Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 129 | 130 | (Page 131) | 132 | 133 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waziri wa Fedha na Uchumi Mhe Dk. Wiliam Mgimwa akitiliana saini na Balozi wa EU Mhe. Filiberto Sebregondi.

  Na Frank Mvungi na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  SERIKALI ya Tanzania imetiliana saini mkataba na Jumuiya ya Umoja wa nchi za Ulaya( EU) utakaowezesha Tanzania kupatiwa shilingi bilioni 20 kusaidia maendeleo katika sekta ya kilimo cha miwa kwa wakulima wa Visiwa vya Zanzibar.

  Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam kati ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mhe Dk. Wiliam Mgimwa na Balozi wa EU Mhe. Filiberto Sebregondi, ambapo unategemewa kuisaidia serikali katika kuondoa umasikini kwa wananchi wake na kuiwezesha nchi kupiga hatua ya maendeleo kupitia sekta ya kilimo.

  Waziri Mgimwa alisema kuwa msaada huo pia utasaidia kuwajengea wananchi uwezo wa kutekeleza kilimo chenye tija na kupanua soko la bidhaa zitokanazo na miwa kwani miundo mbinu ya maeneo ya Uzalishaji pia itaboreshwa katika utekelezaji wa mradi huo.

  “Kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kuishukuru jumuiya ya umoja wa nchi za Ulaya kwa juhudi kubwa wanazochukua kusaidia maendeleo ya nchi yetu, asanteni sana,” alisema Waziri Dk.Mgimwa.

  Naye balozi wa EU, Mhe. Filberto Sebrigondi alisema wameridhishwa na mikakati ya serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ndio maana wanaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kusaidia wananchi kufikia maendeleo ya kweli hivyo wameamua kusaidia sekta ya miwa ili iweze kukua na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

  Pia balozi Sebrigondi alisema kuwa wataendelea kusaidia bajeti ya Serikali ya Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuwa Tanzania imeonyesha nia ya dhati katika kukuza uchumi wake na kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wake ili waongeze tija katika uzalishaji.

  Alisema katika kipindi kilichopita asilimia 87% ya fedha lizizotolewa kwa Serikali ya Tanzania zimeshatumika katika miradi ya maendeleo, hivyo ameahidi kuwasaidia wanachi wanaojihusisha na kilimo cha miwa ili kuwajengea uwezo, kufanya tafiti na kutoa elimu ya utunzaji mazingira katika maeneo yatakayonufaika na msaada huo.

  Umoja wa nchi za Jumuiya ya Ulaya umekuwa kwa muda mrefu ukisaidia sekta mbalimbali za maendeleo hapa nchini ikiwa ni moja ya washirika wa maendeleo wa Tanzania ambapo baadhi ya Sekta zinazonufaika ni sekta ya kilimo cha Kahawa, na Miwa, sekta ya Barabara, Elimu, nishati ya Umeme ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa Tanzania.

  0 0


  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali ina kazi kubwa ya kushughulika na kundi dogo linalojihusisha na lugha za uchochezi wa kidini ambao unachangia kudhoofisha amani ya nchi.
   
  “Tunajua nia yao ni kufanya nchi isitawalike lakini sisi tumesema hatukubali. Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, ulinzi uimarishwe kila mahali, mshingae kuona watu wanawahoji lakini nia njema, ya kurudisha amani yetu,” alisema Waziri Mkuu.
   
  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Mei 10, 2013) wakati akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali wakati wa ibada ya mazishi ya waumini watatu wa Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha waliofariki dunia kutokana na mlipuko wa mabomu uliotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, mwaka huu kanisani hapo.
   
  Waziri Mkuu amewaomba wanachi kutoka ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kwenye upelelezi wa tukio hilo.
   

  0 0

  Meneja Mauzo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa Mkoa wa Morogoro, James Gomile(kushoto) akimkabidhi Vifaa vya michezo,Nahodha wa timu ya Chuo cha SUA, Calvin Mjema wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Vyo shiriki vya mashindano ya mchezo wa Pool kwa Vyuo vya Elimu ya juu Mkoani Morogoro.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Morogoro, Patrick Lugang’ha.
  Meneja Mauzo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa Mkoa wa Morogoro, James Gomile(kushoto) akimkabidhi Vifaa vya michezo,Rais wa Chuo Kikuu cha ARDHI, Moyo Hamza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Vyo shiriki vya mashindano ya mchezo wa Pool kwa Vyuo vya Elimu ya juu Mkoani Morogoro.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Morogoro, Patrick Lugang’ha.


  0 0


  0 0

  Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akiwakaribisha wageni wanahabari katika hafla mchapalo ya kusheherekea Africa Day na Dstv ambapo amesema DStv inatoa nafasi kwa wateja wake kuwa na fursa ya kuchagua vifurushi mbalimbali kulingana na uwezo wa mteja ambacho cha uwezo wa chini kabisa ni Access chenye zaidi ya channeli 40 gharama yake ni nafuu sana ambapo mteja atalipia shilingi 16,500 kwa mwezi. (Picha na Zainul Mzige wa dewjiblog).
  Meneja wa Fedha wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Bw. Francis Senguji akizungumzia malengo ya DStv Tanzania ambapo amesema wao kama waendeshaji wa biashara nyingine barani Afrika wanaojali na kuthamini maendeleo ya jamii wameona ni wajibu kusaidia jamii ili kuweza kuendeleza maendeleo ya kijamii nchini Tanzania.
  Kwa kuendeleza hilo Multichoice ina mfumo wa kutoa elimu mashuleni ( Multichoice Resource Centre) hivyo watamumia jukwaa la Teknolojia kama darasa kwa njia mbalimbali kuwapa jamii nafasi ya kuendeleza vipaji na ujuzi.
  Mfumo huo kutoa rasilimali kwenye shule kama vile ving'amuzi vya Satellite, VCRs/DVD na kifurushi cha elimu cha Dstv. Mpaka sasa Multichoice imeanzisha vituo vya rasilimali jamii katika shule 82 nchi nzima kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Mbeya, Pwani na Tanga.
  Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) akifafanua jambo wakati wa hafla mchapalo katika kusheherekea usiku wa Africa Day na DStv. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Barbara Kambogi.
  Waalikwa katika hafla mchapalo ya kusheherekea usiku wa Africa Day na DStv katika Hoteli ya New Africa ya jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
  Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Blogger John Bukuku wa Fullshangwe Blog, Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo Ronald Shelukindo, Mdau wa DStv na Meneja wa Fedha katika kampuni hiyo Bw. Francis Senguji wakipozi kwa picha.
  Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kulia) akifurahi jambo Wanahabari Sidi Mgumia (katikati) na Mama Mhina.
  Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo Ronald Shelukindo, Meneja wa Fedha katika kampuni hiyo Bw. Francis Senguji na mdau wa DStv wakipozi mbele ya camera yetu wakati wa hafla ya kusheherekea African Day na DStv iliyowakutanisha waandishi wahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini.
  Wanahabari wakiwa bize kujaza Quiz iliyotolewa na kampuni ya Multichoice Tanzania ambapo mshindi kwanza amezawadiwa Full Set ya King'amuzi cha Dstv na 'Subscription' ya mwezi mmoja na washindi kumi wamezawadiwa kofia na T-shirts za Supersport moja ya chaneli zinazopatikana katika king'amuzi cha Dstv.
  Wanahabari wakiendelea kuumiza kichwa huku wengine waki-google majibu ya Quiz hiyo kupitia simu zao za kiganjani.
  Mtangazaji wa Radio Dennis Buslwa a.k.a Ssebo (kulia) akiwa busy kutafuta majibu ambapo tunahisi alikwa anawasiliana na watu wa Mo Blog wampe majibu kamili. Wengine ni Kamera Man wa Channel Ten na Mtangazaji wa Radio Salma Msangi pamoja na mdau wa Star Tv.
  Barbara Kambogi akiteta jambo na Angela Msangi wa TBC.
  Dada Revina Bandihai wa kampuni ya Multichoice Tanzania na HR Manager wa kampuni hiyo.
  Ronald Shelukindo na Dada Furaha Samalu wakifungua mziki wa Kiafrika huku Bw. Francis Senguji akiserebuka na mdau.
  Mkurugenzi wa Fullshangwe Blog John Bukuku akiserebuka na Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi wakati wa hafla hiyo.
  Kwaito ilichezeka kisawa sawa....Chezea Multichoice wewe.....Ilinogaje.!
  Kutoka kushoto ni Blogger Cathbert Angelo wa kajunason Blog, Mpiganaji Fadhili Akida na Blogger Othman Michuzi wa mtaa kwa mtaa Blog wakipoowz mbele ya kamera yetu.
  Bloggers katika picha ya pamoja.
  Dada Revina Bandihai wa Multichoice Tanzania na Bw. Francis Senguji wakisataka Rhumba wakati wa hafla hiyo.
  Meneja wa Fedha wa Multichoice Tanzanua Bw. Francis Senguji akimpongeza Ssebo baada ya kuibuka mshindi katika Quiz iliyoendesha na Kampuni hiyo ambapo alinyakua Full Set ya King'amuzi cha Dstv na 'Subscription' ya mwezi mmoja.
  Pichani juu na chini Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akigawa Kofia na T-shirts kwa washindi wa Quiz ilyoendeshwa na kampuni hiyo wakati wa kusheherekea Africa Day na Dstv.
  Dada Revina Bandihai (kushoto) wa Multichoice Tanzania akishow love na washindi wa Quiz iliyoendeshwa na kampuni hiyo.

  0 0

  Picha juu na chini ni Foleni ya magari ya takataka zaidi ya 30 yaliyokwama katika dampo la Pugu Kinyamwezi kwa takribani siku tatu kutokana na ubovu wa miundo mbinu huku taka zikiendelea kuoza ndani ya magari hayo na kusababisha harufu mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo.(Picha na Dewji Blog).
  Katapila likiwa katika jitihada za kuchonga barabara ili angalau magari ya taka yaweze kufika eneo la dampo kuwamga taka.
  Masela wakifurahia baada ya gari la taka lililokuwa limekwama kufanikiwa kupandisha kilima katika dampo hilo kuelekea kumwaga taka.
  Wanafunzi wa shule ya msingi walipokutwa na camera yetu katika dampo hilo wakikatiza na kuzubaa zubaa eneo hilo wakati wa saa za shule.
  Wakazi wa maeneo hayo wakichambua takataka hizo kujiokotea chupa tupu za maji na mifuko ya plastiki ikiwa ni ajira waliyojitengenezea katika kuendesha maisha yao ya kila siku, shuhuda wa Mo Blog Zainul Mzige anatanabaisha kwamba chupa wanazookota huuzwa kilo moja kwa shilingi 100 kitu kinachowapelekea wafanyaji wa biashara hii kuwa watumwa wa pombe za kienyeji haswa almaarufu kama Gongo au Chang'aa.
  Mitaro ya maji machafu ikiwemo mikojo na vinyesi katika dampo hilo...Je kuna kupona kweli hapa????
  Magari ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni nayo yalikwama kwenye dampo hilo, pichani yakielekea kuwamga taka hizo baada ya barabara kutengemaa kwa kiasi.
  Pichani ni juu na chini Mama lishe wakitoa huduma ya chakula chini ya mti katika eneo lilizongukwa na taka ikiwemo harufu kali na Nzi wanaozunguka hapa na pale lakini vibarua wa dampo hilo hawana la kufanya.
  Moja ya Katapila lililokodiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam likiwa limekufa na kushindwa kufanya kazi kutokana na kukwamisha na miundo mbinu ya eneo hilo la dampo huku mafundi wakihangaika kulifufua.
  Meneja wa Dampo la Pugu Kinyamwezi Bw. Richard Katiti akizungumzia changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika kipindi hiki cha mvua kitu ambacho kinawapelekea kutumia jitihada za ziada ikiwemo kukodisha magari (Vijiko) ili kujitahidi kuhakikisha miundo mbinu ya kufika katika dampo hili inapitika kwa urahisi ili kuondoa vikwazo kwa magari yanayotoa huduma ya kuzoa taka mjini.
  Devera wa gari la Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Ramadhani Sufi akielezea adha wanayoipata ambapo amefafanua kuwa inafika mahali inawabidi kulala siku mbili na gari zenye mzigo wa taka katika mazingira ambayo ndio wanayoshinda na kula kitu ambacho kinaweza kuwasabishia maradhi hivyo ameliomba jiji kurekebisha hali hiyo ili kuwaepusha na mazingira hatarishi kiafya kutokana na uchafu unaolundikana mahali pamoja kuanzia dampo hadi kwenye magari.
  Aidha amefafanua kuwa hali hiyo inasababisha kutuchafulia jina la kampuni yetu na kuonekana kama hatufanyi kazi kumbe tatizo lipo kwenye utaratibu mzima wa Manispaa na suala la miundo mbinu.
  Pia ameshauri jiji liongezewe uwezo kutokana na kuwa na vyombo vichache na chakavu kitu kinachopelekea kuzidiwa katika kutoa huduma katika dampo hilo.
  Mmoja wa madereva wa magari ya taka yaliyokwama kutokana na miundo mbinu mibovu Bw. Frank John akielezea kero ya kwenye dampo la taka lililopo maeneo ya Pugu Kinyamwezi ambapo amesema taka zimelundikana barabara hazipitiki hata magreda ya kuzoa hayana pakupita na kuwaomba watu wanaohusika na dampo kujaribu kutengeneza njia mbadala na kushauri itafutwe njia kipindi cha Masika taka ziwe zinamwaga sehemu nyingine na kipindi cha Kiangazi kiwe na sehemu yake na kushauri mamlaka zinazohusika na usafi zijifunze kutoka kwa wananchi na sisi tujifunze kutoka kwao.
  Aidha Bw. John amewataka viongozi wahusika kutokaa maofisini na kutembelea maeneo husika na kujiuliza kwanini gari zinakwama na kuongeza kuwa tatizo hilo limepelekea lawama kwa baadhi kampuni za usafi kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa wakati.
  Hii ndio hali halisi ya viroba vya uchafu vilivyolundikwa katika eneo la Pugu Kwalala pembezoni mwa barabara na makazi ya watu ambapo wananchi wamekuwa wakizilalamikia kwa sababu kipindi cha mvua vinaweza kuwasababishia magonjwa ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.
  Mkazi wa eneo la Gongo Mwisho wa lami - Pugu Kwalala Bw.Erasto Njau akilalamikia ubovu wa magari ya taka ya Halmashauri ya Manispaa ya jiji la Dar es Salaam na vile vile utaratibu mbovu wa ukusanyaji wa taka ambapo hata kama gari imeharibika yangetumika magari mengine kuja kubeba taka suala ambalo linalohusu uongozi wa Manispaa ambao ndio unaogharamia magari yanayobeba taka kitu ambacho kinaonyesha utaratibu wa ubebaji taka bado haujakaa sawa.
  Mama Lishe Asha Omari Dundo akizungumzia kero ya Mlundikano wa taka katika eneo lake la biashara ambalo sio dampo rasmi la kutupia takataka na anapouliza anaambiwa magari yamekwama dampo kutokana na ubovu wa miundo mbinu kitu ambacho ni hatari kiafya kwa wateja wake wa chakula ambacho ndio biashara anayoifanya kwa ajili ya kusomesha watoto na kila anapouliza hapewi jibu linaloeleweka na ameiomba serikali kutupia macho swala hilo kwa sababu kumekuwa na kauli tofauti malori yamekwama na malori mabovu.
  Mama Lishe Asha Omari Dundo akiwaandalia wateja wake chakula cha mchana katika eneo ambalo ni hatarishi kwa walaji.
  Mkuu wa Afya Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam Bw. Membe Protus Membe akizungumzia jitihada za Manispaa katika kupambana na tatizo la mlundikano wa magari ya taka yaliyokwama katika eneo la Dampo la Pugu Kinyamwezi kutokana na ubovu miundo mbinu ya barabara unaopelekea kukwamisha zoezi la ukusanyaji taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar na kusababisha mlundikano wa taka nyingi kwa muda wa kipindi cha siku hizi tatu.
  Hata hiyvo amesema katika muda wa siku tatu kuanzia leo Manispaa itahakikisha inarekebisha miundo mbinu ya kuelekea dampo ili kuweza kupunguza msongamano uliopo wa magari ya taka yaliyokwama yaweze kurudi mjini kuendelea na ubebaji wa taka.
  Aidha Bw. Membe ameahidi kuwa shughuli za umwagaji taka katika dampo hilo zitakuwa zikifanyika mchana na usiku ili kuondoa mlundikano wa taka mitaani ambao umejitokeza katika muda wa siku tatu.

  0 0


  fibre
  The State University of Zanzibar (SUZA) in partnership with the African Development Resources Center would like to invite you in the four days hands on workshop on Certified Fiber Optic Technician. The Training scheduled on 28th to 31st of May, 9:00AM to 5:00PM at SUZA Main Campus Tunguu, about 17KM from Zanzibar City Center.

  Course overview
  This is an authoritative 4-day unique, high-value, hands-on practical course, which will provide participants with essential skills and knowledge necessary to design, install, splice, connectorize, troubleshoot and test fiber optic systems. Participants will be introduced to the latest developments and techniques in the Optical Fiber industry. The training material is approved by the Fiber Optic Association who also certify the successful candidates..
  Learning objectives
  This is a comprehensive, integrated training program which covers all aspects of both local and wide area optical networks. The courses have both theoretical and practical sessions covering fiber in communications, fiber, cables, splices, connectors, network design, installation, testing and safety and about 28 videos on hands-on processed for fiber optics and communications cabling – yes, even Cat 5.
  For more CLICK HERE

  0 0

  Mzungu Kichaa means “the crazy white man”, a name that raises many questions if you aren’t familiar with the artist. Mzungu Kichaa is considered a pioneer of Tanzanian Bongo Flava, one of the biggest genres in the region. 
  His socially conscious single and video Jitolee (2009) took Tanzania by storm and reached number one on the East African Charts soon after it was released. The video has reached well over a hundred thousand views on YouTube. 
  In Europe he won “Best Upcoming Artist” at the African Achievement Awards immediately after releasing his debut album Tuko Pamoja in 2009. His new release HUSTLE has received good reviews, including a feature in the Guardian UK as well as a nomination at the Danish Music Awards in the category “best world track”. The release includes his first recordings in english, and the hits Twende Kazi and African Hustle.
  The London performance is part of his “unplugged” tour, which has included a visit to Jazz Ahead in Bremen, a concert in his birth town Skanderborg and a concert at the prestigious SPOT festival in Aarhus, where he received a standing ovation in Aarhus Musikhus for his showcase. The artist will also be doing a performance in The Hague in Holland, before heading to Tanzania.
  Mzungu Kichaa is self-managed under his label Caravan Records and uses the social media to reach his fans. 
  You can follow Kichaa on www.facebook.com/mzungukichaa or www.twitter.com/mzungukichaa and listen to his music on www.soundcloud.com/mzungukichaa.


  0 0
 • 05/10/13--13:16: Article 5

 • Taasisi ya kuhamasisha maendeleo na mawasiliano katika jamii yenye makao yake mjini Musoma mkoani Mara yaJAMII INFORMATION NETWORK inatarajia kufanya Kongamano kubwa litakalo wahusisha  Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka Shule 10 za Sekondari za Manispaa ya Musoma Mwezi August Mwaka huu, ikiwa ni njia ya kuhamasishaMaendeleo na kuimarishaji wa Mawasiliano ndani ya Jamii.

  Katika Kongamano hilo mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu waliobobea katika Masuala uhamasishaji wa Vijana Kupambana dhidi ya Ukimwi,ujasiriamali,dhana ya kujiajiri,Changamoto katika Elimu kwa Vijana  pamoja na Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni njia ya kujenga Msingi bora wa Makuzi kwa Vijana wetu.
  Mbali na hivyo vijana hao pia wataelezwa jinsi ya kuwa Wazalendo katika nchi yao,kupambana na rushwa,Umaskini lakini pia wakipata elimu sahihi ya faida za uwekezaji kwa Tanzania,Sababu za Mimba za Mapema kwa watoto wa kike na jinsi ya kujenga Mahusiano na Mawasiliano yaliyo sahihi.
  Pamoja na Mtandao huu kuwa na nia njema katika kuwasaidia Vijana lakini bado kumekuwepo na Changamoto mbalimbali katika kufanikisha Kongamano hilo hasa katika Suala la kifedha,hivyo basi Taasisi ya JAMII INFORMATION NETWORK kwa nia njema inakuomba wewe Mtanzania,Mpenda Maendeleo,unaekaa ndani au nje ya nchi,Mashirika kusaidia Taasisi hii katika kufanikisha Kongamano hilo ili vijana wetu wakue katika Makuzi mema na kujenga Tanzania ya kesho  iliyostaarabika.

   Blog Master

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(Watatu kushoto) akiongoza kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC kilichofanyika jijini Cape Town Afrika ya Kusini leo.Wengine katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo akiwemo mwenyeji Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini(kulia),Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Namibia Bibi Netumbo Nandi-Ndaitwa(kushoto) na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao.
  Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC Dkt.Tomaz Salomao mjini Cape Town Afrika ya Kusini leo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini wakitoka katika ukumbi wa hoteli ya Westin jijini Cape Town Afrika ya Kusini mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalma ya SADc kilichofanyika leo.Rais Kikwete alikuwa nchini Afrika ya Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mkurugenzi Mtendaji na mratibu wa asasi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bwana Mark Suzman jijini Cape Town Afrika ya Kusini.Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Adam Malima.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagana na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Misaada la Marekani USAID Dkt. Rajiv Shah muda mfupi baada ya kufanya naye mazungumzo katika ukumbi wa Cape Town Convention Centre jana.Picha na Freddy Maro.

  0 0

   Mdau Innocent Melleck na mai Waifu wake Hanifa Hussein wakikata ndafu wakati wa tafrija ya ndoa yao iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Sunset (Tembo Hall),Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
   Maharushi Innochent Melleck na mkewe Hanifa Hussein wakiwa sambamba na wapambe wao kwenye tafrija hiyo ya ndoa yao iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Sunset (Tembo Hall),Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
   Maharushi wakiwa ni wenye nyuso za furaha na bashasha tele. 
   Bwana Hasuri Innocent Melleck
  Bi. Harusi Hanifa Hussein.


  0 0
 • 05/10/13--16:25: Article 2


 • 0 0

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyoundwa chini ya Sheria ya Chakula Dawa na Vipodozi Sura ya 219, ili kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi, na vifaa tiba kwa lengo la kulinda afya ya jamii dhidi ya madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo.

  Ili kutimiza wajibu huo, TFDA inasimamia pamoja na mambo mengine udhibiti wa uingizaji wa vyakula kutoka nje ya nchi na utengenezaji wa vyakula ndani ya nchi kwa ajili ya kulinda afya za watumiaji. 

  Katika udhibiti wa vyakula hivyo, michakato mbalimbali hufanywa ili kuwa na uhakika juu ya usalama wake kwa; kufanya tathmini na uchunguzi wa kimaabara, kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa usalama wa bidhaa kwenye soko na hatimaye kusajili majengo na vyakula baada ya kujiridhisha juu ya usalama wake.

  Kutokana na mfumo wa udhibiti uliopo, Mamlaka imesajili bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyofungashwa ikiwa ni pamoja na vinywaji aina ya soda zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje.

  Hivi karibuni kulitolewa taarifa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kueleza kuwa kinywaji cha soda ni sumu. Mamlaka ina mashaka juu ya taarifa iliyotolewa kwa sababu haidhani kama ilitolewa kwa kuzingatia misingi ya kisayansi.

   TFDA inapenda kuwatoa hofu watumiaji wa kinywaji hiki kuwa, soda ni bidhaa ya chakula ambayo inatumika kote duniani na huzalishwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama. Kwa upande wa TFDA, soda zote zilizosajiliwa zimepitia katika mchakato ambao unatoa uhakika juu ya usalama wake kwa lengo la kulinda afya ya binadamu.

  Tunapenda kutoa rai kwa vyombo vya habari kufanya utafiti wa kina hususan katika masuala yanayohusu ushahidi wa kisayansi ili kuondoa uwezekano wa kutoa taarifa kwa umma ambazo zinaweza kujenga hofu na mashaka ambayo hayastahili.

  Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kupitia;

  Mkurugenzi Mkuu,
  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
  Barabara ya Mandela, Mabibo External,
  S.L.P 77150
  Dar Es Salaam, Tanzania
  Simu: +255 22 2450512/2450751/2452108
  Fax: +255 22 2450793
  Barua pepe: info@tfda.or.tz
  Tovuti: www.tfda.or.tz

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil watatu kutoka kulia waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wakuu wa wizara hiyo, Makamishna, Maafisa Bajeti na Ugavi na Ununuzi wa wizara hiyo wanaohudhuria kikao kazi cha kuandaa Mpango Kazi na Ununuzi wa wizara hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa fedha 2013/2014, wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mwamini Malemi na wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Lilian Mapfa.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil aliyesimama akikagua kazi ya Maandalizi ya Mpango Kazi wa Idara ya Uhamiaji katika kikao cha kuandaa mpango kazi huo kinachoendelea mjini Morogoro, anayemtazama ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Piniel Mgonja wa pili kutoka kushoto ni Mhasibu Mkuu wa Idara ya Uhamiaji P. Kabale.kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa fedha 2013/2014.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil akikagua zoezi la Uandaaji wa Mpango kazi na Ununuzi wa Idara ya Magereza akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Bajeti wa Idara ya Magereza ikiwa ni maandalizi ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/2014.
  Baadhi ya Maafisa Bajeti wa Jeshi la Polisi wakipokea maelekezo muhimu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil aliyesimama baada ya Katibu Mkuu huyo kukagua Mpango kazi na Ununuzi unaoandaliwa na Maafisa hao wa Bajeti ikiwa ni sehemu ya Maandalizi ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi aliyesimama akitoa Maelekezo kwa Maafisa Bajeti wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu baada ya kukagua Mpango kazi na Ununuzi wa Idara hiyo unaondaliwa na Maafisa bajeti hao, katika kikao cha kuandaa Mpango kazi na Ununuzi kinachotarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
  Aliyekaa wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii Bw. Fidelisi Mboya akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil kuhusu zoezi la Uandaaji wa Mpango kazi na Ununuzi kwa ajili ya Idara yake kama sehemu ya maandalizi ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2013/2014 aliyekaa katikati ni Afisa Bajeti wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo Michael Msikila pembeni yake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma kwa Jamii Bw. Aloyce Msika.

  0 0  kusoma habari zake zaidi bofya hapa

  0 0

  Nesta Robert "Bob" Marley, OM (6 February 1945 – 11 May 1981) was a Jamaican singer-songwriter and musician. He was the rhythm guitarist and lead singer for the ska, rocksteady and reggae bands The Wailers (1963-1974) and Bob Marley & The Wailers (1974–1981). Marley remains the most widely known and the best-selling performer of reggae music, having sold more than 75 million albums worldwide.He is also credited with helping spread both Jamaican music and the Rastafari movement to a worldwide audience

  0 0


  CHE MUNDUGWAO
  --- 
  MIMI NASHANGAA SANA JUU YA SERIKALI PALE BIFU ZINZPOKOTEZEA KWA RUGE BASI UHINGILIA KATI KUTAFUTA SULUHU KWA KWELI KUNAACHA MASWALI MENGI.
   
  KWA MTAZAMO WA KIUNGWANA NI NI JAMBAO JEMA SANA WALAKINI YANGU KWA NINI IWE KWA RUGE TU AWALI WAZIRI NCHIMBI AKIWA NAIBU WA WIZARA YETU YA HABARI UTAMADUNI,VIJANA NA MICHEZO A AMEINGILIA KATI JAMBO LA RUGE NA MBILINYI (SUGU) NA SASA TUNASIKIA RUGE NA LADY J DEE
  SERIKALI IMEINGILIA KATI MAONI WENGI MBONA KUMBUKA ASHA BARAKA WA TWANGA PEPETA NA MAMAA WA MASHUJAA HATA  TAFF NA BONGO BOVIE, VIKUNDI VYA TAARABU NI BAHADHI TU LAKINI WENGI WAPO WALIKUWA KWENYE MVUTANO MKALI LAKINI SERIKALI IKIWA KIMYA USHAURI WANGU HATUA HIYO NZURI SANA KULETA AMANI KWA WASANII LAKINI
  IWE KWA WOTE BILA KUBAGUA WATATUE INAPOTEA MIGOGORO HATA YA KIMASLAI PIA KUONDOA DHANA KUWA RUGE ANAPENDELEWA SERIKALI MADHALA YAKE KWAHISIA HIZO NI KUBWA SANA,KUSIPO ZIBA UFA KUTAJENGA UKUTA TUCHUKUE HATUA SASA, MAANA SISI NDIO TUPO KARIBU NA WASANII MUDA MWINGI TUNAWAMBUSHA SERIKALI JUU YA UMUHIMU WATOA HUDUMA SAWA KWA WOTE BILAKUJALI UMAARUFU WA MSANII KWA KUANZISHA DAWATI LA  HUDUMA KWA WASANII ITASAIDIA SANA

  MIMI

  CHE MUNDUGWAO
  MWENYEKITI- CHAMA CHA MUZIKI ASILI TANZANIA NA
  MJUMBE WA BODI SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA

  0 0

  Septemba 1973 jijini Algiers, Algeria: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika mazungumzo na Rais wa Uganda Field Marshal Iddi Amin Dadah pembeni mwa mkutano wa nchi zisizofungamana na upande wowote. Kushoto ni Mama Maria Nyerere na kulia ni Waziri wa Nchi za Nje Mhe John Malecela. 

  0 0


  0 0

  Lady Jay Dee

  Na Mwandishi Wetu
  IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
  Mwandishi wa habari hii alimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
  “Mimi kama nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa.
  Mhe Makala
  "Na siyo Waziri Makalla tu, pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
  Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari ameshatoa fuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
  "Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka...."  anasema Ruge.
  Kushoto ni Dkt Emmanuel Nchimbi, wakati huo akiwa Waziri wa  Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo akiwa na Mhe Joseph Mbilinyi '"Sugu" na Ruge Mutahaba baada ya kuwapatanisha
  Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliibuka hadharani kuituhumu Clouds Media Group  kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na blog yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge   na kipaji chake kwa ujumla, tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
  Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa.
older | 1 | .... | 129 | 130 | (Page 131) | 132 | 133 | .... | 3272 | newer