

Dkt. Mdhamin wa Kijiji cha Watoto (S.O.S) Zanzibar Abdulla Mohammed Hassan akimkabidhi Certificate Dkt. Natasha Hussein kwa niaba ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Baadhi ya walikwa katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.


Daktari bingwa. Tarek Meguid wa wodi ya Wazazi Mnazimmoja Hospitali akitoa tarifa ya pili ya watafiti wazalendo kuhusu wajawazito na watoto katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust iliyofanyika Tembo Hotel Mjini Zanzibar.

Naibu Waziri wa Habari afungua mashindano ya Brazuka Kibenki

$
0
0

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wanamichezo kutoka mabenki mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikagua timu wa wachezaji wa Diamond Trust Bank (DTB) wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mratibu wa mashindano hayo kutoka Barclays Bi. Nasikia Berya

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi naodha wa timu ya DTB ngao ya hisani kwa kuwafunga mabao matatu kwa moja timu ya Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Michezo Bw. Rashid Mijuza.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na wachezaji kutoka Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam

Waamuzi wa michezo ya Brazuka kibenki katika picha ya pamoja wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Genofeva Matemu – WHUSM

………………………………………………………………………………

Na Lorietha Laurence-WHUSM

Serikali kupitia sera ya Maendeleo ya Michezo inasisitiza wananchi na jamii kwa ujumla kushiriki katika michezo ili kujenga afya, kuunganisha watu toka makundi mbalimbali bila ubaguzi wa kidini, kisiasa, wala kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Kibenki maarufu kama Brazuka katika viwanja vya Gymkhana leo jijini Dar es Salaam.

Mhe. Wambura ameeleza kuwa ni muhimu kwa wafanyakazi kujumuika kwa pamoja katika michezo ili kuboresha afya na kuimarisha uhusiano baina yao. “Michezo ni kitu kizuri kwani husaidia katika kuimarisha na kulinda afya zetu hivyo ni vyema kila mmoja wetu kushiriki katika michezo ili kuwa nguvu ya kutekeleza majukumu yetu ya kila siku” alisema Mhe. Wambura.

Vilevile alitoa shukrani kwa wakuu wote wa mabenki kwa ushirikiano wao wa kuwaleta pamoja wafanyakazi wa benki ili kufahamiana na kuimarisha ushirikiano baina yao . Kwa upande wake Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Bw. Aron Luhanga amesema kuwa dhumuni la mashindano hayo ni kuendeleza mahusiano baina ya benki kwa kufahamiana na kuimarisha afya na fikra zao.

“mashindano haya ni kwa ajili ya kufahamiana na kuimarisha urafiki kwa wafanyakazi wa sekta ya benki kwa kufanya sekta ya kibenki kuwa sehemu bora ya shughuli za kiuchumi nchini” alisema Bw.Luhanga.

Mashindano hayo ya Brazuka kibenki yanaratibiwa na benki ya Barclays na ni mara ya pili kufanyika nchini ambapo mwaka jana benki ya Diamond Trust (DTB) iliibuka mshindi hivyo kushiriki katika ufunguzi wa michuano hiyo mwaka huu.

Benki zinazoshiriki mashindano hayo ni 18 ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania, NMB, Stanbic, KCB, Exim, Citi Benki, Commrcial Bank of Africa (BOA),CRDB, Letshego, Eco Bwnki, Akiba, Diamond Trust Benki, Bank of India, Banc ABC,Azania na Twiga Bancorp. 

JAJI KIONGOZI WA MAHAKAMA KUU ATEMBELEA UJENZI WA MAHAKAMA YA MWANZO KIGAMBONI

$
0
0

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali akimsikiliza Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadu Kitunzi akimwonyesha Ramani ya jengo la Mahakama ya Mwanzo Kigamboni linaloendelea kujengwa jana jijini Dar es Salaam. Jengo hilo linajengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi.

Jengo la Mahakama ya Mwanzo Kigamboni linalojengwa kwa kutumia Teknolojia ya Moladi.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA JOSEPH EMILIO SENGA.

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Joseph Emilio Senga na wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga kilichotokea tarehe 27 Julai, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Katika salamu zake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesema tasnia ya habari imempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya tasnia ya habari nchini.

“Joseph Senga alikuwa mwanahabari shupavu na hodari, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya tasnia ya habari na kutenda haki katika tasnia hiyo.

“Napenda kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu” 

Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Joseph Emilio Senga kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.

RAHA YA MILELE UMPE EHE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE 

APUMZIKE KWA AMANI

AMINA.

TEMEKE MARKET YATWAA UBINGWA WA NDONDO CUP

$
0
0
FAINALI ya Sports Extra Ndondo Cup imemalizika leo Jumamosi Julai 30, 2016 kwa timu ya Temeke Market kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kauzu FC mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Bandari (Wembly), Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo umeshuhudia timu ya Temeke Market ikiibuka mabingwa kwa kuwafunga Kauzu FC ambapo Mabao ya Temeke Market yalifungwa na Ramadhan Madebe, Shaban Kisiga na Adam Kingwande huku lile la Kauzu FC likifungwa na Rashid Tumbo.

Kwa kutwaa ubingwa huo Temeke Market wamejitwalia kombe pamoja na shilingi milioni 10 huku wakitoa mchezaji bora wa mashindano hayo ambaye Shaban Kisiga aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni moja, viatu na tuzo.

Kisiga amesema kuwa anafurahi kuona kuwa amekuwa mchezaji bora kwa mara ya pili mfululizo na ametaka waandaaji wa mashindano haya waboreshe zaidi ikiwemo kukarabati viwanja vitajavyotumika. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mgeni Rasmi katika Fainali hiyo, alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye (katikati) alieambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine. Pichani ni Timu iliyoshika nafasi ya pili ikipita kukabidhiwa zawadi yao ikiwa ni mfano wa hundi yenye kiasi cha shilingi milioni tano kutoka kwa Kampuni ya Simu ya Airatel Tanzania, iliyokabidhiwa na Meneja Mawasiliano wake, Jackson Mmbando.
Nyanda wa Timu ya Kauzu FC akiondoa hatari iliyoelekezwa langoni kwake katika Mtanange wa Fainali kati ya Timu hiyo na Temeke Market iliyoibuka na Ubingwa wa Mashindano ya Ndondo Cup 2016.
Chenga ya mwili.






Mchezaji wa Temeke Market akiwania Mpira wa Juu mbele ya Beki wa Kauzu FC.
 
Mambo yalivyokuwa baada ya kuruka. 

TAARIFA YA BUNGE KWA UMMA KUHUSU KAMATI ZA BUNGE

RC MANYARA ATAKA KAYA 40,642 WILAYANI BABATI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza juzi na wananchi wa Kijiji cha Duru, Tarafa ya Goroa Wilaya ya Babati juu ya wao kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF).
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera amewaagiza viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhakikisha hadi Desemba mwaka huu kaya 40,642 zinajiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (CHF) hivyo kufikia asilimia 50 ya kaya za wilaya hiyo.

Akizungumza kwenye kata ya Duru Tarafa ya Goroa, Dk Bendera alisema wilaya hiyo ina kaya 81,284 hivyo viongozi wa wilaya hiyo wahakikishe hadi mwezi Desemba wawe wamefanikisha nusu ya kaya zijiunge na mfuko huo.

Dk  Bendera alisema suala la kupatiwa matibabu pindi mtu akiugua halina mjadala hivyo viongozi wa ngazi tofauti kwenye wilaya hiyo wanapaswa kufuatilia ili kaya hizo zijiunge na mfuko huo ambao una manufaa kwao.

Alisema viongozi wote wa eneo hilo wanapaswa kuhakikisha jamii inajiunga na mfuko huo kwani ni ukombozi wao kwenye sekta ya afya na siku wakistaafu wananchi watawakumbuka kwa kusababisha mabadiliko ya huduma hizo.

“Naibu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla alitoa agizo kwa mkoa wa Manyara kuhakikisha baada ya miezi sita ijayo tufikie asilimia 50 ya kaya zote kujiunga na CHF iliyoboreshwa,” alisema.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Hamis Malinga akizungumza mbele ya Dk Bendera, alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa wananchi wa eneo hilo wanajiunga kwa wingi na mfuko huo.

Malinga alisema kupitia timu waliyonayo kuanzia ngazi ya vijiji, kata na tarafa, watatimiza majukumu yao kwa kupeana mrejesho kila mwezi ili kutambua wamefikia hatua gani na wanatarajia hadi mwezi Desemba watafanikisha.

Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) mkoani Manyara, Isaya Shekifu alisema mpango wa CHF ulioboreshwa utawawezesha kila kaya ya watu sita baba, mama na watoto wanne ambao hawajafikisha miaka 18 kupata matibabu kwa gharama ya sh30,000 katika mwaka mzima.

Shekifu alisema bima ya afya ni muhimu kwa sababu siyo kila mtu anapopata ugonjwa ana uwezo wa kugharamia matibabu na nchi zilizoendelea zimefanikiwa kupunguza vifo visivyo na lazima kwa kuhakikisha watu wanajiunga na mfuko.

“Katika CHF ya zamani huduma za nje tu ndizo zilizotolewa, hii iliyoboreshwa huduma ya magonjwa ya nje, kulazwa, upasuaji na vipimo ikiwemo x- ray zinatolewa kwa wanachama waliojiunga bila kulipia,” alisema Shekifu.

Wasanii waaswa kuzingatia maadili katika utengenezaji wa kazi zao

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua studio mpya ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam wa pili kushoto ni mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Studio Bw. Darish Pandit(kushoto) kwa kuhusu maeneo mbalimbali ndani ya studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akiangalia moja ya vyumba vya kurekodia na kutengengeneza video vilivyopo ndani ya studio ya Wanene Entertainment mara baada ya kuizindua studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (aliyekaa) akiangalia moja ya ya kazi zilizorekodiwa na kutengenezwa na kampuni ya Wanene Entertainment Studio wakati alipokuwa akizundua studio hiyo iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam Julai 29, 2016. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

JPM AKOSHWA NA DC WA IGUNGA JOHN MWAIPOPO, AAMURU STENDI YA BASI NA SOKO VIANZE KAZI JUMATATU

$
0
0
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani ambako nako pia wana sehemu za Biashara.
  Rais  Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe. John Mwaipopo wakati akielezea changamoto na hatua alizochukua  kuzitatua za stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
  Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt. Magufuli kuhusiana na  Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. Rais ameitaka SUMATRA ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi Jumatatu. Pia ameiagiza halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu za biashara bila kuzitumia katika soko jipya wathibitiwe mara moja.
 Wananchi wa Igunga wanalipuka kwa furaha na Mzee huyu anatoa  noti ya shilingi 10,000/- akitaka kumtuza  Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua changamoto za Stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
Rais Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele wa grade One kutoka uongozi wa wilaya ya Igunga  wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images