Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Halmashauri ya Mji Njombe yaendelea kuboresha Sekta ya Afya Vijijini

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Fedha Halmashauri ya Mji Njombe wakipata ufafanuzi juu ya ujenzi wa stand mpya ya Mabasi inayofadhiiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa kukuza na kuendeleza Miji (ULGSP), mradi ambao unatekelezwa kwenye Halmashauri 18 Nchini.
Ujenzi wa Jengo la vyumba 04 vya madarasa unaoendelea katika Shule ya Sekondari Mgola.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha Halmashauri ya Mji Njombe wakiwa wamesimama Nje ya jengo la zahanati ya Utalingolo iliyopo katika Kijiji cha Utalingolo ambayo ipo katika hatua za umaliziaji. Wa kwanza kulia ni Mwandisi wa Halmashauri Eng. Ibrahim Mkangalla.

Na Hyasinta Kissima - Njombe

Halmashauri ya Mji Njombe imetoa jumla ya shilingi milioni 128 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ili kukamilisha ujenzi wa zahanati na ununuzi wa vifaa vya zahanati kwenye jumla ya zahanati 12 zilizopo kwenye Halmashauri hiyo.

Akitoa ufafanuzi kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanywa na Kamati ya fedha ya Halmashauri, Mchumi wa Mji Njombe Ndugu Shigela Ganja amesema kuwa fedha hizo zilitolewa ziliambatana na maelezo ya kuhakikisha kuwa zinamalizia shughuli za ujenzi ili kuhakikisha kuwa zahanati hizo zinaanza kutoa huduma kwa wananchi haraka iwezekanavyo na kupunguza adha ya Wananchi hususani waliopo maeneo ya Vijijini ambapo huduma za afya zimekuwa ni za tabu.

Akifanya majumuisho ya ukaguzi wa miradi kwa upande wa Zahanati, Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Mwanzinga amesema kuwa miongoni mwa Zahanati ambazo Kamati yake imezikagua zinaridhisha ingawaje usimamizi wa karibu zaidi unahitajika ili kuhakikisha fedha ambazo halmashauri imezipeleka zinatumika kwa mujibu wa maelekezo na zinakamilika kwa wakati.

“Lengo la kuzisimamia Zahanati hizo ni kuhakikisha kuwa mpaka kufikia mwaka 2017 Majengo yote ya zahanati zilizokwisha patiwa fedha zinaanza kutoa huduma kwa Wananchi kama tulivyoahidi katika Kampeni za uchaguzi. Kuna Kata ambazo licha ya Zahanati zake kupatiwa fedha na Halmashauri tangu mwezi Mei mpaka sasa, fedha hizo bado zipo kwenye Akaunti na Diwani wa kata husika yupo kimya. Zahanati hizo zinakuwa kero si kwa Kamati yangu bali hata kwa wale wananchi wa maeneo husika kwani zinakuwa za muda mrefu na bado ujenzi wake unakua hauna matumaini kwa Wananchi wa eneo husika.

Nawataka Waheshimiwa Madiwani washirikiane na Wataalamu katika usimamizi wa Zahanati hizo” Aidha Mwanzinga ameitaka Halmashauri kuwaandikia madiwani wasiofahamu majukumu yao barua ya kuwakumbusha majukumu yao ya kazi kwani moja kati ya jukumu la diwani ni kufanya usimamizi wa miradi inayoendelea ndani ya Kata yake na kuitolea taarifa kwenye vikao mbalimbali vya Kisheria pale panapokuwa na changamoto inayokwamisha mradi husika kutokabidhiwa kwa Wananchi kwa wakati.

Nae mjumbe wa Kamati ya fedha wa Halmashauri Filoteus Mligo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Lugenge amesema kuwa ni vyema Halmashauri itoe vipaumbele vya zabuni kwa wakandarasi ambao wanamaliza kazi zao kwa ubora na kwa wakati ili kuhakikisha kuwa miradi ya Halmashauri inakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Mligo ameongezea kuwa ni jukumu la Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wa Kata zao kuendelea kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati badala ya kuitegemea serikali pekee.

Miradi mingine iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa madarasa, ujenzi wa stand mpya ya mabasi, ujenzi wa vyoo na ujenzi wa nyumba za kulala waalimu katika shule za sekondari.

KUMBUKUMBU

$
0
0
Ni miaka 25 leo toka baba yetu mpenzi Joseph Cosmas Mango, ametangulia kwa baba yetu Muumba yote. Familia yote ya Mango inaendelea kukumbuka busara na hekima zako daima .Tutakua na misa ya kumbukumbu leo saa 11 jioni katika kanisa la Mashahidi wa Uganda Magomeni.Wote mnakaribishwa.Mwenyezi Mungu aendelee kuilaza Roho yako mahali pema peponi,Amina.

MAKAMU WA RAIS AMJULIA HALI SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai alipofika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India ambapo alikwenda kwa ajilia ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai pamoja na Mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga (kulia) alipofika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

TRL yatangaza mabadiliko ya muda wa treni kuondoka Dar kueleka Bara

$
0
0
Kampuni ya Reli ya Tanzania (TRL) imefanya mabadiliko ya muda wa Treni ya Abiria kulekea mikoa ya Kigoma na Mwanza ambapo kuanzia tarehe 02 Agosti 2016 Treni itaanza kuondoka saa tisa(9) mchana badala ya saa 11 jioni muda wa sasa.

Mabadiliko hayo yametangazwa na Meneja Uhusiano wa TRL Midladjy Maez wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.

Maez amesema kuwa mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya pili ya huduma za Jiji kutoka kituo Kikuu cha Reli cha Dar es Salaam kwenda Pugu ambayo itaanza kutoa huduma mapema siku ya Jumatatu ya tarehe 01/08/2016.

Aliongeza kuwa mabadiliko hayo yanahusu treni za abiria za huduma za kawaida zinazoondoka siku za Jumanne na Ijuma na kubainisha kuwa kwa upande wa huduma za treni ya Deluxe zitaendelea na muda wake wa kawaida.

“Uongozi umeamua kufanya mabadiliko haya kwa sababu za kiusalama zaidi kwani mabadiliko haya yataepusha muingiliano unaoweza kupelekea ajali na kuongeza kuwa kwa safari za kutoka Kigoma na Mwanza muda umebaki uleule”. Alisema Maez.

Meneja Uhusiano huyo aliongeza kuwa huduma za treni ya Jiji kwenda Pugu itakuwa na vituo 10 ambavyoa alivitaja kuwa ni pamoja na Pugu Stesheni, Gongo la Mboto,FFU Mombasa, Banana, (njia panda kwenda Stesheni), na karakata.

Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi,SS Bhakressa, Kamata na Kituo Kikuu cha reli Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa huduma hiyo itakuwa na awamu mbili asubuhi na Alasiri ambapo treni ya kwanza itaondoka kituo cha Pugu saa 12 asubuhi na kuwasili kituo cha Dar es Salaam sa 12:55 asubuhi na kufanya safari tatu zitakazomalizika saa 05:15 asubuhi. 

Jioni kutakuwa na safari tatu ambapo treni itaondoka kituo cha Dar es Salaam saa 09:55 alasiri kwenda Pugu na kuwasili saa 10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka Pugu kuja Kituo Kikuu cha Dar es Salaam saa 03:20 usiku.

Mh Mwigulu Nchemba alipohutubia leo mkoani Singida kwenye ziara ya Rais Magufuli

JAJI MKUU AMSABAHI SPIKA WA BUNGE NYUMBANI KWAKE.

$
0
0

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai alipofika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mke wa Spika Dkt Fatma Mganga. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman aliyefika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akifurahia jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman aliyefika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.(Picha na Ofisi ya Bunge).

VETA YATOA VIFAA VYA UFUNDI VYA SH.MILIONI 11 KWA ATAMIZI YA OSARIKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi Kanda ya Dar es Salaam VETA imetoa vifaa vya ufundi stadi vya thamani ya sh.milioni 11 katika atamizi ya Osarika Woodwork ikiwa ni sehemu ya kuendeleza atamizi hiyo kwa ujuzi na kufundisha vijana wengine wanaoenda kufanya mafunzo ya vitendo katika atamizi hiyo.

Akizungumza leo wakati hafla ya kukabidhi vifaa vya ufundi wa vitu vya samani katika atamizi ya Osarika Woodwork, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam wa VETA, Habibu Bukko amesema kuwa vifaa hivyo walivyotoa kwa kikundi hicho kuongeza uzalishaji samani mbalimbali ikiwa ni pamoja kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaotoka Veta.

Amesema vijana wa Osarika ni zao la VETA ambao wameweza kuunda kukundi na kusajili hivyo wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira lakini wameonyesha njia mpaka kuja kuongeza nguvu ya vifaa.

Bukko amesema vifaa hivyo ni mali kikundi cha Osarika wakivurugana vitu hivyo wanatakiwa kurudisha ili vikaweze kufanya kazi katika atamizi nyingine .

Aidha amesema kuwa VETA kuendeleza ni atamizi ni sehemu yao katika kuhakikisha atamizi zinaendelea katika kuzalisha ajira za vijana kutokana na mafunzo waliopata katika vyuo vya Ufundi.

Naye Mwakilishi wa Diwani wa Kata ya Tandika, Mwenyekiti wa Serikali Mtaa Mabatini ,Sharifu Jumbe amesema kuwa vijana wanatakiwa kujituma katika kufanya kazi na kuwataka wengine waende kupata mafunzo VETA.
 Sehemu ya misaada ya iliyotolewa na chuo cha VETA kanda ya Dar es Salaam leo katika kikundi cha Atamizi ya Orasika iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuongeza nguvu kwa vijana ili kupunguza ongezeko la vijana wasio na ajira.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika  ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akimkabidhi moja ya kifaa cha Kukatia Mbao na Alminium mwanaatamizi ya Orasika-Tandika, David Mshilili jijini Dar es Salaam leo. Kulia aliyevaa Koti ni Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam, Habibu Bukko.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika  ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akimkabi baadhi ya vifaa vya ujenzi vijana wa atamizi ya Osarika jijini Dar es Salaam leo. 

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika  ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe, Viongozi wa chuo cha VETA, wanaatamizi ya Osarika wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanachi wa mtaa huo jijini Dar es Salaam leo.

IDARA ZA UHAMIAJI TANZANIA NA ZAMBIA ZAKUTANA DAR ES ES SALAAM LEO.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu  Jamii.
IDARA ya Uhamiaji nchini imekutana na Idara ya Uhamiaji ya nchini Zambia kujadili masuala ya uhamiaji kati nchi mbili juu wananchi katika nchi hizo kufuata taratibu za uhamiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji na Msemaji wa Idara hiyo, Abbas Irovya amesema  kuwa kuna watanzania walikamatwa nchini Zambia 4000 ambao walikuwa wanajishughulisha na ususi.

Irovya amesema kuwa kuna watu wanaghushi hati ya kusafiria na kudai kuwa wanataiboresha ili wasiweze kughushi hati hizo na wataobanika kuwa na hati hizo watachukuliwa hatua katika vyombo dola.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji wa Zambia, Moola Milomo amesema kuwa kuna fursa za ususi nchini humo na kutaka watanzania kufuata utaratibu wa idara ya uhamiaji.

Amesema kuna changamoto kwa watu wanaoingia nchini Zambia lakini Tanzania na inakabiliwa nazo hivyo kunahitaji utatuzi.
  Naibu Kamishna wa Idara Uhamiaji, Abbas Irovya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maswala mbalimbali yanayojitokeza kwenidara hiyo kati ya Tanzania na Zambia.
Naibu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Abbas Irovya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji nchini Zambia, Moola Milomo.
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji nchini Zambia, Moola Milomo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kumaliza mkutano wa kujadili masula ya uhamiaji kati ya nchi Zambia na Tanzania. Kushoto ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya.





Baadhi ya Watendaji mbalimbali Idara ya Uhamiaji wa Tanzania na Zambia wakiwa katika mkutano wa kujadili masuala ya uhamiaji kati ya nchi ya Tanzania na Zambia katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.




CAMEL OIL YAFAFANUA HATUA KWA HATUA UUZWAJI WA KIWANJA CHA MANZESE.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu. 
KAMPUNI ya Camel Oil  imesema uuzwaji wa kiwanja namba 130 kilichoko Block A, Manzese jijini Dar es Salaam ulizingatia taratibu zote za kisheria na kwamba hakuna sehemu iliyoghushi hati za kiwanja hicho kama inavyodaiwa.

Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kampuni hiyo, Mahfoudh Ally, alisema kampuni yake ilifata taratibu zote za kiubinadamu na kisheria katika kuuza kiwanja hicho baada ya mmiliki wa awali, Mzee Mohamed Fakhi kushindwa kulipa deni la Sh bilioni 1.4.

Amsema ameamua kuweka wazi suala hilo baada ya  kuona utitiri wa habari za nia ya kupotosha ukweli.

Mahfoudh kuuza kiwanja hicho ulikuwa uamuzi wa mwisho kabisa baada ya jitihada za muda mrefu zilizogonga mwamba baada ya ahadi hewa nyingi sana kutoka kwa mdaiwa  Mzee Mohammed.

Amesema kabla ya mwaka 2010 kampuni yake ilifanya biashara kwa muda mrefu na Mzee Mohamed  wa Manzese Filling Station kuhusiana na  kuuza  mafuta kwa mkopo kwa makubaliano kwamba Camel Oil ilipwe kila mwisho wa mwezi.

Mahfoudh amesema Camel Oil iliendelea kukipa kituo hicho mafuta lakini mmiliki wa kituo hicho aliendelea kulimbikiza deni hadi kufikia Sh bilioni 1.6 na mwaka 2012 aliacha kununua mafuta kwenye kampuni hiyo ya Camel bila kutoa taarifa yoyote, na Mzee Mohammed pamoja na mtoto wake wakatokomea kusikofahamika.

“Tulifuatilia kujua kwanini kulikuwa na ukimya wa muda na tulitaka kujua atalipaje deni hilo, baada ya kumtafuta tulimpata na tukakubaliana namna ya kulipa deni hilo. Alitoa hundi ambazo baadhi zilipita na nyingi ziligonga ukuta kwani hakuwa na hela benki. Kwa mara nyingine akatokomea kusikojulikana.  Jitihada za dhati ziliendelea kumtafuta na kumsihi alipe ila palikuwa na kila dalili ya kushindwa kulipa deni. Na tulipoona anashindwa kulipa deni tuliomba kushikilia hati mbili za viwanja vyake kama dhamana,” alisema.

Amesema, Mzee Mohamed alikubali mwenyewe kwa maandishi kwamba viwanja vyake vishikiliwe na Camel Oil kama dhamana ya deni hilo analodaiwa, na ushahidi wote wa maandishi upo.
“Kwa masikitiko Makubwa, Camel tulibaini baadaye kuwa hata viwanja wanavyotaka kuchukua kama dhamana, Mzee Mohamed alishaviweka dhamana kwenye kampuni zingine ambazo zinamdai madeni mbalimbali,” alisema.

amesema kuwa hati moja ya kiwanja cha kitalu A, kilichopo Manzese ilikuwa inashikiliwa na Kampuni ya TOTAL  iliyokuwa ikimdai Mzee Mohamed Sh.milioni 165 lakini Camel Oil ilikubali kulipa deni hilo ili kushikilia hati hiyo kwa makubaliano na Mzee Mohamed kwamba fedha hizo ziongezwe kwenye deni la awali la Sh. Bilioni 1.6, ambazo Camel Oil inamdai. Pia ushahidi wa maandishi upo.

Mahfoudh alisema kwenye mkataba wa kukubali deni iliyosainiwa Septemba mwaka 2010, Mzee Mohamed alikiri kudaiwa na Camel Oil Sh bilioni 1.6 ambazo alikubali kuzilipa kwa mujibu wa masharti na makubaliano kwenye mkataba huo, kitu ambacho hakuonyesha dalili ya kutekeleza alichokiahidi.

Mahfoudh alisema kwenye makubaliano ya mkataba huo, Mohamed ambaye ni mdaiwa alikubali kuweka dhamana kiwanja namba 130 Kitalu A Manzese chenye thamani ya Sh milioni 850 na kiwanja namba 861 na namba 862 cha Msasani Beach vyenye thamani ya Sh. 300,000,000.

“Katika hatua isiyo ya kawaida na ya ajabu, ya kusikitisha na kudhalilisha, hasa kwa mtu mzima kama Mzee Mohammed, ni kwenda kula kiapo Polisi pamoja na Ardhi kwamba alipoteza hati za viwanja vyake akiwa na nia mbaya ya kudhulumu, kufisadi na kuidanganya Serikali mchana kweupe. Hiki kilikuwa kitendo kibaya na cha kitapeli. Nyaraka zote za ushahidi pia zinaonyesha kila kitu kinagaubaga,” alisema Mahfoudh.

“Kweli ukistaajabu ya Musa, uatayaona ya Firauni. Kama vile hii haitoshi, baada ya kugundulika njama zake , Mzee Mohammed alifungua kesi ya kughushi, dhidi ya Camel Oil. Baada ya muda sio mrefu, Mzee Mohammed alikiri mwenyewe kufuta kesi ya kughushi na akamuandikia barua IGP na DPP na Camel wakapata nakala. Katika barua yake, anasema aliamua kufuta kesi ya kughushi, bila ya kushurutiswa na yeyote, ila pengine nafsi ilimsuta,” alisema.

Mahfoudh alisema baada ya jitihada zote kufanyika ili Mzee Mohamed alipe deni hilo ilishindikana na ndipo walipomtafuta dalali kwa ajili ya kuuza kiwanja cha Manzese kujaribu kufidia deni ambalo wanamdai.

Alisema Kampuni ya Udalali ya Bilo Star Debt Collectors ilipewa kazi hiyo na tarehe 3 Julai ilitoa tangazo kwenye gazeti la Mzalendo kwa ajili ya kuuza kiwanja cha Mzee Mohamed kilichoko  Manzese kama sehemu ya kufidia deni analodiwa na taratibu zote za msingi na kisheria zikawa zimezingatiwa.

“Ingawa tulijua hata tukiuza kiwanja kile hatutapata kiasi tunachomdai ambacho kwa mwaka 2016 kilishapungua na deni mpaka Julai 2016 lilikuwa Sh. Bilioni 1.4 lakini tuliamua tu tuuze angalau tupate kitakachopatikana kuliko kukosa kabisa maana mdaiwa alionyesha dalili zote za kushindwa kulipa deni,” alisema.

Aidha, alisema mnada wa hadhara ulifanyika tarehe 9 Julai 2016 na Kampuni ya State Oil ndiyo ilipata kiwanja hicho kwa kununua kwa Sh bilioni moja (1,000,000,000) hivyo kuwa mmiliki halali wa kiwanja hicho namba 130, Block A Manzese jijini Dar es Salaam.

TUNAZISUBIRI NEC NA ZEC KUIPIGIA KURA YA MAONI KATIBA INAYOPENDEKEZWA-DKT.MWAKYEMBE.

$
0
0
 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na watendaji wa wizara ya Katiba na Sheria jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara ya katiba na sheria jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali inazisubiri Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanziba (ZEC) zimalize majadiliano yao ili mchakato wa kuipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa ufanyike.

Mhe. Mwakyembe ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipokutana na uongozi wa Kikosi cha Kupambana na Haki za Mirathi  (KIKUHAMI ) kilichoko chini ya Chama cha Wanawake katika Sheria na Maendeleo  Afrika – WiLDAF.

Amesema zoezi hilo lingekuwa limeshakamilika ila Tume za Uchaguzi ziliona ni bora liahirishwe kwanza ili kupisha zoezi la Kikatiba lililokuwa likiikabili nchi la Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana likamilike na kwamba kukamilika kwa zoezi hilo kunatoa fursa kwa Serikali kuendelea na mpango wake wa kuendesha kura ya maoni juu ya Katiba Inayopendekezwa ili kupata Katiba Mpya ya Tanzania.

Aliongeza kuwa Katiba Inayopendekezwa ina vitu vingi sana ambavyo vitasaidia upatikanaji wa haki za wanawake na kuondoa uonevu dhidi yao na hivyo kufanikisha harakati ambazo wadau mbalimbali wa wanawake nchini wamekuwa wakizipigania na hivyo kukamilika wakati Katiba mpya itakapokuwa imepatikana.

Aidha Mhe. Waziri ameutaka uongozi huo wa KIKUHAMI kupitia WiLDAF kuwasilisha Wizarani mapendekezo yao juu ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za Mirathi nchini wanazoziona zinawakandamiza wanawake ili ziweze kufanyiwa marekebisho na ziendane na wakati uliopo.

“si mnataka sheria mbalimbali za mirathi zibadilishwe?, leteni mapendekezo yenu , hili ni jukumu letu sote, sisi tupo na hapa wizarani tunao wataalamu watazipitia na kuona namna ya kuzifanyia kazi, ili ziendane na wakati uliopo sasa, alisema na kuongeza kuwa ndio maana amesema Katiba Inayopendekezwa ina vipengele vingi ambavyo vitasaidia kuondoa uonevu kwa wanawake nchini  itakapopitishwa na wananchi kupitia kura ya maoni.”

KIKUHAMI chini ya Uongozi wa Bibi Thabita Siwale ulimuomba Waziiri wa Katiba na Sheria Dkt Mwakyembe kuangalia uwezekano wa kuondoa sheria zinazowakandamiza wanawake hasa zile za mirathi kwani zinawafanya wanawake hasa wajane kunyanyasika katika nchi yao.

WATAKAOLETA VURUGU MIMI NITAWASHUGHULIKIA KIKAMILIFU BILA HURUMA,WANANCHI HAWA WANA SHIDA WANATAKA KUTATULIWA MATATIZO YAO-RAIS MAGUFULI

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa serikali itanunua mashine mbili za kisasa za mionzi kwa ajili ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kupata matibabu katika Taasisi hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulu Hassan ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara fupi ya kutembelea Taasisi ya Saratani ya Ocean Road pamoja na Kumtembelea na kumpa pole Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhani Feruzi ambaye anapatiwa matibabu kwenye Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa mkakati uliopo wa serikali unalenga kuhakikisha kuwa hali ya utoaji wa huduma za afya na dawa kote nchini unaimarika maradufu ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwenye maeneo yao kwa ubora unatakiwa.

Kuhusu uhaba wa wahudumu wa afya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameuahidi uongozi wa Taasisi hiyo kuwa serikali itahakikisha wahudumu hao wanapatikana katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Baadhi ya wagonjwa na wananchi wamepongeza utoaji wa tiba katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na wameomba serikali iendelee kuipatia taasisi hiyo vifaa vya kisasa vya kutolea tiba kama hatua ya kuboresha utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu ya saratani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  akizungumza na Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhan Feruzi (katikati) ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Said Mohamed mkazi wa Mafia ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Mkazi huyo wa Mafia alimueleza Makamu wa Rais juu ya ugumu wa upatikanaji wa Dawa. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Bi. Maria Maliseli Boniface wa Kilosa Morogoro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Calist P. Mushi mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani  ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo (kulia) wakati wa kutembelea Taasisi hiyo  iliyopo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  akizungumza na wananchi waliokuja kuwaona ndugu na jamaa zao ambao wamelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Wananchi hao walimueleza Makamu wa Rais haja ya kuongezwa kwa mashine za mionzi suala ambalo Makamu wa Rais aliwajibu kuwa zitafungwa mashine mpya mbili katika mwaka huu wa fedha 2016-2017 ilikurahisisha matibabu.

BREAKING NEWZZZZ.... MOTO WAZUKA KATIKA JENGO LILILO KATIKA UJENZI JIJINI DAR MUDA HUU.

$
0
0

JENGO la ambalo liko katika hatua za mwisho za ujenzi lililopo katika makutano ya Mtaa wa Samora na Mkwepu limengua moto katika Ghorofa ya tatu na kutengeza viyoyozi vilivyokuwepo katika ghorofa hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mashuhuda wameeleza kuwa moto umeanza majira ya saa 11  kwa kuanza kufuka katika ghorofa ya tatu.
Jengo hilo lina ghorofa 16 ambazo katika hizo ghorofa ya tatu imeungua na kuteketea kwa mali zote zilizokuwemo humo.Chanzo cha moto hakijulikana hadi Michuzi Blog inaondoka katika eneo hilo.
Moto wazuka katika Jengo lililopo  mtaa wa Mkwepu na Samora  mida hii jijini Dar es Salaam.
Jeshi la zimamoto likiwa katika harakati za kuzima moto katika jengo lililopo Mtaa wa Samora na Mkwepu jijini Dar es Salaam jijini leo.

Rais Magufuli aanza ziara ya siku nne mikoa minne, aonya watakaothubutu kufanya vurugu

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria.

"Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa."Wananchi hawa wana shida, na siasa nzuri ni wananchi washibe, siasa nzuri ni wananchi wetu wapate dawa" Amesema Rais Magufuli.


Kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali yake ya awamu ya tano tangu aingie madarakani Rais Magufuli ametaja baadhi ya hatua hizo kuwa ni kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya laki moja na kuongeza fedha za miradi ya maendeleo katika bajeti ya serikali kutoka asilimia 26 ya mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia 40 katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017.



Hatua nyingine ni kuondoa wafanyakazi hewa 12,500 katika orodha ya waliokuwa wanalipwa mshahara na serikali, kudhibiti upotevu wa mapato serikalini, kutenga shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard gauge na pia akazungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya wala rushwa na wanaojihusisha na ufisadi kwa kuunda mahakama ya mafisadi huku akiapa kuwa katika kipindi chake hakuna fisadi atakayeendelea kutamba.


Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Ikungi na baadaye amefanya mkutano wa hadhara Singida Mjini ambako amesisitiza kuwa serikali yake haiko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ahadi na Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Singida


29 Julai, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Manyoni Mkoani Singida mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Singida.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wakazi wa Singida mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Manyoni mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
Mbunge wa manyoni Magharibi Yahya Masare akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za asili cha Manyoni kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli kuhutubia mkutano katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ikungi waliomsimamisha wakati akielekea Mkoani Singida. PICHA NA IKULU 

WADAU WACHANGIA VITI NA MEZA KWA SHULE ZA SEKONDARI

$
0
0
Mbunge waMbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete kushoto akipokea meza toka kwa mwakilishi wa Sayona Fruits Ltd ya Mboga iliyo chini ya kampuni ya MMI Steel ya Jijini Dar es Salaam, Abubakary Mlawa wakati wa makabidhiano ya viti na meza 724 kwa Shule tano za Sekondari za Jimbo hilo zoezi hilo lilifanyika kwenye shule ya Sekondari ya Lugoba.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete kushoto akipokea kiti toka kwa mwakilishi wa Sayona Fruits Ltd ya Mboga iliyo chini ya kampuni ya MMI Steel ya Jijini Dar es Salaam, Abubakary Mlawa wakati wa makabidhiano ya viti na meza 724 kwa Shule tano za Sekondari za Jimbo hilo zoezi hilo lilifanyika kwenye shule ya Sekondari ya Lugoba.

Na John Gagarini, Chalinze

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amepokea viti na meza vyenye thamani ya shilingi milioni 80kutoka kiwanda cha Matunda cha Sayona Fruits Ltd kwa ajili ya shule za sekondari za Halmashauri ya Chalinze.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mbunge huyo na mwakilishi wa kampuni hiyo Abubakry Mlawa kwenye shule ya sekondari ya Lugoba na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maofisa toka Halmashauri hiyo.

Akiishukuru kampuni hiyo ya Sayona Ridhiwani amesema kuwa wanawashukuru wadau hao kwani wanaisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa madawati kwa wanafunzi.

Ridhiwani amesema kuwa wamefarijika kuona mchango huo ambao umekuja wakati mwafaka wa kuwasaidia wanafunzi ambao wamekuwa wakisoma kwenye mazingira magumu kutokana na kutokuwa na madawati hali ambayo inwafanya washindwe kusoma vizuri.

Amesema kuwa walikuwa na uhaba wa vitina meza 724  kwa ajili ya shule tano ambapo zingine hazina tatizo la upungufu wa vifaa hivyo huku kwa shule za msingi upungufu ni madawati 1,500 ambapo wanatarajia kukamilisha upatikanaji kwani baadhi bado yanendelea kutengenezwa.

Aidha amesema kuwa Chalinze imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dk John Magufuli la kuhakikisha kuwa wanafunzi hawakai chini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kwenye wilaya ya Bagamoyo.

Amebainisha kuwa changamoto ambayo inaibuka kwa sasa ni madawati kuwa mengi huku kukiwa na upungufu wa madarasa na hiyo imetokana na wanafunzi wengi kujiunga na shule kutokana na serikali kuweka mpango wa wanafunzi kusoma bure hivyo kufanya madarasa kujaa.

Amewataka wadau wengine nao kujitokeza ili kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilo mapema iwezekanavyo na anaamini watafanikiwa kwani wameonyesha moyo wa kusaidia watoto wao waondokane na adha hiyo.

Kwa upande wake Abubakary Mlawa amesema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuwawezesha wanafunzi kukaa kwa nafasi na kwa wale wa shule za msingi wasikae chini ili waweze kusoma vizuri.

Mlawa amesema wameshatoa madawati 600 kwa Halmashauri ya Bagamoyo na watatoa madawati 600 kwa Halmashauri ya Chalinze kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Amesema kuwa wao wako tayari kusaidia ujenzi wa madarasa mapya ili kukabiliana na wingi wa wanafunzi ambao wamejitokeza kwa wingi kutokana na mpango huo wa serikali wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI JULAI 29, 2016

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 29.07.2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MJULIA HALI SPIKA JOB NDUGAI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai  wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika  jijini Dar es salaam kumsalimia  Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai  wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika  jijini Dar es salaam kumsalimia  Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. Picha na Ofisi ya Bunge

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMJULIA HALI SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika jijini Dar es salaam kumsalimia Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika jijini Dar es salaam kumsalimia Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Bunge).

Ratiba ya Usaili Maisha Plus East Africa 2016

$
0
0
Baada ya Usaili kufanyika kwa kishindo katika mikoa ya Mtwara na Dar es salaam usaili wa Maisha Plus unaendelea katika mikoa mingine ndani ya Tanzania. 
30/07/2016 - MBEYA - Ukumbi wa City Pub 
31/07/2016 - IRINGA - Savanna Garden 
02/08/2016 - DODOMA - Matei Lounge 
04/08/2016 - MWANZA - Rock Garden 
06/08/2016 - ARUSHA - Via Via
 13/08/2016 - ZANZIBAR - Ngome Kongwe 


Vijana wote wenye umri wa miaka 18 - 26 wanakaribishwa kujitokeza kwa wingi. Elimu na ujuzi ni kiwango chochote. Zawadi kwa mshindi ni Tzshs. Milioni 30. Fomu zinapatikana BURE kabisa kupitia www.maishaplus.tv na katika maeneo tajwa hapo juu. 

 Maisha Plus East Africa 2016 | #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
   
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images