Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1300 | 1301 | (Page 1302) | 1303 | 1304 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali  tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.

  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayokataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.

  “Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.

  Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.

  Nakuongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.

  Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

  Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).

  Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.

  Jaji Mutungi ametoa rai kwa  Viongozi wa Vyama vya Siasa  waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.

  Katika tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa zitahusika.

  0 0

   Balozi wa Algeria Nchini Saad Balabed akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika Tamasha la uzinduzi wa kitabu cha Safari ya Soka la Tanzania 1926 hadi 2016 ambapo ataitumia pia siku hiyo kusherehekea siku ya Uhuru wa nchi yake pamoja na wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Taasisi wa Michezo na Burudani (TSERP) Omari Bahari akitolea ufafanuzi juu ya uzinduzi wa kitabu hicho kitakachozinduliwa Julai 30 katika Tamasha litakalohusisha maveterani wa zamani wa Simba na Yanga pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali watakaoshiriki kimichezo ikiwemo kucheza mechi.
   Balozi wa Algeria Nchini Saad Balabed akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga.

  Na Zainab Nyamka. 
  KATIKA kukuza soka na kumbukumbu ya mchango wa wachezaji wa zamani katika mchezo wa mpira wa miguu  Taasisi ya Utafiti wa Michezo na Burudani (TSERP) imeamua kuandaa uzinduzi wa kitabu kitakachokuwa kinajulikana kwa jina la Safari ya Soka la Tanzania  1926-2016 huku  siku hiyo ikisindikizwa na bonanza litakalowahusisha mabalozi wa nchi mbalimbali wakiumana na kombaini ya maveterani wa  Simba na Yanga huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye huku Balozi wa Algeria nchini Tanzania Saad Balabed akitumia siku hiyo kusherehekea sikukuu ya uhuru wa ncho yake kwa kutimiza miaka 54.

  Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika  Julai 30 katika uwanja wa Taifa huku likisindikizwa na mechi mbalimbali kati ya Magic FM wakiumana na Kikundi cha uchekeshaji, Kampuni  ya Oryx ikipambana na Kombaini ya watuma salamu kutoka Jijini Dar es salaam wakiungana na wa mkoa wa Pwani, pia kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Simba na Yanga maveterani. 

  Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Omari Bahari amesema kuwa lengo la kufanya tamasha hilo ni kuweza kuwakumbusha wananchi mchango mkubwa uliofanywa na wachezaji wa zamani ambapo umeweza kutufikisha hapa tulipo.

  Bahari amesema kuwa, katika kuwaenzi wachezaji hao na jinsi gani walivyojitolea katika mchezo wa mpira wa miguu kutakuwa na picha mbalimbali za vikosi  vya yimu ya Taifa ambapo kimojawapo ni kile cha mwaka 1980 kilichoipeleka nchi yetu katika fainali za mataifa Afrika, pamoja na hilo pia kutakuwa na kikosi ambacho kilicheza mbele ya Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere na Raisi wa Sudani wakiwa hawajavaa jezi. Mbali na hilo pia, watajumuisha na picha ya Kikosi cha Simba kilichofika hatua ya Fainali kombe la Shirikisho mwaka 1993 na Yanga wakioingia hatua nya robo fainlai mwaka 1986.

  Balozi wa Algeria, Balabed amesema kuwa amefurahi sana kuweza kusherehekea sikukuu ya Uhuru wa  nchi yake kwa kudumisha michezo na akiwa kama balozi hapa nchini kwa takriani mwaka mmoja atahakikisha anasaidiana na Tanzania katika kukuza na kuendeleza mpira wa miguu kama wanavyoshirikiana katika sekta ya elimu. Amesema kuwa katika siku hiyo watafurahi kwa pamoja na watadumisha utamaduni huo kwani anaamini michezo inaunganisha watu wa aina mbalimbali na pia inajenga urafiki.

  Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni ya Property Internatonal Limited Masoud Khalfani amesema hatua hiyo ni nzuri sana kwani itawakutanisha wachezaji wote wa zamani na wao wamefurahi kuweza kushirikiana nao ili kufikia lengo la kumbukumbu ya wachezaji wa zamani na wapi wameufikisha mpira hadi hapa ulipo.

   Na moja ya  mavetreani wa timu ya Yanga, Keneth Mkapa amesema kuwa kwanza wamefurahi sana kuweza kucheza mechi hiyo na maveterani wa Simba kwanza itakuwa ni moja ya mechi nzuri na italeta hamasa kwa vijana wanaocheza sasa hivi kwani wataonesha uwezo wa hali ya juu. 

  Baadhi ya wachezaji wa zamani waliohudhuria ni Keneth Mkapa, Thomas Kipese, Mohamed Mwameja, Iddy Kibobe, Moses Mkandawile, Mohamed Hussein, Mohamed Mmachinga.

  0 0

  NA RAMADHANI JUMA

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imefanikiwa kukusanya asilimia 80.28 ya mapato kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya ndani katika mwaka wa fedha 2015/2016 uliomalizika Juni 30 mwaka huu.

  Katika mwaka huo wa fedha Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ilipanga kukusanya shilingi 4,566,075,181 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani (own sources) ambapo mpaka mwisho wa mwaka huo makusanyo halisi ni 3,665,699,279 sawa na asilimia 80.28 ya makisio.

  Akizungumza katika kikao cha mwaka cha Baraza la Halmashauri ya Manispaa hiyo, Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Jaffar Mwanyemba aliwaambia wajumbe wa Baraza hilo kuwa, mafanikio hayo yametokana na uchapaji kazi wa watendaji na madiwani wa Manispaa hiyo.

  Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa, Mstahiki Mwanyemba aliwapongeza wote waliohusika kwa namna yeyote katika kufikia hatua hiyo huku akitoa wito kwa Ofisi ya Mkurugenzi na Madiwani wa kuimarishwa kwa juhudi zaidi katika ukusanyaji katika mwaka wa fedha 2016/2017.

  "Mwaka mpya wa fedha umeshaanza hivyo Mkurugenzi na watendaji wako anzeni kukusanya kodi mapema...na waheshimiwa madiwani tuongeze nguvu katika kusimamia vyanzo vya mapato katika maeneo yetu" alisema.

  Aidha, katika mkutano huo ambao kwa mujibu wa kanuni unakuwa na ajenda mbili tu ambazo ni kujadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri kwa mwaka uliopita na kupitia na kupitisha ratiba ya vikao vya Halamshauri kwa mwaka unaofuata, wajumbe walipitisha ratiba ya vikao vya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 .

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa NMB,  Ineke Bussemarker akizungumza katika uzinduzi mpango wakuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae katika shule ya msingi Mlimani leo jijini Dar es Salaam.  
    Mchekeshaji Lucas Mhavile (Joti) akichekesha katika uzinduzi mpango wakuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae katika shule ya msingi Mlimani leo jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dk.Edicome Shirima akikata utepe kuashiria uzinduzi mpango wakuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae katika shule ya msingi Mlimani leo jijini Dar es Salaam. 

  Na Mwandishi Wetu.
  Benki ya NMB kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Women's World Banking wamezindua mpango wakuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za  fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae. 

  Akizungumza na  kwenye uzinduzi wa WAJIBU, Mkurugenzi wa Elimu wa Wizara ya  Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dk.Edicome Shirima alisema “Walaji wenye uwezo, wanaojiamini na walioshirikishwa wanaofanya maamuzi sahihi ya kifedha si tu ataboresha maisha yao bali jamii kwa ujumla. Ninafarijika sana leo kuzindua mpango huu wa WAJIBU kwani
  nina Imani kuwa utasaidia kuwapatia watoto na wazazi stadi muhimu zitakazowawezesha kupanga maisha
  yao ya baadae.”

  Amesema serikali imedhamiria kwa dhati kabisa kuboresha na kuendeleza elimu ya fedha katika ngazi
  zote za watanzania – Hususani wanajamii yote ya Tanzania,

  Shirima  amesema mpango  huo wa jifunze, Jipange – WAJIBIKA inajumuisha vipindi vitatu kwa ajili ya shule za sekondari na msingi –Kipindi cha kwanza  kitazingatia mafunzo ya elimu ya masuala ya fedha na taasisi za kifedha itakayowaunganisha wanafunzi na wazazi wao, na kufuatiwa na vipindi viwili maalumu kwa watoto wenyewe katika mafunzo hayo.

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa NMB,  Ineke Bussemarker amesema kuwa mpango huo umepewa jina la WAJIBU mahususi kwaajili ya akaunti za akiba za watoto na vijana,WAJIBU yenye maana ‘Wajibika’ inajumuisha aina tatu za akaunti za akiba ambazo ni  NMB Mtoto Akaunti, NMB  Chipukizi Akaunti na NMB Mwanachuo Akaunti zilizotengenezwa kwaajili ya vijana katika kila hatua ya maisha.

  Bussemarker amesema kuwa  upatikanaji wa huduma za kifedha na uelewa wa kuzitumia kwa vijana itaisaidia benki ya NMB  kutimiza azma ya kujenga utamaduni wa kuhifadhi fedha kwa matumizi ya baadae.

  Amesema kuwa si tu kwa kuwekeza na kuwa na jamii ya vijana yenye uelewa wa  masuala ya fedha tangu wakiwa wadogo bali inaleta tija kwa biashara pia. WAJIBU ni fursa kwa wafanyakazi changia kwa jamii huku wakiisaidia benki kufikia soko jipya la vijana wanaoweka akiba benki.

  Bussemarker  amesema kuwa  WWB kuandaa mpango kazi wa WAJIBU, NMB imefaidika kutokana na uzoefu wa miaka 
  zaidi ya 35 ya taasisi ya kimataifa ambayo imefanya tafiti za kina za kuelewa tabia na uwezo wa kifedha wa 
  wanawake na wasichana na maisha yanayosababisha tabia hizo. 

  Mkurugenzi wa Bidhaa wa WWB, Jennifer McDonald amesema amefarijika sana kushirikiana na NMB ushirikiano ambao umewaletea wananchi mpango wetu wa WAJIBU,kama tunavyojua kuwa na akaunti za akiba ni hatua moja tu,” alisema 

  “Ndiyo maana tunawapongeza NMB kwa kupanua zaidi WAJIBU kwa kuingiza vipengere vya mpango wa kuelimisha jamii kuhusu masuala ya kifedha itakayo wajengea uwezo vijana na kuwawezesha kuwa na maarifa
  na nguvu ya kutumia akaunti za akiba vizuri.

  0 0

  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Waseda kilichoko jijini tokyo, Japan kufuatia mwaliko wa Taasisi ya Association of African Economy and Development (AFRECO) ya Japan. Muhadhara huo ulihusu Uhusiano kati ya Japan na Afrika kuelekea kilele cha mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo Africa (TICAD) utakaofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika tarehe 27-28 Agosti jijini Nairobi.

  Akizungumza na wanafunzi, wanataaluma na mabalozi wa nchi za Afrika walioko Japan, Rais Mstaafu Kikwete ameelezea hali ya uhusiano mzuri ulioko baina ya Japan na Afrika. 

  Ameipongeza Japan kwa kuwa moja ya nchi chache ambazo hazikuondoa matumaini yake kwa bara la Afrika wakati ambapo Afrika ilipita katika kipindi kigumu cha kupoteza umuhimu wake machoni mwa mataifa makubwa, baada ya kwisha kwa vita baridi ya dunia mwanzoni mwa miaka ya 1990. Ni katika kipindi hicho, mnamo mwaka 1993 ambapo Japan ilianzisha mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika. Utaratibu huo umekuja kuigwa na mataifa mengine duniani.
  Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Wasuda University Kutoka kushoto ni Seneta Mstaafu Tetsuro Yano, Balozi Mathias Chikawe, Bi.Kyoko Hasegawa na Afisa Ubalozi Francis Mossongo.

  Akielezea hali ya maendeleo barani Afrika, Rais Mstaafu ameelezea kutiwa moyo na mafanikio ambayo bara la Afrika imeyapata katika kipindi cha miaka 15 ambako pato la taifa limekuwa mara dufu kutoka wastani wa asilimia 2 katika miaka ya 1980 hadi 1990 hadi kufikia asilimia 5 kati ya mwaka 2001 na 2014. 

  Hata hivyo amekumbusha kuwa, kutokana na bara la Afrika kuwa nyuma sana kwa kipindi kirefu, bado safari ya Afrika kujitegemea ni ndefu mno na hapana budi bara la Afrika kusaidiwa kufupisha urefu wa safari hiyo. Kwa hilo, ameipongeza Japan kwa kuongeza mara dufu misaada yake kwa bar ala Afrika kutoka kiasi cha dola za kimarekani milioni 900 mwaka 2007 hadi dola za kimarekani bilioni 1.8 mwaka 2011, huku Mitaji ya Uwekezaji ikiongezeka pia mara dufu kutoka dola za kimarekani bilioni 3.4 hadi dola za kimarekani bilioni 6.2 mwaka 2011 kama ilivyoahidiwa katika Mkutano wa IV wa TICAD.
  Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa muhadhara katika Chuo Kikuu cha Waseda jijini Tokyo mapema leo.

  Pamoja na kupongeza jitihada hizo, Rais Mstaafu Kikwete amehimiza juu ya umuhimu wa Japan kuwekeza zaidi barani Afrika hususan kushajihisha Sekta Binafsi ya Japan kufanya hivyo. Amesema, pamoja kuongezeka kwa uwekezaji wa Japan barani Afrika kutoka dola za kimarekani milioni 758 mwaka 2000 hadi dola za kimarekani bilioni 10 mwaka 2014, kiwango hicho kilichowekezwa katika bara la Afrika lenye nchi 54 bado ni kidogo ikilinganishwa na kiasi cha dola za kimarekani bilioni 20 ambacho Japan imewekeza katika nchi 6 tu za Singapore, Thailand, Malaysia, India, Philipines na Vietnam katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.

  Ameshauri Mkutano wa Sita wa TICAD utakaofanyika Nairobi pamoja na mambo mengine ujikite katika kuchochea uwekezaji wa Japan barani Afrika kwa kujengea uwezo nchi za kiafrika kufany abiashar ana Japan, kuona uwezekano wa kuanzisha Mfuko Maalum wa Kusaidia Uwekezaji wa Sekta Binafsi ya Japan barani Afrika, kurahisisha muingiliano wa kibiashara baina ya wafanyabiashara wa Japan na Afrika, na kuwekeza katika vijana wa pande zote mbili na kuwaunganisha ili kuendeleza mashirikiano yaliyokuwepo baina ya pande mbili.
  Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mirsho Kikwete akimsikiliza mwanafunzi katika kipindi cha maswali na majibu.

  Rais Mstaafu amemalizia kwa kusihukuru Serikali ya Japan na watu wake kwa kuunga mkono jitihada za Tanzania katika kujiletea maendeleo. Amewashukuru wajapani kwa kusaidia ujenzi wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa barabara ya juu ya TAZARA (FlyOver), ujenzi wa miradi ya umeme ya Kinyerezi II, Miundo mbinu ya kuunganisha Umeme ya kati ya Kenya na Tanzania na miradi mingine ya maendeleo. 

  Amewashukuru kwa misaada inayotolewa na Serikali ya Japan nchini Tanzania inayofikia Yeni bilioni 41.9.Amehitimisha kwa kusema kuwa hatma ya uhusiano baina ya Japan na Afrika iko mikononi mwa vijana wa pande zote mbili.

  0 0
 • 07/28/16--08:58: MZIGO LAZIMA UFIKE....
 • Kamera ya Globu ya Jamii imeinasa Taswira ya Mdau huyu mwendesha pikipiki akiwa amebeba shehena ya Mbao kwa mtindo wa aina yake, eneo la Vikindu Mkoani Pwani.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimweleza Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (kushoto) mikakati ya Serikali katika uboreshaji wa sekta ya nishati nchini.
  Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo (kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Lévêque (hawapo pichani)

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijiniDar es salam Julai 28, 2016.
  Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijini Dar es salaam Julai 28, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam baada ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijini Dar es slaam Julai 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kuondoa wafanyakazi wa mkataba kwa anjia ya kuwapa ajira ya kudumu kwa wenye sifa na kuwaondoa wasiokuwa na sifa ifikapo  Julai 30 mwaka huu. Amesema kitendo cha kutowaajiri na kuwatumikisha kwa mikataba kwa muda mrefu kinasababisha wakose stahiki zao jambo ambalo si halikubaliki.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Julai 28, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na kusisitiza kwamba ni lazima sula hilo lishughulikiwe haraka kwa sababu hayo ndio matundu watumishi hewa. “Mnawatumikisha watu kama vibarua kwa muda mrefu, hapa kuna wengine wanafanya kazi kwa mikataba kwa miaka mitano hadi sita hii haikubaliki kwani mnawakosesha stahili zao pale mnapowaachisha kazi,” amesema.

  Awali Kaimu Ofisa Utumishi wa Manispaa hiyo Zaitun Hassan alisema wamekuwa wakitoa ajira za mikataba kwa sababu wamekosa watu wenye sifa za kuweza kuajiriwa husan madereva. “Kwa mara ya mwisho umetangaza lini nafasi za ajira? Katika mkoa wa Dar es Salaam kweli wanaweza kukosekana madereva wenye sifa za kuajiriwa? Alihoji Waziri Mkuu.

  Zaitun alisema kuwa madereva wengi wanaojitokeza pindi wanapotangaza ajira wanashindwa kufikia vigezo ikiwemo kuwa na cheti cha VETA na badala yake wanakuwa na cheti cha kidato cha nne tu. Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa kuna wafanyakazi wengine katika Idara ya Uhasibu na Ujenzi ambao nao wameajiriwa kwa mkataba hivyo amemtaka Ofisa Utumishi kuomba kibali cha kuajiri kwa Katibu Mkuu Utumishi.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufanya tathmini ya maeneo yote ya shule kwenye mkoa wake na watakaobainika kuingia katika maeneo hayo waondolewe haraka. Amesema baada ya kukamilisha utengenezaji wa madawati kinachofuatia sasa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambapo amezitaka halmashauri kuweka mipango  ya kujenga majengo ya madarasa ya ghorofa ili waweze kuwa na madarasa mengi katika eneo dogo.

  Awali Waziri Mkuu alipokea msaada wa madawati 705 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Chamazi wilayani Temeke ambapo kati yake Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umetoa madawati 600 na Jumuia ya Mabohora imetoa madawati 105. Pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Agustino Mahiga alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 85 fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati.

  Dk. Mahija alisema watumishi hao walichanga sh. milioni 100 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ambapo sh. milioni 15 wamekabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe ambaye alikuwa mtumishi wa wizara hiyo ili naye akatengeneze madawati kwa shule za wilayani kwake.


  Kwa upande wake Balozi wa Kuwait nchini Jaseem Al Najem amesema Serikali ya Kuwait itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika shughuli zote za maendeleo hususan katika sekta za elimu na afya.

  0 0

  Mpiga picha Mkuu wa Gazeti la TanzaniaDaima, Mzee Joseph Senga amefariki Dunia huko nchini India alikokuwa akitibiwa usiku wa kuamkia leo. 

   inaelezwa kuwa alishapatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitalini hivyo akaenda hotelini kwa mapumjziko na kujiandaa kwa safari ya kutoka huko Tarehe 5/8/2016 na angefika Tanzania tarehe 6/8/2016.  Kwamba leo hii akiwa hotelini alizungumza na mke wake akamwarifu kuwa anaendelea vizuri na anatarajia kuanza safari ya  kurejea nyumbani nchini tarehe 5 na angefika tarehe 6 mwezi ujao.

   Baadaye aliomba apelekwe bafuni kwa sababu mkono wake mmoja ulikuwa haujiwezi kujikunja kwa sababu ya oparesheni aliyofanyiwa. Aliogeshwa kisha baadaye akaomba apewe chakula na matunda bila kuchanganywa pilipili na akapewa akala. 

  Alianza kujisikia vibaya baadaye kati ya saa 12 na saa 1 jioni jana, akaomba arudishwe hospitalini. Wakati anafuatwa dereva tax chini ya gorofa mbili alimokuwa akiishi Mwalimu Senga, walirudi wakamkuta hali yake imeanza kubadirika. 

  Walimuwahisha hospitalini, kwamba kadri wanavyozidi kupunguza umbali ili hospitali alipokuwa akitibiwa ndivyo hali yake ilivyokuwa ikizidi kubadilika. 

  Walipofika hospitalini, madaktari walimpima na kukuta Mwalimu Joseph Senga amefariki dunia. Mungu acha aitwe Mungu. Mwalimu Joseph Senga, tunakulilia, Mungu akupokee upumuzike kwa amani

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongozwa na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kukagua baadhi ya majengo wanayoishi wazee hao ili kuona namna ya kuyaboresha kadiri inavyowezekana wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi hayo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akitoa Zawadi ya Sabuni kwa viongozi wa wazee wa Makazi ya Kibirizi Katibu Makazi hayo Bi. Veronica Nyaga na Mwenyekiti Bw.Hamisi Sabuni. 


  0 0


  0 0

   Benki ya Advans ya Tanzania imebadili jina kuwa Letshego Bank (T) Limited kufuatia umiliki wa asilimia 75 za hisa za benki hiyo iliyonunuliwa na kampuni ya Letshego Holdings Limited baada ya kuwekeza zaidi ya Shilingi bilioni 19.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw. Yohane Kaduma alisema umiliki huu uliyofanyika tangu mwaka 2015, umefanya Letshego kuwa mbia mkuu wa benki hiyo huku asilimia 25 ikiendelewa kumilikiwa na wanahisa waanzilishi ambao ni Advans SA, na Shirika la Maendeleo ya Uholanzi (FMO) ambao kwa mujibu wa Bw. Kaduma, watendelea kutoa ushirikiano kiuongozi na kiutawala.


  Bw. Kaduma aliongeza kuwa pamoja na kuzindua muonekano mpya wa benki hiyo, Letshego ya Tanzania pia imezindua safari ya mabadiliko itakayoiwezesha kuwa kinara katika kuvumbua na kutoa huduma za kifedha ambazo ni shirikishi kwa wanajamii wote (financial inclusion).Alisema uboreshwaji wa huduma zitakazotolewa na benki hiyo inalenga kusaidia katika kutatua matatizo muhimu ya wateja wao ambayo ni pamoja na kuweka amana, kukopa, kufanya malipo na hata huduma za bima.

  “Mwonekano huu mpya wa Letshego Bank ni badiliko ambalo linafanyika katika nchi zote 10 barani Afrika ambapo tupo, na unazindua upya safari ya mabadiliko inayochukuliwa na Letshego. Kwa Tanzania, mabadiloko tuliyoyafanya kama benki, yanaendana pia na dira ya Serikali ya kuleta mendeleo ya kiuchumi na huduma za jamii kwa wananchi wake,” alisema Bw. Kaduma.


  Aliongeza kuwa benki ya Letshego inashauku ya kujenga utamaduni chanya wa kukopa na ujumuishwaji wa kifedha kwa watanzania.“Tunafanya kazi ili kusaidia kuhakikisha kwamba huduma zetu za kifedha zinaleta maana na mabadiliko kwa Watanzania. Wateja wetu ndiyo wamewezesha jina na huduma zetu kukua kufikia hatua tuliyo nayo leo. Tunawashukuru na tunawahakikishia kwamba tunafurahia kuendelea kutoa ufumbuzi wa kifedha utakao boresha maisha yao,” aliongeza Bw. Kaduma.

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kuboresha huduma zeo ndani ya mwonekano huu mpya, pia benki hiyo itaendelea kufanikisha lengo lao la kutoa huduma jumuishi za kifedha ambazo zitaleta uboreshaji wa maisha ya wadau weo wote.


  “Letshego Bank inaanzisha ufumbuzi wenye lengo la upatikanaji wa mikopo ya kilimo, elimu, afya na nyumba kwa watu wenye kipato cha chini, cha kati na wajasiriamali wadogo. Wateja na wadau wetu wote, wataendelea kupata huduma za kuweka akiba na kufanya malipo. Katika hili, na ili kuhakikisha kwamba huduma zetu zinapatikana maeneo mengi ya Tanzania, Letshego Bank ina mpango wa kutoa huduma za kibenki kupitia vituo zaidi ya 100, kwa kuitumia Faidika kama wakala wake. Tunaamini kwa ushirikiano wa vyombo husika, hili litawezekana, na Watanzania wengi zaidi watafurahia huduma zetu,” alisema Bw. Kaduma.


  Bw. Kaduma alifafanua kuwa hapa Tanzania, Letshego imekuwako kwa miaka 10 sasa kupitia kampuni inayojulikana kwa jina la kibiashara la Faidika.Aliongeza kuwa Advans Bank (ambayo sasa ni Letshego Bank) imekuwako Tanzania kuanzia mwaka 2011. “Katika miaka hii sita ya utoaji wa huduma za kifedha ambapo tumekuwako katika mikoa ya Dar es Salaam (matawi 3), Mwanza na Mbeya, tumetoa ufumbuzi wa masuala ya kifedha ambayo ni rahisi, stahiki, na nafuu kwa zaidi ya watanzania 26,000 nchi nzima,. Huduma hii ikitolewa na wafanyakazi zaidi ya 200 kwenye matawi haya,” alifafanua Bw. Kaduma.

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa Letshego ni neno la ki-Setswana linalomaanisha ‘support’ – au Harambee kwa Kiswahili, neno hili huashiria uwezo wa taasisi  kuweza kushirikiana na serikali na watumishi wa serikali, pamoja na wajasiriamali wadogo na wa kati (MSEs)  ili kuweza kutoa huduma  rahisi, nafuu na mahsusi zitakazoweza kuboresha hali ya jamii.  “Muonekano wetu mpya ni wa kisasa zaidi na ukiendana na dhana nzima ya ‘Harambee’, inaonyesha msingi imara, na kwamba sote tunaweza kukua pamoja,” alisema Bw. Kaduma.

  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Letshego ya Tanzania Bw. Yohane Kaduma (wa pili kulia) akionyesha nembo na muonekano mpya ya benki hiyo iliyobadilishwa kutoka kutambulika kama Advans Bank kuwa rasmi Letshego Bank. Wanaoshuhudia ni Dru Jayaratne (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa FAIDIKA Bw. Mbuso Dlamini (wa pili kushoto) na Meneja Rasilimali watu wa benki ya Letshego Bi. Rehema Ngusar.
  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Letshego ya Tanzania Bw. Yohane Kaduma akiomwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa FAIDIKA Bw. Mbuso nembo na muonekano mpya ya benki hiyo iliyobadilishwa kutoka kutambulika kama Advans Bank kuwa rasmi Letshego Bank.

  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Letshego ya Tanzania Bw. Yohane Kaduma (wa pili kulia) akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa FAIDIKA Bw. Mbuso Dlamini (wa pili kushoto) mara baada ya kuzindua nembo na muonekano mpya ya benki hiyo iliyobadilishwa kutoka kutambulika kama Advans Bank kuwa rasmi Letshego Bank. Wanaoshuhudia ni Dru Jayaratne (wa kwanza kulia), na Meneja Rasilimali watu wa benki ya Letshego Bi. Rehema Ngusar. 


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Benki ya NMB kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Women's World Banking leo wamezindua mpango wa kuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae. Mpango huo umepewa jina la WAJIBU mahususi kwaajili ya akaunti za akiba za watoto na vijana.

  WAJIBU yenye maana ‘Wajibika’ inajumuisha aina tatu za akaunti za akiba: NMB Mtoto Akaunti, NMB Chipukizi Akaunti na NMB Mwanachuo Akaunti zilizotengenezwa kwaajili ya vijana katika kila hatua ya maisha yao huku lengo likiwa kuwasaidia wazazi na vijana kujiwekea akiba na kupanga matumizi wao wenyewe au kwa msaada wa wazazi ili kutimiza azma yao.
  NMB Chipukizi Akaunti ni akaunti ya kipekee na maalumu kama akaunti ya kwanza ya aina yake kutambulishwa nchini, akaunti hii ni maalumu kwa vijana wenye umri kati ya miaka 13 mpaka miaka 17 na wanamiliki akaunti hiyo kwa majina yao. Akaunti hizi zinaunganishwa na msemo kuwa JIfunze, Jipange – WAJIBIKA! Mpango huo mahususi kwajili ya kuwawezesha watoto na wazazi kujua masuala ya kifedha na jinsi ya kutumia taasisi za kifedha kujiwekea akiba kwa maendeleo.

  Akiongea kwenye uzinduzi wa WAJIBU, Mkurengezi Msaidizi wa Udhibiti na Ubora wa Shule Dk. Edicome Cornel Shirima kutokea Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia – alisema “Walaji wenye uwezo, wanaojiamini na walioshirikishwa wanaofanya maamuzi sahihi ya kifedha si tu wataboresha maisha yao bali jamii kwa ujumla. Ninafarijika sana leo kuzindua mpango huu wa WAJIBU kwani nina Imani kuwa utasaidia kuwapatia watoto na wazazi stadi muhimu zitakazowawezesha kupanga maisha yao ya baadae.”

  Hii ndiyo maana serikali imedhamiria kwa dhati kabisa kuboresha na kuendeleza elimu ya fedha katika ngazi zote za watanzania – Hususani wanajamii yote ya Tanzania, aliongeza Dk. Shirima
  Jifunze, Jipange - WAJIBIKA! Inajumuisha vipindi vitatu kwa ajili ya shule za sekondari na msingi – Kipindi cha kwanza kitazingatia mafunzo ya elimu ya masuala ya fedha na taasisi za kifedha itakayowaunganisha wanafunzi na wazazi wao, na kufuatiwa na vipindi viwili maalumu kwa watoto wenyewe. Katika mafunzo hayo, washiriki watajifunza umuhimu wa kuweka akiba benki, jinsi akaunti ya benki inavyoweza wasaidia kupanga matumizi ya fedha zao, kutengeneza malengo ya kuweka akiba na kuweka mkakati wa kuweka akiba, kufungua akaunti ya WAJIBU na kuanza kuitumia.

  “Tumefarijika sana kushirikiana na mashule ili kukamilisha mpango huu, utayari wao katika kusaidia wanafunzi kupata elimu hii itasaidia sana kuwajengea wanafunzi maisha mazuri ya baadae” alisema Bi Ineke, mkurugenzi mtendaji wa NMB Benki.

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua baadhi ya miundombinu iliyopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za wafanyakazi zilizopo Bunju B jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga imeziasa Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi kushirikiana na katika kutatua changamoto zinazokabili makazi ya wazee na watu wenye ulemavu nchini. 

  Akiongea wakati alipotembelea Makazi ya kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga Bi. Sihaba amesema kuwa ametembelea baadhi ya makazi hayo na kuona yanahitaji msaada mkubwa hasa ujenzi wa nyumba za malazi, umeme na madawa hivyo Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi hawana budi kushirikiana na serikali kamaliza kabisa changamoto hizo.

  “nimetembelea makazi kadhaa sasa, changamoto ni nyingi, wazee hawa wanahitaji msaada mkubwa sana hivyo kwa nafasi hii natoa wito kwa Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi kushirikiana na serikali katika kuziondoa changamoto hizi katika makazi haya ili kuweza kuwafanya wazee hawa kufurahia maisha katika makazi haya”.Amesema Bi. Sihaba.

  Naye Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe amewaomba wahisani na serikali kwa ujumla kusaidia katika ukarabati na ujenzi wa majengo katika makazi hayo ili kupunguza changamoto ikiwemo uvamizi wa vijana wanaotumia vilevi na bangi kuingia katika nyumba hizo na kutishia kuwafanyia vitendo vibaya wazee wenye jinsia ya kike.

  Akizungumza kwa niaba ya Wazee katika Makazi ya Kolandoto Mkoani Shinyanga Mzee Samora Maganga amesema kuwa kituo hicho kwa kiasi fulani kipo katika hali nzuri ila wanaiomba serikali iwasaidie katika kutatua changamoto ya umeme na majengo kwani imekuwa kero ya muda mrefu sasa.

  Aidha Bi. Sihaba akiongea na Wazee katika Makazi ya Amani Mkoani Tabora aliwapongeza walezi wa makazi hayo kwa kuamua kutoa kadi za matibabu za CHF kwa wazee hao na kushauri Walezi wa Makazi mengine ya Wazee nchini kuiga mfano huo ili kusaidia katika utoaji bora wa huduma za afya kwa wazee.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Wazee wanaoishi katika Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga na kuwahakikishia serikali kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha kuishi katika mazingira rafiki. Katikati ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara hiyo Bi. Amina… na kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe.
  Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga sehemu ya nyumba zinazohitaji ujenzi kwa ajili ya Makazi ya Wazee hao. Wakati wa Ziara ya Kutembelea Makazi ya Wazee na kuona hali halisi ya makazi hao.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Wazee katika Makazi ya Kulea Wazee ya Amani leo Mkoani Tabora.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akipokea msaada wa bando za bati kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank, Bwana Frank Nyabundege (wa pili kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Mkoa Mpya wa Songwe.Wa kwanza Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mbozi, Erik Ambakisye akifuatiwa na Mbunge jimbo la Vwawa Josephat Hasunga

  Benki ya TIB Corporate leo imetoa msaada wa mabati mia moja kwa mkoa wa Songwe ili kusaidia kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na vyoo mkoani humo.

  Mkoa wa Songwe, ambao ni miongoni mwa mikoa mipya, itatumia mabati hayo katika shughulli za ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wilaya za Mbozi, Mamba, Ileje, Songwe na Tunduma.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya TIB Corporate, Bwana Frank Nyabundege alisema msaada huo umelenga kuonyesha nia na jitihada za benki yake katika kusaidia kukuza elimu na pia kuunga mkono serikali katika jitihada zake za kuboresha elimu nchini.

  'Serikali pekee yake haiwezi kukuza sekta ya elimu hivyo basi ni muhimu tuisaidie serikali katika kuboresha sekta ya elimu kwa kuaanda mazingira mazuri kwa vijana wetu kujisomea’ alisema Nyabundege.

  Akitoa shukrani zake kwa benki ya TIB Corporate, Mkuu wa mkoa wa Songwe Mheshimiwa Chiku Gallawa alisema mchango huo ni muhimu katika kukuza na kuboresha sekta ya elimu ambayo ndio kichocheo cha ukuaji wa sekta ya uchumi na kijamii kwa taifa la kesho.

  ‘Tunaishukuru benki ya TIB Corporate kwa jitihada zake za kushirikiana na serikali katika kukuza sekta ya elimu kwani hakuna taifa linaloweza kuendelea bila kuwa na raia wasomi ' alisema Mheshimiwa Gallawa. 

  0 0


  0 0

  Kampuni ya simu za mikononi Airel Tanzania leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu zikaoshiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ngazi ya mkoa ambayo inatarajiwa kuanza Julai 30 mpaka Agosti 30 2016 kwenye mikoa tofauti hapa nchini.

  Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 200 vimekabidhiwa kwa Wasimamizi wa vituo vyote vya mikoa na Taifa. Vifaa hivyo hivyo ni pamoja na jezi za wachezaji, shin guards, soksi, jezi za marefa, mipira pamoja na glovu.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Katimu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Celestine Mwesingwa alisema ‘ Kwa kutoa vifaa hivi vya michezo,mdhamini ametimiza moja kati ya majukumu yake na ni matarajio yangu kwamba mtarudi kwenye vituo vyenu na kuongeza bidii ya kutafuta vipaji vinavyoibuka vya mpira wa miguu’.

  ‘Tunatarajia kuona mechi zenye ushindani na za kuvutia na natoa wito kwa viongozi wa vyama vya mikoa kuwa makini wakati wa kuchangua timu kombaini ambazo zitakuja kucheza kwenye fainali za taifa ambazo zitafanyika Dar es Salaam tarehe 6 mpaka 11 Septemba mwaka huu.

  Kwa upande wake Meneja Mahusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema ‘Airtel Rising Stars inaungana pamoja na promosheni yetu ya Airtel Fursa ambayo ilizinduliwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao. Kwa mwaka, michuano hii inatoa fursa nyingine kwa wavulana pamoja na wasichana kutambua uwezo wao wa kucheza soka na kuweza kufanikisha ndoto zao. Kwa mantiki hiyo, Airtel Tanzania inatumia program hii kuwezesha vijana wenye vipaji vya mpira wa miguu kuvionyesha kwa makocha na hatimaye kufakinisha ndoto zao’.

  Airtel Rising Stars ni mpango kabambambe kwa Afrika nzima yenye lengo ya kutoa nafasi kwa vijana kuonyesha vipaji vyao mbele ya makocha, na hatimaye kupata fursa ya kuviendeleza na kuvikuza.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.
  Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu wa chama cha soka cha Ilala Daud Kanuti tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.
  Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu wa chama cha soka cha Kinondoni Isack Mazwile tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamechangia kiasi cha Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari nchini.

  Akikabidhi mchango huo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya watumishi wa wizara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi  Augustine Mahiga amesema kuwa watumishi hao wametoa fedha hizo kwa shule ya msingi Chamazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.

  Balozi Mahiga amesema Wizara yake iliwahamasisha watumishi wake walio makao makuu na wale walio kwenye balozi mbalimbali nje ya nchi kuchangia zoezi hilo la upatikanaji wa madawati.

  “Ili kufanisha upatikanaji wa fedha hizi Wizara yangu iliwahamasisha watumishi wake wote walio Makao makuu na wale walio katika balozi zetu duniani kote,  wito huu uliitikiwa kwa ari na hamasa kubwa na kufanikisha kukusanya kiasi cha Shilingi 100,176,825.52 za kitanzania”alisisitiza Balozi Mahiga

  Waziri Mahiga aliongeza kuwa mara baada ya kukusanya fedha hizo watumishi wa Wizara hiyo waliamua kumpatia aliyekuwa Mtumishi wa Wizara ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kiasi cha shilingi Milioni 15 kwa ajili ya ununuzi wa madawati katika Wilaya yake.

  Aidha, amesema kiasi fedha zilizobaki zaidi ya shilingi milioni 85 zilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa  kwa ajili ya mchango wa utengenezaji wa madawati ya shule ya Msingi Chamazi iliyoko Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mahiga aliongeza kuwa mbali na wizara yake kuwa na majukumu mbalimbali bado inalo jukumu la kuhakikisha inaitangaza Tanzania ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimkabidhi hundi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya makabidhiano madawati ikiwa ni fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais Mhe. John Magufuli mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam . Picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  0 0

  Wananchi wa Mbeya- Mbalizi, Shinyanga- Stand Mpya,  Mwanza, Tanganyika Bus Stand, Moshi- Bus Stand na Soko Kibolon na Dar Es Salaam- Mbagala Kuu.
  Wananchi wa mikoa ya  Mbeya, Mwanza, Moshi Watu wakijiandikisha kushinda moja ya magari yatakayotolewa kwa mshindi wa shindano la Whitedent.
   Baadhi ya Wananchi wa kijaza fomu kwaajili ya kushindania shindano linalochezeshwa na kampuni inayozalisha bidhaa za Meno ya Whitedent nchi nzima.
   Wakazi Mkoani Shinyanga wakishuhudia moja ya magari yatakayotolewa kwa mshindi la shindano la Whitedent. Katika msafara wa magari hayo unaozunguka nchi nzima, kama sehemu ya kusherehekea miaka 25 ya bidhaa hiyo katika utoaji huduma nchini.

older | 1 | .... | 1300 | 1301 | (Page 1302) | 1303 | 1304 | .... | 3283 | newer