Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110004 articles
Browse latest View live

Linda heshima ya Tanzania, Rais awaambia wanajeshi wanaokwenda DRC

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya  wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na  jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,  katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013. 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
 Wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wametakiwa kudumisha utamaduni  wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani kwa kuifanya kazi hiyo kwa heshima, nidhamu na utii ili kulinda heshima yao wenyewe na ile ya Tanzania.
Askari hao wamekumbushwa utamaduni huo wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikuwa akiwaaga wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa katika DRC katika hafla iliyofanyika leo, Jumatano, Mei 8, 2012, kwenye Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu la Tanzania yaliyoko Msangani, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na askari hao, Rais Kikwete amewaambia kuwa hana wasiwasi kuhusu uwezo wao wa kutelekeza majukumu yao yanayowapeleka DRC isipokuwa tu kwamba waifanye kazi hiyo vizuri na kulingana na utamaduni wa majeshi ya kulinda amani ya Tanzania katika sehemu mbali mbali duniani.

“Tunakwenda kutelekeza majukumu ya Umoja wa Mataifa, sina shaka kuwa majukumu yenu mnayaelewa vizuri. Kazi yetu ni kulinda amani na wala hatuendi kupigana na yoyote. Kazi ya kijeshi mnaijua vizuri vile vile na kwa hili pia sina wasiwasi hata kidogo,” amesema Amiri Jeshi Mkuu na kuongeza:

“Kubwa ambalo lazima tulikumbuke ni kwamba nchi yetu kila ilikopeleka majeshi ya kulinda amani imejenga utamaduni wa pekee. Imejenga utamaduni wa askari wetu kuifanya kazi ya kulinda amani kwa heshima, kwa nidhamu na kwa utii wa kiwango cha juu. Hii ni heshima kwetu binafsi na heshima kwa taifa letu. Nawashukuruni na nawatakie kila la heri”

Kama ishara ya kuagana na askari hao, Rais na Amiri Jeshi Mkuu amemkabidhi Bendera ya Taifa Luteni Kanali Orestess Cassian Komba, Kamanda wa Kikosi cha Tanzania katika DRC ambacho kitajulikana kwa jina la TANZBATT 1-DRC, akimwambia “Bendera na Ikapepee”.

Katika jukumu la kulinda amani Mashariki mwa DRC, Kikosi cha Tanzania chenye askari 1281, kitajiunga na vikosi vya Malawi na Afrika Kusini ambavyo vyote vitakuwa chini ya Kamanda wa Brigedi hiyo, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa wa Tanzania pia. Kundi la kwanza la askari hao Tanzania linaondoka nchini kesho.

Majeshi hayo ya Tanzania yatalinda amani katika DRC chini ya Azimio Nambari 2098 (2013) la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

8 Mei, 2013




MIKOKO YA ISUZU JOURNEY NA TOYOTA CARINA INAUZWA HARAKA

Mipango ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013

Walk for Hunger in Boston May 5th 2013

$
0
0
Team New England Umoja Foundation, friends & families: Left to Right standing: N.E.U F Chair Sangiwa Eliamani, Makalla Francis, Shaaban Ndungo, Chidzero Nkumba, Abdul Latif Maalim, Steven Tomi, and Judith Mmari. Kneeling on the left is the Team Leader, Sifaeli Eliamani . They finished the 20 mile walk, and they were able to raise $710.00 for the Project bread, Walk for Hunger in Boston May 5th 2013. Thanks to all who supported us on this worthy cause. We truly appreciate for your act of kindness!. Thanks.

Miss Universe Tanzania atoa somo la madhara ya madawa ya kuleva Azania sekondari

$
0
0

Miss Universe Tanzania Winfrida Dominique akitoa somo la madhara ya madawa ya kulevya kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari ya Azania jijini. Winfrida alitoa somo hilo kwa dakika 40 kwa kushirikiana na Dk Johaness Mafwiri wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na taasisi ya New Hope Tanzania Limited (NEHOTA) ambayo inajishughulisha na kazi ya utoaji ushari nasaha kwa watumiaji wa madawa ya kulevya na mambo mengine.
=========  =======  =======
Na Mwandishi Wetu
Miss Universe Tanzania, Winfrida Dominique amewataka vijana nchini kutothubutu kutumia madawa ya kulevya kwani wao ndiyo tegemeo la taifa hili.
Winfrida alisema hayo wakati akitoa mafundisho kuhusiana na madhara ya madawa ya kulevya kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari ya Azania jana.
Mrembo huyo alisema kuwa madhara ya madawa ya kulevya ni makubwa sana hapa nchini hasa kwa vijana na yeye kama mmoja wa vijana, atatumia taji lake kutoa elimu kuhusiana na madhara ya madawa hayo.
Alisema kuwa amejionea mwenyewe jinsi vijana wanavyoathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya na taifa kupoteza nguvu kazi muhimu pamoja na matatizo ya ajira nchini.
“Nitatumia taji langu kutoa elimi mbali mbali ili kuwarejesha baadhi ya vijana waliopotea kurejea katika njia iliyonyoofu na kufanya kazi nyingine hata kwa kujiajiri, nitaendelea kutoa elimu hii kwa wanafunzi wengi zaidi, ” alisema Winfrida.
Mrembo huyo alitoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Dk Johaness Mafwiri  wa taasisi ya New Hope Tanzania Limited (NEHOTA) ambayo  inajishughulisha na kazi ya utoaji ushari nasaha kwa watumiaji wa madawa ya kulevya na mambo mengine.
Mbali ya Winfrida, Dk Mafwiri naye alitoa mada iliyohusiana na madawa ya kulevya na ulevi wa kupindukia ambao ni hatari kwa vijana na kwa upande wa elimu pia.
“Madawa ya kulevya yapo ya aina nyingi, lakini maarufu ni Cocaine na  Heroine, lakini bhangi na ulivi kupindukia ni moja ya madawa ya kulevya na yanatofautiana kwa upande wa madhara yake, si vizuri kwa vijana na hata kwa jamii kiujumla,” alisema Mafwiri.

Mahakama ya Rufani yamrejeshea Dkt Dalaly Peter Kafumu Ubunge wake wa jimbo la Igunga

$
0
0

Mahakama ya Rufaa imemrudishia Ubunge wa jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM Dkt Dalaly Peter Kafumu (pichani kushoto), baada ya kushinda rufaa aliyokata baada ya Mahakama Kuu kanda ya Tabora kumvua Ubunge kufuatia  madai ya kukiuka utaratibu wa uchaguzi wakati wa Kampeni katika Kesi iliyofunguliwa na Bw. Joseph Kashindye aliyekuwa Mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA.


Dkt Kafumu anakuwa mbunge wa pili wa CCM kurejeshwa mjengoni wiki, hii baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania, imethibitisha Mhe Aeshi Hilaly (pichani chini) kuwa mbunge halali wa Sumbawanga Mjini baada ya kushinda rufaa aliyokata kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, iliyomvua ubunge.

Hilaly alivuliwa ubunge na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila Aprili 30, 2012, kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kupitia CHADEMA,  Bw. Nobert Yamsebo. 

 Mhe Hilaly na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) walikata rufani kupinga hukumu hiyo na zote zilisikilizwa kwa pamoja na jopo la Majaji watatu, Edward Rutakangwa, Profesa Ibrahim Juma na Steven Bwana.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA DEMOCRATIC USA IKULU DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Democratic USA, kuanzia (Kulia) ni David Wilhem, Chris Bulinger, (kulia kwa Makamu) ni Michael Granger, na mwenyeji wa ujumbe huo, Dastan Mrutu, kutoka Business Council, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Mei 9, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na David Wilhem (katikati) kutoka Democratic USA, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu kwa mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Mei 9, 2013. Kushoto ni mmoja kati ya walioongozana na ujumbe huo, Michael Granger.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe kutoka Democratic USA, kuanzia (Kulia) kwa Makamu ni David Wilhem, Michael Granger, Chris Bulinger na mwenyeji wao, Dastan Mrutu, kutoka Business Council, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Mei 9,2013 kwa mazungumzo. Picha na OMR.

SERIKALI KUZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI MATUMIZI YA LISHE BORA NCHINI

$
0
0
 Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwa niaba ya Katibu mkuu Kiongozi kuhusu Hali ya Lishe nchini , mkakati wa serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata virutubisho muhimu kupitia vyakula na Kampeni ya uhamasishaji wa matumizi ya Lishe bora  nchini itakayozinduliwa tarehe 16  mwezi huu na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam yakiongozwa na kauli mbiu "Lishe bora ni Msingi wa Maendeleo ,Timiza wajibu wako".
 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula la Lishe Tanzania Faith Magambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu madhara yanayosababishwa na ukosefu wa lishe kwa watoto na umuhimu wa maziwa ya mama katika kujenga  afya bora  ya mtoto. Kulia ni Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo. 
 Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo akipokea na kujibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Dar es salaam. 
Waandishi wa Habari wakiwa Kazini wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

SHEIKH PONDA AACHIWA HURU! Afungwa kifungo cha nnje mwaka mmoja!

$
0
0
Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kusikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu juu mmoja wa wafuasi wake ambao walishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili. 

Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.

Mara baada ya kutolewa hukumu hiyomahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.

Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.

Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote litakalotokea.


 Askari wa Magereza akimfungua pingu Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu., ambapo leo yeye na wenzie 49 wameachiwa huru ila watatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja. PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA
Askari wakiwa kwenye msafara wa kumsindikiza Sheikh Ponda baada ya kuachiwa.


Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.
 Wafuasi wa Sheik Ponda wakimshangilia alipokuwa akihutubia ndani ya Msikiti wa Mtambani.

Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.
Katibu wa Jumuia za Taasisi za Kiisalamu Tanznania, Sheikh Ponda Issa Ponda akifanya mahubiri katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, alipokwenda leo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru jana, yeye na wenzake 49 waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la uchochezi.


Duce yapokea msaada wa kopyuta 20 toka Vodacom Foundation.

$
0
0
 .Mkuu wa shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Prof David Mfinanga, akitazama moja ya Kompyuta alizokabidhiwa na Vodacom Foundation kama msaada  katika harakati za kustawisha maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano shuleni hapo. Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Vodafone Foundation kutoka India, Laura Turkington, na Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule.
 Mkuu wa shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Prof David Mfinanga, akipokea msaada wa Kompyuta kutoka kwa Mkuu  wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule zilizotolewa shuleni hapo eneo la Changombe Dar es Salaam jana, Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Vodafone Foundation kutoka India, Laura Turkington.
 Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi na Hisabati, Elizabeth Mrema, akitumia moja ya Kompyuta zilizotolewa na Vodacom Foundation shuleni hapo kama msaada Dar es Salaam jana, kushoto wanaomtazama ni Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule akiwa na baadhi ya wanafunzi.  Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo, Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi na Hisabati, Anna Daniel, akitumia moja ya Kompyuta zilizotolewa kama msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo Dar es Salaam jana, kushoto wanaomtazama ni Maofisa wa Vodacom Foundation.  Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo.

Mkuu wa Kitivo cha Elimu wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo (kulia) akifafanua jambo mbele ya Maofisa mbalimbali wa Vodacom Foundation muda mfupi baada ya Kampuni ya Vodacom kupitia Mfuko wake wa Kusaidia Jamii kutoa msaada wa Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 kwa leongo la kustawisha matumizi ya Tehama shuleni hapo eneo la Chang'ombe Dar es Salaam.

RAIS JAKAYA KIKWETE KUZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI WA MATUMIZI YA LISHE BORA

$
0
0
Na. Eliphace Marwa - MAELEZO
 
Serikali imesema kuwa itaendelea kutumia njia mbalimbali kuwahamasisha wananchi kuzingatia  matumizi ya lishe bora kwa kuweka msisitizo katika kilimo cha matunda, mbogamboga, ufugaji wa samaki na matumizi ya vyakula vilivyowekewa virutubisho muhimu .
 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri mkuu Peniel Lyimo akiongea na
waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu mkuu Kiongozi ,leo jijini Dar es salaam amesema kuwa hali ya lishe nchini hairidhishi na tatizo la utapiamlo limeeendelea kuiathiri  jamii ya watanzania.
 
Amesema takwimu za mwaka 2010 zinaonesha kuwa asilimia 42 ya watoto walio na umri chini ya miaka mitano wamedumaa, asilimia 16 wana uzito pungufu  na asilimia tano wamekonda.
 
Aidha amesema asilimia  59 ya watoto wenye umri kati ya miezi sita hadi 59 wana upungufu wa damu, asilimia 33 ya watoto chini ya miaka sita wana upungufu wa vitamin A”, alisema Lyimo.
 
Pia ameongeza kuwa asilimia ya wanawake walio katika umri wa kuzaa yaani miaka 15 hadi 49 wanapata changamoto mbalimbali za  kiafya  zinazosababishwa  na  lishe duni za  upungufu wa damu, matatizo ya ukosefu wa madini joto mwilini, upungufu wa uzito na baadhi ya mama wajawazito kuwa na tatizo la ukosefu wa vitamini A.
   
Pia ameeleza kuwa tatizo la utapiamlo unaotokana  na ulaji unaozidi mahitaji kilishe linaendelea kuongezeka na unaathiri zaidi kwa wakazi wa mijini na tatizo hili hupelekea magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama moyo, kisukari na kansa.
 
Kwa upande wake Msaidizi wa Rais masuala ya lishe Dkt Wilbald Lorri amesema kuwa ufumbuzi wa tatizo la lishe bora kwa jamii liko mikononi kwa wanajamii wenyewe kujenga tabia ya kula matunda na mbogamboga  vitu ambavyo hupatikana kwa wingi na urahisi katika maeneo yao.
 
Amefafanua kuwa serikali imeweka msukumo katika kukamilisha mkakati wa taifa wa lishe pamoja na mpango wake wa utekelezaji, kuanzisha kamati ya kitaifa ya ushauri wa lishe nchini, kuanzisha dawati la lishe katika halmashauri zote nchini pamoja na kuanzisha kasma ya lishe katika bajeti ya halmashauri,kuingiza na kuimarisha masuala ya lishe katika kilimo na uongezaji wa virutubisho  katika mafuta ya kula, unga wa ngano na unga wa mahindi.
 
Aidha wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo yatayofanyika kuanzia mei 15 na kufikia kilele chake mei 16 katika viwanja vya Mnazi mmoja yakiongozwa na kauli mbiu isemayo " Lishe bora ni Msingi wa Maendeleo , Timiza Wajibu wako"
 
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya atazindua kampeni ya uhamasishaji wa matumizi ya Lishe bora.

WAZIRI MKUU AZICHARUKIA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Mh.Waziri Mkuu Pinda.

*Akemea matumizi mabaya, kupendelea na kujipa tenda
*Ahimiza usimamizi wa fedha wa umma
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amecharuka na kuwakemea watendaji kwenye Serikali za Mitaa ambao wanatumia nafasi zao kulazimisha kufanya biashara na Halmashauri wanazoziongoza.
 
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Mei 9, 2013) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 29 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hoteli ya Sundown Carnival, nje kidogo ya Jiji la Arusha.
 
Waziri Mkuu alisema haipendezi kusikia baadhi ya wakuu na watendaji katika Halmashauri wakituhumiwa kuwa sehemu ya mitandao ya wizi katika Halmashauri au wana maslahi katika kampuni zilizohusika kutoa huduma na bidhaa duni kwa Halmashauri.
 
Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema kuna malalamiko amepokea kwamba Meya wa Halmashauri moja amefungua kampuni sita na zote anataka zipewe tenda kwenye Halmashauri anayoiongoza.
 
“Kuna Halmashauri zenye taarifa za wizi, upotevu na ubadhirifu ambao kwao umekuwa ni maisha ya kawaida. ALAT mnayo nafasi kubwa kuendelea kuboresha usimamizi wa fedha za Halmashauri kwa vile Jumuiya yenu inawaunganisha watendaji wakuu na viongozi wakuu wa Halmashauri zote chukueni hatua. Waaibisheni na kuwaumbua wale wanaobanika kutumia vibaya fedha hizi za umma.”
 
“Lakini, ili muweze kufanya hayo lazima ninyi wenyewe msiwe sehemu ya uovu huu. Inafadhaisha sana kusikia minong’ono kuwa baadhi ya madiwani wanatuhumiwa kuwa sehemu ya mitandao ya wizi katika Halmashauri .... huo ni ukosefu wa wajibu na ni kuvunja mkataba wenu na umma.
 
Akuzungumzia kuhusu utunzaji wa mahesabu, Waziri Mkuu alisema upo udhaifu katika eneo hilo kwani upo ushahidi unaoonesha kwamba taarifa za vitabuni hazifanani na kazi iliyofanywa (value for money) akimaanisha kwamba kazi inayofanyika hailingani na thamani halisi ya fedha iliyotumika.
 
“Tatizo hili ni kubwa na lina sura mbili kuu. Moja ni kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya watumishi na madiwani katika usimamizi wa fedha za Serikali za Mitaa. Baadhi ya madiwani wamediriki  kushirikiana  na watumishi wasio waaminifu katika kuhujumu fedha za umma.  Pili, ni Watumishi wa Serikali za mitaa kushindwa kutekeleza wajibu wao hivyo kulipwa mishahara ambayo hawaitumikii ipasavyo,” alisema.
 
“Hili nalo nataka lijadiliwe kwa kina na mkitoka hapa kila Kiongozi na Mtendaji ajue ana jukumu gani la kufanya.  Aidha, hili ndilo eneo ambalo nataka hatua zichukuliwe ili kunusuru Fedha za Halmashauri,” alisisitiza.
 
Alisema kwa kutambua ukweli huo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameendelea na ukaguzi wa thamani ya fedha zaidi ya ukaguzi wa kawaida.
 
Wakati huohuo, Waziri Mkuu alipokea hundi ya mfano ya sh. milioni 10 iliyotolewa na Benki ya NMB ili ziweze kusaidia kununua dawa na vifaa tiba kwa ajili ya majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu mkoani Arusha kutokana  na mlipuko wa bomu uliotokea Mei 5, mwaka huu kwenye Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, eneo la Olasiti.
 
Akizungumzia msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa benki hiyo, Bibi Domina Feruzi alisema, kama taasisi wameguswa na maafa yaliyowakumba wakazi hao wa Arusha na wameamua kuchangia kiasi hicho cha fedha ili kiwasaidie kwa dawa na vifaa vya tiba vinayohitajika.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MEI 9, 2013.

Taarifa kwa umma kuhusu ufafanuzi wa usalama wa soda

$
0
0


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyoundwa chini ya Sheria ya Chakula Dawa na Vipodozi Sura ya 219, ili kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi, na vifaa tiba kwa lengo la kulinda afya ya jamii dhidi ya madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo.


Ili kutimiza wajibu huo, TFDA inasimamia pamoja na mambo mengine udhibiti wa uingizaji  wa vyakula kutoka nje ya nchi na utengenezaji wa vyakula ndani ya nchi kwa ajili ya kulinda afya za watumiaji. Katika udhibiti wa vyakula hivyo, michakato mbalimbali hufanywa ili kuwa na uhakika juu ya usalama wake kwa; kufanya tathmini na uchunguzi wa kimaabara, kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa usalama wa bidhaa kwenye soko na hatimaye kusajili majengo na vyakula baada ya kujiridhisha juu ya usalama wake.


Kutokana na mfumo wa udhibiti uliopo, Mamlaka imesajili bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyofungashwa ikiwa ni pamoja na vinywaji aina ya soda zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje.


Hivi karibuni kulitolewa taarifa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kueleza kuwa kinywaji cha soda ni sumu. Mamlaka ina mashaka juu ya taarifa iliyotolewa kwa sababu haidhani kama ilitolewa kwa kuzingatia misingi ya kisayansi. TFDA inapenda kuwatoa hofu watumiaji wa kinywaji hiki kuwa, soda ni bidhaa ya chakula ambayo inatumika kote duniani na huzalishwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama. Kwa upande wa TFDA, soda zote zilizosajiliwa zimepitia katika mchakato ambao unatoa uhakika juu ya usalama wake kwa lengo la kulinda afya ya binadamu.


Tunapenda kutoa rai kwa vyombo vya habari kufanya utafiti wa kina hususan katika masuala yanayohusu ushahidi wa kisayansi ili kuondoa uwezekano wa kutoa taarifa kwa umma ambazo zinaweza kujenga hofu na mashaka ambayo hayastahili.


Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kupitia;

Mkurugenzi Mkuu,

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)

Barabara ya Mandela, Mabibo External,

S.L.P 77150

Dar Es Salaam, Tanzania

Simu:              +255 22 2450512/2450751/2452108

Fax:                 +255 22 2450793

Barua pepe:    info@tfda.or.tz

Tovuti:            www.tfda.or.tz

shukurani

$
0
0

Familia ya Marehemu  Acp (rtd) Bruno Damiani Matembo wa Ukonga, Dar es salaam, inatoa shukurani kwa wale wote walioshiriki kwa hali na mali katika kufanikisha msiba wa Baba yao Mpendwa Mzee Matembo (pichani) ambaye alilazwa katika nyumba yake ya milele Ukonga, jijini Dar es salaam.

Shukurani ziwafikie  Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Viongozi wa dini walioongoza Misa ya kumuombea Marehemu, Madaktari na Wauguzi waliojitahidi kuokoa maisha  ya Mzee Matembo, Majirani na wana Ukonga 

Tutaendelea kukumbuka daima Baba yetu Mpendwa kwa kwamalezi bora uliyo kuwa umetupatia hatutakuangusha kamwe kwani hata wajukuu wako wameyafuata maelekezo yako uliyo kuwa una wapa yakuwa nanidhamu kwa watu Wote Kuipeda Nchi yetu na Kutii Serekali pamoja na Mamlaka zake 

BWANA AMETOA BWANA AMETWAA
JINA LAKE  LIHIMIDIWE 
AMEN

BOSI WA KONYAGI APASUA JIPU, alia na magazeti yanayochafua kampuni yake inayotamba kwa sasa nchini

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL),  David Mgwassa (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, ambapo alilalamikia kitendo cha baadhi ya magazeti yenye uhusiano wa nchi jirani, yanayotumika kuchafua bidhaa za TDL. Kushoto ni Meneja Masoko wa TDL, Joseph Chibehe. Yafuatayo ni maelezo ya Bw. Mgwassa...

Tumeanza kuona magazeti yenye affiliation na nchi za jirani yakitumika ku misrepresent products za TDL.
Articles ninazozungumzia zilichapishwa tarehe 2 may 2013 na tarehe 6 may 2013, kupotosha umma, na kupindisha ukweli. kwa sababu mawasiliano ya kisheria yanafanyika sitataja ni magazeti gani yanahusika, lakini nina uhakika yana uhusiano mkubwa wa kibiashara na nchi jirani.
Ushauri wangu ni kuwa magazeti ya Tanzania, yaepukane sana na vitu vinavyoonyesha kuwa kuna muelekeo wa kurepresent matakwa ya nchi tofauti na kupuuza matakwa ya kitanzania
Kitendo cha kujaribu kuoanisha brand ya Konyagi na accidents za magari au piki piki , ni ya
upotoshaji mkubwa wa jamii ya kitanzania, kwani hakuna bia, hakuna pombe za kienyeji au pombe kali. Huu ni uhuni na ujinga mtupu
Sisi TDL hatuogopi ushindani, sio ushindani wa humu Tanzania, na nasema tutaendelea kuuza products zetu zinazozalishwa Tanzania, huko Uganda, Kenya south Sudan, Rwanda na Burundi, licha ya matatizo makubwa tunayopata
Na tutaendelea kuwasiliana na mabalozi, wa nchi husika, EAC office na wizara zenye mamlaka katika kukuza soko la pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki, kuhusu changamoto za kibiashara tunazozipata.
Kama nilivyozungumza mwanzo sisi hatuzalishi Konyagi tuu, bali tunazalisha Zanzi cream, Knights, Viceroy brandy , siyo kwa sababu hatuwezi kuagiza, bali kwa  kutumia watanzania katika uzalishaji na kuwapa ajira. Msitufananishe sisi na watu wanaoleta makatoni ya pombe kutoka Ireland au Uingereza, sisi tuko tofauti na mahitaji ya nchi hii tunayajua.
Raisi wetu Dr Kikwete kila siku anasema issue hiyo hiyo, value added , value added, mbona masikio yenu mnafunga?
Naomba niwaeleze ukienda South Africa leo utaona kila aina ya magari mapya, utaona Toyota, utaona Nissan utaona Mercedez benz , utaona Kia na kadhalika, lakini magari yote hayo yanaundwa South Afrika, huwezi kukuta gari imetengenezewa Singapore, nia ni kuhakikisha kuwa wenyeji wanapata kazi, na approach yetu  TDL ni same.
Sioni kati ya nyie mtu ambaye anamchukua mtoto wake kumpeleka Nairobi au Dubai, kumtafutia kazi, wote mnawaleta kwetu, hata leo wengine wananiomba kazi, kwa hiyo naomba sana mtu akikujaza akili au upumbavu, na wewe jaribu kuchanganya na akili nzuri za kwako
Ahsanteni sana



Baadhi ya wanahabari wakisikiliza kwa makini wakati Mgwassa akilalamikia jambo hilo

MHASIBU MKUU JAMBO LEO AFARIKI DUNIA

$
0
0
Aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo 
Concepts Tanzania Limited, marehemu Vicky Mgoyo

Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited inayochapisha gazeti la Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania, Vicky Mgoyo (49), amefariki dunia.

Meneja Mkuu wa Jambo Concepts, Ramadhani Kibanike, alisema marehemu Vicky Mgoyo alifariki dunia leo asubuhi kwenye Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alikokimbimbizwa kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa usiku wa kuamkia leo.

Alisema kifo cha Vicky zaidi akijulikana kwa jina la Mama Mgoyo kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia yake bali pia kwa Kampuni ya Jambo Concepts kutokana na kwamba alikuwa ni mtu mwaminifu kazini, lakini pia uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzake.

"Tumepoteza mfanyakazi ambaye ni mchapa kazi na kipenzi cha wengi, tutamkumbuka kwa hilo. Naomba wafanyakazi tuungane na ndugu na jamaa katika kuomboleza msiba wa kipenzi chetu huku tukiamini kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

"Bado hatujapata taarifa rasmi za maziko, ila taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao zinaendelea kufanyika," alibainisha Kibanike.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Juma Pinto alitoa mwito kwa wafanyakazi kuonesha mshikamano katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao.

Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Anicetus Mwesa, akizungumzia msiba huo alisema Mama Mgoyo ametwaliwa na Mungu ilhali akiwa bado anahitajika na familia pamoja na ofisi yake, hivyo ameacha pengo ambalo litachukua muda kuliziba.

"Mwenzetu ametangulia nasi tupo nyuma yake, zaidi tumwombee ili Mungu ampumzishe katika raha ya milele," alisema Mwesa.

Kwa upande wake Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hilo, Richard Mwaikenda, alisema atamkumbuka Vicky kwa kuwa ni mwanamke shupavu ambaye alikuwa anazingatia maadili ya kazi yake ya uhasibu.

Pia alisema alikuwa ni mama mjane makini ambaye alihakikisha anasimamia watoto wake katika suala la kuwapa elimu bora, ambapo katika hilo alikuwa akifanya kila anachoweza kuhakikisha anasomesha nje ya nchi tena kwenye shule bora na makini.

Vicky Mgoyo aliyezaliwa Novemba 26, 1964, ameacha watoto watatu huku wawili kati yao ni wanaume.

Alilazwa katika Hospitali ya Kairuki wiki iliyopita ambako alipatiwa matibabu kwa muda wa siku nne na kuruhusiwa.Jumatatu aliripoti kazini na kuendelea na kazi hadi jana jioni, ambapo usiku alizidiwa na hatimaye leo asubuhi Mungu alimchukua. Mungu ailaze pema peponi roho ya Vicky Mgoyo.


HARDMAN ANAOMBA KURA YAKO

$
0
0
Wimbo wa "tunda" ni wimbo ambao umefanya vizuri sana kule jamaica hata kupelekea baadhi ya wasanii wa kule kuifanyia upya instrumental yake yaani kufanya riddim...
Ni msani anayestahili tuzo ya reggae ya killi mwaka huu

Article 11

DKT. CHARLES KIMEI ACHAGULIWA KUWANIA TUZO YA KIONGOZI BORA WA MABENKI AFRIKA MWAKA 2013

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (pichani) amechaguliwa kwenye mchakato wa kumtafuta “kinara wa Benki wa Afrika”  kwa mwaka 2013 unaoendeshwa na  African Banker Awards chini ya African  Development Bank Group.

 Kinara wa Benki wa mwaka ni tuzo inayotolewa kwa Viongozi (CEO`s) wa sekta ya benki na fedha barani Afrika ambao wamepata mafanikio makubwa kwenye mashirika yao hivyo kuleta maendeleo katika sekta fedha na uchumi katika nchi zao na Afrika nzima kwa ujumla.
African Banker Awards imechagua  vinara watano wa sekta ya fedha Afrika  kuingia katika mchakato huo ambapo mmoja wao ndiyo atakayejitwalia tuzo hiyo. Zaidi ya Dkt. Charles Kimei, wengine waliongia kwenye mchakato huo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni  Segun Agbaje-GTB Bank(Nigeria), Aigboje Aig-Imoukhede-Access Bank(Nigeria), Andrew Allly-Africa Finance Corporation(Nigeria) na Jao Figuerdo- Unico Bank.
Dkt. Kimei ni mtanzania wa kwanza kuingizwa kwenye mchakato huu tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo zaidi ya miaka kumi iliyopita, na ni mtanzania pekee kwenye kinyang`anyiro hicho ambacho kimekuwa kikitawaliwa na mabenki kutoka nchini Nigeria na Afrika ya Kusini. Hii ni fahari kubwa kwa taifa letu kwani Dkt. Charles Kimei ni mtanzania anayeongoza benki kubwa ya Tanzania inayoendeshwa na watanzania wenyewe.
Dkt. Kimei, ambaye ni mchumi mwenye stashahada ya uzamivu, amefanya kazi katika sekta ya fedha kwa zaidi ya miaka 30 akitokea Benki Kuu ya Tanzania alikokuwa Mkurugenzi wa Sera na Utafiti  kabla ya kujiunga na Benki ya CRDB mwaka 1998 kama Mkurugenzi Mtendaji. Akiwa Benki ya CRDB ameingoza kutoka Benki iliyokuwa ikijiendesha kwa  hasara hadi kuwa Benki inayoongoza nchini.
Chini ya uongozi wa Dkt. Kimei, Benki ya CRDB imeweza kupata mafanikio makubwa  ikiwemo kutoka kutengeneza faida ya Shilingi billion 2 mwaka 1998 mpaka kufikia Shilingi billion 108 mwaka huu, kuongeza mtandao wake wa matawi kutoka matawi 16 hadi matawi 97 mwaka huu. Katika kipindi hiki  pia Benki ya CRDB imekuwa kinara wa kuleta bidhaa bunifu kwenye soko ikiwemo kadi zenye nembo za kimataifa za MasterCard na Visa, ATMs za kutolea na kuweka fedha, mashine maalum za kulipa kwa kutumia kadi (POS), Mikopo maalum ya Microfinance na Wajasiriamali pamoja na kushinda tuzo za kimataifa za Chapa Bora yaani SuperBrands kwa miaka minne mfululizo (2010-2013) na  tuzo ya benki bora itolewayo na  Euro-Money mwaka 2004.

Chini ya uongozi wa Dkt. Kimei, Benki ya CRDB imekuwa benki ya kwanza ya kizalendo  kuvuka mipaka na kufungua kampuni tanzu katika nchi jirani ya Burundi hivyo kufungua milango ya ukuaji wa mahusiano ya biashara kati ya nchi hizo mbili na ukanda mzima wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kuingia kwa Dkt.Kimei kwenye mchakato huu wa kupata kiongozi bora  wa Benki wa Afrika kunakuja muda mfupi tu baada ya kuteuliwa kwake bila kupingwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki nchini Tanzania (TBA). Mwenyekiti wa Chama Cha Mabenki huchaguliwa na benki zote wanachama wa TBA.
Tunamtakia kila kheri Dkt.Charles Kimei na Benki ya CRDB katika kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika tuzo hiyo.

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI TFF KUFANYIKA SEPTEMBA 29, 2013

$
0
0

http://blog.tanzaniamwandi.co.tz/wp-content/uploads/2013/03/Tenga-wa-TFF.jpg
Rais  wa TFF 'Sir' Leodegar Chilla Tenga

Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu baada ya ule wa Dharura wa marekebisho ya Katiba ulipangwa kufanyika Julai 13 mwaka huu. 
Tarehe hizo zimepangwa na kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika leo (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais wake Leodegar Tenga ambacho kupokea rasmi maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kupanga utekelezaji wake.
 “Kamati ya Utendaji ya TFF imepokea rasmi barua ya FIFA na kupanga utekelezaji wake. Tumepokea maagizo ya FIFA yanayotuelekeza cha kufanya, si TFF wala mtu mwingine yeyote anayeweza kuongeza jambo lingine.
 “Maagizo ni undeni Kamati ya Maadili, Kamati ya Rufani ya Maadili, fanyeni marekebisho ya Katiba, anzeni tena uchaguzi, waliokuwepo na wengine wapya waruhusiwe. Tumejitahidi kuhakikisha uchaguzi uwe kabla ya Oktoba 30 mwaka huu kama FIFA walivyotuagiza,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kazi kubwa itakuwa ni kutayarisha kanuni hizo, kwani Kamati za Maadili lazima ziwe na kanuni zake na kuhakikisha kuwa hakuna mgongano kati ya Kanuni za Nidhamu na Kanuni za Maadili.
Pia Rais Tenga amesema kuna kazi ya kuangalia jinsi zitakavyoingia katika uchaguzi ambapo maana yake muda wa mchakato wa uchaguzi utakuwa zaidi ya siku 40 za sasa, hivyo mabadiliko hayo yatagusa vilevile Kanuni za Uchaguzi.
Kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji, rasmu ya mwanzo ya Kanuni hizo inatakiwa iwe imetoka kufikia Mei 30 mwaka huu ambapo itapelekwa FIFA kwa ajili ya kupata mawazo yao kabla ya kuendelea na hatua inayofuata.
Juni 15 mwaka huu Kamati ya Utendaji ya TFF itakutana kupokea mapendekezo hayo ambapo baada ya kuyapitisha itayapeleka tena FIFA. Taarifa (notice) ya Mkutano Mkuu wa Dharura ambayo kikatiba ni siku 30 itatolewa Juni 12 au 13 mwaka huu.
 Baada ya Mkutano Mkuu wa Dharura wa marekebisho ya Katiba, Kamati ya Utendaji itakutana kati ya Julai 14 na 15 mwaka huu kuunda Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili ili kuruhusu mchakato wa uchaguzi uanze.

 Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Mei 9, 2013

Viewing all 110004 articles
Browse latest View live




Latest Images