Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

Baada ya kushida jimbo la Sumbawanga, CCM yaibuka tena kidedea jimbo la Igunga

$
0
0

Mahakama ya Rufaa imemrudishia Ubunge wa jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM Dkt Dalaly Peter Kafumu (pichani kushoto), baada ya kushinda rufaa aliyokata baada ya Mahakama Kuu kanda ya Tabora kumvua Ubunge kufuatia  madai ya kukiuka utaratibu wa uchaguzi wakati wa Kampeni katika Kesi iliyofunguliwa na Bw. Joseph Kashindye aliyekuwa Mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA.


Dkt Kafumu anakuwa mbunge wa pili wa CCM kurejeshwa mjengoni wiki, hii baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania, imethibitisha Mhe Aeshi Hilaly (pichani chini) kuwa mbunge halali wa Sumbawanga Mjini baada ya kushinda rufaa aliyokata kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, iliyomvua ubunge.

Hilaly alivuliwa ubunge na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila Aprili 30, 2012, kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kupitia CHADEMA,  Bw. Nobert Yamsebo. 

 Mhe Hilaly na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) walikata rufani kupinga hukumu hiyo na zote zilisikilizwa kwa pamoja na jopo la Majaji watatu, Edward Rutakangwa, Profesa Ibrahim Juma na Steven Bwana.

Wakurugenzi wa Mashtaka wa Afrika Mashariki wakutana jijini Dar es Salaam leo

$
0
0
Na Genofeva Matemu _MAELEZO

Shirikisho la Wakurugenzi wa Taasisi zinazoendesha Mashtaka wa Nchi za Afrika Mashariki wamekutana nchini Tanzania kwa ajili kupitia upya Katiba yao ili kuimarisha umoja wao. 
 Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Shirikisho hilo Dk. Eliezer Mbuki Feleshi wakati wa mkutano na waandishi wa habari. 
Dkt Feleshi, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano,  alisema kuwa wakati wa mkutano wao watazungumzia mikakati ya kimaendeleo ya shirikisho lao pamoja na kupitia katiba ya shirikisho ili kuweza kuifanya iwe na uzito katika utekelezaji wa majukumu yao na ya Shirikisho hilo. 
 Mambo mengine yaliyokusudiwa kuzungumziwa katika mkutano huo ni pamoja na masuala ya uanachama, nafasi ya shirikisho kwenye mashirikisho mengine na namna ya kuongeza rasilimali watu kwenye shirikisho hilo. 
 Dkt. Feleshi alisema kuwa shirikisho hilo liliundwa mwaka 2009 ambapo mwaka 2010 lilianza kutekeleza majukumu yake ili kuleta amani, umoja na utulivu Afrika Mashariki. “Malengo yetu ya kuungani ni pamoja na kuweza kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha kuna umoja amani na utulivu ndani na nje ya nchi zetu,” amesema DK. Feleshi. 
 Aliongeza kuwa hadi hivi sasa Shirikisho limeweza kufanya kazi kwenye vuguvugu la watu waliorusha bomu Uganda, masuala ya uharamia Kenya, pamoja na kuwasaidia madereva kutoka Tanzania waliopata waliokuwa wamekamatwa nchini Burundi ambapo baada ya mawasiliano madereva hao waliweza kuachiwa. 
 Kuhusu changamoto Dk. Feleshi alisema kuwa changamoto zipo nyingi ikiwemo kuchelewa kupata taarifa, kuchukua muda mrefu kushughulikia kesi, na kupata kesi nyingi kwa wakati mmoja inayopelekea kushindwa kuzimaliza wakati muafaka. Shirikisho hilo limehudhuriwa na Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Eliezer Mbuki Feleshi ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa shirikisho hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Jamhuri ya Kenya Mhe. Keriako Tobiko na Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Uganda Mhe. Richard Buteera. 
 Wengine ni Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Jamhuri ya Rwanda Mhe. Martin Ngoga, pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Jamhuri ya Burundi Mhe. Valentine Bagorikunda
Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakurugenzi wa Mashataka wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashitaka wa Tanzania Dkt. Eliezer  Feleshi (kushoto) akiongea na wanahabari akiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka wa  Kenya , Mhe Keriako Tobiko leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa  Mkutano wa Wakurugenzi wa Mashtaka wa  Afrika Mashariki  Dkt, Eliezer  Feleshi (kulia) akiwa pamoja na wajumbe wenzake wa mkutano huo leo katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Chini wakiwa katika picha ya pamoja.

Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

Dkt Shein azungumza na wanafunzi wa skuli ya Fidel Castro, Pemba

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya Fidel Kastro Pemba leo jioni, Rais alichukua hatua hiyo kusikiliza changamoto mbali mbali zinazoikabili skuli pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Skulini hapo,Picha na Ramadhan Othman,Ikulu, Zanzibar

ujenzi wa vituo vya mabasi yaendayo haraka umeanza

$
0
0
 Vitavyokuwa vituo vya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam vimeanza kumea katika barabara ya Morogoro road. Juu ni Mwembechai na chini ni Magomeni Usalama. Kasi ya ujenzi wa barabara hiyo imeendelea katika muda wote huu toka ianze mwishoni mwa mwaka jana

Annual meeting of the Workers' Council of the Ministry of Foreign Affairs meeting in Dar es salaam today

$
0
0

Ms. Naomi Zegezege, Secretary of the Workers' Council of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation gives her opening remarks before welcoming the Chairman of the Workers' Council, Mr. John Haule, Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs.  The Meeting was held today at Karimjee Hall in Dar es Salaam.

Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP) (2nd left), Deputy Minister for Foreign Affairs and International Co-operation listens to Ms. Zegezege, Secretary of the Workers' Council of the Ministry of Foreign Affairs.   Others in the photo are Mr. John M. Haule (left), Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs, who is also a Chairman of the Workers' Council, Ambassador Rajabu Gamaha (2nd right), Deputy Permanent Secretary and Mr. Ali Kiwenge, General Secretary of the Tanzania Union of Government and Health Employees (TUGHE). 


Mr. John Haule, Permanent Secretary and Chairman of the Worker's Council gives few remarks before welcoming Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP), Deputy Minister of Foreign Affairs who was a Guest of Honor during the Meeting held today at Karimjee Hall in Dar es Salaam. 

The Guest of Honor, Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP) (center) and other dignitaries in the high table took a moment of respect to commemorate the two employees of the Ministry of Foreign Affairs  who passed away earlier this year.   

The Guest of Honor, Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP) (2nd left), Deputy Minister for Foreign Affairs and International Co-operation gives his opening remarks during the Workers' Council Annual Meeting of the Ministry of Foreign Affairs held today at Karimjee Hall in Dar es Salaam. 

Ms. Ngusekela Nyerere and Mr. Hangi Mgaka, Members of Secretariat taking notes during the Meeting. 


Directors in the Ministry of Foreign Affairs also were present during the Workers' Council Meeting.  Right is Mr. Mndeme Dush-hood, Director of Administration, Human Resources and Management in the Ministry, Ambassador Mbelwa Kairuki (2nd right),Director of the Department of Asia and Australasia, Ambassador Bertha Semu-Somi (2nd left) and Director of Diaspora.   Others are Ambassador Dora Msechu (left), Director of the Department Europe and Americas and Ambassador Irene Kasyanju (behind right), Director of the Legal Affairs Unit in the Ministry of Foreign Affairs and Internatioal Co-operation. 

A group photo of the Deputy Minister Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP) (7th left) together with the Members of the Workers' Council of the Ministry of Foreign Affairs during their annual meeting held  today at the Karimjee Hall in Dar es Salaam. 

Umoja wa Mataifa kupitia mpango wa UBRAF waendesha semina kwa watangazaji wa radio za kijamii za Afrika Mashariki.

$
0
0
Picha juu na chini ni Mshauri wa Radio Jamii na Mkufunzi wa UNESCO Dar es Salaam Bi. Rose Mwalimu akiendesha majadiliano kuhusu mikakati endelevu itakayowezesha kuihusisha jamii katika program zinazohusu kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wakati wa warsha iliyofadhiliwa na mpango wa Unified Budget Result Accountability Frame Work (UBRAF) uliochini ya Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa Kongamano lililofadhiliwa na UBRAF lililohusisha Redio za Kijamii za Afrika Mashariki kutoka Kenya Community Media network (KCOMNET) Njuki Githethwa akiwasilisha ripoti ya maendeleo na ufanisi wa mtandao huo ambao unalenga kujenga fursa ya kitaifa ya kuratibu, kulinda na kusaidia sekta ya vyombo vya habari vya kijamii nchini Kenya wakati wa warsha ya siku mbili iliyoratibiwa na mpango wa UBRAF uliochini ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika hivi karibuni Terrat Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Picha juu na chini ni Afisa Habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Dar es Salaam Bi. Stella Vuzo akizungumzia umuhimu wa kuwa na mikakati madhubuti ya kushirikishana baina ya Waandishi wa habari na Umoja wa mataifa na pia akafafanua mpango mkakati wa Umoja wa mataifa juu ya usalama wa waandishi wa habari pindi wawapo kazini.
Ambapo amewataka ku-share vipindi na habari mbalimbali na Radio ya Umoja wa Mataifa na kuwafanya wao pia kujulikana kimaifa zaidi.
Bw. Jimmy Okello wa COMNETU akitoa tathmini ya ripoti endelevu za Radio za Kijamii nchini Uganda.
Mwakilishi kutoka Mang’elete Community Radio ya nchini Kenya akizungumzia muelekeo na muafaka wa radio za kijamii na kiwango cha mafanikio kilichofikiwa hadi sasa.
Amos Ochieng wa KCOMNET kutoka Kenya akielezea jinsi watangazaji wa Radio za Kijamii za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanavyoweza Ku-share habari kupitia mtandao wa kijamii wa pamoja kwa wakati mmoja.
Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka tasnia ya habari waliohudhuria semina iliyohusisha Redio za Kijamii iliyofanyika Terrat wilayani Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa kupitia Mpango wa UBRAF.
Pichani juu na chini washiriki wa warsha hiyo iliyowakutanisha Watangazaji wa Radio za Kijamii kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania wakitoa maoni yao ya namna ya kuboresha uandaaji wa vipindi vyao vya Radio za Kijamii sambamba na vikwazo wanavyokumbana navyo katika kazi zao.

Karibu Nyote Kwenye Tutaonana Party live in Oslo Norway

$
0
0

Kama kawaida yetu tukiwa na wageni toka East Africa kama Super Stars.
Basi uwa tunapenda kuwanae saani moja kama hifuatavyo Bongo Flavaz..
Chege Chigunda ni Mgeni wetu hapa nchini Norway pia Europ Tours.
Sasa pia anapenda kushirikiana na mwenzake toka Bongo Kigoma ni
Ommy Dipoz kwa Pozi wanafanya show kambambe hapa Nchini Norway 
Ikifanyika ndani ya Ukumbi wa 
Lakkegata skole 79b Slurpen @ 10-May-2013.
 
 
Cc.200 on door & 150 Nok, booking on www.Djpred.com 
Or call:- +47 96872483- Facebook/ Mpily Oslo Norway
                      Togather tunawakilisha....

msaada tutani: Nianzie wapi kupata mwenza wa Kitanzania?

$
0
0
Dear Ankal,
Kwanza nikupe Big UP!!! sana kwa kuendesha blog yetu kwa weledi wa hali ya juu. Yaani ma-news kila dakika na up-to-date kama CNN mwanangu. Hakika unatisha na hakuna wa kukufikia kaka. Halafu unanikoshaga kwa kutoweka mambo ya udaku, umbea na majungu...

La pili ni kukupongeza kutoa nafasi kwa wadau kutoa madukuduku yao bila chenga. Yaani yule jamaa wa juzi wa Norway anayepima zali la kuja kuomba visa ya Marekani baada ya kuopoa Green Card ni funika bovu. Ndio maana na mimi leo najikunja kuomba ushauri toka kwa wadau wako lukuki duniani kote, japo shida yangu ni tofuti na ya mdau wa visa wa Norway ambaye nami namshauri asinoe stepu na kuhamia Marekani. Mie niko huku mwaka wa 28 leo, na Green Card yangu, lakini acha! Kufa sifi ila cha moto nakiona. Nna kila kitu ila sina mwenza wa kufurahi nae...

Mie Ankal naishi East Coast huku (kwa sasa jina la mji kapuni, wambea naogopa wasinichore). Tatizo langu natafuta mwenza kutoka nyumbani Tanzania, tatizo sijafika huko miaka yote hiyo na pa kuanzia sijui (wazazi wangu wote wametangulia mbele ya haki). Ndugu zangu wengi nimepoteza mawasiliano nao (waliniliza pesa nilizowatumiaga za kujengea, wamezila na wakakata mawasiliano) hivyo sina uhakika kama wote wapo. Nilikuwa naishi Kariakoo, Dar, mtaa wa Narung'ombe, ila katika taswira moja ulioonesha siku za hivi karibuni nimeona nyumbani petu pana bonge la kikwangua anga. Najua tu kuwa jamaa zangu ndio wameshauza nyumba yetu na kulala mbele.

Samahani kama nawakwaza kwa hadisi ndefu ila shida yangu ndiyo hiyo. Nataka kurejea nyumbani mara moja kuja kusaka wa kuishi naye. Mie sasa nagota miaka 51 ila bado niko fiti kila idara, ikiwa ni pamoja na pesa ya kubadili mboga kila siku hainipigi chenga. Maana boxi ninalokula huku si haba. Niliwahi kuishi na mfilipino na baadaye Mvenezuela lakini tukazinguana sasa niko alone. Mfilipino nilizaa naye watoto wa kiume wawili, kakimbia nao kwenda wapi sijui. Huyu mwingine hatukubahatika.

Sasa basi, shida yangu ni wapi pa kuanzia pindi nikija huko???  Halafu huyo mchumba, ambaye sina tatizo la dini wala elimu yake (awe na angalau ya fom foo tu, tosha!), nitampataje wakati nikija nitakuwa mgeni na muda wangu ni wiki tatu tu???

 Naomba mchango wa mawazo toka kwa wadau nifanyeje nipate mwenza wa Kitanzania toka nyumbani Tanzania?? Nikija nianzie wapi?? Kuna agency za kutatua matatizo kama hayo huko???

Mdau
East Coast, USA



Article 0

$
0
0
 David Moyes has signed a six-year contract to succeed Sir Alex Ferguson in charge of champions Manchester United next season. The 50-year-old Scot leaves Everton after 11 years at the Goodison Park helm when his contract expires. Moyes expressed his desire to leave for Old Trafford in a meeting with Everton chairman Bill Kenwright last night and replaces retiring great Ferguson, who joins United's Board of Directors this summer following 27 trophy-laden years as the the club's manager. Moyes will stay on at Everton until the end of the month, leading the Toffees in their remaining two games of the campaign against West Ham and Chelsea. SOURCE: Daily Mail

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA SEMINA YA SOKO LA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI 'DOADOA' JINJA UGANDA

$
0
0
 Mwanmuziki kutoka Kenya, Winyo akitumbuiza katika moja ya matamasha yanayoambatana na semina ya kujadili changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki.
 Wanamuziki wakiimba wimbo wa ushirikiano katika moja ya matamasha yanayoambatana na semina ya kujadili changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki, kutoka kushoto ni Mani Martin kutoka Rwanda, Shamsila kutoka Arusha Tanzania na Staffi kutoka Uingereza.

 Washiriki katika semina ya kujadili changamoto za soko la muziki Afrika Mashariki wakifuatilia moja ya mada kwenye hotel ya Crasted Crane mjini Jinja, Uganda

Kwa picha za matukio zaidi tembelea DOADOA 2013

Airtel yazindua huduma maalumu kwa wateja wake ijulikanayo kama Airtel Premium

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Sunil Colaso akimzawadia bi Rose Maina mmoja wa wateja katika uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam akifuatiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja bi Adriana Lyamba.
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Adriana Lyamba akimzawadia bw. Joseph Mambo .mmoja wa wateja katika uzinduzi wa huduma mpya ya wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam, akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso.
Mteja wa Airtel bw. Picket Robert Miranda (kushoto) akiongea na mkurugenzi wa huduma kwa wateja Adriana Lyamba (kulia) na Meneja wa huduma kwa wateja Hilda Nakajumo (katikati) katika uzinduzi wa huduma mpya ya wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Sunil Colaso (kushoto) na wafanyakazi wengine wa Airtel, Adriana Lyamba (Kulia) akifuatiwa na Meneja wa huduma kwa wateja Hilda Nakajumo wakiongea na mmoja wa wateja wa Airtel David Mukama(wa pili kushoto) katika uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Adriana Lyamba akimzawadia bw. Abdual Salum mmoja wa wateja katika uzinduzi wa huduma mpya ya wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam, akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso.

UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

$
0
0
Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012. 

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012. Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya.

Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji wa mitihani hiyo. Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973 wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika mwaka uliotangulia.

Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

Selestine Gesimba
KAIMU KATIBU MKUU

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
10/05/2013

DKT. SHEIN NA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA WILAYA YA CHAKECHAKE PEMBA

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM Tawi la Ndagoni katika wilaya ya Chakechake leo akihitimisha ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba,ambapo atakamilisha mikoa sita ya Zanzibar,kwa uimarishaji wa Chama cha Mapinduzi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi Kadi ya CCM mwanachama mpya Mwanahawa Mohamed Ussi, Jumuiya ya UWT,baada ya kuweka jiwe la msingi Tawi la CCM Mgogoni Wilaya ya Chake chake Pemba katika ziara ya kuimarisha Chama leo akihitishan ziara kwa Mikoa sita ya Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi Kadi ya CCM mwanachama mpya Said Robed Solela,kutoka CUF Maziwani,baada ya kuweka jiwe la msingi Tawi la CCM Mgogoni Wilaya ya Chake chake Pemba katika ziara ya kuimarisha Chama leo akihitishan ziara kwa Mikoa sita ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa Afrika Mashariki wakutana na Waandishi wa Habari jijini Dar

$
0
0
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa Afrika Mashariki Dr. Eliezer Feleshi akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano wa waandishi wa habari hawapo pichani Mei 10, jijini Dar es Salaam wakati walipokutana kwaajili ya kutoa maazimio ya mkutano wa siku 2, uliowakutanisha Wakurugenzi wa mashtaka wa Afrika Mashariki. Nchi zinazojumuisha shirikisho hilo ni kutokaTanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
.Rais wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa nchi za Afrika Mashariki Martin Ngoga (kushoto) akitoa taarifa ya maazimio ya mkutano wao wa siku 2 kwa waandishi wahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salam.pichani kutoka (kulia) Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Uganda , Richard Buteera, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka Afrika Mashariki Dkt. Eliezer Feleshi , akifuatiwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Burundi , Valentine Bugorikunda.
Mwandishi wa habari wa magazeti ya kampuni ya TSN ya jijini Dar es Salaam , Abdlul Saliboko akiuliza suali katika majumuisha ya mkutano wa siku mbili wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka Afrika Mashariki.
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hotuba ya Rais wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa Afrika Mashariki Martini Ngoga kutoka Rwanda (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam leo.Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.

Na Genofeva Matemu – MAELEZO 

Shirikisho la wakurugenzi wa mashtaka Afrika Mashariki limeazimia kuongeza wigo wa ushiriki wa kikosi kazi ndani ya shirikisho hilo ili kuwajibika zaidi na kuweza kupata njia nyingine ya kupanua ushiriki wa waendesha mashtaka binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, rais wa shirikisho hilo Martin Ngoga amesema kuongezeka kwa wigo kutasaidia kuleta ushirikiano wa kutosha na hatimaye kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

“ kwa kipindi hiki uhalifu umekua na changamoto kubwa sana hivyo kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia kupanua wigo wa kupata mafunzo ya pamoja kwa wanachama wa shirikisho na kupunguza baadhi ya changamoto hizo”, amesema Ngoga.

Naye makamu mwenyekiti wa shirikisho hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Tanzania Dkt. Eliezer Feleshi amewataka waandishi wa habari kutokujadili na kushadadia kesi zilizoko mahakamani kwani kesi ikiwa mahakamani hairuhusiwi kujadiliwa bali kuiachia mahakama kufanya kazi yake.

Mkutano wa Shirikisho hilo ulioanza jana umemalizika leo ukiwa umehudhuriwa na wakurugenzi wa Mashtaka kutoka nchi tano za Afrika mashariki uliokuwa na lengo la kupitia upya Katiba yao ili kuimarisha umoja wao.

TUME YA KATIBA YATOA RASIMU YA MWONGOZO WA UUNDAJI MABARAZA YA KATIBA YA TAASISI, VYAMA, MAKUNDI

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) na Makamu wake Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani katika moja ya mikutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. (Picha na Tume ya Katiba).

Na Mwandishi Wetu
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa rasimu ya mwongozo wa uundwaji wa Mabaraza ya Katiba yatakayoundwa na kuendeshwa na taasisi, asasi, vyama na makundi ili kujadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ya Katiba itakayoandaliwa na Tume.

Kwa mujibu wa rasimu ya mwongozo iliyotolewa na Tume leo (Jumatatu, Mei 10, 2013) na kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo tovuti (www.katiba.go.tz) na ukiwemo ukurasa wa facebook wa Tume hiyo (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania), mwisho wa wananchi na wadau mbalimbali kuwasilisha maoni yao kuhusu mwongozo huo ni Mei 19 mwka huu (2013).

Rasimu hiyo inafafanua kuwa uundaji wa Mabaraza ya Katiba ya asasi, taasisi na makundi hayo unapaswa kutegemea katiba, kanuni, randama au ‘charter’ ya asasi husika.

“Miongoni mwa asasi, taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana yanayoweza kuunda Mabaraza ya Katiba ni kama jumuiya ya kidini, chama cha siasa, asasi ya kiraia, taasisi ya elimu ya juu, chama cha wanahabari,” inasomeka rasimu hiyo ya Tume itakayochapishwa katika magazeti ya Habari Leo, Zanzibar Leo na Mwananchi ya kesho (Jumamosi, Mei 11, 2013) na kurudiwa katika magazeti hayo Jumatatu (Mei 13, 2013).

Kwa mujibu wa Tume, asasi nyingine zinazoweza kuunda mabaraza hayo ni Taasisi ya Elimu ya Juu, Chama cha Wafanyakazi, Chama cha Wakulima, Chama cha Wafugaji, Baraza la Watoto, Taasisi ya Wafanyabiashara, Baraza la Wanawake, Taasisi ya Wanataaluma, Baraza la Vijana, Baraza la Wazee na Kundi au makundi ya watu wenye malengo yanayofanana au yale yenye mahitaji maalum katika jamii.

Katika rasimu hiyo, Tume inapendekeza asasi zinazotarajia kuunda mabaraza kutoa taarifa ya maandishi kwa Tume kuhusu kusudio la kuunda, kuendesha na kusimamia mabaraza ya katiba.

“Taarifa hiyo itawasilishwa katika ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba moja kwa moja Makao Makuu, mtaa wa Ohio, Dar es Salaam au ofisi ndogo Zanzibar au kutumia posta (S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar) au barua pepe (katibu@katiba.go.tz),” inasomeka sehemu ya rasimu hiyo.

Mabaraza ya Katiba yanaundwa kwa mujibu wa kifungu cha 18 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83. Kwa mujibu wa kifungu cha 18(6) cha sheria hiyo, Tume inaweza kuruhusu Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye malengo yanayofanana kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa wanachama wake kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba na kisha kuwasilisha maoni hayo kwa Tume.

Article 18

$
0
0
Unakumbuka? raha za ki-Legendary za muziki wa Silent Inn, Bills, FM Club, Carlifonia Dreamers, Mambo Club na Tazara? Basi DJ John Dillinga (DJ JD) na DJ Fast Eddy tunawakaribisha kujumuika na malegends wenzenu kila Jumamosi kuenzi nyakati hizo Isumba Lounge, Jolly Club kwa mchango wa elfu 10 tu mlangoni, Karibuni Sana.

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA GIRL GUIDES TANZANIA

$
0
0

Mlezi wa Tanzania Girl Guides ambaye pia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na viongozi wa Chama hicho kwenye Makao Makuu yao huko Mwananyamala wakati alipowatembelea tarehe 10.5.2013.
Mke wa Rais na Mlezi wa Girl Guides Tanzania Mama Salma Kikwete akiangalia kazi mbalimbali zilizofanywa na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakati Mama Salma alipotembelea Makao Makuu ya Girl Guides yaliyopo Mwananyamala jijini Dar tarehe 10.5.2013.
Mlezi wa Chama Cha Girl Guides hapa nchini Mama Salma Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano na viongozi wakuu wa Chama hicho mara baada ya kuwatembelea ofisini kwao huko Mwananyamala jijini Dar tarehe 10.5.2013.
Mlezi wa Girl Guides hapa Tanzania Mama Salma Kikwete akiangalia picha za matukio mbalimbali ya Girl Guides yaliyofanyika hapa nchini wakati alipotembelea Makao Makuu ya Chama hicho huko Mwananyamala jijini Dar tarehe 10.5,2013. PICHA NA JOHN LUKUWI.

Jaji Kiongozi Mhe. Fakih Jundu amuapisha Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba

$
0
0
Bw. Charles M. Magesa akila kiapo cha kushika nafasi ya kuwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu, kabla ya uteuzi wake Mhe. Magesa alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa Arusha, anayeshuhudia ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Benedict Mwingwa. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania)

ibada ya mazishi ya waumini wa kanisa katoliki waliofariki dunia kwenye tukio la mlipuko wa bomu huko jijini arusha

$
0
0
Mapadri wa kanisa katoliki wakiwa wamebeba jeneza lenyenye mwili wa mmoja wa waliokufa katika tukio la kutupwa kwa bomu la mkonokatika kanisa la Olasiti Arusha may 5, 2013.
Mapadri wakiwa wamebeba mislaba yenye majina ya marehemu wawili kati ya watatu waliofariki kwenye tukio la bomu la kurushwa kwa mkono kwenye kanaisa la Olasiti jijini Arusha May 5, 2013, katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa hilo may 10,2013.
Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashmu Josephat Lebulu akinyunyuzia maji miili ya waumini wa kanisa hilo waliofariki katika tukio la kurushwa kwa bomu la mkono kwenye kanisa la Olasiti jijini Arusha may 10,2013.
Kiongozi wa kanisa Katoliki nchini, Mhashamu Polycarp kaldinari Pengo akiongoza ibada ya mazishi ya waumini wa kanisa hilo waliouwawa katika bomu lililotupwa kwenye kanisa la Olasiti Arusha May 5,2-13. Kuhoto ni Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais Kikwete awasili nchini Afrika Kusini kuhudhilia kikao cha viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Cape Town, Afrika ya Kusini kuhudhuria kikao cha viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika leo tarehe 10 Mei, 2013.

Viongozi wa SADC wanakutana chini ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo Tanzania ndiye mwenyekiti.

Kikao cha leo kinatarajia kuzungumzia maendeleo na hali ya usalama katika ukanda huu hususan hali ya usalama Mashariki mwa Kongo, DRC, Madagascar na Zimbabwe.

Nchi za Afrika ya Kusini, Malawi na Tanzania zitapeleka vikosi Mashariki mwa DRC kulinda na kuleta utulivu na usalama.

Kuhusu Madagascar, nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi Julai, 2013 wakati nchini Zimbabwe nako uchaguzi unatarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

Mbali na mkutano huo Rais anahudhuria mikutano kadhaa inayoendelea mjini Capetown ukiwemo ule wa Kiuchumi ambao viongozi wa kisiasa, kiserikali na wakubwa wa mashirika binafsi wanahudhuria na kuzungumzia fursa za kibiashara na kiuchumi barani Afrika.

Rais anatarajia kurejea Dar es Salaam kesho tarehe 11 Mei, 2013

“Mwisho”

Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Cape Town – Afrika ya Kusini
10 Mei, 2013
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images